Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu mimi naona tunapishana lugha tu hapa. wanaposema Government Expenditure ni katika lugha ile ile ya makisio na ndio maana tunapanga bajeti ya nchi hata kabla hatujawa na fedha mkononi. Kwa hiyo bajeti walokaa mwaka huu kwa ajili ya 2015 hadi 2016 ni masikio ya matumizi ya serikali kwa mwaka kama tunavyokisia mwaka huu GDP itapanda kiasi gani lakini matokeo halisi ya GDP Kiuchumi yatategemea na mambo mengine muhimu kama mfumko wa bei na kadhalika. Hii ni dhana tu inayotangulia kwa kuthamisha mchango wa serikali katika kukuza GDP.

Hivyo kifupi tunapozungumzia kodi zetu, ni sehemu tu ya mapato mapana ya serikali ili kuiwezesha kutoa huduma zake, hivyo zile specific function za serikali katika uzalishaji ndizo huhesabiwa kama sehemu ya GDP. Kumbuka hapa tunazungumzia kodi za Shinyanga hivyo ndio maana tumechukulia swala hili kwa udogo wake badala ya kuzungumzia njia zote za mapato ya serikali kama sehemu ya GDP. Kwa hiyo matumizi ya serikali iwe vifaa vya kivita, shule, hospital, barabara, social welfare ni mchango wa serikali katika kukuza GDP japo unatokana na mapato mbali mbali mingine misaada na mikopo, lakini mwisho wa siku madeni haya yatalipwa na kodi hata kwa miaka 50 ijayo..

Inawezekana tunapishana lugha lakini lugha nayosisitiza hapa ni kwamba mapato ya serikali (KODI) sio sehemu ya PATO LA TAIFA (GDP). Hilo moja. Pili, lugha nayojaribu kusisitiza pia ni kwamba role ya serikali katika maendeleo ya wananchi na mkoa kwa ujumla, na hata taifa hujengwa na mfumo wa KODI ambayo ni mapato ya serikali kwa njia mbalimbali tulizojadili awali. GDP au pato la taifa will remain as GDP, what matters ni je, serikali inakusanya kodi ambayo ni sawa na asilimia ngapi ya hiyo GDP? Kama GDP ya Shinyanga ni sh trillioni mbili, je mchango wa wananchi wa shinyanga katika hiyo GDP ni kiasi gani kabla ya kuanza lawama juu ya rasilimali? Je, makusanyo ya Kodi shinyanga ni asilimia ngapi ya mchango wa wananchi wa Shinyanga katika GDP? The higher the ratio, the merrier. Kwa Shinyanga tumeona kwamba Taxation to GDP Ratio is only 0.9% (haijafika hata asilimia moja). Kwanini tushambulie GDP kama Adui na sio Taxation? Huduma za kijamii kwa wana Shinyanga zitoke wapi kama sio kwenye makusanyo ya Kodi? Zitawezaje kutoka directly from GDP? Haya ndio masuala ya msingi ya kuyatazama.
 
Waziri anajichanganya pia. Sentensi ya kwanza anazungumzia pato la taifa (GDP), baadae anazungumzia pato la serikali (ambalo kimsingi ni kodi, lakini hafafanui hivyo kuacha hali ya mchanganyiko). Ni kwa sababu bunge limejaa mambumbumbu ndio maana mambo kama haya yanapigiwa makofi na kelele za "ndio".
Basi tuachane na Waziri Kigoda, tumsome Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pato la Taifa- na Mwenendo wa Mfumuko wa Bei15.--- Mheshimiwa Spika, Takwimu za awali zinaonyesha kuwa Pato Halisi la Taifa (GDP) lilikua kwa Asilimia 7.4 mwaka 2008- ikilinganishwa- na Asilimia 7.1 mwaka 2007. Ongezeko hili limechangiwa zaidi na ukuaji katika shughuli za kiuchumi za huduma kutoka Asilimia 8.1 mwaka 2007 hadi Asilimia 8.7 mwaka 2008. Hali kadhalika, kulikuwa na ongezeko la ukuaji katika shughuli za kilimo kutoka Asilimia 4.0 mwaka 2007 hadi Asilimia 4.8 mwaka 2008. Vilevile, viwango vya ukuaji viliongezeka katika Sekta ndogo za mawasiliano, biashara, ujenzi, afya, bidhaa za viwandani, huduma za fedha na elimu. Jitihada zinaendelea kufanyika kwa lengo la kuboresha miundombinu ya barabara za Vijijini na Umwagiliaji, pamoja na utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa Sekta hiyo, na hivyo kuepukana na athari za kuporomoka kwa Uchumi wa Dunia.-
 
While we Continue with these discussions, It is worth to understand a little bit about governments revenues
There are two types of revenues
1. Tax based revenues.
2. Non Tax revenues

Here I will Show some Non Tax based Revenues, These Include

1(a). Aid from another level of government
(intragovernmental aid) - for example, in the United States, federal grants may be considered non-tax revenue to the receiving states, and equalization payments.

1(b) Aid from abroad ( foreign aid)

2. Tribute or indemnities paid by a weaker state to a stronger one, often as a condition of peace after suffering military defeat. The war reparations paid by the defeated Central Powers after the First World War offer a well- known example.

3(a). Loans, or other borrowing, from monetary funds and/or other governments

3(b)Revenue from state-owned enterprises (for
example, revenue from Public Sector Unions )

4. Revenue (including interest or profit) from
investment funds (collective investment
schemes), sovereign wealth funds , or
endowments

5. Revenues from sales of state assets
Rents, concessions, and royalties collected by the state when it contracts out the right to profit from some good or service to a private corporation . An example are contracts for resource extraction (for such natural resources as minerals , timber , petroleum and natural gas, or marine resources) collected privately under license from state-owned lands

6. Fines collected and assets forfeitured as a penalty . Examples include parking fines , court costs levied on criminal offenders

7(a). Fees for the granting or issuance of permits or licenses . Examples include vehicle registration plate permits, vehicle registration fees, watercraft registration fees, building fees, driver's licenses , hunting and fishing licenses , fees for professional licensing, fees for visas or passports, fees for demolition ,rezoning , and land grading (which causes silt ), and sometimes for increasing stormwater
runoff , destroying native vegetation , and cutting-down healthy trees.

7(b).User fees collected in exchange for the use of many public services and facilities. Tolls charged for the use of toll roads are an example

8. Donations and voluntary contributions to the state
 
Inawezekana tunapishana lugha lakini lugha nayosisitiza hapa ni kwamba mapato ya serikali (KODI) sio sehemu ya PATO LA TAIFA (GDP). Hilo moja. Pili, lugha nayojaribu kusisitiza pia ni kwamba role ya serikali katika maendeleo ya wananchi na mkoa kwa ujumla, na hata taifa hujengwa na mfumo wa KODI ambayo ni mapato ya serikali kwa njia mbalimbali tulizojadili awali. GDP au pato la taifa will remain as GDP, what matters ni je, serikali inakusanya kodi ambayo ni sawa na asilimia ngapi ya hiyo GDP? Kama GDP ya Shinyanga ni sh trillioni mbili, je mchango wa wananchi wa shinyanga katika hiyo GDP ni kiasi gani kabla ya kuanza lawama juu ya rasilimali? Je, makusanyo ya Kodi shinyanga ni asilimia ngapi ya mchango wa wananchi wa Shinyanga katika GDP? The higher the ratio, the merrier. Kwa Shinyanga tumeona kwamba Taxation to GDP Ratio is only 0.9% (haijafika hata asilimia moja). Kwanini tushambulie GDP kama Adui na sio Taxation? Huduma za kijamii kwa wana Shinyanga zitoke wapi kama sio kwenye makusanyo ya Kodi? Zitawezaje kutoka directly from GDP? Haya ndio masuala ya msingi ya kuyatazama.
Hapana mkuu wangu swala la kodi unalitumia vibaya kwa sababu wakati wa Nyerere hatukuwa na kodi lakini serikali ilikuwa na dhamana kubwa kwa wananchi. Kodi ni mfumo tu wa Kiutawala ambao unatoza wananchi kugharami matumiuzi ya serikali ambayo haizalishi na hivyo kuwa sehemu ya vyanzo vyake vya mapato.

Zipo nchi hazina hata kodi na zinaendelea GDP inapanda vile vile, na haswa sisi hizo kodi unazolipa zinaenda katika matumizi makubwa ya recurrent tena sio huduma muhimu za maendeleo, fedha za maendeleo na miradi ya serikali tunatenga bakuli na misafara. Hayo matumizi ya serikali uloyaweka katika GDP sehemu kubwa ni tegemezi tukiamini huko nje kuna fedha nyingi wakati tunagawa madini na ardhi bure kwa wageni.

Makuzi ya GDP ni ishara ya maendeleo toka pale mlipokuwa mwaka jana na inategemea mtaji mlokuwa nao kama vile wewe ulikuwa na mtaji wa Mil.50 mwaka jana na unategemea mwaka huu kupanda hadi kufikia Mil. 60 ina maana kuna ongezeko la uzalishaji linalotegemewa na mambo yatakuwa mswano, hivyo unaweza kupanga mambo mengi zaidi na hata kusaidia watu wengine zaidi lakini inapotokea kujipangia Kujirusha na vipapi ukawaacha nyumbani hakuna hata mpango makini wa stock ya chakula hapo story itakuwa tofauti....
 
Labda nikuulize:

1. Pato la Taifa maana yake ni nini?
2. Composition ya pato la taifa ni nini?
3. Nini ni uhusiano baina ya mapato ya serikali (kodi) na pato la taifa?
4. Nini ni tofauti baina ya mapato ya serikali (kodi) na pato la taifa?

Nadhani ufafanuzi wako katika hili litaondoa sintofahamu iliyopo.
Mkuu haya maswali mengine ni kutaka turudi nyuma. Kama wewe unafikiri Pato la Taifa ni kodi za serikali basi imetosha...
 
Kwa sababu lugha alotumia Mchambuzi ni kama kusema Macho ndio sura ya mtu, nami nikasema hapana macho ni sehemu tu ya sura ya mtu. Macho sio sura, ila sura ni mjumuiko wa viungo vingi ikiwa ni pamoja na kope.. Lol na kama ulimsoma vizuri Mchambuzi aliendelea kukazania umuhimu wa macho wakati hata kipofu ana sura ila nikaeleza umuhimu wa macho katika kuona, unabakia pale pale kuwa ni mchago kubwa katika hisia za binadamu.
.

Asante kwa majibu yako.. Kwa hiyo unaweza kusema kodi ni pato la Taifa/serikali..

Swali la pili, kama Mchambuzi alivyosema hapo juu na kuonyesha matumizi ya serikani ni sehemu ya mchango wao ktk GDP ndivyo Zitto alichokuwa akizungumzia kwa matumaini kwamba ikiwa wao wanachangia kwa sehemu kubwa ya GDP lakini imeonyesha mchango mdogo wa serikali (Expenditure) ina maana hii ndio sababu kubwa ya Shinyanga kuwa chini. makuzi makubwa ya GDP ya SHY yatokana na vitu vingine kwa sababu serikali imeendelea kuchangia kiasi kidogo katika maisha yao ndio maana ile dhahabu imethaminishwa juu mchango wake lakini wananchi hawapati kitu na hivyo kuathiri hata mchango wao katika Kodi maana wengi wao hawana ajira.. Kifupi hakuna mzunguko ama trickle down ya kimaendeleo .
.
Hapa ndo umenichanganya ila inawezekana tatizo ni muuliza swali.. Ngoja nijaribu tena kivingine.

Kama nikiuuza Mihogo yenye thamani ya mil.20.. Je hizi mi 20 zitakaweka katika majumuisho ya pato la Mkoa/Taifa? (kumbuka hizi Mil. 20 ziko mfukoni mwangu)

.

Asante kwa majibu yako.. Kwa hiyo unaweza kusema kodi ni pato la Taifa/serikali..
Yah kwa sababu serikali ni sehemu ta Taifa. jana hapa canada tumesherehekea miaka 148 ya Uhuru (serikali) haina maana Taifa hili lina miaka 148...Canada ilikuwepo hata kabla ya Uhuru (serikali)..
Hapa ndo umenichanganya ila inawezekana tatizo ni muuliza swali.. Ngoja nijaribu tena kivingine.

Kama nikiuuza Mihogo yenye thamani ya mil.20.. Je hizi mi 20 zitakaweka katika majumuisho ya pato la Mkoa/Taifa? (kumbuka hizi Mil. 20 ziko mfukoni mwangu)
Yeah ni sehemu ya pato la Taifa kwa sababu wewe pia ni sehemu ya Taifa (Uzalishaji) tena basi wala haitazamwi ukiuza kiasi gani ila tunategemea shamba lako kuzalisha kiasi gani1. Hivyo tunaweza tegemea shamab lako kuzalisha Mil 30 ndio itakuwa pato la Taifa japo kutokana na factors fulani ukaja kuuza Mil.20.

Hapa ndo umenichanganya ila inawezekana tatizo ni muuliza swali.. Ngoja nijaribu tena kivingine.

Kama nikiuuza Mihogo yenye thamani ya mil.20.. Je hizi mi 20 zitakaweka katika majumuisho ya pato la Mkoa/Taifa? (kumbuka hizi Mil. 20 ziko mfukoni mwangu)

]Yah kwa sababu serikali ni sehemu ta Taifa. jana hapa canada tumesherehekea miaka 148 ya Uhuru lakini haina maana Taifa hili lina miaka 148...Canada ilikuwepo hata kabla ya Uhuru..

Sasa kama hizi mil 20 ziko mfukoni mwangu, na mie sijazilipia kodi, je Serikali itatoa wapi pes za kuniletea huduma za jamii? shule, barabara, umeme na nk (tuchukulie kijiji kizima wamelima, wameuza mazao yao, lakini hawakulipa ushuru/kodi)
 
Hapa ndo umenichanganya ila inawezekana tatizo ni muuliza swali.. Ngoja nijaribu tena kivingine.

Kama nikiuuza Mihogo yenye thamani ya mil.20.. Je hizi mi 20 zitakaweka katika majumuisho ya pato la Mkoa/Taifa? (kumbuka hizi Mil. 20 ziko mfukoni mwangu)

Sasa kama hizi mil 20 ziko mfukoni mwangu, na mie sijazilipia kodi, je Serikali itatoa wapi pes za kuniletea huduma za jamii? shule, barabara, umeme na nk (tuchukulie kijiji kizima wamelima, wameuza mazao yao, lakini hawakulipa ushuru/kodi)
GDP ni kama suruali yenye mifuko minne.. haijalishi utaweka kiasi gani mfuko gani ila kila mfuko utabeba kiasi gani, unategemea weka fedha zaidi mfuko wa nyuma zaidi ya mingine lakini in Total fedha ulotegemea kuwa nazo ndizo tunazozungumzia.

Kwa hiyo usipolipa kodi serikalini, bado fedha ulokuwa nayo itahesabika kuwa mchango wako katk GDP pengine wewe umeongeza ukubwa shamba na upo Shinyanga ina maana unategemea kutakuwa na ongezeko la mapato yako mwaka kesho. Ulipaji kodi ni muhimu kwa sababu unaiwezesha serikali kukabiri makadirio uloyafanya katika matumizi yake na kikubwa zaidi ni kutokuwa tegemezi la misaada ya nje badala ya wananchi wenyewe kuwa msingi wa pato lake. Lakini katika mipango yake haiwezi kuzuiwa kwa sababu Shinyanga wamechangia kidogo kwani asilimia kubwa ya mipango ama bajeti ya nchi inatangulia mapato ya kodi itakayo kusanya. Serikali inapanga mwaka 2015 - 2016 itafanya mambo gani mbele ya pato watalokusanya..

Kama vile wewe ukiamua kujenga nyumba haina maana una Tsh. Mil. 200 tayari mfukoni isippokuwa umeweka projection kuwa katika mwaka mzima utaweza kupata hizo Tsh. mil.200, haijalishi utazipata wapi. Hivyo basi unapotaka kujenga nyumba hutazami mshahara wako bali mipango mingi mingine ya mikopo na kadhalika ikiwemo na mshahara.

Shule, barabara, Umeme ni mipango ya serikali inayopangwa kabla ya kodi yako haijapokelewa. Katika upangaji wa utekelezaji huo tunategemea misaada kupitia wafadhili wa nje ambao hutuwekea mikataba mibovu ikiwa ni pamoja na maliasili zetu zimilikiwe na mashirika yao pasipo masharti magumu. Kwao hawa mataifa makubwa neno masharti magumu ni kutaka kupunguza faida zao na uwezo wa kumiliki. Hivyo wapo hapa kuwekeza ili wapate faida zaidi na ndio maana dhahabu yetu tunaigawa karibu na bure ili wao watupe mikopo ama misaada ya kujenga barabara, mashule, umeme na kadhalika..
 
Sitaki kuwaharibia mjadala lakini kuna kitu sijakielewa vizuri

Mkandara kuna sehemu umeandika kuwa Kodi si pato la Taifa bali ni pato la Serikali. Na hapo umeandika kuwa kodi ni sehemu ya pato la Taifa. Swali langu ni je kuna tofauti kati ya Kodi pato la taifa na kodi pato la serikali? Maana mie kwangu mie tunapongelea kuhusu kodi sioni tofauti kati ya serikali na taifa. Ufanunuzi wako tafadhali.

Swali la pili kwako na Mchambuzi

Tusema wanakijji wamelima shamba lao la mihogo na kuvuna mihongo yenye thamani ya mil.20, hizi mil 20 zitahesabika katika pato la Taifa!? (kama nimeelewa vizuri) Lakini hawa wanakijiji hizo mil. 20 wasipozilipia kodi labda kwa sababu ya msamaha ua ukwepaji kodi.. Je likapokuja swala la "gawio" katika maendeleo ya shughuli za jamii, je mgao utalenga hizo mil 20 au utalenga mchango wao wa kodi/ushuru?

(natumaini mtalielewa ili swali maana hizi taaluma zinawenyewe sisi wengine ni kuchota elimu tu)
Alinda,

Mfano wako ni mzuri sana kutusaidia kuliweka suala hili sawa pengine for good. Wanakijiji wakilima na kuvuna mihogo yenye thamani ya soko ya shillingi milioni 20, huo utakuwa ni mchango wao kwa pato la mkoa na hata taifa (GDP). Na hiyo itatoa fursa kwa PATO LA SERIKALI (KODI) kupatikana kupitia tozo katika muktadha wa huo uzalishaji wa mihogo.
Tukirudi kwa wakulima hawa wa Mihogo - If it’s a business case, watatoa gharama zote na kubakisha faida. Wakulima hawa watakuwa na uhuru wa kutumia Faida itakayobakia kwa jinsi watakavyoamua, hata wakiamua kuachana na kilimo chao na kula mtaji wote. Lakini lipo jambo muhimu hapa, nalo ni kwamba – moja ya gharama katika uzalishaji wa bidhaa na huduma, tena gharama ambayo ipo kwa mujibu wa sheria, ni KULIPA KODI, unless kuna tax exemption ambayo pia nayo lazima iwe kwa mujibu wa sheria. Kwahiyo kama sehemu ya gharama za uzalishaji wa bidhaa (mihogo kwa mfano), wakulima hawa watalazimika kulipa kodi kabla ya kupiga mahesabu ya Faida ya jasho lao. Swali linalofuata ni je:

· Kwanini Kulipa kodi ni kwa mujibu wa sheria?

Ni kwa sababu, katika taifa au uchumi wowote ule, zipo aina mbili ya Goods namely - Public goods and Private goods. Awali tulijadili maana ya public goods na kwanini zinaitwa hivyo, kwa mfano taa za barabarani (security lights), traffic lights, bus station, national defense system, light house (for ships) n.k. Bidhaa hizi (Public goods) zina two main features namely (1) Non Excludable and (2) Non-Rivalrous. Kwa maana nyingine, in order for a good to qualify as a "public good", it must be non-excludable and non-rivalrous. Ni such feature ndio hupelekea umuhimu wa serikali kugharamia provision of such goods. Kwanini? Mfano mzuri ambao hutumiwa in classical economics ni light house(Mnara wa meli). Tuujadili mfano huu:

Mnara wa meli ni "non-excludable" kwa sababu its impossible kuzuia meli zisitumie au zisifaidike na mnara husika hata kama hazikuchangia katika kugharamia ujenzi wa mnara huo. Lakini pamoja na hayo, kwa usalama wa meli, abiria na mizigo, meli zote lazima zitumie na zifaidike na mnara huo. Mnara wa meli vile vile ni “Non‐rivalrous” kwa sababu kama tayari meli nyingi zinafaidika na mnara uliopo, hakuna extra cost itakayotokea kwa kuruhusu meli nyingine kufaidika nan a mnara husika. Hii ni tofauti na Private goods kama mkate, boksi la juisi ambazo zote ni “rivalrous good” kwa sababu the more these are provided to someone or to some people itahitaji more and more goods to be produced vinginevyo kutakuwa na shortage. Kwa private goods, such chaarcteritics ndio zinatoa incentives za kuzizalisha na kusambaza kibiashara. Lakini for public goods, the fact kwamba ni ‘non excludable’ and ‘non-rivalrous’, uzalishaji au provision yake by private sector huwa haina tija. Lakini kwa vile such goods ni muhimu sana, serikali lazima iingie gharama kwa maslahi ya taifa. Gharama za serikali katika jambo hili ni KODI, na sio GDP.

Nimetoa mfano huu kwa makusudi. Tukichukulia wananchi wa Shinyanga, Arusha n.k, wote wana mahitaji kama haya mengi tu ambayo bila ya ushiriki wa serikali, provision of such goods haitakuwepo, na italeta a huge crisis. Tukitumia mfano wa wakulima wa Mihogo, iwapo wakulima wa Mihogo uliowatolea mfano wanazalisha zao hili lenye market value tuseme ya T.sh 2,000,000, sasa ili mazao yaweze kufika Sokoni, watalazimika kutumia barabara. Barabara ni moja ya Public Goods, whether ni barabara chini ya Tanroads au zile chini ya Manispaa husika. Katika hali ya kawaida, wakulima hawa watahitajika kulipa kodi ya aina Fulani ili serikali iweze kuendelea kugharamia matumizi ya barabara husika na wakulima hawa lakini pia na watumiaji wengine. Provision of such services ndio maana halisi ya KEKI YA TAIFA. Na uwepo wa Fedha kugharamia mahitaji haya ndio maana hali ya SUNGURA MKUBWA au SUNGURA MDOGO, kule kwenye mijadala Bungeni.

Mgao halali kwa Wananchi?!!?

Mgao kwa wananchi maana yake ni kugawana kwa keko ya taifa. Kugawana kwa keki ya taifa maana yake ni uwepo wa sungura mkubwa na sio mdogo. Sungura hapa maana yake ni MAPATO YA KODI, Not GDP. Kwahiyo katika hali ya kawaida, mgao wa serikali kwa wananchi husika ni lazima utokane na michango ya wananchi husika kwenye PATO LA SERIKALI (KODI), ili wananchi hao wapate huduma wanazostahili. Vinginevyo kama wakulima hawa wamevuna mihogo yenye thamani ya shillingi milioni 20 (na huu ndio mchango wao kwa PATO LA TAIFA/GDP), lakini wakatumia pato hilo kugawana kwa matumizi binafsi na kukwepa kodi, wakulima hao watakuwa na uhalali gani wa kudai kwamba hawapati keki ya taifa? Ndio maana kodi ipo kwa mujibu wa sheria, na upatikanaji wa huduma za kijamii (keki ya taifa) ni lazima iendane na mchango wa wananchi au mkoa husika katika mapato ya serikali.

Ndio maana shughuli za uzalishaji zinatozwa kodi. Shughuli zote za uzalishaji (GDP Output) ambazo hazilipi kodi na kufanya hivyo kinyume cha sheria, maana yake ni kwamba mapato yake yanaenda kwenye mifuko ya wazalishaji kwa matumizi ambayo hayahusu umma bali maisha binafsi. Jamii ya aina hiyo haina uhalali wa kulalamika kwamba wanakosa keki ya taifa. Ndio maana suala la kodi katika demokrasia zilizokomaa ni suala muhimu sana katika chaguzi kuu. Mara nyingi, ceteris paribus, wananchi huwa more concerned zaidi with how their taxes are being spent kuliko suala la GDP.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu haya maswali mengine ni kutaka turudi nyuma. Kama wewe unafikiri Pato la Taifa ni kodi za serikali basi imetosha...

Kodi ni pato la serikali, na pato la taifa ni thamani ya bidhaa na huduma zinaozalishwa katika sekta mbalimbali ndani ya uchumi husika, na thamani hii huwa ni 'thamani ya sokoni'.

Pengine kiswahili kinakuchanganya. Consider kwamba:

1. Mapato ya kodi ni TAX REVENUES na Pato la Taifa ni NATIONAL INCOME. Revenue and income yote yana maana moja kwa lugha ya kiswahili.

2. GDP Inaitwa National "Income" kwa sababu value of output lazima iwekewe thamani ya sokoni kwa kuangalia bei ya bidhaa na huduma husika kule sokoni ni kiasi gani. Kwa maana nyingine, maharage husika yakipelekwa leo sokoni, output yake ina thamani gani kule sokoni in terms of income ambayo mzalishaji angepata? That's where the income notion comes in.

Nashauri kwamba pengine tunapojadili GDP, tusitumie neno "national income" (pato la taifa bali), National Output ili tuweze tofautisha vizuri GDP and Tax Revenues.

Lastly, reason why kuna neno taifa katika GDP (pato la taifa), ni kwa sababu ndogo tu nayo ni kwamba kinachoangaliwa ni output ndani ya mipaka ya "taifa", output katika sekta mbalimbali ndani ya taifa husika. Ukiweza unaweza sema ni pato la nchi. Lakini kwenye suala la "pato la serikali", anayetoza kodi na kuzitumia kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali ni serikali, ndio maana mapato haya yanaitwa 'mapato ya serikali'.
 
Mkuu mimi nayaelewa yote haya isipokuwa wewe ndio unachanganya unapoanza kuyatumia katika mifano yako. Hili ni somo kubwa sana na linaingiliana kila mahala huwezi kuchomoa kitu kimoja kuhalalisha kitu kikubwa.. sasa Soma Kiuchumi wanasema nini kuhusu National Income..

National Income:- A variety of measures of national income and output are used in economics to estimate total economic activity in a country or region, including gross domestic product (GDP), gross national product (GNP), net national income (NNI), and adjusted national income (NNI* adjusted for natural resource depletion).
 
Swali la msingi hapa ni hili
Je Kilimanjaro na Shinyanga ni mkoa gani unachangia GDP ya Tanzania kwa wingi zaidi?
 
Fine, kwa mtazamo wako, tofauti kubwa baina ya Income na Revenue ni nini. Kuwa mwangalifu na utumie lugha ya kiingereza kama hapo maana ukianza kiswahili na mifano ya suruali ya mifuko minne, utaisha kuita vyote - income and revenue kama 'mapato'.
 
Hapa tunazumguza kiswahili, mimi sio kati ya wale walokwenda shule wakasoma kwa kiingereza inapokuja kujieleza kwa kiswahili wanabwaya.. hapana naweza kujieleza japo sii mwandishi mzuri sijui kupanga maneno ipaswavyo lakini naelewa nachoandika.

INCOME ni mapato baada ya matumizi kama kusema net profit na REVENUE ni mapato ya jumla kabla ya matumizi Tumeelewana?
 
Swali la msingi hapa ni hili
Je Kilimanjaro na Shinyanga ni mkoa gani unachangia GDP ya Tanzania kwa wingi zaidi?
Mkuu Gamba la Nyoka.

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu?Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam.
 
Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu inalipa kila mwaka kodi Dar es salaam kiasi gani?
 
Umeona sasa mkuu Ritz, hii disparity sijui kwa nini Mchambuzi haioni. Kutokana na weakness katika taxation regime, ambapo kodi kutoka sehemu moja ya nchi zinakusanywa sehemu nyingine,ni vigumu kuchukulia kodi ya mahala pekee as an indicator ya sehemu hiyo ya kuchangia katika mapato ya serikali compared na sehemu nyinginezo.

Indicator nzuri zaidi, ni kutumia kipimo cha overall production of goods and services ya sehemu fulani kwa mwaka
 
Last edited by a moderator:
Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu inalipa kila mwaka kodi Dar es salaam kiasi gani?
Soma hii hotuba kiduchu ya Lema Waziri Kivuli Mambo ya Ndani alikuwa anamaanisha nini...

Mheshimiwa Spika, Baada ya kuacha jukumu lao la msingi la kusimamia sheria za barabarani na kuanza kukusanya mapato, ajali za barabarani zimeongezeka sana. Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2013, jumla ya ajali za barabarani zilizohusisha magari katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Pwani, Kilimanjaro, Arusha na Morogoro zilikuwa ni 459,931, na ajali hizi zilisababisha vifo vya watu 2,408 na majeruhi 16,040. Kwa upande wa bodaboda watu waliofariki kutokana na ajali ni 1,106 na majeruhi 6,581. Mheshimiwa Spika, Ripoti ya Haki za Binadamu ya 2013, inasema kwamba nchi inapata hasara ya kati ya asilimia 1 hadi 2 ya Pato la Taifa (GDP) kutokana na ajali za barabarani. Kwa hiyo, uamuzi wa Serikali wa kukifanya kikosi cha usalama barabarani kuwa kitengo cha ukusanyaji mapato umekuwa ni hatari kubwa kwa maisha ya raia na uchumi wa nchi.
 
Back
Top Bottom