Tafadhali usiite ZNZ jimbo, katiba ya zanzibar ya mwaka 2010 inaitambua kama nchi ikiwa na bendera,wimbo wa taifa, vikosi vya majeshi,Bunge lao, Rais na makamu wawili, taasisi na mashirika yao.
Watalii wa znz wamechaguliwa kwa kura, ni wabunge kama wabunge wengine na wana kila haki kama wabunge wengine hilo kidemokrasia na katiba unayosema ni kweli, kimantiki, fikra ukweli na uchumi ni watalii wazuri tu, tutafafnua;
Kwanini ni Watalii?
Wamekuja kuwakilisha znz katika bunge la JMT kwa mujibu wa katiba. Tatizo hawatambuliki Zanzibar walikotoka na wao hawatambui Tanganyika walikofikia.
Hapo ndipo dhana ya utalii iliposimama wima.
ZNZ: Kwa mujibu wa katiba ya znz (2010), jambo lolote lililoamuliwa na bunge la JMT lazima likubaliwe na BLW. Shiviji kapotosha kusema tabled as procedure, ukweli ni kuwa katiba ya 2010 imesesema penye mgongano, katiba ya znz ipo juu, kwa maana juu ya katiba ya JMT.
Kama wabunge wamekuja Dodoma kutoka znz na hawawezi kuaminiwa na znz hadi jambo liende BLW, hapo wana kazi gani kama si utalii.
Wakiwa Dodoma waziri mkuu wao ni Pinda, Pinda akikutana nao Unguja hakuna anayemjua.
kwamba, hakubaliki znz nao wanamuona kama talii.
Hawaana kazi znz wala Tanganyika, Dodoma wanafanya kazi gani zaidi ya Utalii.
Wakiwa Dodoma ni wajumbe wa kamati za bunge ikiwemo ya serikali za mitaa.
Serikali za mitaa kwa mujibu wa Shivji si la muungano.
Wabunge wa znz wanapokwenda kukagua shughuli Kahama wanakwenda kufanya kazi ipi? Serikali za mitaa si suala la muungano. Maana yake huenda kutalii na ndio maana tunwaita Watalii.
Wakiwa Dodoma wanajadili suala la gesi Mtwara. Gesi na mafuta wamekimbia BLW kuyaondoa katika mambo ya muungano. Wanajadili gesi ya Tanganyika ili iweje? Si suala la muungano, hapo kama si Utalii ni kitu gani.
Wakiwa Dodoma wanataka pesa za elimu ya juu. Elimu ya juu si suala la muungano, ingawa Shivji amelificha kwasababu lina mafao kwao. Ple Dodoma wanaomba pesa zisizo zao. Huko znz mwanafunzi wa Tanganyika hapati udhamini, pesa za huko zinatoka JMT.
Mwaka jana wamekula bilioni 4, pamoja na wanafunzi 1,000 buree.
Watalii wakiwa Dodoma wanazungumzia uvuvi. Uvuvi si suala la muungano kwa mujibu wa Shivji. Kasema limeingizwa kinyemela na wznz wana haki ya kulifanya lao. Sasa Dodoma wanaongeleaje uvuvi wa Mwanza na Musoma kwa jambo lisilo la muungano. Huo kama si utalii ni kitu gani.
Wizara ya Afya si muungano. Wanapoongelea afya ya Mmachame au Mkirua inawahusu nini kama si utalii.
Bandari wamekimbia kuondoa, lakini wajumbe wa bodi ya bandari za Tanganyika miongoni mwao ni watalii. Wanaongelea bandari zipi ikiwa walishaondoa zao?
Mwaka jana wakadai pesa za radar zilizofisadiwa zigawanywe sawa ili ziende znz. Hoja ya watalii ni kuwa pesa zimetoka hazina Dar. Ina mantiki sana uh, wait a minute! Hapo hazina hawajachangia takribani miaka 10, sasa kama si Utalii ni kitu gani.
Nimalizie kwa kukuambia kuwa hata kama wamechaguliwa na watu 2,500 bado wana hadhi na haki sawa kama wabunge. Tunachotaka si kuwazuia kuja Dodoma, ni kuwaepusha kuzungumzia mambo yasiyowahusu kwasababu ni raia wa nchi ya znz(2010)
Na kwavile wanakuja kwa ajili ya znz basi gharama zao zilipwe na wale waliowatuma ambao ni wznz. Hilo litawezekana tukiweka mambo ya muungano sehemu moja na mengine kila mtu na lake kwa kupitia serikali 3. Wakija katika bunge la shirikisho kwa kulipwa na wananchi wao wana haki na hawatakuwa watalii.
Tofauti yao na Wajerumani kule Serengeti ni kuwa wajerumani wanaleta dollar, hawa watalii wa znz wanachukua hata kisicho chao.