Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Nakubaliana nawe, wala sijasema wabunge (Watalii) wa nchi jirani ni haramu, la hasha.Hata kama wamechaguliwa na watu 1,500 bado wana hadhi ya ubunge.
Kutokana na kuwa na katiba mbovu, znz inapata loophole za kutengeneza ajira kwa gharama za Tanganyika.
watalii hawana kauli znz, wala katika bunge la JMT, wana kazi gani?
Tukikubaliana waendelee kupunga upepo, hoja muhimu inabaki kuwa wametumwa na Zanzibar kwa masilhai ya Znz. Katiba imewapa uwezo wa 2/3 kukataa jambo. Gharama za authority ya 2/3 znz zinapaswa kulipwa na wazanzibar.
Pili, 2/3 kwa mujibu wa katiba ya JMT haiwapi nafasi kukagua shughuli za maendeleo. Kinadharia haki hiyo wanayo, kimantiki na kiakili hawana,wao ni 2/3 ya znz.
Pia hujaelewa wakiwa ndani ya bunge la JMT wanapewa 2/3 kwa niaba ya znz.
Wakirudi znz hawana nafasi ya kufanya shughuli za maendeleo.
Kama watafanya na kumwalika PM Pinda kufuatilia waliyokubaliana Dodoma, Pinda akiteremka znz hajulikani, itabidi aombe kibali cha kazi kama mzanzibar mkazi. Hivi huoni Utalii kweli!!!
Watalii wa znz wakiwa Dodoma wanaweza kupitisha jambo kwa 2/3 wakiwakilisha znz. Huko znz hawatambui (katiba ya mwaka 2010) inasema jambo hilo lipelekwe BLW,kama kuna mgongano katiba ya znz (2010) itakuwa juu.
Kwamba huko znz hawajui kama wana watu wenye nguvu ya 2/3.
Huo kama si Utalii, wewe unaweza kuiita kitu gani.
Hata hivyo una point, kutokana na mkanganyiko huo ni vema kutenga shughuli ili kila mmoja ajue anafanya nini. Leo huwezi kuingia BLW kutalii hata kwa bahati mbaya, vipi tukiwa na Tanganyika halafu tukawa na eneo la pamoja ambalo ni shirikisho.
Mkuu Nguruv3:
Mpaka sasa unashindwa kutetea hoja zako kwa kutumia vithibitisho vyenye nguvu na badala yake unatumia jaziba. Wabunge wa JMT wanatoka katika makundi mbalimbali. Kuna kundi la kutoka katika majimbo uchaguzi ya Tanganyika. Kuna kundi la kutoka majimbo ya uchaguzi wa Zanzibar. Kuna wabunge wa kuteuliwa na vyama vilivyopo bungeni. Kuna wa kuteuliwa na rais. Wabunge wote hawa wana haki sawa. Hivyo wabunge wa majimbo ya Tanganyika wanapodai Marupurupu, ongezeko la Marupurupu litawafikiwa wabunge wa makundi mengine pia.
Pili inaonyesha hujui miundo ya katiba inayotoa uwakilishaji wa minority. Kwa mfano nchini Marekani, kila jimbo linatoa senata wawili. Hawaii inatoa wawili ikiwa na watu nusu milioni na California inatoa wawili ikiwa na watu milioni 38. Hiyo 2/3 ni kuipa Znz sauti. Tukiungana na Malawi nao itabidi tuwape sauti vilevile. Hii ni sawa na kuwapa Hawaii senata wawili na California wawili. Kuna districts zimetengwa hili waMarekani weusi na waspanish wawe na wawakilishi.
Tatu sio kazi za wabunge kufanya shughuli za maendeleo. Wabunge ni watunga sheria. Je wabunge wa kuteuliwa wanafanya kazi gani za maendeleo? Tatizo la watanzania ni mazoea ya kuona wabunge wanarudi kwenye majimbo na kujichanganya na watu hili waonekane wanafanya kazi. Ukweli wa mambo hiyo sio kazi ya wabunge. Watu wanaotakiwa kufanya kazi za maendeleo ni executives kama mkuu wa mkoa au wilaya. Wabunge kazi yao ni kutunga sheria na kufanya check and balance. Hivyo wabunge waZnz kwenda Dodoma na kufanya shughuli za bunge, wanatimiza 100% ya kazi zao. Sio kazi ya mbunge kujenga sekondari.
Katiba ya Tanzania ina kasoro zake. Na kasoro zake sio gharama Tanganyika inayotumia kuendesha muungano. Hata kama Tanganyika na Zanzibar zitatengana, Tanganyika itaendelea kutumia the same amount of money to run her government. Hii ni sawa na serikali ya Marekani inayotumia 1% ya GDP yake katika masuala ya misaada kwa nchi masikini. Nchi ikiwa na matatizo ya kiuchumi kila mwanasiasa anadai kukata misaada ya nje. Misaada inakatwa na bado matatizo ya uchumi yapo palepale kwa sababu 1% is very close to 0%.