Nguruvi3 na Mchambuzi,
Wakuu zangu nimewasoma sana toka mwazo nikasema ngoja niwe msomajj tu kwa sababu wenzangu waliweza kuwapa darasa lakini hamkutaka kuelewa. Na nimejiuliza sana kwa nini inakuwa vigumu kwenu kuelewa hadi nimepata jibu. Tatizo lenu kubwa, kwanza ni kufikiria watu humu wanatetea muundpo wa serikali 2 dhidi ya serikali 3 kama vile muundo wa serikali 2 hauna mapungufu.
Na kama ingelikuwa hivyo ungewaona wasomi wengine wote humu wanaopingana na serikali3 wakitetea mazuri ya serikali 2 Kiuchumi lakini ukiwasoma kwa makini wamekuwa wakipinga tu hoja zetu kuhusiana na serikali 3, hivyo haiwafanyi wao kuwa watetezi wa serikali 2. Imefikia mahala kila mmoja wao kuwaeleza utetezi wake japo pia sii kweli kwamba wanakubaliana na kila kilichomo.
Turudi ktk hoja iliyopo Ubaoni. Sii kweli Zanzibar wanadhani wanayo haki zaidi katika mambo ya uchumi kuliko Tanganyika ama kweli ati Mtanganyika hana kauli kwa sababu yeye ni Mtanzania ambaye ndani yake yupo Mzanzibar. Hii umeipata kutoka wapi? maana Mtanganyika ndiye serikali kuu ya JMT na maamuzi yote yanaanza kwake.
Nitarudia kusema hao walosema Tanganyika inachangia kiasi fulani kwa Zanzibar siwaelewi kabisa ikiwa wao wenyewe wanakiri kuwa hili neno Tanzania lina Tanganyika na Zanzibar. Utawezaje kupima mchango wa watu walioungana kiasi kwamba kuna Wazanzibar wanaishi na kufanya kazi Tanganyika kwa uhamisho wa serikali au mashirika ya Umma kuwa hawa sii Wazanzibar bali Watanganyika.
Unaweza vipi kuitenganisha Tanganyika toka Tanzania ikiwa leo Bakhresa, Mzaanzibar anachangia kodi karibu 1/4 ya kodi zinzokusanywa mkoa wa Dar. Na kisha kuna Wazanzibar zaidi ya mil.2 huku Bara wakifanya kazi na biashara idadi ambayo ni kubwa kuliko wakazi wa Zanzibar kwenyewe.
Hivi kweli unaweza kunambia Mkoa wa Rukwa hauitaji fedha zaidi ili kuendelezwa kwa sababu tu ya mchango wake mdogo ktk mfuko wa Taifa? Na unaweza kunambia kweli ni akili nzuri kuiacha mikoa mlo orodhesha hapo juu kubakia chini kutokana na wao kuchangia kiasi kidogo ktk mfuko wa Taifa! Je, tukiwa na serikali 3 kuna fikra zozote za kuziendeleza mikoa hiyo ama tutabakia na mfumo huu wa serikali ambao umeikwaza mikoa hiyo kwa miaka 30 ilopita.
Tazama mkoa kama wa Mtwara wamegundua gas na pato lake linahamishiwa Dar, sasa hivi ili ugawaji wa umeme ufanyike toka mkoa wa Dar na kuongeza pato la mauzo na kodi zake wakati Mtwara ni njia panda tu (via). Je kulalamika kwa wana Mtwara kuhusiana na hilo ni makosa! Je Mtwara wakitaka kila pato la gas wakatiwe asilimia 40 ya kodi kwa sababu umezalishwa kwao serikali 3 watakubali?
Jamani matatizo yapo ktk mfumo mzima wa Kiutawala, jamaa kawaeleza vizuri kuhusu ukusanyaji kodi Scotland, ni vivyo hivyo uende Marekani au Canada. Kama Zanzibar wanataka pango zaidi haina maana wao wanadai haki zaidi ya Bara - Hapana ni sawa na wanawake wanapo omba mshahara sawa na wanaume haina maana wao wana haki zaidi yetu. Kinachotakiwa ni kutazama Zanzibar ina watu wangapi na kwa nini pato la mwananchi wa Zanzibar ni chini ya hata mwananchi wa Rukwa wakati nchi zetu zimeungana.
Usitazame fedha ngapi zimelipwa ila tumewawezeshaje Zanzibar kama nchi kupata maendeleo zaidi na kuongeza pato la Taifa maana kinachotakiwa ni kodi kutokuwa ktk mambo yasokuwa ya Muungano. Lazima asilimia kubwa ya kodi iende ktk mfuko wa JMT toka kila upande na asilimia ndogo ibakie ktk nchi husika, tena tunaweza shindana kisheria Zanzibar wakawa na Kodi ndogo zaidi ya Bara au vise verse.
Mfano Kodi ya nchi (Zanzibar) inaweza kuwa asilimia 10 ya mauzo na Kodi ya JMT ni asilimi 20 hivyo kila transaction ya kodi wanawajibika kulipa asilimia 30,na bara tukapitisha kodi ya asilimia 15 ya mauzo kuwa yetu na asilimia 20 ya JMT, hivyo tunalipia kodi asilimi 35 ya uwekezaji au transaction yoyote ya mauzo. Hivyo utaona ile asilimia 20 inabakia pale pale tunatofautiana tu kkodi za ndani ya nchi. Na hata kama Znz watakusanya Bil. 2 nasi tukakusanya Bil. 200 kinachotazamwa ni fedha hizo zitumike vipi kuendelea JMT na sii bara tuna Bil. 200 hizo ni zetu.
Utasemaje ati Bara hatuna sauti ikiwa Kati ya mawaziri wa serikali kuu na manaibu wake asilimi 90 wanatoka bara? na mambo yote ya maendeleo ya JMT hupitia mkono wao. Viongozi wengine woote hutega bakuli lao kuomba msaada. Mfumo wa serikali zetu unamfanya hata Mbunge aache kazi yake ya kutunga sheria awe mleta maendeleo na kupewa heshima wasostahili.
Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ni viongozi wawakilishi wa Rais aliyepo madarakani na sii lazima wawe wakazi ama wazawa wa sehemu hizo. Mwananchi hana sauti sehemu yoyote ya uongozi. Miaka miwili ama mitatu utasikia kahamishwa hata kama kaifanya kazi nzuri ktk wilaya au Mkoa huo. Yaani mfumo mzima wa kiutawala bado ni wa Ujima na hapa ndipo tunapolikoroga! Hii habari ya Zanzibar na matumizi makubwa ya Muungano ni habari za mitaani tu hakuna ukweli wala hatutaki ku learn kama vile imani ya dini. Ukizaliwa Mkristu/Muislaam ni vigumu sana kubadilisha imani yako hata kama kuna mambo yanakukwaza. Inatakiwa moyo wa kishujaa na kujaliwa UFAHAMU kukubali kubadilika.