Nguruvi3,
ningependa kuchangia katika maeneo kadhaa ya hoja zako hapo juu. Kama ulivyojadili mkuu
Nguruvi3, CCM ilikataa katakata kukubali wazo la katiba mpya na umejadili vizuri sana suala hili hivyo nisingependa kuingia kwa ndani sana; lakini ningependa kusema hivi, bearing in mind kwamba kuna uwezekano wa katiba ya 1977 kuendelea kutumika per scenarios ulizojadili hapo juu:
CCM walikuwa wanapinga hoja ya katiba mpya kwa hoja zifuatazo:
1. Katiba iliyopo (1977) ilikuwa properly adopted, mchakato ulifuata njia zote sahihi ambapo wawakilishi wa wananchi enacted the constitution, hivyo katiba hiyo ni legitimate na taifa halihitaji katiba mpya;
2.Serikali ya ccm imechaguliwa na wananchi na ni serikali halali kwahiyo hakuna haja ya kuwa na transitional government itakayosimamia mchakato wa katiba mpya kufuatia mageuzi ya kisiasa nchini;
3. Chama kilipinga mapendekezo ya national constitutional conferences kwa hoja kwamba such conferences are held only when kunakuwa na transfer of power kutoka kwa serikali ya mkoloni kwenda kwa serikali huru;
4. Pia ccm ilijenga hoja kwamba haja ya katiba mpya inakuja pale tu kama taifa lipo clearly divided into political groupings zenye strong support in the electorate suala ambalo linapelekea chama tawala kupoteza credibility;
Vyama vya siasa wakati ule (miaka ya mwanzo ya tisini) vikajibu hoja kwamba wao kama vyama vilivyosajiliwa vina wanachama ambao ni watanzania kama ilivyokuwa kwa ccm kwahiyo hata wao wana haki ya kushiriki katika kutengeneza katiba mpya ya nchi. Hoja nyingine ya upinzani ilikuwa kwamba - katiba iliyopo only carters for partisan interests (CCM) na sio national interests. Majibu ya CCM kwa hoja hii yakawa kwamba: suala la vyama vya upinzani kwamba na wao vinawakilisha matakwa ya wananchi kama ilivyo kwa wana ccm, suala hili litakuwa determine wakati wa chaguzi kuu ndani ya mfumo wa vyama vingi; kwahiyo vyama vya upinzani wajibu wao ni to walk the talk-to prove themselves kwenye sanduku la kura kama kweli vinaungwa mkono hivyo vinastahili kushirikishwa katika mchakato wa kutunga katiba mpya; CCM ikaenda mbali zaidi na kusema kwamba: usajili wa vyama husika unavitambua tu kama taasisi halali za kisiasa na ruksa kwa vyama hivi ni katika kujitengenezea sera zao, itikadi, establish their positions on various issues na kujipigia kampeni mbele ya umma; kitendo cha kuvisajili kama vyamma vya siasa, ccm argued further, doesn't necessarily mean kwamba vina haki ya kushiriki let alone kuwa consulted katika maamuzi muhimu ya kitaifa;
Hizi ndio zilikuwa ni hoja za msingi za CCM kwa miaka karibia 20 kabla ya Rais Kikwete kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya; validity of such arguments ni kitu that we can spare for later, lakini kwa sasa kilicho muhimu ni uwezekano wa taifa kuendelea na katiba ya sasa kwa hoja ya wana ccm kwamba ni katiba halali;
Kama nilivyojadili hapa and elsewhere, hoja juu ya legitimacy ya katiba ya JMT (1977) is full of fallacious (not true/accurate); hoja hii ni lazima ipingwe kwa nguvu zote na kwa ushahidi wote kwamba the 1977 Constitution isn't a people's constitution; at no point, katiba hii ilihusisha wananchi; katiba hii ilikuwa drafted na kamati ya chama (CCM), ikapata baaka za NEC-CCM, ikawa enacted na bunge la katiba lenye wajumbe walioteuliwa na rais, ambao literally walikuwa ni wana ccm wote; kati ya wajumbe 212, ni wajumbe 101 tu (chini ya nusu) walitokana na uchaguzi majimboni! Wengine wote waliteuliwa moja kwa moja kwenda kuwakilisha the interest of the "executive branch"; hakuna tofauti kubwa sana na kilichotokea katika mchakato wa sasa na
Nguruvi3 amejadili hili vyema; kwa kifupi, hata kwa standard za CCM tu, bunge lile wasn't a real representation of the people;
Tuseme basi hoja juu ya uhalali wa katiba ya 1977 inapita kwa kuzingatia mazingira ya wakati ule, hii haina maana kwamba taifa halihitaji katiba mpya; katiba mpya ni muhimu kama tunataka kuwa na a peaceful transition na kama tunataka kubakia na amani na utulivu; vinginevyo hatari za umwagaji wa damu na taifa kuwa categorically listed as a failed state ni dangers that are imminent;
Kobello katika mjadala wetu mwingine anasema hatari hizi hazipo;pengine ni kwa mtazamo huu, ccm inaendelea kujiamini kwamba inaweza kuendelea kuwaendesha wananchi kwa jinsi inavyotaka;
Iwapo ccm italazimisha turudi kwenye katiba ya 1977, ni muhimu itambue kwamba katiba ya sasa haifai in practice and in principle:
Kwanza, na hii ni on purely practical level, katiba ya sasa is unworkable! Hii ni kwa sababu, licha ya mapungufu tajwa hapo juu and elsewhere, katiba hii msingi wake ni nguzo kuu mbili: one party monopoly system and two government union structure. Nguzo zote hizi mbili no matter how much ccm is trying to hold, these two pillars are crumbling if not crumbled already; kama alivyojadili
Nguruvi3 hapa and elsewhere, chama na bunge lake vimekaa vikao vingi na kuunda tume kadhaa kujaribu kutatua mgogoro wa muungano bila mafanikio; ndio maana
Nguruvi3 anauliza, je haya maneno ya ccm kupitia
Nape Nnauye kwamba msimamo ni serikali mbili kwa nia ya kuboresha mfumo uliopo, ccm itakuja ni kipi kipya? Isitoshe, ccm ilishindwa wakati ule zanzibar bado ni sehemu ya JMT kwa mujibu wa katiba ya znz na ya JMT, lakini sasa znz ni moja ya nchi zinazounda JMT kwa mujibu wa katiba ya sasa ya znz; all in all, the ongoing crisis of the union should be (to any reasonable person) a sign that the 1977 constitution isn't workable;
Pili, ni katika suala la principle; katiba ya nchi isn't simply a legal document or technical document, bali its a "political document"; ili document hii ipate political legitimacy na istahili obedience and loyalty ya watawala na watawalwa, lazima iwe na national consensus (iridhiwe kitaifa), sio iridhiwe kichama (ccm) kama nape et al wanavyojaribu kulazimisha; katiba ambayo haina national consensus, moja kwa moja looses its political legitimacy;
MwanaDiwani,
Nape Nnauye,
Kobello and others of the same vein:
Katiba genuine ni ile yenye political legitimacy, kitu ambacho hakipo katika aina ya katiba mnayotaka kutulazimishia wananchi; katiba inayokosa political legitimacy kwa kawaida huwa imposed on the populace na hakuna mtu ambae huijali, both ruled and rulers alike; sasa ndugu zangu, pengine mnapojichanganya ni hapa:
Kuwa na katiba ya aina hii haina maana kwamba serikali ya ccm hasa miaka ya nyuma didn't have legitimacy kwa kutawala chini ya katiba ya 1977. Ukweli ni kwamba it had legitimacy lakini such legitimacy was derived from other sources, the source of its legitimacy wasn't the 1977 constitution; utawala wa chama kimoja wakati wa ujamaa ulikuwa na legitimacy iliyokuwa derived from:
1. Ujamaa
2. Historia ya harakati za uhuru.
3.Na kutoka kwa a popular and charismatic leader (Nyerere).
Je, yepi kati ya haya mnaweza kuyatumia kuhalalisha uhalali wenu wa kutawala chini ya katiba ya 1977 endapo hiyo ndio njama yenu?
Kumbukeni, kupitia sources hizi tatu za legitimacy chini ya Mwalimu, umma haukujali sana juu ya katiba na content yake na wengi hawakujali sana iwapo katiba ilikuwa inaheshimiwa au lah; lakini leo hii mazingira sio kama yale ya awali mnayojaribu kulazimisha:
*Historical legitimmacy ya TANU na ASP kama independent movements imeshachuja;
*hatuna tena charismmatic leaders ndani ya ccm;
*itikadi ya ujamaa imechinjiwa baharini na viongozi wa ccm (bila kushirikisha wanachama wake); maswali yanayofuatia ni je:
Karika hali hii, ni kitu gani kitatusaidia kuleta maridhiano ya kitaifa? Jibu ni katiba mpya ambayo inatokana na wananchi regardless of their political orientations and persuasions;
Je, ni kitu gani kitaleta uaminifu kwa upande wa watawala na upande watawalwa kwa taifa lao? Jibu ni hilo hilo hapo juu - yani Katiba Mpya;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums