Hizi serikali 2 kila Upande umezipata vipi maanake sikuelewi. Nachojua mimi tuna serikali 2 tu nazo n serikali ya Mapinduzi ya zanzibar na Serikali ya Muungano kama ilivyoelezwa ktk katiba ya Jamhuri ya Tanzania. Nje ya hapo inabidi inefahamishe vizuri maanake yaonyesha mattatizo tunayo sisi wananchi hatujui majukumu ya shghuli za serikali zote mbili. Kikatiba hakuna mambo ya serikali ya bara hakuna ila tumeyafanya yapo. Wabara wote ni Watanzania kwa uananchi na Uraia hakuna Ubara ila ktk misemo ya kutofautisha tu sehemu hizi mbili na sii kikatiba. Kama ndivyo Mzanzibara utamweka ktk kundi gani?Mkuu Mkandara, katika kujibu swali lako, naomba nikurudishe nyuma kidogo...hivi kwa kusema kweli mfumo tulio nao sasa ni wa serikali ngapi? Mimi naamini kiuhalisia tayari tunazo serikali tatu. Kwa nini nasema hivi? Kwa sababu kwa upande wa nchi ya Zanzibar kuna serikali mbili na kwa nchi ya Tanzania pia tunazo serikali mbili; sasa swali ni je, ndani ya hizi nchi mbili tuna jumla serikali ngapi? Kama tunazo serikali mbili nchini Tanzania, hizo serikali bila shaka moja inashughulikia mambo ya Muungano na nyingine inashughulikia mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) na kama nchi ya Zanzibar pia ina serikali mbili, ni wazi moja inashughulikia mambo ya Muungano na nyingine mambo ya Zanzibar. Je mpaka hapo niko sahihi?
Sasa basi kwa kuwa kuna mambo ya Tanzania bara, mambo ya Zanzibar na mambo ya Muungano, je kiuhalisia tunazo serikali ngapi? Ni kipi kipya kimeletwa na Rasimu ya Katiba kama ilivyosomwa na Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba kwa wajumbe wa Bunge la Katiba? Tunaye Kiongozi wa serikali bungeni ambaye eneo lake la kujidai linaishia Chumbe. Tunaye kiongozi wa serikali ndani ya Baraza la Wawakilishi ambaye eneo lake la kujidai halivuki bahari. Halafu tunayo serikali ambayo mamlaka yake hayana mpaka ndani ya Jamhuri, au nakosea? Si tumeaminishwa yapo mambo ya Muungano? Kwa kujibu swali lako; Naamini tayari tunazo serikali tatu ila kwa uhuni tu tukaamua kuziita mbili, sasa Rasimu inasema uhuni sasa basi! Koleo liitwe kwa jina lake! Uswahili sasa basi!
Muundo na taratibu za serikali 3 tayari tunao kwani Rasimu ya Jaji imewasha taa tuongee tukionana na siyo kuendelea kuendesha mambo gizani. Kwa kukaa gizani katiba ilivunjwa, hakuna aliyeweza kuona; uhaini ulifanywa, hakuna aliyeona na kukekemea; mambo ya kipuuzi hayakuhitaji kufumbiwa macho kwani giza nene tayari lilitamalaki mbele ya macho yetu. Rasimu imetuletea mwanga, waliozoea kufanya mambo gizani sasa wanajifungia kwenye semina wakipanga watakavyohujumu mwanga usiwamulike (masikini CCM!). Hapana Mkuu Mkandara, wamechelewa! It was just a matter of time and the right time has arrived, it is here and it wont go away that easily. Kikwete beware!
Tanganyika haipo, na hakuna mfuko wa Tanganyika hivyo hakuna mambo ya Tanganyika au bara, na ndio maana tunaitaka serikali ya 3 ili nayo ishughulikie mambo ya bara. Kama Tanganyika ipo basi bila shaka pia serikali yake pia ipo! sasa mnaitaka serikali ya 3 ni ipi hiyo? na ndipo hapo tunapokwaruzana na Wazanzibar. Tunapoiomba Tanganyika iwe na serikali ina maana hatujui kuwa gharama za kuiunda hiyo serikali zitatoka wapi kwa sababu mfuko wa fedha uliopo ni wa JMT.
Hivyo basi Ili Tanganyika iwe na serikali yake inabidi tuanze upya kuchagua kiongozi wa nchi (rais ama waziri kiongozi wetu),Wabunge na madiwani wa hii nchi Tanganyika ili rais au waziri mkuu huyo aunde serikali maana ktk hao wabunge ndio tutapata viongozi wa serikali yetu kama tutafuata mfumo wa zamani yaani mawaziri watatokana na Ubunge. Baada ya hapo ndipo tutaipata serikali ya Tanganyika. Hiyo sijii itakuwa lini tukianza kufikiri leo?
Sasa swali langu linakuja hivi, ni mfuko gani utakao gharamia kuundwa kwa hiyo serikali ya Tanganyika maana Tanganyika haina mfumo wake isipokuwa tuna mfuko wa Taifa na Zanzibar wanao wa kwao. Pili ni muda gani utachukua kufanya uchaguzi wa rais (waziri kiongozi),wabunge, madiwani wa nchi hii ya Tanganyika ili tupate kuunda serikali (wizara zake) ambazo hadi sasa hazifahamiki kutokana na kuwepo na kero za Muungano. Warioba na wasomi wametoa tu maoni yao kwa idadi ya wizara hizo lakini je washiriki wameafikiana kuwa na wizara hizo ktk shughuli za Muungano na zisizo za muungano? Na kama wameafiki tuneshindwa nini kuafikiana leo ktk mfumo huu kwani pingamizi liko wapi kama sio kero zennyewe?
Tatu, kutokana na pande zote mbili kutokubaliana na mamlaka ya mambo ya Muungano na yale yasiyokuwa ya muungano, hatuwezi kuunda serikali ya Tanganyika pasipo kumaliza tatizo hilo kwanza ili tukubaliane ni mambo gani yatakuwa ya Muungano na yapi hayatakuwa ya Muungano. Hapo ni sawa kabisa na kurudi nyuma hapa hapa tulipofikia leo, jana au mwaka jana. Hoja kubwa ilotuweka hapa kwa miaka 50 ni kero za Muungano. Sidhani kama itakuwa rahisi tena kufikia muafaka ktk mambo ya Muungano na yasokuwa ya Muungano.
Ama tuchukulie tumefikia muafaka sijui kwa kupitia bunge hili la katiba au bunge ka JMT au tume nyingine, binafsi sielewi ni muda gani swala hilo pekee litachukua na wala tusiliombee. Tukisha kubaliana ktk mambo yasokuwa ya Muungano hapo ndipo Tanganyika itaweza kutunga mimba kwa kuunda kwanza bunge lake, kisha serikali yake na mahakama yake na sielewi serikali ipi itagharamia uchaguzi huo - Tanganyika haina mfuko. (mfano ule wa Nassoro Moyo na embe 3 ktk mifuko miwili) Lakini kumbe hata kama leo tukifikia muafaka ktk maswala ya kero hizi za Muungano tunaweza kupata katiba mpya inayolenga mapungufu ya Kikatiba kulingana na mazingira tuliyopo maana tumeshamaliza kero zetu.
Kinachotuweka hapa na kukwama ni kutokubaliana mamlaka na shughuli za Muuungano na zile zisokuwa za muungano basi, hakuna kitu kingine hizi habari za kujitenga, Kuomba Uhuru na mamlaka kamili, kuunda serikali 3 ni hasira na majibu ya kijeuri kwa pande zote mbili pasipo kukaa chini na kuzitazama kwanza kero zenyewe kwa sababu huko mbele tutakutana nazo tena ili kuunda serikali ya JMT.
Nitarudia kusema kuunda serikali ya Tanganyika ni mbinu tu inatumiwa na wanasiasa kutufumba macho maana ukweli upo wazi kabisa ya kwamba hatukubaliani ktk mfumo mzima wa serikali 1,2 wala 3 kutokana na kero zilizopo. Tumalize kero kwanza japo wananchi wengi hawazijui isipokuwa wanasikizia tu magazetini na mitandaoni. Kero, kero, kero zimekuwa kero!
Last edited by a moderator: