Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #41
Haya ni marudio ya mambo tuliyojadili wiki 4 zilizopita.Sehemu ya IV
Wapinzani na wale waisokubaliana na mfumo wa sasa kwa idadi yao ni ngumu kupata 2/3 ya kuunga au kukataa mapendekezo. Nafasi waliyo nayo ni katika yafuatayo
1. Waungane kwa pamoja na liswepo kundi litakalounga mkono 'katiba ya mafichoni ya CCM'
2. Wasikubali majadiliano na serikali nje ya ukumbi wa bunge kuepuka kulaghaiwa tena
3. Watumie makundi machache yaliyobaki kuwavuta kwa hoja
4. Watumie ushawishi wa baadhi ya wanaCCM wanaoona lipo tatizo linalohitaji utaifa
5. Kuhakikisha maamuzi yanakuwa kwa kura za siri
Ufafanuzi;
-Kupoteza mpinzani hata mmoja ni pigo kwao kwasababu idadi yao inahitaji zaidi na si kupoteza
-Penye ugumu na rais atawaita kwa ahadi kama za siku za nyuma, wakiondoka mambo yanafanyika kinyume. Walikubaliana kutosainiwa mkataba, walipoondoka rais akasaini tena baada ya kusitisha maandamano. Hakuna ushahidi makubaliano na serikali yamewahi kufanyiwa kazi.
Kukubaliana na JK halafu kwenda kupingana na Lukuvi au Wasira ni kuamini kuwa JK na mawaziri wake ni vitu tofauti. Wakati huu lazima majadiliano yawe ya wazi na si juu ya glasi za juisi za maembe.
-Katika makundi yaliyopendekezwa yapo machache yanayoweza kuungana nao.
Wapinzani watumie fursa hiyo kuyavuta kwa hoja.
Mfano, waeleze ni kwanini serikali 3 zitapunguza gharama kwa takwimu.
Wahoji, ni kipi ambacho CCM haijakifanya kwa miaka 50 ambacho inataraji kufanya kuondoa kero.
Waoyeshe ni jinsi gani muungano ulivyotegemezi na matarajio ya siku za usoni
Na waonyeshe kwa namba na takwimu faida za serikali 3 ukilinganisha na 2.
-Ndani ya CCM si wote wanounga mkono serikali 2. Wapo wazee wenye ushawshi na uzoefu wanaoelewa matatizo ya muungano na kwamba imeshindikana hadi mbadala upatikane.
Mfano, viongozi hao wameachwa makusudi ili kutotibua dili linalopangwa nyuma ya pazia na rais na CCM.
Tunafahamu msimamo wa Warioba kupitia tume ni serikali 3.
Msimamo wa Malecela kupitia G55 ni serikali 3
Msimamo wa Msuya ni serikali 2 na msimamo wa Sumaye ni serikali 3.
Msimamo wa EL ni serikali 2 kupitia 'katiba ya mafichoni'
Viongozi hawa wana ushawishi wa makundi na viongozi wenzao kupitia uzoefu wao.
Japo wapo nje ya bunge (Kwasababu tu ya JK kutoona umuhimu wa utaifa) wapinzani wanaweza kuungwa mkono kupitia hao. Si rahisi lakini inaweza kusaidia kukabiliana na wingU zito la 'katiba ya CCM'
-CCM wanajipanga kumpata Spika atakayeendesha mambo kwa utaratibu 'wao'.
Katika kuhakikisha kila mmoja anakuwa na uhuru wa kuamua anachokiona ni sahihi bila kufungwa na minyororo ya chama maamuzi yawe kwa njia ya kura na si 'ndiyo' au hapana.
Kinyume chake mazingaombwe tunayoyaona bunge la JMT yataendelea.
Lakini pia kuwepo na utaratibu wa kuzungumza utakaotoa nafasi kwa pande muhimu za mjadiliano vinginevyo kutakuwa na kuchaguana kwa mpangilio ili kukidhi haja iliyokusudiwa ambayo sasa tunaiona ikiwa na mkono wa mwenyekiti wa CCM.
Kuna mwenzetu kaniuliza na bila shaka hataki kutambulika au kutambulishwa.
Swali ni, kwanini mjadala unahusu sana muungano? Je, katiba ni muungano tu bila mambo mengine?
Jibu ni kuwa makosa aliyofanya JK ya kuandika katiba bila kupata ridhaa na dira ya taifa ndiyo yanayotufikisha hapa. Ukifungua rasimu kuanzia kifungu cha kwanza hadi cha miwsho hutaweza kuvijadili hadi utakapokuwa na uhakika unajadili nini.
Kwa mfano, kifungu cha kwanza kabisa kinasema katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Swali linakuja, kuna ushahidi gani kuwa wananchi waliulizwa na kukubali muungano hadi neno hilo litumike.
Bunge la katiba litafanya makosa ya JK kama wakianza kujadili vifungu vya katiba kwanza.
Utajadili vipi vifungu bila kujua structure ya serikali unayokusudia?
Kuna kifungu gani ambacho hakigusi serikali. Na je, serikali inayoguswa ni ipi.
Hali iliyopo Dodoma inaashiria kutokuwepo kwa muafaka wa kitaifa.
Mtu wa kubeba lawama hizo ni Rais, kila jambo lilikuwa wazi kuanzia mwanzo. Maonyo yalitolewa kuhusu utaifa na si uchama.
Rais badala ya kuangalia utaifa amekjikita katika uchama.
Jana kaita kamati kuu ikaja na msimamo wa kushindilia kuhusu kura za wazi.
Ni kwanini CCM imekwama eneo hilo? Tujadili.
Huko nyuma tumeeleza dhana ya rais kuteka mchakato ilikuwa kudhibiti maoni ya wananchi kwa kutumia tume ya Warioba.
Kwa bahti nzuri na mbaya kutegemea upande uliopo tume imefanya kazi kutokana na matakwa ya wananchi. Hapo serikali ikakwama.
Njia ya pili ilikuwa kutumbukiza maoni kupitia mabaraza, nako imekwama.
Njia ya tatu ilikuwa rasimu mbadala nayo imeshatunguliwa kabla haijawasilishwa.
Njia ya nne ilikuwa kujaza wabunge wengi wa CCM kwa makundi yasiyo na maana kwa mfano wa malengo yanayofanana.
Kuchagua makada wa CCM kwa vigezo vya makundi. Nako wamekwama
Njia ya tano ni hii ya kura ya wazi inayowagawa wajumbe.
Kwanini CCM ina haha?
Jibu ni kuwa ndani ya CCM wapo wabunge walio tayari kusimamia masilahi ya nchi.Wapo waliochoshwa na ubabaishaji wa akina Nape na hao wapo tayari kusimama na kuitetea nchi yao dhidi ya uhuni uliokithiri wa CCM.
Ili kuwafunga mikono na midomo CCM inataka kura ya wazi kama kigezo cha kuwatambua. Wamekuja na njia ya kusema watakaokiuka maagizo wataanyang'anywa kadi.
Katika mchezo huo mchafu CCM wamemrubuni mwenyekiti wa BMLK aingie katika vikao vyao akijua wazi hapaswi kuchukua upande.
Huko alikwenda kupewa maagizo ya nini kifanyike ili katiba wanayoitaka CCM itimie. Ndivyo watakavyofanya kama wakifananikiwa kuvuka vikwazo, kwamba wanataka maoni yao na si ya wananchi.
Kuna mambo mawili yaliyopo mbele.
Bunge kuvunjika kabla ya wakati na bila muafaka. Hali ilipofikia inaweza kuwafikisha wabunge wa CCM wenye uzalendo kusema liwalo na liwe nchi kwanza CCM baadaye. Hapo CCM itaanza safari ya kulekea kule UNIP na KANU walipo.
Au, CCM watafanikiwa kufanikisha mambo yao kwa njia za hila.
Haitachukua muda suala la Tanganyika litarudi upya kwa kupitia wabunge wa kama ilivyokuwa kwa G55 na safari hii kwa nguvu zote tena wajumbe wakiwa wengi zaidi.
Tatu, kuna uwezekano wajumbe wa znz wakaamua kuondoka na kuwaacha wachache. Hadi sasa CCM znz ndiyo imegawanyika kuliko bara na hakuna namna ya kuziba ufa uliopo. Hilo likitokea basi muungano utakuwa umehitimishwa haraka sana.
Kwa hali yoyote iwavyo hadi sasa CCM wana wakati mgumu kwa wakati huu na siku za mbeleni.
Ni dhahiri kukwama kwa bunge ni matokeo ya CCM kushinikiza hoja zao na si za wananchi. Hapa maana yake ni kuwa wapinzani na wale wasio na makundi wanazidi kuungwa mkono na wananchi.
CCM wanaweza kutoliona hili mapema lakini mbele ya safari linagharama kubwa.
Njia ya kura ya wazi nayo pia ni mwiba siku zaijazo.
Wanachokifanya ni kuwa expose wabunge kinyume na matakwa yao.
Wananchi wataona nani alikuwa upande wa CCM bila kujali nini ilikuwa dhamira yake.Adhabu itatolewa si kwa CCM bali kwa mbunge binafsi kutokana na kura yake kwa maana kuwa alishiriki uhuni wa CCM.
Adhabu hizo zitawanufaisha sana wapinzani kama watajipanga. Ni silaha nzuri mbele ya safari ya kuwaelezea wagombea wa CCM kama wasaliti wa umma.
Vyovyote iwavyo CCM ipo katika wakati mgumu sana na kifo chake kinaweza kutokea mikononi mwa JK.
Inaweza isiwe kifo cha kupelekwa kaburini lakini kifo cha CCM kupelekwa nyumba ya kuhifadhi wafu kinaonekana dhahiri kama KANUna UNIP
Watatumia ubabe lakini itakula kwao. Hadi sasa ni CCM dhidi ya wananchi na sijui lini nguvu ya umma iliwahi kushindwa na dola au chama cha siasa.
Labda CCM watakuwa wa kwanza kutudhihirishia hilo!
Tusemezane