Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

WIKI KATIKA MTAZAMO

Kuna mambo yametokea wiki hii yenye utata kuhusiana na utawala mpya

Vyombo vya habari: Katika mkutano wa CPAC, Trump alishambulia media kama kawaida
Hoja ni media zitaje source za habari kinyume na uandishi unaotaka source kulindwa

Kabla na baada ya kampeni, Trump amekaririwa baadhi ya sehemu akitaja neno 'source' bila majina, mfano, aliwahi kusema 'source' zake zimemeweleza Obama si Raia wa US

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya vyombo vya habari vilizuiwa kuingia katika mkutano wa waandishi. Mwaka jana Trump hakuhudhuria mkutano huo

Trump kasema hatahudhuria tafrija ya waandishi 'media gala' unaofanyika kila mwaka
Gala ni mkusanyiko wa kijamii tu na si sehemu ya habari, ni wakati wa utani na mizaha

Trump amelalamikia leak ya habari wakati akiita habari za media ni phony na fake
Inakuwaje leak zinazojadiliwa na media ziwe za kweli na mjadala uwe fake?

Mtifuano na media umeendelea kama 'mbinu' ya kufunika habari za maafisa na Russia
Gazeti moja limetoa taarifa kuhusu uhusika wa maafisa na wa Russia katika uchaguzi

Inte community ilishasema Russia wanahusika. Kinachoendelea ni nani walishirikiana nao

WH iliita maafisa wa FBI kuwashawishi wapuuze taarifa na kutoendelea na uchunguzi
WH pia imewasiliana na kamati ya bunge katika kuzuia habari hizo zisifanyiwa kazi

Ilikuwaje FBI wakakutana na WH wakati uchunguzi unaendelea?
Je, hili halikumbushi Lynch alipokutana na Bill uwanja wa ndege na kuwa 'agenda'?

Kwanini WH inajitahidi kuzuia uchunguzi ikiwa hakuna aliyehusika kutoka kampeni?
Kwanini FBI walitoa taarifa hawakubali kusitisha uchunguzi kama ilivyoombwa na WH?

Kama mtakumbuka wakati wa kampeni tulisema mbinu ya kuingiza 'jambo' ili kuondoa watu katika mijadala ilifanikiwa sana,kwa sasa ni ngumu ni utawala kuna macho mengi

Media zimetambua mashambulizi dhidi yao ni 'distractions' hasa kwa hili la Russia
Inaonekana media zimeanza kupuuza na kutilia mkazo suala zima la Russia na wahusika

Ipo hoja ya kuunda kamati huru ya uchunguzi au mchunguzi huru 'special prosecutor'
Hili ni baada ya kutilia shaka maafisa DOJ na FBI hakuwezi kutoa hali halisi

Katika 'state of Union' Trump anatarajiwa kuongelea Obamacare ili kuleta distractions
Tatizo ni Obamacare ni tatizo wanalokumbana nalo wabunge na maseneta wa GOP

Na wala Obamacare haiwezi kufunika Russia,tayari mgogoro na media unachagiza kutafuta ukweli. Trump akisema media na news ni fake, media zikitaka ku prove si fake

Wakati huo huo kuna 'kaugomvi' na IC ambako habari zinavuja huenda kwa makusudi

Tusemezane
 
US President Donald Trump has said he believes Barack Obama is behind the protests against Republican lawmakers, and national security leaks.

He told Fox News: "I think President Obama's behind it because his people are certainly behind it", but added: "I also think it's just politics".

Source: BBC
Trump says Obama behind leaks - CNNPolitics.com
Original source: Fox News.
=============
Haya yote Obama Kajitakia, kitendo cha kushindwa kukaa kimya baada ya kumkabidhi mwenzake mamlaka lazima kimgharimu.
 
Haya yote Obama Kajitakia, kitendo cha kushindwa kukaa kimya baada ya kumkabidhi mwenzake mamlaka lazima kimgharimu.
Mkuu kwani Obama amesema nini?
George Bush kasema nini? Na jana Trump kasema nini kuhusu Obamacare?
 
Mkuu kwani Obama amesema nini?
George Bush kasema nini? Na jana Trump kasema nini kuhusu Obamacare?
Bush alimfanyia hivi Obama, na Obama amemfanyia hivi Trump
========
By Kelly Riddell - The Washington Times - Monday, January 30, 2017

President George W. Bush stayed out of President Barack Obama’s business for the eight years Mr. Obama ruled the country. It took a little more than one week for Mr. Obama to criticize President Donald Trump.

Through his spokesman, Mr. Obama said he was “heartened” by all of the anti-Trump protests that have erupted throughout the nation.

“President Obama is heartened by the level of engagement taking place in communities around the country. In his final official speech as president, he spoke about the important role of citizen and how all Americans have a responsibility to be the guardians of our democracy — not just during an election but every day,” Kevin Lewis, Mr. Obama’s spokesman, told The Hill Monday.

“Citizens exercising their Constitutional right to assemble, organize and have their voices heard by their elected officials is exactly what we expect to see when American values are at stake,” Mr. Lewis told the Hill
====
Obama criticizes Trump a little more than one week after leaving office
Obama, in a rare move for an ex-president, breaks silence to criticize Trump on immigration
 
Mkuu TUJITEGEMEE

Kama utakumbuka tuliwahi kusema Obama alitoa kauli baada ya rekodi yake kupotoshwa Kwa mfano, suala la visa, Obama hakuzuia visa, alichofanya ni 'extreme vetting' .

Baada ya kusemwa alizuia nchi 7 kitu ambacho si kweli alizungumza

Lengo lake lilikuwa kuweka rekodi sawa, na baada ya hapo Trump admin imeacha
Utakumbuka tulisema alituma salam kuwa upotoshaji hautavumiliwa

Jana, sijui kama uliangalia news, G.Bush alizungumzia mambo mengi katika interview
Moja ya mambo aliyozungumzia ni kuhusu Russia na kuzuiwa kwa media

Kwa Russia alisema 'wamarekani wanapaswa kujua ukweli kuhusu Trump adm na Russia'
Kuhusu media alisema inasaidia katika demokrasia kwasababu power is addictive and corrosive , ni lazima kuwe na media za kuweka mizania

Jana hiyo hiyo Trump alisema hakujua suala la Healthcare ni 'complicated' kiasi hicho
Alikuwa anaongelea repeal and replace Obamacare na viongozi wa senate na house

Trump aliyesema atafuta Obamacare siku ya kwanza sasa anakiri hakujua ni complicated. Hii maana yake alikuwa anazungumza bila kujua ugumu wake

Nilikusoma hapo nyuma ukieleza mkutano wa CPAC na Obamacare.
Ulitaka kueleza Obamacare atafuta,tulikaa kimya kwasababu tulijua ni complicated

Hapa Jamvini tulijadili kwa mitazamo tofauti siku za nyuma.
Wapo waliovutika na kusema atafuta na kalamu na walionukuu alilosema bila kuchuja.

Waliofanya tathmini wana la kusema leo kwasababu Trump amekiri ni complicated

Unapochukua kauli Obama yupo nyuma bila evidence kwakweli humuelewi Rais Huyo. Jiulize, Obama alikuwa na wafuasi, atawazuiaje wanapotaka kufanya mambo yao?

Trump alisema 'Russia waendelee na hacking ya Clinton' na ndiye leo anawasachi wafanyakazi wa WH simu zao kwa Leak

Trump alisema hana Imani na Intel comm, leo asema IC zimesema jambo abcd.

Aliyesema hatapeleka majeshi nje kulinda,unajua kuna 30,000 askari wanaelekea Syria?

Mkuu maswali niliyokuuliza hayahusiani na ulichojibu, bali habari za 24 hrs

Ukipata habari ni vema ukaziangalia kwa mtazamo mpana si wa mwandishi tu
 
Haya yote Obama Kajitakia, kitendo cha kushindwa kukaa kimya baada ya kumkabidhi mwenzake mamlaka lazima kimgharimu.
Kuna sera ya 'one president at a time'
kwamba Rais ni yule aliyeko madarakani hadi siku anaapishwa mwingine

Najaribu kuangalia unachosema nikiwaza kidogo.

Obama alizungumza alipotoka madarakani

Unasahau siku aliyoiwekea Russia vikwazo, M. Flynn ambaye alikuwa mshauri wa ulinzi wa Trump alizungumza kwa simu na Balozi wa Russia kuhusu vikwazo

Hii ilikuwa kinyume na taratibu za 'one president...'.
Kwamba Obama akiwa ofisini Trump na team walikuwa wanamwendea kinyume

Vipi uliweza kuona Obama akizungumza baada ya kukabidhi ofisi ni jambo baya na usiweze kuliona la Trump na Flynn wakati Obama akiwa madarakani?
 
....

Unasahau siku aliyoiwekea Russia vikwazo, M. Flynn ambaye alikuwa mshauri wa ulinzi wa Trump alizungumza kwa simu na Balozi wa Russia kuhusu vikwazo

...
Kipindi kile sidhani kama Flynn alikuwa mpiga kampeni rasmi (official) wa Trump zaidi ya kujitokeza kumuunga mkono kwa utashi wake (kama kumbukumbu zangu ziko sahihi). Kama angekuwa ni kampeni meneja wa Trump, hoja yako ingekuwa na nguvu zaidi, maana Lewis ni msemaji rasmi wa Mr. Obama.
 
Kipindi kile sidhani kama Flynn alikuwa mpiga kampeni rasmi (official) wa Trump zaidi ya kujitokeza kumuunga mkono kwa utashi wake (kama kumbukumbu zangu ziko sahihi). Kama angekuwa ni kampeni meneja wa Trump, hoja yako ingekuwa na nguvu zaidi, maana Lewis ni msemaji rasmi wa Mr. Obama.
Kwanini alijiuzulu?
 
Kuna sera ya 'one president at a time'
kwamba Rais ni yule aliyeko madarakani hadi siku anaapishwa mwingine

Najaribu kuangalia unachosema nikiwaza kidogo.

Obama alizungumza alipotoka madarakani

Unasahau siku aliyoiwekea Russia vikwazo, M. Flynn ambaye alikuwa mshauri wa ulinzi wa Trump alizungumza kwa simu na Balozi wa Russia kuhusu vikwazo

Hii ilikuwa kinyume na taratibu za 'one president...'.
Kwamba Obama akiwa ofisini Trump na team walikuwa wanamwendea kinyume

Vipi uliweza kuona Obama akizungumza baada ya kukabidhi ofisi ni jambo baya na usiweze kuliona la Trump na Flynn wakati Obama akiwa madarakani?
Mkuu nguruvi, Mimi nimeamua kukaa kimya kwani nilifikiri katika hii mada tunapashana Tu habari kwa jinsi tunavyotofautina katika kuijiua Marekani kupitia sources mbalimbali.

Mara wengine tukajikuta tunashambuliwa kwa kupotosha mambo kwa vile tu eti mpenzi wetu Clinton kashindwa! Kwa sasa mengi tulioonya na kuyatabiri tayari yanatokea.

Hii ya trump kujaribu kumuingiza Obama wakati mambo yanamwendea kombo ni sawa na jitihada za mfa maji. Tuzidi kuvuta subira...Marekani Ni zaidi ya tunavyodhani.
 
Mkuu nguruvi, Mimi nimeamua kukaa kimya .
Mwalimu Mag3,
Salaam,

Mwalimu ukikaa kimya wakati kuna jambo la muhimu, unashusha morari ya wanafunzi wako. Ebu angalia idadi ya wanaosoma uzi huu uone kama ni sawa na wanaosoma na kuchangia. Somaji tu ni wengi...maana wengi tuna kuja kuchota maarifa hapa (ni wanafunzi wasaka elimu). Mwalimu, unajua udhaifu wetu sisi wanafunzi wa JF, hatuna namna ya kukulazimisha utufundishe. Tafadhali usitumie udhaifu wetu huu kutuadhibu kwa kukaa kimya bila kushusha 'nondo' za maarifa. Wanafunzi wa sampuli ingine (huko uraiani sijui wanajitambua ama la) wangeandamana, ama kufanya migomo na uharibifu wa mali za shule. Na wengine ambao nina uhakika hawajitambui wangeshangilia kwa mwalimu kutooneka darasani...! Wanafunzi wa hapa JF tuna adabu na tunajitambua, japo kuna baadhi yetu huwa tunateleza kwenye kauli, tunahitaji elimu. Usikae kimya mwalimu.

-Mwanafunzi mtiifu
TUJITEGEMEE
 
Kwanini alijiuzulu?
Leo mwalimu quiz zako mbona za kushtukiza ?
-----------------------------------------------------------------


Michael T. Flynn, the national security adviser, resigned on Monday night after it was revealed that he had misled Vice President Mike Pence and other top White House officials about his conversations with the Russian ambassador to the United States, according to a person close to the Trump administration.
Flynn Resigns
====
Mwalimu unaona, kumbe Flynn 'ameadhibiwa' kwa kosa ambalo amelitenda tayari Donald Trump ni rais. Flynn alimuongopea Makamu wa rais juu ya issue zake za huko nyuma. Hivyo, nadhani Obama anakosa kwa kuingilia utawala wa mwenzake.
 
Mwalimu unaona, kumbe Flynn 'ameadhibiwa' kwa kosa ambalo amelitenda tayari Donald Trump ni rais. Flynn alimuongopea Makamu wa rais juu ya issue zake za huko nyuma. Hivyo, nadhani Obama anakosa kwa kuingilia utawala wa mwenzake.
Kuna mambo mawili hapa.

Kujiuzulu kwa Flynn kulifanyika makusudi na kwa kiasi kumefanikiwa kama tunavyokusoma

1. Hoja ilibadilishwa kuwa amemdanganya Makamu wa Rais.
Hiyo si hoja ya msingi. Imetumika kuhalilisha kujiuzulu kwake ili kuepusha yafutayo

2. Kwamba, kama alizungumza ni katika capacity gani. Kuna sheria Logan act

''Summary The Logan Act, codified at 18 U.S.C. § 953, states: Any citizen of the United States, wherever he may be, who, without authority of the United States, directly or indirectly commences or carries on any correspondence or intercourse with any foreign government or any officer or agent thereof, in relation to any disputes or controversies with the United States, or to defeat the measures of the United States, shall be fined under this title or imprisoned not more than three years, or both.....

3. Namba 2 ingemlazimisha Flynn ima kushtakiwa au kusema nani kamtuma

4. Hapo kwa nani alimtuma ndipo pangegusa kampeni ambapo Trump angeweza kuwa testified. Zaidi, uhusiano wake na Russia ambao hadi sasa una mashaka ungekuwa wazi

Kwa mantiki hii, hoja ilifunikwa kwa kumtumia makamu wa Rais.

Kumdanya makamu ni suala moja, kuzungumza na balozi ni suala jingine na kuzungumza kukiwa na Rais madarakani ni jingine

Kuhusu Obama kuzungumza, utaratibu unamtaka mstaafu kutozungumzia sera za aliyempokea kwa kukosoa au vinginevyo. Utaratibu huo hauwazuii viongozi kuzungumza

Ndiyo maana Bush jana kaenda mbali kukosoa sera za Trump hakuna anayeona ni tatizo. Nimeeleza kilichomsukuma Obama ni kupotoshwa alichofanya ili ku cover udhaifu uliojitokeza

Obama akatuma salamu kuwa ana uwezo wa kuweka rekodi sawa na ikawa tatizo
Kuanzia muda huo hakuna katika timu ya Trump aliyezungumza kinyume tena

Lakini pia uelewe, Obama kama marais wengine watakuwa na shughuli zao na hawazuiliwi kuzungumza kama unavyoamini. Jimmy Carter alimkosoa sana Bush kuhusu middle East

Bill anaitwa kuongea katika mikutano ya dunia kama ambavyo Obama ataitwa
Ni muhimu kuelewa haya mambo yana play vipi
 
Mkuu nguruvi,
Hii ya trump kujaribu kumuingiza Obama wakati mambo yanamwendea kombo ni sawa na jitihada za mfa maji. Tuzidi kuvuta subira...Marekani Ni zaidi ya tunavyodhani.
Mkuu mbinu hiyo wameitumia na hata sasa wanaitumia kuhusu Russia

Kama unakumbuka kiongozi wa House commitee Nunes anasema wameambiwa hakuna lolote kuhusiana na Russia na Trump kufutia habari za Washing Post

Waandishi wanahoji ni kwa investigation iliyofanywa hadi kufikia conclusions?
Wapo kama Dem na GOP wanaotaka independent investigators

WH wanafanya taarifa ya W.Post kama ndilo tatizo, lakini wanabwanwa zaidi waeleze uhusiano wa Russia na WH, wakati wa kampeni n.k.

Katika kuhakikisha wanafunika udhaifu wanasema investigation ianzie kwa Obama, lini alijua na hatua gani alichukua. Tayari wanabadili maongezi na kuficha hoja

Kwa US, magazeti yana info na yanajua wakati gani wa kuzitoa.
Hata iweje ipo siku suala zima litakuwa wazi au kama halipo halitaongelewa tena

Kwa US hakuna habari inayokufa kifo kwa kuzuiliwa tu kama WH wanavyojitahidi sasa
 
Mkuu mbinu hiyo wameitumia na hata sasa wanaitumia kuhusu Russia

Kama unakumbuka kiongozi wa House commitee Nunes anasema wameambiwa hakuna lolote kuhusiana na Russia na Trump kufutia habari za Washing Post

Waandishi wanahoji ni kwa investigation iliyofanywa hadi kufikia conclusions?
Wapo kama Dem na GOP wanaotaka independent investigators

WH wanafanya taarifa ya W.Post kama ndilo tatizo, lakini wanabwanwa zaidi waeleze uhusiano wa Russia na WH, wakati wa kampeni n.k.

Katika kuhakikisha wanafunika udhaifu wanasema investigation ianzie kwa Obama, lini alijua na hatua gani alichukua. Tayari wanabadili maongezi na kuficha hoja

Kwa US, magazeti yana info na yanajua wakati gani wa kuzitoa.
Hata iweje ipo siku suala zima litakuwa wazi au kama halipo halitaongelewa tena

Kwa US hakuna habari inayokufa kifo kwa kuzuiliwa tu kama WH wanavyojitahidi sasa
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa yako mambo ambayo yanasubiri wakati muafaka tu yatolewe na kinachofanyika sasa ni ama kumpa kamba mtu arahisishe kujinyonga. Marekani watu hawakurupuki na wakimpata mtu anayekurupuka kama huyu waliyempata, watampa nafasi za kutosha azidi kujitundika kamba shingoni. Yapo maswali anaulizwa na yeye kwa tabia zake hutoa majibu ya haraka haraka bila kujiuliza ipasavyo kwa nini anaulizwa maswali kama hayo.

Mfano moja ni juzi alipofyatuka kwa kujitetea kwamba hajawahi kuwa na mawasiliano wala uhusiano wa moja kwa moja na viongozi wa Urusi kwa muda wa miaka kumi na hiyo imeshaingia kwenye daftari. Siku daftari ikijaa kiberiti kitawashwa na moto wake unaweza kuwaunguza waliomo na wasiokuwemo. Mfano mwingine ni pale alipojaribu kumhusisha Obama na shambulio lililofanyika nchini Yemen na sasa babake askari aliyepoteza maisha anadai maelezo zaidi.

Kwamba Obama aliweza kumaliza miaka yake minane huku wamarekani walio wengi wakiwa bado wana imani naye ni jambo ambalo kwa Trump litakuwa ni tatizo sana. Ingawa juhudi zinafanyika kufuta legacy ya Obama lakini hii tuhuma ya kujaribu kumhusisha na Leaks ndani ya WH zinaweza kumuathiri anayezitoa kuliko anayetuhumiwa. Naona muda huu Rais mpya amesign EO za kufanya review za regulations zote alizoweka Obama kwa mambo mbalimbali.

Swali ni kwa nini anataka review na asitumie madaraka yake kuzifuta tu kama alivyoahidi...tuvute subira.
 
"Mag3, post: 19928837, member: 10873"]Niliwahi kusema huko nyuma kuwa yako mambo ambayo yanasubiri wakati muafaka tu yatolewe na kinachofanyika sasa ni ama kumpa kamba mtu arahisishe kujinyonga. Marekani watu hawakurupuki
Washington Post wamekaa kimya kana kwamba walindika 'fake'
Ipo siku habari zitaibuka tu. Emails za Clinton hazikuwafunza jambo!
Sasa hivi tax return aliyosema ipo katika audit imemalizika harak. Kwanini!
Ni katika kuziba excuse ndiyo maana unaona suala la tax linarudi kwa kasi
Yapo maswali anaulizwa na yeye kwa tabia zake hutoa majibu ya haraka haraka bila kujiuliza ipasavyo kwa nini anaulizwa maswali kama hayo.
Obamacare ataifuta siku ya kwanza ilikuwa kauli ya kukurupuka. Jana kasema hakujua ni so complicated kiasi hicho
Mfano mwingine ni pale alipojaribu kumhusisha Obama na shambulio lililofanyika nchini Yemen na sasa babake askari aliyepoteza maisha anadai maelezo zaidi.
Taarifa za kwanza za WH, Trump ameidhinisha shambiulio la kwanza Yemen
Taarifa ya pili kutoka kwa Sean Spicer, shambulio lilikuwa successful na wamekusanya information nyingi sana

Baada ya watu kuhoji ilikuwaje navy seal akafariki na kwanini ni successful, kibao kikabadilika ulikuwa mpango wa Obama. Walisahau Obama alishakabidhi WH likifanyika
Naona muda huu Rais mpya amesign EO za kufanya review za regulations zote alizoweka Obama kwa mambo mbalimbali.

Swali ni kwa nini anataka review na asitumie madaraka yake kuzifuta tu kama alivyoahidi...tuvute subira
Obamacare ni mfano mzuri wa jinsi sheria zilivyo complicated na zililivowekwa kwa ufundi.

Republican baadhi wanasema Obamacare iwe improved, wengine isiguswe, na wale wanaosema repeal and replace hawana mbadala. Siyo tatizo la Dem tena

Kuna Dodd Frank anayo 'scrap' kidogo kidogo.
In the end atakuwa amejifungamanisha na wall street aliowalaani.

Kampeni inayokuja itakuwa issue

Lakini je, recession ilyosababisha Dodd Frank kuandikwa imekwisha na haitarudia tena?
 
Breaking news!

Kuna tetesi kwamba Rais Donald Trump baada ya kuona hali isiyo salama mbele ya safari akiendeleza msimamo wake wa awali, anaweza akawashangaza wengi kwenye hotuba yake inayosubiriwa kuanza baada ya saa moja hivi kutoka sasa. Anaweza akapiga about turn katika msimamo wake utakaowashangaza na kuwaacha wapenzi wake wengi midomo wazi kuhusiana na mambo makuu manne ambayo ni uhamiaji, matibabu, kodi na mahusiano na mataifa mengine. Hivyo tununue pop corn zetu tukae tayari kumsikiliza na tusishangae kuona analegeza msimamo wake ikilinganishwa na ule wa wakati wa kampeni.
 
Dakika yoyote sasa Trump ataanza kutoa hotuba yake...naam huyo anapanda jukwaani. Ameanza...

Je tetesi zangu zitakuwa kweli au Donald atabakia yule yule WA kampeni? Tuendelee kusubiri...
 
Naona Donald Trump ameamua kukomaa na kukataa ushauri alopewa. Inasemekana hiyo ndiyo ilisababisha hotuba yake kuchelewa kwa kiasi Fulani.

Kwa hotuba yake hii nadhani njiani ataendelea kukwaa visiki...haya Ni maoni yangu Tu ndugu zangu na niko tayari kukosolewa.
 
Breaking news!

Kuna tetesi kwamba Rais Donald Trump baada ya kuona hali isiyo salama mbele ya safari akiendeleza msimamo wake wa awali, anaweza akawashangaza wengi kwenye hotuba yake inayosubiriwa kuanza baada ya saa moja hivi kutoka sasa.

Anaweza akapiga about turn katika msimamo wake utakaowashangaza na kuwaacha wapenzi wake wengi midomo wazi kuhusiana na mambo makuu manne

uhamiaji, matibabu, kodi na mahusiano na mataifa mengine. Hivyo tununue pop corn zetu tukae tayari kumsikiliza na tusishangae kuona analegeza msimamo wake ikilinganishwa na ule wa wakati wa kampeni.
Baada ya kumaliza hotuba tupitie baadhi ya hoja ikiwemo mambo 4 tuliyonukuu

Ameanza hotuba kwa kutambua black history month na anti-semetic akilaani chuki dhidi ya Jews
Kwa mara ya kwanza mbele ya Taifa lake amelaani vitendo hivyo kwa kauli kali

Hapa alitaka kuwafikia watu weusi baada ya kushindwa kufanya hivyo katika siku iliyokuwa rasmi
Alitaka kuwahakikishia Jews wanaomuona kama kiongozi wa 'ubaguzi' kwamba yupo nao

Tone yake ilikuwa nzuri ukilinganisha na hotuba ya kwanza siku ya kutawazwa

Hili ni jema kwa wale waliokuwa na hofu kuhusu kauli zake za kila siku.
Hata hivyo, kwa wale wanaomjua na waliokuwa na shaka, kuna la kujiuliza. Je alikuwa yeye?

2. Hotuba ilikuwa ya America na mambo ya ajira zaidi. Ameongelea kuhusu infrastructure na kuomba zaidi ya Tri 1. Hili la Infrastructure litaleta ajira kama Congress itapitisha kiasi hicho

Kuna hoja ya wapi pesa zitapatikana ikiwa ameahidi tax cut kwa corporate

Hapa atakuwa amewagusa conservative, spending na debt si sera yao
Katika congress kutakuwa na mgawanyiko kwa Republican huku Dems wakitaka chanzo cha pesa

3. Uhamiaji: Ile kauli ya kujenga ukuta wa Me alichoongelea zaidi ni ku secure border
Baada ya Mexico kuonyesha 'makucha' na kwa kutambua umuhimu wake, kauli ya ukuta ilikuwa soft kidogo kuliko ilivyokuwa siku za nyuma

3. Islamic terroist: Hili limeleta mjadala, mawaziri kama Gen. Mattis wakimtaka asilitumie kwa maana ya kuleta picha mbaya na jumuiya ya waislam na hivyo kuweka masilahi ya US katika wakati mgumu

Trump alitumia neno hilo, si kwa bahati mbaya bali kuwafikia wafuasi wake wanaopenda kulisikia
Swali linabaki, kauli hiyo ita play vipi katika muslim world?

Kodi: Ametanga kupunguza kodi kwa mashirika ili yaweze kushindana katika soko la dunia
Anasema hilo litasaidi makampuni kutoondoka na kuwekeza Marekani hivyo kutoa ajira

Endapo atafanikiwa kwa hili, ajira zitakuwepo tena nzuri. Changamoto ni kuwa makampuni yanataka faida. Gharama za uzalishaji itabidi zipunguzwe ili kumudu ushindani. Je, makampuni yakifanya kazi za automation ajira zitatoka wapi?

Obamacare: Hili amelirudisha katika house, na kwamba anataka ku repeal and replace Obamacare
Jana alisema ni suala complicated hakujua.
Hili ni suala linalowagawa Republican kutokana na reaction wanayoipata katika majimbo yao

Tatizo lilikuwa kauli zake kuhusu ubaya wa Obamacare ambayo kura za maoni zinaonyesha ni maarufu kuliko ubaya anaousema. Hivyo kwa mtazamo wa haraka Dems na watu walioko iliwaudhi

Kukiwa na Dems halafu kukawa na split katika Republican, Obamacare inaweza kufutwa kwa gharama kubwa sana za kisiasa mbele ya safari.

Hilo ameliona na ameanza kwa kusema 'wenye pre existing condition' wataendelea nazo
Kwa kiasi alikuwa anacheza na hoja za Dems na Republican.

Kwa mfano, hoja ya FDA kufanya deregulation ni ya Bernie Sanders aliyoongea wiki moja iliyopita
Kwa namna yoyote Obamacare ni tatizo kuliko alivyoieleza kirahisi

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom