He is stuck between a rock and a hard place and no matter which way he goes, it is going to be hard to do. Lenye nafuu kidogo kwake ni kukomaa na kugoma kujiuzulu kwa utetezi wa kisheria kwamba kwa kufanya hivyo hajavunja sheria. Lakini akijiuzulu amejipalia mkaa wa moto pamoja na bosi wake aliyemteua...Marekani watu hawakurupuki...tuvute subira!
Mkuu tulisema, Wamarekani hawatupi jambo katika media bila sababu
Washington Post walipoambiwa ni fake news walikaa kimya kama vile wanafunga kampuni
CNN nao walipoambiwa waliendelea kusisitiza tu kuwa wapo sahihi
The W.Post wameanza kutoa dose na wana dossier kubwa, wanavuta kamba kidogo kidogo mtu akitisika, kitanzi kinabana chenyewe
Katika senate hearing, Sessions aliulizwa kama kulikuwa na mawasiliano aliyojua
Akasema hakuna kwa kadri anavyojua. Tayari swali lile lilikuwa na 'mtego'
Jana anasema ni kweli alizungumza na Balozi wa Russia na kwamba ni kawaida kwa member wa senate katika kamati zao kuzungumza na viongozi wa mataifa
Na huo ni ukweli kwani wenzake katika kamati wamethibitisha ni kawaida
Kwa namna isiyoeleweka, mwezi wa 10 alizungumza tena na Balozi huku wenzake hao hapakuwepo aliyezungumza na Balozi huyo.
Hii ilikuwa ni wakati Utawala wa Obama ulikuwa na taarifa za hacking kutoka intel community, hivyo alikuwa katika 'rada'
Kama umemsikiliza Seneta Lindsey Graham na McCain jana, ni kama vile walijua kitu fulani na hoja ni kuwa Sessions anaweza kuwa hakufanya jambobaya, lakini katika mazingira yaliyopo wanataka kujua alizungumza nini
Leo Republican baadhi wanasema Sessions afanye recuse, yaani ajitoe katika kushughulikia uchunguzi wa Russia kama Mwanasheria. Dems wanataka ajiuzulu
Hii maana yake akiji recuse suala linabaki hewani na anaweza kuitwa kwa mahojiano.
Aking'ang'ana analirefusha na hapo kutakuwa na chimba chimba.
Gen Flynn aliona ni vema ajiondoe ili kuepusha 'fukunyua fukunyua'
Washington Post na Media zilizoitwa 'fake' zinataka ku prove kuwa si fake.
Kitendo cha kumtaja Sessions kuna jambo nyuma. Wanataka watu waingie kichwa kichwa
WH wamegundua jambo, jana wamesema hizo ni jitihada za Dems katika kuvuruga mantiki ya hotuba ya Trump katika congress.
Hapa hawakusema Media au IC au Leak
Wanajitahidi kutafuta mchawi Dem kwasababu wanajua kuna 'mzigo' wa nondo
Kama mtakumbuka tulisema , ugomvi wa Trump na IC na Media utaishia pabaya.
Hizi zote ni katika kuhakikisha wana m-prove wrong na wanatafuta ushahidi
Trump alisema hakuna afisa wake aliyejihusisha, hili la Sessions kama mshauri wa kampeni linamweka mahali pagumu
Katika kufunika habari, leo au kesho utasikia WH ikitangaza jambo 'controversial' kama EO ya wahamiaji. Itakuwa kuahirisha tatizo maana tayari 'upele umempata mwenye kucha'
Tusemezane