Nadhani kwa sasa hivi ni wazi kuwa :
(a) Trump hana sera yoyote anayosimamia!
Mag3 na rafiki yake wanafanya watu wasisome wala kufuatilia kwa umakini kinachoendelea U.S.
Ukitaka kujua sera ya Trump & Republicans ya healthcare inakubidi usome key issues za healthcare bills zinazopigiwa kura halafu utofautishe na ACA. The same applies kwenye kodi, ulinzi mipakani, immigration, trade, sera za nje, military, welfare, veterans, social security, elimu, uchumi, climate change, space, n.k
Ukiishia tu kusoma posts za humu na kuangalia/kusoma/kusikiliza media zinazoimba habari za 'Russia collusion' kila siku ni wazi hutaona anachosimamia Trump. Utajua tu kile wanachotaka ujue. Jaribu ku-challenge taarifa unazopata, usimezeshwe tu.
lengo lake kubwa ni kufuta lolote lile lililofanywa na Obama hata kama ni zuri.
Hakuna Rais US anaeweza kufuta kila kilichofanywa na predecessor wake kwa sababu mazuri lazima yatakuwepo. Kuna mambo mengi sana yaliyofanywa na Obama ambayo Trump hata hajazungumzia kufuta.
Lakini ni kitu cha kawaida kwenye demokrasia kwamba Rais wa chama kingine anapoingia madarakani anategemewa kufanya mabadiliko mengi ukilinganisha na Rais wa chama kile kile. Hata Ted Cruz au Marco Rubio angekuwa Rais leo ungemuona anajitahidi kufuta mambo mengi yaliyofanywa na Obama.
Lakini pia wagombea wanaahidi vitu wakati wa kampeni na wanapigiwa kura kutekeleza hayo. Wazungu wako serious na ahadi za kampeni, huwezi tu kuwanunulia kanga na kofia na kuwawekea wasanii kipindi cha kampeni halafu wakakurudisha awamu ya pili wakati hujatekeleza uliyoyaahidi.
Kama ulifuatilia debates kwenye Primaries hasa za Republican candidates ungejua misimamo yao kuhusiana na sera za Obama. Tena wagombea wengine walikuwa so agressive zaidi ya Trump kuahidi kufuta vitu vingi vilivyofanywa na Obama.
Kila anachokifanya Rais Trump ni kile alichowaahidi wananchi kuwa akishinda atakifanya. Hilo ndilo lengo lake kubwa.
Kwa sasa hivi yeye anachotaka ni muswada wowote kutoka Congress unaofuta Obamacare hata kama muswada huo ni mbaya kiasi gani ukifika kwenye desk lake, atatia saini bila hata kuusoma.
Kwanza, Trump anafanya kazi na Republicans kwenye healthcare bills. Tom Price (Sec. HHS) na team yake pia wako kwenye constant consultations na Congress kuhusiana na miswada ya repeal & replace ACA na mambo mengine.
Trump anachotaka na anachosisitiza ni kwamba vitu viende haraka. Kwa mfano, anawashangaa R's kwamba wameimba ku-repeal na ku-replace ACA kwa miaka 7 kwa sababu hawakuwa na WH, sasa hivi wanayo na bado wanachelewa.
Ndio maana angetamani kuona Senate rule ya filibuster inabadilishwa kwenye baadhi ya vitu ili kuruhusu kupitishwa miswada kwa simple majority ('nuclear option') badala ya kutumia 'budget reconciliation' yenye conditions na isiyoruhusu full changes.
Kuna miswada 200+ imekaa Congress haijapitishwa na sio kila mswada R's wanaweza kutumia 'budget reconciliation' kupitisha. Rais Trump anachotaka ni kuona R's walio Congress wanafanya kazi na sio kuongea tu.
Kwahiyo kusema kwamba atatia saini bila kusoma ni kuwa naive, kwa sababu atarudi kuelezea kwenye re-election na wananchi watakuwa wameona matokeo ya sheria alizosaini.
Lakini pia, Rais kulilia miswada ni kitu cha kawaida kwenye demokrasia, kwani hata Obama kipindi chake cha pili alikuwa analilia miswada (kwa bahati mbaya chama chake hakikuwa na Congress) na haikuja kama alivyotaka.
(b) Wakati republican wana kampeini dhidi ya Obamacare, walikuwa wanatafuta kura tu, hawakuwa na plani yoyote ya kui-replace.
Ungefuatilia Republican primaries ungejua kila mmoja akiwemo Trump (then candidate) alieleza sera yake ya healthcare na sera zingine.
Kampeni ya Republicans dhidi ya Obamacare haikuanza kipindi cha kampeni mwaka 2016 bali ilianza 2010. Mwaka 2015 mwishoni R's walimaliza kufanyia kazi ACA repeal and replace bill iliyoitwa Healthcare Freedom Reconciliation Act kwenye Senate baada ya kupita kwenye House (240-181). Waliipitisha kwa 'budget reconciliation'. Obama alii-veto mwaka jana mwanzoni.
Kinachowakumba R's sio kwamba hawana bill ya ku-replace ACA, hapana, ni kwamba wana healthcare bills na ideas nyingi zinazoshindwa kupata kura za kutosha. Ndio maana utasikia wako kwenye majadiliano ili wa-compromise kwa sababu Senators kama Susan Collins (Maine), Lisa murkowski (Alaska) au John McCain (Arizona) hawawezi kupata 100% ya kila wanachokitaka.
Kuna wapiga kuwa wengi wa trump wanaofaidika na Obamacare, lakini hawataki jina Obama.
Political witchhunt continues.
Kitendo cha kusema hawataki jina Obama una-insinuate kwamba wao ni wabaguzi. Hao unaowaita wabaguzi walimpigia kura Obama mara mbili mwaka 2008 na 2012 na akashinda. Walikataa sera za Obama mara ya tatu kupitia kwa Hillary mwaka 2016. Kosa lao ni kuhitaji mabadiliko au kosa lao ni nini?
Na kama walihitaji mabadiliko ina maana hawakufurahishwa na yaliyotokea ikiwemo Obamacare. Kwa sababu kama walifaidika na Obamacare iweje walimpigia kura mtu aliyewaahidi kuwa atai-repeal na ku-replace badala ya yule aliyewaahidi kuiboresha?
Pengine mwaka 2012 walimpigia tena kura Obama kwa sababu Obamacare haikuwa na madhara sana kwao kama ilivyokuwa mwaka 2016. Maana kama walikuwa na tatizo na jina 'Obama' wasingempigia kura mara zote mbili na kumpa ushindi. Hasahasa wasingempigia kura Obama mwaka 2012 maana kipindi hicho Obamacare tayari ilikuwa na miaka miwili.
Kwa hiyo ukiichukua sera zima ya Obamacare kama ilivyo lakini ukaibadili jina na kuiita Trumpcare, utashangaa itakavyoshangiliwa!
Ukifuatilia debates za healthcare zinazoendelea Congress, watu wanajadili provisions za ACA na zile za R healthcare bills, Senators wanapeleka amendments na kuongeza provisions kwenye repeal and replace bills. Hawana shida ya a.k.a ya sheria, wana shida na effects zake.
Wapiga kura nao hawana shida na a.k.a kama unavyodhani. Ndio maana hujasikia Republican yeyote anasema hataki Obamacare kwa sababu ina jina la Obamacare.
Hivi unajua kuwa hata Dems wenyewe wanakubali kuwa ACA ina matatizo? Na wao ndio kabisa hawajui hata watatue vipi maana wengi wao hawakujua walichopitisha? Wamebaki kuzungumzia spending cut kwenye medicaid mara wapiga kura wa Trump watakosa coverage huku hawana alternative.
Kwamba Dems wanampenda sana Trump hadi wamkumbushe kuwa anapoteza wapiga kura aki-repeal ACA?, wanasahau alipata kura kwa kuahidi kui-repeal ACA? Well, as a matter of fact, Trump atapoteza wapiga kura asipo-repeal ACA.
Kuna watu wana shida na provisions za ACA kwa miaka 7 sasa toka ipitishwe.