Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Nakumbusha tu kuwa tax reform bill imepita Congress (House na Senate) na ishafika mezani kwa Trump kwa ajili ya kusainiwa kuwa sheria.

Wale waliotaka 'major legislative achievement' tayari wameona, wengine tulisema haya yatatokea lakini tuliambiwa ni ndoto.

Leo tunasema tena, legislative achievements kubwa bado zinakuja kwenye serikali ya Trump. Wenzetu bado wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa Mueller kuhusiana na kioja cha 'Russian meddling'.

Republicans walichonifurahisha ni kuwa 'individual mandate penalty tax' ya OBAMACARE nayo IMEFUTWA kupitia muswada huo wa kushushwa kwa kodi US. Tukumbuke kuwa kipengele cha 'individual mandate penalty' kwenye ACA inawalipisha fine watu wasio na bima ya afya (bila exemption).

Kuna mengi mazuri katika huo mswada uliopita Congress, kwa kifupi kila mtu anashushiwa kodi, kwa mfano, kodi ya mapato ya makampuni inashushwa kutoka 35% hadi 21%.

Mswada huo ukishakuwa sheria utaongeza ukuaji wa uchumi wa US, utaongeza ajira na uzalishaji, utaongeza nguvu ya ushindani kwa makampuni ya US, utapelekea makampuni ya US kurejesha nchini mwao fedha zao zilizopo nje, utaongeza fedha mfukoni mwa wananchi kwa ajili ya matumizi mengine n.k.
 
Donald Trump has taken time from his busy holiday schedule to wish millions of Americans – including his “enemies” and “haters,” as well as “fake news” outlets, a happy and healthy New Year.
“As our Country rapidly grows stronger and smarter, I want to wish all of my friends, supporters, enemies, haters, and even the very dishonest Fake News Media, a Happy and Healthy New Year. 2018 will be a great year for America!” Trump tweeted from his Florida Mar-a-Lago resort where the first family is celebrating the start of the New Year. “HAPPY NEW YEAR! We are MAKING AMERICA GREAT AGAIN, and much faster than anyone thought possible!”

Trump wishes his enemies & haters ‘happy and healthy’ New Year
===
Walimu wangu Heri ya Mwaka mpya. Nawatakia heri ya Mwaka Mpya wachangiaji wote kwenye uzi huu. Kipekee nilete salamu kwenu walimu wangu hapa JF (Nguruvi3 na Mag3 ) kutoka kwa Donald Trump rais wa Marekani, ni salamu za mwaka mpya.🙂
 
Mafanikio dhidi ya ISIS:

Square miles walizonyang'anywa ISIS (Trump: 26,000 -- Obama: 13,200)

Jumla ya Square miles zinazoshikiliwa na ISIS (Trump: 1,930 -- Obama: 17,500)

Kadirio la idadi ya wapiganaji wa ISIS: (Trump: 1,000 -- Obama 35,000)

Idadi ya watu waliookolewa kutoka kwa wapiganaji wa ISIS: (Trump: 5.3M -- Obama 2.4M)
 
Walimu wangu Heri ya Mwaka mpya. Nawatakia heri ya Mwaka Mpya wachangiaji wote kwenye uzi huu. Kipekee nilete salamu kwenu walimu wangu hapa JF (Nguruvi3 na Mag3 ) kutoka kwa Donald Trump rais wa Marekani, ni salamu za mwaka mpya.🙂

TUJITEGEMEE , hawa ndugu zetu nadhani wanasubiri taarifa ya uchunguzi wa Mueller.

Mafanikio ya Trump mwaka 2017, not limited to:

1. ISIS obliterated
2. Gorsuch on the Supreme Court
3. Stock Market hit 70 record highs
4. 1.7 million NEW jobs created
5. Largest tax cut in US history
6. Most new conservative judges on the court
7. Massive economic deregulation, more than any President in 100 yrs.
8. Big League VA reform
9. Consumer confidence at all time high
10. Illegal immigration down 70%.
11. Travel ban reinstated.
12. Canceled TPP.
13. Removed the ACA individual mandate
14. Opened up markets to allow billions of $$ of US goods to be exported
15. Embassy in Jerusalem

Courtesy of Charlie Kirk @Charliekirk11.
 
1. ISIS obliterated
Ahsante sana Mkuu.
Mengine nakubaliana naye lakini hili nadhani linahitaji mjadala.

Taarifa kutoka Mashariki zinasema Syria ikisaidiwa na Russia, Iran na kikundi cha Hesbollah na Wakurdi na China kwa mbali ndiyo hasa wamemaliza nguvu za ISIS. Wanasema majeshi washirika wa US ikiwemo Israel walikuwa hawashambulii ISIS haswaa bali walikuwa wanashambulia majeshi ya serikali ya Syria inayoongozwa na Assad na washirika wake (ushahidi upo). Pia US na washirika wake walikuwa wanakwamisha harakati za washirika wa Syria kwa kuwanyima kwa makusudi taarifa muhimu juu walipo ISIS na mahali ambapo US watakapofanya harakati zao ili kuepusha ajari za kivita. Hii ni huko Syria.

Kwa upande wa Iraq, nako hawawezi kujivunia ushindi. Maana baada ya Iran kuisaidia kwa nguvu zote Iraq kupambana na ISIS na ikaelekea kuwakama wakiwa hai hao ISIS bila kuleta madhara kwa raia ndipo US na washirika wake wakaja hatua za mwisho na kupiga mabomu bila kujali kwa kuua raia wengi zaidi (nadhani kuficha ushahidi wa mahusiano na kikundi hicho) na kisha kuua baadhi tu ya wanakikundi cha ISIS.

Katika propaganda zao mitandaoni hao ISIS inasemekana ni sehemu ndogo sana ama hakuna kabisa ambapo walikuwa wanawalaani US na washirika wake kwa kuwapiga mabomu. Sana walikuwa wanata kumung'oa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia wa Syria , B. Assad. Ni lengo hilo hilo lililokuwa linachagizwa kutekelezwa na US na washirika wake.

Kwa ufupi US chini ya Trump imeshindwa katika masuala yake ya mambo ya nje mfano Syria na kwenye vikao vya UN (128 vs 9).

Karibu Mkuu unipe elimu zaidi juu ya masuala haya ya Trump na US.
 
TUJITEGEMEE , hawa ndugu zetu nadhani wanasubiri taarifa ya uchunguzi.
Hauko peke yako ndugu yangu El Jefe, hapa Bongo watu kama wewe mmejaa tele. Siku hizi naona hata uvivu kujaribu kuwaelimisha...taking the bush out of you people is a tall order if not an impossible task.

Marekani watu wanaelewa maana ya uhuru kwani walimwaga damu zao kuupigania. Chezea kingine lakini usije ukachezea haki ya watu kuwa huru. Trump angezaliwa Tanzania hivi sasa angekuwa anaabudiwa na watu kama wewe kuliko hata huyu Pombe wetu.

Nixon pamoja na kashfa kibao aliweza kushinda na kuwa Rais kwa kipindi kingine. Baada ya uchunguzi uliochukua karibu miaka miwili alijiuzulu na hivyo kukwepa kifungo. Ilifika wakati watetezi na washikaji wake wa karibu walianza kumkimbia moja baada ya mwingine!

Ni kweli tupo tunaosubiri kwa hamu ripoti ya Mueller, je wewe?

Alamsiki.
 
Republicans ask DOJ for criminal probe of ex-British spy Steele who penned ‘Trump dossier’
====
Leading members of the Senate Judiciary Committee, Senators Chuck Grassley (R-Iowa) and Lindsey Graham (R-South Carolina) have sent a criminal referral to the Department of Justice for former UK spy Christopher Steele.
The former MI6 intelligence officer authored the so-called “Steele Dossier,” commissioned by the opposition research firm Fusion GPS and funded largely by Hillary Clinton’s presidential campaign through the Democratic National Committee. The dossier alleged ties between then-Republican presidential candidate Donald Trump and the Russian government.
____
Muller afanye uchunguzi kwa haki
 
Mkuu TUJITEGEMEE


Mwaka 2014 ISIS walianzisha 'caliphate' (chini ya Al Baghdadi) iliyokuwa ndani ya nchi mbili za Iraq na Syria lakini yenye kuungwa mkono na wapiganaji wengi kwenye nchi nyingi.

ISIS ilikuwa inatawala eneo lililo sawa na jimbo la Ohio (US) ndani ya Iraq na Syria.

ISIS walianzia Iraq kama wapiganaji (sunni) waliokuwa wakiipinga serikali ya waziri mkuu Al Maliki na uvamizi wa US mwaka 2003 na kuongezeka nguvu baada ya majeshi ya US kuondoka mwaka 2011. Kabla ya US kuondoka Iraq, ISIS walikuwa wakizidiwa nguvu katika mapigano hayo.

ISIS walikimbilia Syria mwaka 2011 baada ya kuibuka kwa mapigano kati ya Rais Assad na vikundi vya kijeshi (waasi) na wananchi waliokuwa wakiupinga utawala wake na kumtaka aondoke madarakani. ISIS walitumia upenyo wa hayo mapigano kupata wapiganaji na kujipatia maeneo karibia 1/3 ya Syria ndani ya miezi 18. Wakaanzisha mjii mkuu wao Raqqa.

Baada ya kunyakua maeneo ndani ya Syria, ISIS walirudi tena Iraq wakiwa na wapiganaji wengi na silaha bora na kuwazidi nguvu wanajeshi wa Shia wa Iraq na kunyakua maeneo makubwa ndani ya Iraq hadi Mosul (Juni 2014) na kuelekea Baghdad (Tikrit) na kuanzisha 'Caliphate'. Abu Bakr al-Baghdadi akajitangaza kuwa ndiye "caliph" and "kiongozi wa waislamu duniani kote".

Nchini Iraq, majeshi washirika (Australia, Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Jordan, Uholanzi, Uingereza) Wakiongozwa na US walianza mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS Agosti 2014. Hadi desemba 2017, mashambulizi ya anga 13,200 yamerushwa dhidi ya ISIS (Pentagon, 2017).

Nchini Syria, majeshi washirika (Australia, Bahrain, Ufaransa, Jordan, Uholanzi, Saudia Arabia, Uturuki, UAE, Uingereza) wakiongozwa na US wamefanya mashambulizi karibia 14,000 dhidi ya ISIS (Pentagon, 2017).

Mabomu ya anga yaliyodondoshwa na majeshi washirika wa US dhidi ya ISIS kila mwezi katika kipindi cha miezi minane (8) ya mwanzo ya mwaka 2017 inazidi mabomu yaliyorushwa na majeshi hayo katika kipindi Obama ni Rais (Pentagon, 2017).
Ndio maana Trump anapata 'credit'.

Ndicho kilichopelekea waziri mkuu wa Iraq Haider Al Abadi kutangaza mwezi uliopita kuwa vita dhidi ya ISIS 'imeisha'. Russia na washirika wake hawakuwashambulia 'magaidi' ndani ya Iraq bali ndani ya Syria.

Majeshi ya kidemokrasia ya Syria (SDF) wanaoshirikiana na majeshi washirika wakiongozwa na US, walifanikiwa kuwaondoa ISIS katika mji wa Raqqa (75%). Kumbuka Raqqa ndio ulikuwa mji mkuu wa ISIS.


SYRIA:

Baada ya 'Arab Spring revolution' kutua Syria, wananchi wengi waliandamana kumshinikiza Rais Assad aachie madaraka.

Ila kwa vile ni king'ang'anizi kama alivyokuwa Gaddafi, baada ya mwaka na nusu wapiganaji wa 'Free Syrian Army' na makundi mengine yanayotii FSA yaliamua kuanzisha mapigano dhidi ya majeshi yake (SAF).

FSA ni mjumuiko wa wanajeshi wa Syria waliokaidi kumtii Rais Assad pamoja na raia wanaomtaka aondoke madarakani.

Kumbuka kuwa malengo ya ISIS na makundi kama FSA (pamoja SDF n.k) ni tofauti. ISIS walitaka kuanzisha 'caliphate' chini ya Al Baghdadi wakati FSA wanataka kumuondoa Assad madarakani kwa sababu ni dikteta na amekaa madarakani mda mrefu (toka mwaka 2000).

Kuibuka kwa makundi yanayohusiana na Al-Qaeda na ISIS kumemfanya Rais Assad na washirika wake (Iran na Urusi) kutangaza kuwa hao wanaopigana ili kumtoa Assad madarakani (FSA) ni magaidi pia. Kwahiyo wanadai wanapigana na 'magaidi', ingawa kiuhalisia hao ni waasi na sio magaidi.

Mwezi Mei 2017, Urusi, Iran na Uturuki walikubali kutekeleza 'de-escalation zones' ili kupunguza mapigano na kusaidia raia wenye uhitaji. Lakini majeshi ya Syria bado yanashambulia maeneo waliokubaliana wasishambulie kama Idlib, East Ghouta, Homs kaskazini na Kusini mwa nchi (Aljazeera, 2017).

Urusi waliingia Syria kumsaidia Assad mwaka 2015. Wakatekeleza kampeni yao ya mashambulizi ya mabomu dhidi ya waasi wa FSA na makundi yanayowaunga mkono, huku wakisaidiwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran, lengo ni kumsaidia Raia Assad aendelee kubaki madarakani.

Urusi, Iran na Syria waliwazidi nguvu waasi wa FSA na kufanikiwa kuchukua mji wa Aleppo (uliokuwa chini ya waasi) desemba mwaka 2016.

Mwezi ulipoita Rais Putin alitangaza kuwa wameshinda vita dhidi ya 'magaidi' na kwamba wataanza kuondoa majeshi yao Syria.

Maeneo yenye mapigano makali Syria kwa sasa (Aljazeera, 2017):

(i) Maeneo ya Ghouta Mashariki:
Yanashikiliwa na FSA. FSA wanasaidiwa na US, Uturuki na Gulf States kadhaa. Haya maeneo yapo katika 'de-escalation agreement' ila bado yanashambuliwa na majeshi ya Syria.

(i) Maeneo ya Idlib-Hama:
Yashikiliwa na kundi linaloitwa Hay'et Tahrir al sham (HTS). Hawa wanahusiana FSA ila ZAMANI waliokuwa wanahusiana na Al-Qaeda.

(ii) Maeneo ya Mashariki mwa nchi kati ya Mayadin na Al-Bukamal. Haya maeneo bado yanatumiwa na ISIS kushambulia majeshi ya Assad na majeshi washirika wa US.
 
Taarifa kutoka Mashariki zinasema Syria ikisaidiwa na Russia, Iran na kikundi cha Hesbollah na Wakurdi na China kwa mbali ndiyo hasa wamemaliza nguvu za ISIS. Wanasema majeshi washirika wa US ikiwemo Israel walikuwa hawashambulii ISIS haswaa bali walikuwa wanashambulia majeshi ya serikali ya Syria inayoongozwa na Assad na washirika wake (ushahidi upo).

Kuwaondoa ISIS Iraq ni kazi iliyofanywa na Iraq na majeshi washirika wakiongozwa na US. Russia au Syria hawakuwahi kuwashambulia ISIS nchini Iraq.

Lakini pia ISIS wapo nchini Syria ambako walijitwalia 1/3 ya Syria, mji mkuu wao ulikuwa Syria (Raqqa). Raqqa inashilikiwa na SDF (Syrian Democratic Forces) wanaoiunga mkono FSA.

Majeshi washirika wakiongozwa na US wamewashambulia ISIS hadi ISIS wamekimbia huo mji na wameelekea huko maeneo ya Syria ambako Assad ana udhibiti nako.

Tukumbuke kuwa Assad hana udhibiti (control) wa Syria nzima. Assad anawezaje kuwashambulia ISIS walio Iraq wakati yeye mwenyewe hana udhibiti wa maeneo yote ya Syria? Assad anashambulia ISIS nchini Syria tu na anawajumuisha na FSA.

Majeshi washirika wakiongozwa na US wamefanya mashambulizi Syria (mashambulizi karibia 14,000) na Iraq (mashambulizi 13,200).

Huko ambako wapiganaji wa ISIS walipoelekea ndiko Assad na washirika wake wanaweza kuwamalizia maana hata hivyo wamebaki wachache.

Kwa hiyo, hizo taarifa zinazodai kuwa Syria ikisaidiwa na Russia, Iran na kikundi cha Hesbollah na Wakurdi na China kwa mbali ndiyo wamemaliza nguvu za ISIS zina walakini.

Kwa kifupi US na washirika wake walikuwa wanapigana vita na ISIS na wameshinda kwa kiasi kikubwa, huku US (na baadhi ya washirika wake) wakisaidia mapigano ya FSA dhidi ya Assad (na washirika wake) (ila sio moja kwa moja). Hiyo inaitwa 2 in 1.

Pia US na washirika wake walikuwa wanakwamisha harakati za washirika wa Syria kwa kuwanyima kwa makusudi taarifa muhimu juu walipo ISIS na mahali ambapo US watakapofanya harakati zao ili kuepusha ajari za kivita. Hii ni huko Syria.

Syria na washirika wake waliwachukulia FSA na washirika wake kama magaidi na wanawashambulia wao na ISIS kwa pamoja bila kuwatofautisha.

US na washirika wake walikuwa hawashambulii FSA maana US, Uturuki na nchi za Gulf ndio wanafadhili hilo kundi kwa malengo na kumtoa Assad madarakani.

Katika mazingira kama hayo US anashirikiana vipi na Syria?

Kwa upande wa Iraq, nako hawawezi kujivunia ushindi. Maana baada ya Iran kuisaidia kwa nguvu zote Iraq kupambana na ISIS na ikaelekea kuwakama wakiwa hai hao ISIS bila kuleta madhara kwa raia ndipo US na washirika wake wakaja hatua za mwisho na kupiga mabomu bila kujali kwa kuua raia wengi zaidi (nadhani kuficha ushahidi wa mahusiano na kikundi hicho) na kisha kuua baadhi tu ya wanakikundi cha ISIS.

Kwani Iran alishusha mabomu mangapi dhidi ya ISIS katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita?

Sikatai kwamba Iran hawakuisaidia Iraq kwa sababu zote ni serikali za Shia, na ISIS wanajiita wapiganaji na watetezi wa waislam wa Sunni.

Sijui utakamataje watu zaidi 30,000 wakiwa hai katika vita na magaidi, si mtakesha mkuu?

Mabomu ya US na washirika wake dhidi ya ISIS yalizidi sana baada ya Donald Trump kuingia madarakani. Idadi ya mabomu ya kila mwezi kwa miezi minane ya mwanzo ya mwaka 2017 yalizidi idadi ya mabomu ya mda wote katika kipindi cha Rais Obama.

US na washirika wake wanao utaratibu wa kupunguza madhara ya mashambulizi kwa raia wasio na hatia. Ila hao magaidi wanajificha kati kati ya watu unategemea nini? Huwa wanajitahidi ku-minimize ila magaidi ni majanja hayataki kufa yenyewe. Kwa sababu mashambulizi yaliongezeka madhara kwa raia nayo yaliongekeza. Ila kuna watu zaidi ya Mil. 5 waliopata uhuru baada ya ISIS kushindwa.

Katika propaganda zao mitandaoni hao ISIS inasemekana ni sehemu ndogo sana ama hakuna kabisa ambapo walikuwa wanawalaani US na washirika wake kwa kuwapiga mabomu. Sana walikuwa wanata kumung'oa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia wa Syria , B. Assad. Ni lengo hilo hilo lililokuwa linachagizwa kutekelezwa na US na washirika wake.

Mkuu , kwahiyo 'caliphate' ya Al Bhaghdadi ya mwaka 2014 haikuwa na wapiganaji??

Labda sijaelewa unasema ISIS ni stori tu wala haipo na haikuwahi kuwepo? Kama ni hivyo, hapo mwanzoni uliposema Syria na washirika wake 'ndiyo hasa wamemaliza nguvu za ISIS' ina maana 'walimaliza nguvu' za kikundi ambacho hakipo??

Kwa ufupi US chini ya Trump imeshindwa katika masuala yake ya mambo ya nje mfano Syria na kwenye vikao vya UN (128 vs 9).

Mkuu utasemaje ameshindwa wakati ndiyo kwanza ana mwaka mmoja? Ndani ya huo mwaka mmoja ISIS wamepotezwa hadi viongozi wa kijeshi wa US na nje ya US waliopo na wastaafu wamempa credit Trump katika vita dhidi ya ISIS.

Pia katika hiyo UN resolution (128 vs 9) unasahau kuna nchi 35 zilijiondoa na mara ya mwisho unajua ni nchi ngapi zilijiondoa kwenye kura ya Jerusalem? Hata hivyo kila nchi ilipiga kura kwa utashi wake, ila kumbuka kuwa hiyo resolution ni non-binding.

Trump ni pro Israel, binafsi nadhani atakutana na changamoto katika kutafuta suluhu baina ya Palestina na Israel. Lakini hamna makubaliano ya amani yasiokuwa na changamoto. Rais Obama alishindwa miaka minane aliyokaa madarakani, Trump ndio kwanza ana mwaka mmoja.
 
Hauko peke yako ndugu yangu El Jefe, hapa Bongo watu kama wewe mmejaa tele. Siku hizi naona hata uvivu kujaribu kuwaelimisha...taking the bush out of you people is a tall order if not an impossible task.

Marekani watu wanaelewa maana ya uhuru kwani walimwaga damu zao kuupigania. Chezea kingine lakini usije ukachezea haki ya watu kuwa huru. Trump angezaliwa Tanzania hivi sasa angekuwa anaabudiwa na watu kama wewe kuliko hata huyu Pombe wetu.

Nixon pamoja na kashfa kibao aliweza kushinda na kuwa Rais kwa kipindi kingine. Baada ya uchunguzi uliochukua karibu miaka miwili alijiuzulu na hivyo kukwepa kifungo. Ilifika wakati watetezi na washikaji wake wa karibu walianza kumkimbia moja baada ya mwingine!

Ni kweli tupo tunaosubiri kwa hamu ripoti ya Mueller, je wewe?

Alamsiki.
Mag3, mimi napenda demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria, uhuru na haki. Kingine huwa na-base kwenye Facts tu, sio hearsays na rumors. Pia mimi ni independent (ila sio kama Bernie Sanders) hivyo nakuwa huru sana kutoa maoni yangu.

Trump akipatikana na hatia ambayo ni 'beyond reasonable doubt' nitasema Trump 'I like you but sorry, just step down.' So far, hamna kitu.

Kwahiyo hiyo notion kwamba naabudu watu sio kweli. Trump akikosea hutaona natetea uovu au makosa. Unajua wewe umechukua position ya Democrats in full kwahiyo hata hutaki kusikia au kukubali mazuri yoyote ya Trump.

Mfumo wa kiutawala wa US is way better, tungekuwa na mfumo kama huo Tanzania naamini maendeleo yangepatikana haraka sana. Viongozi wengi wa serikali na upinzani wasingeweza kuendana nao.

Ila tukiiga mfumo wa US, tusiige kila kitu, kuna mabaya pia. Congress is so griglocked, I prefer bunge la nchi liwe na wabunge wasio na vyama kabisa yani wawe Independents watakuwa huru sana kuisimamia serikali na kutunga sheria. Bunge la vyama kwa Tanzania litazidi kuchelewesha maendeleo.
 
Mag3, mimi napenda demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria, uhuru na haki.

Trump akipatikana na hatia ambayo ni 'beyond reasonable doubt' nitasema Trump 'I like you but sorry, just step down.' So far, hamna kitu.

Kwahiyo hiyo notion kwamba naabudu watu sio kweli. Trump akikosea hutaona natetea uovu au makosa. Unajua wewe umechukua position ya Democrats in full kwahiyo hata hutaki kusikia au kukubali mazuri yoyote ya Trump.
Wakati ukuta...vuta subira ndugu yangu! Siku hizi nimekaa kimya, hata ya bongo nayachungulia tu kwa mbali.
 
SIASA ZA MAREKANI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA

Wanajamvi kwa muda mrefu tumekuwa nje ya ukumbi kwa sababu anuai na za kibinadamu
Kwa kadri muda utakavyoruhusu tutajulishana nini kinaendelea katika siasa za Marekani

Kama mtafuatilia mabandiko ya uzi, mengi tuliyosema ambayo mengine hayakuwapendeza baadhi wakiyaita 'utabiri, obsessions' na kila aina ya dhihaka yanajidhihiri yenyewe

Siasa za Marekani zinahitaji ufuatiliaji wa kina na weledi. Moja ya mabandiko yaliyoitwa ubashiri ni hilo hapo chini

Mwanzoni mwa mabandiko tulisema kutawala si sawa na kampeni za uchaguzi

Kwa siasa za ndani ya US, yapo mengi yamefanyika na mengi yameshindikana, si kwasababu hayawezekani bali hali ya kiutawala tofauti na kampeni hasa kwa Taifa kama Marekani ambalo kufuata sheria ni sehemu ya utawala

Hata yale yaliyofanyika kuna hoja nyingi nyuma yake. Kwa mfano, hali ya uchumi kwa ujumla imeimarika wa kinachosemwa Trump factor. Nyuma ya hilo hakuna anayezungumzia uchumi ulikuwaje miaka 8 kabla

January 2009 Obama akiingia madarakani alikutana na great recession (mdororo wa uchumi) watu wakipoteza kazi kwa malaki, masoko yakiputkitisha mitaji kwa mabilioni na kiwango cha ajira kikiwa katika asilimia 9

Kwa utambuzi tu wa haraka, Marais wa Marekani waliorithi utawala katika recession ni LBJ, Carter, Reagan, Clinton na Obama. Nukta muhimu kama hizi hupuuzwa wakati wa mijadala mingi

Nini walifanya viongozi hao ni mjadala utakokuwa na bandiko lake, muhimu kuelewa waliitoa US katika mdororo

Kuna hoja ya masoko ya mitaji kuongezeka. Wengi wanapuuza ukweli kuwa masoko kama Dow Jones hayakuanza na point za juu. Kila muda unavyopita ndivyo uwezekano wa kufikia point za juu unavyoongezeka

Na wala masoko si dalili ya kukua kwa uchumi kwa mujibu wa Trump miaka ya nyuma na ni 'bubble'

Na hoja ya Tatu ni kuhusu unemployment rate imefikia 17 years low katika kiwango cha 4.1%
Muhimu si 4.1 bali namba hiyo imetoka kuanzia wapi. Mathalan, Obama akiingia ilikuwa takribani '9'
Akiondoka ilikuwa 4.9%.

Kusema ni 17 yrs low kuna kuchanganya mambo, je, 4.1 ni kuanzia wapi, 17 yrs au 1 yr. Tutajadili mbelen

Kuhusu siasa za nje, mkataba wa NAFTA bado unajadiliwa na hali inaonekana wabunge wengi wa Marekani na wataalam wa uchumi wakionya tatizo linaloweza kujitokeza. Hili Rais Trump alisema atalifuta mara moja

Tulisema kama inavyosemeka hapo chini, uhusiano wa US na Israel, Rusia-Iran-China', Taiwan na North Korea litakuwa tatizo. Na hali ilivyo ni tatizo kubwa kuliko ilivyodhaniwa

Kuhusu Russia na uchaguzi, tulieleza siasa za Marekani zilivyo na jinsi Trump anavyosogelewa kitaalamu

Mzunguko ulianza mbali na tulisema ipo siku utafika Oval office, leo umeingia na mjadala umeacha samaki wadogo. Upana wa uchunguzi ni tatizo kubwa, si suala la collusion bali upana wake

Tulieleza kilichomuondoa Nixon si kashfa ya Watergate,Impeachment ya Clinton si Monica Lowensky. Kinachoendelea na Russia investigation kwasasa kinachukua sura ya Nixon na Clinton

Tutapitia hoja zote taratibu kuelewa nini kinachoendelea kwa upana wake

Tusemezane

KWANINI IRAN?

Kabla ya kujadili hilo , tuseme kuwa katika mashambulizi yaliyofanyika Ulaya, magaidi yamekuwa na uhusiano na Algeria, Tunisia. Kuna nchi nyingine kama Egypt ambazo zimetajwa tajwa mar kadhaa

Zipo ishara za mashambulizi kama yale ya Mali kuhusishwa na makundi ya kigaidi
Nigeria nayo imewahi kuhusishwa na gaidi mmoja aliyeshindwa kulipua na pia Boko Haram

Lakini pia nchi kama Pakistan na Afghanistan zimekuwa katika 'watch list' ya Raia wake kwa muda
Magaidi waliofanikiwa au waliojaribu kwa namna moja au nyingine wamehusishwa na mataifa hayo

Ni nadra sana kusikia magaidi yakihusishwa na nchi ya Iran. Inapotokea nchi hiyo kuwa katika orodha ya 7 ya awali na kuziacha nchi zinazoonekana 'hotbed' inafikirisha kidogo kimantiki

Trump amekaririwa mara nyingi akizungumzia nuclear deal ya Iran kama tatizo.
Majuzi Waziri mkuu wa Israel BB alisikika akisema, inaelekea Trump analielewa tatizo la Iran

Ikumbukwe kuwa Israel ilichagiza sana US ishiriki katika kupiga mabomu au uinge mkono Israel kuishambulia Iran katika vinu vya zana za Nyuklia. Obama hakukubaliana na hatua za vita

Hilo ni moja ya mambo yaliyokuwa na tofauti kubwa kati ya BB Nyahu na Obama

Ni kwa mtazamo huo, inaelekea uwepo wa Iran hata kama ni sehemu ya kuzalisha magaidi bado kuna hoja ya kuitibua 'provoke' ili mpango mwingine ufanyike katika kubomoa vinu vya Nuklia.

Kuna uwezakano wa taarifa za Iran kusaidi au kufadhili magaidi
Pamoja nna hayo suala la vinu vya Nyuklia haliwezi kuwekwa pembeni katika sintofahamu hii

Suala la exec order ya wakimbizi au Visa si kosa.
Ni haki ya taifa lolote kuamua nani anaingia nani anatoka na kwa utaratibu gani.

Tatizo ni kuwa masuala kama haya huanzisha mizozo au malumbano kati ya mataifa
Katika dunia ya leo iliyojaa mawaa na mawenge wenge 'complicated' haya si mambo ya kiutawala tu

Mambo haya yatagusa sekta za uchumi, siasa na mahusiano ya wananchi wa dunia hii.

Kuna uwezekano tension iliyopo ikaathiri sana mwelekeo wa uchumi hasa mzozo wa Iran na US
Athari zingine zitagusa mizozo mikubwa kama wa Syria, North Korea n.k.

Kwa kuzingatia mahusiano mazuri sana ya Trump na Putin wa Russia, uhusiano wa kindugu US na Israel, Urafiki wa Iran na Russia, na ushirika wa Iran, Russia na China, pamoja na turufu ya Taiwan na North Korea, kuna tatizo mbele ya safari.

Rais Trump atakuwa na wakati mgumu kwa siasa za nje at least kwa mwanzo wa utawala

Kwanini mzozo unaweza athiri uchumi wa dunia? Tutajadili hili kwa mantiki.
Si la Dow Jones ina point 25K au 30K kwasababu imenukuliwa na blog. Ni zaidi ya hapo
What Kind Of 'Jobs President' Has Obama Been — In 8 Charts
Tusemezane
 
SIASA ZA MAREKANI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA
Tutapitia hoja zote taratibu kuelewa nini kinachoendelea kwa upana wake
Tusemezane
Mkuu Nguruvi3, usione kimya, wengine bado tumepigwa butwaa kutokana na yanayoendelea si nchini kwetu tu bali duniani kwa ujumla wake. Kwa sasa tunao vichaa wengi wamekamata dola, tofauti ni kwamba wapo ambao pamoja na kupewa rungu wamefungwa luku na wapo walio huru wakitumia rungu walilopewa wanavyotaka. Kinacholeta taabu ni kiwango cha ustaarabu tu. Tusemezane...
 
Andrew McCabe AJIUZULU

Andrew aamjiuzulu leo ghafla ikiwa ni siku si zaidi ya 60 kwa muda wa kustaafu
Huyu alikuwa Deputy Director wa FBI, akifanya kazi pamoja na Comey aliyetimuliwa na Trump

Habari hii ni kubwa na tusimama kuongelea suala la uchumi ili kuangalia kwa undani nini kinaendelea
Kujiuzulu kwake kunatokana na Russia investigation ingawa haisemwi hadharani kwasababu za kisiasa

Andrew ameshambuliwa na Republican wanaotaka uchunguzi wa Russia ima usitishwe au matokeo yake yasiaminike
Sababu za kushambuliwa kwa Andrew ni kuhusika na uchunguzi wa Clinton huku mkewe Andrew akihusishwa

Inatosha kusema mkewe aligombea jimbo la Virginia na alipokea msaada wa mchango wa Clinton
Hilo lilitokea miezi miwili kabla ya Andrew kuteuliwa kuwa Deputy!

McCabe aliitwa na kamati ya bunge kuhojiwa kuhusu suala hilo. Ni mkakati wa Republican katika kutaka aondoke
Kwa bahati mbaya mkakati huo ulifaytuka kwani katika mahojiano AMcCabe alieleza tatizo la Comey

Huu si mkakati wa bahati mbaya , ni mkakati mkali unaoendelezwa katika kubeza uchunguzi wa Russia

Kwanza, tutakumbuka Nunes alivyokwenda WH kueleza jinsi Susan Rice(Mshauri wa Obama) alivyotoa majina katika kile kinachoitwa surveillance iliyonasa mawasiliano kati ya washirika wa Trump kampeni na Russia

Susan Rice aliitwa katika kamati ya Bunge, alichokieleza huko hoja ya surveillance ikafa kabisa

Mkakati wa pili ulikuwa kuhusu Clinton foundation, ukilenga kuonyesha FBI walikuwa biased
Hilo nalo halikufika mbali kwani lilishafanyiwa uchunguzi na hakuna cha 'maana' Republicana wanachoweza kupata

Ukaundwa mkakati wa Clinton na Uranium iliyohusisha Russia, kwamba alifanya mauzo kama hongo kwa Russia
Kilichobainika ni kuwa kuna agency sabab zilifanya vetting na Dept of state ni sehemu tu hivyo kukosa mashiko

Ukaundwa mkakati wa Dossier iliyotoka GPS fusion kwamba ilikuwa ndicho kigezo cha FBI kufanya uchunguzi
Dossier ilikuwa ni kampuni ya opposition research iliyoanza na Republican kabla ya Democrat

Hoja ilikamata, majuzi ikabinika mshirika wa Trump, Papadopoulous aliyeitwa ''Coffee boy'' alizungumza na mshirika wa intelejensia wa Australia kuhusu dirty on clinton. Mshirika huyo kwa kubaini ni jambo la usalama akawatonya FBI

Hivyo GPS walipofikisha dossier tayari FBI walikuwa na habari na hilo lilikuwa uthibitisho wa kile walichojua
GPS waliposhinikizwa kufika mbele ya kamati ya bunge walieleza mengi yaliyowaacha Republican wakitaharuki

Hoja ikahamia kwa text message za maafisa wawili wa FBI wapenzi. Majuzi ikakamatwa text moja inayosema 'wakutane secret society'. Republican wakishikia bango kwamba kuna society ndani ya FBI inayotaka kumuondoa Trump

Walipotaka text zaidi wakijua kuna jambo, ikabainika ni utani wa moengezi hakuna kinachoitwa secret society

Inaendele
 
McCabe

Inaendelea

Wakati hayo yakiendelea, Trump alimwandama AG Sessions akimlaumu kwa kujiondoa kusimamia uchunguzi
Alimwita kila aina ya majina akimfanyia kila vitimbwi na dharau ili Session ajiuzulu

Huu ni mkakati kwamba Sessions akiondoka, Trump atamteua AG mwingine atakayesimamia Russia inestigation
Kumtimua Sessions hawezi kwani atakuwa ameudhia conservatives na kutilia shaka nia yake

Sessions aliuza kiti chake cha seneti ili awe AG, na miongoni mwa Maseneta wa awali kumuunga mkono

Kwasasa anayesimamia uchunguzi wa Russia ni Deputy wa Sessions bwana Roseintstein
Hesabu ni kumuondoa Sessions, ateuliwe mwingine ili usimamizi uondoke kwa Roseinstein kwenda kwa AG mpya

Hilo liliposhindika kwa Sessions kutojiuzulu, mwezi wa 6 kwa taarifa za karibuni Trump alimuagiza Don Mcgahn amwagize Session kumfukuza Roseinstein. Don alikataa kwa kuchelea madhara ya hatua hiyo

Kamati 4 za congress zimegawanyika kichama na hata sasa kuna suala la memo lililiondaliwa na Nunes linalorindima.
Hili tutalijadili mbeleni

Mtiririko wa matukio yote umelenga kuzima uchunguzi wa Mueller ambao sasa umeingia oval office

Kwanini kuna hofu juu ya uchunguzi wa Mueller?

Kuna kila kiashiria kuwa washirika wa Trump 'watakuwa wamechoma utambi'

Ieleweke utambi tunaongelea si wa Russia collusion peke yake.

Kuna mambo mengi yanayohusu money laundering, mengi investment n.k.
Tunajua hakuna anayejua tax return za Trump wala business zake kwa undani

Mengine hayawezi kuwa tatizo, bali yata expose financial dealing za Trump!

Collusion kwa mujibu wa wanasheria si kosa isipokuwa ushiriki conspiracy ni kosa.
Hakuna ajuaye nini Mueller alicho nacho hivyo kusema kuna au hakuna collusion si sahihi

Mtu akisema hakuna collusion lazima aonyeshe ni kwa mujibu wa taarifa gani
Trump kwa kutambua wafuasi wake nje na ndani ya US na uwezo wa kupambanua anapigia debe 'hakuna collusion'

Hata hivyo kuna hofu nyingine imetanda WH.
Hofu ya 'obstruction of justice' kwa kuangalia mtiririko mzima kuanzia kufukuzwa kwa Comey na mengine yaliyofuata

Nixon hakuwa na hatia ya ushiriki wa Watergate bali obstruction of justice, kama ambavyo ngono haikuwa tatizo kwa Clinton bali obstruction of justice

Uchunguzi wa Watergate ulianzia mbali, kilichomsibu Nixon ni Tofauti
Uchunguzi wa Bill ulianzia kwenye land, Monica lakini kilichomsibu ni tofauti

Itaendelea..
 
Mkuu Nguruvi3

Kuna uwezekano Trump akamfukuza kazi Mueller kama ilivuokuwa kwa kina Comey? Ikiwa atafanya hivyo nini itakuwa athari zake?
 
Mkuu Nguruvi3
Kuna uwezekano Trump akamfukuza kazi Mueller kama ilivuokuwa kwa kina Comey? Ikiwa atafanya hivyo nini itakuwa athari zake?
Mkuu, Trump anaweza kumfukuza Mueller kama Nixon alivyofanya 'Saturday Night Massacre, oct 20 '

Kisa cha Nixon ni kuitwa (subpoena) kisheria mbele ya special prosecutor Archibald Cox
Nixon akamuagiza AG kumfukuza Cox. AG na Deputy wake hawakuona,wakajiuzulu

Nixon akamteua Solicitor general ambaye ndiye aliyemfukuza special prosecutor Cox
Taarifa zilizopo Trump alimtuma WH counselor Don Mcgahn kumuagiza AG amfukuze Mueller. Don alikataa, hakuona sababu na anajua nini kilitokea kwa Nixon

Njia inayotumika kwasasa ni kama ya kumuondoa Andrew McCabe kwanza
Anayefuata ni Roseinstein ambaye ni deputy AG anayemsimamia Mueller

Hayo yanafanyika kwasababu mbinu za kum 'frustrate' Sessions ajiuzulu zimeshindikana
Kumuondoa Roseinstein kutawezesha kumteua mtu 'loyal' atakayemfukuza Mueller

Kuanzia sasa utasikia Roseinstein akiandamwa na tayari kuna 'memo' iliyoandikwa na Republican ambayo Nunes ameridhia itolewe hadharani.

Mchakato mzima una ukakasi wame 'cherry pick' page 4 kutoka katika lundo la pages
Kwanini wanafanya hivyo? Ni kuonyesha FBI ni biased katika FAISAL warrant iliyomweka Carter page matatani. Hilo litajenga uwezo wa mambo mawili

Kwanza, public iamini kuna tatizo katika uchunguzi mzima wa Mueller
Pili, kutoa mwanya wa kumfukuza Mueller

Hata hivyo, hiyo ni miscalculation. FBI wamesema hakuna tatizo katika memo
Nunes amekataa kushirikisha vyombo vingine kwasababu issue nzima itakuwa Debunked

Hofu iliyopo sasa hivi inatengenezwa na vitu viwili au vitatu.
Kwanza, kuna kila dalili ya Obstruction of justice kama ilivyotokea kwa Comey
Bahati mbaya Trump alithibitisha kumfukuza Comey kwa Russia

Pili, washirika akina Flynn wanashirikiana na FBI. Kitendo cha wanasheria wa Flyyn kuwaandika wa Trump kwamba wamekata mawasiliano kina maana ana cooperate na FBI

Tatu, idadi ya wanaotoa ushirikiano FBI ni kubwa wakiwemo maafisa wa WH na kampeni

Trump na wanasheria wake hawaelewi hao wanaotoa ushirikiano wanaeleza nini
Wakati huo huo Mueller anaelekea kumhoji Trump 'deposition'

Kuna mswada unaandaliwa ili kumlinda Mueller asifukuzwe na Trump.
Kama mswada huo utapita basi hakutakuwa na namna bali kusubiri matokeo

Kosa linalofanyika la kuwatimua akina Comey na McCabe litavujisha habari nyingi
Swahiba wake Steve Banno alieleza hili katika mahojiano juu ya Comey

Katika wiki au mwezi utasikia media zikiwa na breaking news, subiri

Trump ana hofu si kwa Russia investigation. Pengine hakuna ushirika kati yake na Russia wenye uhalifu 'conspiracy' ingawa ushahidi wa collusion wanasheria wanasema si 'crime'

Kuna hofu ya obstruction of justice, kauli na tweet za Trump zinaipa hoja nguvu
Ile draft ndani ya Air force one kuhusu Don Jnr na utata wa mkutano Trump Tower ni sehemu tu

Kuna hofu ya money laundering ambayo inaweza kuibua deal za Trump ikiwemo uhusiano wa investment zake Russia, tax return n.k.

Steve Bannon katika kitabu cha fire and fury alieleza kuhusu Don Jr atakavyokaangwa kama mayai. Banno anaelewa jambo gani kuhusu pesa?

Pamoja na hayo bado kuna makosa ya kifundi, kwa mfano, vikwazo dhidi ya Russia vilivyopitishwa na congress kwa wingi,Trump amekataa kuvitekeleza

Ndipo maswali yanakuja, ni kwanini amekuwa laini kwa Russia? Kuna quid pro quo?

Kudharau maamuzi ya congress kunaweka wakati mgumu wa kumfukuza Mueller
Moderate Republican wanaungana na Dems kuiona dharau na shaka ya uswahiba na Russia

Wakati Trump akiwa moto kwa North Korea, wiki hii meli za Russia zimezengea fukwe za US Trump akiwa kimya. Yote ukiyaweka katika kapu yanpunguza kuungwa kwake mkono

Moderate Rep wanaondoka kambi ya Trump taratibu kutokana na mtiririko wa matukio

Salama ni kumfukuza Mueller, investigation ikiisha hasa ya Mueller itaibu japo jambo
Ili kumfukuza Mueller lazima dept of justice ihusike, bila kumuondoa Roseintein, ni ngumu

Nini kitatokea, tutajuzana

Tusemezane
 
Taarifa zilizopo Trump alimtuma WH counselor Don Mcgahn kumuagiza AG amfukuze Mueller. Don alikataa, hakuona sababu na anajua nini kilitokea kwa Nixon

Hizo ni taarifa kutoka anonymous source.

Njia inayotumika kwasasa ni kama ya kumuondoa Andrew McCabe kwanza
Anayefuata ni Roseinstein ambaye ni deputy AG anayemsimamia Mueller

Kwanini McCabe anaondolewa siku moja baada ya Wray (Director FBI) kwenda Capital Hill na kuona kilichomo ndani ya memo? Kama Roseintain anahusika na matumizi ya kisiasa ya vyombo vya usalama kwanini asiondolewe? Au ukishakuwa Deputy AG ndio huwezi kupatikana na hatia?

Huyu McCabe anayetetewa hapa ndiye aliwaagiza maafisa wa FBI kutochunguza Foundation ya Hillary Clinton. Mke wake alipokea $700,000 kutoka kwa Super Pac ya Hillary. Halafu bado DOJ ya Obama ilimuweka kama mmoja wa wachunguzi wa Hillary kwenye sakata ya e-mail za Hillary, wala hakuji-recuse. Si ajabu Hillary alikuwa exonerated hata kabla ya kufanyiwa interview na FBI!!

Hayo yanafanyika kwasababu mbinu za kum 'frustrate' Sessions ajiuzulu zimeshindikana
Kumuondoa Roseinstein kutawezesha kumteua mtu 'loyal' atakayemfukuza Mueller

Mueller kama ataondolewa sio kwa sababu mtu loyal kwa Trump ameteuliwa kuwa Deputy AG, hapana! Ni kwa sababu huyu mtu ana 'conflict of interest' zilizo so clear ambazo zinamfanya asiwe mtu sahihi kufanya huo uchunguzi anaoufanya kwa sababu ya biasness.

Kuanzia sasa utasikia Roseinstein akiandamwa na tayari kuna 'memo' iliyoandikwa na Republican ambayo Nunes ameridhia itolewe hadharani.

Kwanini Democrats wote walio kwenye House Intel. Committee walikataa hiyo memo isitolewe hadharani? Umemsikiliza Rep. Adam Schiff (Top dem kwenye House Intel committee) sababu alizotoa kuhusiana na hiyo memo-release iliyoidhinishwa na House Intel Committee?

Kwani kuna wasiwasi gani ikitolewa hadharani?

Roseintain ndiye aliye approve FISA warrant kwa ajili ya kum-spy Carter Page.

Roseintain kama alitumika vibaya kisisasa dhidi ya Trump na team yake kwanini asiandamwe?

Mchakato mzima una ukakasi wame 'cherry pick' page 4 kutoka katika lundo la pages
Kwanini wanafanya hivyo? Ni kuonyesha FBI ni biased katika FAISAL warrant iliyomweka Carter page matatani

Kama wana-cherry pick kurasa nne umesikia Democrat (Senator au Representative) akisema zitolewe hizo lundo zote? Hata hizo chache zenyewe hawataki zitoke.

Biasness ya FBI inakuja baada ya FBI kupotosha Mahakama ya Foreign Intelligence Surveillance Act (FISA) kwa kutotoa taarifa kuwa ushahidi waliotumia kudai FISA warrant kwa Carter Page ulitokana na dossier za Steele (aliyepewa kazi na Fusion GPS ambao nao walipewa kazi na chama cha Democrat kuchunguza uhusiano wa Trump na Russia).

Haya mambo ya vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kisiasa wenzetu hawajazoea, haya mambo yapo sana nchi za dunia ya tatu. Rais Obama alitumia kila njia kumzuia Trump kuingia ikulu, DOJ na FBI ilitumika sana kisiasa. Na Obama ana historia hiyo toka kipindi IRS (Internal Revenue Service) walipotumika ku-target conservatives.

Hilo litajenga uwezo wa mambo mawili.
Kwanza, public iamini kuna tatizo katika uchunguzi mzima wa Mueller
Pili, kutoa mwanya wa kumfukuza Mueller

Hapa sio suala la Public kuamini, hapa ni suala la Public kuchunguza Facts halafu waone nani anastahili kuwajibishwa.

Kama Je, ni wale wa Trump-Russia collusion (hoax) au ni wale waliotumia madaraka yao na vyombo vya usalama na taasisi za nchi kisiasa?

Hii itatupa picha kamili hasa kinachochunguzwa na Mueller, kama ni kitu ambacho kimetengenezwa au sio, na kama kimetengenezwa kunakuwa hakuna haja ya kuendelea na uchunguzi hewa chini ya Mueller badala yake wahusika wa hoax wanawajibishwa.

Hata hivyo, hiyo ni miscalculation. FBI wamesema hakuna tatizo katika memo

Director wa FBI, Christopher Wray alitoka Capital Hill kuchunguza kilichomo kwenye Memo, masaa machache baadae Deputy Director wake Andrew McCabe anaondolewa. Hapo unasemaje FBI wamesema hakuna tatizo?

Nunes amekataa kushirikisha vyombo vingine kwasababu issue nzima itakuwa Debunked

Memo itakuwa de-classified kila mtu ataweza kuona ina nini ndani yake. Rais Trump anayo siku tano (5) kutoa approval ya kuachia memo hadharani. Nadhani isingekuwa 'State of the Union' angeiachia hata leo.

Hofu iliyopo sasa hivi inatengenezwa na vitu viwili au vitatu.
Kwanza, kuna kila dalili ya Obstruction of justice kama ilivyotokea kwa Comey
Bahati mbaya Trump alithibitisha kumfukuza Comey kwa Russia

Ikishathibitika kuwa uchunguzi wa Trump-Russia collusion ni hoax na ilitengenezwa kisisasa, kunakuwa hamna hicho kinachoitwa 'obstruction of justice' kwa Trump. Hiyo memo inasemekana kuna watu wengi humo walitumika kisiasa dhidi ya Trump, Comey mwenyewe, McCabe, Roseinstein n.k. Kwa kifupi uchunguzi utafungwa rasmi na waliotumika kisiasa watawajibishwa.

Pili, washirika akina Flynn wanashirikiana na FBI. Kitendo cha wanasheria wa Flyyn kuwaandika wa Trump kwamba wamekata mawasiliano kina maana ana cooperate na FBI

Mkuu, hivi kweli unadhani washirika wa Flynn na Trump hawawasiliani?

Tatu, idadi ya wanaotoa ushirikiano FBI ni kubwa wakiwemo maafisa wa WH na kampeni. Trump na wanasheria wake hawaelewi hao wanaotoa ushirikiano wanaeleza nini. Wakati huo huo Mueller anaelekea kumhoji Trump 'deposition'

Big news hapa ni kuwa uchunguzi wa Mueller ni hoax. Wakati unawaza 'deposition' ya Trump inabidi uangalie Facts tu mpaka hapa tulipofikia.

Democrats wengi tu wanasema hamna evidence ya Russia collusion. Of course, then wakarukia 'obstruction of justice' ambako nako wanaona giza, sahivi wanazungumzia tax returns na 'money laundering'. I hope huu uchunguzi feki utasitishwa ili kuokoa fedha za walipa kodi zinazoenda bure.

Kuna mswada unaandaliwa ili kumlinda Mueller asifukuzwe na Trump.
Kama mswada huo utapita basi hakutakuwa na namna bali kusubiri matokeo

Hata kama huo muswada utapita kama Democrats wanavyotaka, kama Mueller anafanya uchunguzi hewa haitamsaidia maana hakutakuwa na haja ya kumzuia 'asifukuzwe na Trump' kwa sababu kutakuwa hakuna uchunguzi.

Kosa linalofanyika la kuwatimua akina Comey na McCabe litavujisha habari nyingi

Unachokiona ni 'obstruction of justice' peke yake katika suala zima la Comey na McCabe kuondolewa? Hauoni mengine? Ila nadhani baada ya memo kuwekwa hadharani utaweza kuona mengine.

Swahiba wake Steve Banno alieleza hili katika mahojiano juu ya Comey

Steve Bannon leo ni credible source kwa liberals? Unafiki hauwezi kuisha! Kwa kumponda kote huko kabla hata hajateuliewa kuwa WH Chief Strategist, leo hii anaonekana mtu wa maana? Ama kweli adui wa adui yako ni rafiki yako!

Katika wiki au mwezi utasikia media zikiwa na breaking news, subiri

Breaking News zitatokana na ukweli kwamba uchunguzi wa Mueller ni hoax na watu watajiuzulu wengi tu, Andrew McCabe kaanza wengi tu watamfuata. Ila mwishowe atakaeumbuka kuliko wote ni Rais mstaafu Obama.

Trump ana hofu si kwa Russia investigation. Pengine hakuna ushirika kati yake na Russia wenye uhalifu 'conspiracy' ingawa ushahidi wa collusion wanasheria wanasema si 'crime'

Ohh kumbe sasa hivi kuna uwezekano 'hakuna ushirika kati ya Trump na Russia na ushahidi wa collussion si crime'? Hii kauli inatoka kwa waliobebea bango suala zima la Trump-Russia collusion toka lilipoanza!!

Mlianza na Russia wali-hack vifaa vya uchaguzi katika majimbo ya Wisconsin, Michigan and Pennsylvania, mkatoka kapa. Leo Russia Collusion ishaonekana chenga, mmerukia wapi sasa?

Kuna hofu ya obstruction of justice, kauli na tweet za Trump zinaipa hoja nguvu
Ile draft ndani ya Air force one kuhusu Don Jnr na utata wa mkutano Trump Tower ni sehemu tu

Mmerukia 'obstruction of justice'. Kimsingi, hivi sio vitu viwili tofauti, kwa sababu hiyo justice inayodhaniwa kuwa imekuwa obstructed inatokana na investigation ambayo ishaonekana chenga!! Swali la msingi ni kuwa Trump anawezaje ku-obstruct justice kwa kitu ambacho kimetengenezwa?

Kuna hofu ya money laundering ambayo inaweza kuibua deal za Trump ikiwemo uhusiano wa investment zake Russia, tax return n.k.

Mmerukia na huku kwenye 'money laundering na tax returns'? Ama kweli Trump anatafutiwa kosa lolote sasa!! Hii yote kisa Hillary (mwanasiasa mzoefu) alishindwa uchaguzi na mtu ambaye hajawahi kufanya kazi serikalini na akalia machozi!

Je, mkimkosa huko kwenye money laundering na tax return, mtarukia wapi? Au popote tu ili mradi uchunguzi uwepo?

Steve Bannon katika kitabu cha fire and fury alieleza kuhusu Don Jr atakavyokaangwa kama mayai. Banno anaelewa jambo gani kuhusu pesa?

Unawezaje kutumia kitabu cha 'white Supremacist' kama Steve Bannon kutetea hoja yako? Ukizingatia kitabu chenyewe kiliandikwa na Michael Wolff ambaye Democrats wengi tu akiwemo Obama walimponda na kum-discredit?

Pamoja na hayo bado kuna makosa ya kifundi, kwa mfano, vikwazo dhidi ya Russia vilivyopitishwa na congress kwa wingi,Trump amekataa kuvitekeleza. Ndipo maswali yanakuja, ni kwanini amekuwa laini kwa Russia? Kuna quid pro quo?

The last time Rais Obama alikuwa soft kwa Russia alikutana na Republicans na Democrats waliomuambia hayupo strong kwa Russia. The same way Rais Trump anakutana na Congress inayomuambia yale yale. Swali ni Je, kipindi Obama alivyokuwa analalamikiwa kuwa yupo weak kwa Russia kulikuwa na quid pro quo?

Bado hujagundua kuwa suala la Russia linatumika sana kisiasa US?

Kitu kikipitishwa na Congress kwa wingi hakimaanishi kuwa Rais naye anatakiwa kukipitisha bila kukiangalia kwa undani kwa mda wake!! Ndio maana Rais ana uwezo wa ku-veto au kukataa kutekeleza jambo.


Kudharau maamuzi ya congress kunaweka wakati mgumu wa kumfukuza Mueller
Moderate Republican wanaungana na Dems kuiona dharau na shaka ya uswahiba na Russia

Mueller hatafukuzwa na Trump, ajajifukuzisha mwenyewe, itakapobainishwa hadharani kuwa anachunguza hoax au hafai kufanya uchunguzi dhidi ya Trump.

Wakati Trump akiwa moto kwa North Korea, wiki hii meli za Russia zimezengea fukwe za US Trump akiwa kimya. Yote ukiyaweka katika kapu yanpunguza kuungwa kwake mkono

Yaleyale, 'anatakiwa awe strong kwa Russia'. Obama aliimbiwa sana huu wimbo mwanzoni mwa utawala wake. Hivi kwani Russia nao wamesema wanataka kushambulia US?

Hizo habari za Meli za Russia zimetoka Pentagon na State Dept walisha-respond. The same way leo Ndege ya Russia imekaribia ndege ya Navy ya US futi tano juu ya Black Sea kwenye anga za kimataifa na State Dept wametoa onyo. Kesho unaweza kusikia manowari ya US imekaribia Crimea then Russia wanatoa onyo. Russia hawezi kushambulia US.

Rais Trump hayupo kimya, anaandaa State of the Union atakayoitoa leo.

Moderate Rep wanaondoka kambi ya Trump taratibu kutokana na mtiririko wa matukio

Moderate Republicans wamesaidia kupitishwa kwa bill ya mabadiliko ya kodi, na wapo pamoja na Trump kwenye Immigration reform proposal ambayo Trump ameweka mezani. Pia kuna Democrats wanaenda kwenye mid election mwaka huu, wengi wao wanatiririka kwa Trump.

Salama ni kumfukuza Mueller, investigation ikiisha hasa ya Mueller itaibu japo jambo
Ili kumfukuza Mueller lazima dept of justice ihusike, bila kumuondoa Roseintein, ni ngumu

Mueller atajiondoa mwenyewe kwenye huu uchunguzi wala hamna atakayemuondoa. Roseinstein naye atajipima then atafanya maamuzi sahihi, ambapo anaweza kujiondoa pia.

Suala la matumizi ya vyombo vya ulinzi na usalama kisiasa ni suala ambalo linapaswa kukemewa na watu wote wanaopenda demokrasia na haki. Hasa pale ambapo chama tawala kinafanya hivyo dhidi ya chama cha upinzani kama ambavyo Obama (Democrat) alivyofanya kwa Trump (Republican) ili kujaribu kumsaidia Hillary kushinda uchaguzi.
 
Hizo ni taarifa kutoka anonymous source.
Mueller atajiondoa mwenyewe kwenye huu uchunguzi wala hamna atakayemuondoa. Roseinstein naye atajipima then atafanya maamuzi sahihi, ambapo anaweza kujiondoa pia.

Suala la matumizi ya vyombo vya ulinzi na usalama kisiasa ni suala ambalo linapaswa kukemewa na watu wote wanaopenda demokrasia na haki. Hasa pale ambapo chama tawala kinafanya hivyo dhidi ya chama cha upinzani kama ambavyo Obama (Democrat) alivyofanya kwa Trump (Republican) ili kujaribu kumsaidia Hillary kushinda uchaguzi.
[B]El Jefe[/B], historia hujirudia, mechi kama hii iliwahi kuchezwa huko nyuma na matokeo tunayajua. Tofauti ni kwamba mwindwa wa wakati huo kwa sasa ndiye mwindaji na mwindaji wa wakati huo sasa ni mwindwa.

Mimi najaribu kufuatilia kwa makini sana kinachoendelea na ndio maana siongei sana kwa sasa. Siasa za Marekani ni za kiwango kingine kabisa...stay tuned! Kama una popcorn kaa mkao wa kula, mimi tayari nimewahi seat!
 
Mkuu Nguruvi3 Kuna uwezekano Trump akamfukuza kazi Mueller kama ilivuokuwa kwa kina Comey? Ikiwa atafanya hivyo nini itakuwa athari zake?
[B]Mwalimu[/B], Trump hatamfukuza Mueller, lengo ni kumfanya awe frustrated hadi ikiwezekana aachie ngazi mwenyewe. Historia imemzuia kumfukuza ingawa alikuwa tayari kufanya hivyo kwa vision yake fupi wahenga wakamtonya.
 
Back
Top Bottom