Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

ACCESS HOLLYWOOD TAPE YARUDI KWA SURA MPYA
STORMY DANIEL ALETA 'STORM' WH
TIMUA TIMUA NI TAMU CHUNGU ' NGUMU KUMESA'

Access hollywood tape ni video iliyotoka wakati wa uchaguzi ikimuonyesha mgombea Trump alivyowazungumzia vimwana waliofika kumlaki akiwa na washirika wake. Ni tape iliyoonekana kuhitimisha kampeni za Trump

Kuna kitu kilitokea siku ambayo TV zilionyesha tape kwa umma. Kwamba, habari ilikuwa kubwa kwa muda mfupi kwani siku hiyo hiyo emails za Democrats za akina Podesta na Hillary zilitoka

Email zilitolewa na Wikileaks. Hapo ndipo uhusiano wa Hollywood tape-Wikileaks-Russia- Democrats emails unapofikirisha wachunguzi. Timing ya kutoa emails hizo ilikuwa mahususi kupunguza nguvu ya hollywood tape

Hollywood tape inarudi kwa mlango mwingine. Kwamba, upekuzi uliofanywa kwa Michael Cohen, wakili wa Trump ulihusisha mawasiliano ya Trump na wakili Cohen, kwa mujibu wa vyombo vya habari.

Mtifuano kati ya Stormy Daniel,kahaba, anayedai kummegea penzi Rais Trump, lilimvuta mchunguzi Mueller kujiridhisha kama kuna lolote kuhusu uhusiano wa Cohen-Trump-Stormy na dolari 130,000
Kumbuka Cohen alimpa Stormy 130K kama kiziba mdomo siku chache kabla ya uchaguzi

Hilo likapelekea Mueller kuwa na hisia za 'uhalifu' na kuwakabidhi FBI ambao baada ya kupata vibali husika walimpekua wakili Cohen. Hapa ndipo Rais Trump anapowaka moto kwani yanaweza kuibuka yasiyotarajiwa

Upekuzi unarudisha hollywood tape kwa kuunganisha na vipande,haijulikani kwanini Trump ameingiwa na wahka Njia iliyobaki ni kuua uchunguzi wa Mueller. Wapi kuanzia? Ni kwa Rosenstein

Tatizo linalomkabili Rais Trump ni kujenga uhalali wa kumuondoa Rosenstein na kisha Mueller.
Bila kuwa na sababu za kuridhisha hilo litazaa tatizo jingine la obstruction of justice ambalo ni tatizo kubwa
Obstruction of justice itakuwa tatizo la pili baada ya lile la kumtimua James Comey alililkiri kuwa alifanya hivyo

Hivyo tatizo linalomsumbua Rais Trump ni jinsi ya kuwatimua watu wawili, deputy AG-Rosenstein na Mueller
Kwa mbali congress inasema kuwatimua hao kutazua balaa jingine linaloweza kuhitimisha safari ya Don

Tayari kamati ya sheria ya seneti inaandaa mswada wa kumlinda Mueller, mswaada ambao Republican wamekataa usiowepo kwa muda mrefu. Hofu ya Republican, ikitokea tatizo watabeba lawama

Kwa vile kuna uchaguzi wa kati 'midterm election' November, uwezekano wa kupoteza mabunge yote upo

Hapa kuna mtego, kwamba Republican katika senate na congress wanaweza kupoteza viti vyao, lakini pia hali si njema kwa Rais Trump, Democrats wakichukua congress yote, ''impeachment is imminent ''

Kuna swali watu wanajiuliza, kahaba Stormy anataka nini hadi kumsumbua Rais Trump kiasi hicho ili hali amesema alitoa penzi la mchepuko kwa ridhaa na wala hahitaji fidia. Sasa kisa kinachomsumbua ni kipi?

Tujadili hili kwa ufupi

Tusemezane
 
STORMY ANATAKA NINI KINACHOSABABISHA AMSUMBUE RAIS TRUMP?
KAREN McDougal naye ana yake

Kwa ufupi, Stormy anaendesha maisha yake kama star katika picha za ngono.
Hadi sasa anaendelea na show zake na hasa baada ya timbwili lake na WH, show zake zinafurika.

Stormy alimgea penzi Rais Trump miaka zaidi ya 10, wakati huo tajiri Trump akimfanya mchepuko

Katika mazingira tata ya uchaguzi, wakili wa Trump alimlipa kifunga mdomo siku chache kabla ya uchaguzi.
Stormy anakiri hilo na kwamba walikuwa na mkataba huo

Bibie anasema, toleo la penzi halikuwa na shinikizo, ilikuwa ridhaa yake na yeye si miongoni mwa 'MeToo movement' Anasema hakupata shinikizo wakati wa faragha na kila jambo lilikwenda sawia na salimini

Kinachomsumbua ni kuwa habari zimevuja na hivyo angependa aweke rekodi sawa.
Kwamba, aliwahi kula maraha na mzee. Hilo tu, hahitaji kishikizo chochote, anajitosheleza kifedha

Sasa kama ni hivyo, kwamba, penzi lilitoka kwa tajiri miaka 10 na kwa ridhaa ya bibie, nini kinawahusu wachunguzi hadi kuingilia mambo ya kifamilia yaliyofanyika hata kabla Trump hajawaza Urais?

Wakili wa Trump bwana Cohen ameingia katika malumbano na Stormy kupitia wakili wake Avennati
Cohen anasema, ni kweli alitoa 130,000 kwa Stormy lakini si kwa ajili ya penzi alilomgea mzee Trump

Hapa ndipo malumbano yalipo, kwamba, Cohen alitengeneza kampuni ikafanya malipo akafunga kampuni!

Hili nalo si tatizo ikiwa aliamua kutoa pesa, lakini je, wakili anagawa dolari kama njugu bila sababu?
Ni wapi wakili aliwahi kumlipia mteja gharama za ku settle kesi na kama alifanya hivyo ni kwa malipo gani?

Malumbano baina yao mahakamani ndiyo yaliyovuta wachunguzi. Kuna maswali mengi kuliko majibu.

Kwanza, muda wa malipo ulikuwa wakati wa uchaguzi. Je, fedha zilitoka mfukoni mwa Trump au zilitoka katika kampeni ya Trump? na kama zilitoka mfukoni, kwanini ilifunguliwa kampuni kisha kufungwa?

Kwa sheria za Marekani kila senti ya uchaguzi lazima ijulikane imetoka wapi.
Bila kuonyesha ni kukiuka sheria za uchaguzi. Hapa ndipo wachunguzi wanazidi kuvutika ili kupata jibu

Wachunguzi wanakwenda mbali kuona mahusiano ya Trump na wakili Cohen, hakuwa sehemu ya kampeni.
Je, malipo aliyofanya yalikuwa na mahusiano na mambo ya uchaguzi na kwanini hayakuorodheshwa?

Mvuto zaidi nikutaka kumjua Cohen kwani kumpuuza ni kosa kama la kuamishwa Papadopolous alikuwa mgawa kahawa katika kampeni. Imedhihirika alikuwa muhimu na chanzo cha uchunguzi wa Russia na wala siyo Dossier

Kumchunguza Cohen ndiko kumepelekea pekua pekua ya FBI ambaypo haijulikani imetoka na nini
Ndivyo Stormy anamwingiza Rais Trump katika wakati mgumu sana kwa namna anavyoonekana ku-panic

Tatizo si penzi, anakiri bibie Stormy! Tatizo si shinikizo, anasema ni alikuwa radhia!
Tatizo si Russia hayo hayamhusu yeye ni porn star. Tatizo si pesa hahitaji malipo.
Tatizo si madaraka yeye si mwanachama wa siasa

Stormy anakiri, alijua Tajiri Trump alikuwa na mke, alichokifanya ni kuchepuka kutoka baraba kuu, na kwamba ni kweli alimgea tunda tena akionyesha DVD kwa kusema 'if a picture worth 1000 words, what about DVD'?

Tatizo la yoote ni nyayo za mgegedo zinazoelekeza wafukua 'makaburi' kuelekea kwingine

Tusemezane
 
LEO KATIKA SIASA ZA US

KAMPENI YA KUMDHALILISHA ROSEINSTEIN NA MUELLER
JAMES COMEY KUTOKA NA KITABU KUHUSU YALIYOJIRI
RAIS TRUMP APIGA U-TURN MKATABA TRANS-PACIFIC PARTNERSHIP

Kumekuwa na kampeni za kumdhalilisha deputy-AG Rosenstein na Special counselor Mueller
Baada ya upekuzi kutoka kwa wakili Cohen, hali si shwari ndani ya jumba jeupe 'WH'

Kampeni inafanyika kuaminisha umma hakuna collusion hata kama haijulikani ni kwa kigezo au uchgunguzi gani
Haya ni maandalizi ya kumwezesha Trump kuwatimua wahusika na kuzika uchunguzi wa Russia

Chagamoto, hakuna ajuaye ni kiwango gani hatua hiyo inaweza kuzua sekeseke na athari zake

JAMES COMEY
FBI Dir James anakuja na kitabu kitakachoeleza mengi kuhusu Trump.
Kwa mujibu wa Washington post, sehemu ya kitabu imeanza kutolewa katika harakati za kukinadi

Huko nyuma tulieleza kumtimua kazi Comey halikuwa kosa kwa mamlaka ya Rais wa US
Tatizo ni namna gani timua hiyo ilifanyika na kwa kutumia vigezo gani

Comey analalamikiwa na pande zote, Dems na kampeni ya Trump.
Rais alipaswa kuwa mwangalifu kwa namna alivyomtimua hasa kwa kumdhalilisha

Ilikuwa ni dhahiri alikuwa na malengo na alitaka kutumia FBI kumalizana na matatizo yake
Ugomvi wake na Comeny na McCabe wenye kujua mengi, hautmwacha bila athari. Kitabu kitaeleza

TRANS-PACIFIC PARTNERSHIP
Moja ya mikataba iliyopingwa na Rais Trump wakati wa kampeni ni Trans-pacific partnership akiuita mkataba wa kipumbavu uliofanya na Rais Obama. Trump aliaufuata na mwezi July wakiiacha China kama kiongozi

Mkataba ulifanyiwa tathmini ya kiulinzi na kiuchumi na Rais Obama. Kwa maana, ili kukabiliana na nguvu za uchumi kutoka China, ni muhimu kuwepo na udhibiti wa washirika ili kupunguza nguvu

Katika mtiririko wa mabandiko tuliwahi kueleza kuwa mivutano ya nchi za Iran/Russia/China/North Korea/ na mashariki ya kati yana mahusiano makubwa Marekani na anachokifanya kitakuwa na athari

Vita ya biashara aliyoanzisha Rais Trump inawaathiri wapiga kura wake.
Wakati anaweka tariff kwa nchi ya China, nchi hiyo imelipiza kisasi kwa tariff kutoka wapiga kura wa Trump

Hatua ya Trump inaonekana ku backfire kuliko kuleta tija huku ikiweka masoko katika mihemuko
Kupoteza thamani kwa masoko kama DJ kunaondoa maana ya matokeo ya tax cut. Trump amekiri hilo

Katika tathmini, gazeti la WSJ linasema Rais Trump ameagiza maafisa wake kufikiria kujiunga tena na Trans-pacific partnership. Pengine ni baada ya kubaini kuwa US inaendelea kujitenga na kupoteza ushawishi wake

Hatua hiyo ina madhara katika mikataba mingine. Mazungumzo ya NAFTA hayaonekani kufikia kikomo hivyo Canada na Mexico zitapata nguvu ya majadiliano kwa kubaini Marekani inatikiswa na mikataba

Paris agreement ambayo US ilijitoa itaendelea kwa kuelewa Marekani inapoteza ushawishi na kwamba ile dhana ya America first inakuwa America alone na inatikisa Taifa hilo

Tayari US imepoteza ushawishi kwa suala la Israel-Palestina. Uhusiano na nchi washirika wa Ulaya unasua sua
Ushawishi wa nchi za Ujerumani,Ufaransa na China unaongeza. Mkataba wa Iran unabaki kama ulivyo

Hayo yanatuacha na swali moja

Je, kwa siasa za Rais Trump na sera za twiiter kabla ya sera kuandikwa, unatoa ushawishi au unapunguza ushawishi wa Taifa hilo katika siasa za dunia kiuchumi na usalama?

Tusemezane
 
MWISHO WA WIKI KATIKA SIASA ZA US

SAKATA LA MICHAEL COHEN NA FBI
SHAMBULIZI LA SYRIA KUTOKA US, US NA UFARANSA

Hati ya mashtaka ya wakili binafsi wa Rais Trump imetolewa akikabiliwa na 'shtaka la uhalifu'
Pekua pekua imeondoka na nyaraka na mikanda ya mawasiliano kati ya Cohen na wahusika wengine

Kushtakiwa kwa wakili Cohen kuna mtia hofu Rais Trump na timu yake ya wanasheria kwakujua kuwa cohen alikuwa ni 'fixer' kwa maana ya mpambe wa madili. Ni madili yapi, haijulikani, hivyo ni kama 'kufungua milango'

Kumbuka Cohen ni wakili pekee kwa Trump na msiri wa muda mrefu. Kukamatwa mawasiliano yake na FBI si jambo jepesi kwani mengi hata yaaliyo nje ya mijadala yanaweza kuibuka

Rais Trump amelalamikia FBI kuingilia mahusiano ya wakili na mteja yanayopaswa kuwa siri (Attorney-Client privilege) Kwamba, wakili ana haki ya kuhifadhi siri za mteja isipokuwa kama mteja ataridhia kutolewa

Kwa haraka haraka ni kweli, kuingilia mawasiliano ya wakili-mteja yanayopaswa kuwa siri si sahihi
Hata hivyo, Wakili Cohen na Rais Trump wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa kutoa fursa ya kuingiliwa

Cohen alinukuliwa akisema pesa alizompa kahaba Stormy hazikutoka kwa Bwana Trump
Naye Trump alipoulizwa kuhusu mahusiano ya fedha alijibu 'hajui lolote labda wamuulize wakili Cohen'

Kwa maana hizo mbili, ni wazi hakuna mahusiano ya siri ya Cohen na Trump kwasababu Cohen amekana pesa hazikutolewa na Trump, na Trump akisema hajui lolote kuhusu pesa. Kama ni hivyo, siri itatoka wapi?

Lakini pia sheria za US zinasema attorney-client haiwezi kulinda uhalifu ikiwa wakili mhusika katenda.

Kinachofanywa sasa hivi si kuingilia mahusiano ya wawili hao bali kumchunguza Cohen kama mhalifu
Katika uchunguzi huo, client hawezi kulindika kwasababu uchunguzi unamhusu wakili mtuhumiwa

Somo linalopatikana hapa ni kuhusu kauli wakati mhusika yoyote anapokuwa katika uchunguzi.
Kauli ya Trump ilionyesha kumkana Cohen, huku wakili Cohen akimuondoa Trump katika zozo la kahaba

Kwa sura nyingine, tukio hili licha ya kuleta taharuki ya kimahaba, tuhuma za kukiuka sheria za uchaguzi n.k. linamweka Rais Trump katika wakati mgumu kwa kuzingatia anataka kumtimua Deputy AG Rosenstein na Bob Mueller wanaochunguza suala la Russia.

Kuwatimua wawili hao kutahitimisha uchunguzi au kuwa mwanzo wa mwisho wa Urais, itategemea congress ita react vipi

Kwa hili ambalo FBI wanalishikilia, Trump hana namna ya kuwatimua kazi kwani kufanya hivyo ni obstruction of justice bila kupepesa macho. Nini maana yake? Ni kuwa kuuzima uchunguzi wa Russia kunakuwa kugumu zaidi

Inaendelea sehemu ya II, Shambulizi la Russia
 
Sehemu ya II

SHAMBULIO LA SYRIA

US, UK na France wameshambulia sehemu za Damascus kilichosema ni kutekeza maeneo kutengeneza silaha za sumu zilizotumika katika mji ulioshikwa na waasi

2017 muda kama huu, kulitokea matumizi ya silaha za sumu dhidi ya waasi, Rais Trump alituma makombora

Haikujulikana tija ya makombora.Ni wakati huo Marekani ilitumia bomu la MOAB kwa utani 'mother of all Bombs', kiuhalisia ni massive ordinance air ballistic, maeneo ya Afghanistan.
Ilikuwa msimu wa piga piga kutishia dunia, wakisema 'there's a new sheriff in town'

Shambulio la juzi halikuwaridhisha Russia na kwa mbali China.
Kubwa zaidi kuna maswali yanayoulizwa katika viunga vya DC kuhusiana nalo

Je, inatosha kumshambulia Assad kwa mabomu? Mbona alishambuliwa na karudia tena kutenda hilo?
Je, Marekani na washirika waingilie kati kumuondoa Assad? Jibu linalowatatiza ni la Gadafi, lakini pia Assad anawapiga ISIS ambao ni 'waasi' kwa namna nyingine

Je, Marekani iingie katika vita mpya? Kumbukumbu za Iraq bado zipo, hilo linawatia shaka
Nini sera za Rais Trump? Hapa ni kutokana na kutokuwa na sera , kubadili misimamo na kuyumba yumba

Wiki iliyopita Rais Trump alisema ni wakati US waondoke Syria na kuachia wengine wa'take care'.

Kauli hiyo aliitoa bila kuwasiliana na vyombo vya usalama na kwamba hakukuwa na sera yoyote ya nini kifuate

Baraza la usalama lilimweleza, Syria ikiwa middle east ina masilahi mapana na nchi ya Marekani, kukimbia si sawa

Mwaka 2013 Syria ikiwa na vita yake, Rais Trump kiwa Raia alimshambulia Rais Obama kuwa hakuna sababu ya kuingiza wanajeshi Syria kwa vile hakuna masilahi ya Marekani.
Alimuonya Rais Obama kuwa kushambulia Syria bila idhini ya Congress ilikuwa kinyume cha taratibu

Rais Obama aliomba congress iidhinishe kushambulia, na congress chini ya Republican haikufanya hivyo.
Leo Rais Trump ameshambulia nchi isiyo na masilahi na bila ridhaa ya Congress wala hana sera juu yake

Zaidi ya hapo, safari hii ameomba washirika wa Ulaya kusaidia katika mashambulizi kinyume na kauli yake kuwa Marekani inaweza ikiwa pekee. Ni kwali Marekani ina uwezo huo na inanguvu za kufanya hivyo bila msaada

Kitendo cha kushirikisha UK na France ni kuepuka tuhuma za ubabe wa Marekani kutoka jumuiya ya kimataifa. Lakini kubwa ni kutaka kutoonekana kuwa Marekani inashambulia nchi za 'Kiarabu' kwa masilahi ya Israel.

Ukiangalia shambulio na mtiririko wa matukio picha moja inajitokeza bila shaka.
Rais Trump hana ufahamu wa siasa za dunia na kwamba kauli zake za nyuma hazikuwa na uhalisia

Kwanini hazikuwa na uhalisia? Suala la Syria hana tofauti na Obama isipokuwa kurusha mabomu bila malengo
Suala la Iran alilosema ni bad deal ya stupid Obama ameshindwa kulifanya tofauti na lipo vile vile
Israel-Palestina hali ni mbaya kuliko wakati mwingine, US ikipoteza kabisa ushawishi
Rais Trump anairudisha marekani katika mkataba wa TPP, mkataba alioufuta mara moja
Nyuma ya pazia, US inataka kurudi Paris agreement lakini isikilizwe madai yake, washirika wakisema NO!
Sera za nyumbani kama afya na Obamacare zimeshindikana, sasa ni hujuma zishindwe na si mbadala
Suala la watoto wahamiaji DACA limekwama wakati alitangaza kuwaondoa mara moja
Ujenzi wa ukuta unasua sua na Mexico hawatalipa gharama bali walipa kodi wa Marekani
Tishia tishia za Biashara zinaleta madhara, wakati akitaka kurudi TPP, NAFTA inabaki kuwa mwiba

Suala moja watu wanaongelea ni hali ya uchumi kuimarika. Kiuahalisia anayepaswa kupewa pongezi ni Obama aliyeitoa nchi katika mdodoro, recession, akatengeneza ajira na kuweka mifumo ambayo sasa inatoa matunda

Mathalani, wasioelewa wanaambiwa ukosefu wa ajira umefikia kiwango cha chini kabisa kwa miaka 17

Wakati Obama anaingia, baadhi ya maeneo yalikuwa 10% na akiondoka ilifikia takribani 4.7%.

Kwasasa imeshuka hadi 4.1%. Utaona licha ya recession Obama alirudisha takribani nusu, iweje basi mtu aseme ni chini kwa miaka 17?

Katika kutengeneza ajira, takwimu zinaonyesha miezi 74 ya Obama mfululizo na kwamba hakuna tofauti ya kiwango kutokana na hali ya mwezi kwa mwezi

Jambo moja ambalo Rais Trump ana uwezo nalo ni kuuza. Huyu ni salesman kwa asili ya kazi zake za biashara

Anaweza kukuazima shati na akaukuuzia kwa mnada shati lako. Anajua kucheza na akili na maneno

Anapokwama ni pale ambapo kutawala kunakuwa si deal za mitaani,ndipo unaweza kuona matundu

Tusemezane
 
US, UK na France wameshambulia sehemu za Damascus kilichosema ni kutekeza maeneo kutengeneza silaha za sumu zilizotumika katika mji ulioshikwa na waasi

2013 muda kama huu, kulitokea matumizi ya silaha za sumu dhidi ya waasi, Rais Trump alituma makombora
Fact: 2017 na siyo 2013(mwaka huo Trump hakuwa rais)
===
Mpaka sasa nimekubali kuwa US inaedeshwa na Deep State. Mwanzo dhana hii ya Deep state nilihisi ni 'myth'! Ila sasa nimeamini this thing is real. Ni kwa kugeuzwa geuzwa Trump kwenye maamuzi yake. Trump, mtu mwenye 'ego' ya kutisha, kubadilibadili misimamo yake ambayo inahatarisha hadhi yake kama rais kumeniondolea mashaka kuwa kuna nguvu kubwa inayomshinda kusimamia maamuzi yake.

Kwa kifupi, kwa sasa Trump asilaumiwe kwani imedhihirika hana nguvu za kimaamuzi hapo 'Oval office'! Hizi vurugu wanazisababisha wao 'Deep State'! Nadhani kwa sasa Deep State ndiyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho, imechoka, imeshindwa kuweka miongozo sahihi ya US.
 
Fact: 2017 na siyo 2013(mwaka huo Trump hakuwa rais)
Mkuu, unasoma kutafuta spelling erro/ omissions au kupata mantiki!!!

Ukisoma nilichoandika it was obvious nilimaanisha mwaka jana.

Sikumaanisha kupotosha, Trump hakuwa Rais 2013. Soma tena utaona maneno yanayoonyesha MOAB, muda kama huu, Trump etc yakionyesha muda unaoongelewa

Kwa muelewa, bomu la MOAB limetumika mwaka jana wakati wa Trump!

Ahsante kwa sahihisho na sioni kwanini useme fact wakati ni typo error inayoonekana

Angalia contents, contexts and logic itakusaidia sana katika uelewa, ufahamu na majadiliano kuliko kutafuta typo error na kuifanyia hyperbole!!
 
Fact: 2017 na siyo 2013(mwaka huo Trump hakuwa rais)
===
Mpaka sasa nimekubali kuwa US inaedeshwa na Deep State. Mwanzo dhana hii ya Deep state nilihisi ni 'myth'! Ila sasa nimeamini this thing is real. Ni kwa kugeuzwa geuzwa Trump kwenye maamuzi yake. Trump, mtu mwenye 'ego' ya kutisha, kubadilibadili misimamo yake ambayo inahatarisha hadhi yake kama rais kumeniondolea mashaka kuwa kuna nguvu kubwa inayomshinda kusimamia maamuzi yake.

Kwa kifupi, kwa sasa Trump asilaumiwe kwani imedhihirika hana nguvu za kimaamuzi hapo 'Oval office'! Hizi vurugu wanazisababisha wao 'Deep State'! Nadhani kwa sasa Deep State ndiyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho, imechoka, imeshindwa kuweka miongozo sahihi ya US.

Could you please enlighten me the meaning of deep state and how it works against Trump's administration?
 
Could you please enlighten me the meaning of deep state and how it works against Trump's administration?
Anzia hapa kwanza.
----
In the United States the term "deep state" is used within political science to describe influential decision making bodies within government that are relatively permanent and whose policies and long-term plans are unaffected by changing administrations. The term is often used in a critical sense vis-à-vis the general electorate to refer to the lack of influence popular democracy has on these institutions and the decisions they make

source>> Deep state in the United States - Wikipedia

Definition: The hybrid association of elements of government and parts of top-level finance and industry that is effectively able to govern the United States without reference to the consent of the governed as expressed through the formal political process.
------
Waweza kutizama jinsi wanaJF wengine walivyolitumia neno hili kwenye uzi huu.
>>>Ushabiki usio na huruma: Sababu ya wazungu kuwa radicalized dhidi ya wageni
====
How it works against Trump's administration?
---
Trump alchaguliwa kwa sababu alionekana kama atakuja kufumua mfumo huu . Sasa hivi Trump hana tena msimamo, wanamyumbisha tu!
 
Anzia hapa kwanza.
----
In the United States the term "deep state" is used within political science to describe influential decision making bodies within government that are relatively permanent and whose policies and long-term plans are unaffected by changing administrations. The term is often used in a critical sense vis-à-vis the general electorate to refer to the lack of influence popular democracy has on these institutions and the decisions they make

source>> Deep state in the United States - Wikipedia

Definition: The hybrid association of elements of government and parts of top-level finance and industry that is effectively able to govern the United States without reference to the consent of the governed as expressed through the formal political process.
------
Waweza kutizama jinsi wanaJF wengine walivyolitumia neno hili kwenye uzi huu.
>>>Ushabiki usio na huruma: Sababu ya wazungu kuwa radicalized dhidi ya wageni
====
How it works against Trump's administration?
---
Trump alchaguliwa kwa sababu alionekana kama atakuja kufumua mfumo huu . Sasa hivi Trump hana tena msimamo, wanamyumbisha tu!

If you allow a follow up question, please help on this one. If the term deep state translates to what you describe above, why President Trump keep firing his own appointees? He's an outsider and according to the sources you have enumerated above, he was elected to shake up the establishment and with him, he brought a cadre of outsiders such as Fylnn, Tillerson, Scaramucci, Hicks and the list goes on and on. Why Trump can keep his own appointees?
 
Why Trump can keep his own appointees?
I guess this is typo i.e. kwamba ulimaanisha 'Why Trump can not keep his own appointees?'
--------
This is an intriguing question; however, as a recent mere Nguruvi3 student in geopolitics, I can argue that they (establishments) are 'twisting' Trump's arm very awkwardly! For instance, do you believe the Russians compromised the robust US electoral system to favour Mr. Donald ? That is one of the twisting I am trying to put on the spot. The Stormy, the tax...etc etc. it is just twisting. Currently, I guess Trump has already yielded; he has to do what they direct him to do. Otherwise, he (Trump) may succumb to the one term president syndrome.

Kwa kifupi hivyo ndivyo ninavyotazama suala hilo.
 
If you allow a follow up question, please help on this one. If the term deep state translates to what you describe above, why President Trump keep firing his own appointees? He's an outsider and according to the sources you have enumerated above, he was elected to shake up the establishment and with him, he brought a cadre of outsiders such as Fylnn, Tillerson, Scaramucci, Hicks and the list goes on and on. Why Trump can keep his own appointees?
Mzuvendi, could I just chip in if you don't mind? Deep State is just a figment of imagination perpetuated by conspiracy theorists majority of whom have no confidence to the established machinery of justice , law and order. Their main objective is to undermine the system when they feel it is not to their benefit by claiming there is a shadow government controlled by imaginary bureaucrats. In congress fringe rights, centrist observers and leftist critics have all used the term deep state at different periods when things are not going their way but the truth is that in the US there is nothing like DEEP STATE.
 
Da289wmWAAUQJEo.jpg


Congress ya Marekani kwa mbali inafananafanana na Bunge letu kwa sasa...!​
 
I guess this is typo i.e. kwamba ulimaanisha 'Why Trump can not keep his own appointees?'
--------
This is an intriguing question; however, as a recent mere Nguruvi3 student in geopolitics, I can argue that they (establishments) are 'twisting' Trump's arm very awkwardly! For instance, do you believe the Russians compromised the robust US electoral system to favour Mr. Donald ? That is one of the twisting I am trying to put on the spot. The Stormy, the tax...etc etc. it is just twisting. Currently, I guess Trump has already yielded; he has to do what they direct him to do. Otherwise, he (Trump) may succumb to the one term president syndrome.

Kwa kifupi hivyo ndivyo ninavyotazama suala hilo.

That's was a typo. Thanks for the correction. Personally I believe Trump and the media that supports him have deliberately miss-characterized the term deep-state to deflect issues which have engulfed the Trump administration from the beginning. Truly, there's a good number of people within and outside the US government who would like to see Trump go. However, we can't characterize those people, individually or collectively as deep state in the context of the United States politics.

As you have explained in one of your previous posts, the term deep states is used within political science to describe influential decision making bodies within government that are relatively permanent and whose policies and long-term plans are unaffected by changing administrations. Take for example American policies towards Israel, NATO or UK. Those policies don't change. Each administration has executed almost the same policies.

In other countries, on contrary, the term deep state describes the state within the state. Take for example Egypt, Pakistani and Turkey. In these countries, the military (deep states) can dictate the course of the action the civilian government should follow. For instance, the military can tell the civilian government to resign. It can tell the government the amount of money the government should spend in the military and the foreign policy it should pursue.

Now if you make a comparison, you find out that the use of the term deep states in the USA isn't in the same vein as that used in the Turkey, Egypt or Pakistan even though Trump and his media want us to believe the opposite. Trump needs to address every issues that have engulfed his administration head on. He shouldn't try use the term deep states as described in Pakistan to deflect his own issues. It won't work. Moreover, he isn't the first president to be engulfed with various unethical issues. Do you remember Bill Clinton? Throughout his presidency, he fought against various issues, some were real and others imaginary.
 
Could you please enlighten me the meaning of deep state and how it works against Trump's administration?
Nimemuuliza swali hili mara nyingi, hakuwa na jibu
He once mentioned the then SoS Rex Tillerson as a ''deep state'' , i was totally flabbergasted
I couldn't decipher how possible an outsider and Trump appointee could be a deep state!!
The 'deep state' is a misnomer invented by Trump and his cronies to mislead the public
 
I can argue that they (establishments) are 'twisting' Trump's arm very awkwardly! For instance, do you believe the Russians compromised the robust US electoral system to favour Mr. Donald ? That is one of the twisting I am trying to put on the spot. The Stormy, the tax...etc etc. it is just twisting. Currently, I guess Trump has already yielded; he has to do what they direct him to do. Otherwise, he (Trump) may succumb to the one term president syndrome.

Kwa kifupi hivyo ndivyo ninavyotazama suala hilo.
Angalia hapa, umebadilisha position na kusema 'the establishment'. Ndugu yangu the establishment na deep state ni vitu viwili tofauti kabisa.
Msome Mag3 na Mzuvendi kwa umakini na utulivu utajifunza kitu

Kuhusu Russia meddling, hivi kweli hadi sasa huelewi kuwa wanaothibitisha hilo si congress wala media, ni Security and intelligence community ya US.
FBI Chris Wray amethibitisha hilo na huyu kateuliwa na Trump baada ya Comey

Congress imepitisha vikwazo kwa Russia kutokana na meddling kwa more than 95%
Hivi unadhani ukiwa na right wing, conservative, freedom caucus hilo lingetokea kwa bahati mbaya. Please

Kwavile Trump anasema Russia haikubadili matokeo,unabeba maneno yake bila kuangalia
Hakuna anayesema Russia ilibadili kura yoyote kwasababu uchaguzi haupo connected kama hapa kwetu

Na hata sasa hivi hakuna anayeweza kuweka takwimu ni kwa kiasi gani Facebook n.k. walitumika kubadili matokeo hata kama Russia waliweza kubadili mawazo. Ni kitu kigumu ku-quantify

Yote hayo hayaondoi ukweli kuwa intelligence community zimeafiki kuwa Russia ilifanya hivyo.
Na wala si US, hata Ujerumani na Ufaransa Russia waliingia, waliwa wahi mapema baada ya matokeo ya US

Kuna taarifa za UK kufanya utafiti kuhusu matokeo ya Brexit. Naachi hapo
 
For instance, do you believe the Russians compromised the robust US electoral system to favour Mr. Donald ? That is one of the twisting I am trying to put on the spot. The Stormy, the tax...etc etc. it is just twisting
Mkuu kuna wakati nakushangaa kidogo.
Hili jambo nimelizungumzia mabandiko mawili au matatu yaliyopita hasa la Stormy

Stormy na Karen wanasema wamefanya mapenzi na Trump wakieleza hadi vyumba walivyoingia
Michael Cohen, wakili wa Trump amekiri kutoa 130,000$ kuziba midomo

Michael Avinnati, wakili wa Stormy, anasema Trump au wakili wake wasimame kukanusha.
Hakuna anyekanusha. Wanachotaka ni arbitrations nje ya court, kwamba suala limalizwe kiutu uzima

Malipo yaliyofanywa na Cohen kukiri siku 13 kabla ya uchaguzi yakazua swali kama ilikuwa ni sahihi kwa kuzingatia sheria za uchaguzi na kwamba gharama hizo ni sehemu ya pesa za kampeni au la

Fukua fukua ikamkuta Mueller ambaye aliona kuna `crime`na kupeleka kwa FBI, nao wakata kupata kibali cha kumpekua Cohen.

Walimtumia prosecutor aliyeteuliwa na Trump kutaka ruhusa ya mahakama ya Jaji aliyeteuliwa na Trump. Kumbuka FBI ipo chini ya Wray aliyeteuliwa na Trump, AG aliyeteuliwa na Trump na Deputy AG Pia. Hapa kuna nani ana `twist`

Tatizo linalojitokeza, ukisharuhusu kupekuliwa chochote na lolote linaweza kutokea

Nikupe mfano rahisi unaoweza kuulewa, Polisi wanaweza kuja kkukupekua nyumbani kwako kwa hisia kuwa una nyaraka zilizotumika kuiba pesa ofisini.

Katika upekuzi wakakutana na kichwa cha mtoto au mguu wa mtu
Usitegemee Polisi wataacha hilo kwasababu eti wanatafuta nyaraka. Umeelewa!

Jaribu kuwa na information za kutosha kuhusu mada, usiwe na `bias blind`
 
Mzuvendi, could I just chip in if you don't mind? Deep State is just a figment of imagination perpetuated by conspiracy theorists majority of whom have no confidence to the established machinery of justice , law and order. Their main objective is to undermine the system when they feel it is not to their benefit by claiming there is a shadow government controlled by imaginary bureaucrats. In congress fringe rights, centrist observers and leftist critics have all used the term deep state at different periods when things are not going their way but the truth is that in the US there is nothing like DEEP STATE.

Mag3;

I am sorry I didn't see this one. Now with regard to your post, I can't agree with you more. The term deep state has been misused by a segment of population, particularly in the US, to misrepresent the facts of ground. Take for example Trump. Before the election, he thought the establishment will rig the election so Hilary could win the presidency. That didn't happen.
 
Back
Top Bottom