Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #581
ACCESS HOLLYWOOD TAPE YARUDI KWA SURA MPYA
STORMY DANIEL ALETA 'STORM' WH
TIMUA TIMUA NI TAMU CHUNGU ' NGUMU KUMESA'
Access hollywood tape ni video iliyotoka wakati wa uchaguzi ikimuonyesha mgombea Trump alivyowazungumzia vimwana waliofika kumlaki akiwa na washirika wake. Ni tape iliyoonekana kuhitimisha kampeni za Trump
Kuna kitu kilitokea siku ambayo TV zilionyesha tape kwa umma. Kwamba, habari ilikuwa kubwa kwa muda mfupi kwani siku hiyo hiyo emails za Democrats za akina Podesta na Hillary zilitoka
Email zilitolewa na Wikileaks. Hapo ndipo uhusiano wa Hollywood tape-Wikileaks-Russia- Democrats emails unapofikirisha wachunguzi. Timing ya kutoa emails hizo ilikuwa mahususi kupunguza nguvu ya hollywood tape
Hollywood tape inarudi kwa mlango mwingine. Kwamba, upekuzi uliofanywa kwa Michael Cohen, wakili wa Trump ulihusisha mawasiliano ya Trump na wakili Cohen, kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Mtifuano kati ya Stormy Daniel,kahaba, anayedai kummegea penzi Rais Trump, lilimvuta mchunguzi Mueller kujiridhisha kama kuna lolote kuhusu uhusiano wa Cohen-Trump-Stormy na dolari 130,000
Kumbuka Cohen alimpa Stormy 130K kama kiziba mdomo siku chache kabla ya uchaguzi
Hilo likapelekea Mueller kuwa na hisia za 'uhalifu' na kuwakabidhi FBI ambao baada ya kupata vibali husika walimpekua wakili Cohen. Hapa ndipo Rais Trump anapowaka moto kwani yanaweza kuibuka yasiyotarajiwa
Upekuzi unarudisha hollywood tape kwa kuunganisha na vipande,haijulikani kwanini Trump ameingiwa na wahka Njia iliyobaki ni kuua uchunguzi wa Mueller. Wapi kuanzia? Ni kwa Rosenstein
Tatizo linalomkabili Rais Trump ni kujenga uhalali wa kumuondoa Rosenstein na kisha Mueller.
Bila kuwa na sababu za kuridhisha hilo litazaa tatizo jingine la obstruction of justice ambalo ni tatizo kubwa
Obstruction of justice itakuwa tatizo la pili baada ya lile la kumtimua James Comey alililkiri kuwa alifanya hivyo
Hivyo tatizo linalomsumbua Rais Trump ni jinsi ya kuwatimua watu wawili, deputy AG-Rosenstein na Mueller
Kwa mbali congress inasema kuwatimua hao kutazua balaa jingine linaloweza kuhitimisha safari ya Don
Tayari kamati ya sheria ya seneti inaandaa mswada wa kumlinda Mueller, mswaada ambao Republican wamekataa usiowepo kwa muda mrefu. Hofu ya Republican, ikitokea tatizo watabeba lawama
Kwa vile kuna uchaguzi wa kati 'midterm election' November, uwezekano wa kupoteza mabunge yote upo
Hapa kuna mtego, kwamba Republican katika senate na congress wanaweza kupoteza viti vyao, lakini pia hali si njema kwa Rais Trump, Democrats wakichukua congress yote, ''impeachment is imminent ''
Kuna swali watu wanajiuliza, kahaba Stormy anataka nini hadi kumsumbua Rais Trump kiasi hicho ili hali amesema alitoa penzi la mchepuko kwa ridhaa na wala hahitaji fidia. Sasa kisa kinachomsumbua ni kipi?
Tujadili hili kwa ufupi
Tusemezane