Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Trump hivi sasa yuko kwenye panic mode, kawashambulia China kwamba wanataka kuvuruga mid term elections!
 
Trump hivi sasa yuko kwenye panic mode, kawashambulia China kwamba wanataka kuvuruga mid term elections!
Pona ya Trump kama ipo itakuwa short-lived kwa sababu tu Congress kwa sasa inamlinda. Bado chini ya miezi miwili mid-term elections inafanyika na ole wake apoteze Congress, atajuta kwani dalili zote zinaonyesha uwezekano huo upo. Hii ndiyo sababu amekuwa kama mtu aliyepagawa, anaropokaropoka tu hovyo na kuwarukia wanaomkosoa kwa matusi.

Anajua siku zake zinahesabika ingawa kumuondoa madarakani si rahisi kihivyo kulingana na Katiba yao. Hata hivyo atapata taabu sana kwani hata miongoni mwa Republicans, wengi wamemchoka ila kwa unafiki tu na woga wa kutukanwa wameamua kukaa kimya. Lakini pia tusiwasahau wako wale ambao wako tayari kufa naye hata angefanya nini kama hapa kwetu.
 
Trump hivi sasa yuko kwenye panic mode, kawashambulia China kwamba wanataka kuvuruga mid term elections!
Mkuu Mwalimu

Trump anafanya mambo kwa 'trick' sana lakini kuna wakati yanamrudi
Jana katika press conference alikuwa anakatiza wauliza maswali na kueleza alichotaka watu wasikie. Katika kufanya hivyo alItoa maelezo yanayomrudi

1. Kwamba, Rais Obama hakujaribu kuchagua jaji?
Watu wanauliza ina maana hajui nini kilitokea kwa Jaji Garland.
Hili linamfanya aonekane out of touch and ill informed!
Alikusudia kumchafua Obama akajichafua unfortunate

2. Hili la China kuingilia midterm lina maana mbili, kwanza, kujiosha kwamba si Russia pekee bali nchi nyingine. Kumbuka huko nyuma aliwahi kusema pengine ni Russia au nchi nyingine
Alichotaka ni kuthibitisha kuwa kuingilia uchaguzi ''is not an isolated case''

3. Kauli ya China inalenga kuzungumza na Wakulima. Kuna joto kali sana linatoka kwa wakulima kama wa Soya Beans waliopoteza mabilioni ya pesa kutokana na 'retaliation' ya China dhidi ya tariff. Aliyeanzisha trade war ni Trump bila kujali consequences kwa watu wake

Kwasasa Rais Trump anaogopa kupoteza sehemu ya Wakulima inayotengeneza wapiga kura wa kundi lake (political base). Katika kujinasua na utata huo, Rais Trump anatumia China kuwashawishi kuwa hatua ya China imelenga kuingilia mid term elections na siyo kutokana na trade war

Of course China inapiga panapouma na imelenga wakulima lakini si kwasababu ya uchaguzi.
Ni katika kulipiza kisasi kutokana na tariff zinazotokana na trade war

Tukiongelea trade war kwa ujumla, kutakuwa na mambo mawili yatakayojitokeza kuelekea 2020

1. Ni kweli tariff zitalazimisha makampuni kurudi US ili kupunguza gharama za bidhaa
Hilo litasaidia viwanda vya US kupanuka na kuongeza idadi ya ajira

2. Makampuni yatarudi lakini yakiathirika kibiashara.
Kwa mfano, kampuni ya GM inauza magari Asia badala ya kutegemea soko la US.

Kampuni ililenga watu Billion 2 kati yao kuna wenye uwezo wa kununua bidhaa katika idadi nzuri. GM inalalamikia mapato kwa kuwekewa mizengwe kutoka China

3. Gharama za uzalishaji US ni kubwa kuliko kutengeneza na ku import
Maana yake, gharama zikipanda makampuni yatakuwa na njia mbili
Kuchukua gharama na kupunguza mapato au kupitisha gharama kwa watumiaji

Likely gharama hizo zitakwenda kwa walaji na watumiaji. Kutakuwa na ongezeko la gharama za maisha katika vitu vilivyozoeleka kuwa katika uwezo wa kawaida wa mnunuzi

4. Kwa wafanyakazi kutakuwa na ongezeko la ajira na mishahara kutokana na mahitaji

Katika biashara lazima makampuni yatatafuta njia mbadala.
Mbele ya safari Robot zitachukua nafasi ya wafanyakazi hasa utengenezaji wa vitu kama magari. Suala la ajira litarudi pale pale
 
Mkuu Nguruvi3 na wengineo

Naona Senate Committee inapiga kura juu ya uteuzi wa Jaji Cavanaugh...

Chama cha Republican ambacho miaka na miaka kimekuwa kikijinasibu kuwa kinasimamia maadili kimewekwa njia panda tangu kuingia kwa Trump... wamejikuta wanalazimika kutetea watuhumiwa wa kashfa za ngono kwa sababu tu wanatoka chama chao. Kuanzia Trump mwenyewe na kashfa ya kuwatomasa wanawake "grab them by the p***" na sasa Jaji Cavanaugh ambaye wanaenda kumpitisha kuwa Jaji wa Supreme Court pamoja na kashfa inayomkabili.

Uamuzi wa leo una impact kubwa sana kwenye mid term November... yetu macho
 
Wamarekani hawastahili haya...kwamba mteuliwa wa rais naweza kuzuiwa kudhibitishwa kisa tuhuma zisizona udhibitisho!!
Umefanya vizuri kufuta mchango wako wa awali, sijaona mawazo ya hovyo kama uliyoyaandika hapo mwanzo, hongera sana. Pamoja na hayo naomba nikuulize swali moja linalonisumbua sana...kwa nini unaonekana kupenda sana utawala wa kiimla? Unavutiwa nini na watu kama Putin, Mseveni, Kagame bila kumsahau Magufuli?

Hawa ni viongozi ambao hawana uvumilivu na ukosoaji (upinzani), hawataki kabisa demokrasia ndani au nje ya nchi zao. Katika orodha hiyo namuongezea na Trump ambaye kama isingekuwa ni kwa sababu ya misingi imara isiyotetereka ya utawala nchini mwake angeweza kabisa kuwa dikteta kama walivyo wenzake hapo juu.
 
Mkuu Nguruvi3 na wengineo

Naona Senate Committee inapiga kura juu ya uteuzi wa Jaji Kavanaugh...

Chama cha Republican ambacho miaka na miaka kimekuwa kikijinasibu kuwa kinasimamia maadili kimewekwa njia panda tangu kuingia kwa Trump... wamejikuta wanalazimika kutetea watuhumiwa wa kashfa za ngono kwa sababu tu wanatoka chama chao. Kuanzia Trump mwenyewe na kashfa ya kuwatomasa wanawake "grab them by the p***" na sasa Jaji Cavanaugh ambaye wanaenda kumpitisha kuwa Jaji wa Supreme Court pamoja na kashfa inayomkabili.

Uamuzi wa leo una impact kubwa sana kwenye mid term November... yetu macho
Mwalimu , hili suala linachukuliwa kirahisi kwa kukosa mantiki nyuma yake

1. Dr Ford alieleza madai kabla ya Kavanaugh hajawa nominated ikabaki kuwa siri hadi ilipovujishwa katika vyombo vya habari.

Ilipovuja Dr alifanya 'test' kubaini kama madai yake ni ya kweli au uongo , akafaulu na ndipo wanasheria walipokubali kufanya naye kazi

2. WH ilikataa kutoa nyaraka za nyuma wakati Kavanaugh anafanya kazi Ikulu.
Hili likafanyika kwa ubabe ambapo kurasa 48,000 zilizotolewa ili zisomwe katika masaa 12

3. Baada ya leak, Dr Ford alitaka uchunguzi wa FBI. Republicans wakakataa na Kavanaugh mwenyewe. Hapa ndipo shaka ilipoanza, kama alikuwa clean kwanini aogope uchunguzi?

4. Dr Ford akakubali ku testify mbele ya kamati ya seneti. Alitaka kuleta mashahidi wahojiwe
Republicans wakakataa mashahidi. Mmoja wa mashahidi ameandika kitabu akimtaja Brett kama Brad Kavanaugh akileza enzi zao. Kwanini GOP hawakutaka mashahidi?

5. Dems wanasema ni vema kufanya FBI investigations, GOP wanasema kamati ya seneti imefanya uchunguzi hakuna kitu kilichoonekana

6. Jaji Kavanaugh kaenda kwenye TV akijieleza kama mtu msafi.
Hili lilikuwa kosa kubwa, wenzake wengi wamejitokeza na kusema si kama alivyojieleza, alikuwa mlevi wa kupindukia n.k.Hili likaondoa credibility yake

Alichotakiwa ni kukiri tu akiwa kijana alifanya alibofoa. Marais G.Bush na Obama walikiri

Mbele ya kamati, Cavanaugh akabadili msimamo na kusema aliwahi kunywa kupita kiasi huku marafiki wakisema wanamjua kama cha 'pombe' na hivyo kuonekana ile credibility ina shaka

7. Dr Ford ali testify akihojiwa na mwanasheria aliyechukuliwa na GOP senate member. Kisa ilikuwa kuogopa wanaume 11 kumhoji mwanamke. Kisiasa ingewagharimu Republicans

Dr Ford alieleza jaji kufanya kazi katika bar store kama kalenda ya Kavaugh ilivyoonyesha

8. GOP wakalazimisha kura ndani ya kamati leo. Maseneta wachache wakaonyesha kutoridhishwa na kumpitisha Cavanaugh kukiwa na wingu la ''kasema hivi kasema vile''

Baada ya hayo, tuseme kuwa hakuna anayejua nani mkweli kati yao.

Ni uchunguzi tu wa FBI ndio unaweza kumsafisha Jaji Kavanaugh
Huko nyuma kulikuwa na kashfa kama hii kwa Judge Clarence Thomas. FBI ilimsafisha

Uchunguzi wa FBI haumaanishi kumtia hatiani, ni kumsafisha Kavanaugh ili akithibitishwa awe na uwezo wa kutoa hukumu za kura katika supreme court bila matatizo

Bila hivyo atakuwa 'accused sexual assault supreme court judge'

Hilo litakuwa na impact kwa court yenyewe kwasababu lita 'adulterate' nguvu na maamuzi yake

Mfano, accused Kavanaugh' atatoaje maoni kuhusu kesi za wanawake kama ya Wade vs Roe?

Kavanaugh anasema hana makosa 'innocent' kwanini asikubali FBI wamsafishe?
Hili linakwenda sambamba na kauli za Rais Trump ambazo nyingi zimemtia doa

Ni kauli kama aliyotoa jana katika mahojiano akisema ni harakati za Democrats na hasira za kushindwa uchaguzi zinazochagizwa na Clinton

Mbona Judge Gorsuch aliyesoma naye na katika rank moja hakupata mazonge zonge ?

Kamati ya seneti ilitaka kufanya mambo haraka ikijua nyuma kunaweza kutokea matatizo

Sasa kamati imelazimika kupisha uchunguzi kwa siku 7 ili FBI wakamilishe uchunguzi

Of course kuna politics kwa pande zote za GOP na Dems na hili tutalijadili
 
Naona Senate Committee inapiga kura juu ya uteuzi wa Jaji Cavanaugh...
Jaji Kavanaugh tukiacha tuhuma zilizoelekezwa kwake, utetezi wake mbele ya kamati ulimuondolea kabisa sifa ya kuingia Supreme Court ya Marekani na kwa Marekani ambayo wengine tulibahatika kuifahamu, asingepita. Utetezi wake uligubikwa na hasira, hamasa, hamaki na ushabiki wa kisiasa sifa ambazo haziendani na nafasi hiyo na hasa katika nchi kama ya Marekani. Ni bahati mbaya kwamba nchi hiyo imefikia hali kama hiyo kutokana vitimbwi vya uongozi ambao uko madarakani chini ya Donald Trump.
Uamuzi wa leo una impact kubwa sana kwenye mid term November... yetu macho
Wamarekani walio wengi bado wanajiuliza ilikuwakuwaje hata mtu kama Donald Trump akachaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo na bila hata hili swala la Kavanaugh, huu uchaguzi wa mid-term una umuhimu wake. Hata hivyo uteuzi wa Kavanaugh ni kweli umechochea na kuongezea changamoto inayowakabili wananchi mwezi November...vyovyote vile Democrats wakichukua Congress tutashuhudia vituko ambavyo hatujawahi kuviona...yetu macho.
 
"Mag3, post: 28567703, member: 10873"]Jaji Kavanaugh Utetezi wake uligubikwa na hasira, hamasa, hamaki na ushabiki wa kisiasa sifa ambazo haziendani na nafasi hiyo na hasa katika nchi kama ya Marekani. Ni bahati mbaya kwamba nchi hiyo imefikia hali kama hiyo kutokana vitimbwi vya uongozi ambao uko madarakani chini ya Donald Trump.
Kavanaugh alipaswa kuelewa uteuzi wake ulikuwa na mawenge wenge. Jaji huyo alitoa kauli kuhusu Rais kutoshtakiwa na kauli nyingine wakati uchunguzi wa Russia ukiendelea

Pili, alitakiwa afahamu uteuzi wake unaonekana kama kinga ya Rais Trump siku za mbeleni kama itabaidi mazonge zonge yanayomwandama yakafika supreme court

Tatu, alitakiwa afahamu uteuzi wake unahusishwa na falsafa ya 'conservatism' ambayo imelenga kubadili sheria nyingi kwa vile supreme court itakuwa na 5 vs 4.

Tendo la kwenda Fox new akiwa nominee halijawahi kutokea. Ilikuwa dhahiri alifuata maelekezo kutoka WH. Katika interview ile, Kavanaugh aliboronga hadi media za conservative zikajiuliza nini hasa alichojaribu ku achieve

Akiwa mtajwa wa nafasi anapaswa kuwa impartial. Opening statement yake kwa kuchomeka siasa za uchaguzi na akina Clinton zilionyesha wasi wasi uliokuwepo kwa liberal kuhusu yeye
Hilo limechagiza sana liberal kuwa na msiamamo kiasi cha kuwalazimisha GOP kupinda kama ilivyotokea leo. Ingekuwa senate ya zama hizo jina lingeshachomolewa haraka sana
Hata hivyo uteuzi wa Kavanaugh ni kweli umechochea na kuongezea changamoto inayowakabili wananchi mwezi November...vyovyote vile Democrats wakichukua Congress tutashuhudia vituko ambavyo hatujawahi kuviona...yetu macho.
Kuna impact kubwa sana katika midterm hasa kwa wagombea wa Republicans na siyo Trump

Ndiyo maana senator 11 hawakukubali kumhoji bali walitumia mwanamke.

Wanatambua GOP ina matatizo makubwa na wanawake, urban residents na colored people
Trump alishinda uchaguzi kwa 52% ya white women, alishindwa katika ujumla wa wanawake

Kavanaugh kupitishwa bila uchunguzi kutakuwa nI kuwadharau 'survivor' wa sexual assault. Itawapa Dems hoja hasa kwa wanawake. Itavunja imani ya GOP wanaoishi mijini n.k.

House na senate Republicans wapo njia panda. Ima wakubaliane na Rais Trump ili awasaidie katika rural areas kwa wale political base yake au wakubaliane na fundamentals za conservative ambazo zinajali family values.

Hapa wamechagua Trump kwa short term solution mbele ya safari itakuwa tatizo.

Kukiwa na utata mkubwa wa wagombea wa GOP katika midterm anything can tip the scale

Jambo hili linawatatiza sana, na anayechagiza ni Rais Trump ambaye alikuwa Dems, Independent na sasa Republicans bila kufuata values za GOP
 
Kavanaugh alipaswa kuelewa uteuzi wake ulikuwa na mawenge wenge.

Alipaswa kuelewa uteuzi wake ulikuwa na mawenge wenge yapi hasa?

Jaji huyo alitoa kauli kuhusu Rais kutoshtakiwa na kauli nyingine wakati uchunguzi wa Russia ukiendelea

Muktadha ni karibu kila kitu. Hizo kauli zilitolewa katika muktadha gani hasa?

Pili, alitakiwa afahamu uteuzi wake unaonekana kama kinga ya Rais Trump siku za mbeleni kama itabaidi mazonge zonge yanayomwandama yakafika supreme court

That's too speculative. Hayo mazonge zonge yanayomwandama ni yapi? Russian collusion illusion? Kama ni hayo ya 'collusion' basi there's no there there!!

Tatu, alitakiwa afahamu uteuzi wake unahusishwa na falsafa ya 'conservatism' ambayo imelenga kubadili sheria nyingi kwa vile supreme court itakuwa na 5 vs 4.

Brett Kavanaugh ni conservative. Wewe hapo umeandika kana kwamba yeye hafahamu kwamba siasa zake ni za mrengo upi. Unaandika eti "alitakiwa afahamu uteuzi wake unahusishwa na falsafa ya 'conservatism"

Mtu ambaye alifanya kazi na/ chini ya Ken Starr [a Republican], former Independent Counsel aliyeongoza uchunguzi dhidi ya Rais Clinton na kupendekeza kuwa rais Clinton awe impeached, mtu ambaye alikuwa ni mmoja wa mawakili wa G.W. Bush kwenye recount ya Florida kwenye uchaguzi wa mwaka 2000, mtu ambaye baadaye akaja kufanya kazi kwenye White House ya W. Bush kama Staff Secretary, mtu ambaye mrengo wake wa kisiasa na misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali inajulikana, huyu ndo unasema kwamba "alitakiwa afahamu uteuzi wake unahusishwa na falsafa ya 'conservatism"?

Come on man! Everybody and their mama knew that he is a conservative jurist. He knows it, I know it, and almost everybody else knows it. It's not a secret where he stands on the US political spectrum. He is a former political operative.

Tendo la kwenda Fox new akiwa nominee halijawahi kutokea.

So? Angeenda wapi sasa ilhali kila siku anashambuliwa kwenye mainstream media ambayo ni largely liberal? Angeenda CNN akahojiwe na Chris Cuomo?

Ilikuwa dhahiri alifuata maelekezo kutoka WH.

Una ushahidi au unahisi tu? Angalia usije kuwa kama Christine Blasey Ford! Unatoa tu tuhuma bila ushahidi....

Katika interview ile, Kavanaugh aliboronga

Aliborongaje?

hadi media za conservative zikajiuliza nini hasa alichojaribu ku achieve

Media zipi za conservatives zilijiuliza hivyo?

Akiwa mtajwa wa nafasi anapaswa kuwa impartial. Opening statement yake kwa kuchomeka siasa za uchaguzi na akina Clinton zilionyesha wasi wasi uliokuwepo kwa liberal kuhusu yeye.

Siasa zipo kila sehemu. Tuache kujidanganya kuwa eti hata kwenye US Supreme Court hakuna siasa.

Siasa zipo sana na ndo maana unaona Dems wapo kwenye full destroy mode kwa sababu wanajua Kavanaugh akiwa confirmed basi SC itakuwa na permanent conservative majority ya 5-4 for at least a generation kwa sababu Kavanugh anaenda kum replace Ret. Justice Anthony Kenedy, ambaye. licha ya kuwa Republican nominee/ apointee, kwa kiasi kikubwa alikuwa ndiye 'swing vote' kwenye bench ya SC.

Hata uteuzi wa Jaji Merrick Garland 2016 ulipigwa stop na GOP kwa sababu ya siasa. Garland aliteuliwa na Rais Obama kwenda kujaza nafasi ya Jaji Antonin Scalia. Scalia ndiye alikuwa jaji conservative kuliko wote kwenye bench ya US SC.

Kwa vile GOP walikuwa na majority ya kuzuia nomination yake [thanks to Harry Reid, a Democrat], wakaizuia hadi baada ya uchaguzi. Bahati nzuri wakashinda uchaguzi wa 2016 na Rais Trump akamteua Neil Gorsuch kwenda kujaza nafasi ya Scalia.

Gorsuch hakupata pingamizi sana kwa sababu alikuwa anaenda kujaza nafasi ya jaji aliye conservative huku na yeye [Gorsuch] akiwa conservative. Uteuzi wa Gorsuch hau ku tip balance of power kama ambavyo huu wa Kavanaugh utavyo tip balance of power.

Kikubwa ambacho Dems na base yao wanakihofia ni Roe vs Wade [natumai unaifahamu ni nini] kuwa overturned one day.

Hilo limechagiza sana liberal kuwa na msiamamo kiasi cha kuwalazimisha GOP kupinda kama ilivyotokea leo. Ingekuwa senate ya zama hizo jina lingeshachomolewa haraka sana

Hapo unazungumzia suala la uchunguzi wa FBI?

Mbona hata zama hizo [1991] FBI walifanya uchunguzi dhidi ya tuhuma za Anita Hill kwa Clarence Thomas....it's been done before.

Kuna impact kubwa sana katika midterm hasa kwa wagombea wa Republicans na siyo Trump

Impact ipo ingawa sina hakika kama ni kubwa sana. Na hata kwa Dems ipo. Hususan wale Dems waliopo kwenye ballot mwaka huu kwenye majimbo ambayo Trump alishinda.

Ndiyo maana senator 11 hawakukubali kumhoji bali walitumia mwanamke.

Hawakutaka kuwapa Dems fodder ya matangazo kwenye midterm elections. Pia hawakutaka ionekane kama wanamwonea huyo mama anayedai alishambuliwa na Kavanaugh.

Wanatambua GOP ina matatizo makubwa na wanawake, urban residents na colored people
Trump alishinda uchaguzi kwa 52% ya white women, alishindwa katika ujumla wa wanawake

Kwa ujumla wa kura za wanawake Trump alishindwa kwa asilimia ngapi?

Kavanaugh kupitishwa bila uchunguzi kutakuwa nI kuwadharau 'survivor' wa sexual assault. Itawapa Dems hoja hasa kwa wanawake. Itavunja imani ya GOP wanaoishi mijini n.k.

Well, FBI wameshapewa order ya kufanya uchunguzi. Sidhani kama watakuja na jipya maana wameshamfanyia uchunguzi mara 6 sasa.

Na wakifanya tena huu uchunguzi, kwa mara ya 7, na kurudi na matokeo yale yale kama ya mwanzo, naamini kabisa Dems watahamisha goli. Watch this space...

House na senate Republicans wapo njia panda. Ima wakubaliane na Rais Trump ili awasaidie katika rural areas kwa wale political base yake au wakubaliane na fundamentals za conservative ambazo zinajali family values.

Hapa wamechagua Trump kwa short term solution mbele ya safari itakuwa tatizo.

Kukiwa na utata mkubwa wa wagombea wa GOP katika midterm anything can tip the scale

Jambo hili linawatatiza sana, na anayechagiza ni Rais Trump ambaye alikuwa Dems, Independent na sasa Republicans bila kufuata values za GOP

Maybe....

Naamini Kavanaugh atapita tu.
 
"Nyani Ngabu, post: 28568550, member: 188"That's too speculative. Hayo mazonge zonge yanayomwandama ni yapi? Russian collusion illusion? Kama ni hayo ya 'collusion' basi there's no there there!!
Ninachoongelea ni mahojiano kati ya Mueller na Trump yanayoonekana kuleta utata huku Rais Trump akikataa kuhojiwa kwa kuogopa 'trap' ingawa anasema hakuna Collusion. Kuhusu collusion msimamo wangu ni ule ule kuwa sijui kuna nini hadi hapo Mueller atakapotoa taarifa yake. Siwezi kusema ipo au haipo kama alivyosema Trump

Utakumbuka kauli ya kwanza ilikuwa 'hakuna contact na Russia'' . Sasa inajulikana kulikuwa na contact na kijana wake akiwa sehemu ya contact nyingi. Ikaja statement ya Jay Skulow 'Trump hakuandika statement' well, wamekiri ameandika statement. Ikabadilika kuwa contact si 'crime' Collusion si crime etc. Unaweza kuona inavyobadilika kila siku kutokana na mashahidiKuna indictment zimetokea za watu wa ndani wa Trump. Silazima ziwe collusion ndiyo maana nasema ni mapema mno kusema hakuna au kipo kitu hadi Mueller amalize kazi
Brett Kavanaugh ni conservative. alifanya kazi na/ chini ya Ken Starr [a Republican], former Independent Counsel aliyeongoza uchunguzi dhidi ya Rais Clinton na kupendekeza kuwa rais Clinton awe impeached, mtu ambaye alikuwa ni mmoja wa mawakili wa G.W. Bush kwenye recount ya Florida kwenye uchaguzi wa mwaka 2000, mtu ambaye baadaye akaja kufanya kazi kwenye White House ya W. Bush kama Staff Secretary,mrengo wake wa kisiasa na misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali inajulikana, huyu ndo unasema kwamba "alitakiwa afahamu uteuzi wake unahusishwa na falsafa ya 'conservatism"?
Kama ulinisoma mapema huko nyuma kuna mahali nimesema suala hili haliwezi kutengwa na siasa kama ilivyotokea kwa Garland. Ni wazi Dems wanahofu ya Wade v Roe. Hoja yangu ilikuwa ni kwamba, Kavanaugh alitakiwa awe mwangalifu katika mitego. WH walimshauri akomae na kukataa uchunguzi wa FBI. Hilo lilikuwa kosa ambalo leo wame 'pay the price' aliwapa hoja Dems. Laiti angesema yupo tayari kwa FBI investigation angejinasua na mtego. Alipoulizwa na Senator Turbin kuhusu FBI hakuweza kujibu. Si kwamba ana makosa bali alifuata misleading ya WH
So? Angeenda wapi sasa ilhali kila siku anashambuliwa kwenye mainstream media ambayo ni largely liberal? Angeenda CNN akahojiwe na Chris Cuomo?
Tatizo si kwenda Fox ni kwenda katika media. Angeuchuna ingemsaidia sana kama alivyofanya Clarence Thomas. Wakati timbwili linaendelea ni kama alikuwa anachagiza tatizo.
Angalia usije kuwa kama Christine Blasey Ford! Unatoa tu tuhuma bila ushahidi....
Well, at least yeye under oath alitaka uchunguzi wa FBI.
Aliborongaje?
Yes aliboronga kwa kujieleza kama mtu mwema kuanzia 17

Picha aliyotoa ni ya 'utakatifu'. Kutokana na hilo waliosoma naye wamejitokeza na kusema hapana, aliyoeleza hasa kinywaji si kweli.

Baada ya interview alitambua kosa, ndani ya seneti akasema 'yes alikuwa anakunywa na nyakati nyingine kupita kiasi'.Ieleweke kunywa pombe si kosa na hata kupita kiasi si kosa. Kosa ni credibility baada ya kushindwa kuoanisha aliyosema katika TV na yale ndani ya Seneti. Yote hayo ni kwasababu aliji expose katika TV bila sababu
Siasa zipo kila sehemu. Tuache kujidanganya kuwa eti hata kwenye US Supreme Court hakuna siasa.
Ndiyo maana kuna conservative na Liberal ndani ya SC
Kikubwa ambacho Dems na base yao wanakihofia ni Roe vs Wade [natumai unaifahamu ni nini] kuwa overturned one day.
Hili nalo nimeliongelea huko nyuma. Ndiyo maana nasema Kavanaugh alitakiwa ajue kuna 'trap'. Laiti angekubali au kushauri FBI wafanye kazi kesho angekuwa confirmed. Hesabu za majority hazikuwa sawa kama ilivyotokea leo.

Majority ya GOP ni 2 na VP kama tie breaker. Walitakiwa waelewe Jeff Flake, Murkowisk, Susan Collins ni ''swing vote''. Kavanaugh aliweka matumaini WH na shinikizo badala ya kuchanga karata. Ilikuwa simple, akubali FBI investigation mambo yangeisha huenda
Hapo unazungumzia suala la uchunguzi wa FBI?Mbona hata zama hizo [1991] FBI walifanya uchunguzi dhidi ya tuhuma za Anita Hill kwa Clarence Thomas....it's been done before.
Again nimelisema hili bandiko la wali, kwamba kesi ya Kavanaugh si ya kipekee. Clarence alifanyiwa uchunguzi na FBI kukawa hakuna conclusion ya kumzuia kuteuliwa. Clarence hakukimbilia katika media au kukataa FBI. Aliacha sheria ifuate mkondo ikamsaifisha
Impact ipo ingawa sina hakika kama ni kubwa sana. Na hata kwa Dems ipo. Hususan wale Dems waliopo kwenye ballot mwaka huu kwenye majimbo ambayo Trump alishinda.
Pressure ilikuwa kubwa sana, lakini kwa mwendo wa mambo yalivyopelekwa na senate GOP yametoa nafasi kwao kupumua.

Trump amekwenda kukampeni dhidi yao ili wawe upande wake
Tatizo ni kuwa hili limegeuka kuwa la 'wanawake' na hiyo imepunguza pressure kwao

Hata hivyo kwa undani zaidi pressure ipo sana kwa Republicans.
Jeff Flake hayupo katika ballot box lakini vipi pressure aliyoipata leo hadi kuweka ngumu? Just imagine kwingine hali ikoje
Hawakutaka kuwapa Dems fodder ya matangazo kwenye midterm elections. Pia hawakutaka ionekane kama wanamwonea huyo mama anayedai alishambuliwa na Kavanaugh.
Seneta wa GOP walikwepa ukweli kuwa hilo lingekuwa tatizo la kisiasa kwao. Na inaeleza hali ilivyo kuelekea midterm. Siyo wote wapo katika ballot box, lakini katika margin ya 2 ni risk kuitumbukiza GOP yote katika mtafaruku na wanawake. Kumbukumbu za primary GOP zilizomwacha mtu nje kwa kura za wanawake bado zinarindima na kuwatisha
Kwa ujumla wa kura za wanawake Trump alishindwa kwa asilimia ngapi?
Mkuu hili nalo unauliza!
Well, FBI wameshapewa order ya kufanya uchunguzi.Sidhani kama watakuja na jipya maana wameshamfanyia uchunguzi mara 6 sasa.. Na wakifanya tena huu uchunguzi, kwa mara ya 7, na kurudi na matokeo yale yale kama ya mwanzo, naamini kabisa Dems watahamisha goli. Watch this space...
Kuna mawili matatu ya kujadili

1. Kwamba, Trump hadi Jana alisema hakuna uchunguzi wa FBI kwamba 'wamesema haliwahusu'. Well, leo amejikuta anawataka wafanye uchunguzi yeye mwenyewe

2. Uchunguzi umekuwa limited kwa tukio la Ford na Kavanugh tu! si mengine

Kwangu mimi sidhani tuhuma pekee zinatosha kumzuia mtu katika uteuzi.
Figusu figus za kisiasa ni mambo ya kawaida kama ilivyokuwa kwa Garland

Hata hivyo wanaotoa tuhuma wanapaswa kusikilizwa. Haikuwa jambo jema kwa GOP kumsikiliza Ford wakijua lengo lao ni kumpitisha Kavanaugh kuwe na ukweli au la.

Ilikuwa kum brush yule mama, na kama ni hivyo kwanini walimwita?
Tena wakikataa uwepo wa mashahidi wake

Kavanaugh asipokuwa na hatia hilo ni jambo jema kwanini mkondo wa sheria na taratibu zimefuatwa. Ni nzuri kwake kwani anakwenda SC akiwa hana mizigo au kuangaliwa jicho pembe. Akiwa na hatia hatakuwa tofauti na Bill Crosby, uteuzi utachomolewa
 
.....sijaona mawazo ya hovyo kama uliyoyaandika hapo mwanzo.....
Kwa kauli zenu hizi, na zile za 'deplorable' kutoka kambi ya DEM nitaachaje kumuunga mkono Trump kwa baadhi ya kauli zake; mfano, aliposema hata angemteua George Washington bado DEM wangempinga.

Uovyo wa mawazo uonyeshwa na kukosolewa hapo hapo..na yule aonaye uovyo huo. Kitendo cha kuona mawazo yale kwa takrabani zaidi ya masaa nane na kushindwa namna ya kuyakosoa ama kuonyesha uovyo wake nakitafsiri kama kuelemewa na hoja na kupata unafuu wa hoja hiyo baada mtoa hoja kuamua kuondoa hoja hiyo ili kutoa furusa ya kuendelea na mjadala bila baadhi ya wachangiaji kujisikia wameelemewa.

Kwa ufupi niliondoa hoja hiyo, ili mjadala huu uendelea bila kuwafanya baadhi ya wachangiaji hapa kujiona wako kwenye " guilt side".

Nimeshindwa kuunga mkono hoja yako juu ya uovyo wa mawazo yangu kwani ulishindwa kuonyesha uovyo wa mawazo yangu kwa zaidi ya masaa nane kabla sijaondoa hoja hiyo kwa nia njema ya kuunga juhudi za mleta mada kutoa furusa ya kutoa mawazo kwa wote bila hamaki.

Tuendelee na mjadala.
 
TUKIO LA JANA LIMETOA MAFUNZO

Katika timbwili la Jaji Kabanaugh kuna mafunzo kadhaa tunayopa kujifunza

1. Kwamba, kauli ya Rais haiwezi kuwa ya mwisho bali kauli ya wananchi.
Rais Trump kwa namna yake ya utawala ambao sheria huwekwa pembeni amejikuta akilazimika kuwataka FBI kufanya uchunguzi.

Hii ni baada ya kushindwa jaribio la kulazimisha kura. Imebidi arudi katika mstari
Amerudi katika mstari kutokana na kauli za akina mama wawili tu

2. Seneta Jeff Flake aliyekuwa na kura ya turufu alikabiliana na wanawake hao wakimueleza awaangalie usoni kama wahanga wa sexual assault na kwamba anakwenda kupiga kura kwa Kavanaugh bila kujali madhila na masahibu yanayowasibu akina mama

Hilo limetokea ndani ya ofisi za Seneti. Akina mama walimkalia wima wakizungukwa na askari

Kazi ya askari ilikuwa kulinda usalama wa wazungumzaji na Seneta Flake.
Hawakuingilia maongezi, hawakuzuia watu kuelezea hisia, alitimiza wajibu wa kulinda usalama

Jeff Flake alilazimika kuweka msimamo uliobadilisha mawazo ya maseneta akiwemo manafiki Lindsey Graham. Huyu ni mnafiki kwasababu alisema tukio la Kavanaugh lilikuwa kubwa katika historia yake ya siasa.Ni Graham alishiriki kuzuia hata kuletwa jina la Garland mbele ya seneti.

Jeff alisikiliza kauli za wananchi bila kujali wanatoka eneo gani.
Alikubaliana nazo kwasababu ya mantiki. Sauti ya umma ikatawala mbele ya sauti za viongozi.
Maseneta wanajua wasiposikiliza umma wanakaribisha adhabu katika sanduku la kura

Hapa kwetu Wabunge wanatolewa nje kindaki ndaki na Polisi kutoka ukumbi wa Bunge
 
TUKIO LA JANA LIMETOA MAFUNZO

Katika timbwili la Jaji Kabanaugh kuna mafunzo kadhaa tunayopa kujifunza

1. Kwamba, kauli ya Rais haiwezi kuwa ya mwisho bali kauli ya wananchi.
Rais Trump kwa namna yake ya utawala ambao sheria huwekwa pembeni amejikuta akilazimika kuwataka FBI kufanya uchunguzi.

Rais Trump anatawala kwa kutofuata sheria? Are you serious?

Ni jambo gani ambalo sheria iliwekwa pembeni?
 
Rais Trump anatawala kwa kutofuata sheria? Are you serious?Ni jambo gani ambalo sheria iliwekwa pembeni?

Juzi kasema FBI wamesema hawawezi kufanya uchunguzi wa Kavanaugh.
DOJ hawajasema lolote. Jana kasema FBI wafanye uchunguzi wa Kavanaugh
Sheria ndiyo muongozo, ipi aliifuata katika hayo mawili?

Majaji (3)wamesema uchunguzi wa Mueller upo kisheria.
Trump anasema DOJ wafunge uchunguzi ni fake. Yeye ndiye mwenye DOJ kumbuka.
Anaongozwa na sheria gani? Na kama ipo kwanini asiitumie kuzima uchunguzi wa Mueller?
 
Juzi kasema FBI wamesema hawawezi kufanya uchunguzi wa Kavanaugh.

Unaweza kunipa quote/ video ya hicho unachodai alikisema juzi?

DOJ hawajasema lolote.

Hawajasema lolote kuhusu nini?

Jana kasema FBI wafanye uchunguzi wa Kavanaugh

Wait...mi nilidhani Senate Judiciary Committee ndo ilipendekeza kwamba ifanyike supplemental investigation iliyo limited in scope, wakapeleka hilo pendekezo kwa rais, na rais akalikubali ndo akatoa hiyo order.

Sasa wewe hapa unadai kwamba jana kasema FBI wafanye uchunguzi as if GOP senate caucus haikuhusika! Come on man!!

Sheria ndiyo muongozo, ipi aliifuata katika hayo mawili?

Unazungumzia sheria gani hasa? Hebu itaje, ukiweza weka na vifungu kabisa....

Majaji (3)wamesema uchunguzi wa Mueller upo kisheria.
Trump anasema DOJ wafunge uchunguzi ni fake. Yeye ndiye mwenye DOJ kumbuka.
Anaongozwa na sheria gani? Na kama ipo kwanini asiitumie kuzima uchunguzi wa Mueller?

Naona unachanganya maoni yake binafsi na sheria.

Maoni yake binafsi si sheria. Sheria zipo kwenye U.S. Code.

Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.
 
"Nyani Ngabu, post: 28580079, member: 188"]Unaweza kunipa quote/ video ya hicho unachodai alikisema juzi?
Hawajasema lolote kuhusu nini?
Kwamba suala hilo hawawezi 'siyo lao'
Wait...mi nilidhani Senate Judiciary Committee ndo ilipendekeza kwamba ifanyike supplemental investigation iliyo limited in scope, wakapeleka hilo pendekezo kwa rais, na rais akalikubali ndo akatoa hiyo order.
NN kwanza Trump alisema 'FBI' wanasema hawawezi kuchunguza siyo yao hayo

Senate judiciary ikaamua kwenda mbele. Mapema Jana Jeff alikubali, baadaye akagoma kwa sharti la FBI kufanya uchunguzi baada ya kukabiliana na akina mama.

Senate judiciary haikuwa na vote na haikuwa na mbadala ispokuwa kukubali uchunguzi wa FBI. Hapo ndipo wakaagiza WH iagize FBI kufanya uchunguzi.

Hata Kavanaugh alikataa kusema anaunga mkono uchunguzi wa FBI ndani ya kamati

Elewa senate judiciary ilikuwa tayari ku vote hata Dems waliposema watatoka nje.

Walikuwa na majority. Flake na wenzake walipoweka ngumu ikawa haiwezekani ku vote

Kama wange vote wangeshindwa na hivyo jina kuondolewa.
Kupeusha hilo wakakubali uchunguzi wa FBI ambao wao na Trump waliukataa lakini ''under pressure of do or die'' wakakubali
Sasa wewe hapa unadai kwamba jana kasema FBI wafanye uchunguzi as if GOP senate caucus haikuhusika! Come on man!!
Imehusika sana. Mwanzoni alikataa, na hata senate judiciary walikataa. Flake ndiye aliyebadilisha equation

Kumbuka Trump alikuwa na uwezo wa kuwaambia FBI wafanye uchunguzi hata kabla ya Senate Judiciary, narudia tena alikataa na Kavanaugh alikataa kusema anaunga mkono kwasababu alikuwa na back up ya WH na angesema anakubali angemwadhiri Rais.
Naona unachanganya maoni yake binafsi na sheria.Maoni yake binafsi si sheria. Sheria zipo kwenye U.S. Code.Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.
Yeah, nakumbuka alitoa maoni binafsi kuwa Obama admin ilifanya 'surveillance Trump tower'' Intel community ikiwemo FBI wakafanya uchunguzi na kubaini si kweli. Yale yalikuwa maoni yake lakini yakafanyiwa kazi kisheria
 
Nyani Ngabu hoja hapa si kuwa Kavanaugh ana hatia. Kati yake na Ford wakiwa wanajuana ni ngumu kusema nani mkweli.

Kitendo cha senate judiciary kukataa mashahidi wa Ford kilianzisha shaka.

Baada ya kulazimisha majority wakikataa FBI kukatia shaka zaidi

Kuna uwezekano kabisa Kavanaugh ni innocent. Jambo moja tukubaliane, senate judiciary GOP na WH walishindwa kuona mbele.

Kama mtu ni innocent kwanini wasingekubali mapema hayo yaishe?
Sasa wamerudi kule kule walikokataa. Ilikuwa obvious , ita FBI ondoa shaka confirm Kavanaugh. Walitegemea sana majority, ilipo flip flop wakawa flat

Kosa la kutegemea majority bila plan nyingine walilifanya katika Obamacare wakakwama. Unapokuwa na 'thin majority' chochote kinaweza kutokea, si GOP pekee hata Dems
 
Nyani Ngabu hoja hapa si kuwa Kavanaugh ana hatia. Kati yake na Ford wakiwa wanajuana ni ngumu kusema nani mkweli.

Ni kweli. Na ndo maana naamini hata hiyo supplemental background check haitokuja na lolote jipya litakalobadili uteuzi wa Kavanaugh.

Kitendo cha senate judiciary kukataa mashahidi wa Ford kilianzisha shaka.

Baada ya kulazimisha majority wakikataa FBI kukatia shaka zaidi

Kuna uwezekano kabisa Kavanaugh ni innocent. Jambo moja tukubaliane, senate judiciary GOP na WH walishindwa kuona mbele.

Kama mtu ni innocent kwanini wasingekubali mapema hayo yaishe?
Sasa wamerudi kule kule walikokataa. Ilikuwa obvious , ita FBI ondoa shaka confirm Kavanaugh. Walitegemea sana majority, ilipo flip flop wakawa flat

Kosa la kutegemea majority bila plan nyingine walilifanya katika Obamacare wakakwama. Unapokuwa na 'thin majority' chochote kinaweza kutokea, si GOP pekee hata Dems

Kilichopo hapa ni siasa tu.

Kwa nini nasema hivyo?

Kwa sababu:

Kavanaugh aliteuliwa na Rais Trump tarehe 9 Julai [2018]. Mwezi huo huo Senator Diane Feinstein akapata barua toka kwa Dr. Ford kuhusu tuhuma dhidi ya Kavanaugh.

Baada ya uteuzi, Kavanaugh akaanza 'rounds' za hapo Capitol Hill za kukutana na ma senator. Mmoja wa ma senator aliokutana nao ni Diane Feinstein.

Katika mkutano baina yao [Kavanaugh na Feinstein], senator Feinstein alikuwa tayari keshaipata hiyo barua lakini akauchuna. Hakusema chochote kwa Kavanaugh kuhusu hilo.

Kama hiyo haitoshi, Feinstein, huku akijua FBI watafanya background check nyingine dhidi ya Kavanaugh kwa ajili ya huu uteuzi mpya, hakuwatonya FBI na wala hakuwatonya maseneta wenzake kwenye judiciary committee.

Hearings za confirmation zikaanza. Ilipoonekana Kavanaugh atapata kura za kutosha toka kwenye judiciary committee na kwenye senate floor, mara ghafla eti barua ikavuja. Barua ambayo Dr. Ford alisema hakutaka ajulikane.

Diane Feinstein kakana kuwa yeye hakuivujisha hiyo barua. Na ni yeye tu [au ofisi yake] ndiye aliyekuwa na hiyo barua.

Hivi kweli unataka kunambia kuvuja kwa hiyo barua na timing yake ni coincidence tu au ni jambo lililokuwa limepangwa tokea awali?

Kama kweli Dems walikuwa na nia ya kum vet Kavanaugh, kwa nini waliishikilia hiyo barua na kuja kuivujisha kwenye dakika za mwisho mwisho?

Hitimisho langu ni hili:

Hapo kinachochezwa ni siasa tu. Dems wanataka ku delay confirmation ya Kavanaugh for as long as they can.

Kama nia yao ilikuwa ni kuhakikisha aliyeteuliwa ni msafi basi wangeshea hiyo barua na FBI mwanzoni kabisa pale walipoipata hiyo barua.

Lakini hawakufanya hivyo. Wameishikilia barua kwa karibu au zaidi ya miezi miwili huku political calculus yao ikiwa imelenga katika kuchelewesha confirmation ya Kavanaugh until after the election huku wakitumaini labda watashinda viti vya kutosha kwenye bunge la seneti na hivyo kuuzima kabisa uteuzi wa Kavanaugh.....kama vile tu ambavyo GOP waliweza kuuzima uteuzi wa Merrick Garland kabla ya uchaguzi wa 2016 na waliposhinda huo uchaguzi ndo akateuliwa Neil Gorsuch.

Jana baada ya GOP kukubali FBI wafanye huo uchuguzi wa ziada/ nyongeza, wakili wa Dr. Ford [ambaye ni mkereketwa wa chama cha Democratic] kasema eti wiki moja haitoshi kufanya huo uchunguzi. Kimsingi wanataka uchunguzi uendelee hadi chaguzi za midterm ziishe. Wanahamisha magoli.

Ford's attorney: We can't impose 'artificial limits' on this FBI investigation

Kwa hiyo ndugu yangu kilichopo hapo ni siasa mwanzo mwisho na Dr. Ford ni political pawn wa Democrats.

Kama kweli Democrats walikuwa na nia njema ya kuhakikisha Kavanaugh hana makandokando basi wangeiwasilisha hiyo barua mapema kabisa kwa FBI pindi tu walipoipata.

Lakini, hawakufanya hivyo. Hawakufanya hivyo kwa sababu walikuwa wanataka waje kuitumia baadaye kama silaha ya kuchelewesha confirmation.

Natabiri:

FBI wakimaliza huo uchunguzi wao ndani ya siku 7 na wakisema hakuna jipya, Democrats watadai muda zaidi unahitajika ili kuweza kufanya uchunguzi kikamililifu na kwamba wiki moja haitoshi kufanya uchunguzi wa madai kama hayo....hapo hapo wakijitoa fahamu kuwa waliikalia hiyo barua ya Dr Ford tokea mwezi Julai.....
 
FBI wakimaliza huo uchunguzi wao ndani ya siku 7 na wakisema hakuna jipya, Democrats watadai muda zaidi unahitajika ili kuweza kufanya uchunguzi kikamililifu na kwamba wiki moja haitoshi kufanya uchunguzi wa madai kama hayo....hapo hapo wakijitoa fahamu kuwa waliikalia hiyo barua ya Dr Ford tokea mwezi Julai.....
''Very unlikely'' kwa mujibu wa habari za leo.Inaonekana kuna jingine linafukuta ngoja tusubiri
 
Back
Top Bottom