Ingawa wengi hawamjui Sondland kikamilifu, Rais Trump anajuta kumjua.Sondland ameshika baadhi ya makomeo ya kasri jeupe mtaa 1600 Penn!
Mashahidi wameendelea kufika mbele ya kamati ya Bunge
Kwa marejeo, tulisema Balozi Gordon Sondland atakuwa tatizo, na hadi leo amekuwa tatizo
Gordon ameeleza mengi akimhusisha Rais Trump, SoS Pompeo, WH Maulveny na Guillian.
Kwanini ushahidi wake umekuwa mzito?
Kwanza, Gordon alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Rais Trump.
Alikuwa na mawasiliano na viongozi wote akiwemo VP Pence
Yeye anasema ''kashfa ya Ukraine, kila mmoja alikuwa ndani ya ''loop'' '
Hii maana yake amevunja nguvu ya hoja moja ya Republicans kwamba ni habari za kusadikika na kwamba hakuna first hand information. Hoja hiyo imekufa kwa sasa.
Gordon Sondland ni mfanyabiashara aliyeteuliwa na Trump kuwa balozi wa US katika EU
Gordon alimchangia Trump milioni 1 dola katika kampeni na kupewa ubalozi kama ahsante
Ukraine ilipopamba moto Trump alikuwa na Gordon pamoja baada ya mahojiano ya awali na kamati ya Bunge ambako alionekana kumtetea Trump.
Trump akamsifia kama mtu mwema na anayeheshimika '' well respected man''
Huko nyuma tuliwaambia kuhusu watu watatu , Balozi Yonavovitch, Volker na Rudy Guilllian
Tulisema wingi huo unatosha kuingiza waliokuwemo na wasiokuwemo na hivyo kutajana.
Kutajana ndiko kulikomweka Balozi Gordon katika wakati mgumu kwani ushahidi wake wa awali aliomtetea Trump ulionekana kuwa na matatizo.
Ili kuepukakikombe cha kudanganya chini ya kiapo, Gordon akapeleka nyongeza ya anachokijua akimtuhumu Trump kufanya nipe ni kupe au quid pro quo.
Trump akamtosa chini ya basi kama kawaida yake, ndipo Gordon akaona hamkani si shwari tena na kwamba jela inamuandama, akaamu kueleza wazi nini kimetokea.
Gordon ni mfanyabiasha hana cha kupoteza kisiasa hana sababu za unyenyekevu kwa Trump.
Alibanwa kulia kushoto, kwamba, akiendelea na Trump ataenda jela,wakati Trump keshamtosa.
Mashahidi wengine nao wamevunja nguvu za Republicans.
Leo imejulikana Ukraine walijua uhusu kuzuiwa kwa msaada na Trump tangu mwezi wa saba, Republicans walisema Ukraine walijua mwezi wa 9 hakuna uwezekano wa quid pro quo.
Republicans wanabadili hoja. Sasa wanalalamika mashahidi kama Joe Biden na Hunter hawaitwi. Balozi Volker kavunja hoja hiyo kwa kusema hakuna kosa lolote analojua juu yao.
Utetezi wa Republicans kuna nyakati unaleta matatizo.
Hoja ya kwamba whistleblower aitwe, inapingika kisheria kuna kinga ya kisheria kuhusu hilo.
Muhimu ni kuwa ikiwa wanahitaji mashahidi kama whistleblower na Biden,itabidi waeleze kwanini Trump hataki Maulveny, Pompeo na Giullian kuja kutoa ushahidi?
Katika kuhangaika na utetezi, Republicans wanasema Trump ana haki ya kuzuia misaada.
Wasichokumbuka ni kuwa Rais Nixon alifanya hivyo na mwaka uliofuata ikatungwa sheria kuwa misaada inayoidhinishwa na Bunge Rais hawezi kuizuia. Hivyo kuizuia ni kukiuka sheria.
Pamoja na ushahidi wote Republicans wamesimama na Trump na wala haionekani kama yupo atakayebadili msimamo. Hata hivyo, impeachment itakuwepo, hoja itabaki seneti.
Kuna vitu vinamsaidia Trump. Kwanza, ni muda ambao Democrats wanataka suala lisiingiliane na uchaguzi na hivyo hawana subira ya mahakama kuamua ikiwa wanaozuiliwa kutoa ushahidi na Trump wanalazimika kufika mbele ya Bunge.
Pili, Trump amewakamata Republicans kiasi kwamba hata kwenye ukweli hufikiri hatma yao.
Rais Trump ni popular sana kwa GOP na base yake. Ingawa ameshindwa kufanikisha chaguzi mbili za mgavana, bado ana nguvu. Hivyo Republicans katika congress ni mbwiga
Tatu, Rais Trump haachi alama. Michael Cohen alisema huongea kwa ''code' hatoi maandishi, wala hawasiliani moja kwa moja.
Hapa Giullian ndiye alikuwa mpambe hivyo kuna utetezi kuwa wapi alitoa maagizo?
kwa maana hakuna 'tape wala maandishi''
Suala linalobaki ni moja, nani anajua kesho italeta nini?
Tusemezane