Inasemwa, ajira 110 zitabaki Indiana na hilo linaonekama kama ushindi kwa kuanzia
Inaendelea
Wakati akiongea kuna mtu alipingana naye. Trump alkerwa na kusema 'wapo wasioamini kuwa HC amepoteza' Kwa kauli hii, akiwa Rais mtarajiwa haikuwa njema.
Alichotakiwa ni kukaa kimya aendelee na hotuba yake.
Masahili kama hayo yalimkuta Obama North Carolina, tofauti na Trump Obama aliwazuia wafuasi wake akiwataka waheshimu haki ya mtu kujieleza
Trump akazungumzia uchumi na biashara akisema atafuta mkataba wa NAFTA ulioasisiwa na Bill Clinton na kupigiwa Debe na Hillary.
Hapa haikuwa sahihi, angezungumzia mkataba bila kuwataja
Kuwataja ni kuamsha hisia kwa kundi analohitaji
Trump akarejea kauli ya ku repeal and replace Obamacare.
Inaonekana kana kwamba kuna nyakati anataka kufanya na nyakati anarudi nyuma
Trumpa akasema atafuta regulations zinazouia ukuaji wa biashara na kazi.
Akaendele kusisitiza kupunguza kodi kutoka 35 hadi 15% kwa makampuni
Katika hoja hii kuna jambo la kuangalia.
George Bush alifuta sheria zilizokwaza kazi na ajiri, na kupunguza kodi
Matokeo yake ni mdodoro wa uchumi mkubwa sana.
Haina maana kaongea jambo baya, angeangalia historia pengine kauli zingekuwa tofauti
Obama alipoingia madarakani wakati wa mdororo wa uchumi alipunguza kodi, matokeo hayakuwa kama ilivyokusudiwa. Pengine Trump ana mtazamo tofauti wenye tija.
Trump akamshambulia Obama kwa kauli za 'viongozi wasiojua wanafanya nini'
Matamshi yake dhidi ya Obama yalikuwa kauli za kampeni bila kujali ni Rais mtarajiwa
Katika siasa za nje, kasema ataimarisha visa kwa wale wanaokwenda Marekani kwa kazi za kitaalam zenye manufaa. Hadi sasa visa hutolewa kwa mtindo huo
Katika immigration, Trump kasema lengo ni kuzuia watu wasiojulikana wanatoka wapi, na wale wanaotoka maeneo 'unsafe'
Trump akatolea mfano wa mauaji ya st Bernadino, Orlando, Paris na WTC
Akasema shambulio la chuoni Ohio ni kutokana na upuuzi wa viongozi wa sasa
Trump akasema ataimarisha jeshi na kupambana na ISIS na ugadia
Hapa ndipo Trump anapoonyesha udhaifu. Kwanza, hadi leo hakuna shambulio kubwa Marekani kutoka nje. Mashambulio au mauaji ni ya watu walioko Marekani.
Kwa mfano,kijana aliyeshambulia Ohio alikuja mdogo na kuwa radicalized na mafunzo ya Alwaki
Pili, ISISI wana ideology hawana makao makuu.
Huko walipo ni ngom, mashambulizi hasa ya Ulaya yanafanywa na lone wolf kwa ushawishi.
Ili kukabliana na hali hiyo, haieleweki anawezaje kuzuia mashambulizi yanayotokana na waliokuwa radicalized ndani ya Marekani. Na je itakapotokea atasema nijni?
Inaendelea
Inaendelea
Kuhusu kupambana na ISIS hili nalo kaonyesha udhaifu.
Hadi sasa ISIS wanashambuliwa katika ngome zao.
Kuna uwezakano katika siku zilizobaki Iraq ikakombolewa.
Hoja ya ISIS itahamia Syria na huo utakuwa mtihani kwake kwasababu ya Russia
Trump hajaelewa kuwa dunia inabadilika kila uchao.
Kwa mfano, Obama alipoingia madarakani challenge ilikuwa Alqaeeda.
Alielekeza nguvu zake huko hadi kumpata Osama.
Bila kutarajia, ikazuka Arab spring iliyokuwa'complicated' ku solve kutokana na interest za America na iliyosambaza ISIS zaidi
Hivyo kutumia ISIS pekee bila kujua nini kinaweza kutokea katika dunia ya leo ni jambo litakalomkwaza mbele ya safari.
Litamkwaza kwasababu amesema hata hangaika kuondoa madikteta , anataka amani
Hapa anamaanisha kuwaondoa akina Saddam na Gaddafi ni chanzo cha matatizo
Lakini asiasahu maeneo kama Iran yanaweza kuleta usumbufu kwa US kwa njia nyingine
Hoja ni kuwa kuongelea 'item' na si ujumla wa matatizo litakuwa tatizo kwake
Na pia aliongelea kuunda kamati ya maadili.
Hili la maadili litakwenda sambamba na shughuli zake litamrudi mbele ya safari
Kwa ufupi, ameongea mengi, hayo ni kwa tafsi yetu unayoweza kuwa si sahihi na maoni binafsi
Tutaendelea na sehemu nyingine baadaye
Rais wa Taiwan amempigia simu Trump kumpongeza kwa kushinda Urais tayari liberals na democrats wameshaanza kuzungumza mambo mengi ya kuhisihisi.CHINA/TAIWAN
Kama tulivyosema, simu ya Trump kwa kiongozi wa Taiwan imeleta mjadala mzito katika media
Ni kawaida Rais mteule kuongea na viongozi wa dunia akiwa kipindi cha mpito 'tranistion'
Simu ya Trump kwa kiongozi wa Taiwan si tatizo, tatizo ni suala zima la kidiplomasia
Hilo limepanuka na mjadala kuelekea maeneo ambayo Trump asingependa yaende
Sera ya USni Taiwan ni sehemu ya China. Marekani ina uhusiano wa kidiplomasia na China si Taiwan. Mara ya mwisho kwa kiongozi wa Marekani kumpigia simu kiongozi wa Taiwan ilikuwa 1978
Kuanzia hapo uhusiano wa Taiwan unatambuliwa kupitia China kama Jimbo na si moja kwa moja
Maongezi yote ya kimataifaat least hjulikana na state dept kwa kuwa yana masilahi na US
Hapa ndipo lilipo tatizo halisi, kwamba, Trump amevunja utaratibu wa kidiplomasia na kuongea na kiongozi wa Taiwan kama 'Taifa' katika hali itakayoudhi China na utaratibu uliokuwa nje ya diplomasia
Maongezi ya Trump na kiongozi huyo ynasemwa kuwa ;private' na hapo kuchochea udadisi zaidi.
China wamefuata Diplomasia, badala ya kuongea na Trump, wametuma ujumbe WH kwa Obama kutaka maelezo ya nini kinaendelea kati ya Trump na Taiwan na China kufuatia simu hiyo
Tatizo la Simu ya Trump kwenda Taiwan
1. Trump amevunja sera za Marekani kwa Taiwan/China uliodumu kwa Marais 4, Republican na Democrat na kwa takribani miaka 40. Hii ndiyo hoja na si kwanini ameongea na kiongozi wa nje
2. Endapo anataka kubadilisha sera (policy) dhidi ya China/Taiwan kuna utaratibu
Hii ni pamoja na kusbiri aapishwe kwa mantiki kuwa kuna Rais mmoja kwa wakati mmoja
Mathalan, mzozo wowote wa kidiplomasia utakaozuka sasa hivi , mwenye mzigo ni Obama
3. Trump hakufanya mawasiliano na state dept wala WH.
Imesemwa, walioandaa ni wafanyabiasharaHapa linazuka suala jingine
Je maongezi yalihusu biashara za Trump au masilahi ya Marekani?
Tayari kuna habari Trump aliwahi kuongea na Meya wa Taiwan kuhusu uwekezaji huko
Ndivyo ilivyokuwa kwa Trump na interest za uwekezaji kule Philippine
Matatizo mbele ya Safari
1. Kwasasa WH inapaswa kuijibu China kuhusiana na maongezi. Ni wazi, lazima wapate details za maongezi hayo. Yawe yenye masilahi au binafsi kuna tatizo kwa tranisition team leo au miaka ijayo
2.China itataka kulipa kasi. Kumbuka huu ni uchumi namba 2 duniani na una influence kubwa
a) Utaanzisha trade war na china wanaweza kuleta madhara makubwa US
b) China itatunisha misuli kwa kuunga mkono North Korea. China ni muhimu kwa mzozo wa Korea
Ikiamua kumuunga mkono dogo Kim Jong Un, US na washirika kama Japan, S.Korea wana tatizo
c)Kuna mzozo wa South China Sea. Hadi sasa Philipine imeungana na China. Katika hali ya kutoelewana US ipo katika nafasi ya kupoteza kimasilahi kuliko ilivyo sasa
d)Mzozo wa Kidiplomasia utaunganisha China , Iran , Russia naTurkey inayoelekea mashariki na kuweka umoja wa NATO katika mazingira tata kuliko ilivyo sasa
3. Itakapobainika vinginevyo, washirika wa US hasa Ulaya watakuwa na misimamo yao na si ya pamoja kama nchi za NATO. Ulaya haiwezi kukubali kuingia katika mzozo wa Kidiplomasia uliosababishwa na Trump na si Marekani bila maongezi
Allie wa Marekani watakwenda 'solo' na hilo ni tatizo kubwa kwa uchumi na usalama
4. Hoja ya Blind Trust inayomhusu Trump itapata mashiko zaidi
Tusemezane
Mkuu kwanza, kabla sijaeleza mengi napenda nikufahimishe hakuna mahali nilisema kauli zako zina ji contradict."El Jefe, post: 18728496, member: 387168"]Sir, the following statements you quoted are not contradicting each other
Wasomaji , Uchaguzi umekwisha wiki tatu zilizopitaThe study that came up with a 3 million illegals figure was a nationwide study, not specific to any state.
The study can be discredited by many but it may not necessarily mean it is wrong.
Pew Research conducted their own study and found out that approximately 24 million (1 in 8) voter registrations in the US are no longer valid or are significantly inaccurate.
Ignoring these irregularities, we have the election results the way it is. The last quote is my statements with regards to the election results in its current form.
Ndugu wasomaji, Rais Reagan alipoingia WH hakuongea na CEO's wa makampuniSamahani mkuu, ila ni ajira 1100 na sio 110.
Na hili amelifanikisha hata kabla hajaapishwa kwa kupiga simu na kuzungumza na CEO. Rais Obama yupo na viongozi wengine wa serikali yake wapo ila waweshindwa kushawishi US companies kubaki US.
Wasomaji, katika bandiko la awali tulisema upotoshaji unapita kiwango na kuchukua sura ya upuuzi! samahani kwa kukosa neno mbadala na niloKuhusu NAFTA, Trump alisema hakuwa na haja ya kutaja walioanzisha au waliotetea NAFTA anachoweza kusema ni kuwa atai-fix au kujiondoa kwenye huo mkataba..
Wasomaji, wengi wanadhani ISIS ilianza kwa Obama na Hillary. ISIS ilikuwepo wakati wa Bush ndipo neno caliphate lilipoanza kusika.ISIS ni failure ya Rais Obama na Hillary, waliondoa majeshi yao huko Iraq na kutengeneza vacuum waliochipukia. Mwanzoni Rais Obama aliwadharau sana na kuwaita JV (Junior Varsity)Team, hakufikiria kuwa ipo siku wataenea zaidi ya nchi 28.
Wasomaji, kitu kama hik ni Anachronism!Rais wa Taiwan amempigia simu Trump kumpongeza kwa kushinda Urais tayari liberals na democrats wameshaanza kuzungumza mambo mengi ya kuhisihisi.
Hiki ulichoandika hapa ndicho alichokizungumza Anderson Cooper wa CNN umebeba kama kilivyo umeleta huku.
Rais Obama aliwahi kuwa-support waandamaji wa Hong Kong walipotaka kujitenga na China na aliwahi hadi kumualika Dalai Lama wa Tibet White House, cha kushangaza kelele zilipigwa na China na Liberal media za US zilikuwa kimya.
Trump kuzungumza na Rais wa Taiwan kelele zinapigwa na China kama kawaida lakini wakisaidiwa na Liberal media za US ambazo zimekuwa biased kwa Trump kwa mda mrefu, funny
Wasomaji, katika bandiko la awali tulisema upotoshaji unapita kiwango na kuchukua sura ya upuuzi! samahani kwa kukosa neno mbadala na nilo
Jana nilieleza kuhusu mkutano wa Trump Ohio nikanukuu maneno yake kuhusu NAFTA
Alisema kuwa ' ...sasa haogopi kusema NAFTA ilianzishwa na Bill na kuungwa mkono na Hillary''
Hoja yetu haikuwa NAFTA, tulisema, katika wakati huu kuwataja akina Clinton ni kuamsha hisia za wafuasi wake. Kwa mgawanyiko uliopo haikuwa sahihi, kazi ya kuuunganisha Taifa itakuwa ngumu
Sikiliza video hii chini kuanzia dakika ya 34 hadi 36 Trump akisema maneno, akiwataja akina Clinton na kuita NAFTA disaster. Akasema ataifuta au fix.
Sikiliza dakika hizo halafu usome nukuu hapo juu uone upotosha wa hali ya juu
Nina shaka comprehensions ipo katika mitaala na kama watu wanajua maana yake ni nini.
Kuandika ni jambo moja, kuelewa kilichosemwa ni jambo jingine na kuwakilisha ni kitu kingine.
Kuondoa maneno katika sentensi ni kupoteza maana, kubadili maneno ni kupoteza maana
Inafika mahali mjadala unavurgwa bila sababu za maana.
Mtu anabadili sentensi ili kukidhi haja bila kujali wanaofuatilia na wenye hamu ya kutaka habari zaidi
Inasikitisha
Nilisema, PE Trump alikuwa anaelezea concerns zake na huu utakuwa mwanzo wa kuangalia namna ya kuhakikisha kuwa hakuna illegals wanaopiga kura US na kwamba wanaopiga kuwa wote wanakuwa valid na accurate.Hoja hii surrogates wa Trump waliulizwa waithibitishe kwa facts na research. Hakuna aliyeweza
Ndugu wasomaji, Rais Reagan alipoingia WH hakuongea na CEO's wa makampuni
Alipoondoka hali ya uchumi ilikuwa nzuri na kufanya kile kinchoitwa Regan Republican
Rais Bush snr akiingia WH hakuzungumza na CEOs wa makampuni. Ha ali ya uchumi ikayumba
Rais Bill Clinton akiingia WH hakuzungumza na CEOs, alipoondoka aliacha ajira takribani 15M
Aliacha US ikiwa na surplus
Bush Jnr hakuongea na CEOs kwa bahati mbaya akiondoka aliacha nchi na recessio tunayojua
Watu walipoteza kazi katika kiwango cha malaki, masoko kupoteza thamani na deni la Taifa
Bush aliacha vita mbili zikiendelea Iraq na iran
Obama alipoingia WH alikuwa na challenge nyingi na hakuongea na CEOs hadharani.
Kwanza, kuzuia 'bleeding' ya jobs, Pili, kufanya jitiihada kama za ku bail makmpuni
Tatu kusimamia majukumu mengi ya vita zilizokuwa zinaendelea alizorithi
Kuokoa makampuni kama GM kulisaidia na kuokoa ajira kwa maelfu.
Obama alikuwa na kazi ya kutoa nchi katika negative growth, akiwa na unemployment takribani 9, na kupoteza ajira kwa kiwango cha laki kwa mwezi
Economy recovery inaonekana arguably slow lakini si negative.
Kwa mieizi 74 kwa mujibu wa Bureau of stat mfululizo serikali yake imentengeneza ajira, haikupoteza
Infalation rate imeshuka na kufikia 4.6% kwa mujibu wa takwimu
Mwezi wa 11 ajira zilizotengenezwa kwa mujibu wa stat ni 178,000
Katika mazingira hayo, hatuwezi kubeza mafanikio na mapungufu ya kila kiongozi.
Ni makosa kuchukulia deal ya Carrier kama mafanikio makubwa ya uchumi katika wiki 3 si sahihi
Ajira 178,000 tukizigawa kwa siku 30 na kwa minajili ya mjadala huu ni sawa na ajira takribani 6,000 kwa siku. Kwa maneno mengine katika siku 7 ni sawa na ajira 42,000!
Mfano huu unaonyesha kila mmoja ana njia za kutawala kama tulivyoona mlolongo wa Marais
Surrogates wa Trump wanadai Obama hakuongea na CEOs, hivi ni lazima kufanya hivyo?
Surrogates hao hawawelezi kingine chochote wakijua wapo watu watabeba tu kama yule mama wa NC aliyeulizwa na bado anaamini Obama hakuzaliwa Marekani.
Watu wa aina hiyo wamesambaa duniani. Watabebe sentensi kama walivyosikia bila kuangalia kingine
Rais Obama alivyomkaribisha Dalai Lama (Tibet's spiritual Leader) White House unaweza kusema alikosea?Wasomaji, kitu kama hik ni Anachronism!
Tulieleza kwa Rais Mteule hana tatizo kuongea na Marais wa nchi za nje.
Obama na viongozi waliofuata huo ni kama utamaduni wao.
Wiki iliyopita kabla ya hiyo simu tulisema safari hii Trump kavunja mwiko (si sheria kumbuka) kwamba Rais wa US huongea na ally kama UK kwanza
Safari hii May kawa wa 14 akitanguliwa na Nigel Farage.
Hakuna tatizo wala mpangilio bali ni utamaduni tu ambao ni tofauti.
Tukasema kilichotokea si tatizo la simu wala kuongea, ni kinyume na sera ya Marekani ya 'one China policy' tangu China ilipopata kiti UN na Mzee Salim Ahmed Salim analijua hili vema sana
Tatizo la simu ni kuwa US haina uhusiano wa diplomasia wa moja kwa moja na Taiwan kutokana na hali ya kisiasa ambayo China huona Taiwan ni jimbo na si nchi.
Hivyo maongezi hayo yatazua kile tulichosema ni diplomatic row kati ya China na US
Maongezi si lazima yasimamiwe na state dept lakini kwa hali ilivyokuwa ingalikuwa vema state dept ikawa na taarifa kwasababu US wana Rais mmoja kwa wakati na mzozo wowote utaleta taabu kwa serikali iliyopo madarakani. Kama Trump anataka kubadili policy, angesubiri aapishwe
Maneno hayo hayakupita bure, asubuhi na mapema China wakawa wamewasiliana na WH kujua kuhusu suala hilo. China hawakumjibu Trump kwasababu yeye ni mtarajiwa, serikali ipo kwa Obama
Na wala China hawakuzozona na Taiwani hadharani kwasababu mzozo ni wa kidiplomasia
Tukaendelea kusema, mbele ya safari hili litakuwa tatizo kwa Marekani
1. Litazua' trade war' isiyo na ulazima wakati huu recovery ikeiendelea na ku derail focus
2. Itaisukuma China kumuunga mkono N.Korea kama kulipa kisasi na udhibiti wa utakuwa tatizo
3. Kuna mzozo wa South China sea ambao utazidi kupanuka
Kwa hili tukaeleza kuhusu ushiriki wa Philipine na Rais wao alivyobadilika
4. Tukasema nchi za Russia, Turkey, China, Iran n.k. zitaungana dhidi ya US na kuleta matatizo
5. Tukasema washirika wa US ulaya wataamua kwenda 'solo' kwasababu US inakwenda solo
Hivi ndivyo tulivyoliangalia suala hili kwa mtazamo wetu na si suala la simu nani kapiga nani kapigiwa
Ni matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na simu ikiwemo diplomatic row kati ya US, China na mataifa mengine kwa kujua ukubwa na umuhimu wa US katika siasa za dunia
Kwa hayo 5 hapo juu tunaweza kufafanua mjadala na kufikia kurasa 50 kupata uelewa wenzetu wanafikiria nini , wanafanya nini na inaweza kutuathiri vipi.
Ndio mjadala si suala la conservative , liberal wanasema au simu just simple
Kwanini kuna competition ya east na west kuelekea Afrika?
Tunawezaje ku ignore hayo wakati US ni mkubwa wa dunia na mbabe, halafu China ni namba 2?
Chukua mfano, hoja ya 4.
Russia, Turkey, Iran, China zikitengeneza alliance, Europe na NATO itakuwa katika hali gani?
Israel itakuwa katika hali gani wakati huu inapoiangalia Iran kama tishio na wakati Iran ikiwa na washirika? Je, Trump atabadili policy ya US dhidi ya Israel?
Wasomaji, mtuelewe tunaangalia kutoka angle tofauti na ndio utamaduni wa jamvi hili
Tutaulinda tamaduni huu licha ya jitihada za kutaka kuvuruga heshima ya jamvi hili
Tusemezane
Obama na wachambuzi wote wa habari walitafuta facts kutokana na madai ya Trump
1. Si kweli kuwa ISIS ilianza wakati wa Obama, ilikuwepo kuanzia wakati wa Bush.
2. Si kweli kuwa Obama aliondoa majeshi mapema, majeshi yalianza ondoka wakati wa Bush
Hoja hizo zilipowekwa hadharani si Trump au mwingine aliyepinga, hoja ikafikia mwisho
Trump aliendelea kuitumia kwa njia nyingine kama kuenea kwa ISIS akitambua katika 'watu' wake wapo watakaobaki na utata alioanzisha, na kwa hilo mnaweza ona alivyofanikiwa