Rais wa Taiwan amempigia simu Trump kumpongeza kwa kushinda Urais tayari liberals na democrats wameshaanza kuzungumza mambo mengi ya kuhisihisi.
Hiki ulichoandika hapa ndicho alichokizungumza Anderson Cooper wa CNN umebeba kama kilivyo umeleta huku.
Rais Obama aliwahi kuwa-support waandamaji wa Hong Kong walipotaka kujitenga na China na aliwahi hadi kumualika Dalai Lama wa Tibet White House, cha kushangaza kelele zilipigwa na China na Liberal media za US zilikuwa kimya.
Trump kuzungumza na Rais wa Taiwan kelele zinapigwa na China kama kawaida lakini wakisaidiwa na Liberal media za US ambazo zimekuwa biased kwa Trump kwa mda mrefu, funny
Wasomaji, kitu kama hik ni Anachronism!
Tulieleza kwa Rais Mteule hana tatizo kuongea na Marais wa nchi za nje.
Obama na viongozi waliofuata huo ni kama utamaduni wao.
Wiki iliyopita kabla ya hiyo simu tulisema safari hii Trump kavunja mwiko (si sheria kumbuka) kwamba Rais wa US huongea na ally kama UK kwanza
Safari hii May kawa wa 14 akitanguliwa na Nigel Farage.
Hakuna tatizo wala mpangilio bali ni utamaduni tu ambao ni tofauti.
Tukasema kilichotokea si tatizo la simu wala kuongea, ni kinyume na sera ya Marekani ya 'one China policy' tangu China ilipopata kiti UN na Mzee Salim Ahmed Salim analijua hili vema sana
Tatizo la simu ni kuwa US haina uhusiano wa diplomasia wa moja kwa moja na Taiwan kutokana na hali ya kisiasa ambayo China huona Taiwan ni jimbo na si nchi.
Hivyo maongezi hayo yatazua kile tulichosema ni diplomatic row kati ya China na US
Maongezi si lazima yasimamiwe na state dept lakini kwa hali ilivyokuwa ingalikuwa vema state dept ikawa na taarifa kwasababu US wana Rais mmoja kwa wakati na mzozo wowote utaleta taabu kwa serikali iliyopo madarakani. Kama Trump anataka kubadili policy, angesubiri aapishwe
Maneno hayo hayakupita bure, asubuhi na mapema China wakawa wamewasiliana na WH kujua kuhusu suala hilo. China hawakumjibu Trump kwasababu yeye ni mtarajiwa, serikali ipo kwa Obama
Na wala China hawakuzozona na Taiwani hadharani kwasababu mzozo ni wa kidiplomasia
Tukaendelea kusema, mbele ya safari hili litakuwa tatizo kwa Marekani
1. Litazua' trade war' isiyo na ulazima wakati huu recovery ikeiendelea na ku derail focus
2. Itaisukuma China kumuunga mkono N.Korea kama kulipa kisasi na udhibiti wa utakuwa tatizo
3. Kuna mzozo wa South China sea ambao utazidi kupanuka
Kwa hili tukaeleza kuhusu ushiriki wa Philipine na Rais wao alivyobadilika
4. Tukasema nchi za Russia, Turkey, China, Iran n.k. zitaungana dhidi ya US na kuleta matatizo
5. Tukasema washirika wa US ulaya wataamua kwenda 'solo' kwasababu US inakwenda solo
Hivi ndivyo tulivyoliangalia suala hili kwa mtazamo wetu na si suala la simu nani kapiga nani kapigiwa
Ni matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na simu ikiwemo diplomatic row kati ya US, China na mataifa mengine kwa kujua ukubwa na umuhimu wa US katika siasa za dunia
Kwa hayo 5 hapo juu tunaweza kufafanua mjadala na kufikia kurasa 50 kupata uelewa wenzetu wanafikiria nini , wanafanya nini na inaweza kutuathiri vipi.
Ndio mjadala si suala la conservative , liberal wanasema au simu just simple
Kwanini kuna competition ya east na west kuelekea Afrika?
Tunawezaje ku ignore hayo wakati US ni mkubwa wa dunia na mbabe, halafu China ni namba 2?
Chukua mfano, hoja ya 4.
Russia, Turkey, Iran, China zikitengeneza alliance, Europe na NATO itakuwa katika hali gani?
Israel itakuwa katika hali gani wakati huu inapoiangalia Iran kama tishio na wakati Iran ikiwa na washirika? Je, Trump atabadili policy ya US dhidi ya Israel?
Wasomaji, mtuelewe tunaangalia kutoka angle tofauti na ndio utamaduni wa jamvi hili
Tutaulinda tamaduni huu licha ya jitihada za kutaka kuvuruga heshima ya jamvi hili
Tusemezane