McCain(Rep) ameongelea kwa uhakika kuwa Russia wali ingilia akiwa ni senior senator
Hivi huyo babu ana credibility gani?
Ulimsikia kipindi kile cha kabla ya uvamizi wa Iraq?
Babu hana credibility kabisa huyo.
Jionee mwenyewe hapo....
Sasa hapo vipi baada ya kuziangalia hizo video? Babu alikuwa sahihi? Au hakuwa anaongea kwa kujiamini?
Hadi hapo hoja si matokeo, wala hacking iliyoathiri matokeo bali alleged external influence
Na wala hakujatolewa uthibitisho, kinachotaki ni investigation itakayohusisha IC na kamati za Bunge
Ndo maana nasema kuna kila harufu ya propaganda za kisiasa tu. Election cycle ya Marekani huwa haina mwisho. Ni endelevu.
Ukidhani hakuna nia za kisiasa hapo basi lazima utakuwa naive sana.
Kinachoshangaza ni kuwa investigation haiwezi kutoa matokeo nje ya yale yaliyopatikana kwa uchunguzi wa vyombo husika. Hivyo kwanini Trump anakataa hilo ilihali Urais wake upo pale pale?
Mimi naamini there is no there there.
Hivi unadhani roles zingebadilishwa na tuseme Dems ndo wangekuwa beneficiaries wa hiyo alleged hacking ya Russia wasinge react kama anavyo react Trump?
Kilichopo hapo ni siasa tu.
Trump amehoji credibility ya security apparatus zake kama CIA.
Na ana hoja ya msingi kabisa.
Kwani uongo kwamba CIA huwa hawadanganyi? Ni uongo kwamba CIA huwa hawakosei?
Kabisa unadhani kuwa huko CIA kila mtumishi ni apolitical?
Ni Trump aliyemsifia James Comey na kutumia taarifa tu za kufungua uchunguzi kuhusu email.
Leo inakuwaje ni jambo asiloamini vyombo ambavyo sasa vitakuwa chini yake?
Hahaaaa mimi ni bonge la political junkie. Nasikiliza talk radio za pande zote [left and right] kila siku. Naangalia politcal shows kwenye cable networks.
Kwa hiyo, kuhusu hilo la Trump kumsifia Comey halafu baadae kuonekana kana kwamba haamini [baadhi ya] kazi zinazofanywa na hivyo vyombo ambavyo vitakuja kuwa chini yake, mimi nakwambia hapo ni siasa tu.
Kama huamini hebu cheki hizo video hapo chini uone jinsi ambavyo Democrats walivyokuwa wanamwagia masifa kemkem huyo huyo James Comey pale aliposema FBI haitapendekeza mashitaka dhidi ya Bi. Clinton halafu baadae walipokuja kumgeuka aliposema FBI wanafufua tena uchunguzi dhidi yake.
Republicans nao walimlaani Comey aliposema Hillary hatafunguliwa mashitaka halafu alipokuja kusema kuwa wanafufua tena uchunguzi wakaanza kumsifia.
Hivyo mimi nakuhakikishia kuwa hapo kuna malengo ya kisiasa tu kwa sababu kwenye siasa perception ndo reality.
Ukifanikiwa kumjengea mpinzani wako taswira flani...haijalishi kama ni ya kweli au la...halafu hiyo taswira imgande, basi huo ni ushindi kwa kiasi flani.
Ndo maana sishangai kuona Dems wamekomalia huo uchunguzi na hizo habari za Russia kuingilia uchaguzi wao kwa sababu hilo linahusiana na 'bromance' kati ya Putin na Trump.