Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Clinton ameshinda Washinton state blue state
 
kwakukusanya 234 naona Trump kawanyamazisha wapinzani wake ndani ya chama na nje ya chama. Na akishinda (nategemea ashinde) atafanya kazi yake ya Urais kwa uhuru zaidi kama Rais wetu Magufuli.
 
Kuna state ya Maine, hawa wana EV 1 ambayo ni muhimu sana hasa kwa Trump kwasababu inaweza kumfikisha 270 kama , narudia kama matokeo mengine yatabaki kama yalivyo

Maine inatoa EV kwa congressional district
 
Hakuna namna Clinton anaweza akapata tena ushindi...katika hali hii, natamka kwamba Trump ndiye Rais mteule wa Marekani! Clinton sasa akamate simu tu akampongeze Trump.
Mkuu unakumbuka hii?
 
Trump ameshinda Iowa

Kama tulivyosema mwanzoni, Ohi na Iowa zitakwenda Trump na hivyo ndivyo ilivyo
 
Reactions: PNC
Pennsylvania imebadilika na sasa ni kwa Trump

Trump akishinda hii, tayari anakuwa president elect

Hali kwa Dem ni mbaya kuliko ilivyotarajiwa kwani Pen haijaenda Republican tangu 1992
 
Hakuna namna Clinton anaweza akapata tena ushindi...katika hali hii, natamka kwamba Trump ndiye Rais mteule wa Marekani! Clinton sasa akamate simu tu akampongeze Trump.
Mkuu naungana na ww no way, jamaa hata hizo state zilizobaki anongoza pia, ngoja tusubiri final results, ni maajabu tu Clinton kushinda
 
Mkuu naungana na ww no way, jamaa hata hizo state zilizobaki anongoza pia, ngoja tusubiri final results, ni maajabu tu Clinton kushinda
Kama Michigan na Wisconsin zingebaki blue, huenda kungekuwa na matumaini kwa Clinton

As it is now, game imebadilika anayetafuta njia ya 270 ni Clinton na si Trump
 
Main Stream Media na kura za maoni zilimdanganya HRC!! na yeye akadanganyika!! Wamarekani waliiona hatari iliyokuwepo ya 'Mama' kuiporomosha Marekani kwa mwendokasi wa ajabu!
 
Utah Trump atashinda kutokana na namba zilizopo.

Nevada Clinton atashinda kutokana na namba

Minnesota Clinton atashinda

Arizona Trump atashinda

Maine congressional district bado ni tight kuna EV 1

Hizi hazijawa projected ni kutokana na tofauti ya namba tunazoona. Zisichukuliwe kama final tafadhali
 
Masoko yametetereka kama ilivyokuwa Brexit ambapo Dow J imepoteza 4.5%
 
Wanajamvi

Kutokana na namba zinaoonekana Trump atashinda Pennyslavania

Kwa mantiki hiyo na kwa kuangalia Wisconsin na Michigan :

DONALD TRUMP IS PRESIDENT ELECT

Hakuna namna Hillary anaweza ku recover

Hesabu ni kama hizi
New Hamshire Trump anaongoza na hakuna mahali Dem watapata kura. EV 6
Michigan ina EV 18. Wisconsin 10. Jumla ni 34.

232 + 34= 268

Hapa kuna Arizona yenye EV 10 na hivyo kuwa na EV 278
 
Trump ameshinda Utah red state
 
Reactions: PNC
Jambo linalowaumiza Clinton kampeni ni moja
Kwamba Trump angeshinda swing state zote bado asingekuwa Rais.

Walichotaka ni kushinda New Hampshire tu.
Hii ingewekana kama wangelinda Wisconsin na Michigan

Uchaguzi umeamualiwa na blue state, hilo watajiuliza na watalia nalo sana

Pamoja na hayo kuna mambo yatakayotokea

Kutetereka kwa masoko kwasababu market hazitaki uncertainty

Comey atakuwa mjadala kuelekea mbele

WikiLeaks iliyoingilia democrat na si Republican itakuwa katika mjadala

Kwa upande wa Democrat

Kwanini wameruhusu mchezo kuchezewa 'maeneo yao' kama WI na MI

Bernie Sanders factor 'Bernie or bust' itakuwa katika mjadala

Lag time kabla ya Comey ilikuwa obvious kwani hawakufanya mikutano mingi

Kwa upande wa race

Swali litakalojadiliwa, Latinos wana impact gani pamoja na expolisions kule FL

Je, hii ni rebellion ya white kwamba Rais wao anachaguliwa na competition ya race (black/Latinos)

Je, wananchi wamechoka na 'the establishment' ?

Baadhi ya haya yatakuwa katika mjadala, lakini kwa sasa President elect Trump atakutana na incumbent president Obama siku ya Alhamisi

Kwamba uchaguzi umeisha hilo halina mjadala tena, na kwamba Trump kashinda uchaguzi
 
Tathmini , maoni, mafunzo yataendelea katika bandiko hili

Hakuna ukweli mwingine isipokuwa ukweli kuwa Trump kashinda.

Dunia imeshangazwa lakini ndiyo demokrasia ya wenzetu inavyofanya kazi.

Kwenda mbele kuna mambo yatakayojitokeza haraka

- Je, Rep waliomkataa Trump watafanya naye kazi?

- Trump atapitishaje agenda zake kukiwa na resentment

- Atafuta Obama care katika siku 100

- Atajenga ukuta kama alivyoahidi?

-Atabadili mikataba ya biashara?

-Ataondoa majeshi ya Marekani yaliyoko nje?

Haya ni mambo yanayomkabili akiwa na divided Republican. Shaka hapa ni kuwa kama hakuwaunganisha wakati wa uchaguzi ataweza mbele ya safari?

Kinachofanyika sasa ni postmortem na way forward kwa ulimwengu kutokana na matokeo ya Taifa lenye nguvu za kila aina duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…