1. Baadhi tulijua madhara ya wikileaks, na tukajaribu kuyaeleza hapa, ingawa hatukueleweka!
2.Wanawake wanapendana ila wanachukia ulaghai na kusingiziana. Ile ya Hillary kutumia wale wa mama kumsema vibaya Trump tena bila ushahidi iliwakera wanawake wengi. Mwanzoni Hillary kabla ya kuharibu alikuwa na back up kubwa ya wamama kiasi cha Trump kusema Hillary hana lolote isipokuwa nakuwa protected na 'woman factor '!
3.Ni kweli policy za serikali ya Obama na establishments wao hasa zile za ndani zinazolenga kuwadhibiti middle class na wale wa vipato vya chini zimechangia Trump kushinda.
4. Zimepigwa na butwaa kwani kwa nguvu kubwa iliyotumika kumbeba Hillary kwenye kampeni ingeweza kuwa dissolved na jeshi la 'mtu mmoja, Trump '
Mkuu it's too early kujua nini kimesababisha na bandiko langu ulilonukuu sija single out sababu halisi
Nilichosema ni kuorodhesha wachunguzi wanayoyafanyia kazi kwa takwimu
The notion kwamba alibebwa bila kuwa na back up evidence(s) hazileti mantiki
Kwa mfano, kushindwa kwa Clinton katika blue state utakuelezaje kwa hoja hapo juu?
Tayari wachunguzi wanasema Clinton alichukulia Wisconsin for granted.
Tangu primaries hakurudi tena, Trump amekwenda mara kadhaa VP wake na Speaker Ryan wakizunguka, wapiga kura walipiga kwa kusikiliza hoja za Trup pekee
Sasa ukitazama 'facts' zako hakuna inayo fit narrative hata moja.
Pili, wanafuatilia kwanini idadi ya white imeongezeka wakati blacks ikipungua na Latinos wakiwa hawana effect iliyotarajiwa kwa Clinton?conclusion yako hai fit popote
Tatu,wanaangali ni Comey au WikiLeaks ipi ilikuwa na impacts. Kwa mfano, WikiLeaks zilitoa habari za kampeni za primaries, je, wafuasi wa Sanders walio retaliate
Nne, Kampeni ya Clinton kabla ya Comey ilikuwa inafanya mkutano mmoja kwa siku, Trump akifanya mine au mitano. Je, kampeni iliwafikia watu wa vijijini?
Tano, ukiangalia mikutano ya Trump ilikuwa inajaza watu . Hawa walikuwa wapi na wana reservation gani kuhusu system au mgombea?
Ni watu wa Republican? Ni watu wa GOP na Sanders, ni independents au ni kitu gani
Sita, kwanini wanawake waliotegemewa kumuunga mkono hawakufanya hivyo.
Lazima data zipatikane kwa locations n.k. Kama wanawake wamechukizwa na kashfa za wenzao, wanaume wamechukizwa na nini? Kwa analysis yako hakuna jibu
Saba, kunatakiwa takwimu za college educated, non educated na kwanini kuna tofauti
Nane, kunatakiwa analysis kuhusu uchumi na suala zima la jamii kama race
Tisa, kama chuki ni establishment kwanini katika congress na senate wamerudi wengi?
Kumi, yale aliyozua Trump yalipokelewaje na wapiga kura
Kumi na moja, kuna uhusiano gani wa BREXIT na Uchaguzi.
' Is it the new world order politically''
Orodha inaendelea. Ndiyo maana watu wanachanga akili kujua nini kimetokea
Hapa wenzetu wanapotuzidi, kwamba, wanafanya postmortem ya kila jambo kwa kina
Kusema Prof kasema si fact, ni maoni Prof mwingine anaweza kuwa tofauti.
Nimeandika haya kama yupo atakayenielewa.
Watanzania hatuna utamaduni wa kufuatilia mambo.
Nimesoma maoni ya mswada unaopelekwa kuondoa watumishi baadhi kutoka utumishi
Hakuna anayehoji ni kwanini imetokea, huko nyuma ilikuwaje na imelenga nini na impact yake ni kitu gani. Mwisho wa siku watu wanashtukizwa tu na kuanza kulalama
Hili linazidi kueleza hata upande wa siasa. Baada ya uchaguzi hakuna anayefanya analysis kwanini CCM ikiwa imechukiwa na wananchi bado imeshinda.
Je, ni system ilitotumika kuwahujumu? Na kama ni ndiyo ni ipi na kwa njia gani?
Je, ni sera zao zisizokubalika, kama ni hivyo eneo gani hawakugusia
Je, ni wagombea wao na agenda za taifa? Na kama ndivyo nini kinafanyika
Dunia ya sasa is all about how you interpret information etc
Tusemezane