''ROLL BACK'' ?
Kama mtakumbuka katika nyuzi ya primaries tulieleza tatizo la kutokuwa na ''specifics'' katika sera
Baada ya uchaguzi
Mag3 amekuwa akileta update the popular vote
Haitegemewi popular vote kubadili matokeo lakini tulisema ina maana
Mkuu
TUJITEGEMEE aliuliza nini hatma baada ya uchaguzi?
Mahojiano ya Trump na NY times yanaeleza mengi kuhusu hali ilivyo
1. Tunaelewa Obamacare haitafutwa day one kama ilivyoahaidiwa.
Hili limeongelewa siku za nyuma. Kinachoonekana ni kukosa mbadala wa nini kifanyike na uwezekano wa kuleta mtafaruku kwa kufuta tu
2. Mahojiano, Trump ameeleza kutokuwa na nia uchunguzi dhidi ya Clinton.
Huko nyuma alisema 'lock her up' na kuahidi AG kuunda timu ya uchaguzi. Sababu alizotoa jana suala litaligawa Taifa zaidi.
Hapa popular vote inapoonekana kuwa na nguvu,na tofauti ya kampeni na reality
3.Trump ameeleza mahusiano ya kazi za binadamu na Climate change.
Huko nyuma alisema Climate change ni Hoax iliyotengenezwa tu
Suala la coal litawezekana?
4. Ame ''signal'' kupitia upya mikataba ya NAFTA
Katika video aliyotuma mahusiano na TPP kwa negotiations maalum
Nchi kama Japan zilieleza kwenda 'solo' na TPP. Marekana itafanya 'protectionism' iki trade na nani? Kumbuka Brexit itakuwa na makovyu pia
Kwa maana hiyo, Trump hakuwa na sera za mbadala kwamba atafanya nini
Kinachofanyika sasa katika transition ni kutengeneza sera mbadala
Tatizo lake hizo mbadala zinaweza zisi reflect ahadi zake
Au, zinaweza kukabiliwa na matatizo yatakyolazimisha zibaki zilizopo
Kwa mfano, Brexit inategemewa kuleta mtafaruku wa uchumi Europe
Katika ''Global economy'' impact itafika kila kona.
Ni kama ilivyokuwa kwa Greece na Italy.
Hivyo kujitoa NAFTA au TPP inaweza kutokuwa na uhalisia
Huko nyuma alisema Obamacare, NAFTA, TPP ni disaster na atazifuta mara moja. Inaelekea huko ?