Duru za siasa - Matukio

Inaendelea.....

Tanzania: Ujio wa Obama Tanzania ni wa kiuchumi zaidi.
Tukumbuke kuwa Rais wa China mara baada ya kuapishwa alikuja Tanzania.

China ina miradi mingi sana Afrika hata kufikia kujenga makao makuu ya AU kwa gharama zao. Imejiingiza katika kila nchi kutoa misaada ya ujenzi, ufundi n.k.

Interest za China kwa Tanzania ni zaidi ya sehemu nyingine za Afrika kwasababu, kwanza, Tanzania ilisimama kidete wakati wa suala la China kuwa katika UN.
Ni kwa kutazama hilo China inaona Tanzania ni muhimu na ni rafiki anayeaminika.

Kwa kulipa fadhila hizo China walijenga Tazara, mradi mkubwa waliowahi kuufanya barani Afrika.

Lakini pia kimkakati Tanzania ipo mahali pazuri. Sasa hivi China imejiingiza sana maeneo kama Congo na Zambia, na Tanzania ni eneo muhimu la kuingiza na kutoa bidhaa zao.

Tanzania inaonekana kuwa ni uchumi unaokua, kwamba hilo lina ukweli inabaki kujadiliwa.
Kilicho na ukweli ni kuhusu maliasili kama madini na gesi ambazo ni muhimu sana kwa matumizi ya nishati ambayo China inayahitaji kukuza uchumi wake.

Ukuaji wa uchumi wa china ni kiwango cha asilimia 8-9 kwa mwaka, na wachumi wanatabiri kuwa kama hali itabaki kama ilivyo China itakuwa na uchumi nambari 1 baada ya miaka 10-15 ijayo

China na Marekani zinatambua kuwa uchumi wa Afrika unakua kwa kasi na ni moja ya chumi 10 zinazokua kwa kasi duniani(namba 6)

Wachumi wanatabiri kuwa katika miaka ijayo Afrika utakuwa uwanja wa vita ya kiuchumi kati ya Mashariki na Magharibi,Kwahiyo ziara ya rais wa China ilikuwa kuweka mambo sawa kabla ya wapinzani hawajatia timu(U.S.A)

Ujio wa obama umelenga kiuchumi zaidi na kwa kiasi fulani kiusalama.
Kiusalama ni kuzingatia kudorora kwa hali ya pembe ya Afrika (Somalia) ambako ni kiota cha kuzalisha magaidi wa siku za baadaye, na pia usalama wa maziwa makuu

Tanzania ina moja ya balozi kubwa za Marekani katika sub sahara.
Balozi za Marekani ni za kiusalama na kiuchumi na uwepo wake una sababu.
Hivyo Tanzania kama ilivyo Senegal ipo katika eneo la mkakati kiusalama

Ziara ya Obama itamchukua hadi kuzindua mradi wa umeme unaosimamiwa na GE Co.
Hii ni kampuni kubwa sana Duniani kiasi cha kujiuliza kuna nini hadi iwekeze Tanzania katika nishati?

Jibu hapa ni geresha tu kuwa Wamarekani wana interest ya kusaidia katika nishati .
Nyuma yake kuna suala la gesi na madini kama vile Uranium.

Mkakati ni kuhakikisha kuwa maliasili hizo hazitumiki au kutumiwa ''vibaya'' na wapinzani wa Marekani kiuchumi.

Siku zijazo watakuwa na sababu za kusema wao walianza kuwekeza katika nishati miaka mingi iliyopita

Na katika kuficha lengo la ziara hiyo Rais wa zamani G.Bush amekuja kusimamia ujenzi wa Clinic ya Kansa. Ni Bush huyu huyu aliyesaini Millenium Challenge na ni Bush huyo huyo aliyegawa vyandarau kuzuia Malaria. Rais wa Marekani agawe vyandarau???

Bush atakuwepo katika round table na CEOs na wafanyabiashara. Leo tunaonyeshwa picha akipaka rangi clinic. Hapo hapo kuna Clinton foundation ambayo nayo kama zingine inashughulikia mambo ya afya!!!

Haya yote ni kuhakikisha kuwa lengo la ziara ambalo ni kiuchumi linafunikwa ili kuepuka vita isiyo ya lazima ya kiuchumi na China au nchi za BRICS

Inaweza kuchukua miaka 10 kabla ya rais wa Marekani hajaietembelea Tanzania tena.
Kazi kubwa imeshafanywa na akina Clinton na Bush na Obama anamalizia tu.
Shughuli nyingine zitaendelea kufanywa na balozi na maafisa wa serikali ya Marekani

Tunasisitiza kuwa kazi za balozi za wenzetu si kutoa visa na kupokea wageni.
Ni pamoja na ulinzi na usalama ambavyo haviachani na uchumi.

Ni wakati sasa tujifunze kuwa balozi zetu si vituo vya visa au mapunziko kwa viongozi wastaafu, ni sehemu muhimu sana za usalama na uchumi wa nchi.

Sina hakika kama balozi zetu zilizopo Kigali, Kampala au Nairobi zinaweza kutueleza kwa ukamilifu nini kilichopo nyuma ya mkutano wa Kagame, Uhuru na Museveni.

Hiyo ndiyo sehemu ya kazi za ubalozi na lazima tubadilike na kuelewa kuwa usalama wa taifa au nchi si bunduki au kung'oana kucha ni pamoja na uchumi kwa dunia tuliyo nayo

Tusemezane
 
Dah!
mkuu hilo la ujio wa obama umemaliza. sijui Majirani zetu Kenya wanalichukuliaje!!
bado najiuliza maswali ni kwanini swala la ushoga Obama hajalizungumza hapa kwetu TZ? au kasoma upepo!
Tunasubiri uchambuzi wa matukio ya Misri.
 
Dah!
mkuu hilo la ujio wa obama umemaliza. sijui Majirani zetu Kenya wanalichukuliaje!!
bado najiuliza maswali ni kwanini swala la ushoga Obama hajalizungumza hapa kwetu TZ? au kasoma upepo!
Tunasubiri uchambuzi wa matukio ya Misri.
Kuhusu Kenya, hakika imewauma sana. Tatizo moja la Kenya ni kuamini kuwa Obama ni Mkenya aliyetokea kuwa Rais wa taifa kubwa.
Wanasahau ukweli kuwa Obama ni Raia wa Marekani mwenye unasaba na watu wa Kenya, baasi.

Siku za karibuni imegundulika kuwa Prince William ana unasaba wa Kihindi kupitia ukoo wa mama yake marehem Diana.

Hili limetokana na kuangalia kitu kinaitwa 'family tree'' historia na Technology ya DNA.
Je, Wahindi nao wapige mayowe hovyo?

Kwetu sisi kuna nadharia kuwa watu wa visiwa vya Fiji ni wenyeji kutoka Rufiji. Nisichokielewa ni kuwa kwanini hawatumii technology na kubaini ukweli huo.Hiyo haitamfanya mfiji awe Mtanzania bali mfiji atakuwa ana unasaba na Tanzania kama itatokea na kama nadhari hiyo ni kweli.

Kuhusu Ushoga, kwa ziara ya rais wa Marekani lazima ifanywe homework ya kutosha.
Kuna wataalam wa mambo ya sosholojia/Mahusiano/ Ushirikiano wa kimataifa walikuwepo kitambo sana ambao wanaielewa Tanzania.

Kwahiyo Obama alikuwa na information zote kuhusu Tanzania na jinsi gani ushoga unavyoweza kuleta mtafaruku na kutibua mipangilio yake. Pengine anajua hata bunge kuahirishwa kwasababu tu ya neno ushoga na uliberali kutamkwa

Ziara zake si kuja kutembea ilikuwa ni mission kwa jambo mahususi.
Hiyo ajenda ya ushoga itasukumwa kwa njia nyingine za haki za binadamu n.k.

Zumbe mkuu, ziara za rais wa Marekani ni ghali sana na mwisho wa siku wapo watu wanaoangalia kama kuna tija iliyopatikana. Labda nikuibie kasiri kuwa Obama alipaswa kutembelea mbuga za Wanyama.

Ghafla ziara ikaondolewa katika ratiba. Hiyo ilitokana na vyombo vya habari kuhoji kama hii ni ziara ya kiserekali au vacation.

Na kama ni vacation kwanini zitumike pesa za walipa kodi. Maandalizi ya kwenda mbugani yangegharimu mamilioni ya fedha na hivyo administration ikaona ili kutovuruga ziara suala hilo liachwe na ndivyo suala la ushoga au kile ambacho hakikusemwa lilivyoshughulikiwa. Ndivyo intelejensia inavyofanya kazi siyo kung'oa kucha za raia kwa 'plaizi'


(Hebu tutupie macho kidogo Tahariri square na brotherhood usiku huu.)
 
HALI TETE NCHINI MISRI: ANGUKO LA MORSI LAKARIBIA

Wiki hii Tahariri square nchini Misri imerudi kama ilivyokuwa mwaka 2011. Ni Tahariri square ndio ilikuwa anguko la Hosni Mubarak na inavyoonekana hakuna shaka tena kuwa historia itajirudia.

Tayari watu zaidi ya 15 wameshapoteza maisha kufuatia mapambano kati ya makundi yanayounga mkono serikali na wanaopinga serikali ya Rais Morsi chini ya Muslimbrotherhood. Kwa undani wa Muslim Brotherhood tafadhali rejea katika nyuzi za nyuma kama zilivyoorodheshwa hapo ukurusa wa mwanazo.

Maandamano ya safari hii ni makubwa yanayokadiriwa kufanywa na watu zaidi ya milioni 14. Misri ina idadi ya watu milioni 90 takribani, ikiwa ni moja ya mataifa ya ulimwengu wa kiarabu yenye watu wengi.

Maandamano na mikusanyiko hiyo inamtaka rais Morsi aachie madaraka kwasababu za kushindwa kuleta mabadiliko tarajiwa. Hadi sasa serikali ya Morsi imeshapoteza mawaziri 5 akiwemo waziri wa mambo ya nje, na maafisa wa Ikulu kama msemaji wa rais na msemaji wa baraza la mawaziri.

Jeshi la nchi hiyo likiongozwa na Gen Abdul Fettah el Sisi limetoa masaa 48 hadi Jumanne kwa Morsi kupata mwafaka na wapinzani. Asubuhi ya Jumatano jeshi limetoa mwongozo 'road map' ya nini kitatokea. Katika mwongozo huo jeshi linasema kutaundwa baraza la uongozi chini ya jaji mkuu litakaloongoza nchi hadi uchaguzi.

Wakati hayo yakitokea wapinzani wamepingana na jeshi kwa kusema hilo ni suala la kisiasa na halipaswi kuingiliwa kijeshi.Wakati huo huo Rais Morsi anasema yeye alichaguliwa kidemokrasia na kumuondoa ni sawa na kuleta mapinduzi.

Vikundi vya waislam wenye misimamo mikali tayari vimeshatoa tamko kuwa suluhu ni kuwa na uchaguzi tena.Vikundi hivyo kikiwemo cha Nuuru vinataka uchaguzi ufanyike haraka wakati watu wakiwa wamegawanyika ili Brotherhood waweze kushinda tena.

Kikubwa kinacholeta mzozo ni serikali ya Morsi kushindwa kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa, kuigeuza katiba ya nchi na kuchomeka mambo yanayokinzana na waliberali, na serikali ya Morsi kutwaa madaraka ya vyombo vya sheria na kuonekana kuelekea katika kuliingia jeshi.

Hakuna sababu za kuhofia kuwa jeshi litachukua nchi kwasababu nchini misri jeshi ni taasisi inayojitegemea(institution) ikiwa na taratibu zake zenyewe. Ingawa jenerali El Sisi ametoa kauli bado kuna kusigana na kauli ya baraza la kijeshi linalosisitiza jeshi kuwa mbali.

Gen El Sisi aliteuliwa na Morsi kuchukua nafasi ya Gen Tantawi ikiwa ni katika jitihada za kuondoa masalia ya Mubarak.Kwa bahati mbaya Morsi asingeweza kuondoa kila mtu kwa kuzingatia ukubwa wa jeshi.

Jeshi la Misri lina askari nusu milioni na ni la tano kwa ukubwa duniani. Hivyo haitarajiwi kuwa kila mtu aliridhia mabadiliko ya Morsi kumuondoa Gen Tantawi na upinzani unaonekana kutoka ndani ni matokeo ya misiguano ndani ya jeshi.

Kitakachotokea kesho na kuendelea ni kuanza kuona magari na deraya za kijeshi zikiingia mjini. Zitaingia mjii ili kuepusha vita ya kiraia ambayo sasa ni wazi. Ni vita ya wale wanaompinga Morsi na Wafuasi wa Brotherhood. Kwahiyo tutegemee jeshi kuingia ili kuyatenga makundi hayo.

Katika mkusanyiko wa wakati huu wafuasi wa Morsi na Brootherhood wanaonekana kuwa wachache ukilinganisha na wapenda mabadiliko kama ni sahihi kusema hivyo.

Hivyo basi anguko la rais Morsi ni wazi na kutatokea mapambano makali kufuatia kauli yake ya kulikemea jeshi lisiingilie mambo ya kisiasa.

Swali la kujiuliza kwanini Tahiri imerudi na kwanini Morsi yupo katika njia panda?

Itaendelea.....
 
Inaendelea.....

Kwanza tumjue kidogo huyu Gen Fatteh el Sisi. Gen ana umri wa miaka 59 na amepata mafunzo ya kijeshi nchi Misiri.

Alipanda ngazi za uongozi katika jeshi na kuwa mnadhimu wa jeshi kabla ya kuwa kamanda wa vikosi vya kaskazini.

Uteuzi wake kutoka kwa Morsi haukutegemewa sana kwa kutambua kuwa hakuwa katika ngazi za wazee wa jeshi kama akina Gen Tantawi.
Ni mtu mwenye ushawishi wa hoja katika maongezi hasa yanayohusu jamii na ana mahusiano ya kidiplomasia na ushirika na Marekani.

Mwanzoni hakuonekana kuwa maarufu sana lakini kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo umaarufu wake unavyozidi.Waandamanaji wanamtegemea sana Gen Sisi kuingiza deraya na vifaa vya kijeshi ili kumuondoa Morsi Madarakani.

Na pengine uteuzi wake uliwagusa washirika wa Tantawi kitu kinachopelekea atafute umaarufu wa kuungwa mkono.

Matarajio ya wana Tahariri ni kuona jaji mkuu akichukua uongozi wa nchi na kuitisha uchaguzi. Hata hivyo tusitegemee uchaguzi katika kipindi cha miezi 3 had 6.

Hii ni kutoa nafasi kwa vyama vya kisiasa kujipanga na kutorudia kosa la awali ambapo Brotherhood walishinda kwa maandalizi yao ya muda mrefu.

Kinachomponza Morsi ni makundi ya waislam wenye misimamo mikali kushinikiza kubadilishwa au kuchomekwa vifungu katika katiba na sheria kwa mitazamo ya kidini.

Makundi haya siyo ya Brotherhood halisi. Tumeshaeleza huko nyuma kuwa Brotherhood ni watu makini na wenye weledi sana na wasingeweza kufanya mambo kiholela.

Kwa bahati mbaya ajenda yao imetekwa na manazi na washabiki ambao kila uchao wanataka mabadiliko bila kuzingatia nafasi za Wamisri wengine katika ujenzi wa taifa lao.
Hawa ndio waliomfikisha Morsi hapo alipo na wala si Brotherhood halisi.

Sababu ya pili ni kushindwa kutimiza ahadi. Brotherhood walikuwa na matarajio makubwa ya kufanya mageuzi ya kijamii na kiuchumi kwa muda mfupi. Watu waliweka matumaini yao na sasa ni mwaka hakuna kiachoendelea. Bado umasikini umezidi kupamba moto majumbani na mitaani

Tatizo si kushindwa kwa Brotherhood kutimiza ahadi, ni kutokana na uchumi uliodorara sana kuanzia anguko la Mubarak.Matarajio ya watu yalikuwa makubwa na hivyo kusahau kuwa unahitajika muda kuyakidhi.

Tatizo lingine ni Morsi kutaka kutwaa madaraka ya vyombo vya sheria na kumiliki jeshi.
Hili wamisri wanaliona kama kukaribisha udikteta kwasabau kutakuwa hakuna 'watch dog'.

Wao wanaamini kuwa vyombo vya sheria kama mahakama na jeshi ni watch dog na jitihada za kutaka kuviteka ni jitihada za kudumaza demokrasia.

Sasa mambo hayo ukichanganya na hali mbaya ya maisha ndiyo yanayoplekea maandamano ya kutaka kumuondoa Morsi.

Lakini pia tukumbuke kuwa ushindi wa Morsi ulikuwa katika asilimia kama 51 au zaidi kidogo na hivyo wapinzani wanaona kumpa nafasi kutekeleza ajenda zake ni kutafuta msiba wa kisiasa ''commit political suicide' Hivyo njia rahisi ni kumdhibiti mapema.

Ukweli unabaki kuwa Morsi alichaguliwa kidemokrasia na yapaswa apewe muda wa kutimiza ajenda zake. Kumuondoa kwa maandamno si njia nzuri kwasababu itatoa nafasi ya kuibinya demokrasia pale mtu au kikundi cha watu kitakapoona ni muafaka.
Njia hiyo haitasaidia taifa kuwa na muafaka(political stability) na ni njia hatari sana kwa ustawi.

Lakini pia jeshi linapaswa kuwa mbali na mambo ya kisiasa. Kinachoonekana sasa hivi ni ushabiki wa kisiasa kwa kisingizo cha kulinda amani.

Mbona ilichukua miezi kabla ya jeshi kuingia mitaani wakati wa Mubarak? Iweje jeshi lile lile lililomvumilia Mubarak litoe ultimatum kwa morsi tena ya masaa 48? Je hapo hakuna double standard.

Tutaendelea kufuatilia habari za Misri na kuwaletea kila kinachoendelea

Tusemezane
 
UPDATE KUTOKA VYANZO MBALI MBALI (MISRI)

Jeshi limekizingira kituo cha utanganazaji cha serikali karibu na ukingo wa mto Nile. Wafanyakazi wasio wa lazima wamerudishwa majumbani kwao
Kuna habari pia za uwanja wa ndege kufungwa na kuzuiwa kwa Morsi na wafuasi wengine 30 wa brotherhood kuondoka

Jitihada za Morsi kuongea na wapinzani ili kuunda serikali ya kitaifa zimegonga mwamba.
Viongozi wa upinzani wapo katika maongezi na viongozi wa jeshi la Misri.

Hali inavyoonekana ni kuwa jeshi litasimamisha katiba ya nchi hiyo na kumweka Jaji mkuu aongoze katika kipindi cha mpito
Hilo linaungwa mkono na vyombo vya sheria kwasababu Morsi amekuwa katika wakati mgumu navyo.

Kwasasa ni ngumu kuwa na uchaguzi kwasababu hakuna tume inayoeleweka na wapinzani wangependa kuwa na muda wa kutosha kwa maandalizi.

Bei za mafuata katika soko la dunia imepanda na kufikia dollar 100 kwa pipa.
Pengine inaweza kuendelea kuongezeka kutokana na hali ya wasi wasi mashariki ya kati.
Ieleweke kuwa mto Nile ni kiungo muhimu sana kwa usafiri wa bidhaa kutoka na kuingia mashariki ya kati.

Kutokana na uchumi wa dunia kutotengamaa vema ongezeko la bei ya mafuta kwa kiwango hicho linatia hofu ya mdororo wa uchumi kujirudia. Ni hofu kutokana na kutokuwa na muafaka jambo linalotikisa masoko ya mitaji duniani.

Tutaendelee kufuatilia na kuangalia nini hasa kinaendelea hapo mashariki ya kati
 
Hongera Jenerali Abdel Fattah al-Sisi(Mkuu wa Majeshi Misri) na wananchi wa Misri kwa kuipindua serikali yao.Siogopi mitazamo ya wenye akili ndogo kuchukulia hili kwa mtazamo wa uhaini(treasonable perception),nipo tayari kwa lolote.Nililalumiwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kuunga mkono Msimamo wa Jeshi la Misri kusimama na Wananchi.Leo yametimia.Bado naunga mkono na ninalipongeza jeshi la Misri kwa kumpindua Mohammed Morsi.Huu ndiyo mfano bor a wa jeshi linalojiita la wananchi.Sina shaka na uwezo na uzalendo wa jeshi letu la wananchi(JWTZ),natoa wito kwa vijana wote waliotimiza vigezo vya kisheria kujiunga na jeshi waendelee kujiunga kwa wingi……………!!!!!!!Msinihoji,watch this space!

Pamoja na kwamba najua marekani haikutaka kuona Morsi anashinda uchaguzi(tulijadili hili kwa kina kule Jamii Forums kwenye Jukwaa la Great thinkers katika Thread ya DURU ZA SIASA by,Nguruvi3)na nilisema kwamba Marekani kupitia shirika la kijasusi la CIA lingemgeuza Morsi kuwa Salvador Allende wa Afrika na zama hizi,lakini bado Morsi aliwapa fursa kupitia makosa yake na ulevi wa madaraka aliouonyesha.Wanamapinduzi wa kweli hawafanyi hivyo.Nilimshangaa sana alipojipendekeza kwa mataifa ya Magharibi na kumponda Rais Bashar Al-Assad wa Syria na kutaka Regime Change.Mnafiki mkubwa,malipo ni hapa hapa duniani.

Alisahau kuwa Marekani walitumia jeshi kupitia CIA kumpindua Hugo Chavez kule Venezuela lakini jenerali Morales alituma kikosi cha makomando wa kutisha na ku,muokoa Rais huyo aliyechaguliwa na wananchi.Similar incident appeared in Greece back in 1974 when a CIA instigated military coup overthrew the anti-American prime minister Andreas Papandreou and then the caretaker prime minister Mr. Kanelopoulos.

Ikumbukwe mwaka 2011 Wananchi wa Misri walimiminika katika viwanja vya Tahrir Square kutaka Rais Hosni Mubarak (kibaraka wa Marekani ) aondoke madarakani na baadaye katika matunda ya mapinduzi yale Uchaguzi ulifanyika na Mohammed Morsi wa Chama cha FJP(Freedom and Justice Party) ambacho hapo kabla kilikua chama cha kundi lenye msimamo mkali la Muslim Brotherhood akachaguliwa kuwa Rais mbele ya mgombea aliyekua akiungwa na Jeshi lakini pia alisadikika kuwa kibaraka wa Mubarak kwa kuwa alikua mkuu wake wa idara ya usalama.Chama Cha Muslim Brotherhood nilikua nikikiunga Mkono sana hasa watu kama El-Baradei(aliyekua mkuu wa shirika la kudhibiti niuvu za atomiki duniani) walipokuwa wakisimama katika majukwaa ya kimataifa na kujenga hoja.Mohammed Morsi hajatimiza matakwa ya umma,wananchi wameingia barabarani na kutaka mabadiliko ila yeye kwa jeuri akaendeleza ubabe.Jeshi limeamua kusimama na wananchi maana jeshi lilimpa masaa 48 awe amesikiliza matakwa ya wananchi na muda huo ulifika mwisho leo mida ya sa 10:35 jioni hivyo jeshi likaamua kuteka maeneo muhimu ikiwemo televisheni na redio ya taifa.Hili ndiyo aina ya Jeshi ambalo hata mimi katika maisha yangu nitatamani kuwa amiri jeshi mkuu wake.

Haya ni mapinduzi ya kipekee Afrika,tumepiga hatua moja kubwa zaidi.Ukiniambia nichague kati ya demokrasia ya kizuzu na mapinduzi ya kijeshi,always my option ni military takeover.Nina special passion na jeshi

Umoja wa Afrika wana tabia chafu ya unafiki kwa kuwa ni club ya madikteta tu,utasikia wanakurupuka kama chafya kutaka kuitenga Misri na kutaka kujenga hoja kwamba katiba haijazingatiwa,huo ni upuuzi maana katiba inatokana na wananchi ambao waliingia mitaani na jeshi likawaaunga mkono hata mimi ipo siku kama uonevu na ukandamizaji hapa Tanzania utaaendelea hivi name nitazidi kusukuma wananchi wadai haki zao kwa njia hii.Nimefurahi kuona mkuu wa majeshi wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameasema pamoja na suspension ya constitution lakini serikali ya mpito itaongozwa na Jaji mkuu wa mahakama ya juu.Huu ni uamuzi wa Busara nauunga mkono

Bernard Membe,haraka sana anatakiwa kuitambua serikali mpya ya misri na aache sera za kivivu za kuegemea msimamo wa AU(club ya madikteta ambao siku zao zinahesabika). Mwezi March mwaka huu ilikua zamu ya Jamhuri ya afrika ya kati ambako Waasi wa kundi la SELEKA walichukua serikali dhidi ya mafisadi na walevi wa madaraka,niliwaunga mkono na nitaendelea kuwaunga mkono wanaosimama na wananchi hadi siku yangu/yetu itakapofika kuongoza mapinduzi.

Goodbye Morsi. One can blame Americans as some of us are doing here. But as they say, devil can't enter until we lay out a way for it to enter. Morsi should have paid greater heed to the concerns of protesting Opposition groups, liberal sections and various sectarian minorities (Muslim and Non-Muslims) of Egypt. Democracy and Tyranny of electoral majority are not one and the same thing……..
 
HALI YA MISRI BAADA YA MAPINDUZI BARIDI

Tuliyoyasema yametimia sasa rais Morsi na wafuasi wapatao 300 wa Brotherhood wapo chini ya ulinzi, jeshi limechukua madaraka na kukmabidhi Jaji mkuu. Uchaguzi ni baada ya mwaka mmoja.
Vituo vya radio na TV vya muslim brotherhood vimefungiwa kwa muda.

Hali bado ni tete sana kwa kuzingatia kuwa Brootherhood wana kundi la wapiga kura asilimia 30(base) ambao hawajaridhika na hatua za kumuondoa kiongozi wao kwa njia zisizo za kidemokrasia. Hivyo Tutegemee vurugu za aina nyingine kwa njia nyingine kama kulipa kisasi.

Kitakachofuata ni kumtia Morsi katika mashitaka ili kumzuia asigombee tena.
Yeye na wafuasi wake wataachiwa huru wakiwa na kesi za kubambikiwa.

Kwanini tutarajie vurugu?
Chama cha Freedom and Justice(FJP) ni sehemu ya Muslim brotherhood. Kwasababu za kiufundi imebidi wakiite hivyo ili kutowaondoa au kuwabagua wale wasio na mrengo wa Brotherhood.
Bortherhood(MBH ukifupisho kwa minajili ya majadiliano) kilikataa kutumia vrugu katika harakati zake katika miaka ya 1970.

Ndani ya MBH kukawa na wakereketwa ambao walioona njia ya majadiliano si sahihi hivyo walijitenga na kutengeneza makundi kama Gamal Isslamiya na Jihad Issilamiya.

Ni makundi hayo yaliyohusika na mauaji ya rais wa zamani Anwar el Saadat.
Mmoja wa washiriki akiwa Ayaman al Zawahiri ambaye baada ya kifungo alikwjiunga na Alqaeeda ya Osama na kwasasa yeye ndiye kinara wa kundi hilo.

Unaweza kuona Dr Alzawahiri alishindwa kuishi na Muslim brotherhood kwasababu ya tofauti za kiitikadi katika siasa.MBH ni wasomi waliomkubali Dr Zawahiri lakini hawkubali vurugu wakati ambao Dr anaamini katika nguvu.

Kwa maana hiyo jeshi litaweza kutuliza hali kwa muda fulani na wakati huo Muslim Brotherhood watakuwa wakijitahidi kuwakomboa wanachama wao na kuanza kujijenga upya.

Tatizo si Brotherhood,MBH wamechimbia katika vitongoji na misikiti(Grass-root level) na uwezekano wa kukabiliana na hali ya kisiasa kwa kutumia wasomi wao upo.

Shida itatoka katika wanachama wa Brotherhood ambao hawataweza kudhibitiwa na MBH kama ilivyotokea huko nyuma ambapo makundi ya Gamal na Jihad issilamiya yalivyoshindwa kudhibitiwa.

Hapo ndipo fanatics watakapotokea na tutaanza kusikia milipuko na mauaji ya kigaidi.
Hilo ni suala la muda tu!

Na katika kushadidia hoja hii tunaona kuwa baada ya Morsi kuapishwa si makundi ya Brotherhood yaliyokuwa yanamshinikiza kutengeneza 'mambo' kwa mtazamo wanaoutaka.

Ni makundi ya Sufi (waumini wa Sufism) na Nuur. Makundi haya ndiyo yaliyoharakisha kila jambo kiasi cha Morsi kuonekana anaipeleka nchi katika siasa za kidini.

Hebu tuangalie nini hasa kimemgharimu Morsi na kujikuta anaondolewa baada ya mwaka mmoja?

Katika safu hii tutaangalia mambo kwa njia aliyopendekeza mdau wa duru za siasa jouneGwalu kuwa ziwepo nyakati tufanye case study

Inaendelea........
 
Last edited by a moderator:
KILICHOMSIBU MORSI NA SOMO KWA TANZANIA

Morsi akiwa na JFP aliingia madarakani ili kuondoa hali iliyokuwepo ya kiutawala(status quo)
Ndiye kiongozi wa kwanza wa kuchagulia kidemokrasia nchini Misri.
Aliahidi kuinua uchumi, kupunguza umasikini, kuweka utawala wa kisheria na kuleta nchi pamoja.

Kwa ufupi Misri ina mchanganyiko wa watu wenye itikadi mbali mbali.
Wapo Orthodox na Papa, Kuna Waislam wa madhehbu mbali mbali kama Shia, Sunni na Sufi.
Sufi wanafalsafa ya Sufism na wao huamini katika kufanya mambo kama yalivyokuwa enzi za kuingia kwa Uislam, ni wachache lakini wenye nguvu kwa misimamo yao

Kuna Waliberali ambao wengi ni wasomi na wana uraia wa nchi nyingine.
Inakadiriwa wapo Wamisri wenye Uraia wa Marekani katika idadi ya Mamilioni.

Leo baraza la kijeshi likitangaza kumuondoa Morsi mkuu wa majeshi aliambatana na Mohamed Albaradei aliyekuwa mkuu wa IAE ambaye ni mliberali,sheikh mkuu na mkuu wa Kanisani. Kitendo kile kiliashiria kuileta nchi pamoja.

Morsi alipoingia alikuta mfumo wa utawala uliokuwepo enzi na enzi. Haikuwa rahisi kwake kufanya mabadiliko ya haraka na alikutana na vikwazo. Hili ni suala lililohitaji muda kulikamilisha
Alikuta uchumi katika hali mbaya na aliahidi kufanya mageuzi yatakayoleta nafuu kwa watu. Nalo pia ni suala lililohitaji muda.

Dhidi ya mambo yote hayo yaliyohitaji muda, kilichomponza Morsi ni kuligawa taifa.
Alifanya hivyo kwa shinikizo kutokana na makundi yaliyo na msimamo mikali kama tulivyojadili.
Morsi akajikuta anaegemea kutekeleza sera za akina Bortherhood, Sufism, Nuur badala ya kuunganisha taifa

Hilo ndilo lililowaudhi hata waliompigia kura kujitenga naye na ndiyo maana upinzani dhidi yake ulikuwa mkubwa sana ukiwahusisha hata waliomchagua

Tukiiangalia hali ya Misri kama case study tunaonautofauti wa Rais Morsi na Rais Kikwete upo katika mtazamo huu

JK aliingia madarakani kwa ushindi wa asilimia 80 tofauti na Morsi aliyeingia na asilimia 52.
JK kama Morsi aliingia kwa kauli za kuinua uchumi (misha bora) kwa kila mtanzani, kusimamia nidhamu na utawala wa sheria,kushughulikia wauza mihadarati, wahujumu na walarushwa kama kurudisha nyumba za serikali n.k.

JK kama Morsi umaarufu wake umeshuka kiasi kwamba uchaguzi uliopita haieleweki alipata asilimia ngapi kwasababu ushahidi unazidi kutolewa kuwa kulikuwa na msaada wa ziada kama alivyodai Prof Lipumba. Tofauti na Morsi yeye ni baada ya miaka 5 lakini wote wakishindwa kusimamia ahadi zao.

Inaendelea....


 
Inaendelea.......

Morsi aliburuzwa na wahafidhina wa mrengo kuigawa nchi kwa kupendelea upande wa Brotherhood kuliko kulileta taifa pamoja. JK naye aliburuzwa na mafisadi waliopelekea serikali yake kunuka rushwa. Tofauti ni kuwa Morsi alizama katika dini wakati JK alizama katika uswahiba na wote kusahau umaarufu uliowafikisha walipo.

Morsi aliligawa taifa kwa kuegemea upande wa kidini na kusahau kuwa Misri ina mchanganyiko wa Waliberali na secularists. Kitendo hicho kiliiigawa nchi na kuwa sehemu ya anguko lake.

JK na CCM nao pia wamejaribu ingawa hawajafanikiwa kuchomeka mbegu za udini hasa kwa upande wa wapinzani.Walifanya hivyo kwa CUF na sasa Chadema bila kujua wanaligawa taifa

Ingawa JK hajawa na mrengo wa kidini lakini serikali yake imeshindwa kulileta taifa pamoja na mmomonyoko wa maadili katika ukabila na udini umekuwa mkubwa kuliko kipindi kingine.
Huu ni udhaifu kama wa Morsi katika kushughulikia mambo mazito hasa ya kidini

Misri inafanana kimazingira ya kisiasa na Tanzania kwa namna fulani.
Misri ilikuwa nchi iliyobinya sana demokrasia kukiwa na ulaghai wa viongozi na kutumia mabavu kuondoa(suppress) demokrasia.

Wananchi walivumilia na walipoanza kuchomoza moto wa Tahariri ndio huo tunaona.
Watu wapo tayari kufa na wala hawaogopi tena askari au mabomu.

Tanzania nayo ilikuwa katika chama kimoja na katika mbinyo wa kidemokrasia kama Misri. Taratibu watu wameanza kuleta upinzani na kwabahati mbaya watawala wameamini kuwa mabomu na virungu, hata viongozi kuamuru Polisi wapige watu ni suluhu nzuri.

Tunaona watu wanavyoanza ku-resist na hiyo ni dalili kama iliyokuwepo Misri miaka 5 hadi 10 iliyopita.

Morsi alishindwa kusimamia utawala wa sheria kwa watu wake wote kwa kuwasikiliza majority na minority, secularist, liberal na conservative. Ndicho kinachotokea kwa JK na serikali yake kwa sasa. Bunge halijali wachache wanasema nini kwa niaba ya wananchi, serikali haijali malalamiko ya watu kuhusu haki zao n.k.

Sasa swali litakuja kama kuna kufanana kwa kiasi kikubwa kwanini basi tusifanane hadi mwisho!!!

Jibu lake rahisi ni kuwa uwezo wa wananchi katika kujitambua unatofautina katika nchi hizi mbili.

Tumalizie kwa kusema hili ni funzo zuri kwa watawala wetu kuwa katika historia ya dunia hakuna dola iliyowahi kushinda nguvu ya umma.

Na kwamba umma ni wananchi wenye nchi bila kubagua kwa msingi wa itikadi za kisiasa, kidini, kikabila au kiuchumi.

Watawala waelewe kuwa suluhu ya kitaifa ni kukaa katika meza na kuongea na wala si dereya na vifaru, mizinga na bunduki. Waelewe kuwa hata Misri walikuwepo Polisi na walikuwa WANAPIGA,na hivyo kupiga si suluhu.

Watawala wajifunze kutoka Misri kama case study na wawe tayari kubadilika

Huu ni mtazamo wa duru za siasa na hauna maana nyingine iliyokusudiwa bali kujiufunza na kujadiliana

Tutaendelea kujadili hoja za mwana duru Ben Saanane hapo juu.

Tusemezane

cc. Mamndenyi
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio hasara ya kufanyia majaribio damu za watu! Kwangu mimi ni upumbavu kutoa damu yako kwa ajili ya kutafuta, kuitetea ama kuilinda Demokrasia-Afrika! Wengi wanaojua wasichokitaka, pia ni wengi wanaojua wanachokitaka, lakini ni wachache sana wanaojua gharama sahihi na njia ya kufikia kile wanachokitaka!
Ni MANTIKI tu ndiyo iliyopewa uhalali wa kumwaga damu za watu kwa idadi yoyote, sio mifumo wala sera zaliwa na hulka za watu wapumbavu! Ni MANTIKI tu ndiyo ipasayo kufiwa! Nayo tuweza kuipata hvi, je kuna uhalali wa kuondoa kilichopo? Je, kuna uhalali wa kuleta tutakacho? Je, kuna uhalali wa namna ya kuleta kile tutakacho? (uhalali ni kwa mazingira na nyakati zetu mahususi) Kama jibu ni ndio kote, basi DAMU yangu i radhi hata leo, maana huo ni UTU! Lakini kama hata moja tu ni hapana, ni dhambi kubwa kutumia hisia zako na zangu kumwaga damu yangu, ni DHAMBI na ULAANIWE, kwa maana kamwe damu haitakauka aridhini kila uchao na hautaota mmea! Hakuna mzazi atakayekataa kuwekewa kisu shingoni kwa kukitoa kwenye shingo ya mwanae, ILA TU ASIWE MFU maana haitakuwa na maana tena bali ni ULIMBUKENI!
Serikali mfu ni zetu, wahanga wa kwanza ni watoto wetu, ndani ya aridhi yetu. TUSIPENDE KUKURUPUKA! Kila kitu ni HESABU, zikisukwa vizuri hakutakuwa na kujutia hata ikigharimu damu nusu ya watoto wetu! Alaaniwe anayesabisha damu ya mtu mweusi kumwagika, ati kwa ajili ya Demokrasia! Alaaniwe kwa kumwaga damu za watu bure! Alaaniwe kwa upunguani na ulimbukeni wake! TUSIFANYIE MAJARIBIO DAMU ZA WATU, KILA KITU KINAWEZEKANA ILA NI HESABU.
a4afrika. Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Maandamano ya kwanza yaliyomwondoa Mubarak hayakuwa organised na Muslim Brotherhood au chama kingine cha siasa bali ilikuwa ni mkusanyiko vikundi mbali mbali vya wananchi wa kawaida, hii ikiwa ni muitikio wa kilichotokea Tunisia ambapo Ben Ali aliondolewa madarakani. Muslim Brotherhood walipata nafasi ya kuchukua madaraka kutokana na kuonekana kuwa 'organised" zaidi kuliko vikundi vingine vya upinzani nchini humo.

Bahati mbaya walipoingia madarakani walianza kutekeleza sera kinyume na matarajio ya waasisi wa movement ya kumwondoa Mubarak. Mfano kitendo cha Morsi kujiwekea madaraka juu ya mahakama nchini humo kilitafsiriwa na wengi kuwa kumbe huyu nae hana tofauti na dikteta aliyeng'olewa. Pia alijiaminisha kuwa katika iliyomweka madarakani inaweza kumlinda kwa kipindi chote cha uongozi hata kama atavuruga mambo kwa kiasi gani.

Na hili ni fundisho kubwa sana kwetu sisi tunapoendelea na mchakato wa katiba mpya...
 
Mkuu Mwalimu, nakubaliana nawe kwa hilo la maandamano kwa upande mmoja. Upande mwingine naweza kusema Brotherhood walikuwa na mkono wao.

Muslim Brotherhood wapo miaka mingi sana na kila utawala ulipambana nao kwa namna moja au nyingine. Si rahisi kuona lakini wao ndio 'brain' ya Al Azhar na chimbuko la akina Gamal Issilamiyya na Jihad Isilamiyya.

Wamejijenga siku nyingi ingawaje walikuwa 'crushed' kila wakati.
Wakaamua kufanya mambo 'behind the curtain' au passive movement

Ni wasomi sana ambao kazi yao ilikuwa kuwazindua wananchi kuhusu kujikomboa bila wao kujionyesha. Wananchi walipoingia mitaani taratibu brotherhood waka seize hiyo opportunity.

Walikuwa well organized wakitoa misaada ya matibabu, vyakula n.k.Ukweli ni kuwa walijua matokeo ya kazi yao ya uhamasishaji na ilikuwa suala la muda tu. When the right time came it was on their side and favor.

Baada ya Morsi kuingia madarakani, Brotherhood hawakuwa na haraka bali wanachukua muda ili kila jambo lifanyike kwa muda muafaka bila dunia kuwashtukia

Kwa bahati mbaya wanazi na washabiki kama Gamal na Sufi ambao wangependa ulimwengu ubadilike kama wanavyotaka usiku mmoja wakachukua agenda.
Makundi haya ukilinganisha na Brotherhood hayasogei hata kidogo kwa usomi

Hata hapa nchini kuna mifano kama ya Misri. Mathalan, agenda ya katiba mpya ilikuwa ya Chadema. Ghafla CCM wakaiuchukua kama chama na serikali na kuidhibiti.

Maana yake ilikuwa moja tu, kuwa japo agenda ni CDM kulikuwa na uwezekano ikachukuliwa na makundi yasiyo sahihi na hivyo kuhatarisha usalama au agenda za CCM.

Tayari makundi hayo yalikuwa yanasema vunja muungano, rais ashtakiwe n.k.mambo yaliyokuwa na masilahi na CCM na serikali yake. Wala CDM hawakuwa na agenda mbaya lakini uwezekano wa ku-slip out of hand na kuangukia kwa fanatics n.k. ulikuwa mkubwa. Ikifika hapo ni down spiral.

Tatizo la Morsi siyo Brotherhood ni makundi yaliyochukua agenda na kumshinikiza Morsi ndiyo yameondoka naye.

Na kukuthibitishia hili uchaguzi ujao Brotherhood watakuwa as strong as today hata kama hawatashinda.
 
Mkuu Ben Saanane
Katika bandiko lako 227 umeelezea mambo ambayo nakubaliana nayo na mengine nina mtazamo tofauti.Kwanza nikubaliane nawe kuwa Marekani hawakupenda Brotherhood waingie madarakani.

Jana wameomyesha kuguswa na kamata kamata ya viongozi wa Brotherhood ili kuwa neutral. Ukweli ni kuwa hawakupenda Morsi atawale sana kwasababu tayari alishaanza kuingiza mambo ambayo yangeubadili ulimwengu wa kiarabu na kuhatarisha masilahi yao
Hakuna ajuaye kuwa nyuma ya mapinduzi haya hakukuwa na mkono wa mtu!

Pili nakubaliana nawe pia ya kuwa jeshi ni chombo cha wananchi na hivyo libaki kwa masilahi ya umma.

Lakini natofautiana nawe kuhusu mamlaka ya jeshi na wajibu wake.
Nafahamu kuwa kuna mambo yanayotokea ambayo yameongeza hisia zako kwa namna flani na hasa ukilinganisha na yaliyotokea Misri na pengine kukusukuma either far right au far left
Naelewa msukumo ulio nao katika suala hili vema na nadhani wengi wana 'reservation' pia

Jeshi la Misri.
Tumeshaona ni jeshi la tano kwa ukubwa duniani. Ni jeshi lenye wataalamu na utalaam wa hali ya juu na sehemu kubwa ya ufadhili wake ni matokeo ya mkutano wa Camp David.
Pamoja na ugumu wa maisha bado hali ya jeshi la Misri ni tofauti na taasisi nyingine.

Jeshi la Misri limeundwa na kulelewa katika misingi ya kujitawala.
Ni nadra kwa mkuu wa majeshi anapoteuliwa kuondolewa na Rais.
Ndiyo maana Gen Abdel el Sisi aliteuliwa na Morsi na ndiye alimuondoa madarakani.

Jeshi la Misri lina mabaraza yake na linajitegemea sana kwa kila kitu.
Muundo wake tu ni serikali hata kabla ya serikali yenyewe.
Hivyo kuna nidhamu fulani iwe nzuri ama mbaya ambayo jeshi hilo linao ikiwa ni pamoja na 'immunity' iliyo nayo kwa watawala.Inapofika wakati wa kufanya maamuzi kunakuwa na 'impartial'kwasababu ni chombo huru

Muundo wa jeshi la Misri ndio kama wa jeshi la Turkey na nchi nyingi za dunia iliyoendelea.
Moja ya kazi za majeshi hayo ni pamoja na kupendekeza nafasi za uongozi katika nyanja mbali mbali, kupanga na kuratibu shughuli na kujisimamia katika nidhamu

Majeshi ya nchi nyingine kama za sub Saharan hayajafikia kiwango cha muundo kama huo.
Yamebaki kuwa ni sehemu ya watawala na vyombo vya watawala kuendelea kutawala na kusahau majukumu yao ya mwanzo.

Viongozi wake wanateuliwa na kuweza kuondolewa na wakuu wa nchi kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
Majeshi ya nchi hizi masikini si taasisi kamili bali taasisi zinazomegewa bajeti ili ziendelee kuwepo kwa mtindo wa quid pro quo.

Hayana uhuru wakuweza kuwa impartial inapobidi. Sheria zake zimewekwa katika misingi ya ukandamizaji na wala si sheria au amri za kijeshi kama zinavyopaswa. Kuna element flani za kunyang'anywa mamlaka na wanasiasa.

Sikubaliani na hoja kuwa majeshi haya ya nchi masikini yanaweza kubeba majukumu mazito ya kuongoza nchi. Hapa sina maana hayawezi, la hasha nina maana itakuwa ni vurugu tu kila siku. Kila mmoja atataka kufanya anavyojua na hapo sina hakika kama kutakuwa na amani.

Tumeona ya Yahaya Jameih na Dauda al Jawara, ya William Tolbert na Samwel Doe n.k. Hakuna kilichofanyika kikubwa zaidi ya status quo na pengine mbaya zaidi.

Kuliko kudhania kuwa majeshi yanatakiwa yawe sehemu ya siasa, nilidhani yanapaswa yapewe autonomy ili yaweze kukidhi mahitaji ya malengo yao.

Yaondolewe katika tawala za kisiasa na kauchwa kujiendesha kama ilivyo kwa nchi zilizosonga mbele au zinazosonga mbele kwa mfano wa Turkey na Misri.

Tutaendelea.....
 
Last edited by a moderator:
BADO MTAFARUKU UNAFUKUTA MISRI

Baada ya kuondolewa rais Morsi, Jaji mkuu ameapishwa kuchukua uongozi wa nchi.
Huyu ataongoza baraza la mpito kuelekea uchaguzi mkuu.

Baraza hili ni chombo tu cha kutekeleza matakwa ya baraza la kijeshi ili kuondoa dhana kuwa haya ni mapinduzi ya kijeshi.

Wanajeshi walifanikiwa kuwatwanya watu kutoka Tahariri square na hali ikaonekana kuwa imetengemaa.

Katika mabadiko yaliyopita tulisema kuwa kitendo cha kuwakamata akina Morsi na Brotherhood ni cha kufunga nguvu za rais huyo na kuwatisha wale watakaojaribu kuleta upinzani.

Tulisema kuwa hatua hizo hazitakuwa na muda mrefu na vurugu zitarudi tena.
Hayo ndiyo yaliyojiri leo kwa Brotherhood kuingia mitaani na tayari watu zaidi ya 10 wameuawa

Kitu kisichoeleweka ni kuhusuBrotherhood.
Ukitafuta habari zao kwa ukamilifu utaona ni taasisi yenye mikakati inayoandaliwa na wasomi.

Brotherhood wana matawi dunia nzima lakini hawana fujo. Wao wanaongozwa na weledi na hivyo kipigo kimoja cha kuwakimbiza si kuwa wamekimbia ni kwamba wame-retreat na wanaporudi inakuwa kazi.

Niwakumbushe wasomaji wa duru kuhusu Katuni za Denmark zilizokuwa zinakashf uislam. Katuni zile zilitoka na hakuna aliyeshtuka. Tafsiri nzima na uhamasishaji ulifanywa na Brotherhood. Hawa ndio waliibua hoja hadi dunia nzima ikawa inawaka moto.

Tofauti na makundi mengine kama Alqaaeda, Brotherhood si watu wa vurugu.
Ni watu wanaotumia filosofia ya uamsho nikimaanisha (sensitization ).

Fikiria katuni imechorwa Denmark hoja ya katuni ikaibukia Cairo, watu wakafa Pakistan, India, Nigeria na kwingine. Nguvu iliyotumika siyo kujifunga mabomu ni nguvu ya hoja za Brotherhood

Brotherhood haina wanachama magula gula, wanachama wake ni wachache laikini wasomi waliobobea. Wapo watu katika fani ya dini (Ulmaa), Engineers na Madaktari, wanasaikolojia, jiografia, uhusiano wa kimataifa n.k. Wanachama wanapikwa kutoka moja ya vyuo vikuu vikongwe dunia AlAzhar na wameiva.

Kama kuna taifa limeupumua kufuatia mapinduzi ni Marekani na Israel.
Marekani na Israel wanajua kuwa ushawishi na nguvu za hoja za Brotherhood zinaweza kuushawishi ulimwengu wa kiarabu vinginevyo.

Marekani imeshawaonya wanajeshi kuwaachia Brotherhood na kutokamata hovyo watu. Wanachokifanya hapa ni kuhakikisha kuwa Brotherhood hawalipi kisasi kwasababu wakiamu hapakaliki.

Tumalizie kwa kusema hali bado ni mbaya na kadri siku zinavyozidi kwenda mbele tutashuhudia mtafaruku zaidi.Brotherhood wanaungwa mkono na asilimia 40 na kati ya hiyo asilimia 30 ni base yao ambayo imetamka kuwa kulichofanywa ni kinyume cha taratibu na uonevu

Tusemezane

Mgeni wa leo Tuko
 
Last edited by a moderator:
MTAFARUKU NA HASIRA ZA MUSLIM BROTHERHOOD

Watu zaidi wameuawa na hadi leo ni takriban watu 35. Mpambano kati ya wanaopinga utawala wa Morsi na wanaomuunga mkono yanaendelea. Upinzani zaidi dhidi ya jeshi ni katika miji nje ya Cairo(tutalieleza hili)

Jitihada za kumteua waziri mkuu aliyekuwa mkuu wa taasisi ya nuklia duniani Mohamed Al Badei umekwama kwasababu ya mivutano.

Al Baradei alikuwa miongoni mwa wapinzani wa Mohamed Morsi, ni mliberali anayetaka Misri ya ki-secular zaidi ya kidini.

Brotherhood wana hoja kuwa Morsi alichaguliwa kidemokrasia na kumuondoa ilikuwa mapinduzi kinyume na matakwa ya watu. Hoja ina uzito kwa kuzingatia kuwa kuingia kwa Morsi kulitokana na sanaduku la kura.

HAWA MUSLIM BROTHERHOOD NI CHAMA?
Tungependa tuliweka jambo hili sawa. Muslim Brotherhood ilianzishwa mwaka 1928 na Sheikh Hassan al Banna ikiwa ni movement ya kupinga uonevu. Taratibu ikakua na kuwa movememnt inayozingatia religious, social and political issues.

Muslim Brotherhood siyo chama cha kisiasa lakini kupitia wao kumekuwa na vyama vya kisiasa. Mathalan, chama cha Morsi kinajulikana kama Freedom and Justice Party(FJP).
Brotherhood wamesambaa sana katika ulimwengu wa Kiarabu na wana vyama kama ilivyo JFP.

Wao ndio walikuwa nyuma ya uanzishwaji wa Hamas kule Gaza na West bank, katika nchi ya Bahrain kuna Al Esla scoiety,Islamic action front kule Jordan, Syria, Lebanon, Indonesia na hata Saudi Arabia kwa uchache wa kuvitaja.

Ni kwa maana hiyo mageuzi yalipoanza Misri kumuondoa Mobarak ghafla ukawa kama moto wa nyikani na kugusa falme zote ikiwemo Jordan, Bahrain na Saudia.

Na ni kwa hali hiyo ndiyo maana Misri inaangaliwa kwa ukaribu sana na tawala za Uarabuni na zile za Magharibi na imekuwa na ushawishi mkubwa mashariki ya kati

Morsi alipokuwa madarakani( Ben Saanane )alimtaka Al Asad aheshimu matakwa ya raia.
Si kuwa alikuwa anaunga mkono nchi za Magharibi, alichokuwa anafanya ni kuunga mkono Brotherhood tawi la Syria.

Tatizo kubwa la Brotherhood ni kuwa movement inayozalisha matawi ambayo hayana uvumilivu na kuna nyakati yanafanya uasi kuondoka katika misingi ya Brotherhood na kuwa radical.

Mifano ya taasisi hizo ni kama ;
-Takfir wal-Hijra ambao nao walikuwa na radical wing ya Jamaat al Isslmiya
-Al Gamal al Isslamiya

Makundi hayo yameondoka katika msingi wa Brotherhood ambao ni kufuata Quran, sunna na hadithi kama muongozo wa maisha.

Makundi hayo yanakuwa na radical wasio na subira na yamehusika sana na mauaji ya viongozi.
Uhalifu wowote unaofanywa na makundi tanzu lawama huwaendea Brotherhood kwasababu wao huonekana kama ndio hasa chanzo, ukweli ni kuwa wao si chama bali movement na kwa bahati mbaya vyama hutokea humo (out of control)

Kutokana na kuondoka kwa Morsi hali ya mashariki ya kati hasa Israel itakuwa na utata.
Hamas lazima wataanza tena mashambulizi kwasababu 'mentor' wa kuwatuliza hayupo ambaye ni Morsi anayewakilisha matakwa na mwongozo wa Muslim Brotherhood.

Tutaona mashariki ya kati ikichafuka tena na vurugu zitaendelea sana nchini Misri pengine kwa miezi mingi ijayo.Brothehood wameapa kusimama kidete hadi Morsi arudishwe.

Sisi kama Tanzania tunapata somo gani kuhusu uanzishwaji wa taasisi kama za kidini?
Je, kuna umuhimu wa serikali kuziangalia au tuziache zijiendeshe kwasababu kuna uhuru wa kuabudu?

Tutajadili safu inayofuata.

cc.mgeni wa leo Mwali
 
MISRI KWAENDELEA KUCHAFUKA

Tulisema mabandiko yaliyopita kuwa hali haitakuwa nzuri kwasababu wafuasi wa Freedom and justice Party wamedhamiria kuyakataa mapinduzi kwa imani kuwa chama chao kilishinda kwa uhalali na kilichofanyika ni kuwaondoa kwa hila.

Watu zaidi ya 51 wameshauawa kwa muda wa siku mbili na mapambano kati ya wanajeshi na wafuasi hao. Pengine kitakachopunguza kasi ya waandamanaji ni mfungo wa ramadhani.

Kinachotokea ni hali mbaya sana kwasababu makundi yaliyotokana na Brotherhood ambayo ni radical zaidi yatakuwa na huruma na ndugu zao wa FJP. Kuna uwezakano mkubwa wa milipukoa ya mabomu kuanza tena na pengine mauaji ya viongozi kwa mtindo wa ugaidi.

Kumekuwa na kukinzana kwa nadhari za makundi hasimu. Kundi linalounga mapinduzi linadhani Marekani ipo nyuma ya Brotherhood na isingependa kuona mapinduzi. Kundi hili linaongozwa na dhana kuwa Brotherhood waliokuwa mstari wa mbele kupinga Israel na mkataba wa Camp David hawajafanya lolote ikiwa ni ishara ya kukubaliana na matakwa ya Marekani.
Wanaamini kuwa isingekuwa hivyo basi kasi ya misuko suko kwa Israel ingekuwa imeshaanza.

Kundi hili la Pro revolution linashindwa kuelewa kuwa Brotherhood waliingia madarakani dunia ikiwaangalia kama 'wakorofi' na wasi wasi ulikuwa juu ya mkataba wa Camp David.

Brotherhood walijua hilo na walikuwa na subira ili dunia isiwaelewe kama ilivyodhani.
Lakini nadharia yao ya pili ilikuwa kujenga mambo ya ndani kwanza kwa kuweka sheria za kidini ili kuweza kuwahamasisha wafuasi wao muda muafaka. Ilikuwa ni suala la muda tu ajenda ya Israel ingekuwa mezani.

Kundi la pili ni lile linalopinga mainduzi ambalo ndilo la Morsi na Brotherhood. Kundi hili linaamini kuwa kuna nchi za magharibi zimeingilia mambo ya ndani na kwamba Marekani haikuta Brotherhood waongoze nchi.

Hoja ya kundi hili ina mashiko sana kwasababu Marekani na washirika wasingependa kuona Brotherhood wanajitanua nchini Misri kwasababu kufanya hivyo ni kuuachia ulimwengu wa Kiarabu maikononi mwa Brotherhood.

Ni kwa msingi huo Marekani imekuwa inachanga karata zake kwa uangalifu sana ikielewa nguvu ya Brotherhood wakati huo huo ikiwa na shaka na uwepo wao madarakani.

Marekani imekuwa ina cheza kati na kati ikiangalia wapi hasa masilahi yao yalipo na hatari yake kwa kuegemea upande fulani, ndiyo maana hakuna msimamo thabiti juu ya kinachoendelea Misri

Hali ni ya hatari sana kuliko ilivyokuwa wakati wa Mubarak na tunaendelea kuifuatilia.

Tutarudi katika uchambuzi wa rasimu katika safu zijazo huku tukiendelea kutupia macho mashariki ya kati

Tusemezane


cc mgeni wa leo Remote
 
For personal reasons nitajiziwia kuchangia katika mjadala huu.
Natoa tu maon yangu (sitakuja kuyatetea tena ila mnaweza chambua):
1. I Support the right of people to demonstrate (both pro and anti Morsi)
2. I condemn the "Coup" of the Egyptian army and the killing of Morsi's supporters.

kwanza upande wa Demonstration, some have argued that thinjgs were runing out of control, hivo the army HAD to intervene to calm the situation and avoid a mahem. I don't agree with this excuse. Morsi was a democratically elected president and the only way to take him out of power was to go through democratic means. SInce he was elected by the sovereign people, the only way to take him out was to organise a referendum as soon as possible. The army should have calmed the crowed and force Morsi to organise this referendum through a neutral electoral committee.

Sasa upande wa Coup yenyewe, France na other western powers have argued that it is a "soft coup" or a "fortunate coup". there is nothing such as soft or fortunate coup. A coup is a coup. When the army takes the democratically (or non democratically) elected president into custody, when they gun at his supporters, when they send them in jail and when the army becomes the most powerful body of the state, it is a coup and it is deplorable in a democratical country.

Egypt will organise elections in March next year. I wish them well, but I am worried that there might be other praisals as soon as a group of people are not happy with the government. Demonstration is not a suitable way of people to express their views and should only be used when the parliament has failed to do so.

Waasalam
 
Mwali ahsante sana kwa mchango wako.
Nikubaliane nawe kuwa hakuna excuse ya jeshi kuingilia kati democratic process. Lakini pia ulikuwepo umuhimu wa kuingilia ili kuzuia civil war.

Waliokaribisha hali hiyo ni wa Misri kwa kuamini kuwa jeshi ni ‘supreme' na kungefika wakati itabidi liingilie kati. Kwamba wanaamini demokrasia wakiwa na mkoba wa jeshi ubavuni.

Kosa alilifanya Morsi kwakutosikiliza watu wake.Kulikuwa na grievance ambayo ilidharaulika. Siku moja kabla ya kuondolea ndipo alipokubali kukaa meza moja na wapinzani akaendelea kusisitiza at eleventh hour just before the coup.

Matatizo ya Morsi ni kama ya viongozi wengi Afrika. Kwamba huamini nguvu zaidi ya majadiliano. Hili tuliangalie kwa macho mawili kwasababu wananchi watakapochoka ‘kupigwa' hakutakuwa na muda wa majadiliano tena.

Ni ujanja ule ule wa kuunda tume zisizo na majibu na wananchi wakichoka basi hakuna muda wa kusikiliza tume au majadiliano.

Kuhusu nchi za magharibi, nimeeleza hapo juu kuwa zipo njia panda. Kuunga mkono Brotherhood ni tatizo kwao, kukataa demokrasia iliyomuingiza Morsi madarakani na ambayo wana ihubiri ni tatizo pia. Ndio maana tunaona hayo maneno ya soft coup.

Hofu ya nguvu ya Misri mashariki ya kati ni kubwa sana na magharibi wanachokifanya ni kuchanga karata zao vema ili wasije jikuta mahali wasipotarajia.

Ulimwengu wa Kiarabu unaingalia Misri kwa kauli ya ‘Misri um al-dunya' yaani mama wa dunia. Sababu tumezieleza ikiwemo historia na influence wa vikundi kama Brotherhood na ndilo tishio kwa magharibi

Tatizo linaloikabili Misri siku zijazo ni kuondoa viongozi kila baada ya muda.
Hili la Morsi lime set precedent kwa tawala zijazo, kwamba watu wakijisikia kuingia mitaani wanamatumaini jeshi litaweka mambo sawa in their favor.

Kwa kweli jeshi la Misri halikufanya mediation, lilichukua side ingawa Morsi alikaribisha hali hiyo kwa kuachia kila kitu hadi alipopoteza control
 
RASIMU YA KATIBA MPYA

Baada ya kuangalia hali ya mambo mashariki ya kati na tutaendelea kufuatilia na kuhabarisha, duru za siasa inarudi katika rasimu ya katiba mpya kama ilivyokuwa katika mabandiko yaliyotangulia184,188,190,191,192,193,194,19 7,198

Umuhimu huu ni kuzingatia kuwa mabaraza ya kata na vyama vya siasa vimeshaanza kutoa mitazamo yao. Wanasiasa na manguli wa sheria na katiba nao pia wametoa maoni.

Hapa JF naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara Mwigulu Nchemba ameleta uzi akitahadharisha baadhi ya mambo ndani ya katiba na ndivyo ilivyokuwa kwa UVCCM.
Chadema nao wametoa maoni ingawa hayakuwa ya kina kama ilivyotarajiwa.

Wakati mabaraza ya kata yanakaa tayari kuna ushawishi wa kisiasa ima kwa kupotosha au kutishana. Kwa Mh Mwigulu Nchema, yeye akiwa naibu katibu mkuu wa CCM na mshiriki wa vikao muhimu sana vya chama chake, kauli zake zinapewa uzito kwa mtazamo mpana

Mwigulu alisema kuwa katiba italeta mgongano katika suala la ulinzi na usalama.
Kwamba kutakuwa na mgongano wa vyombo vya serikali ya muungano na vile vya serikali za washirika.Sina uhakika kuwa Mwigulu hafahamu alichokuwa anaongelea kwa undani(mapungufu) au alisema ili kupotosha umma.

Vifungu anavyoongela Mwigulu ni hivi hapa:

227.-(1) Kutakuwa na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litakalokuwa na jukumu la ulinzi wa watu na mali zao chini ya masharti ya Katiba hii.
233.-(1) Kutakuwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya Muungano,(2) Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Muungano itahusika na shughuli za kuimarisha usalama wa Jamhuri ya Muungano na kulinda Katiba hii

inaendelea229. Kutakuwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano ambaye atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa

Alichokiongelea na pengine kumshtua (sijui kama ni kweli au kupotosha) ni kifungu hiki:

232.-(1)
Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, nchi washirika wa Muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi vitakavyosimamia
masuala ya usalama wa watu na mali katika maeneo yao.235. Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Washirika wa Muungano wanaweza kuanzisha Idara au Taasisi zitakazoshughulika na mambo ya kiusalama katika mamlaka zao ambazo zitafanya na kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na Idara ya Usalama ya Jamhuri yaMuungano

Kwa mtu aliyesoma katiba haraka au asiyeisoma rasimu ni rahisi kukubaliana na Mwigulu kutokana na vifungu hivyo.

Nashawishika kuamini kuwa Mwigulu ambaye ni kiongozi mkubwa katika maamuzi ya nchi hawezi kutojua jambo kama hili kama si kutisha watu au kuwapotosha. Nitafafanua.

Nchi kama Marekani kila jimbo(state) ambayo mengine ni makubwa kuliko Tanzania yana Polisi wake kwa mfano(LAPD, BOPD, NYPD n.k.).

Hakuna mkuu wa jeshi la Polisi kwa utaratibu wao lakini wanachombo kingine kama FBI ambacho kinafanya kazi na Polisi wa majimbo katika baadhi ya mambo kama yalivyoanishwa.
Polisi hao wa majimbo wana vitengo vyao upepelezi na uchunguzi vinavyofanya kazi kwa pamoja na taasisi nyingine kama FBI na CIA ikibidi.

Nchini Canada kuna Polisi wa shirikisho(RCMP) na kila jiji au mji una idara zake za Polisi kamili kuanzia ajira, uchunguzi, upelelezi n.k. Lakini kuna masuala ambayo jeshi la shirikisho (RCMP)linashirikiana na majeshi ya majimbo na miji katika majukumu.

Uingereza kuna M15 la usalama, kuna Scotland yard na territorial police sehemu nyingine, na zote zinafanya kazi kwa ushirikiano bila kuingiliana. Ndivyo ilivyo katika nchi kama India n.k.

Hata rasimu hii imeelezwa vema kabisa,lakini kwa makusudi kabisa Mwigulu ameacha vifungu hivyo ili tu kushadidia hoja yake. Vifungu hivyo vinasema

232(2) Vikosi vya ulinzi vya Washirika wa Muungano, vitatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano ili kuepusha mgongano wa mamlaka katika utekelezaji wa majukumu katika maeneo hayo.

235. Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Washirika wa Muungano wanaweza kuanzisha Idara au Taasisi zitakazoshughulika na mambo ya kiusalama katika mamlaka zao ambazo zitafanya na kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa lugha rahisi Polisi wa Tanganyika na idara ya uslama wa Tanganyika itakuwa na mambo yanayoihusu ambayo hayaathiri kwa namna yoyote shughuli za serikali ya Jamhuri.
Mfano Polisi wa Tanganyika wanaweza kutafuta njia za usalama kutokana na ongezeko la vibaka. Hilo ni tatizo local na linashughulikiwa hivyo.

Endapo litakuwa kubwa na kuhatarisha usalama wa nchi kwa ujumla, Polisi wa Tanganyika watashirikiana na Jamhuri.

Lakini ikitokea Polisi na wana usalama wa Tanganyika wakabaini mambo mazito kama ugaidi, udini n.k ambayo ni lazima washirikiane na wa jamhuri kukabaliana na tatizo kwasababu issue ya vibaka haina taswira ya kimataifa, lakini ugaidi ni jambo litakalomhusu rais wa Jamhuri na hivyo vyombo vyake lazima vishirikishwe.
Bila kushawishi kuwa yaliyomo katika rasimu ni sahihi au la, hoja yetu duru za siasa ni kuwa mchakato huu unaingiliwa na sina uhakika katika mabaraza ya kata ni wangapi wanaweza kuona upotoshaji huu wa dhahiri. Kutokokujua siyo tatizo kubwa kama upotoshwaji.

Mwigulu amelenga kuueleza umma kuwa serikali 3 ni hatari kwa usalama wao ili kukidhi haja ya chama chake. Hii ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na mustakabali wa taifa.

Katiba ni chombo cha kila raia na inapaswa isiangaliwe kwa mtazamo wa kichama ili tu watu kulinda masilahi yao au vikubdi vyao.

Ni jukumu letu sote kusimama kwa pamoja na kuonyesha wapi umma unapotoshwa.

Namwalika mh Mwigulu Nchemba aje hapa duru tuyajadili kwa utulivu na ustaraabu kwa faida ya nchi.

mgeni wa leo Ngongo

(Tutaendelea kuangalia Tanganyika inavyotumiwa kama ngao ya muungano)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…