Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #241
MBOWE KUSAKWA NA POLISI USIKU WA MANANE
Tukio la mwenyekiti wa CDM kusakwa saa 7 usiku na polisi wenye silaha kama lilivyothibitishwa na mwenyekiti wa CDM mbowe na msema wa chama Tumaini Makene ni la kushtua na kusikitisha
Kinachoshtua ni kuona matukio ya namna hii yakiendelea bila serikali kuchukua hatua na wala kuona hatari inayolikabili taifa siku za mbeleni.
Mbowe ni mbunge wa Wilaya ya Hai na ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani na kiongozi wa upinzani bungeni. Nyadhifa hizi zinaendana na idadi kubwa sana ya wafuasi wake kisiasa na kijamii.
Kama ilivyokuwa kwa mbunge Lema kusakwa usiku hili limekuwa muendelezo wa tabia hii ya hatari sana katika mustakabali wa taifa.
Viongozi ni watu wanaofahamika katika jamii na katika fursa walizo nazo ni pamoja na kuwa 'public figure' na upatikanaji wao ni rahisi sana kuliko mtu mwingine.
Na katika mazingira fulani watu hawa huweza hata kujidhamini kwa baadhi ya tuhuma kwasababu ya nafasi zao katika jamii kwa kuaminika.
Hivi karibuni kulikuwa na mlipuko Arusha ambao Mbowe na Lema walikuwepo.
Katika mlipuko huo hadi sasa hakuna anayejua nani alitupa bomu na kwa madhumuni gani.
Mbowe alitakiwa aripoti kituo cha Polisi na yeye alifanya hivyo bila kushikiwa silaha au kutafutwa na mtu yoyote bali kuitikia wito wa Polisi
Siku za karibuni mwanachama wa Chadema Henry Kileo alitakiwa kufika kituo kikuu cha Polisi.
Alikwenda huko ambako aliishia kukamatwa. Hakufuatwa kwa silaha bali walikwenda mwenyewe kwa kuitikia mwito wa Polisi.
Inapotokea hali ya Mbowe kutafutwa usiku wa maanane tena askari wakuu wakiwa hawana habari kama alivyodai mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ni jambo la kusikitisha.
Haieleweki kuwa kweli ni Polisi waliomfuata au ni majambazi.
Lakini ukweli unabaki kuwa Polisi wanatupiana mpira ikiwa ni ushahidi kuwa wanajua nini kilichotokea. Na hata kama ni majambazi tulitaraji Polisi washirikiane na walinzi wa Mbowe kuwatafuta.
Hilo Polisi hawajalifanya ikiwa ni dalili nzuri kuwa hawaguswi na maisha ya kiongozi huyu iwe kwa bahati mbaya au kukukusudia.
Yapo matukio ya watu kuumizwa kama lile la Dr Ulimboka ambalo hadi sasa hakuna anayejua nani alifanya hivyo na kwanini.
Kuna tukio la mwandishi Kibanda na lile la Kanisani Olisati.
Matukio yoye hayo yamehusishwa na vyombo vya dola huko mitaani na kwingineko.
Hatudhani kuwa Polisi walishindwa kumtumia Mbowe ujumbe kama walimuhitaji.
Na hata baada ya kujua yupo safarini Polisi hawajamkamata kwa maana kuwa hawakumuhitaji kama walivyokuwa wanaMtaka usiku wa manane.
Sijui madai ya Polisi kumtaka Mbowe usiku yalihusisha nini na hilo linabaki kuwa Swali.
Hatari inayolinyemelea taifa ni ukweli kuwa matukio haya yanayohusisha Polisi sasa yanaonekana kushamiri na kuwa sehemu ya utawala. Leo kama waliomfuata Mbowe ni majambazi sijui nani angeamini kuwa ni majambazi na si vyombo vya dola.
Kesho vibaka wakimdhuru Mbowe nani ataamini kuwa ni vibaka na si vyombo vya dola.
Keshokutwa Mbowe au kiongozi mwingine akidhurika kwa namna ambayo haitaeleweka kwa jamii nani atakubali kuwa si vyombo vya dola.
Kwa maneno mengine serikali inazidi kujitia katika 'kibano' cha kuhakikisha usalama wa Mbowe na viongozi wengine. Hakuna maelezo yatakayojitosheleza iwe kwa bahati mbaya au makusudi kwa lolote linaloweza kuwasibu viongozi hao kwasababu tayari serikali imeonyesha kuwa sehemu ya mipango michafu kama uvamizi wa saa 7 usiku.
Ni kwasababu hizo duru za siasa zinaiona hatari kubwa sana inayolikabili taifa.
Machafuko hutokea kwa mambo kama haya. Habyarymana wa Rwandara aliuawa jambo lililochochea mauaji ya kimbari. Si kwasababu alikuwa rais bali nyuma yake walikuwepo wafuasi.
Sheikh Abdul Rogo wa Mombasa alipouawa yalitokea machafuko Mombasa, si kwasababu ni kiongozi wa serikali bali kiongozi wa jamii na ana wafuasi.
Na ndivyo mauaji mengine duniani yalivyo, kwamba hutanguliwa na kichocheo 'precusor' kabla hayajotokea.
Katika nchi yetu hali ya kiuchumi, kiusalama na kijamii si nzuri.
Kumekuwa na mivutano ya kidini,kisiasa na kikabila kuliko wakati mwingine wowote wa uhai wa taifa hili.
Haya ni mambo kama tembo aliyelala 'sleeping giant' kama ni sahihi kusema hivyo.
Yanasubiri kichochoe kidogo tu yalipuke.Katika mazingira ya kuhisi, kuona na kuusema uonevu, uvunjwaji wa sheria na utawala usiozingatia haki za watu, hakihitajiki kichocheo kikubwa.
Duru za siasa kama walivyo Watanzania wengine tunatoa thadhari kuwa mchezo huu mchafu ima wa kisiasa au vyovyote iwavyo hasa kwa kutumia vyombo vya dola ni hatari sana kwa taifa hili kwa wakati huu.
Wananchi waliokata tamaa hutafuta mahali pa kumalizia machungu yao,na fursa hiyo ikijitokeza basi wataitumia ipasavyo.
Rais JK, taifa linaingia na kupita katika wakati mgumu sana kiutangamano katika uongozi wako.
Tanzania ni yetu sote na wala hakuna atakayekuwa salama hali ikichafuka.
Rais kama hatachukua hatua za makusudi na za haraka basi historia ya kuvurugika kwa taifa hili pengine na maumivu, machungu au damu hazitakuwa mbali na mikono ya serikali yake.
Tusemezane!
Mgeni wa leo Radhia Sweety
cc. Invisible Dr.W.Slaa Nape Nnauye Zitto