Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Nilitarajia Prof Lipumba kwa usomi wake angetoa maoni nini kifanyike ili gesi iliyogunduliwa Mtwara isaidie kuinua kiwango cha maisha bora kupitia miradi ya kiuchumi kama ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa,ujenzi wa miundombinu ya kisasa reli,barabara na bandari itakayotoa huduma kwa wilaya na mikoa inayopakana na Mtwara.

Gesi ya Mtwara Ni nyingi sana kuna jarida niliwahi kulisoma wana sema gesi ni nyingi kuliko mahitaji ya Tanzania !.Kama ni kweli basi gesi ya Mtwara ni lazima isafirishwe sehemu mbali mbali za nchi si Dar bali mikoa mingine ya Tanzania ikichagizwa zaidi na sababu za kiuchumi zaidi.

Nilitarajia pia angezungumzia uwazi wa mikataba ya gesi,angezungumzia sera ya gesi,angezungumzia uimarishwaji wa TPDC kwa maana ya kujengewa uwezo wa kutafuata na kuchimba mafuta na gesi siku za usoni.

Hoja hizi nilitarajia zingetolewa na Prof Lipumba lakini kinyume chake kakimbilia kujivika umiliki wa gesi ya Mtwara na ukombozi wa waislam Tanzania
Much respect Ngongo. Tanzania haina upungufu wa mawazo wala gesi.
Tanzania ina upungufu wa watu wasikivu, ina upungufu wa watu wanaojali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3, per bandiko lako namba 263, is it pre mature to conclude kwamba katika sakata hili, ccm haina matumaini ya kurudisha imani za wana mtwara tena kama chama na badala yake, tumaini lililobakia kwa ccm kurudisha imani kwa wananchi ni kupitia chama cha CUF?

Vile vile kuhusiana na hoja yako juu ya kwanini tume maalum ya bunge ndio ishughulike na mtwara badala ya wabunge wa mtwara, je unajadili vipi hili katika muktadha wa Katiba ya JMT inayosema mbunge sio mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake tu bali mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa Tanzania nzima; Je kipengele hiki cha katiba kiliwekwa kwa ajili ya mambo kama haya au kiliwekwa kwa nia njema ila kinatumiwa vibaya?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Ngongo nilisoma taarifa ya kuwa gesi iliyopo ni zaidi ya cubic ft trillion 33 ambayo inaweza kutumika kama nishati ya nchi kwa zaidi ya miaka 20.
Kumbuka hiyo ni sehemu tu ya visima vingi vinavyoendelea kugunduliwa.

Kinachoshangaza ni kuona gesi inaanza kuchimbwa kabla ya sera kutengenezwa.
Sasa hivi ndio kuna draft ya sera ya gesi! OMG!

Kwa kuwakumbusha wasomaji gesi iligunduliwa Tanzania kule songo songo miaka ya 1980 Nyerere akiwa madarakani. Yeye aliamua kuacha kuifanyia kazi kwa kutambua uwezo wetu hasa kwa wasomi. Alifahamu tutakapokuwa tayari tutaichimba kwa faida ya taifa.

Miaka ya 1970 Nyerere alipoulizwa kuhusu madini alisema 'hayaozi yaachwe Watanzania wakiwa tayari watayachimba'. Ghafla tulipoanza kuwa tayari japo kibubusa bubusa tukaona akina Mkapa wakiita wawekezaji bila sera ya madini.

Wakachimba mpaka wananchi walipouliza mashimo yanaongezeka hali zao zinakuwa duni nini maana na manufaa ya madini?

Mara tukaona kamati ya kuchunguza mikataba iliyoundwa na rais ambayo iliwajibika kwake na si kwa taifa. Taarifa ikatolewa na kuwekwa katika makabati. Mashimo yanaendelea kujaa.

Hivi kwa kujua yote hayo hakuna aliyeweza kuwaza kuwa gesi kama madini nayo inahitaji sera!

Katika majadiliano hapa JF kuna siku moja Mchambuzi aliuliza swali moja ambalo sina majibu kama walivyo wengi. Hivi hii gesi ni kwa matumizi yapi? Ni LNG! na matumizi yake hasa ni industrial au ni yaweza kuwa domestic au ni vipi.

Hakuna aliyejibu kama ambavyo viongozi hawawezi kuwaeleza wananchi.
Ndio maana nasema si Mtwara tu sote hatujui nguvu hii inayotumika katika miradi bila wananchi kujua inakusudia nini hasa. Mchambuzi hebu tusaidie kidogo maana eneo hili umewahi kulieleza vema sana.

Juzi waziri mmoja amesema mwaka kesho tutajitosheleza kwa umeme na kuuza nje ya nchi kama matokeo ya uwepo wa gesi. Kwanza najiuliza, kujitosheleza ni kupi huko?
Kwamba umeme ukiwa katika miji mikubwa bila kukatika ambako ni aslimia 10 ya nchi hapo kuna kujitosheleza?

Kwanini waziri afikirie kuuza umeme nje na wala si mkakati wa kusambaza mawilayani na vijijini ili upatikane tena kwa bei nafuu kwa kila mmoja kumudu kama ndio kujitosheleza?

Huyu mwananchi wa Mtwara akisikia kuwa bomba lililopita uani mwa nyumba yake litatoa umeme wa kuuza nje, kwanini asijiulize yeye anafiadika vipi na umeme huo!

Kuna sera gani ya kuhakikisha kuwa naye atakuwa sehemu ya kujitosheleza kwa umeme kama hajawahi kuona nguzo hata moja karibu na kwake. Kwanini asihoji! na akihoji kwanini aonekane mhalifu.

Kuna mahali nilimsoma mbunge Zitto akisema uwepo utaratibu wa kugawana mapato ya rasilimali kama gesi na madini bila kuingia katika mkondo wa serikali.

Hapa alimaanisha iwepo sera kuwa mapato yanayopatikana yapangiwe shughuli nje ya utaratibu wa kuziingiza TRA, hazina n.k. Kwamba gesi ikiingiza bilioni X basi tutajenga vituo vya afya 5000 kwa uwiano wa kila mkoa.

Hoja ya Zitto ambayo nakubaliana nayo ilimaanisha kusema jambo moja, kuwa iwepo sera ya kumnufaisha mwananchi bila urasimu wa TRA na Hazina ambako ni machaka machafu ya uhalifu.

Pesa zikiingia huko zinaishia kupeleka wake wa wakubwa kutibiwa chunusi Appolo na kuwaacha wenye mali wakiendelea kuchangia simcard.

Tunafanya makosa kushabikia propaganda kuwa watu wa Mtwara hawataki gesi itoke, kwamba wanataka kuivuna kwa masururu na masuFuria wenyewe.

Lazima tuwasikilize concern zao ni zipi hasa na tutawaeleze kama tunaweza kama hatuna majibu tukae nao pamoja na kujadili.

Endapo tuliweza kujenga kituo cha Afya Nanyamba na Nakapanya kwa pesa ya kahawa kutoka Kilimanjaro na Kagera, kwanini tusiamini kuwa tunaweza kujenga Hospitali ya rufaa kigoma kwa pesa za gesi kutoka Mtwara?

Na hapo ndipo nasema hili si tatizo la wanamtwara ni tatizo letu, ni ugomvi kati ya Watwana Vs Mabwana na wala tusiwaachie wao.

Tusimame nao tuelezwe contract ya kuchimba inasemaje, ni ya muda gani inahusu maeneo gani, itatekelezwaje na return yake ni ipi.
Nini wajibu wa wananchi na nini wajibu wa serikali.
Tuonyeshwe EIA kama livyosema gfsonwin na wapi wananchi wameshirikishwa.
Tufafanuliwe yale aliyouliza Ngongo nukuu#261

Tulifanya makosa ya kuwaachia wananchi wa Kigoma na Mwanza suala la reli ya kati.
Mikataba ikaingiwa kwa nguvu kama huu wa gesi.

Leo tunajua kuwa Wahindi walioshindwa kuendesha reli kwao walikuja hapa kwa ajili ya kung'oa reli kama chuma chakavu na tumewalipa. Tumebaki bila miuondo mbinu ya reli na sote kama taifa tunaumia.

Tulikataa kuhoji, wakachukua 10% na kutuachia madeni na uchakavu wa reli.
Haionekani kama tumejifunza, leo hatuna majibu ya gesi Mtwara wapi tunapata ushujaa wa kusota vidole japo wale wanaojaribu kuhoji?

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3, per bandiko lako namba 263, is it pre mature to conclude kwamba katika sakata hili, ccm haina matumaini ya kurudisha imani za wana mtwara tena kama chama na badala yake, tumaini lililobakia kwa ccm kurudisha imani kwa wananchi ni kupitia chama cha CUF?

Vile vile kuhusiana na hoja yako juu ya kwanini tume maalum ya bunge ndio ishughulike na mtwara badala ya wabunge wa mtwara, je unajadili vipi hili katika muktadha wa Katiba ya JMT inayosema mbunge sio mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake tu bali mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa Tanzania nzima; Je kipengele hiki cha katiba kiliwekwa kwa ajili ya mambo kama haya au kiliwekwa kwa nia njema ila kinatumiwa vibaya?Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu Mchambuzi, CCM imepoteza matumaini ya wananchi wa Mtwara kwasababu nyingi.

Tunafahamu huu ni mkoa mtiifu sana kwa CCM na wananchi wa Mtwara walielewa kuwa CCM inajali na kuwasikiliza.

CCM haijafanya hivyo na wala haipo tayari kuwasikiliza. Imeamua kutumia maderaya ya kijeshi na risasi za moto kuwasiliana nao. CCM imekiuka 'makubaliano' yao yasiyo rasmi na kuondoa utiifu wa wananchi wa Mtwara kwayo.

Wananchi walitegemea kuwa Mtwara yenye wabunge wote wa CCM ingewasikiliza pengine zaidi kuliko 'waasi' wa maeneo kama Arusha.

Kilichotokea ni CCM kuamuru wabunge wao kuwekwa ndani, kutembeza mijeledi na bakora ili kuwatia adabu wana Mtwara

Wananchi wa Mtwara wanaelewa kuwa CCM haina sera wala nia njema na wao isipokuwa wakati wa kura.Hapo sijui CCM watarudi Mtwara kuwaeleza nini tena wananchi wa huko wawaelewe.

Na wala tumaini lao si kwa CUF tena. Wananchi wa Mtwara wanazungumzia gesi bila kujali itikadi zao za kidini, kisiasa, au kikabila.

CUF imedaka ajenda kwa mguu wa dini na hilo haliwezi kurudisha imani si kwa CUF wala CCM bali kwa wanasiasakwa ujumla.

Tatizo linaloikabili CCM ni hasira na hivyo yoyote yule atakAyeonekana kuwaelewa au kuwaeleza wakaelewa huyo ndiye atakayekuwa nao.

Kuhusu suala la wabunge, nikubaliane nawe kuwa wabunge si mali ya jimbo ni mwakilishi wa wananchi wa Tanzania.

Tatizo la Mtwara lilipelekwa bungeni kujadiliwa na wabunge wote kama tatizo la taifa.
Wabunge wa Mtwara kama wawakilishi wa watu wa Mtwara na ambao wanafanya kazi nao na kuwaelewa si kijamii na kimazingira tu bali kiuchumi na utamaduni ndio walipaswa wapewe nafasi ya kueleza nini hasa malalamiko ya wananchi wa Mtwara.

Kwamba wao kama mawakili wa wananchi wangefikisha kesi mbela ya jopo 'bunge' ijadiliwe kutokana na hoja zao katika muktadha wa kitaifa kama inavyopaswa kuwa.

CCM ikanyakua hoja hiyo na kuizima isijadiliwe kitaifa na wabunge wote ambao ni wa taifa na si jimbo kwa kupitia Spika wa Bunge ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama na halmashauri kuu ya taifa na kamati ya wabunge wa CCM.

Ikachaguliwa kamati kwenda kuchunguza tatizo ambalo halikujulikana na bunge kwasababu halikuzungumzwa bungeni!! CCM kupitia spika na wingi wao walikataa kulijadili kwahiyo kamati iliundwa kwenda kuchunguza isichokijua.

Hii maana yake ni kuwa kulikuwa na maagizo au maandalizi ya kamati hiyo ili kukidhi haja ya CCM na serikali na wala si kuwasikiliza wananchi wa Mtwara.
Taarifa hiyo sikumbuki kama ilijadiliwa na wabunge wote ambao ni mali ya taifa.

Kutokana na kutosikilizwa kwa wabunge wa Mtwara au wale walioko serikali kutowakilisha matatizo ya wananchi wa Mtwara, mtafaraku ukazuka.

Tukasikia wabunge wamewekwa mahabusu kwa kuungana na wananchi.
kwavile suala lipo mahakamani hatutalijadili,lakini ninachotaka kueleza hapa ni kuwa wabunge hao walinyimwa fursa ya kueleza walichotumwa na wananchi wao ndani ya bunge na hivyo kuwanyima fursa kama wabunge wa majimbo ambao walitaka suala lijadiliwe na wabunge wote kama suala la taifa kulingana na katiba ya JMT.

Ukiangalia mtiririko wote wa matukio hakuna shaka kuwa tatizo la wananchi wa Mtwara ni CCM. Ni CCM ambayo imekuwa kikwazo kwao kwa njia ya uwakilishi na kama chama chenye serikali.

Kuwaelekezea mitutu na maderaya ni maelekezo ya CCM kwa serikali yake unless mtu aniambie CCM na serikali ni vitu visivyohusiana!
 
Mkuu Nguruvi3, per bandiko lako namba 263, is it pre mature to conclude kwamba katika sakata hili, ccm haina matumaini ya kurudisha imani za wana mtwara tena kama chama na badala yake, tumaini lililobakia kwa ccm kurudisha imani kwa wananchi ni kupitia chama cha CUF?

Vile vile kuhusiana na hoja yako juu ya kwanini tume maalum ya bunge ndio ishughulike na mtwara badala ya wabunge wa mtwara, je unajadili vipi hili katika muktadha wa Katiba ya JMT inayosema mbunge sio mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake tu bali mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa Tanzania nzima; Je kipengele hiki cha katiba kiliwekwa kwa ajili ya mambo kama haya au kiliwekwa kwa nia njema ila kinatumiwa vibaya?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi,Habari yako Ndugu yangu,ni tumain langu kuwa ni u-bukheri wa afya,huku sisi hakuchi kunakucha,matumain tumepoteza na watawala hawa wa nchi hii...

Nachukua fursa hii kusherehesha hoja ya Mkuu Nguruvi3 na kwa kweli namshukuru sana kwa jins anavyosimama kwenye reli katika kutoa fikra zake pevu na hisia zake kali katika hili,i wish wamakonde wenzangu wote wangekuwa na access za kufika maeneo kama haya na kuona ni kwa jins gani watu wanaelewa zaid ya wanavojielewa wao wenyewe..

Suala hili lazima nikiri wazi wazi kwamba kwa kias kikubwa sana wana mtwara na kusini kwa ujumla tunajilaumu sisi wenyewe kwa kushindwa kutambua kuwa zama za siasa safi za CCM katika taifa letu zilishaondoka mara tuh baada ya kuondoka mwalimu j.k nyerere,hilo sisi bado tulikuwa tumelala,tulikuwa tumelewa propaganda za CCM na danganya toto zao za kanga,kofia,ming'oko,chikandanga na ubwabwa pasi na kutambua kuwa hawa jamaa kwa sasa wanachukua tuh kila kilicho chao na kuondoka,

Usishangae kule bungeni kumuona Mh Habibu Mnyaa,mbunge kutoka zanzibar anapata uchungu zaid katika suala hili la gesi na kulizungumzia bungeni hata kufikia hatua ya kutoa hoja binafsi zaid ya anavyoumia hawa ghasia na mkuchika,
Anaumia zaid ya anavyoumia Mathias chikawe na Juma Njwayo,anaumia zaid ya anavyoumia bernad membe na Asnein Murji,hivo ndivyo sisi wana kusini tulivyokula hasara kwa kuweka matumain kwa wanasiasa wa CCM,
Leo hii Chadema wakija huku kufanya siasa utashangaa jopo kubwa la wana CCM wanapitisha SUMU na kusema hiki ni chama cha kikristo na kisichaguliwe,utadhani huko CCM ni chama cha WAISLAM,wanakuja na propaganda ovu kabisa za kutumia uislam kwa kuwa wanajuwa kuwa percent kubwa ya sisi huku ni waislam kwahiyo kwa kusema hivo tutakichukia moja kwa moja chadema na kwa kias kikubwa wamefanikiwa sana kwa hilo,

Sasa sisi wamakonde wengine kwa kukosa maono ya mbali tukajua kwamba kwa mantiki hiyo basi chama cha kukipa matumain ni kile ambacho kina mrengo wa kiislam kiislam na kusahau moja kwa moja kwamba uislam wetu hauhitaji nguvu ya wanasiasa au chama chochote cha siasa,tukalewa propaganda hiyo na kuwapa matumain CUF ambao ni hao hao CUF sasa wanaonekana kuwa washirika wakuu wa CCM katika kuudhoofisha mkoa na kanda hii kwa miaka nenda,miaka rudi,

Ndani ya miaka hamisin ya uhuru sisi hatuna bara bara ya kudumu ya kutuunganisha na sehemu kuu ya uchumi wa nchi hii ambayo ni dsm,tumepiga sana kelele,tumelia sana kulieleza hili hakuna anaetusikiliza,
Ilifikia wakati nakumbuka kipindi naenda masomoni 0'level na A'level hadi chuo nikitokea zangu kijijin Litehu kwenda zangu kaskazani kusaka elimu hii,nilikuwa nasafiri kwa gari kwa takriban mwez na miez nasota kuelekea huko kusotea elimu hii,wamakonde wenzangu waliokawa wanahangaika kwenda dsm kwenye matibabu sikumbuki hata idadi yao waliofia jian kutokana na kadhia ya barabara,tumeteseka na bado tunateseka sana,kwa masikitiko makubwa bara bara hii hadi leo haijasha,CCM bado inaendelea kututukana na kutudhihaki sisi wamakonde,sijui tumewakosea kitu gani,kosa letu ni kusikiliza uongo wao na kuwapa kura zao ili wao wapate kula taifa hili??

Hiyo ya bara bara ni moja tu ya changamoto,ukija kuhusu afya,elimu na miundombinu mingine ndiyo usiseme kabisa,hali inatisha,

ukija hapa CCM makao makuu ya Mkoa,kuna kombe ambalo utawala wa CCM umetoa kwa mkoa wa Mtwara kwa kuwapongeza kwa kuwapa kura nyingi kwa kishindo kwa uchaguz wa mwaka 2010 uliopita,ni kweli kwamba Mtwara wameiweka CCM juu,wameiweka CCM mbele huku CCM wameiweka Mtwara NYUMA,hiyo ndiyo hali halisi...

kitu ambacho wanapaswa kufaham CCM na wanasiasa wengine ni kwamba watu wa mtwara kwa sasa wameshaghaili moja kwa moja,na nachelea kusema kwamba wawe makini sana na watu wa mtwara katika kuelekea suala hili la gesi na mengineyo,hali si shwari na watu wamechukizwa na kukata tamaa moja kwa moja,

Nadhani mmeskia kuhusu kupigwa mawe gari iliyobeba mabomba ya kusambaza gesi bila woga bila hofu,je ni nani alishawahi kuwadha pamoja na uwepo wa JWTZ na kipigo walichokipata watu watakuwa na ujasiri wa kutokea hadharani na kuyashambulia magari hayo??

Haya sasa,tujaalie wametandaza hayo mambomba,swali ni kwamba je wataweza kuyalinda??wataweza kuyalinda kwa kipindi chote hiki yasidhuriwe na watu hawa waliokata tamaa ya maisha??

Kazi ni kwao CCM na wanasiasa uchwara,kazi ni kwao kusuka ama kunyoa,lakini nawahakikishia katika suala hili mengi sana yatasikika,labda CCM na serikali yao hii ya kifisadi wayatekeleze yale yote ambayo wana mtwara wameyaweka mbele kwenye sakata hili zima la rasilimali hii ya gesi asilia...
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Nikushukuru kwa mwaliko wako na mchango mkubwa wa Jukwaa hili la GT.


Nianze kwa kuyatupia macho maudhui ya kitabu kiitwacho "Why Government Succeeds and Why it Fails" (tafsiri isiyo rasmi Kwanini Serikali wakati mwingine inafanikiwa na Kwanini Wakati mwingine inashindwa")kilichoandikwa na Wanauchumi na Wanataaluma wa Sera za Umma A.G na L.R wa Marekani. Ni kitabu cha muda kidogo (2001) lakini kitaendelea kuwa kipya kwa muda mrefu naona kutokana na mwenendo wa dunia unavyokwenda hivi sasa.

Waandishi hawa wanajiuliza maswali kadhaa juu ya Serikali namna zilivyo hodari kutekeleza mambo ambayo magumu, kwa gharama kubwa na hayana maslahi ya moja kwa moja kwa wananchi walio wnegi lakini zinashindwa kufanikisha mambo ambayo ya msingi, muhimu na yanagusa maisha ya watu wengi ikiwa pamoja na kuondoa umaskini, kuboresha huduma za afya, elimu maji na huduma nyinginezo.




Waandishi wanajenga hoja kwamba, Serikali inafanikiwa katika utekelezaji wa Sera/mipango yake ikiwa Maafisa wa Serikali watakuwa na dhamira ya dhati ya kusimamia na kufikia lengo walilojiwekea. Lakini malengo/sera za Serikali zitashindwa ikiwa malengo ya wanasiasa yanaenda kinyume na malengo ambayo Serikali imejiwekea. Au, makundi maslahi (interest groups) yana uwezo wa kupindisha dhamira na malengo ambayo yamewekwa. Hii mana yake ni kwamba iwapo malengo ya Serikali yanakinzana na maslahi ya wanasiasa au makundi maslahi, basi Sera au malengo hayo hayatafanikiwa na Serikali itashindwa kufikia malengo yake. Wanamalizia kwa kusema, Serikali inafanikiwa ikiwa itakuwa na uwezo na mkakati madhubuti wa kubaini na kufanya malengo yake yaendane sambamba na matakwa ya watu na makundi ya kijamii (policy-interest-matching). Na pia ili matakwa ya jamii/watu yaendane na mipango ya Serikali, yapaswa jamii/watu wahabarishwe ipasavyo. Kadri jamii inapohabarika vizuri juu ya mpango au lengo husika, ndipo kunakuwa na matokeo mazuri ya mipango/malengo hayo ya Serikali. (Kuna hoja pana hapa nitaikimbia kwa sasa)




Kitabu hiki kinaweza kutupa mwongozo wa kile kinachoendelea nchini kwetu ikiwa pamoja na sakata la gesi ya Mtwara na maneno ya Prof. Lipumba. Kwa kifupi naweza kusema, ulimwengu wa sasa umejawa na taharuki ya mshangao kwa kila pembe na utaalam/wataalam wengi wa kuuliza maswali kuliko wenye uwezo wa kujibu maswali. Dhana hii inatupeleka kwenye swali mshangao moja: Ni kwanini baadhi ya mambo ambayo jamii/watu wangependa yafanyike, hayafanyiki na yale wasioyapenda yatendeke ndio yanatendeka/yanatendwa. Kwa mfano, (mathalan) watu wangependelea kuona badala ya kupanua barabara ya Dar/Chalinze/Morogoro ili kupunguza foleni ni vema ingeimarishwa Reli ili mizigo inayosafirishwa na malori iende kwa Treni ambayo daima dumu huwa haithiriki na tatizo la foleni. Wana Mtwara wangependa kuona mchakato wa Gesi unafanyika Mtwara, badala ya kwenda kufanyikia Dar! (Na binafsi nakubaliana kabisa ya kwamba matumizi ya gesi Dar ni muhimu na makubwa kuliko kwa Mtwara na Lindi kwa wakati huu), lakini je tumehabarishwa kuhusu hili vya kutosha?. Watu wangependelea kuona wafanyabiashara wakubwa (au watu wenye uwezo mkubwa) wanatozwa kodi kubwa ili kufidia wananchi masikini ili waweze kupanda na kuwa wananchi wa daraja la kati! Watu wangependela kuona badala ya Mkurugenzi mmoja kunuliwa gari ya V8 kwa gharama ya zaidi ya milioni 200 la kumchukua na kumrudisha kwake Kimara mwisho ni vema Wizara/Idara/Taasisi ingenunua Coaster kwa gharama ya chini ya milioni 100 itakayotumika kwa watumishi wote(akiwemo mkurugenzi) wanaokaa Kimara mwisho.




Mwalimu Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema ili tuendelee tunahitaji mambo manne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na uongozi bora. (Hata hivyo ukweli ni kwamba ni watu, siasa safi na uongozi bora/muundo wa kitaasisi, hili la ardhi halina mashiko kwa kuwa ni natural given). Wanauchumi na wataalamu wa siasa ya jamii siasa-uchumi leo wanakubaliana kuwa kuelezea mwenendo wa ulimwengu na matukio yake kunahitaji mambo matatu ya msingi watu(interests), siasa safi(interactions) na uongozi bora (institutions): interests, interactions and institutions; maamuzi yanategemea maslahi ya jamii/makundi ya watu, namna makundi hayo yanavyoingiliana kufikia malengo na namna taasisi zinavyoweza kuwa imara kusimamia mwingiliano huo. Hapa tunaona kuwa taasisi ndiyo inayotawala makundi haya mengine mawili kwa hivyo kuwa na taasisi imara ndiyo msingi mkuu wa Maendeleo na mafanikio ya Taifa lolote. Je tujiulize, Taifa letu lina taasisi imara zinazoweza kuratibu watu/makundi ya watu namna yak u-interact ili kupata matokeo chanya? (Narudisha kwako hili bwana Nguruvi3 kulitolea majibu)




Suala la Gesi ya Mtwara. Kama nilivyosema hapo juu, msingi mkuu wa mafanikio ya Taifa lolote ni uimara wa taasisi kuweza kuratibu maingiliano ya watu/jamii(actors), na uimara wa Taasisi unatokana na watu kupitia kura ambao unatoa kitu kiitwacho IMANI ya wananchi kukubali Taasisi husika iwasimamie. Iwapo Taasisi itapoteza IMANI kutoka kwa wananchi, basi jua jambo lolote itakalopanga litapata upinzani mkubwa hata kama upinzani husika hauna manufaa yoyote kwa wanaopinga. Kinachotokea Mtwara ni matokeo ya wananchi kupoteza IMANI kwa Taasisi waliyoiamini na si madai ya kufaidika na Gesi. Narudia tena, kinachoendelea Mtwara si madai ya Wanamtwara kufaidika na gesi ila ni kupoteza IMANI kwa Taasisi ya Serikali. Nasimamia hili kwa sababu, hata kama Serikali itaamua kujenga hizo plants Mtwara, hakuna uhakika wa moja kwa moja kuwa wana Mtwara watafaidika na hivyo kuwa "nchi ya maziwa na asali". Lakini pia madai ya Wana Mtwara ni "Kun-faya-kun". Kitu ambacho kinaleta ugumu wa Serikali kueleweka na wana Mtwara kwa kila inaloahidi kuwafanyia wana Mtwara, The Big Show anajua haya)




Why? Wamepoteza IMANI kwa Taasisi yao! Na imani imezidi kupotea pale Taasisi hiyo waliyoiamni ilivyowapelekea majeshi kwenda kuwasimamia. Kwa kifupi wana Mtwara wamekuwa "silent rebels" au "rebels by mentality". (Uasi wa chuki ya nafsi) Je, ni kwanini wamepoteza IMANI? "Because of the powerful interest groups to mold public policies in favor of minority interests". Wamerejea historia yao, wamerejea yaliyotokea kwingineko Tanzania ambako waliojenga nyumba za tembe juu ya dhahabu wanaendelea kuishi kwenye nyumba zao za tembe huku makundi-maslahi ndiyo yanayofaidika ilihali Taasisi yao ipo inaangalia wala haitoi uhalisia wa mambo yalivyo. Do we have powerful institutions? Nguruvi3 atakuja kujibu hili mimi wacha nimalizie kwa yafuatayo.



Je nini kifanyike? Mimi nina mtizamo kuwa kwa mazingira yaliyopo sasa, ni wazi gesi isafirishwe kwa njia bomba (yaani mradi uendelee). Kwa sababu mbalimbali. Mosi mradi huu unajengwa kwa fedha za mkopo ambazo kupatikana kwake kulitokana na terms of agreements zilizowasilishwa na kuridhiwa kwamba zinastahili kupewa mkopo, kubadili matumizi ya mkopo ni kukiuka taratibu za mkopo jambo ambalo litakuwa na madhara mengi kwa Taifa. Pili, Mradi huu unatekelezwa na Kampuni (tena ya kigeni) ambayo imeshaingia makubaliano na Serikali ikiwa pamoja na kuingia katika baadhi ya commitments na baadhi yao zaweza kusababisha ‘sunk costs'na hivyo kuleta madhara mengine kwa Serikali ya kutoka nje ya mkataba. Tatu, Malengo ya Taasisi yetu (Serikali) yamechambua, kubaini na kujiridhisha na hivyo kuelekeza nguvu kwamba kutekelezwa mradi huo ni kukamilisha hatua moja ya kuleta maendeleo katika Taifa letu, hivyo tuache waitekeleze hatua hiyo. Nne, hakuna uhakika wa moja kwa moja (strong augment) kuwa kuchakatwa kwa gesi Mtwara kutayabadili maisha ya wana Mtwara mara moja. Tano, kwa kuwa gesi itakayosafirishwa kwenda Dar ni sehemu ndogo ya gesi inayopatikana kusini, Serikali bado ina nafasi nyingine ya kuandaa project proposal ya kuchakata sehemu nyingine ya gesi Mtwara (kama wanavyotaka wana Mtwara) na kusambaza manufaa yake maeneo mengine ya kusini bila kuathiri mradi wa huu wa Dar na Serikali iishirikishe jamii ya wana Mtwara mwanzo mwisho. Sita, ni ukweli usiopingika kwamba kinachohitajika Dar si Umeme pekee bali gesi ambayo ina matumizi makubwa Dar kuliko Mtwara kwa hali ilivyo sasa. Hivyo, basi Serikali bado ina fursa zote za kuendelea na mradi huu huku ikiwa na nafasi ya kutekeleza mradi wa kuchakata gesi Mtwara kama wana Mtwara wanavyotaka iwe.




Sasa tatizo ni nini basi? "The better informed the Public, the better the public policy outcome". Kama nilivyosema hapo juu, wana Mtwara si waasi ni wenye chuki na Taasisi yao, ni wenye kupoteza IMANI na taasisi yao. Kama ingelikuwa ni waasi, obvious dawa yao ingelikuwa ni mtutu wa bunduki, vifaru na vikosi vya jeshi, lakini kwa kuwa si waasi (rebels) bali wana "donge moyoni" basi dawa yao ni maneno/kuhabarishwa/kuelimishwa (information). Hili ndilo linalowafaa wana Mtwara. Hivyo basi, kwanza Serikali iondoe vikosi vyote vya kijeshi na Polisi Mtwara, Pili, Mheshimiwa Rais asilisemee "ughaibuni" suala hili, yeye ni Rais wa wote, bado Mheshimiwa JK nyota yake inang'aa machoni mwa watanzania walio wengi; afanye Ziara ya Maendeleo Mikoa ya Kusini (Mtwara na Lindi katika Wilaya zote), na asione ni udhaifu wa Serikali kuwaeleza wana Mtwara kuwa Serikali ili overlook katika suala hili kulikotokana na nia njema kwa watanzania wote hata hivyo madai ya wanamtwara ni ya msingi na Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kujenga mradi mwingine wa kuchakata gesi hapo hapo Mtwara lakini kwa hatua iliyofikia sasa, wana mtwara wasizuie mradi wa bomba la gesi (Black and White). Si suala la kuwaweka wana kusini kwenye kundi la "wachoyo" wasiotaka gesi inufaishe wengine-la hasha hili si dai la wana Mtwara. Ziara hii itasadia kubaini ukubwa wa tatizo na hivyo kujiridhisha ikiwa kweli tatizo la gesi Mtwara linahita military deployment auvinginevyo.




Je ni madhara ya Serikali kundelea na mradi kwa njia mtutu wa Bunduki? Mradi hautakamilika? Hakuna, mradi utaendelea, utakamilika lakini utazalisha hatari Fulani kiuchambuzi (fuatilia makala za duru za siasa ipo siku utaja juzwa).

Nihitimishe kwa fundisho moja linalopatikana katika Maisha ya Nabii Yusuf, kwamba hali ya mavuno katika nchi siku zote haiwi sawa kwa kila mwaka, hivyo mwaka unaovuna sana, uweke utaratibu wa kuhifadhi kwa ajili ya miaka ya ukame inayokuja. Serikali kupita CCM iliaminiwa vya kutosha na Wananchi lakini ikajisahau kwamba ule ni wakati wa mavuno tu hivyo wanapaswa kuilinda na kuindeleza imani waliyopewa katika siku zijazo ambazo zina ukame(maendeleo ya mawasiliano na kupanuka kwa elimu). Si zaidi ya miaka 15 iliyopita, Tanzania ilikuwa inajulika kuwa na vyuo vikuu 3 tu (UDSM, Mzumbe, SUA); leo hii kuna vyuo na Taasisi za elimu ya juu zaidi ya 40! Ilikuwa muhali kuwasiliana baina ya mtu na mtu mpaka mtembeleane au mkanunue stamp Posta, leo hii watu ambao hatujuani tukiwa sehemu mbalimbali za dunia tunaongelea mustakabali wa Tanzania (as if tuko Dar)! Daraja la Manzese lilipojengwa, kila mmoja alikuwa anapenda kuchukua picha pale kwamba ni kitu cha pekee kuwapo duniani, leo hii watu wanaangalia Madaraja yaliyojengwa Japan, Korea, China n. k na hivyo kubaini kuwa Daraja la Manzese si lolote si chochote. Watanzania walikuwa wakijazana kwa wingi kwa wenye Radio KUSIKILIZA bbc ikiripoti vita ya Iraq na Kuwait, leo hii WANAANGALIA mageuzi yanayotokea Tunisia, Egypt, Syria kupitia simu zao za mkononi. Miaka michache iliyopita, huyo Raia wa Lupaso Mtwara huko hakuwa hata na "imaginary figure" ya DAR ikoje, leo hii anaweza funga dishi lake na kuona taswira ya DAR ikiwa imejaa magari barabarani, hali ya kuwa yeye hata baiskeli ya kwenda kumsagia nafaka mkewe KM 20 hana, unazani huyu mtu atakuwa na level gani ya uzalendo kwa Nchi yake? Hii ni mifano inayoonyesha kwamba, sasa si kipindi tena cha kuvuna kwa Serikali na Chama kinachoshika Dola bali ni kipindi cha kufikiria ni vipi wananchi wa DAR watapata huduma zinazofanana na watu wanaoishi Tokyo,Japan; vipi Wananchi wa Zanzibar watapata huduma zinazofanana na watu waishio Taiwan! na vipi wananchi wa Morogoro watapata huduma zinazofanana na watu wa Kuala Lumpur, Malaysia na vipi wananchi wa Mafia watakuwa na maisha yanayofanana na waishio Busan, Korea. "Government fails when public interests outweighed by interests of politicians and special interests groups".

Kuhusu Prof. Lipumba, naomba nichangie wakati mwingine hususan kama nitafanikiwa kuona machapisho yake ya miaka ya 2011/2012/2013, kwani hii ndio itatupa mwangaza wa kujua anachofikiria hivi sasa (mtizamo wake wa sera za kijamii).
 
Update July 22 2013
Ni mtoto wa Kiume aliyezaliwa. Jina litafahamika baadaye but likely Alexander

Kwa sasa urithi wa kiti unafuata utaratibu huu

Prince Charles
Prince William
Prince ''baby cambridge'' aliyezaliwa leo
Prince Harry

Kama longevity itaendelea kama ilivyo sasa kwa Elizabeth kupitisha miaka 60 akiwa katika utawala it is unlikely kizazi hiki kumuona baby cambridge kama King.

Hii maana yake sasa ni kuwa itachukua miaka takribani 60-100 pengine kuwa na Queen.
Na kuwa mkuu wa Jumuiya ya madola atakuwa King kwa muda mrefu ujao.

Kama tulivyowahi kuandika bandiko la hapo chini, ujio wa mtoto huyu umeongeza biashara sana uingereza kutokana na souvenir, mapambo, vyombo vya habari n.k. na itaendelea hivyo kwa muda wa kama wiki mbili.
Picha ya kwanza ni deal kubwa sana.

Lazima tujifunze namna ya kuthamini vitu vyetu. Ni sehemu ya uchumi, wenzetu wanatupia bao kwa mambo madogo tu.




UZAO WA MTOTO FAMILIA YA KIFALME UINGEREZA

Prince William na mkewa Kate Middleton wanataraji kupata mtoto wa kwanza wakati wowote.
Hadi tunaandika bandiko hilo wawili hao bado wapo Hospitali na hakuna tangazo la uzazi.
Inasemekana tarehe za kuzaliwa mtoto zimepita kwa muda fulani jambo la kawaida katika uzazi

Wanahabari wamepiga kambi kupata habari za uzao wa mtoto huyo ambaye hadi sasa anajulikama kama baby Cambridge. Haijulikani ni wa kiume au wa kike.

Utaratibu wa kufuata katika kutangaza habari za uao ni kwa prince William kumpigia simu malkia kwanza halafu wana familia wa Buckingham kutoa taarifa za ujio wa mtoto katika familia ya malkia. Huyu atakuwa kitukuu cha malkia Elizabeth II

Imefika wakati watu kuhoji jina la mtoto huyo litakuwa ni nani huku kukiwa na orodha ndefu ya mapendekezo.

Swali kubwa linaloulizwa ni hili, kwanini mtoto huyo apewe 'attention' ili hali kuna mamia ya watoto wanazaliwa kila siku tena wengine katika hali ngumu zaidi?

Kuna majibu mengi juu ya hili.
1. Jambo linalohusu familia ya kifalme Uingereza hufungamanishwa sana na biashara.
Inasemwa kuwa ndoa ya Kate na William iliingiza mabilioni ya dola kupitia bidhaa, matangazo, utalii n.k.

Na hili halionekani kwenda mbali na ukweli huo. Bidhaa zinauzwa kuhusiana na mtoto huyo mtarajiwa na vyombo vya habari vikitoa makala na habari za kibiashara.

2. Waingereza ni wazuri wa kupiga debe katika mambo yao.
Wanapoamua kulifanya jambo dogo kuwa kubwa wanauwezo huo.
Hili linagusa sana tamaduni zao na ni moja ya mambo yanayowaunganisha waingereza.

3. Mtoto mtarajiwa ana uhusiano na siasa za nchi yake na za kimataifa.
Hapa ndipo tuanzie kwasababu ni sehemu muhimu sana ya uzao huu.

Kwanza, tuangalie kwa uchache kuhusu familia ya kifalme. Familia hii ndio inayotoa mkuu wa nchi ya falme za uingereza (United Kingdom).
kuna tofauti ya united kingdom na England na ni rahisi sana kuchanganya mambo hayo.

Waziri mkuu wa Uingereza ni mkuu wa serikali na siyo mkuu wa nchi. Yeye hupata ridhaa ya kutawala kutoka Buckingham Palace ndipo anaelekea number 10 Downing street.

Familia ya kifalme ndio pia wakuu wa kanisa la Uingereza la Church of England.
Kutokana na ukoloni tulikuwa na kanisa la England church ambalo limebadilika kwa jina kutokan sasa hivi linajulikana kama Anglican na sehemu nyingine wanaita African Inland church n.k.

Kwa muda wa miaka 300 taratibu za utawala zilihusisha unasaba wa damu, kwamba kurithi kiti cha enzi wanaume walipewa kipaumbele. Iwapo mfalme au malkia alikuwa na watoto 3 wakwanza wa kike na wa pili wa kiume, kiti cha enzi kilimruka mwanamke na kwenda kwa mwanaume(throne)

Malkia Elizabeth alikuwa mtoto pekee wa King George na hivyo hakukuwa na chaguo bali yeye.
Kuna mambo yasiyosemwa kuhusu yeye kurithi kiti hicho kwani aliyepaswa kwa taratibu alikuwa mwanafamilia wa ndugu ambaye alikuwa ni mwanaume. hilo tutalijadili wakati mwingine.

Katika familia zilizofuata utaratibu wa uzao ni ile ya Diana na Charles ambao walipata watoto wawili Harry na William,William ndiye mrithi wa kiti na Harry ni kama spea.

Kwavile falme ilikuwa inafuta utaratibu wa miaka 300 iliyopita, urithi wa malkia ulikuwa ufuate utaratibu wa Elizabeth II, Prince Charles, William na Harry.

Utaratibu huu uliwaruka watoto wa Elizabeth wasichana kwasababu watoto wa kiume walifuatana na wao ndio warithi.Kwa muktadha huo prince Harry ni mrithi wa tatu(3rd in throne).
Kumbuka hili lina umuhimu katika mjadala.

October 28 2011 ufalme ulibadili taratibu na kuwa urithi wa kiti sasa hautachagua jinsia tena.
Kwa maneno mengine kama mtoto wa kwanza atakuwa mwanake basi atakuwa malkia hata kama wanaomfuata ni wa kiume.

Hii maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa mtoto mtarajiwa wa William na Kate siku moja atakuwa mfalme au malkia wa Uingereza na hivyo kiti cha enzi kitafuta utaratibu ufuatao:
1. Prince Charles
2. Prince William
3. 'Babay Cambridge' ambaye hajazaliwa
4. Prince Harry

Kwamba nafasi ya prince Harry sasa ni namba 4 na si tatu kama tulivyosema hapo awali.
Kwa kuangalia umri wa maisha 'longevity' wa malkia Elizabeth ni wazi prince Harry hatakuwa mfame.

Baba yake ana zaidi ya miaka 60,kaka yake ni mdogo katika miaka 30 na sasa kichanga na kila mmoja atakula shea yake kabla ya Harry ambaye hataonja ufame labda tu litokee janga kubwa sana lisilotarajiwa.

Ni kwa muktadha huo baby cambridge anategemewa kukalia kiti cha enzi kama mfalme au malkia na hapo atakuwa mkuu wa Anglican, mkuu wa nchi na mkuu wa jumuiya ya madola
(commonwealth).

Hivyo msisimko ni wa jumuiya kubwa ya kimataifa ni kwasababu mtarajiwa atakuwa na ushawishi mkubwa katika medani za kiutawala na kiimani ndani na nje ya Uingereza, na hili hasa ndilo linaleta msisimko duniani.

Endapo baby cambridge atakuwa wa kike basi uwezekano wa kuitwa Elizabeth au Victoria ni mkubwa sana. Sababu kubwa ni kuwa Victoria ndiye malkia aliyeongoza Uingereza kwa muda mrefu akifuatiwa na Elizabeth wa sasa ambaye itakapofika september 5 mwaka 2015 ataukuwa ameifikia rekodi ya Victoria.

Kwa uchache mtoto mtarajiwa atakuwa sehemu yetu Watanzania na mataifa ya madola kwasababu ndiye atakayekuwa mkuu wa jumuiya hiyo hata kama ni miaka 100 ijayo.

Haya ndiyo yanajiri na tutaendelea kuwaletea habari zaidi kadri zitakavyopatikana.

Tusemezane

Mgeni wa leo
 
Mkuu nguruvi3,

Kwa mujibu wa bandiko lako #263 :

Katika majadiliano hapa JF kuna siku moja Mchambuzi aliuliza swali moja ambalo sina majibu kama walivyo wengi. Hivi hii gesi ni kwa matumizi yapi? Ni LNG! na matumizi yake hasa ni industrial au ni yaweza kuwa domestic au ni vipi.

Hakuna aliyejibu kama ambavyo viongozi hawawezi kuwaeleza wananchi.
Ndio maana nasema si Mtwara tu sote hatujui nguvu hii inayotumika katika miradi bila wananchi kujua inakusudia nini hasa. Mchambuzi hebu tusaidie kidogo maana eneo hili umewahi kulieleza vema sana.

Nilijadili suala husika miezi kadhaa iliyopita kupitia uzi wangu titled:

"Sakata La Gesi Mtwara: Tuache Unafiki na Woga, Tuchambue Mchele na Pumba",

Na ilikuwa katika moja ya hoja zangu kujadili hoja zako motomoto ulizokuja nazo katika uzi husika; Nadhani niiweke tu tena hapo chini kama nilivyojadili kule badala ya kujirudia tena hapa; Nilisema hivi:

Nguruvi3,

Karibu sana katika mjadala;Kimsingi, naunga mkono hoja zako zote katika bandiko namba 34, lakini nikienda mbali zaidi, inaamsha mawazo mengine ambayo nadhani ni muhimu kwa huu mjadala kama nitakavyo fafanua;

Kwanza - hoja zako zinatulazimisha pengine tuangalie kwa undani the socio-economic profile ya eneo husika (Mtwara) kisha tuoanishe na thamani ya gesi asilia from the business and economic point of view, hasa nini kinaweza kupatikana kama benefits kwa wananchi wa eneo husika - both directly and indirectly;

Kama nilivyokwisha jadili, future value ya gesi asilia ni kwenye suala la nishati ambalo demand yake itazidi kukua siku hadi siku, huku projections zikiweka wazi kwamba mahitaji ya umeme wa gesi will outstrip umeme wa makaa ya mawe, nuclear na hydro duniani in the next 30 years;kuna sababu nyingi kwanini ni hivi, na partially Waziri Muhongo alielezea jana katika kuhitimisha hoja yake kwamba ukiondoa umeme wa hydro, umeme wa gesi ni bei nafuu per unit, huku akijadili kwamba pamoja na umeme wa maji kuwa nafuu, gharama zake za uwekezaji na uendeshaji, ni kubwa kuliko gesi; hivyo ndivyo nilivyomuelewa; Kwa maana hii, nishati ya gesi ndio where the future of this resource holds, hivyo uwekezaji wetu pamoja na faida kwa maeneo husika ujikite zaidi huko.

Lakini haina maana kwamba uwekezaji kwenye LNG plants hauna maana, kwani maana ipo, lakini cha msingi hapa ni kwamba matumizi haya yatazidi kupotea with stages of economic development yani matumizi ya gesi kwa ajili ya residential, commercial, industrial, na world energy outlook wanaweka wazi jinsi gani demand ya gesi kwa ajili ya matumizi haya inafikia saturation point marekani na sehemu mbalimbali za EU; Point yangu ya msingi hapa ni kwamba tuendelee to take advantage ya demand ya gesi kwa ajili ya residential, commercial and industrial wakati bado tupo kwenye take off stage of economic development ili tuvuke low levels of development ya sasa; Lakini kwa manufaa ya vizazi vijavyo, mbali ya kuwekeza ipasavyo na kupata short term and medium term gains ambazo zitatunyayua pia, tusijisahau kujipanga kisera tukapitwa na suala la gesi as the major source of energy for the future relative to thermal, hydro and nuclear;

Pengine hoja yangu hapo juu itaeleweka zaidi nikifafanua kama ifuatavyo:

Energy/Nishati ni basic input ambayo inahitajika kukidhi mahitaji mbalimbali ya binadamu kama vile heating, motive power (e.g water pumps, transportation etc) and lighting; businesses, industry na public services za kisasa kama vile afya, elimu, mawasiliano vyote hivi vinategemea sana access to energy services;as a matter of fact, ukosefu wa huduma za nishati upo directly linked na matatizo ya umaskini kama vile high mortality rates, low life expectancy, illiteracy and many other poverty indicators; katika nchi nyingi maskini, ukosefu wa huduma ya nishati pia huchangia sana tatizo la rural - urban migration; Kwetu Tanzania, Nishati ya gesi ni fursa muhimu sana ya kutusaidia kutatua matatizo yote haya, sio tu kwa mtwara bali nchi nzima; Ni katika muktadha huu, Waziri Muhongo alijeng hoja wakati wa hitimisho la bajeti ya wizara yake kwa kusema kwamba gesi ni mwokovu wa maskini wa Tanzania na serikali yake imejipanga kuitumia rasilimali hii kuiandaa Tanzania sio tu ipande na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini pia itatuandaa kuingia karne ya ishirini na mbili kama taifa imara na bora kabisa socially, economically n.k; Naungana na hoja hii ya Muhongo lakini only if we manage to invest vizuri on where the future holds when it comes to suala zima la matumizi ya gesi baina na energy na Matumizi mengine;

Nikiwa bado katika hoja hii kuhusiana na faida za gesi asilia kwa uchumi, nadhani ni muhimu tukafanya profiling ya mkoa wa mtwara ili tupate fursa ya kuelewa jinsi gani viongozi wetu wanaweza kukaa nao na kukubaliana katika mambo ya msingi kuliokoa taifa letu; kwa maana nyingine, wengi tunasahau kufanya a profile analysis na ndio maana we fall short of understanding jinsi gani tulimalize tatizo la mtwara na kurudisha taifa letu katika hali yake ya amani, umoja, upendo, mshikamano na utulivu tuliyoizoea;Nitagusia machache kwa haraka haraka ili hata huko mbeleni, yakitokea matatizo kama haya mikoa mingine basi tutazame masuala kama haya:

1. At the turn of the new millennium (the year 2000) mtwara ilikuwa ni the second smallest region in Tanzania after Kilimanjaro; Sasa kwa wale wenye hoja kwamba gawio la bajeti lazima liendane na ukubwa wa eneo husika, suala la kilimanjaro kuwa top ten consistently na mtwara kuwa bottom five in terms of mgawanyo wa keki ya taifa, katika hili hoja zao zinakosa mashiko;

2. Mgawanyiko wa eneo per square kilometa, masasi ina cover 53% ya mkoa mzima huku newala, mtwara vijijini na tandahimba iki share the remaining area; implicationa zake hapa ni nyingi na tutazijadili baadae;

3. About 85% ya ardhi mkoani mtwara ni arable land, huku chini ya 25% of the 85% ikiwa katika matumizi ya kilimo; zao kuu la kilimo cha biashara ni korosho lakini pia wanalima karanga, sorghum,mihogo, paddy, mahindi, millet na simsim; Tukumbuke pia kwamba mtwara wana historia kubwa sana ya baa ya njaa na ni moja ya mikoa ambayo bado haijitoshelezi kwa chakula pamoja na ukweli kwamba sehemu kubwa ya uchumi wake ni subsistence based;

4. Mtwara unapakana na mikoa minne ya Tanzania - Morogoro, DSM, Ruvuma na Lindi; ni muhimu kuangalia economic linkages kati ya mtwara na mikoa hii kwa undani ili kubaini kwamba wapi kuna inputs muhimu kwa wanamtwara in the context of natural resource base yao, hivyo kuwekeza huko accordingly badala ya kuamua tu kwamba DSM is the only choice;

5.Mtwara ni moja ya mikoa iliyoathirika sana na net migration - net lifetime migration ni moja ya the highest in the country; Hii ni kwasababu mkoa huu umekuwa very unattractive kwa vijana lakini pia vizazi vipya, kwahiyo wanaenda kwingineko for greener pasture and by coincidence, vivutio vikubwa kwa wanamtwara ni ile mikoa niliyojadili kwamba throughout history imekuwa inapewa kipaumbele when it comes to keki ya taifa (bajeti); ni kwa mantiki hii, hata tume ya mipango katika taarifa yake ya mkoa wa mtwara inawaita vijana wa mtwara wanaohamia miji mingine kwamba ni "ECONOMIC REFUGEES"; kumbuka, hii ni serikali; Katika hili, tume ya mipango inajadili kwa uwazi kabisa kwamba ili kutatua tatizo husika, ni muhimu kwa serikali kuwekeza ili kuvutia nguvu kazi ya mtwara ibakie mtwara; Tume ya mipango inaenda mbali zaidi na kutaja maeneo muhimu ya kufanya ili kuinua mkoa huu kwamba ni pamoja na development of infrastructure, viwanda based on "local available resources", n.k, huku ikijadili kwamba - "this will make mtwara attractive to youths so that they don't need to go beyond its borders to seek a secure economic future";

6. Mtwara wakati wa mwalimu nyerere ulikuwa na viwanda - agro based industries, vitano vya kubangua korosho, viwili vya mkonge ambavyo vilikuwa vinatoa ajira na kuleta economic benefits mbalimbali kwa mkoa; leo katika hili, hali ni mbaya;

Tume ya mipango katika ripoti zake miaka nenda miaka rudi imekuwa very optimistic na maendeleo ya mtwara and mentions potential areas kuwa ni pamoja na maendeleo ya tourism industry, kilimo, forestry, ufugaji nyuki, uvuvi na VIWANDA; Sasa kama haya yamekuwa yakiwekwa bayana na tume ya mipango (serikali), basi ujio wa gesi ni fursa muhimu ya kutekeleza kwa vitendo;

Nguruvi3, maeneo mengine uliyojadili ni suala la quality na ajira kwa mtwara; naunga mkono hoja, na kwa kuongezea, ni muhimu kwa taifa sasa kuanza kuwa serious na national innovation systems ambayo itajenga skills, capabilities and entreprenuership drive kwa wanamtwara na watanzania kwa ujumla katika maeneo ya gesi na mafuta; na kwa mtwara, seriousness ni muhimu ianze kwa serikali kujenga chuo kitakachotoa mafunzo ya gesi na ambacho wawekezaji watalazimika kukichangia na pia kukishirikisha katika shughuli zao; kwa kifupi - faida ya gesi kwa wanamtwara itakuwa na manufaa tu iwapo itajitokeza katika economic output ya mkoa na employment na haya yalenge katika value chain ya sekta ya gesi - exploration, extraction, production, transportation, storage, distribution, servicing, maintenance, legal services, well services, construction, power generation, engineering services etc;inawezekana kwa leo hakuna such skills lakini tukiwekeza sasa, mtwara can become the centre of excellence afrika mashariki na kati katika utaalam wa gesi within the next 25 years;"

The Big Show, heshima mbele mkuu, unajadili hoja zako kizalenda sana, hakuna ushabiki wa kisiasa, sote tungekuwa tunajadiliana kwa mtindo huo, hakika tungelipeleka taifa letu mbali sana;
 
Mkuu Nguruvi3,shukran sana kwa kunistua kuhusu hoja ya Mkuu Mchambuzi,
Kwa kweli haijaacha kitu,mara nyingi huwa najifunza mambo mengi sana baina yenu nyinyi watu wawili kwenye hoja zenu,huwa mnasimama kwenye mstari na mnatumia lugha elekezi katika udadavuaji wenu wa hoja,
Bado nipo naendelea sana kuwasoma na kunufaika nanyi kwa kias kikubwa sana,
Kwa mara nyingine tena shukrani sana,mungu awabariki sana,na kwa kweli taifa hili linahitaji watu sampuli hii...
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi umesaidia sana kwa uchambuzi wako kama ulivyolirejea katika bandiko namba 270, shukrani. Kwa hakika bandiko hilo linaonyesha jinsi gani safari ya Tanzania kuelekea middle income country na nafuu ya wana Mtwara kufuta historia yao ni ngumu kidogo. Kwani inaonekana kuna mgongano unaokosa political will ya kutekeleza kwa vitendo yaliyobainishwa na Tume ya Mipango juu ya maendeleo ya Mtwara. Na political will ni silaha kubwa katika utekelezaji wa miradi katika nchi zenye mfumo wa kisiasa kama huu wetu. Ukipitia website ya EPZA, katika maeneo yaliyokuwa earmarked kwa ajili ya SEZ, utaona kwamba Mtwara imekuwa earmarked lakini hakuna maelezo ya ufafanuzi wa kiasi gani cha eneo kilichotengwa. Vilevile, Mkoa wa Lindi pametengwa Ha 250. Kwa mujibu wa The Guardian la 15/05/2013, Mkurugenzi Mkuu wa EPZA amenukuliwa akisema kwamba Mtwara ni next Target baada ya Bagamoyo na hivyo pametengwa Ha 110 kwa ajili ya Free Port Zone na wame-earmark Ha. 2600 kwa ajili ya SEZ. Kinyume chake maeneo mengine yanayopakana na mikoa hii miwili yametengewa eneo lenye ukubwa wa Ha. 12207 (Bagamoyo 8,000+1000?, Morogoro 2000, Ruvuma 2207). Hizi namba zinatuleta kulekule kwenye ukweli kwamba, Mtwara itaendelea kutoa Economic Refugees kwa wingi kwa kukosa political consideration.

Aidha, ningependa kupata ufafanuzi kwenye projections za mwelekeo wa Taifa na uthabiti katika utekelezaji wa miradi kadhaa inayohubiriwa hususan katika sekta ya nishati na gesi. Nikiangalia matukio mengi yanayotokea hivi sasa, nahisi kama vile mihimili mitatu ya nchi haifanyi kazi kama ilivyokusudiwa na badala yake mhimili mmoja umepora mamlaka za mihimili mingine hususan Bunge hali inayoonyesha kuwa tatizo la Bunge kutoweza kuisimamia Serikali litaendelea kuwepo, na hivyo hali ya uendeshaji wa mambo ikiwa pamoja na miradi na mikataba itaendelea kuwa business as usual. Hii pia huenda inachangia katika utokeaji wa matukio ambayo mhimili mmoja (Serikali) unayafanya pasipo kujali mipaka au labda kuna sehemu itawajibika kutoa maelezo na kuwa sued iwapo imeenda aganst na mipaka yake. Mbaya zaidi mhimili huu unaelekea kudharau au hata kuvamia haki za raia(raia kuingiwa na woga wa kufanya maamuzi yaliyo katika haki zao).

(Given that, misuguano iliyoanza kujitokeza kwenye katiba itapelekea aidha kutokuwa na Katiba mpya au kuwa na Katiba isiyo na meno kama tuliyonayo sasa hapo 2015), nachelea kusema kwamba maamuzi ya wananchi yanaweza pia kumezwa na mhimili huu katika uchaguzi ujao na hivyo hali ya kisiasa kuendela kama ilivyo (CCM kuendelea kushika dola).

Hivyo basi, wasiwasi wangu na swali langu kwako Mchambuzi na Nguruvi3 ni hivi,ukiangalia aina ya viongozi wanaotarajiwa kuwa watoa maamuzi wakuu wa CCM katika kipindi cha 2015 na kuendelea, kiukweli wanakatisha tamaa na wamekuwa ni kama opportunists zaidi kuliko viongozi wa kijamii (Makao Makuu na Jumuiya zote za CCM), ni kama walioishiwa mbinu za kufanya siasa. Kadhalika, kuna kila dalili kwamba watu wenye hekima zao ambao wangesaidia kuunda CCM imara either wamewekwa bench au wameamua kukaa pembeni kuangalia drama inavyokwenda. Je katika mazingira haya unadhani kutakuwa na ufanisi/ matokeo mema katika utekelezaji wa Miradi na shauku ya maendeleao kama Ndugu Mchambuzi alivyojaribu kuanisha "What should be done for better realization of future dreams on the way towards middle income country". Je tuwe na optimistic view kwa Mtwara mpya na tanzania kwa ujumla ambayo 2025 inaweza kufikiwa?
 
Wakuu nashukuru sana kwa mimi kupata muda mzuri kuja kuendelea na mjadala huu.
Nguruvi3 nafikiri utakumbuka maneno yangu hasa kuhusu project implimentation kwa nchi yetu hii. Leo hii wana mtwara wamekuwa watu wa kwanza kabisa kuhusu kuiamsha serikali kuhusu namna ya ushirikishwaji wa wananchi kwenye mradi ya maendeleo.

Nashukuru kuona THE BIG SHOW ametuambia bayana kwamba wananchi wa mtwara wana kitu gani nafsini mwao. tena amejaribu kuwakilisha nafsi ambayo yeye anaiishi na hivyo kuwapa watu kama mimi na wewe na nafasi ya kujua nini kipo mtwara na nini maoni ya wana mtwara.
Zinedine ameeleza vyema juu ya siasa safi na utawala na hilo pia Mchambuzi aliwah kulisema, lakini naomba binafsi niseme jambo moja tu hapa. Ya kwamba siasa safi zinaendana na uwajibikaji safi wenye tija.

Hebu turudi tuanze kuiangalia wizara hii ya nishati na madini toka mwanzo, na binafsi nitasemea mifano michache sana, tuanze na miradi ya madini je miradi hii ya madini imewah kuwa na tija kwa wanachi wa eneo husika?? je miradi hii imewah kuwa na usalama wa kiafya na mazingira kwa wananchi wa eneo husika? je wizara kama wizara inatuambia nini juu ya haya?? nilifikiri wakati mto mara unaleta uharibifu wa mazingira, ilipaswa wizara hii ijiulize je tulikosea wapi?? nafikiri wanachi wa shinyanga, mirerani, sijui geita wanabaki na maisha duni wizara hii ingejiuliza tumekosea wapi?? Mbaya zaid wananchi hawa walikaa kimya ama ikiwa ni kwasababu ya woga, ama kwasababu ya ubize wa maisha.

tusiishie hapo tukienda kwa kihansi, tujiulize je mradi huu chini ya wizara hii hii je ulikuwa salama wa mazingira na wenye tija kwa wananchi?? kama hapana je wizara hii inatuambia nini??

Tuendelee mbali zaid, tujiulize mradi wa umeme wa Kakobe je mradi huu una tija kwa wananchi?? je usala wa mazingira??
Leo hii tunaongelea swala la gesi je mradi huu utakua tija kwa wananchi?? usalama wa mazingira je??

narudia kusema kwamba uwajibikajia wenye tija ndicho kikwazo hapa. Hakuna kiongozi ambaye anayaona haya maisha kwa jicho ambalo sasa wananchi wanayaona. wananchi sisi tulikuwa kwa muda mrefu tunapelekeshwa na viongozi wetu, hakuna ushirikishwaji sasa tumechoka wananchi wanachotaka ni ushirikishwaji tu.

muulize THE BIG SHOW wananchi wa mtwara wangeshirikishwa ( hapa siongelei viongozi bali mwananchi wa kawaida kabisa) wakaulizwa kama wanataka huo mradi na wanataka utekelezwe vipi haya yasingelikuwepo kabisa. Kitendo cha serikali kudharau na kuona wananchi hawtahoji ama hawajui haki zao ndicho kinachoighariimu serikali na kufanya kupoteza imani kwa wanachi kabisa.

bado nitazidi kusema kwamba kama kweli swla la mradi wa gesi wa mtwara kulikuwa na EIA basi tupewe iyo ripot tuisome tuone je kweli wananchi wa mtwara wao walishirikishwa?? sijui kwann hata wabunge hakuna aliyewah kuhoji juu ya hili manake tungepewa ripot tungejua nani ndiye mchawi kwenye hili sakata.

serikali na yenyewe imekaa kimya na kusubiri kutumia mabavu sasa ninachoiuliza hii serikali hivi itapiga na kuua watu wangapi kwa kigezo cha anaye kaidi ""apigwe""?? na je kwanini kwenye maswala ambayo majibu yake ni mepesi bado serikali inapiga chenga??

ningekuwa mimi ni rais wala nisingahangaika kuumiza kichwa ningesema tu jamani hebu wapeni wana mtwara ile EIA REPOTI WASOME WENYEWE walitaka nini. pale angekuwa amewashinda manake ripoti kama ilifanywa inamaana hoja za wana mtwara zingesikika na hivyo kukata mzizi wa fitina.

sasa hapa EIA hakuna kama ipo ni zile za kupikwa tena bila hata kufika site na kujionea wewe unategemea iweje??

Ndugu zangu leo wana mtwara wanalia hawataki gesi itoke, serikali italazimisha itakapofikia watu wanaaza kulaza maboamba ya gesi chini pataibuka swala jingine kwamba wanachi wanakataa ardhi yao kupitisha gesi hadi walipwe fidia sasa sijui hawa nao watauwawa ama kupigwa ama nado kile kipengele cha sheria kwamba ardhi ni mali ya serikali kitatumika??

sishangai hapo laki utashangaa ya kufanana na yale ya kihansi toad yakaibuka ukaskia kuna pango la ajabu lenye nyoka wa tofauti kabisa dunian sasa mradi kupita hapo kiumbe hiki kitatoweka. na watu wa mazingira wakilishikia bango mradi utasimama tena.

kwangu mimi kutokufanyika kwa EIA kwenye mradi mkubwa kama huu naona ndio chanzo cha haya yote yanayojitokeza sasa.

Leo mchana nilipita maeneo ya jangwani nikaona ujenzi ulivyoendelea pale jangwani wa stendi na gereji ya RBT nilishangaa from no where naanza kuwaza why putting it just close to the mouth of msimbazi river?? imagine pale ndio eneo la mwisho ambapo maji yanamwagika baharini na hii ilikuwa ni swampy area ambayo ilikuwa inaact kama NATURAL WASTE STABILIZATION POND, hivyo maji yalikuwa yanatibiwa pale na yale majani unayoyaona pale kazi yake kubwa ni kupunguza sumu kwenye hayo maji machafu. sasa ona wameiua kabisa tell me ni uchafu kiasi gani utakuwa unatupwa direct baharini?? je marine ecosystem tunaiharibu ka kiasi gani?? je how much will it cost the goverment as kuna penalties za amount ya BOD ambayo tutakuwa tunaaingiza baharini??

tukumbuke kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa makubaliano ya kimataifa ya utunzaji wa mazingira duniani. Usishangae ni kwamba hatupewi tu data ila Tanzania huwaga inatozwa faini sana tu kwa kuharibu mazingira. lkn bado hatujifunzi.
 
Last edited by a moderator:
Zinedine bandiko lako #273 limenifanya nijiulize maswali makuu mawili hivi kwanini Bgamoyo?? huwa najiuliza sana sipati jibu kabisa. bandari mpya ijengwe Bagamoyo, EPZE ijengwe bagamoyo, barabara ya kwenda kaskazini ijengwe bagamoyo, hospitali kuu ya mkoa wa pwani ijengwe bagamoyo. hvi huko bagamoyo kuna nini??

ile evenly distruibution ya resources ipo kweli?? mbona siskii maeneo mengine jamani?? mbona singida siiskii kabisa?? ama wao hawaaitaji kufaidika na uwekezaji?? mbona tabora nako ama wao wabaki na asali tuuuuuuuu ambayo hata mnunuzi wa uhakika hakuna??

hii nchi inahitajika mapinduzi ya kifikra ya kikweli kabisa vinginevyo kuna watao neemeka zaid na wengine wabaki maskini kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Zinedine bandiko lako #273 limenifanya nijiulize maswali makuu mawili hivi kwanini Bgamoyo?? huwa najiuliza sana sipati jibu kabisa. bandari mpya ijengwe Bagamoyo, EPZE ijengwe bagamoyo, barabara ya kwenda kaskazini ijengwe bagamoyo, hospitali kuu ya mkoa wa pwani ijengwe bagamoyo. hvi huko bagamoyo kuna nini??

ile evenly distruibution ya resources ipo kweli?? mbona siskii maeneo mengine jamani?? mbona singida siiskii kabisa?? ama wao hawaaitaji kufaidika na uwekezaji?? mbona tabora nako ama wao wabaki na asali tuuuuuuuu ambayo hata mnunuzi wa uhakika hakuna??

hii nchi inahitajika mapinduzi ya kifikra ya kikweli kabisa vinginevyo kuna watao neemeka zaid na wengine wabaki maskini kabisa.
gfsonwin
Heshima kwako Mkuu,nimekusoma kwa utuvu wa hali ya juu katika hilo bandiko lako la juu lililojaa uchambuz wa kina na wa hali ya juu,mimi sina mengi sana ya kusema,
Kwani mengi yameshasemwa sana,kikubwa kilichopelekea kufikia hali hii ni kama hiko ulichokisema "USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA ENEO HUSIKA"

Wananchi ama watanzania wengi wao tumekosa matumain na iman na serikali yetu hata pale inapokuwa na nia njema wakati mwingine kutokana na kukosa kwao uwajibikaji na uzalendo katika kusimamia rasilimali za taifa na madudu yao viongoz na wataalamu wetu katika kuingia kwao mikataba mibovu mibovu inayoliingizia taifa hili hasara kubwa,madeni na ugumu wa maisha kwa wananchi wa kipato cha chini,

Usishangae sana hili la bagamoyo,kwani Huyu Mkuu wa nchi anachokifanya sasa ni kuvutia kwake,ni mwamba ngoma mwenye nguvu za ziada kwa sasa ndan ya taifa hili,na unyonge huu tulionao watanzania pamoja na kukosa kwa uzalendo kwa hao wanaomzunguka ndio kwa maana ngozi hii inawambwa kuelekea bagamoyo katika miaka miwili hii ya kumalizia muhula wake,
Potelea mbali na ni hasara yake yule Chinga Mkapa kama yeye alidhani kwamba JK akija atakuja kuendeleza Plan ya Mtwara Corridor kama alivyokaisisi yeye,hasara iyo kaipata yeye,JK anachofanya kwa sasa ni kuvutia kwake kwa nguvu zake zote ili apate cha kukumbukwa na wakwere wenzake,kwani anajua fika kwa watanzania amefeli na hakuna atakaemkumbuka kama atavyokumbukwa kwao...
Shukrani sana...
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin
Heshima kwako Mkuu,nimekusoma kwa utuvu wa hali ya juu katika hilo bandiko lako la juu lililojaa uchambuz wa kina na wa hali ya juu,mimi sina mengi sana ya kusema,
Kwani mengi yameshasemwa sana,kikubwa kilichopelekea kufikia hali hii ni kama hiko ulichokisema "USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA ENEO HUSIKA"

Wananchi ama watanzania wengi wao tumekosa matumain na iman na serikali yetu hata pale inapokuwa na nia njema wakati mwingine kutokana na kukosa kwao uwajibikaji na uzalendo katika kusimamia rasilimali za taifa na madudu yao viongoz na wataalamu wetu katika kuingia kwao mikataba mibovu mibovu inayoliingizia taifa hili hasara kubwa,madeni na ugumu wa maisha kwa wananchi wa kipato cha chini,

Usishangae sana hili la bagamoyo,kwani Huyu Mkuu wa nchi anachokifanya sasa ni kuvutia kwake,ni mwamba ngoma mwenye nguvu za ziada kwa sasa ndan ya taifa hili,na unyonge huu tulionao watanzania pamoja na kukosa kwa uzalendo kwa hao wanaomzunguka ndio kwa maana ngozi hii inawambwa kuelekea bagamoyo katika miaka miwili hii ya kumalizia muhula wake,
Potelea mbali na ni hasara yake yule Chinga Mkapa kama yeye alidhani kwamba JK akija atakuja kuendeleza Plan ya Mtwara Corridor kama alivyokaisisi yeye,hasara iyo kaipata yeye,JK anachofanya kwa sasa ni kuvutia kwake kwa nguvu zake zote ili apate cha kukumbukwa na wakwere wenzake,kwani anajua fika kwa watanzania amefeli na hakuna atakaemkumbuka kama atavyokumbukwa kwao...
Shukrani sana...

ndugu yangu na kaka yangu THE BIG SHOW shukrani za dhati zikufikie kwa kutoa maoni yako juu ya post yangu.

hapo bold pamenifanya niwaze kitu cha tofauti kabisa na hapa nitaomba mnisahihishe. Hivi kila rais anayekuja madarakani huwa anakuja na priorities zake sio??Lakini je huwa hatakiwi pia kuvipa vipaumbele miradi iliyo asisisiwa na seniour wake??

nashindwa kuelewa na niliposoma bandiko lako #266 niliogopa kuuliza hivi ni ipi sababu ya Mtwara corridor kutokuisha??
sijui kama rais anapokuja madaraka huwa anakuja na washauri wapya kama ndivyo basi nisishangae kuona Mtwara corridor haijaisha, lakini kama washauri wa raisi hubaki wale wale nikiwa namaana kwamba ni watu wanaoajiriwa na katibu mkuu kiongozi sion sababu ya watu hawa kuwa waoga kumshauri rais juu ya kumalizia miradi iliyoachwa pending

lakini pia hebu tuhoji hizi Ilani za uchaguzi ambazo vyama vya siasa huwa inazitoa je huwa zina lenga nini hasa?? manake kwa staili ya utendaji wa serikali iliyko madarakani napata picha kwamba ilani hizi ni political themes ambazo ni ngumu kuwa implimented na hivyo kumfanya rais awajibike pasi action plan.

sasa kama kikwete anaondoka mwaka keshokutwa inamana hilo swala la bandari ya bagamoyo litafia hapo sio?? na mradi wa EPZE nawenyewe sio?? haya sasa ndio matumizi mabaya ya madaraka ya rais. ndo maana napenda hata kwenye katiba mpya tumpunguzie madaraka rais na action plan awe anapewa na katibu mkuu kiongozi na sio na chama chake.
 
Last edited by a moderator:
ndugu yangu na kaka yangu THE BIG SHOW shukrani za dhati zikufikie kwa kutoa maoni yako juu ya post yangu.

hapo bold pamenifanya niwaze kitu cha tofauti kabisa na hapa nitaomba mnisahihishe. Hivi kila rais anayekuja madarakani huwa anakuja na priorities zake sio??Lakini je huwa hatakiwi pia kuvipa vipaumbele miradi iliyo asisisiwa na seniour wake??

nashindwa kuelewa na niliposoma bandiko lako #266 niliogopa kuuliza hivi ni ipi sababu ya Mtwara corridor kutokuisha??
sijui kama rais anapokuja madaraka huwa anakuja na washauri wapya kama ndivyo basi nisishangae kuona Mtwara corridor haijaisha, lakini kama washauri wa raisi hubaki wale wale nikiwa namaana kwamba ni watu wanaoajiriwa na katibu mkuu kiongozi sion sababu ya watu hawa kuwa waoga kumshauri rais juu ya kumalizia miradi iliyoachwa pending

lakini pia hebu tuhoji hizi Ilani za uchaguzi ambazo vyama vya siasa huwa inazitoa je huwa zina lenga nini hasa?? manake kwa staili ya utendaji wa serikali iliyko madarakani napata picha kwamba ilani hizi ni political themes ambazo ni ngumu kuwa implimented na hivyo kumfanya rais awajibike pasi action plan.

sasa kama kikwete anaondoka mwaka keshokutwa inamana hilo swala la bandari ya bagamoyo litafia hapo sio?? na mradi wa EPZE nawenyewe sio?? haya sasa ndio matumizi mabaya ya madaraka ya rais. ndo maana napenda hata kwenye katiba mpya tumpunguzie madaraka rais na action plan awe anapewa na katibu mkuu kiongozi na sio na chama chake.


Mkuu gfsonwin,nimefurahi kukusoma kwa mara nyingine tena,nafarijika sana...
Unajua kwa nchi za wenzetu,hizi tunazoziita dunia ya kwanza huwa wanavipaombele vya taifa ambavyo huwa haviyumbishwi na siasa zao,
Kwa mfano Bill clinton(Democrat) alipoiacha nchi ile kwa George Bush(Republican) na kisha G Bush kuondoka na kuiacha nchi hiyo hiyo tena Barack Obama wa Democrat hawatofautiani katika kusimamia vipaombele vya taifa lao,
Ima iwe ni uchumi,usalama na kadhalika,
Huku kwetu inashangaza sana,kila anaekuja huwa anakuja na sera zake na ajenda zake na kuacha kuangalia lipi ni la msingi na la kitaifa la kuliendeleza na lipi la kulipa muda,suala la Mtwara Corridor JK kalipuuza ili hali suala hili lilikuwa na umuhimu kitaifa na si kikanda,mwezangu yeye nadhan kaja kulichukulia kuwa sual hili chinga Mkapa alifanya katika kutafuta kujikomba na kuwasaidia wamachinga wenzake na sio taifa na ndio kwa maana hatushangai kwa yeye kulipuuza na kuhamishia akili yake kwao bagamoyo kwa kipindi hiki cha miaka miwili ilyobakia,najiuilza sana huyo rais ajaye atakuwa na misimamo ipi??sijajua kama atatokea CCM au la,

Ila kikubwa kinachonishangaza ni kwamba wenzetu hawa nchi zao hizi huwa wanabadilishana badilishana,
Msimu huu chama hiki,msimu ujao chama kingine,lakini linapokuja suala la national interests siasa na ubabaisha huwekwa kando na kufanya kazi,sasa hawa jamaa hupokezana vijiti wenyewe kwa wenywe,sasa najiuliza tatizo linatokea wapi??
Kwanini huyu anakuja kulipindisha la yule hali ya kuwa wote ni wamoja??na huwa wote kwenye meza moja za maamuz kichama na kiserikali??
Inashangaza sana kwa kweli...
 
Last edited by a moderator:
Ningeomba nizipitie hoja zenu kama zilivyonigusa.
Kutoka bandiko la MchunguZI #270 anasema ''Tume ya mipango katika ripoti zake miaka nenda miaka rudi imekuwa very optimistic na maendeleo ya mtwara and mentions potential areas, tourism industry, kilimo, forestry, ufugaji nyuki, uvuvi na VIWANDA, yakiwekwa bayana na tume ya mipango (serikali) basi ujio wa gesi ni fursa muhimu ya kutekeleza kwa vitendo;kwa kifupi - faida ya gesi kwa wanamtwara itakuwa na manufaa tu iwapo itajitokeza katika economic output ya mkoa na employment na haya yalenge katika value chain ya sekta ya gesi - exploration, extraction, production, transportation, storage, distribution, servicing, maintenance, legal services, well services, construction, power generation, engineering services etc;inawezekana kwa leo hakuna such skills lakini tukiwekeza sasa, mtwara can become the centre of excellence afrika mashariki na kati katika utaalam wa gesi within the next 25 years;"

Tume ya mipango imeweka mipango mara nyingi .Kuna mradi wa Mtwara Corridor uliokuwa kipaumbele, upanuzi wa bandari ya Mtwara unakuwa nyuma ya ujenzi wa Bagamoyo.
Mabomba yanalazwa haraka haraka bila hata ya kuongea kuhusu yale ya tume ya mipango! Wamtwara wakiuliza economic output as a result of value chain of gas exploration hakuna majibu. Hivi kweli hawana hoja?
gfsonwin nakuhakikishia kuwa hakuna EIA. Kuna ufungamano kati ya sera na vitu vinavyohusika kama EIA. Hivi tunavyoandika hakuna sera za gesi kuna draft sijui kama EIA Ipo.

Kwanini rais mmoja akija mambo yanabadilika, jibu ni kuwa hatuna institution bali personality(s).
Hivi hushangai waziri mkuu mwenye sera ya elimu anajiuzulu leo, kesho waziri mkuu mwingine anakuja na sera za kilimo kwanza!! leo Mtwara corridor kesho Bagamoyo kwasababu ya personality tu

THE BIG SHOW, wenzetu wana institutions, India waliwahi kukaa miezi 6 bila PM , UK wiki 3 hawana PM, Japan miaka 5 mawaziri wakuu 7 na maisha yanakwenda kwasababu institutions hazina uhusiano na personalities katika kutekeleza majukumu. Tena Kikwete anatetea hoja yangu pale aliposema 'waziri mkuu amejiuzulu nchi imetetemeka' please, aliyejiuzulu ni mtu siyo ofisi ya PM!!

Zinedine umesema haya
"What should be done for better realization of future dreams on the way towards middle income country". Je tuwe na optimistic view kwa Mtwara mpya na tanzania kwa ujumla ambayo 2025 inaweza kufikiwa?
Ukaongezeka kuwa CCM kuna tatizo ima la watu makini kukaa pembeni au kuaachwa katika maamuzi

Kwanza hali ya CCM sidhani kunasababu za kuamini kuwa ni chama cha siasa kama ilivyokuwa huko nyuma. CCM imebaki kuwa sehemu ya kuganga njaa na wala si sera ubunifu na uongozi. Ni ngumu kujua nani kaachwa nani kajitoa kwasababu it all about chaos, hakuna discipline wala leadership hence no vision no misssion. Mchambuzi atasita kidogo lakini nadhani kuna mahali tutakubaliana.

What should be done, well tujitambue kama wananchi, watanzania wenye commmon enemies i.e Ujinga, umasikini, maradhi na sasa Ufisadi. Halafu tujitambue kuwa maadui hao wanatushambuliwa kwsababu ya uanadamu.

Pili, ni lazima tuwe sehemu ya maamuzi yanayotuhusu. Tusikimbie au kuacha mambo kama siasa, na wale wanaoingia huko tuwakumbushe kwanini wanaingia huko, wametoka wapi na nini matarajio yetu kwao.

Tuwakatae wanaotuletea hadithi, hizi ni zama za delivery. Hivi tunapoambiwa mtu analeta maendeleo kwahiyo tumchague, maandeleo ni tangible things? maendeleo ni goods! kwanini tusiangalie rekosi ya mtu kwanza, weledi na wapi anasimamia.

Mfano, leo kuna wabunge mabubu kuhusu gesi Mtwara. Kesho wanarudi na kuomba kura halafu wanashinda.
Leo kuna afisa yupo Dar anasoma mikwaju na mikanda magazetini, kesho anateremka Mtwara anapewa Ubunge.Viongozi ni lazima waishi kama sisi na watufahamu, wafahamu interest zetu wasikilize tunataka nini

Muhimu tuache kugawanyika katika makundi kutokana na siasa, na siku hizi ujinga wa dini n.k.
Tunaogopa kusimama katika ukweli kwasababu za kisiasa au kidini.

Hawa wanaofaidika na 10% za gesi wanatumia udhaifu huo. Leo ukisimama kidete kuhusu hoja za Wanamtwara kusikilizwa kwanza unaonekana mpinzani.
Ukisema hakuna haki unaambiwa wewe si muumini. Kwamba gesi ya Mtwara ni ya madhebu na dini.

Tunachotakiwa ni kukataa ujinga wa kugawanywa, kusimama katika haki na kuunga mkono haki.
Kwanini tusiunge mkono watu wa Mtwara ili mikataba,sera na EIA n.k. viwekwe wazi?
Nani kasema Hospitali ya Ligula ikiwa na CT itakuwa ya wamakonde na Wayao peke yao?

Leo tunawaacha Wamtwara kwasababu tuliwaacha wa Nyamongo, Geita na Bulyamhulu.
Kesho tutawaacha wa Mchuchuma na Kiwira kwasababu tuna uzoefu wa kuwaacha wenzetu.
Kikundi cha watu wachache kinazidi kutumaliza eti kusimamia haki ya kujua haki yako ni uchochezi, eti ni ukorofi, udini na upinzani.

Tukifanikiwa kugoma kugawanywa na kusimamia haki hapo tutakuwa na jibu la swali la Zinedine.



 
Last edited by a moderator:
Zinedine bandiko lako #273 limenifanya nijiulize maswali makuu mawili hivi kwanini Bgamoyo?? huwa najiuliza sana sipati jibu kabisa. bandari mpya ijengwe Bagamoyo, EPZE ijengwe bagamoyo, barabara ya kwenda kaskazini ijengwe bagamoyo, hospitali kuu ya mkoa wa pwani ijengwe bagamoyo. hvi huko bagamoyo kuna nini??

ile evenly distruibution ya resources ipo kweli?? mbona siskii maeneo mengine jamani?? mbona singida siiskii kabisa?? ama wao hawaaitaji kufaidika na uwekezaji?? mbona tabora nako ama wao wabaki na asali tuuuuuuuu ambayo hata mnunuzi wa uhakika hakuna??

hii nchi inahitajika mapinduzi ya kifikra ya kikweli kabisa vinginevyo kuna watao neemeka zaid na wengine wabaki maskini kabisa.

Gfsonwin,
Hii hofu uliyonayo ni wengi wanajiuliza maswala ya namna hiyo. Hata hivyo mi naona pamoja na mengineyo nadhani uendelezaji wa Bagamoyo, Kisarawe(Chuo Kikuu cha Afya) na maeneo yaliyo karibu na Dar pia inachangiwa na hofu ya Serikali kutotaka kuhama Dar kwa vile kuna maslahi yao mengi hali itakayopelekea ku-collapse kwa vitega uchumi vyao. Ndio maana wanajaribu kuendelea kuwapo around Dar. Kigezo cha uenyeji wa mkuu wa kaya (hivyo huenda upendeleo) mimi sikipi asilimia kubwa sana kwa sababu haya tungeyatarajia zaidi Chalinze na maeneo ya karibu. Kwa hivyo uendelezaji wa kasi wa Bagamoyo pamoja na sababu unazojaribu kujenga lakini ni policy option ya ku-offload uwezo wa Dar katika kuhmili ongezeko la watu na uwekezaji na badala yake pawe kama na mji mdogo Bagamoyo (which is not bad). Hata hivyo nikubaliane nawe kwamba hili tatizo lipo na ni la muda mrefu, limefanywa na viongozi wengi na wanaendelea kulifanya (kuna visa vingi sana katika eneo hili hususana katika uendelezwaji wa Miundombinu ya Barabara, maji, hospitali, Umeme, mashule na mgawanyo wa makao makauu ya maeneo mapya). Ni tatizo hilohilo la unequal distribution of national cake ndilo linalojenga msingi wa madai ya wana Mtwara leo hii. Na limezidi kuwa tatizo kwa sababu, "some people are becoming better off by making other worse off". Na hiki ndicho kinachoonekana hapa leo. Watu wamekuwa "givances and greed" kwa kiwango cha juu sanakitu ambacho kitatupeleka kwenye tatizo la separatism(kudai kujitenga) na/au irredentism (kutaka wawe raia wa nchi jirani) ndani ya nchi yetu hususan maeneo yanayotengwa na mgawanyo wa keki ya Taifa yakiwa ni yale maeneo ya pembezoni (Mtwara, Ruvuma nk). Tuombe salama lakni tuendako ni giza zaidi.
 
Back
Top Bottom