Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

TUMEFIKAJE HAPA HADI KUALIKA FBI (Sehemu ya pili)



Inaendelea.......

Katika mazingira ya kawaida, wataalamu wa Tanzania wanaoifahamu kijiografia, kisiasa, kikabila, dini n.k. ndio walipaswa waongoze uchunguzi. Endapo tungekuwa na vyombo vya usalama vya miaka ya 70 na 80 nina hakika tungekuwa tunafahamu mengi zaidi ya tuyajuayo leo.

Ninashangaa eti serikali ya mapinduzi Znz impeiga maruku CD, DVD na kila kinachohusu uchochezi.
Huku bara nako kumekuwa na kamati za usuluhishi kana kwamba tatizo ni la waumini na si watu wachache.

Mbinu zote hizo ni dhaifu sana na zinaonyesha kiwango gani usalama wa taifa ulivyo njia panda.
Ningedhani uchunguzi ungefanywa na wataalam katika fani mbali mbali kuja na suluhu na si masuala ya kisiasa.

Kuzuia CD na DVD bila kuwashughulikia wanatoa maudhui, wanaotengeneza na kusambaza hizo DVC na CD ni kazi bure na ya kiwango hafifu sana.

Tatizo si DVD au CD, tatizo ni wale wanaotengeneza vitu hivyo kwa kushirikiana na wale wenye maudhui ndani ya vitu hivyo.

Kuwaita viongozi wa dini wazungumze ni njia nyingine dhaifu na ya ajabu sana ya kukabiliana na tatizo.
Viongozi wa dini hawana matatizo na wala waumini wao hawana matatizo.

Matatizo yapo kwa vikundi vya watu wachache ambavyo vimeteka ajenda ya dini na kuingizia hisia zao kwa ajili ya masilahi yao.

Sidhani kuwa kadinali Pengo anaweza kuzuia wendawazimu wachache wanaotaka kufanya uhalifu.
Sidhani kuwa sheikh mkuu anaweza kuzuia wendawazimu wachache wanaotaka kufanya uhalaifu.
Na wala sidhani kuwa kadinali na sheikh mkuu wametoa amri za vikundi hivyo kuendeleza chuki na fitna katika jamii.

Sasa kama hilo siyo, kwanini basi wao wabebeshwe mzigo wasiojua unatoka wapi na kwanani na unaelekea wapi?
Kuwaita wajadiliane ni upotezaji wa muda, ukosefu wa maarifa na umbumbu wa hali ya juu sana the least to say.

Nilidhani hili lilikuwa jukumu la idara ya usalama wa taifa siku nyingi sana.
leo wangeshakuwa na orodha ya watu wenye kunuia au wanaojipanga kufanya uhalifu.

Kazi yao ingekuwa kuchuja na kubaki na mashudu.
Eti hawajui na wanawaita FBI? Real! kwamba FBI wanawajua wadogo zetu zaidi ya sisi wenyewe.

Vyombo vya usalama vinahitaji modernity. Hizi si zama za kubeba bunduki au kufuatilia wanasiasa majukwaani.
Hizi si zama za kung'oa watu kucha au kutuma watu wakamtoe mtu jicho.
Kweli ndio usalama wa taifa? I mean serious!

Nabaki kusema vyombo vya usalama ndio tatizo, mabomu na risasi, mauaji, mateso na kiwacho ni matokeo ya ulegevu wa vyombo hivyo. Ni matokeo ya vyombo hivyo kuwa sehemu za ajira tu kwa watu kwavile wazazi au ndugu zao wanalindana na wala hakuna suala la utaalamu

Lingekuwepo basi wataalamu hao wangeshaiona hatari tuliyo nayo mapema sana na wala tusingefika hapa tulipo.
Lakini inatosha kuvilaumu vyombo hivyo?
Jibu ni ndio kwa vile vimebeba dhamana, na ni hapana kwasababu vinafanyakazi chini ya maelekezo ya serikali.

Ni kwa msingi huo viongozi wake ni wateule wa Rais na wanawajibika kwakwe.
Sasa vyombo hivyo vikishindwa kazi maana yake si kuwa vimeshindwa bali serikali imeshindwa kuvisimamia vifanye kazi tarajiwa.

Kwa msomaji wangu wa duru nadhani utakuwa umeelewa japo kwa uchache maana na dhana nzima ya kile ninachokiongelea

Tusemezane
 
DURU ZA SIASA ZA TANZANIA

PROF LIPUMBA HATAGOMBEA TENA UONGOZI WA NCHI
KAULI ZA MZEE MTEI ZAGEUKA KUWA SHUBIRI KWA CHADEMA

sehemu ya kwanza

Mwenyekiti wa chama cha CUF amenukuliwa na kuonekana katika video akihutubia katika msikiti mmoja maarufu Kariakoo

Katika maongezi yake Prof Lipumba ametoa maneno mazito na mengine yakiwemo mafumbo.
Prof alisema katika uchaguzi wa mwaka 2010 ''jahazi lilikuwa linazama'' na masheikh walihaingaika kulikwamua hata hivyo wamesahaulika.

Yeye akiwa mwenyekiti wa CUF haieleweki alishiriki vipi kuokoa jahazi lililokuwa linazama na nini yalikuwa matarajio baada yaku uokoa jahazi hilo. Haieleweki kuwa kulikuwa na ushirika wa CUF na CCM au yalikuwa ni mambo ya watu binafasi

Lipumba akadai kuwa yeye aliombwa kuchukua uongozi ili kutetea wanyonge na wala hakufahamu kazi hiyo itakuwa nzito na kumchukua muda mrefu kiasia hicho. Akadai kuwa waislam wanapaswa kuwa raia wa daraja la kwanza.

Katika madai mengine, prof alisema kada maarufu wa CHADEMA aliwahi kusema katika tume ya uchaguzi waislam walikuwa wengi na hiyo ikamlazimu rais abadailishe mfumo wa tume.

Prof Lipumba akadai kuwa ''wenzetu'' wanajipanga na ni wakati wao pia kujipanga pengine akimaanisha kuelekea 2015.

Tathmini ya duru za siasa:
Kwa hadhi na heshima ya Prof Lipumba maneno yake yanachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu sana.
Kwanza ni kwa weledi wake na pili ni kutokana na ukweli kuwa yeye ni mwenyekiti wa chama cha siasa, chama kilichowahi kuwa cha upinzani bungeni. Kwa mantiki,kauli zake haziwezi kutengwa na usomi au siasa za chama chake.

Kumbe ile ndoa ya CUF na CCM zanzibar haikuishia huko, hata huku bara kulikuwa na ndoa ya siri.
Kumekuwepo na madai kuwa CUF ni chama cha kidini na kwa kauli za mwenyekiti wake, hilo halina shaka tena.
Kinachosumbua akili ni kuona kuwa kumbe mbegu hizo chafu zimeota mizizi hadi ndani ya chama tawala.

CCM inajukumu la kusimamia amani ya nchi hii, ni chama kilichojengwa katika misingi ya kuwaunganisha watanzania na si kuwagawa na kama hilo lilitokea basi CCM imedhihirisha kupoteza mwelekeo,dira na misingi iliyokiasisi.

Chama cha CUF haraka haraka kimetoa kauli za kujitenga na matamshi ya mwenyekiti wake.
Jambo hilo limefanyika kwa kauli dhaifu kutoka kwa afisa wa chama.

Pengine aliyetakiwa kukemea kauli za Lipumba alitakiwa nguli Seif Sharif Hamad ambaye jina lake tu ni alama ya CUF. Kwabahati mbaya haikutokea hivyo pengine naye kuogopa kuudhi wanachama wake wasio rasmi katika kambi za kidini.

Hii maana yake ni kuwa CUF sasa imejidhihirisha kupoteza maana halisi ya chama cha kisiasa na pengine kuchukua hadhi ya tawi la CCM. Sitashangaaa kama kuna atakayeiita CUF CCM-B.

Kwa vile mwenyekiti wa CUF ametoa kauli nzito zinaoonyesha yeye kutokuwa tayari kuleta utangamano wa taifa, ni wazi kuwa Prof Lipumba amekata tamaa au ameahidiwa mengine na hataonekana tena katika kinyanga'nyiro cha uongozi wa taifa hili. Kauli zake tayari zimemuondolea sifa ya kuwa kiongozi wa taifa kwa hali yoyote na kwa sehemu kubwa ya jamii

Haitegemewi kuwa mtu anayetarajiwa kuwa kiongozi wa taifa aje na kauli za kuwagawa Watanzania kwa madaraja achilia mbali kuwa na mikakati inayoshabihiana na udini.

Jambo wasilotambua viongozi wa kisiasa ni kuwa katika nchi kama Tanzania hakuna mtu anayeweza kuwa kiongozi kwa kutumia mwamvuli wa dini. Ingawa haionekani kwa haraka, Watanzania wengi sana wanakereka na siasa za udini na hawa ndio huamua nani awe kiongozi wa nchi.

Duru za siasa tunadhani Prof Lipumba anaelewa jambo hilo vema, lakini kwasababu ameamua kutogombea uongozi wa nchi hii tena, sasa anatoa kauli ambazo hazimdhuru kisiasa.
Pengine anatafuta mahali pa kujiweka baada ya kuondoka katika uongozi wa nchi na siasa kwa ujumla.

Duru za siasa inasisitiza kuwa kauli za Prof Lipumba hazikuja kwa bahati mbaya, ni kauli za kuaga siasa na kutafuta mahali mbadala baada ya maisha ya kisiasa ingawa ni katika mmomonyoko wa maadili(lack of moral authority)

Prof Lipumba amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa taifa na amekipotezea chama chake hadhi na uhalali wa kuwa chama tawala.

Prof ameamua kustaafu siasa kwa kuacha makovu makubwa ndani ya CUF.

Leo kwa mtu mwenye weledi na fikra timamu itamchukua muda sana kufikiria kujiunga na CUF kwasababu tayari chama hicho kimepoteza maana ya chama cha siasa na kimepoteza kitu kinaitwa Diversity(mchanganyiko)

Kutokana na madai ya huko nyuma kuhusu CUF, Prof Lipumba amepigilia msumari wa mwisho tena wa moto katika ''jeneza' la chama cha CUF.

Hatuoni ni kwa vipi na njia gani CUF itajinasua na tuhuma za nyuma na hizi zinzotolewa na mlezi wa chama, mwenyekiti wa chama, msomi na profesa aliyebobea.

Lipumba anaondoka, je kaacha kovu gani ndani ya CHADEMA akishirikiana na Edwin Mtei?

Itaendelea.....
 
Inaendelea.....

sehemu ya pili.

Tumeonyesha ni kwa jinsi gani kauli za prof Lipumba zimekiumiza chama cha CUF.
Lakini pia kauli zake zimeunganishwa vema na kauli za Edwin Mtei, mlezi na Mwenyekiti wa CHADEMA.

Prof Lipumba amedai kuwa kiongozi mmoja wa chama cha siasa alitoa madai ya udini katika tume ya warioba kuhusu wakristo kuwa wachache ndani ya tume hiyo na hivyo kumlazimiu rais kubadilisha muundo.
Kwa maneno mengine alichokuwa anaonyesha ni nguvu ya imani fulani dhidi ya matakwa ya serikali.

Kwamba kauli hiyo iliyotolewa na Edwin Mtei haikuwa yake bali ya chama chake.
Kwa vile hapo awali tulisema kuwa kauli ya Lipumba si yake kwasababu yeye ni mwanasiasa(active) ni vema pia tukasema kauli ya Edwin Mtei haikuwa yake kwavile alikuwa ni mwasisi wa chama na Mwenyekti wa kwanza.

Hii maana yake kisiasa ni kuiweka CHADEMA katika spotlight kama ambavyo CUF imejidhihiri.
Tulimwambia mzee Mtei kuwa kauli yake itatumika kukiletea chama chake madhara mbele ya safari.

Tukamwambia kuwa kwa hali ilivyokuwa hakukuwa na uwezekano wa kupata wajumbe wa tume kutoka visiwani ili kuleta uwiano wa mambo ya dini.

Muhimu sana tuliamwambia kuwa tume ya Warioba si ya dini ni tume ya kutafuta muafaka wa kitaifa.
Bila kujali nani ana jina gani jambo la kuzingatia ni weledi wa wajumbe wa tume.

Tulimalizia kumweleza kuwa yeye akiwa kiongozi wa kisiasa mstaafu hakupaswa kutoa kauli ile na ingekuwa vema akaomba radhi au kukitenga chama chake na kauli zake binafasi.
Binafsi ninashukuru kuwa nilikemea jambo hilo awali kabisa

Kwa bahati mbaya hata CHADEMA hawakuonekana kuwa makini na kuji ''dissociate'' na kauli za mwasisi wao.
Leo tunaona kauli ile inavyoanza kutumiwa dhidi ya chama alichokiasisi mzee Mtei
Kisiasa hili ni kosa kubwa sana na sijui kama vyama vya siasa na wanasiasa vimejifunza kutokana na hilo.

Duru za siasa tunasema, kuna wakati viongozi wanatoa kauli kama kauli za vyama vyao.
Lakini pia viongozi hao wana haki kama raia wengine kutoa maoni yao bila kufungamana na siasa za vyama vyao.

Ni vema viongozi wa siasa wakawa makini sana wakati wanatoa maoni au kauli.
Kauli zao binafsi zinapaswa kuelezwa hivyo ili kuzitenganisha na kauli za vyama vyao.
Hili linakwenda mbali na kuwagusa wabunge pia.

Pamoja na hayo kuna kuwajibika kwa viongozi wa kisiasa.
Ni lazima wanasiasa wapime kauli zao kama zimelenga kuleta tija na muafaka wa kisiasa.

Ni jambo la hatari sana kiongozi kutoa kauli kwa minajili ya kuwafurahisha watu au wapiga kura wake.
Kiongozi mzuri ni yule anayesimamia anachokiamini, anayewaambia wafuasi ukweli hata kama ukweli huo unauma.

Social responsibility ni kitu muhimu sana hasa wakati huu taifa likiwa katika tension ya mambo ya udini.
Tunaelewa kila mmoja ana imani yake, lakini basi imani hiyo lazima iwe na mipaka.
Hautuwezi kuwa na taifa lililojengwa katika misingi ya tofauti za kikabila, imani au rangi.

Hakuna mahali popote dunia suala hilo limewahi kufanikiwa.
Si Rwanda ambako watu wamechinjana na sasa nchi imeanza kusimama kutoka katika majivu.
Hakuna mshindi bali maumivu makali ya historia.

Siyo Bosnia Herzegovina au kule India ambako imani zimewatenga watu.
Nigeria imekuwa katika machafuko yasiyoisha na hakuna mshindi wa vita ya kidini hadi leo.
Kinachoendelea ni kutoana roho kwa misingi ya dini zile zile zinazozuia kutoana roho!!!

Marekani bado kuna makovu ya ubaguzi wa rangi na hilo linabaki kuwa donda kubwa lisilopona.
China kuna mvutano usioisha kati ya wachina na akina Dalai Lama.

Mifano ni mingi sana ya kuonyesha kuwa kuwagawa wananchi na nchi kwa misingi ya ukabila au dini hakujaweza kufanikiwa popote pale duniani achilia mbali kuwa na tija kwa jamii husika.

Duru za siasa tunawaasa viongozi wa dini na siasa waangalie matamshi yao kama yanalingana na maandiko au yana tija kwa jamii. Yanapotokea machafuko kama kule Liberia, Cameroon, au milipuko ya Bali, Boston, New York, Misiri, Syria, Irag, Afhanistan na kwingineko hakuna aliye salama. Si viongozi au wachochchezi watakaokuwa katika amani.

Lakini pia wananchi wanajukumu muhimu sana, nalo ni kutambua kuwa katika machafuko ya aina yoyote wao na watoto wao ndio waathirika wa kwanza.

Tumeona jinsi wazee na vikongwe, wakina mama na watoto wakitembea km zaidi ya 100 kwa miguu kutafuta amani na mahali pa kusitiri nafasi zao.

Hayo yanaonekana na tunayashuhdia kwa macho yetu.
Nadhani Mwenyezi mungu anatupendelea kwa kutufundisha kwa mifano inayoonekana.
Sisi hatuoonekani kujifunza na itakapofika wakati kila mmoja atasaga meno, atajuta na kusema ningalijua.

Kabla hayo hayajatimu tuchukue hadhari na hatua za mapema kabisa.
Hatua hizo ni kuwakataa wote wenye malengo ya kutufarakanisha kwa misingi ya dini au ukabila

Wao wanapesa Uswiss kwa mamilioni. Talaa linatokea lisilotarajiwa tayari watoto wao wanaosoma huko nje kwa pesa zetu watawatafutia wazazi wao makazi ya kukimbilia.

Swali ni kuwa wewe na mimi tutakimbilia wapi ikiwa hata hapo nchi jirani hatujawahi kukanyaga?

Tusemezane
 
RASIMU A KATIBA YA TANZANIA

Katika duru za matukio, jambo kubwa linalozungumzwa kwa sasa ni uzinduzi wa rasimu ya katiba mpya ya nchi.
Ingawa uzinduzi umefanyika na mchakato unaendelea, duru za siasa matukio zinasimama na kauli ya awali kuwa mchakato wa katiba haukuzingatia misingi ya utunguji wa katiba. Hilo litabaki hivyo na duru inaamini hivyo.

Katika uzinduzi huo wa rasimu, rais JK hakuwepo kwasababu bado yupo ziarani.
Kwa tukio zito linalogusa masilahi makubwa ya taifa ni jambo la jabu mkuu wa nchi kutokuwepo.

Killichofanyika ni rais kuondoka ili kutoa picha kuwa yeye hahusiki na mambo ya utungaji wa katiba.
Hata pale ambapo tunajua anahusika, bado serikali imeendelea kuwafanya watanzania kama majuha.
Kama rais asingehusika basi asingetangaza ratiba nzima ya kupata katiba mpya.

Jaji Warioba ametoa muhatasari wa kile kilichopo ndani ya rasimu huku akisema rasimu nzima itapatikana katika tovuti ya tume ya katiba. Hadi sasa hakuna kitu kama hicho na wananchi katika mitandao wamebaki wakijadili muhtasari.

Haieleweki kunatatizo gani lakini ni wazi kuwa hilo limefanyika kwa makusudi kabisa ili kupima kimo cha maji na jinsi gani wananchi watapokea muhtasari huo. Kuna hisia za kutosha kuhusu hili.

Kwanza, tume imepewa pesa na nyenzo za kutosha ambazo ni pamoja na wataalam wa IT.

Pili, Jaji Warioba ametoa muhtasari akiacha mambo muhimu sana.
Mfano, suala la Uraia halikuongelewa kuwa tume imependekeza nini.
Suala la rais wa muungano na upatikanaji wake nalo pia halikuongelewa na hivyo ni vigumu kujadili chochote.

Hizi zote ni hila zinazofanywa na tume ya Warioba ambayo kimsingi na kimantiki ni ngumu sana kusema ipo huru.
Ni tume hiyo imepuuza maoni ya wananchi kuhusu rais kuondolewa kinga kwasababu ya kuingiliwa.

Hili ni katika kuwalinda viongozi waliopita na waliopo kwasababu ya madhambi makubwa waliyo nayo.
Tume haizingatii umma unataka nini bali inazingatia masilahi ya watu wawili watatu

Hayo si matakwa ya tume ni maelekezo pengine kutoka kwa wahusika.
Ndio maana tunasema suala zima la mchakato wa katiba lina mizengwe na haionekani kama kuna katiba ya dhati.

Ni wazi katika zama hizi ambazo chama chake cha CCM kimepoteza uungwaji mkono, zipo hila na njama za makusudi za kuchomeka mambo kinyume cha matakwa ya wananchi.

Pamoja na hayo kile kilichopo kitajadiliwa kama kilivyo kwasababu viongozi wa Tanzania wanapoukodolea macho mkate ni ngumu sana kuwabadili, watalazimisha hata hatari na kuita mafanikio.

Kwasasa ni ngumu sana kujua nini hasa kimeandikw yapo mambo ambayo Watanganyika wanapaswa kuyaangalia kwa macho mawili. Tunasema Watanganyika kwasababu hii ni katiba yao na kwabahati mbaya wzn hawajulikani wanataka nini.

Kuelekea katika uchambuzi wa rasimu tungewashauri Watanganyika waangalie mambo yafutayo
1. Sula la Uraia.
Ni muhimu sana hasa tukienda katika mashirikiano ya kimataifa. Katika ukanda wa Afrika mashariki ni Tanzania peke yake mtu anaweza kupata Uraia kama kupata cheti cha Daktari. Ni ngumu sana kupata Uraia kwa wenzetu kwasababu wao wametanguliza utaifa.

Lakini pia ni muhimu sana kwasababu hilo ndilo litaamua mustakabali wetu na wznz.
Wazanzibar wanatautaka Uraia wa Tanganyika ili wakamilishe haja zao hata kwa kujua kuwa Mtanganyika hawezi kupata uraia wa kwao.Wanachotaka hasa ni kutumia uraia katika kujimilikishia ardhi, ajira, mikopo kama ya elimu n.k.

Inaendelea.......
 
Inaendelea.......
Ni muhimu kuangalia namna huyo Rais wa Jamhuri ya muungano atakavyopatikana.
Itakuwa ni kituko kama rais atachaguliwa kwa kuangalia zamu za upande mmoja.

Ukweli unabaki kuwa wznz hawaonekani kujua wanataka nini.
Wakati tunaandaa taifa kwa awamu nyingine kama zilivyokuwa za miaka 50 iliyopita duru itashangaa sana kuukabidhi uongozi wa nchi kwa watu wasio na mapenzi na Watanganyika.

Hakuna sababu ya kupata kiongozi kwa kuangalia uzanzibar wake.
Hawa ni watu chini ya lakini tano kwasababu waliobaki wanaishi Tanganyika.
Ni kituko cha kutaka kupata kiongozi kwa kuangalia jina la sehemu.

Kuna ushahidi kuwa viongozi wa znz hasa waliberali hawataki Watanganyika.
Yanini basi wakabidhiwe uongozi wa nchi yetu?

Suala lingine ni kuangalia kati ya yale mambo 7 yaliyoamuliwa ni vipi Tanganyika itanufaika na gharamazake zitakuwaje kwa kugawana na wala si uwiano.

Tunasema si uwiano kwasababu znz ilikuwa na wajumbe sawa na Tanganyika na imepewa hadhi sawa kama Tanganyika katika majadiliano.

Sasa kwanini basi kusiwe na usawa katika mambo mengine?
Itanishangaza sana kama Watanganyika watakubali kubeba gharama kwasababu znz ni ndogo kieneo na idadi ya watu.
Ingekuwa hivyo wasingedai usawa wa tume.

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia na kujiuliza. Kwa mfano wapi thamani za taifa zilijadiliwa.
Haiwezakani tume ije na mambo ambayo wananchi hawakupata fursa ya kuyajadili.

Lakini pia ni lazima tuangalie ni namna gani viongozi wamejiwekea kinga ili kuendelea na uhalifu kama tunaoushuhudia.
Haiwezekani Jaji mkuu ateuliwe na rais? Kwanini Jaji mkuu awajibike kwa Rais? Kwanini .

Halafu inabidi tutupie macho mambo mengi muhimu kama yahusuyo uchumi n.k.

Ujumbe wangu ni kuwa mchakato mzima ni wa ubabaishaji lakini katitka ubabaishaji huo ni makosa kukaa pembeni.
Tutaendelea kutoa mawazo na kusema tukitambua kuwa huu ni ubabaishaji
Hakuna kisicho na mwisho na wala hakuna dola iliyowahi kushinda nguvu za umma.

Jambo moja la muhimu ni kuweka itikadi za kisiasa, kidini na kikabila pembeni na kuaiangalia rasimu kama dira na urithi tutakaowaachia watoto wetu.

Tutangulize Utanganyika na pengine ni wakati sasa tuwaunge mkono wzn katika jitihada zao za kuondoka.
Hakika uwepo wao unaathiri sana nijadala yetu na katika athari hizo hakuna tunachopata kutoka kwao.

Hivyo tujikite kuijadili Tanganyika ya kesho, tuikinge na unyonywaji rahisi na tuijengee ramani ya kudumu.

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3 heshima kwako...

Haiwezekani ukadai NCHI huru iliyo na mamlaka kamili halafu wakati huo huo uwe ndani ya kitu kinachoitwa Serikali ya Muungano.. hapa tunaweweseka tu pengine kwa kuogopa mzimu wa Mwalimu Nyerere utatushukia kwa hasira.

Suluhisho hapa ni kuwa na Zanzibar huru (kama wanavyotaka) na Tanganyika (Tanzania Bara au vyovyote vile tutakavyoiita) huru halafu tutafute namna nyingine ya kushirikiana nao kama majirani zetu. Lakini tusidanganyane kwa hili koti ya MUUNGANO ambalo kwa hakika sasa limepauka, limetoboka na halitutoshi tena!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 heshima kwako...

Haiwezekani ukadai NCHI huru iliyo na mamlaka kamili halafu wakati huo huo uwe ndani ya kitu kinachoitwa Serikali ya Muungano.. hapa tunaweweseka tu pengine kwa kuogopa mzimu wa Mwalimu Nyerere utatushukia kwa hasira.

Suluhisho hapa ni kuwa na Zanzibar huru (kama wanavyotaka) na Tanganyika (Tanzania Bara au vyovyote vile tutakavyoiita) huru halafu tutafute namna nyingine ya kushirikiana nao kama majirani zetu. Lakini tusidanganyane kwa hili koti ya MUUNGANO ambalo kwa hakika sasa limepauka, limetoboka na halitutoshi tena!
Nakubalina nawe kabisa kuhusu hili. Hakuna namna ambayo Mtanganyika ataweza kumridhisha mzanzibar.

Nimeangalia rasimu ya katiba hakika Tanganyika itabeba mzigo mzito sana.
Mzigo wa kuendesha serikali ya Muungano
Mzigo wa kuendesha serikali ya Tanganyika.

Serikali ya muungano ni kubwa sana na gharama zote atazibeba Mtanganyika.
Hivi znz isiyoweza kuplipa umeme inawezaje kuchangia gharama za JMT ambayo ni kubwa sana.

Shughuli za serikali washirika zinaratibiwa na tume maalum ili zilingane na matakwa ya JMT.
Hapo ni udanganyifu wa hali ya juu sana. Hii yote ni kuwapa wzn unafuu pale watakapo kwama.

Nauliza kila mara, hivi inawezekanaje znz yenye mapato ya bilioni 120 kwa mwaka na ambayo ina pengo la bajeti la bilioni 510 zinazolipwa na Tanganyika ili iweze kukidhi bajeti yao, leo iwe na uwezo wa kuchangia bajeti ya JMT ambayo kwa kadirio dogo sana si chini ya trillioni 2. Nani anayefidia hilo pengo.

Lakini kibaya ziaidi ni kuhusu uwiano. Mathalan,bunge la JMT litakuwa na wabunge wa mikoa wakati znz watatoka katika wilaya.
Nani anagharamia wabunge hawa na kuna uwiano gani wa mkoa na wilaya kwa idadi ya uwakilishi.

Nazidi kuiangalia rasimu lakini ni wazi kuwa akina Profesa Baregu ambaye ni msomi aliebobea, Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa mkamu wa rais na wenzao 'wamewasaliti' Watanganyika. Kuwabebesha gharama ni 'usaliti'

Duru za siasa tunaangalia rasimu kwa undani na tutachambua kipande kimoja hadi kingine.
 
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI Y MUUNGANO WA TANZANIA

Duru za siasa series; (1)

Ndugu wana duru, rasimu ya katiba imezinduliwa na Jaji Warioba juzi.
Ni rasimu hiyo (draft) ndiyo itakayofanyiwa kazi kupata katiba ya kudumu ya Jamhuri wa muungano.

Kuweka kumbu kumbu sawa, sisi duru za siasa tulikataa uundwaji wa tume ya Warioba.
Kwavile rasimu hiyo imeshaletwa duru itakuwa inaleta mtiririko wa vipengele ili kuonyesha usahihi au upotofu wa katiba kwa minajili ya kuwaeleza wananchi kile wanachokijadili, manufaa na athari zake kwa maisha yao.

Duru ilikataa uundwaji wa tume ya Warioba kwasababu zifuatazo.
1. Kwanza ni kuchelea kuwa hilo lilikuwa takwa la rais JK na wala si la serikali au chama chake
2. CCM ipo katika rekodi za kukataa katiba mpya kwani iliyopo inawapa nafasi kuliko vyama vingine
3. Hiyo ilikuwa agenda ya wananchi na wao ndio walipaswa kuamua utaratibu wa kupata ktiba uwe vipi
4. Serikali ambayo ni mdau wa katiba haipaswi kuongoza mchakato wa kupata katiba bali kusimamia taratibu

5. Utaratibu wa kupata katiba una mlolongo mkubwa
a)kwanza mjadala wa kitaifa kama ipo haja ya kuwa na katiba mpya na kwanini
b)Mjadala wa taifa kuamua tunataka kujenga taifa gani na kwa njia gani
c)Mkutano wa kitaifa wa makundi mbali mbali kleta muafaka wa kile tunachokitaka
d)Utaratibu wa kupata tume na kupewa hadidu za rejea na wananchi
e)Kuundwa kwa tume na kupewa muda wa kukamilisha hatua zitakazofuata
f)Kuandikwa kwa rasimu ya katiba na kupitiwa na wananchi
g)kuundwa bunge huru la kikatiba
h)Kupigiwa kura ya maoni ya kukubali au kukataa katiba.

Hayo hayakufanyika na tume ya haraka haraka ikaundwa. Pengine ilikuwa kuchelea kuwa wananchi watakapodai kwa kupitia vyma vya siasa huenda likaathiri sana taswira ya uongozi wa CCM

Pia kulikuwa na hofu ya kuachia mchakato huo uendelee kwa taratibu zinazokubalika kungeweza kuhatarisha mambo ambayo CCM na serikali wanadhani ni yao na wala si ya taifa.

Ni kutokana na makosa hayo ya haraka haraka leo hii rasimu imeanza kwa matatizo.
Wale wanaoipongeza hakika hawajaipitia au hawajaona matatizo makubwa yaliyomo.

Katiba ni chombo kinachotoa muongozo ambao utazaa sheria na taratibu zingine za nchi na hivyo haipaswi kuwa na utata hata kidogo. Tatizo la utata litapelekea kutokea:

1. Mgogoro na migogano ya kikatiba
2. Mwananchi kushindwa kuielewa na hivyo kushindwa kujua au kutatizika na haki zake
3. Vurugu na hata maparaganyiko wa taifa.

Kwa kuanzia tutatoa mfano mmoja ambao rasimu inaonekana kulichanganya taifa.
Muungano: Hili ni tatizo kubwa na lilisubiri rasimu kutoa mwelekeo.
Rasimu haionekani kulieleza tatizo zaidi ya kulikuza.

Kwanza, ilitakiwa kuwepo na muafaka wa kitaifa(angalia 5(b na c) hapo juu.
Ni kupitia mijadala hiyo wananchi wangekubaliana kama muungano uendelee au ufikie kikomo.
Kama ni kuendelea, je ni mfumo gani utumike.

Rasimu imekuja na muundo wa serikali 3, ya muungano, Zanzibar na Tanganyika.
Ni kwa njia gani tume iliweza kujua kuwa wananchi wanahitaji muungano?

Kilichotakiwa kwanza ilikuwa ni kura ya maoni na hasa kwa zanzibar ambayo inaona inaonewa.
Kama wangekataa basi suala la muungano lingekaa pembeni na kila mmoja kuendelea kwa wakati wake.
Kama ingekubalika basi kinachofuata ilikuwa kuamua ni aina gani ya muungano unatakiwa.

Inaendelea...
 
series(1)
Inaendelea.....

Kwakuruka hatua muhimu tume imekuja na serikali 3, Serikali ya muungano haina katiba, serikali ya Tanganyika haina katiba, na zanzibar wana katiba.

Kinachofuata ni kurudi kwanza kwa Tanganyika halafu iwe na katiba ndipo mshirika wa pili apatikane.
Hii ilitakiwa kuwa hatua za awali kabisa kama mjadala wa kitaifa ungefanyika kama tulivyoeleza hapo juu.
Hili ni kosa kubwa kimantiki kwasababu serikali ya muungano imezaliwa na mzazi mmoja, halafu ikazaa mtoto!

Kwa ufupi pamoja na tatizo la tume kutofuata taratibu bado kuna makosa ya kiufundi.

Sehemu ya kwanza ya rasimu 1(i) Jamhuri ya muugano wa Tanzania ni shirikisho la Tanganyika na Zanzibar.
3(2)(a) Sikukuu za kitaifa; Siku ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 desemba 1961

Kwa kuanzia ni kuwa rasimu imetambua uwepo wa Tanganyika kama mshirika wa muugano.
Baada ya hapo Tanganyika haitajwi tena kama Tanganyika bali Tanzania bara.
Ibara zote ziliofuata zimeonyeshakuwa mshirika wa muungano ni Zanzibar na Tanzania bara.

Hapa tayari kuna tatizo.
Tatizo ni kuwa Tanganyika iliyotajwa kama nilivyoonyesha imebadlikaje ghafla na kuwa Tanzania bara?

Na kama tuna Tanzania bara kwanini tusiwe na Tanzania visiwani?
Nasema hivyo kwasababu hakuna kitu kinaitwa Zambia Mailand, Uganda Mainland au Kenya Mailand.

Kwahiyo Tanzania kuwa Manland ni kwa kuwa kuna Zanzibar Island.

Endapo tume imeamua kuhifadhi jina la zanzibar basi jna la Tanganyika lirudi kama ilivyo ili tuwe a Jamhuri ya muungano wa Tanzana. Jina la Tanzania bara lisitumike na kama litatumika basi litumike likiwa na Tanzania visiwani

Lakini mumhimu ni kujiuliza tukiacha tume nani mwingine aliyewahi kuulizwa au kutakiwa kutoa maoni kuhus majina ambayo ni fahari ya utaifa ?

Na je, taerhe 9 desemba tutakuwa na sherehe za uhuru wa Tanganyika kama ilivyosemwa 3(2)(a) au Tanzania bara kama ilivyotajwa zaidi ya mara 20 katika rasimu?

hii ni kuonyesha utata unapoanzia, tutaendelea kuchambua kipengele kimoja hadi kingine.

Kinachofuata katika series (2)
Thamani za taifa
Muundo na ukubwa wa serikali ya muungano
Uwiano na usawa katika shuguli za muungano
Gharama za muungano.

Itaendelea
 
SERIES: 2

Rasimu ya katiba mezitaja tunu za taifa (national treasure)
zifuatazoa (a)utu;(b) uzalendo;(c)uadilifu;(d)umoja;(e)uwazi;(f)uwajibikaji; na(g)lugha ya Taifa.


Tume ya warioba ilipokuwa inajadili maoni, sikuwahi kusikia tunu za taifa zikitajwa.
Kuna uwezekano makundi maalumu yalitaja hata hivyo kwa raia wa kawaida hilo ni suala geni kama si kutolifahamu kabisa na lilipaswa liwekwe wazi na kwa kipaumbele

Nashawishika kusema dhana ya tunu imetoka katika tume au maagizo ya serikali au inawezekana Ni jambo zuri kwasababu kila taifa lina tunu zake.

Tukiziangalia kama zilivyo Uzalendo, umoja, utu na lugha vinaweza kuwa tunu za taifa.
Uwajibika, uwazi na uadilifu hizo sina hakika kama ni tunu za taifa.
Hivyo ni vitu vya lazima kwa kila mwanadam sijui kama taifa kwanini tuvione ni tunu.

Tunu za taifa ni kitu au vitu vinavyofanya utaifa (nationalism) na vitu hivyo ni vya kipekee ambavyo taifa inavyo kama sehemu ya tamaduni zake au fahari(proud) ya taifa

Uzalendo, umoja na lugha ya kiswahili kwetu vinaweza kuwa tunu.
Tumekuwa taifa moja na tumesimama pamoja.

Kiswahili kama lugha yetu inayobeba tamaduni zetu hata kama ni tofauti ndivyo vitu tunaweza kusema ni tunu za taifa.

Mtaifa mengi yamekuwa yakitumia vitu hai au visivyoishi wakiwemo wanadamu kama tunu zao za taifa.Tunu za taifa inaweza kuwa majengo, thamani (artifacts), wanyama, watu, miinuko na miundo ya nchi, nyaraka.Kwa ufupi ni vitu vinavyofanya utambulisho wa utaifa fulani.

Nitoe mifano kidogo, Uingereza Malkia ni tunu kwao, wimbo wao wa taifa 'god bless our Queen/king au bendera yao ya taifa ''union jack'' hizo kwao ni tunu.

Ukitaka kuona waingereza wanungana ni pale vitu hivyo vitakapokuwa mbele yao.

Pengine ungeniuliza ni zipi tunu za taifa, mimi ningekwambia lugha ya kiswahili, mbuga za wanyama,mlima Kilimanjaro na umoja wetu.
Kila mmoja hutaja japo kimoja ya hicho anapouliza Tanzania ina nini au utofauti gani na eneo jingine. Mambo niliyotaja ndiyo ''unique'' na hakika thamani zetu.

Uwazi, uwajibikaji na uadilifu hizo hazijawahi kuwa tunu zetu na wala hazikidhi ukweli kuhusu taifa letu.Hizo ziondolewe na tunu za taifa ziangaliwe upya.

Rasimu haijakidhi tunu za taifa kama tutakuwa sahihi na neno hilo tunu ambalo kwa kiingereza ni national treasure.

SERIKALI YA MUUNGANO
Tunajadili serikali ya muungano kwasababu ni tatizolinaloonekana katika siasa za nchi na Ni muhimu kwakuzingatia mipango mingi inayofuata ndani ya rasimu.


Tutaendelea kuangalia vipengele kwa kwa uhumi wake. Kwasasa tuangalie muungano.

Inaendelea......
 
Inaendelea.......

Muungano na muundo wake:
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu ambazo nia) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na (c) Serikali ya Tanzania Bara.

Katika sehemu ya kwanza ya rasimu 3(2)(a)(c) Tanganyika imetajwa.
Ghafla katika muundo wa muungano Tanzania bara imeingia. Tumeeleza wasi wasi huu huko nyma kuwa jambo hilo lina utata. Je, wananchi wa Tanganyika walipendekeza wabaki kama Tanganyika au Tanzania bara. Ni lazima watakuwa wamesema pale walipopendekeza serikali 3 kama ilivyosema tume. Swali ni kuwa tume imepataje jina la Tanganyika sehemu moja ya rasimu na Tanzania bara sehemu nyingine?

(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
naa) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano

Mambo ya muungano
1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
3. Uraia na Uhamiaji;
4. Sarafu na Benki Kuu;
5. Mambo ya Nje;
6. Usajili wa Vyama vya Siasa; na
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na
mambo ya Muungano

Tume huru ya uchaguzi:
77.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano,

92(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitozidi kumi na tano

Katiba imetoa nafasi 15 za mawaziri na hivyo tunategemea kuwa na wiizara si chini ya 12, manaibu mawaziri 15 au zaidi kwasababu hawakuwekewa kiwango, na makatibu wakuu 15 au zaidi ikiwa ni pamoja na manaibu wao.

Kilichowekwa hapo si muundo kamili wa serikali ya shirikisho ni sehemu tu kwa minajili ya mjadala.

Tumeona uwepo wa serikali za washirika ambazo zitabeba majukumu ya nchi zao kwa mujibu wa taratibu zao.

Katika mambo yaliorodheshwa kuwa ni ya muungano yote ni huduma za jamii na hakuna jambo linalotoa au kuzalisha kipato hata moja.

Serikali ya muungano haina mapato kutoka kodi bali kutegemea mapato na ruzuku kutoka katika serikali za washirika. Kwa maneno mengine serikali ya muungano haina chanzo cha mapato lakini inahitaji matumizi katika sehemu kama tulizoorodhesha hapo juu.

Hii maana yake ni kuwa serikali washirika zitatakiwa kuchangia uendeshaji wa serikali ya muungano. Tukiangalia gharama za sehemu moja kama bunge au mahakama ni wazi kuwa serikali ya Zanzibar haitamudu kugawana gharama.

Haiwezi kumudu kwasababu eneo kama la ulinzi na usalama bajeti yake ya mwaka ni zaidi ya trilioni 1.2 ikiwa ni mara 2 ya bajeti ya znz

Mapato ya serikali ya Zanzibar kwa 2012/2013 ni bilioni 120 kiasi kisichoweza kuendesha hata tume ya uchaguzi kwa nusu mwaka.

Tanaganyika iatabeba gharama zote za kuendesha serikali ya muungano.
Wakati huo huo itakuwa na jukumu la kuendesha serikali yake.
Rasimu haitaji gharama za uendeshaji kwa kutambua kuwa hilo litawaudhi Watanganyika.

Kibaya katika rasimu hii kuhusu muungano ni kuwa umetoa haki nyingi sana kwa Zanzibar kutumia rasilimali za Tanganyika hata kama Watanganyika hawatatumia zao.
Rasimu imewalinda na kuwaepusha na gharama za uendeshaji.

Tatizo litakalojitokeza ni kuwa Rais wa muungano hatakuwa na nguvu na Rais wa Tanganyika atakuwa na nguvu kwasababu yeye ndiye anayebeba muungano huku Rais wa znz akionekana kama msadizi.

Litakuwa jambo la kushangaza kama Watanganyika watafumba macho na kukubali kubeba gharama za kuendesha serikali kuu. Gharama hizo Tanganyika imezibeba kwa maika 50 katika matusi na sasa ni wakati wa kugawana mzigo wa kubeba.

Kama ZNZ imepewa nafasi za uwiano na hadhi ya mshiriki sawa wa muungano, ushiriki wake katika gharama utatoka wapi?
Kwanini rasimu haielezi jambo hilo na kuwaficha Watanganyika.

Series 3 tutaangalia
Muundo wa serikali ya muungano na
Tutaangalia, Tanganyika ilipaswa ije kwanza halafu rasimu ya muungano au kinyume chake
Madaraka ya rais

itaendelea......
 
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

KIKAO CHA CC YA CCM
Awali tuwatake radhi kwa kukatiza mtirirko wa kuiangalia rasimu kama ilivyosemwa hapo juu.
Ni kutokana na habari za kikao cha kamati kuu ya CCM kujadili rasimu na umuhimu wa kikao hicho.

Tukumbuke suala la katiba halikuwepo katika ilani ya uchaguzi ya CCM na wala kujadiliwa katika ngazi zozote za chama. Kama tutakuwa sahihi rais JK alitoa tamko la kuanza mchakato katika hotuba za mwezi na hakuna mahali aliponukuu kikao cha chama. Tunachokumbuka ni kuwa ilikuwa ajenda ya wananchi na wapinzani

Uundwaji wa tume ya Warioba ulikwenda kwa kasi sana kiasi cha kukiuka hatua za lazima katika kuandika katiba kama tulivyowahi kuzieleza huko nyuma.

Hofu kubwa ilikuwa ni kuhusu wapinzani na wananchi kuichukua ajenda hiyo na hivyo kuhatarisha mambo ambayo CCM inayajua kuwa ni ya kulindwa kwa masilahi yao.

Hata pale tume ilipoundwa mswada ulikwama bungeni na ukapitishwa kwa nguvu nguvu tu.
Hii ni wazi kuwa tume iliundwa kwa makusudi kadhaa na hapo ndipo tunasema mchakato una dosari.

Inashangaza kuona CC ya CCM sasa inataka kutoa tamko kuhusu rasimu.
Rais aliwahi kuchukua majukumu ya tume kwa kutangaza ratiba nzima ya shughuli za tume wakati mchakato wa kukusanya maoni unaendelea si kama mwenyekiti bali mkuu wa seriali.
Ni kujidanganya kudhani kuwa CCM haijui nini kilichomo ndani ya rasimu na kwasababu gani.

Ni kujidanganya kwasababu tangu lini ajenda ya mtu binafsi(Raisi iliyoinyakua) ikageuka kuwa ajenda ya chama tena bila kuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi wa chama?

Kikao kinachokaa jumatatu kujadili rasimu si kwa ajili ya kutoa msimamo wa chama kama ilivyoelezwa na wakuu wa chama. Kikao hicho ni cha kurekebisha mambo kwasababu ni wazi '' watu wamenawa'' kabla ya chakula kutengwa.

Kuna nadharia mbili zinazotokana na kikao hicho.

Nadharia ya kwanza
Kikao kitajadili namna ya kuunda serikali ya Tanganyika, taratibu za kuiunda na namna gani ya kuwaeleza wananchi.
Kikao kitapendekeza tume ya Warioba itumie maoni yake katika kuandaa rasimu ya serikali ya Tanganyika na hivyo kujigeuza kuwa sehemu ya tume ya Tanganyika, au kuwekwa watu watakaochukua maarifa ya kupandikizwa kutok tume ya Warioba.

Hii inatokana na ukweli kuwa kwavile rasimu imeshatoka na Watanganyika wanahoji mambo mengi hasa gharama za serikali ya muungano, utaifa wao wa Tanganyika na pengie kutaka kuondoa mambo zaidi ni vema kuwazuia mapema.

Kwa kukusanya maoni mara ya pili, kuna uwezekano Watanganyika wakakataa huo muungano na hapo haifahamiki nani atawalazimisha kwasababu rasimu haina nguvu na wala Tanganyika haina kiongozi au sheria.
Ili kuepuka tatizo hilo kikao kitatoka na msimamo nilioutaja.

Nadhria ya pili
Ni kutaka kuonyesha ulimwengu kuwa hata CCM wana concern na rasimu hiyo na hawakubaliani nayo hivyo kuipa tume uhalali wa kuwa huru hata kama kuna ushahidi wa kutosha kuhusu rais kuingilia shughuli za tume kama kutangaza ratiba.

Kazi ya kikao itakuwa kuunda mkakati wa wananchi kukubaliana na rasimu hiyo baada ya kuanza kuonekana huenda ikakumbana na upinzani huko mbeleni.
Tutanarajia kusikia kuwa CC imeridhika na rasimu na hivyo kuanza kuwahamasisha wananchi kuiunga mkono.

Katika nadhari hizo, jumatatu tutasikia matamko ya kisiasa ya kupendeza au kupindisha mambo kwasababu serikali imeshafanya makosa ya kuweka mkokoteni mbele ya farasi(cart before the Hose).
Udharura wa kikao hicho ni kujaribu kuepusha matatizo hasa linalohusu uundwaji wa serikali ya Tanganyika.

Uundwaji wa serikali ya Tanganyika ndio hasa unaumizakichwa. Kwanza mchakato wake unaweza kuzuia tume ya Warioba kuendelea na kazi kwasababu lazima kwanza Tanganyika irudi halafu ndio katiba rasmi ya muungano ipate uhalali.

Kurudi kwa Tanganyika kunaweza kuleta mambo yasiyotarajiwa.
1. CCM inaweza kushindwa kudhibiti wimbi la mageuzi linalofukuta na hivyo kujikuta kikiwa na wakati mgumu sana.
Upo uwezekano wa vyama kama Chadema na CUF au vingine vidogo kutoa idadi kubwa ya wabunge katika serikali ya Tanganyika na hivyo kuwa kikwazo kwa mambo mengi

2. Wananchi wa Tanganyika wanaweza kugomea rasimu wakaitaka kufahamu ndani ya muungano wanafaidika na kitu gani
3.Migongano ndani ya CCM inaweza kutoa kiongozi ambaye si miongoni mwa wananchama wa chama ''vanguard' na hilo linaweza kuleta mtafaruku.

Hoja kubwa inayosumbua ni kuwa ili rasimu ipate uhalali na nguvu lazima kwanza serikali ya Tanganyika irudi.
Hakika hii ndiyo iliyokuwa iwe hatua ya awali kwasababu sasa hivi washirika wa muungano wangekuwa wanajadili kuhusu rasimu kwa usawa.

Sasa Tanganyika itajadili rasimu yake kwa kuangalia rasimu ya muungano jambo ambalo ni kuwanyima haki Watanganyika. Pengine walikuwa hawataki muungano, lakini wafanyeje?

Hayo ndiyo mambo yanayoiumiza serikali na CCM kwa ujumla. Ni masuala ya ufundi ambayo haieleweki kwanini manguli wa katiba ndani ya tume hawakuweza kuyaona na kuyazuia.

Wakati tunasubiri jumatatu, tutaendelea na kuangalia vifungu vya katiba.
Jambo moja tuliloliona ni kuwa znz itakuwa katika wakati mgumu kwasababu mambo mengi wanayoitegemea Tanganyika yameondolewa kiufndi sana na itabidi baadhi ya mambo wapige magoti, ingawa Tanganyikaitaendelea kubeba zigo la gharama..

Tusemezane
 
RASIMU YA ATIBA

Tumejiuliza mara nyingi kuhusu ukubwa wa serikali ya Jamhuri ya muungano na kuona kuwa vyombo viufatavyo vitakuwa ni sehemu ya Jamhuri wa muungao.
1. Bunge. 2)Serikali.3)Mahakama 3)Ulinzi na usalama. 3)Mambo ya nje 4)Vyama vya siasa 5)Benki kuu
6)Uraia na uhamiaji 7)Ushuru wa mapato yasiyo ya muunagano.

Hata kama serikali shirikishi zimepewa uwezo na rasimu kuanzisha vyombo vyao katika mambo hayo bado kunahitajika huduma na bajeti ya kuendesha yale ya muungano. Hii maana yake ni kuwa bajeti ya muunagno bado itakuwa kubwa kwa hesabau zozote.

Mambo yote yalitotajwa kusimamiwa na muungano ni huduma za jamii pengine ukiacha benki kuu tu.
Yaliyobaki ni huduma zinazohitaji ruzuku au mapato.

Imeandikwa katika rasimu kuwa mapato yatatokana na vyanzo vifuatavyo(Sura ya 14 (215)
1. Ushuru 2)maduhuli yataokanyo na shughuli za muungano 3)michango kutoka kwa washirika wa muungano 4) Mikopo kutoka ndani na nje ya jamhuri ya muungano.

Tunaposema ukubwa wa serikali tunaangalia 1)matumizi vs mapato 2) tunaangalia michango ya washirika wa muungano kama ilivyoelezwa hapo namba 3.

Tumeona kuwa vyanzo vya mapato ni vidogo kulinganisha na matumizi.
Kikubwa zaidi ni michango ya washirika wa muungano.
Pengine bajeti ya muungano na gharama zote isingeonekana kama washirika wangekuwa sawa kiuchumi.

Hatujui kanuni gani itatumika kuchangia muungano kutoka kwa washirika kwasababu tukichukua kitu kimoja tu kama ulinzi na usalama tayari gharama zake zinakaribia trilioni 1. Sasa uchumi wa Zanzibar ni nusu ya hapo,vipi itaweza kuchangia bajeti ya ulinzi.

Hatakama ZNZ itapewa ichangie robo ya ulinzi na usalama hiyo itakuwa bado ni mzigo mzito kwasababu bado itakuwa na majukumu ya kuchangia sehemu nyingine na jukumu la kuendesha serikali yake. Vipi basi gharama hizo zitalipiwa!!!!

Hadi hapo ni wazi kuwa Tanganyika itabeba mzigo mzito sana. Pengine tuwaulize watu wa tume watoe ufafanuzi. Kwa hali ilivyo Mtanganyika atamnyeka sana katika kugharamia shughuli za muungano.

Tuangalie znz imepoteza nini katika serikali muundo uliopenekezwa!
Inaendelea......
 
Inaendelea......

Kwa upande wa zanzibar, malalamiko yamekuwa kupata uhuru wa kuamua mambo yao.
Katika kufikia lengo hilo wao wamependekeza iwepo serikali ya Tanganyika.
Mara zote wamekuwa wanataka Tanganyika irudi halafu wakae meza moja kama wabia sawa.

Hilo sasa limetokea, cha kujiuliza ni kuwa ubia sawa utapatikana kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano!

Wakati CUF wakilalamika na kuitaka serikali ya 3, duru za siasa tuliwashauri wafikirie uamuzi huo kwa makini kwasababu kuna sehemu kubwa sana watapoteza.

Rasimu imetoa uwezo wa serikali washirika kuanzisha mambo yao yasiyokuwa ya muungano.
Jeshi la Poisi litakuwa na jeshi la serikali washirika (Sura ya kumi na tano,232).
Kwa maneno mengine znz iakuwa na jeshi lake la Polisi litakalohudumiwa na SMZ na si kama ilivyo sasa.

Elimu ya juu: Si katika mambo ya muungano. Mwaka jana serikali ya muungano ambayo ilichangiwa na Tanganyika kwa asilimia 99 ilidhamini wanafunzi wa elimu ya juu znz wapatao 1000 huku serikali ya mapinduzi ikidhamini wengine 800. Sasa SMZ itabeba mzigo huo kwasababu si suala la muungano tena.

Nishati: Si suala la muungano. Huko nyuma znz imelalamika kuhusu gesi na mafuta na hakika yameondolewa. Lakini sasa znz lazima iwe tayari kulipia gharama za umeme kwasababu Tanganyika haitakuwa tayari kupoteza mapato yake.

Ardhi: Suala la ardhi halimo katika mambo ya muungano.
Hilo nalo pia itabidi liangaliwe na kila mshirika wa muungano kwa masilahi yake.

Baraza la mitihani: Hili nalo ni jambo lililokuwa linaleta mzozo. Kwasasa si la muungano na hivyo znz iina baraza lake ambalo litahudumiwa na SMZ.

Utumishi na Ajira: Ukiacha nafasi za utumishi na ajira za muungano, kila mshirika atakuwa na namna yake ya kutengeneza na kulinda ajira. Kwahiyo ile nafasi ya znz kutumia mwanya wa muungano kwasasa hivi haitakuwepo na wzn wa chini wataumia sana.

Mali asili na utalii: Hili halipo katika mambo ya muungano, kwahiyo Tanganyika itakuwa na fursa sawa kama znz katika kukuza utalii na matumizi ya mali asili zake. Kitakachofuata ni suala la ushindani na znz itakuwa katika wakati mgumu.

Mapato: Si suala la muungano na kila mshirika atakuwa na mamlaka yake ya mapato.
Kutokana na hali hiyo ushuru na tozo za kodi zitakuwa wajibu wa kila mshirika.
Wafanyabiashara wa znz watakuwa na wakati mgumu kuingia katika soko la Tanganyika.

Bandari na mamlaka za anga: si muungao tena na hivyo kila mshirika wa muungano itabidi aendeshe kwa njia za kibiashara. Uwepo wa bandari kama inayojengwa bagamoyo hakutoi nafasi nzuri kwa znz.

Hii ni orodha fupi tu kwa minajili ya majadala.
Sasa zipo hoja kuwa kama uraia na uhamiaji ni sehemu ya muungano basi kuna mambo kama umiliki wa ardhi, utumishi n.k zitampa mzn nafasi ya kupumua. Apparently ni hivyo lakini kwa kusoma katiba vizuri kuna kikwazo cha kiufundi. Hebu tukiangalie

Inaendelea.......
 
Tuendelee tulipoachia hapo juu.....

Tumeona kwa uchache sana mambo ambayo si ya muungano na jinsi yatakavyoiathiri Zanzibar kiuchumi.Pengine hoja ni kuwa hakutakwa na tatizo kwasababu uraia ni suala la muungano na linatoa fursa kwa raia wa pande mbili kushiriki shughuli za upande mwingine kama ilivyoelezwa hapa : Sura ya tano (1) Mtu ambaye,kabla ya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri
ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Tanzania

Na pengine yupo atakayefarijika na uwepo wa tume ya mashirikiano ya serikali washirika kama ilivyoelezwa hapa: Sura ya tisa104(b) kusimamia, kuratibu na kuhakikisha kwamba kuna kuwiana kwa sera na sheria za Washirika wa Muungano katika masuala yasiyo ya Muungano.

Mtu huyo pia aangalie kifungu hiki kama kinamsaidia :
Sura ya sita (62.)-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote
juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka
hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano nanmshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawakwa ajili ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano

Hapa maana yake ni kuwa sheria itakayombana Mtanganyika kule Zanzibar basi itambana Mzanazibar Tanganyika

Lakini basi anayedhani mambo yatakuwa rahisi kiasi hicho hasa kwa mzanzibar inabidi asome vifungu hivi : Sura ya sita (61)-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni
Tanzania Bara na Zanzibar.Sura ya tisa(2) Mamlaka ya kutunga sheria katika Tanzania Bara na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanzania Bara na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar

Halafu hitimisha na kifungu hiki: Sura ya tisa(2) Mamlaka ya kutunga sheria katika Tanzania Bara na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanzania Bara na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar

Technically inaonekana madai ya Zanzibar yametimizwa katika kutafuta ubia sawa wa muungano kama inavyoelezwa hapa Sura ya sita (5) Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano

Ukweli ni kuwa Zanzibar sasa inalazimika kuwa na mambo katika uwiano huo huo wa ubia sawa. Tumeona jinsi serikali za washirika zilivyopewa nafasi katika maamuzi ya mambo yasiyo ya muungano.

Kwa uhakika hakuna kitu ambacho tunaweza kusema uwepo wa serikali 3 umeikomboa znz. Tunasema hivyo kwasababu ni wazi Znz badala ya kupumua itabidi iwe inapiga magoti kwa tume ya mashirikiano kila asubuhi.

Sehemu kubwa ya utegemezi ukiacha wa serikali ya muungano sasa umekwisha.
Fursa za wznz nazo zimezidi kubinywa kwa kuwapa uhuru zaidi huko kwao na si Tanganyika.
Hatuna hakika kama wznz walioona tatizo kabla ya kurukia hoja za serikali 3.

Kwasasa wanaongelea kuhusu mkataba. Sasa haiewlewi katika mambo 7 yapi wasiyoytaka tena na kwanini basi watake mkataba na wala si kukazania kuvunja muungano?

Tutaendelea...





 
Mkuu Nguruvi3, hongera sana kwa kazi pevu ya kuichambua na kuijadili rasimu ya katiba; kabla sijaenda mbali, ningependa kujua - je, ni sahihi kwamba washiriki wa muungano ni Tanzania Bara na Zanzibar? Kwanini isiwe Tanganyika na Zanzibar? Kwa maana nyingine, serikali ya tatu inayopendekezwa ni ya Tanzania bara au Tanganyika? Serikali ya Tanganyika in practice imeendelea kuwepo tangia muungano uanzishwe 1964 na imekuwa ikongozwa na rais wa JMT; Kwa maana nyingine, mambo yote yasiyokuwa ya muungano (ya TANGANYIKA)yamekuwa chini ya rais wa JMT kwa miaka 49 huku pia akisimamia masuala ya muungano; nachojaribu kueleza hapa ni kwamba kuna kiini macho cha miaka 49 cha serikali tatu huku rais wa JMT akiwa ni kiongozi wa Tanganyika ambayo anaitumia kuongoza serikali ya muungano na ya zanzibar kwa gharama kubwa sana; baada ya wajanja kuliona hili, kiini macho sasa kinapatiwa ufumbuzi lakini kwa kuendelea kumkataa mzazi wa Tanzania (Tanganyika) kama serikali kamili kama alivyotambulika chini ya hati na sheria ya muungano, na badala yake anaitwa Tanzania bara chini ya katiba mpya, jina ambalo Tanganyika alibatizwa rasmi chini ya katiba ya 1977; Kwanini basi na zanzibar asiitwe Tanzania visiwani, ili awe sawa na mwenzake Tanzania bara? Hauwezi mwacha mzazi mmoja wa 1964 aendelee na jina lake (Zanzibar) huku mzazi mwenza (Tanganyika, yeye akibatizwa jina lipya la Tanzania bara;Zanzibar chini ya katiba ya JMT 1977 walifutwa na kupewa jina jipya - Tanzania visiwani lakini wakagundua kiini macho husika na kupigania jina lao lirudi kwa mujibu wa katiba kwani lina implications kubwa katika kujitawala kisiasa, na kiuchumi na kijamii; Inawezekana sijaeleweka katika hoja yangu hii lakini kwa mwelewa, suala hili lina implications na pia complications kubwa sana kwa suala zima la serikali tatu ijayo; nauliza tena, rasimu ya katiba inatambua washiriki wa muungano kama zanzibar na Tanzania bara? Kama ni sahihi, basi hili ni tatizo kubwa, hatuta tatua kero za muungano zilizopo bali kuhairisha tu matatizo;
 
Mkuu Nguruvi3, hongera sana kwa kazi pevu ya kuichambua na kuijadili rasimu ya katiba; kabla sijaenda mbali, ningependa kujua - je, ni sahihi kwamba washiriki wa muungano ni Tanzania Bara na Zanzibar?

Kwanini isiwe Tanganyika na Zanzibar? Kwa maana nyingine, serikali ya tatu inayopendekezwa ni ya Tanzania bara au Tanganyika?

Serikali ya Tanganyika in practice imeendelea kuwepo tangia muungano uanzishwe 1964 na imekuwa ikongozwa na rais wa JMT; Kwa maana nyingine, mambo yote yasiyokuwa ya muungano (ya TANGANYIKA)yamekuwa chini ya rais wa JMT kwa miaka 49 huku pia akisimamia masuala ya muungano; nachojaribu kueleza hapa ni kwamba kuna kiini macho cha miaka 49 cha serikali tatu huku rais wa JMT akiwa ni kiongozi wa Tanganyika ambayo anaitumia kuongoza serikali ya muungano na ya zanzibar kwa gharama kubwa sana; baada ya wajanja kuliona hili, kiini macho sasa kinapatiwa ufumbuzi lakini kwa kuendelea kumkataa mzazi wa Tanzania (Tanganyika) kama serikali kamili kama alivyotambulika chini ya hati na sheria ya muungano, na badala yake anaitwa Tanzania bara chini ya katiba mpya, jina ambalo Tanganyika alibatizwa rasmi chini ya katiba ya 1977; Kwanini basi na zanzibar asiitwe Tanzania visiwani, ili awe sawa na mwenzake Tanzania bara?

Hauwezi mwacha mzazi mmoja wa 1964 aendelee na jina lake (Zanzibar) huku mzazi mwenza (Tanganyika, yeye akibatizwa jina lipya la Tanzania bara;Zanzibar chini ya katiba ya JMT 1977 walifutwa na kupewa jina jipya - Tanzania visiwani lakini wakagundua kiini macho husika na kupigania jina lao lirudi kwa mujibu wa katiba kwani lina implications kubwa katika kujitawala kisiasa, na kiuchumi na kijamii; Inawezekana sijaeleweka katika hoja yangu hii lakini kwa mwelewa, suala hili lina implications na pia complications kubwa sana kwa suala zima la serikali tatu ijayo; nauliza tena, rasimu ya katiba inatambua washiriki wa muungano kama zanzibar na Tanzania bara? Kama ni sahihi, basi hili ni tatizo kubwa, hatuta tatua kero za muungano zilizopo bali kuhairisha tu matatizo;
Mkuu Mchambuzi, ukiangalia hapo juu bandiko 189, nimeuliza hivi kwanini tuwe na sherehe za Uhuru wa Tanganyika desemba 9 1965 wakati huo sehemu ya rasimu ikiitambua kama Tanzania bara! Sehemu ya kwanza 3 (2)((a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
DisembaNikahoji kuwa kama rasimu inatambua Tanzania bara, neno bara linakuwepo kwa sababu kuna visiwani na hivyo yapasa kuwa na Tanzania visiwani. Nimeuliza hivi kuna nchi inayoitwa Zambia mailand, Uganda Mainland au Malawi Mainland.Kwahiyo mainland inatokana na ukweli kuwa kuna island.

Zanzibar wamebaki na utaifa wao wa Zanzibar, hakuna sababu kusiwepo na utaifa wa Tanganyika kama ilivyosemwa hapa katika rasimu : Utangulizi(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

Na pia 1.-(
1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru

Jina Tanganyika limetajwa mara 9 katika rasimu na Tanzania bara mara 48.
Rasimu inachanganya mambo lazima utaifa wa Tananyika uwepo ili kuondoa sintofahamu

Tume ya Warioba inahofia kuwa kuondoa neno Tanzania katika washirika kutaunguza nguvu za Jamhuri ya muungano na pengine kuongeza pengo linaloonekana sasa la utaifa.

Hata hivyo dhana hiyo ni potofu kwasababu Zanzibar kama wanataka utaifa wao na Mtanganyika anataka wake. Sasa ikifika wakati wa uraia kila mtu atasema ni mtanzania lakini wa eneo kadha.

Tume ilifanya makosa hapo mwanzo. Tumeeleza katika mabandiko ya awali kuwa, Warioba na wengine walikubali tu kubeba mzigo wasiojua ndani kuna nini.

Walirukia hatua za mwanzo wa utungaji katiba na sasa wanarudi nyuma.
Katika hali hiyo lazima warejee na kuwaeleza Watanganyika utaifa waouko wapi.

Katika kujichanga, sasa ndio wanakwenda ''kumzaa'' mtoto Tanganyika.
Mtoto ana mzazi mmoja halafu anatakiwa akue haraka ili wazazi hawa wamzae Jamhuri ya muungano ambaye tayari yupo. Unaona jinsi mambo yalivyokuwa messed up!

Tanganyika itabidi itengeneze katiba yake kwa kuangalia katiba ya muungano ili asije kinzana nayo. Wakati huo huo Zanzibar alikuwa na katiba wakati ya muungano inaundwa na hivyo ya muungano ilimwangalia zanzibar na sasa Tanganyika inamwangalia muungano! mess up

Mtanganyika hawezi kusema lolote kuhusu yale mambo 7 hata kama hakubaliani nayo kwasababu rasimu inamlazimisha akubali. Hata kama asingependa kubeba mzigo sasa ataubeba kwasababu tayari keshaambiwa aubebe. Mess up!

Sasa kujibu swali lako, rasimu ya katiba haimtambui Mtanganyika au Mtanzania bara, inatambua chotara ambaye hana jina. Haimtambui Mtanganyika kwasababu Tanzania bara imetajwa mara 48, Tanganyika mara 9, huyu ndiye chotara ninayemuongelea.

Tunataka tume ya Warioba ieleze, kufuatana na article ya union utaifa wa Tanganyika ulikoma wapi na lini. Rasimu inatambua uwepo wa Tanganyika, sasa huyu Tanzania bara katokea vipi na wapi katika rasimu hiyo kiasi cha kutajwa mara 48.

Tume itueleze Tanzania bara ametokea wapi. hilo ni muhimu sana kwasababu rasimu itapigwa chini mapema sana. Kuna matumizi ya fedha yasiyokidhi haja.

Na hapa Tungemwalika mh Zitto kwasababu yeye ni pro-3 gov na ameandika paper kuhusu jambo hili.


 
RASIMU YA KATIBA

Kuna mambo yamejitokeza katika rasimu inayojadiliwa. Moja ya mambo hao ni suala la Ardhi
Wengi wameshangaa kwanini ardhi ambayo ni msingi mkubwa sana wa maendeleo ya jamii halikuzungumziwa katika rasimu

Tukumbuke kuwa katika masuala yaliyokuwa na manung'uniko ni pamoja na hilo la ardhi.
Suala hilo ni zito si kwa muungano tu hata katika shirikisho la EAC.
Nchi wanachama wa EAC walishinikiza kwa bidii sana suala la ardhi liwe la jumuiya na kwamba umiliki wake uondolewe vikwazo.

Tunakumbuka serikali ya Tanzania ilivyolazimika kulitolea ufafanuzi na hadi leo limeachwa kuwa ni suala la nchi husika.
Katika ukanda wetu Tanzania ndiyo yenye ardhi kubwa na yenye kufaa kilimo na shughuli nyingine kuliko majirani zetu.

Hata Znz ina tatizo hilo na kadiri siku zinavyokwenda mbele ndivyo tatizo linavyozidi kuwa kubwa kwa ongezeko la watu.
Hivi karibuni znz ilishindwa kuchoma ngano kwa kukosa eneo na kuingia kwa wawekezaji katika sekta utalii kumezidi kuwabana wanachi masikini ambao wengi wanahamia Tanganyika.

Ni kwasababu za uhaba wa ardhi, Zanzibar imekuwa katika migogoro na Tanganyika.
Tunakumbuka jinsi Watanganyika waliokuwa wanafanya shughuli zao znz walivyochomewa vibanda vyao na wazanzibar kwa chuki ya ardhi

Ingawa inasemwa sababu ilikuwa ni kueneza uchangudoa, ukweli unabaki kuwa mbona ni znz hiyo hiyo yenye mashoga wengi na hakujaonekana hatua kama walizochulkuliwa Watanganyika za kuwachomewa vibanda vyao na wao wenyewe.

Kumewekwa sheria za ardhi za znz ambazo ni mahusi kwa ajili ya kumzuia Mtanganyika kufidika na rasilimali hiyo.
Juzi rais wa znz amezindua baraza la mahakama ya ardhi ikimaanisha kuwa tatizo hilo linachombo maalum cha kushughulikia nje ya muungano na kwa masilahi ya znz.

Watanganyika wamekuwa wanajiuliza ni kwanini basi wznz waje na wafadike na rasilimali yao ya ardhi bila masharti au unyanyaswaji wa aina yoyote. Kwahiyo hilo limekuwa ni nung'uniko kwa Watanganyika.

Lakini pia tukumbuke kuwa mafuta na gesi ambayo yanapatikana ardhini si masuala ya muungano.
Kwahiyo umiliki wa ardhi ni sehemu ya umiliki wa mafuta na gesi. Hili nalo wznz wamekataa kuwa suala la muungano.

Kwa mantiki hiyo suala la ardhi halimo katika yale 7 ya muungano.
Hii maana yake ni kuwa suala hilo litashughulikiwa na serikali za washirika.
Tanganyika itaweka taratibu zake za umiliki wa ardhi na Znz pia itakuwa na zake.
Hivyo ieleweke kuwa Ardhi si suala la muungano na hivyo rasimu haikulitaja bali litatajwa katika rasimu ya washirika wa muungano.

Kama kutakuwa na makubaliano miongoni mwa serikali za washirika basi makubaliano hayo lazima yawe na sheria sawa kama tulivyoona vipengele vyarasimu hapo juu.

Kwa upande wa Tanganyika hili ni suala zuri na pengine wangeliacha kama lilivyo. Linawawezesha Watanganyika kuamua namna ya kutumia ardhi yao wenyewe.

Tutaendelea.......
 
Tumekuwa na mfululizo wa mabandiko ya rasimu ya katiba. Tutaendelea kuingalia kwa vipengele zaidi.
Kutokana na matukio mengine leo tutaangalia matukio ya wiki hii duniani.

NSA MAREKANI: KUVUJA KWA SIRI ZA USALAMA MAREKANI

Tukio lilianza kwa habari zilizoandikwa na mgazeti ya Marekani na ulaya kuhusu kuvuja kwa siri inayohusu kuingiliwa kwa mawasiliano ya wananchi wa marekani kama simu na internet.

Tukio hili lilipewa uzito kwasababu linaonekana kupingana na katiba kuhusu uhuru na usiri(privacy)ya wananchi.

Mara nyingi serikali ya Marekani imekuwa inakataa kuwa haifanyi kitendo hicho bila sababu na kwamba zipo sheria zinazoruhusu serikali kupata habari kwa kupitia mashirika makubwa kama Google na yale ya simu.

Marekani ina wakala wapatao 16 wanaofanya kazi kwa niaba ya serikali. Swali likabaki nani amevujisha siri hiyo ya kuchunguliwa wakati wa mawasiliano.

Kitendawili kiliteguliwa wiki hii baada ya mtu aliyefanya hivyo bwana Edward Snowden kufanya mahojiano na gazeti la the guardian la Uingereza akieleza kuhusu kukerwa kwake na tabia ya kuingilia mawasiliano inayofaywa na serikali.
Kwa wakati huu Snowden anaishi nchin Hong Kong na aliondoka marekani wiki 3 ziliziopita

Snowden alikuwa ni mfanyakazi wa chombo kimoja cha usalama. Amedai kuwa yeye hakuwa na sababu za kuuza au kutoa siri za nchi yake kwasababu kama ni kufanya hivyo basi angeweza kuingilia mawasiliano hata ya rais wa Marekani.

Mshahara wake ulikua ni dollar 200,000 kwa mwaka akiishi maisha mazuri.

Wataalam wa mambo ya usalama wanasema madai ya Snowden kuhusu kuingilia mawasiliano yana mipaka na si rahisi kama anavyotaka ulimwengu uamini.

Kitu kimoja kinachowasumbua Wamarekani kwa sasa ni ukweli kuwa hakuna anaejua Snowden amebeba mzigo gani kuhusu usalama wa taifa lao.

Snowden anasema aliamua kutorokea Hong Kong kwasababu ni eneo analoweza kupata hifadhi.
Hata hivyo kuna ushirikiano kati ya Hong Kong na Marekani kuhusu kurudisha watuhumiwa ''extradition''.
Kwasasa ameondoka hotelini na hajulikani alipo.

Snowden alikiri kuwa kama CIA wanamtafuta mtu,basi wana uwezo wa kumpata kwa wakati muafaka.
Inawezekana amekimbilia china kwa ajili ya usalama zaidi.

Kutoa siri za nchi kutoka vyombo vya usalama si jambo geni Marekani.
Miaka ya 70 bwana Christopher Boyce alitoa siri za makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon na kuhukumiwa jela miaka takriban 10. Tofauti na Snowden, Boyce alibaki Marekani kutetea kile alichokiona si sahihi.

Hilo ndilo linamtofautisha na Snowden ambaye kama kweli ni mzalendo basi hakupaswa kukimbia nchi yake.Jamii imeganyika kuhusu usaliti au ushujaa wake huku wengi wakisema kitendo hicho pamoja na kuwashtua kuwa walikuwa wakisikilizwa lakini bado kinahatarisha usalama wa nchi.

Mpango wa kuingilia mawasiliano ulianza wakati wa Bush na unasemwa kuongezeka zaidi wakati wa Obama ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi. Kisiasa tukio hili haliwezi kumtia Obama katika mgogoro wa kisiasa kwasababu mpango huo unaungwa mkono na Republican ambao hasa ndio waliuanzisha.

Pamoja na hayo bunge la Marekani kupitia kamati ya usalama ya Congress na senate ya Marekani inajua kuhusu mpango huo. Hivyo Obama ana kinga nzuri na ndiyo sababu jambo lenyewe linaonekana kukosa nguvu za kisiasa zaidi ya zile za kiusalama.

Hatari anayokabiliana nayo Snowden ni kuhusu kurudishwa. Hilo inawezekana kwasababu ikifahamika yupo Hong Kong, Marekani naweza kufuta kumfutia uraia kwa kuzingatia kipengele cha mkataba wa kimataifa kuwa mtu anapokuwa katika nchi nyingine akafutiwa uraia basi hurudishwa katika nchi aliyokuwa raia.

Swali ambalo msomaji atauliza ni kuwa kama kunakipengele cha namna hiyo kwanini basi Tanzania isifute uraia wa mafisadi ili warejeshwe hapa nchini kukabiliana na mkono wa sheria?

Jibu ni jepesi kuwa mafisadi wengi nchini Tanzania wana urai wa nchi nyingine na hivyo kumfutia uraia hakutasaidia kwasababu bado atakuwa na uraia wa nchi nyingine.

Na zaidi ya hapo wengi wana uhusiano na viongozi wakubwa wa serikali na hivyo si rahisi masuala yao kushughulikiwa kama inavyopaswa.

Lakini pia kwa tukio hili lazima tujifunze kuwa usalama wa nchi ni zaidi ya silaha na maghala ya siasa.
Zama hizi za teknolojia kila kitu kipo katika mfumo wa dijitali kwahiyo siri za nchi ni rahisi sana kuibwa.

Je, vyombo vyetu vya usalama vinafanya kinachopaswa kufanywa ili kuhakikisha kuwa wenye dhamana ya usalama ni watu wanaoaminika na wanofahamika?

Kwa mwingiliano wa kikanda na kimataifa kosa moja katika usalama wa taifa linaweza kuigharimu nchi.
Ni muhimu sana ajira za nchi zikaangaliwa kwa macho mawili tofuti na hali ilivyo sasa

Tuangalie mashariki ya kati kwa ufupi......

Itaendelea..
 
MASHARIKI YA KATI UTURUKI NA SYRIA

Wiki hii kumekuwa na maandamano na ghasia katika majiji ya Istambul na Ankara nchini uturuki.
Ghasia zilianza kupinga ujenzi katika eneo la wazi (park).

Kwa bahati mbaya, kama zilivyo nchi nyingine za dunia ya pili au ya tatu, serikali ya waziri mkuu Recep Erdogan ikatumia nguvu kupambana na waandamanaji.

Katika sakata hilo waziri mkuu akaongeza chuki pale aliposema kuwa hayo walikuwa waporaji na si waandamanaji.Hali ilikuwa mbaya kwa ghasia katika nchi iliyokuwa na utulivu kwa kiasi ikilinganishwa na majirani zake.

Waziri mkuu Erdogan amefanikiwa katika kuleta amani hasa kuendeleza majadiliano na waasi wa Kurdish.
Chama chake cha kiislam chenye mrengo wa kadri kinaonekana kuwa na mafanikio ukilinganisha na serikali iliyopita.

Zipo habri kuwa waandamanaji walikuwa na chuki nyingine na wala haikuwa katika kiwanja hicho cha wazi.Wapo watu wa mrengo wa kulia na wale wa kushoto walioshindwa katika chaguzi na bwana Erdogan ambao wanamshambulia kwa njia mbadala.

Ikumbukwe kuwa hawa AK Party wanamsimamo wa kati na hivyo wenye misimamo ya mbali 'far left or right' wanaunganishwa na mazingira kuwa hawamtaki huyu wa kati na kati na wala siyo kuwa wao wanapendana.

Chuki nyingine inayosemwa ni kitendo cha Erdogan kuunga mkono juhudi za kuiondoa serikali ya Al asaad wa Syria madarakani.

Turkey inafanya biashara sana na Syria katika eneo la mashariki ya kati na uchumi wake umestawi sana pengine kuliko nchi nyingi za EU

Hata mafanikio ya Erdogan kuweka mfumo thabiti wa kifedha na kuzuia uchumi uliokuwa mahututi kutoendelea kuanguka, na hakika kuusimamisha vema nalo linakuwa ni sababu katika maandamano.

Hapa kuna tatizo la mashariki ya kati pamoja na ukweli kuwa yalikuwa maandamano ya kawaida ya wananchi wenye hasira zao. Hadi sasa kiwanja kimezuiliwa na Erdogan kuendelezwa na hivyo kutuliza ghasia kidogo.

Hatari kubwa ni hii ya kusambaa vita ya Syria katika nchi za ukanda wa mashariki ya kati kama ambavyo Turkey inaingia taratibu

Hivi karibuni wanamgambo wa Hezboulla chini ya Imam Hassan Nasrallah wamemsaidia Al Asaad na kuweza kuwarudisha nyuma waasi hata kukomboa baadhi ya miji.

Hezboullah wanafaidika na Syria kwasababu hiyo ndiyo njia ya kupitishia silaha zao kutoka Iran.
Uwepo wa utawala mpya utakuwa ni kikwazo cha silaha kufika Lebanon kusini na hivyo wao kuweza kushambuliwa kirahisi na Israel.

Hata hivyo hali haionekani kuwa njema kwasababu Iran ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria ipo katika uchaguzi.Hadi sasa mgombea kutoka wizara ya mambo ya ndani ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa usuluhishi ''negotiator'' kati ya Iran na nchi za Mgahribi anaonekana kuongoza. Hadi muda huu tunapoandika.

Mgombea huyo yupo mbali ya mpizani wake ambaye ni meya wa jiji la Tehran. Inataarifiwa kuwa uandikishaji na upigaji wa kura umefikia aislimia 80.

Sasa haiujulikanai nani atakuwa mshindi na ataingia na sera gani kuhusiana na mzozo wa mashariki ya kati.Hili linazidisha wasi wasi kwasababuni bora ''zimwi unalolijua kuliko malaika usiyemjua''

Marekani imetumia ombwe hilo na lile la Uturuki kutangaza kuwa itawasaidia askari waasi wa Syria kwa silaha.Hii inafuatia uchunguzi uliobaini Syria kutumia silaha za sumu dhidi ya raia wake.

Wakati huo huo kunamngawanyiko mkubwa miongoni mwa nchi za kiarabu kuhusu Syria.
Hayo yakitokea vita ya Syraia inaonekana kuanza kusambaa taratibu.

Jambo lisilofahamika ni je, Marekani itaweza kuweka askari ikiwa bado na vita nyingine?
Je, Israel itapewa jukumu hilo na kama ikiwa hivyo hali itakuwaje kati ya Israel,Turkey, Syria, Lenbanon na Jordan nakwingneko?

Tusemezane
 
Back
Top Bottom