Hapo sasa ni lini Simba akaacha asili yake?.. utamfuga na hata kumchezesha sarakasi lakini siku akirudi nyikani ule Usimba wake hurudi palepale..Mkuu Mkandara hili jambo la kuhusu wawekezaji linanitatiza kidogo.Wamarekani wenyewe walitaka uhuru kwasababu sheria ilikuwa ikiwataka wapeleke mapato mengi in forms of taxes nk,back to the "mother land" yani kwa malkia uingereza.Walipokwa wakipinga,makampuni ya marekani yakawekewa vikwazo.Wakati ule biashara kubwa ikiwa ni chai.
Kampuni ya uingereza ambayo haikuwekewa vikwazo,ilikuwa na mzigo ya chai kwenye bandari ya Boston,wafanyakazi wakamwaga chai yote kwenye maji na ndipo ikaanza ile kauli ya "Taxed enough already" aka tea party...Haya ni baadhi ya matukio tu yaliyo highlight path waliyoichukuwa wamarekani ili kupambana na mwekezaji beberu wa uingereza ambaye aliwacolonise.Baadae wamarekani walipata uhuru baada ya kumwaga damu dhidi ya mwingereza.Na pia mmarekani aliyegombea uhuru ni mwingereza pia aliyehama kutoka uingereza akitafuta uhuru wa kujiamulia mambo na kuwa na mawazo ya tofauti.Lakini cha kushangaza kwasasa,ni kama the same thing is going on,especially dhidi ya Africa,bado tusitegemee eti kuwa wawekezaji wataleta maendeleo kama hawatabanwa.Na hakuna kampuni ya nje ambayo hailinufaishi taifa ilikotoka,ndo ubepari huo,yale mambo ya "mother land" yapo lakini kwa namna ya tofauti.Kwa wenzetu,kampuni hizo hata kama zinakwenda kuwekeza nje,bado zina majukumu kwa motherland kwasababu ndo wenye kuzilinda na kuzipatia ile "superiority" ndo ubepari huo.
Tunachotakiwa sisi ni kujihadhari kama tuwajuavyo Simba au nyoka, nasi kama Ngo'mbe nadhani tuna experience kubwa kuliko mataifa mengi lakini ajabu ni kwamba tumekuwa kama mbwa na chatu. na huwezi kuwalaumu Marekani kwa Ubeberu wao maana ndio uzawa wao ambao halikuwa na rasimali nyingi isipokuwa kipaji cha uwindaji kuwa na na kucha na meno K9 nasi kama ngo'mbe tuna kwato, maziwa, nyama na hata ngozi yetu ni chakula kwao, kwa nini tunashangaa Simba kuendelea kuwinda ng'ombe! - kazi kwetu.