Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Shukran Nguruvi3,
Binafsi yangu leo sijapata usingizi na saa hizi ni saa tisa Usiku nipo macho makavuu..Kuhusiana na KATIBA wananchi wengi wameweka tumaini ktk ujenzi wa mwongozo mpya ambao kusema kweli nisingependa kuwakatisha tamaa, badala yake nitajaribu kuwa objective ktk hli maana sina jinsi..

A (i) Ningeandika isomeke - UZALENDO - NATIONALISM
Why? ni kwa sababu this is what we are missing...Watanzania tumepoteza Uzalendo kabisa, hatuna National pride, Patriotism maana tayari tumeisha poteza tumaini hivyo sii rahisi watu kuwa devoted na loyal kwa Utaifa wetu. Hivyo uzalendo kwa nchi ni lazima wala sio ombi na pekee ndio utaweza kufanikisha mengine yote yanayohusu tofauti zetu. Uzalendo utaondoa Ufisadi, Uzalendo utaondoa chuki, fitna na kuipenda nchi yetu badala ya nafsi zetu..

ii) Kitu cha kwanza kabisa katiba lazima itazame WATU na MAZINGIRA tuliyopo leo ili kutunga katiba inayofanana nasi ili tupate dira ya wapi tutakwenda. Kwa kuzingatia UTU wa mwafrika ni lazima tuendelee kuenzi yaliyo asisiwa na katiba ya mwanzo ya mwaka 1976 kwa kulinda UHURU, HAKI na USAWA.

WATU
Kwa kuzingatia UTU kiholela hakuwezi kuwa na maana yoyote ndani ya katiba kama katiba hiyo haitawalenga WATU wake na nadhani hakuna tafsiri ya walengwa zaidi ya WAZAWA.. Wapo watu wanaosema Uzawa ni fikra za Kibaguzi lakini nani ulimsikia akinadi Uzalendo pasipo kuhusiana na uzawa?..Nchi zote duniani zinatunga kativba zao kwa kuwalenga wazawa, wewe mgeni ukienda makwao ndiye unayetakiwa ubadilike uwe kama wao japokuwa hukatazwi kufuata Utamaduni wako usiopingana na katiba yao..

Katiba lazoma iwalenge wazawa mna sio wageni ama kuwafurahisha wageni - interes zetu kwanza. Hivyo kizazi cha watanzania na tofauti zao ndicho kinatangulia kuwa sababu ya kutungwa katiba mpya. Maadam nchi yetu ni TAJIRI lakini wananchi wake ndio maskini basi ni lazima tukubali kujitazama sisi, kama kile kifungu kisemacho Nchi yetu haina dini isipokuwa watu wake ndio wenye dini na makabila (nimeongezea langu)..Hivyo kwa ujumla nasema nchi yetu ni tajiri, haina dini wala kabila isipokuwa wananchi wake..

Hawa ndio watu tulokuwa nao hivyo katiba kwa ujumla wake ni lazima pzingatie tofauti hizi maana huwezi kusimamisha UHURU, HAKI na USAWA (equal opportunity) in order to create a unified community na ikiwa katiba yenyewe itachelea kuwatazama watu wake kwa tofauti ili kuwajenga desire for national unity and advancement basi haya yatakuwa makosa ya kwanza.

Katiba hii mpya itaweza vipi kuwahamasisha wananchi hawa maskini na wenye dini na makabila tofauti? Bila shaka kwa kusimamisha doctrine inayojali UTU kwa tafsiri niliyoiweka hapo juu. Sisi Watanzania hatuhitaji kubadilika, nimewahi kuwasikia watu wengi sana wakisema jamani eeh tubadilike..eeeh? Tubadilike ili tuwe nini? tuwe kama wazungu au! Jamani Sisi ndio sisi kama tulivyoumbwa kwa vipaji vyetu na tunapobadilika ina maana tunaiga mila na desturi za watu wengine ambao kwao ndivyo Walivyo. Kwa nini tuvae suti kuubwa jua la nyuzi 40? mbona mzungu akija Afrika huvua hadi shati akatembea tumbo wazi sasa tubadilike kivipi ilihali sisi ni maskini na wajinga eeeh! - tutaweza vipi kubadilika?. Tunachotakiwa ni UZALENDO. na sio kubadilika.

MAZINGIRA
Kama nilivyosema huko nyuma mazingira ni sehemu kubwa sana utata tunaokabiliana nao na sehemu kubwa ya umaskini wetu imetokana na kutojali mazingira yetu zaidi ya kuuza kutumia na kufaidika ilihali tunashindwa kuelewa kwamba tuna maziwa mengi kuliko nchi yoyote ya Afrika lakini idadi kubwa ya wananchi hawana maji..Sasa ikiwa maji ni UHAI na asilimia sijui 80 hawana maji hivi kweli tunategemea tunaweza kuendelea. Mazingira yetu sii kuwepo kwa madini na wanyama pekee bali ni pamoja na matumizi bora ya riziki hizi alotujalia Mwenyezi Mungu.

Kuna wakati huwa nikisikia ule wimbo wa -Ukitazama ramani utaona nchi nzurii - yaani huwa natamani kulia machozi jinsi mwenyezi Mungu alivyotupendelea. Pia tazama basi na vipaji tulivyokuwa navyo ktk kilimo, uvuvi na mifugo lakini maajabu tumekuwa watumwa wa ukoloni mamboleo ambao wanajipanga kuivamia Afrika. Mzungu haji Afrika kuijenga Afrika bali kutazama fursa za kutajirika yeye ama kwao.. Hawa wana Uzalenfo tayari kwa nchi zao hivo hawezi kuja kichwa kichwa wekeza mahala ambapo kesho mnaweza kumfukuza. I mean huhitaji Phd kulifahamu hili. Pasipo kuthamini MAZINGIRA yetu hatuwezi ku overcome Umaskini na Maradhi maana hatutaweza kuwa na chakula cha kutosha (food insecurity), kuwa na maji safi, malazi mazuri kuzalisha kazi wala adequate energy supply.

Hayo maswali mengine ya B yote yamejibiwa ndani ya mtazamo wangu..Kuuthamani UTU kwa kusimamisha uhuru, haki na usawa tukajitazama kwenye kioo na kujiuliza sisi ni watu gani, kisha tunakubali for who you are, tuujenge Uzalendo wa kuwa sisi ni Watanzania japokuwa maskini, wajinga na wenye maradhi kisha basi lazima tutakuwa na kiburi cha kuchukia Ukoloni mamboleo kwa umaskini wetu. Na mfumo pekee unaotufaa sasa hivi ni NATIONALISM, kupiga vita fikra za kubadilika na sijui kuiga sana ya nje ambayo ndio chachu ya Ufisadi...

Napingana na mawazo ya Ujamaa uloogopa wezi (wakoloni) tukajifungia wenyewe gereza tuloyajenga sawa na majumba ya Mikocheni na masaki yaani hawa wanaogopa wezi badala ya kuweka ulinzi kuzuia wezi, wanajenga uzio wa kuta futi 12, na waya za umeme juu kuzunguka nyumbani mzima..minondo hadi vyumbani, kiasi kwamba wao wenyewe wanakuwa wafungwa kwa majumba yao wenyewe na kwa gharama kubwa sana lakini kumbe ndio kwanza wanawavuta majambazi wakiona vile wanakuwa curious kujua kuna nini ndani mle!..Sasa kama wao wanaona raha kuishi ktk mazingira yale ama ya Ujamaa, binafsi yangu siyapendi na mara nyingi mtu alofungiwa akipata mwanya hufanya mabaya zaidi ya yule aliyeko huru..
 
JingalaFalsafa

Umeongelea hoja hii ya sheria za kimataifa katika muktadha wa demokrasioa na Haki za binadamu. Tukichimba mambo deep tutakuja kukuta kwamba Utumwa wa Fikra ndiyo ulioleta haya yote. Ubepari umeathiri sana dunia katika Aspects zote za Utu.

Ubepari unazaa utumwa kwa kuwa haulindi Utu ila kulinda nafasi ya Ubepari wenyewe. Na hili tulishuhudia hata kukiuka sheria za kimataifa ambazo ili kulinda ambition binafsi. Leo hii Tunashuhudia Taifa kinara kabisa kuhubiri demokrasia na kuweka Msingi wa modern Era katika Siasa za kimataifa yaani Uingereza na Marekani wakiwa Mstari wa mbele kuvuruga kanuni tu zinazozuia uvamizi kwenye ubalozi wa kigeni. Case ya assange italeta arguinment nyingi kuhusu uhallai wa uingereza kuwa na sheria ambayo iko against na vienna convention ya kutoingilia kinga ya ubalozi wa nchi nyingine

Hapa tunaona wanafanya hivyo na kutupilia mbali hofu ya mamcho ya walimwengu katika ukiukaji wa sheria za kimataifa.Hiki ni kiburi ambacho msingi wake ni ubepari tu. Maslahi mbele, Mengine yote yatakuja baadae. Ujanja ujanja mbele
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz tupo sana tu. Si unajua siasa ni kama draft? Hata kama sie ni watazamaji, si kila kitu tutasema. Wakati mwingine tunaachia vyombo vya Dola kama mahakama viseme zaidi. Au unataka mifano hai?
 
Last edited by a moderator:
Tunaendelea
Mkuu Mkandara kafunguka na Nationalism na kutetea hoja yake kimantiki kabisa.
Nataraji wakuu wengine wanajipanga.
Ben Saanane yeye hataki kusikia kitu ubepari kabisa! naye pia tutamiskia akirejelea bandiko #310.
 
Mkandara, kabla sichangia kuhusiana na maswali ya Nguruvi3, napenda niseme kuwa nakubaliana na wewe kwenye kuhusu patriotism. We definitely lack it.

Lakini uzalendo wa kweli ni lazima ulindwe na katiba ya kizalendo.However, kuna mikinzano inayoletwa na mfumo wa kisiasa na kiuchumi unaotawala dunia kwa ujumla.

Kwa mfano, inakuwa shida sana kwa Taifa tegemezi na masikini kuwa na viongozi wazalendo. Uzalendo has something to do with "msimamo",kitu ambacho ni unachievable kwa ombaomba. Uzalendo ni kuhakikisha kwamba mikataba yote inazingatia maslahi ya Taifa.Uzalendo ni kukataa rushwa nk.

Matatizo yote tuliyonayo has something to do with lack of patriotism. Kwa mfano wamarekani wana patriotic act ambayo primarily ni ya kudeal na issue za immigration na wahamiaji..Tukibadilika na kuwa serious na taifa letu huo tayari ni mwanzo wa uzalendo...tunaweza kuweka sheria kali dhidi ya ufisadi as an act of patriotism kwa kuanzia.

Patriotism inaanza na mapenzi ya kweli kwa nchi.Mtu aliyekuwa na mapenzi kama hayo ni mwalimu Nyerere. Patriotism can sometimes be described as "self sacrification"? Kufanya mambo ambayo yanaweza yasiwe na maslahi ama manufaa binafsi ama immediate results. Lakini yakawa mambo yenye maslahi kwa taifa na ambayo yanaweza kuwa na a longer term results.
 
S

A (i) Ningeandika isomeke - UZALENDO - NATIONALISM
Why? ni kwa sababu this is what we are missing...Watanzania tumepoteza Uzalendo kabisa, hatuna National pride, Patriotism maana tayari tumeisha poteza tumaini hivyo sii rahisi watu kuwa devoted na loyal kwa Utaifa wetu. Hivyo uzalendo kwa nchi ni lazima wala sio ombi na pekee ndio utaweza kufanikisha mengine yote yanayohusu tofauti zetu. Uzalendo utaondoa Ufisadi, Uzalendo utaondoa chuki, fitna na kuipenda nchi yetu badala ya nafsi zetu..

Mkuu Mkandara,

Nimeipenda analysis yako especially kwenye suala hili la uzalendo. Hata hivyo bado nimebaki na maswali kadhaa;

1. Uzalendo unajengwa na nini? Vitu gani vinachangia mimi/wewe/yule kuwa mzalendo kwa nchi yako?
2. Uzalendo unajengwa kuanzia ngazi ya juu (uongozi) kwenda chini (wananchi) au kinyume chake?

Tumekuwa tukizungumzia uzalendo kupotea miongoni mwa watanzania lakini hebu tutazame kwa kina zaidi nini kimetokea hadi uzalendo kupotea miongoni mwetu? Nafikiri tukipata majibu katika hili basi tutaweza kupata mwanga zaidi juu ya wapi tunataka kwenda.

Nawasilisha
 
Pamoja sana wakuu wangu:

Sijakawia nadhani; Ngoja nami nitoe machache:-

Kwanza nakubaliana kabisa kuhusu Uzalendo, kama hatua muhimu ya kufikia ustawi wetu kama watanzania (waafrika wa Tanzania). Hata mimi ningependa kuona Katiba iliyoipa kipaumbele cha kwanza dhana hii ya UZALENDO! Katiba huundwa na Sera za nchi, ambazo nazo hutungwa kulingana na Mfumo wa Maisha wa taifa husika! Katiba tarajiwa haiwezi kutoka nje ya misingi ya Sera za nchi yetu ambazo ni zao la Ubepari kama mfumo wetu mkuu wa maisha kwa sasa! Laiti kama sera zetu za ndani na nje zingebadilika, basi walau tungetarajia kitu tofauti japo kidogo! Lakini kwa sasa mi KUJIDANGANYA! Siwakatishi tamaa, japo pia TUSITARAJIE UZALENDO KATIKA KATIBA MPYA, bali kulinda minority interests!

UZALENDO unajengwa na mila, desturi, taratibu, imani, falsafa, itikadi, mitazamo, mienendo, miiko, n.k. yenye TIJA-MANTIKI kwa eneo husika, yote hayo nayo ili kuzaa uzalendo, ni lazima yabebe MANTIKI ndaniye...nayo ndio UTU-KUFIKIRIANA! Hayo yote ndiyo yapasayo kuzaa SERA za nchi yetu, SERA hizo ili kuzifanya RASIMI kuweza kusimamiwa kwa nguvu yoyote ile na mamlaka kamili, ndipo zinaporasimishwa na kuitwa Sheria, zipo ndogo ndogo na kubwa, na hiyo ndio KATIBA! Sheria yoyote ikiukayo misingi hiyo katika kupatikana kwake, basi itakuwa imekiuka Uzalendo!

Kumbe basi, hata turekebishe sheria kwa kiwango gani, kama hazitakuwa na zana hii ya KUFIKIRIANA ni KUPOTEZEANA MUDA! Hatutafikia uzalendo Milele!

Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkandara,kabla sichangia kuhusiana na maswali ya Nguruvi3,napenda niseme kuwa nakubaliana na wewe kwenye kuhusu patriotism.We definetly lack it.Lakini uzalendo wa kweli ni lazima ulindwe na katiba ya kizalendo.However, kuna mikinzano inayoletwa na mfumo wa kisiasa na kiuchumi unaotawala dunia kwa ujumla.Kwamfano,inakuwa shida sana kwa Taifa tegemezi na masikini kuwa na viongozi wazalendo.Uzalendo has something to do with "msimamo",kitu ambacho ni unachievable kwa ombaomba.Uzalendo ni kuhakikisha kwamba mikataba yote inazingatia maslahi ya Taifa.Uzalendo ni kukataa rushwa nk.Matatizo yote tuliyonayo has something to do with lack of patriotism.Kwamfano wamarekani wana patriotic act ambayo primarily ni ya kudeal na issue za immigration na wahamiaji..Tukibadilika na kuwa serious na taifa letu huo tayari ni mwanzo wa uzalendo...tunaweza kuweka sheria kali dhidi ya ufisadi as an act of patriotism kwa kuanzia.Patriotism inaanza na mapenzi ya kweli kwa nchi.Mtu aliyekuwa na mapenzi kama hayo ni mwalimu Nyerere.Patriotism can sometimes be described as "self sacrification"?kufanya mambo ambayo yanaweza yasiwe na maslahi ama manufaa binafsi ama immediate results.Lakini yakawa mambo yenye maslahi kwa taifa na ambayo hayana immediate results.
UZALENDO ni sawa na Imani ya dini. Inatokana na wewe kuamini UTU wako (uhuru, haki na usawa) na kutambua wajibu wako kama binadamu. Pasipo Uzalendo ni sawa na kuandika vijitabu vya kiimani (sunna) na sio Biblia ama Kuruan inakuwa ni mawazo ya watu tu. Lakini kwa kutanguliza Imani ya Uzalendo, ule moyo wa kutambua Uhuru wetu, Utaifa wetu, haki na usawa na above all The goal of all economic and political nationalists has been the creation and then maintenance of our sovereignty. For that we are writing a new Constitution!.

Binafsi yangu naamini adui yetu sio Zanzibar au Malawi bali adui yetu ni Umaskini na umaskini huu umepangwa makusudi kiasi kwamba haiwezekani nchi iwe tajiri lakini watu wake maskini. Nchi za Ulaya ni maskini lakini watu wake ndio Matajiri..Hivyo tunzi zote za economic system zimelenga wao, kuhakikisha wao wanaendelea kupata riziki ya chakula chao kupitia njia walizozoea (maliasili zetu). Na ndio hofu ya kina Nyerere hadi wakatujengea mikuta ya futi 12 tukajifungia kwa miaka 25..

sasa maadam tunatoka nje haikutakiwa sisi kupoteza UZALENDO wetu, nadhani leo hii tunahitaji nationalism kuliko wakait wowote kuandika katiba mpya japokuwa tunajua tunaingia ktk uwanja wa fisi. hatukuzaliwa sisi kuwa swala, Pundamilia ama nyumbu ambao kila mwaka lazima tuvuke mto mara kupambana na Mamba. Halafu watu wanakuja laumu hawa Mamba wa mto mara wanavyo nenepeana. Sisi ndio tunawalisha na sio swala la Ubepari, ubepari ni sawa na KULA ili upate shibe ubepari unatoa tu ruksa kwa kila kiumbe kula unachotaka. Viumbe wote wako huru kuwinda malisho wanayotaka kula tusilazimishane kuwa hii ni tamaa bali ndivyo tulivyoumbwa.Ubepari ni nature ya mwanadamu lakini wapo binadamu wabaya ktk kuendesha Ubepari.

Kama chakula chako ni nyasi huwezi kulazimisha Mamba naye ale nyasi, mamba ataendelea kuwinda swala na pundamilia mto Mamba n jukumu la swlaa hao kutafuta makazi mengine au kuendelea ku risk kuvuka lakini Mamba hawezio kuhama mtoni ama kubadilisha chakula. Ujamaa ni sawa na itikadi ya bainiani inayopinga kula nyama na ukiisoma kwa makini kusema kweli inaleta maana sana kwa nini binadamu tunakula wanyama wengine na kulaani vitendo vya wala nyama..

Lakini Ubepari unajibu ya kwamba hata wewe vegetarian unakula mimea yenye uhai vile vile japokuwa haina macho, Ubepari unasema kula nyama ni nature yao, ni maumbile ya binadamu hivyo unapojitenga na kulaani ulaji wa nyama ni witumike falsafa ile ile kuatzama pia ulaji wa mboga maana hata mimea ina ihai wake..Zile sababu za Ujamaa kulaani Ubepari ndizo sikubaliani nazo kwa sababu mbona wapo Paka, mbwa, kenge na mijusi hawali swala wala Pundamilia. Hivyo ni kujumu letu kujua chakula cha nchi za Ulaya ni rasilimali za Afrika na ndio maana wananenepena lakini sisi chakula chetu nini?.. Kama ni maliasili hizi hizi basi nasi tunayo meno ya kula nyama, sio lazima tukawinde Swala ama Pundamilia kule mto Mara maana sisi sio Mamba vile vile. Sisi ni kina nani hadi leo hatujui wala hatutaki kujua ila kulaumu tu Ubepari.

Sisi ni binadamu tumeumbwa na akili zaidi ya wale nyumbu au Pundamilia japokuwa ni lazima uchumi wetu upitie kwao (mabeberu). Nationalism ni lazima, pia ni lazima katiba yetu itambue kwanza kabisa sisi ni viumbe wa aina gani wala nyama au mboga na inaandikwa kulinda uzawa wetu..Ni imani yangu ili kuamini lazima sisi tujitambue who we are na maadam tumepoteza Uzalendo ni lazima kurudishwa as long as Nationalism unites people of different classes and ideologies, link our past to our present and give us sense of identity. Katiba itaweza tu kumlinda Mtanzania dhidi ya Mamba wa Mto mara ( mabeberu) kwa kutanguliwa na Uzalendo wa viongozi waliopo. Ndio maana nawapenda Mbowe, Dr, Slaa na Zitto ktk hilo japokuwa wana tofauti zao. Na maadam wengine hawana uzalendo hiyo katiba inayotakiwa kuandikwa ni bomu jingine..(sikutaka kuandika mstari huu)
 
Mkuu wangu Mkandara,

1. Kwanza nimesema UTU ni MANTIKI KUU, yaani UUWIANO SAHIHI (si uuwiano tu), yaani KUFIKIRIANA, ndicho pia ulichogusia "The quality of Compassion or Consideration for Others (one another)" niseme kuwa, hakuna KUFIKIIRIANA kama hakuna UUWIANO SAHIHI. Tafsiri ya UWIANO SAHIHI ni "KUTOKINZANA"

Ninaamini Gender balance si Uwiano Sahihi, huwezi kumlinganisha mwanamke na mwanaume kwa chochote! Ila kuna neno HAKI-UHURU-UHALALI, hayo ndiyo yapindishayo dhana ya "UTU-MANTIKI-UUWIANO SAHIHI-KUTOKINZANA-KUFIKIRIANA" hata kwenye kuandika huwa tunaambiwa kupanga hoja zetu kiwantiki, yaani ziwe na mtiririko sahii, zisikinzane!

2. Ni sahihi kabisa kuwa tumeumbwa tofautitofauti sana, na tofauti hizi ndizo ziletazo machafuko baina yetu, sasa ili tofauti hizi zetu zisituingize matatizoni, ni lazima kuwepo kwa UWIANO SAHIHI-KUTOKINZANA (mizani sawa na si Haki)! Yaani hakuna tofauti kati ya MANTIKI, UUWIANO SAHIHI, KUFIKIRIANA, KUTOKINZANA, UTU. Usiseme tu UUWIANO bali UUWIANO SAHIHI.

3. Hakika kabisa UTU si kuthamini HAKI, UHURU na USAWA! Kwani mambo hayo matatu yanakinzana kwa kiasi kikubwa, kwenye HAKI kuna UHURU lakini si USAWA, sawa na kwenye UHURU Haki inapatikana lakini si USAWA, lakini katika Usawa kuna Haki na Uhuru, lakini si haki na uhuru huu mnaoutaka na kuuishi kwa sasa. Pigania Usawa, kwani ndani yake kuna Haki laki usipiganie Haki kwani ndani yake kuna Ubinafsi. Haki ijengwayo na Usawa, ni zao la UTU.

Mungu wetu anaita sasa.
Shukuran sana kunipa darsa ktk UUWIANO SAHIHI hapo nakuunga mkono sana tu lakini lazima nikujibu ktk swala la UHURU, HAKI na USAWA..maana umesema Usawa haupo ktk UHURU ama HAKI.. Nitakwambia kwamba kutokuwepo kwa usawa (equal opportunity) ndio sababu ya migogoro yote unayoiona. Binafsi yangu wewe umetumia neno Uuwiano sahihi kama tafisri ya UTU kumbe Uuwiano sahihi ndio USAWA naozungumzia mimi, hivyo hii ni sehemu tu (kati ya tatu) ya UTU wa mwanadamu.. Neno Uuwiano SAHIHI ndilo nalitumia mimi kama USAWA kwa maana hiyo hiyo na huwezi kujenga sheria ya usawa pasipo KUFIKIRIANA na KUTOKINZANA..
 
Shukuran sana kunipa darsa ktk UUWIANO SAHIHI hapo nakuunga mkono sana tu lakini lazima nikujibu ktk swala la UHURU, HAKI na USAWA..maana umesema Usawa haupo ktk UHURU ama HAKI.. Nitakwambia kwamba kutokuwepo kwa usawa (equal opportunity) ndio sababu ya migogoro yote unayoiona. Binafsi yangu wewe umetumia neno Uuwiano sahihi kama tafisri ya UTU kumbe Uuwiano sahihi ndio USAWA naozungumzia mimi, hivyo hii ni sehemu tu (kati ya tatu) ya UTU wa mwanadamu.. Neno Uuwiano SAHIHI ndilo nalitumia mimi kama USAWA kwa maana hiyo hiyo na huwezi kujenga sheria ya usawa pasipo KUFIKIRIANA na KUTOKINZANA..

Nakuelewa mkuu wangu, nadhani tuko pamoja katika hili.
UTU huzaa Usawa nakubali kabisa-Uwiano Sahihi-Kutokinzana. Nachokihofu kwenye utatu wako ni "HAKI na UHURU(sio ule wa kutoka kutawaliwa, bali wa kujiamulia mambo)" Kwa kawaida Uhuru ndio uzaao Haki (uhalalishaji wa uhuru wake mtu). Hapa ndipo tunapopaswa kutafakari, yepi ni matokeo ya mwanadamu kuhalalishiwa Uhuru wake wa kufanya mambo? Je, mwanadamu siye huyu aliyeumbwa na matamanio na hulka? Nini kitafuata baada ya kuachwa huru kufuata matamanio na hulka zake? Kwangu mimi hapa ndipo UMIMI-KUJIFIKIRIA-UBINAFSI unapoibuka-mimi kwanza-hapa ndipo panapoibuka ukandamizaji, unyonyaji, unyanyasaji, unyonge, utumwa, umasikini n.k. basi kumbe USAWA unajitenga kutoka dhana ya Uhuru na Haki, havichangamani navyo.
Kumbe basi ili kuua Umimi kwanza, uletao unyonge na umasikini na maovu tele, ni lazima tumfunge kwa vigingi imara kabisa na nyororo mpya kwa kumfungia uhalali wake wa kufuata hulka zake, kwakuwa si mmoja bali sisi wote, basi kifungo chetu kituongoze kwenye dhana ya KUFIKIRIANA-UUWIANO SAHIHI(usawa)-KUTOKINZANA, na hakuna msingi mwingine wa kufanya hayo ila UTU, kwani ndiyo MANTIKI pekee iliyomo nafsini mwa kila mtu...UTU Kwanza!
Kikubwa kabisa nachokisema ni kuwa "Binadamu hatakiwi kuachwa huru kujiamulia mambo yake, jamii itageuka samaki baharini mkubwa kummeza mdogo, lakini kwakuwa sote tumejaliwa maarifa, basi mapambano yataibuka, haitokuwa rahisi"
Mungu wetu anaita!
 
Kama ni damage control basi ccm wameshindwa kuifanyia kazi. Hiyo kitu inahitaji watu ambao ni proactive na si reactive ili mwisho wa siku mambo yaweze kisawazishwa. Nguruvi3 unazungumziaje sakata la ulimboka, majaji, ufisadi wa wabunge, n.k relative to hii damage control?
 
Last edited by a moderator:
Nakuelewa mkuu wangu, nadhani tuko pamoja katika hili.
UTU huzaa Usawa nakubali kabisa-Uwiano Sahihi-Kutokinzana. Nachokihofu kwenye utatu wako ni "HAKI na UHURU(sio ule wa kutoka kutawaliwa, bali wa kujiamulia mambo)" Kwa kawaida Uhuru ndio uzaao Haki (uhalalishaji wa uhuru wake mtu). Hapa ndipo tunapopaswa kutafakari, yepi ni matokeo ya mwanadamu kuhalalishiwa Uhuru wake wa kufanya mambo? Je, mwanadamu siye huyu aliyeumbwa na matamanio na hulka? Nini kitafuata baada ya kuachwa huru kufuata matamanio na hulka zake? Kwangu mimi hapa ndipo UMIMI-KUJIFIKIRIA-UBINAFSI unapoibuka-mimi kwanza-hapa ndipo panapoibuka ukandamizaji, unyonyaji, unyanyasaji, unyonge, utumwa, umasikini n.k. basi kumbe USAWA unajitenga kutoka dhana ya Uhuru na Haki, havichangamani navyo.
Kumbe basi ili kuua Umimi kwanza, uletao unyonge na umasikini na maovu tele, ni lazima tumfunge kwa vigingi imara kabisa na nyororo mpya kwa kumfungia uhalali wake wa kufuata hulka zake, kwakuwa si mmoja bali sisi wote, basi kifungo chetu kituongoze kwenye dhana ya KUFIKIRIANA-UUWIANO SAHIHI(usawa)-KUTOKINZANA, na hakuna msingi mwingine wa kufanya hayo ila UTU, kwani ndiyo MANTIKI pekee iliyomo nafsini mwa kila mtu...UTU Kwanza!
Kikubwa kabisa nachokisema ni kuwa "Binadamu hatakiwi kuachwa huru kujiamulia mambo yake, jamii itageuka samaki baharini mkubwa kummeza mdogo, lakini kwakuwa sote tumejaliwa maarifa, basi mapambano yataibuka, haitokuwa rahisi"
Mungu wetu anaita!
Mkuu wangu haya maneno yote UHURU, HAKI na USAWA yanahitaji kuyaelewa kwa undani wake na sii tafsiri ya kwenye kamusi maana maumbile ya viumbe wote hayawezi kutafsrika tu sii kwa fikra na logic bali hata kisayansi.. Katika UTU wa mwanadamu kuna historia nyuma ya maneno haya kama ilivyo Biblia au Kuruan. Kila sura na aya imetokana na mwanzo ama niseme sababu ya kuwepo sura hiyo. Hivyo UHURU ukiwa na maana ya FREEDOM umetokana na Upinzani wa UTUMWA baada ya sisi wanadamu kupoteza UTU wa kuthamini wanadamu wengine. Hivyo hata kama unatawaliwa ndani ya nchi kuna freedom unayotakiwa kuwa nayo kama binadamu usiwe mtumwa wa mtu mwingine.

Hivyo kwa kiasi gani tunaweza kuima utumwa ndipo hapo wigo hupanuka kila generation maana siku hizi imefikia hadi kuna watumwa wa sex, vijakazi, ajira kwa watoto na kadhalika. In fact binafsi yangu napinga kabisa wajakazi wanaofanywa watumwa majumbani mwetu wakipewa chakula na malazi kama malipo halali ya kazi wanazozifanya. Hapa hakuna Uhuru, haki wala usawa lakini siwezi wabadilisha fikra Watanzania wote kutokana na U mimi wao.

HAKI ama Justice imetokana pia na ulazima ulokuwepo toka zamani kuwepo wa baadhi ya watu above the law (U mimi). Hawa waliruhusiwa kuwa na watumwa, kutawala au kufanya madhambi mengine yakahalalishwa na wasihukumiwe kwa haramu zao. Sheria ilikuwa inakata upande mmoja tu pasipo uzingatia haki ni kwa watu wote. Hivyo kumtendea binadamu mwenzako haki ni pamoja na kuzingatia haki na Uhuru wa mtu huyo, vitu hivi vitatu vinaambatana kila sehemu. Huwezi kuitoa haki pasipo kuzingatia freedom na equality baina ya mtu na mtu, kiongozi na mfuasi wake. Sema ktk hili la HAKI na UHURU ndilo hadi leo linatushinda sana kutokana na kwamba Uuwiano sahihi hauwezi kuwepo ikiwa hatutathamini Uhuru na haki ya kila mmoja wetu. Kila kiongozi anajiona yeye ni Mtawala hivyo tunavunja nguvu ya freedom na Justice. Kwa ujumla wake UTU ni mtihani mkubwa wa mwanadamu kutokana na HISIA ( Complex) za kisaikologia zinazoambatana na emotions zetu. iwe kumbukumbu, mitazamo,matakwa kwa kila mmoja wetu. Unconscious tumegubikwa na TAMAA, INDA na kadhalika.

Hivyo Complexes ama niseme hisia zetu ndizo hu influence individual's attitude and behavior na sio mfumo wowote wa kiuchumi. Kuwepo kwa haki ni muhimu sana ku control hizi complex maana hata Malkia hufikiria ni haki yake kutawala na anaweza kutufikiria na tutokinzana. Unapotanguliza Uhuru wa mwananchi mwingine unaondoa mamlaka alojikabidhi Malkia na wale wengine wote wanaojiona wao wabora kuliko viumbe wote na ni haki yao kuwa hivyo. Huo U mimi unaozungumzia ni kutokana na kwamba Uhuru na haki unampa mtu mmoja badala ya watu wote, unawapa kundi la watu badala ya taifa zima.. U mimi ni pale unapofikiria kuna mbora zaidi anayestahili Uhuru, haki na usawa zaidi ya wengineo kutokana na nafasi yake lakini kama utawapa watu wote Uhuru wa kutokuwa watumwa, haki, fursa na nafasi sawa ktk utawala basi huo U mimi hautakuwepo maana kila mtu anaweza kuwa ulivyo wewe hazuiwi na sheria ama kanuni kufikia dream yake hata iwe Umalkia..

Kwa hiyo hivi vitu vyote vinategemeana kama kiuchumi tunavyopambana na Umaskini, Ujinga na maradhi hivi vitu vyote huwezi kuanza na kimoja ukasimisha kingine. Huwezi kuondoa Ujinga ikiwa wananchi wako ni maskini na wakiwa maskini, maradhi lazima yataibuka baina yao. Hivi vyote vinakwenda sambamba ktk vita na ndio mamlaka ya Utawala bora.
 
Nakuelewa mkuu wangu,
Kikubwa kabisa nachokisema ni kuwa "Binadamu hatakiwi kuachwa huru kujiamulia mambo yake, jamii itageuka samaki baharini mkubwa kummeza mdogo, lakini kwakuwa sote tumejaliwa maarifa, basi mapambano yataibuka, haitokuwa rahisi"
Mungu wetu anaita!
Nadhani kuna namna Mkandara hajaeleweka. Anaposema kumwacha mwanadamu huru hana maana kila mmoja afanye atakavyo. Ana maana kila mmoja aachwe huru lakini uhuru huo uwe na mipaka ya kutoingilia uhuru wa mwingine. Na ukisoma bandiko lake kuhusu Nationalism amejieleza vizuri kuhusu hili.

Mimi bado nawasubiri wakuu huko walipo nadhani wakipata fursa watarejea kwa kuliangalia bandiko 310.

Jambo moja nisiloweza kumwelewa JingalaFalsafa ni pale anaposema pa kuanzia ni UTU ambao ni kufikiriana. Wakati huo huo anasema haki na uhuru ni tatizo katika kufikiriana.

Ingawa amekiri kuwa ni lazima tuishi kwa sheria ili tusiwe kama samaki nabaki kujiuliza hivi unawezaje kuuweka utu miyoni mwa watu tukijua kuwa binadamu hata wazaliwao tumbo moja wanatofauti? Nina maana unawezaje kuingiza UTU katika jamii ya kitanzania, njia gani zitumike.

Mkandara kasema kuhusu Nationalism na kaelezea inasimamishwa na vitu gani.
Sasa JingalaFalsafa UTU kama ndiyo dira ya taifa tunaifanyaje practically
 
Nimekupata mkuu wangu Mkandara:
Ni sahihi kabisa, kuwa tafsiri ya haya maneno HAKI & UHURU, isitoke kwenye kamusi wala fulani amesema nini! Bali iwe imetoka katika tafakari ya kina, yenye mantiki na huru! Hapa ndipo napoomba msaada, wa kujuzwa zaidi, ni ipi tafsiri ya UHURU na HAKI katika misingi ya KUTOKINZANA, yaani UTU? Hapo ndipo nipatapo mkanganyiko!
Mkuu Nguruvi3:
Mtu kuishi hivi au vile ni kutokana na kufungwa na Mfumo wa maisha! Mfumo wa maisha unapolea Ubinafsi basi watu nao watakuwa Wabinafsi, na mfumo unapolea UTU basi watu nao Watafikiriana! Swala muhimu ni kutambua kipi kinaunda mfumo?
1. Mfumo bora, ni ule uzaliwao kutokana na MAZINGIRA na NYAKATI za eneo husika! Mazingira ni Watu na Sura ya Nchi yao. Nyakati ni mahusiano yaliyopo katika eneo husika, baina ya mtu na mtu na baina ya watu na Sura ya Nchi yao! Hapa ndipo panapoibuka Falsafa, itikadi, mila, desturi, mienendo, mitazamo, imani, n.k, SASA vyote hivyo ili visikinzane katika maisha, yaani kusiwe na ukinzani wa kimazingira na kinyakati, basi MANTIKI inapaswa kutumika kuunda utaratibu wa jumla (mfumo) kuratibu maisha pasi kuwa na ukinzani! Na hakuna MANTIKI KUU duniani kushinda UTU! UTU ndio kila kitu! Hatusemi tufuate UTU sasa, ila tuseme TUTUMIE MANTIKI SASA KATIKA KUHOJI, KUCHAMBUA NA KUTAFAKARI HILI NA LILE, mwishowe tutakuja kugundua kumbe ndio UTU wenyewe! Mfano: Tunaweza kuhoji, Je, kuna mantiki yoyote ya kutembea mtupu? Tafakari yetu ikiegemea mantiki ya hilo, basi automatically utajikuta umeangukia kwenye UTU! Tuelewana hapa, UTU si kingine ila MANTIKI KUU! Lets live "LOGIC", mwishowe tutagundua kumbe ndio UTU wenyewe!
Mungu wetu anaita!
 
Wakuu,
Naona hoja zimegota na endapo ni hivyo basi tufanye majumuisho ya kila mchangiaji hususan nyuzi hii ya mwisho iliyokuwa na changamoto na vionjo vya kila aina. Darsa hili ni zito na nyote tunawashukuru sana sana.
Shukurani za kipekee ni pale mlipooonyesha ukomavu wa kupingana bila kugombana, hoja kwa hoja.
Hakika namna hii tunajenga ingawa si rahisi kuyaona matokeo yake moja kwa moja.

Nakumbuka mwaka mmoja uliopita tulikuwa na nyuzi iliyohusisha namna ya kutumia miundo mbinu ya reli kurahisha usafiri.
Nadhani tumeona watu wanavyoweza kuchukua mawazo na kuyafanyia kazi.
Nina uhakika yapo yanayochotwa hapa ni kwa vile hakuna haki miliki ya maandiko yenu.

Duru za siasa (mgongano wa mawazo) imetimiza mwaka mmoja juzi tarehe 26. Tunawapongeza wote walioshiriki kwa kuandika na kusoma, kukosoa na kupongeza kwani sote ni wadau muhimu sana wa safu hii.

Kabla hatujafanya majumuisho, ningedokeza kuwa tunazo mada mbili mbele yetu na hizi zinatugusa sana kama zilivyo nyingine.

1. Kujadili kuhusu shirikisho la EAC na utayari, ushiriki na hadhari kwa Tanzania

2. Kujadili nini kinatakiwa kiwepo au kisiwepo katika mchakato unaoendelea wa katiba hata kama hatukubali taratibu zilizotumika kuunda tume

Tunataraji kupata ushirikiano kama ilivyo ada.
 
Mnakasha unaendelea vizuri wengine tunafyonza shule ya ukweli kuna mwanajamvi Mchambuzi hajaonekana kabisa nina uhakika akitia mguu kwenye thread hii kabla haijafungwa kuna baadhi ya mambo anaweza kuyaweka sawa.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
Naona hoja zimegota na endapo ni hivyo basi tufanye majumuisho ya kila mchangiaji hususan nyuzi hii ya mwisho iliyokuwa na changamoto na vionjo vya kila aina. Darsa hili ni zito na nyote tunawashukuru sana sana.
Shukurani za kipekee ni pale mlipooonyesha ukomavu wa kupingana bila kugombana, hoja kwa hoja.
Hakika namna hii tunajenga ingawa si rahisi kuyaona matokeo yake moja kwa moja.

Nakumbuka mwaka mmoja uliopita tulikuwa na nyuzi iliyohusisha namna ya kutumia miundo mbinu ya reli kurahisha usafiri.
Nadhani tumeona watu wanavyoweza kuchukua mawazo na kuyafanyia kazi.
Nina uhakika yapo yanayochotwa hapa ni kwa vile hakuna haki miliki ya maandiko yenu.

Duru za siasa (mgongano wa mawazo) imetimiza mwaka mmoja juzi tarehe 26. Tunawapongeza wote walioshiriki kwa kuandika na kusoma, kukosoa na kupongeza kwani sote ni wadau muhimu sana wa safu hii.

Kabla hatujafanya majumuisho, ningedokeza kuwa tunazo mada mbili mbele yetu na hizi zinatugusa sana kama zilivyo nyingine.

1. Kujadili kuhusu shirikisho la EAC na utayari, ushiriki na hadhari kwa Tanzania

2. Kujadili nini kinatakiwa kiwepo au kisiwepo katika mchakato unaoendelea wa katiba hata kama hatukubali taratibu zilizotumika kuunda tume

Tunataraji kupata ushirikiano kama ilivyo ada.
Swala la EAC kusema kweli binafsi yangu siwezi kuchangia sana kutokana na imani yangu kuwa hatuwezi kwenda mbele ikiwa tumeshindwa kupiga hata hatua ya kwanza. Mimi naamini kabisa hapa tumekwama, hizi jitihada zote za kukuza uchumi ni sawa na yule kaa aliyeko ndani ya tenda anasubiri kukaangwa. Atahangaika weee kutoka nje ya tenga na wakati wote anaweka imani atakuja kutoka nje mwisho wa siku ataishia ktk kikaango cha mafuta ya moto.

UZALENDO kwanza, tuunde katiba inayotazama maslahi ya Watanzania mbele ya kila kitu. hakuna mtu wala nchi inayotakiwa kutuchagulia hata marafiki, sisi wenyewe tutachagua nani mwenye faida kwetu sisi. halafu maswala ya EAC yatafuata ikiwa lengo ni kutafuta Umoja na nguvu ya nchi za kiafrika kimataifa. Kama hatuna Umoja huo, ambao Kenya au Uganda watakuwa na misimamo yao pekee basi hii kitu EAC haina manufaa kwetu. Ujirani mwema tu unatosha...
 
Nadhani siku nguruvi3 anaweka hii post, nilikuwa nimeamka vibaya kwani nilisoma lakini nikashindwa kabisa to decipher maana ya "Sakata la AR", hivyo kushindwa kushiriki vizuri kwenye majadiliano. Sikutambua kwamba baadae mada hii ingekuja evolve kuwa kitu kingine zaidi and more stimulating to the mind. Asante sana nguruvi3 kwa hilo, na vile vile Ngongo kwa kunirudisha kundini.

Iwapo sijachelewa, ningependa kujadili dhana za UTAIFA NA UZALENDO. Kimsingi nakubaliana na wengi juu ya umuhimu wa haya katika Maendeleo, lakini nina tatizo moja: Sidhani kama wengi wetu tunaelewa kwamba Utaifa na Uzalendo ni vitu viwili tofauti ingawa vinaweza kutokea kwenye tumbo la mama mmoja. Nitajadili kwanini binafsi naona hivyo.

Nionavyo binafsi (ingawa naweza nisiwe sahihi kwa hili), watanzania wengi tunashindwa kutofautisha juu ya UTAIFA na UZALENDO. Kwa uelewa wangu, haya ni mambo mawili tofauti, na repercussion yake katika Maendeleo ya nchi, vile vile huwa tofauti sana. Nitafafanua.
Enzi za harakati za TANU, shughuli kuu iliyokuwa inaendelea ni Watanganyika kudai taifa lao kutoka kwa mkoloni. Ni dhahiri hapakuwa na taifa la Tanganyika kabla ya ukoloni bali mchanganyiko wa jamii mbalimbali kama historia inavyotueleza, na ni baada ya kikao cha wakubwa kule Berlin 1884/5, mkusanyiko wa jamii mbalimbali uliojikuta umeswekwa kwenye mipaka mipya ukapewa jina la Tanganyika kama KOLONI (sio Taifa). Ni miaka ya baadae chini ya TANU, TANU chini ya Mwalimu ikaanza harakati za kuligeuza kuwa TAIFA (sio koloni tena) huru. Hapa ndio UTAIFA ulipozaliwa na kufanikiwa kumtoa mkoloni. Tukumbuke kwamba at this stage (mid 1950s to early 1960s), suala la UZALENDO lilikuwa very premature!! Nitatoa mifano michache, tena kutoka kwa Mwalimu ambapo tukimsoma between the lines, tutagundua kwamba, wakati wengi ya wenzake Nyerere katika TANU walikuwa wanapigania UTAIFA, ni wachache waliokuwa wanapigania UZALENDO. Katika TANU na RAIA (1962) Mwalimu anasema hivi:

["Wakoloni walipokuwa hapa walipanga mishahara bila ya kujali uwezo wetu kuilipa mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapat ya watu wetu. Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali ya ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila ya kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo.

Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na ufahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tama yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila kujali maisha ya watu."].

Tutalijadili zaidi hili baadae, lakini kwanza tuangalia tofauti za msingi baina ya UTAIFA na UZALENDO.

Tikianza na UTAIFA, unaweza kuwa na maana mbili; Kwanza ni simply an attitude iliyopo miongoni mwa watu wa taifa fulani, inayobebwa na dhana mbalimbali kama vile utambulisho rasmi wa taifa (national identity), mwafaka kuhusu their common origin, muafaka kuhusu ethnic diversity iliyopo, mahusiano ya kitamaduni n.k; Lakini vile vile, UTAIFA unaweza kuangaliwa in the context ya mfano nilio toa juu ya TANU na harakati za uhuru – yani action taken na wananchi ndani ya koloni au taifa fulani kudai au kulinda uhuru wao, self determination n.k, lengo ikiwa ni kuhakikisha wanatitwalia mamlaka yote ya ndani (domestic) na nje (international affairs). Kama tunavyoelewa, Mwalimu alijaribu sana hili na kufanikiwa kiasi kikubwa (hasa katika kipindi cha miaka kumi ya mwanzo ya Ujamaa i.e. 1967 – 1977). Katika kipindi hiki, Mwalimu alifanikiwa sana KUHIMIZA, KUSHAWISHI na KUHAMASISHA watanzania to redeem haki yao ya kuishi in a better world by defending humanity, justice and equality.

Suala lingine muhimu kuhusu Utaifa ni kwamba, hujenga hisia kwamba "taifa letu" ni bora kuliko mataifa mengine – bila ya kujali madhaifu ambayo yanaweza ambatana na ubora wa taifa letu. Ndio maana mara nyingi (sio mara zote), Utaifa unaweza pelekea wananchi wa taifa husika kuwa very aggressive au kuwa under constant hostility dhidi ya mataifa mengine, hasa juu ya masuala yanayotishia their superiority, au uhuru wao, au rasilimali zao n.k.

Project ya kujenga UTAIFA chini ya Nyerere kwa bahati mbaya haikumalizika. Na mbaya zaidi ni kwamba, ni wakoloni wale wale ambao waliona project kama hizi kuwa ni threat to their interests, hasa kama Utaifa unaendana na UMMA kulinda rasilimali zao na kutafuta uhuru wao wa kiuchumi. [By the way wakoloni hawa hawajali sana kuhusu uhuru wa kisiasa kwani wametukamata pabaya kwenye suala la Liberal Democracy ambalo limepewa nafasi ya ‘midfield' katika mechi ya Maendeleo ya uchumi ambao ni wa mwendo wa Liberalization, Marketization and Privatization.]. Lakini tunashuhudia jinsi gani suala la ‘national interest' linapopewa kipaumbele huko kwenye mataifa yao, hasa iwapo taifa jingine linaingia sekta nyeti kwa nchi zao! Ebu sasa tujadili kidogo dhana ya Uzalendo.

UZALENDO – dhana hii ni tofauti kidogo na ile ya UTAIFA, ingawa inaweza kutoka kwenye tumbo moja la uzazi na UTAIFA. Tofauti kubwa baina ya dhana hizi mbili ni kwamba – kwa mfano, wakati UTAIFA unahimiza zaidi imani ya Sisi ni Bora Kuliko Wao, Uzalendo ni simply:
· Hali ya kujivunia what we have accomplished as a nation, lakini muhimu zaidi not giving up kama we are not satisfied with the current progress (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Sisi ni taifa la wakata tamaa!!!
· Uzalendo pia is about giving back to your country or society (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Wanaochuma kihalali au kuiba hawawekezi nchini, wanaenda wekeza nje au ficha mali nje ya nchi.

· Uzalendo ni imani kwa serikali yako kwa maana kwamba Actions and Policies za serikali zina akisi (reflect) matakwa, matumaini, na matarajio ya walio (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Imani kwa serikali ya CCM iliyokaa madarakani kwa miaka zaidi ya 50 imeshuka sana, watu wamechoka na wanataka mbadala wa CCM!!

· Uzalendo is also about "What One Can DO for His/Her Country, na sio What Can the country do for me/him/her (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Serikali ya CCM imekuwa serikali ya kutembeza bakuli nje ya nchi miaka nenda, miaka rudi, na tabia hii imejijenga hata miongoni mwa wananchi walio wengi. Dhana ya uchapa kazi kwa ajili ya taifa lako haipo tena, na badala yake, watu wanasubiri vya dezo.

· Uzalendo unathamini zaidi UWAJIBIKAJI, sio kama UTAIFA ambao zaidi unalenga Uaminifu kwa nchi yako. Mzalendo uenda zaidi ya kuilinda nchi yake; Mzalendo yupo tayari kufanya lolote liwezekanalo kuijenga nchi yake; (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Sote tunajua moja ya vikwazo vikubwa kwa Maendeleo yetu ni tatizo la watu (hasa viongozi) kutowajibika…

· Mzalendo ana huruma na nchi yake pamoja na mali ilizojaliwa; na ana mahaba/mapenzi ‘unconditional nchi yake; (JE TUPO WAZALENDO KIASI GANI KWA MAANA HII)? Kwa wenzetu nchi zilizoendelea, wao hupenda na kuthamini kila kitu kilicho chao, kuanzia lugha, utamaduni, elimu, huduma zao za kijamii kama vile afya n.k. Lakini kwetu sisi, lugha ya Kiswahili hatuikubali kwa dhati bali kisiasa tu; pia hatuthamini utamaduni wetu bali wa wageni; vilevile hatujivunii sekta zetu za elimu au afya, badala yake tukipata uwezo kidogo tu (kwa njia halali au ufisadi), tunawapelekwa watoto wetu nej au shule za kimataifa na kuwaachia maskini waende shule za kata; huduma za kiafya - ni hivyo hivyo, tukipata kikohozi kidogo tu, tunakimbilia nje - India, South Africa, Ujerumani, n.k, na kuachia maskini wategemee hospitali za kina Ullimboka;

Kwahiyo mimi sidhani kama sisi tuna Uzalendo, na kama upo badi sio wa dhati bali wa shingo upande; vinginevyo suala la Utaifa, wengi tunalo, ndio maana hata wakubwa wakisikia mipaka yetu inavamiwa na Malawi, tunajumuika nao katika Utaifa juu ya hilo, lakini sio Uzalendo kwani ikitokea mgeni akachimba mafuta ziwa nyasa, hatugawani keki ta taifa kama taifa. Kwa watanzania wengi, Uzalendo kwa bahati mbaya sana unajidhihirisha zaidi kwenye mazingira ya kikabia, sio ngazi ya taifa.

Tunaondokaje katika tatizo hili? Huu ni mjadala mwingine lakini ni muhimu tuka kamilisha project ya Utaifa aliyoianza Nyerere in the 1960s – hasa kulinda uhuru wetu na kujitwalia mamlaka kamili on ‘domestic' and ‘international affairs'; halafu tuingio kwenye Uzalendo. Hii inaonyesha ni jinsi gani bado tuna kazi kubwa mbele yetu, na changamoto inakuwa kubwa zaidi pale tunapobaini kwamba kwa miaka karibia 30 sasa, Tanzania sio taifa la kujitambua tena. Ni muhimu tuamue: What type of future society do we want to build in Tanzania? Tukipata jibu, tutakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kusonga mbele kama Taifa la Wazalendo.
 
Mchambuzi karibu na wala hujachelewa.

Kuhusu Utaifa na uzalendo, nikushukuru kwa maelezo yako mwanana.
Nachelea kukubaliana na hoja yako kuwa hakuna uzalendo nchini. Hata hivyo nakubaliana na ukweli kuwa uzalendo umepungua.

Kwa wale walioishi nyakati za 1978 na kuona vita vya Kagera, mimi naweza kusema ile ilikuwa ni testimony ya utaifa na uzalendo. Wapo waliotoa nafsi zao, wapo waliotoa mali zao na wapo waliotoa jasho na kile wasiokuwa nacho.
Ule ni uzalendo ninaoweza kujiuliza, umekwenda wapi!

Nyuma ya uzalendo ule kulikuwa na uongozi kwasababu uzalendo hauteremki bila muongozo na hamasa.
Nasema uzalendo umpepungua na si kutoweka kwa kuzingatia mfano wako wa vurugu za Malawi.

Nakuhakikishia kuwa litokee lisilotarajiwa(mungu aepushe) bado wapo watakaokubali kutangulia mbele kwa uzalendo wao na utaifa. Kwa kiasi gani ! hilo linabaki kuwa swali. Maana ya hii ni kuwa uzalendo umepungua lakini bado upo.

Tunajenga vipi uzalendo linabaki kuwa swali gumu kama lile la kujenga UTU. Hivi ni vitu visivyoshikika na vibaki kuwa vya kifikra na pengine 'kiroho'. Ninachoweza kusema ni kuwa ni lazima tuwe na uongozi wa kutuwekea misingi ya uzalendo.
Je, uongozi upo? Je sisi wenyewe tufanye nini. Wapi pa kuanzia kuhusu hili.

Kuhusu utaifa nadhani utamuunga mkono Mkandara katika bandiko lake 311 kuhusu maswali yaliyojitokeza bandiko 310.

Labda nikuulize swali moja, tunamaliziaje kazi ya ujenzi wa utaifa kwanza. Wapi pamebaki au pameharibika na kwanini.
 
Back
Top Bottom