Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

YANAYOJIRI ARUSHA KISIASA: KULIKONI?

#65 hapo juu nilieleza kuhusu majimbo moto na yenye ushawishi wa kisiasa nchini. Nilisema CCM itafanya kila iwezalo ili kushinda Arumeru. Kilichotokea ni wingi wa kura uliokuwa dhahiri kuwa CDM wameshinda. Pamoja na ulizini madhubuti wingi huo wa tofauti ya kura uliweka mazingira 'magumu

Kwa msingi huo CCM ilipeleka timu yote tena ikitumia rsilimali za taifa ili kulitwaa jimbo la Arumeru ambalo lilikuwa ni ngome isiyohitaji kampeni kwao.

Arusha ni 'hot spot' kutokana na ushawishi wake katika duru za siasa nchini.
Kama ilivyokuwa kwa Tarime na wimbi la mageuzi kanda ya ziwa, Arusha ni sehemu muhimu sana kisiasa.
Ambukizo lake linatoka Karatu na Kilimanjaro sasa limeingia Arumeru.
Hakuna jimbo salama tena mikoa ya Kilimanjaro na Arusha

Ni muhimu kukumbuka kuwa mbio za urais 2015 zinategemea sana wagombea watakavyojipanga na kuungwa mkono.
Jimbo la Arusha lilikuwa na mgombea mwana mama Matilda Buriani ambaye anahusishwa sana kisiasa na waziri mkuu aliyejiuzulu Lowassa.

CCM wanafahamu kuchukuliwa kwa ngome zao watakuwa wamepoteza ilenafasi ya kwenda vijijini na sehemu nyingine kwasababu itabidi wapige kambi mikoa michache yenye ushawishi kama Arusha, Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.
Wanaelewa hali haitabiriki Kagera wala Kigoma na Iringa ni tia maji tia maji.

Kwa maneno mengine ngome imeingiliwa na kuvunjwa.Mikoa kama ya Tanga, Mtwara, Pwani, Dodoma, Sumbawanga, Katavi itabaki kuwa mikononi mwao, swali ni je ina wapiga kura wakutosha achilia mbali wenye ushawishi?

Kutenguliwa kwa ubunge wa Mh Lema kumeleta kiwewe sana kambi ya upinzani.
Sote tunaimani na yombo vyetu vya sheria maana hata Chadema wasipotendewa haki huenda huko.
Pamoja na imani yetu hakuna shaka kuwa mfumo wetu wa sheria unawalakini mkubwa sana.
Vongozi na majaji huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.

Wasi wasi siyo tu unasemwa na watu mitaani, hata jaji mkuu mstaafu Barnabas Samata, Nyalali wameshasema hayo.
Wiki mbili zilizopita jaji mkuu wa Tanzania Mh Othman alikaririwa akisema serikali inaingilia utendaji wa mahakama.
Ingawa hakusema ni vipi lakini inatosha sana kufahamu kuwa kuna tatizo na limesmwa tena ndani ya wiki mbili tu zilizopita

Tukirudi nyuma tunakumbuka hukumu ya marehemu jaji Rugakingira kuhusu mgombea binafsi. Hadi sasa hakuna haki iliyotolewa na mahakama. Jaji Augustino Ramadhani ameingia na kuikuta kesi na amestaafu na kuiacha.
Wazungu wanasema 'justice delayed justice denied' ucheleweshaji wa sheria ni unyimaji wa haki kwa tafsiri isiyo rasmi.

Tumeshuhudia msuguano wa mihimili ya dola kama bunge na serikali na ilifikia mahali mahakama ikawa katika msuguano na bunge. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo katika mgawanyo wa madaraka na serikali ina nguvu sana katika kutunga sheria na kusimamia sheria hizo hizo ikiwa ni pamoja na kutoa haki.

Kilichonishtua kuhusu hukumu ya Lema ni jinsi Ikulu ilivyojibu haraka sana tuhuma hizo chini ya masaa 12 tangu zitolewe.
Ikulu yetu haina utamaduni huo hata kidogo. Hata pale Rais anapohusishwa na kashfa nzito na zenye aibu hatujawahi kuona Ikulu ikijibu au kutolea ufafanunuzi. Hili la Mh Lema lina nini? Kwanini kurugenzi ya mawasiliano iwe 'effective na efficient' kwa Lema? Kwani Lema ni nani zaidi ya mbunge nchi hii. Hapa lipo jambo.

Tukiunganisha dot yanaweza kupatikana majibu ya kweli na ya uongo lakini yote yakawa ya kweli kimazingira.
Haiwezekani Rais ahusishwe na Kagoda Ikulu ikae kimya, ahusishwe na Richmond Ikulu ikae kimya n.k halafu hili la Lema lijibiwe masaa chini ya 12 tangu kutokea? Why Lema! who is Lema? Kuna jambo

Kisiasa maana yake ni kuwa tuhuma hizo zitatibua mpango mzima wa kulitwaa jimbo la Arusha. Wananchi wataingiwa na hasira na kupiga kura ya hasira endapo tuhuma hizo zitaachwa zienee vichwani mwao.
Huo ndio mtazamo wangu kisiasa na kila mmoja wetu anaweza kuwa na wake.

Chadema wafanye nini?
Ningewashauri CDM wasikate rufaa kwasababu mazingira yanaashiria kutokuwa na haki, yamegubikwa na mazingira yanayotatiza sana. Waitumie fursa waliyopewa na Ikulu kufikisha kesi Mahakama ya juu ya wananchi.
Kitengo chao cha uenezi kifanye kazi hiyo kikamilifu.

Kwa vile bado kuna joto la Arumeru,CDM watumie nguvu hiyo kukabiliana na uchaguzi ndani ya siku 90.
Tatizo la kukata rufaa ni kuwa hukumu inaweza kutolewa mwezi wa 12. Wakati huo suala litakuwa mahakamani na ni kosa la kisheria kulizungumzia. Hapo CDM watakuwa wamefungwa mdomo wakati CCM wakijijenga kutokana na makovu ya Arumeru. Hukumu ikija kama inavyotarajiwa basi CDM watakuwa wamepoteza nafasi iliyo wazi kwa sasa.

Chadema wafikirie sana mtego huu wa CCM na serikali yake. Kinachofanyika ni kupitisha muda 'buy the time' suala likiwa mahakama kuu, wakati huo huo CDM wakiwa wamefungwa midomo kisheria na CCM wakijijenga.

Kupitisha muda kuna maana ya kuua nguvu na moto wa kisiasa walio nao CDM kwa sasa na kampeni zikianza mathalani mwezi wa 12 hakuna atakayekumbuka Arumeru na wote watakuwa wameanza upya.

Tusemezane
 
YANAYOJIRI ARUSHA KISIASA: KULIKONI?

#65 hapo juu nilieleza kuhusu majimbo moto na yenye ushawishi wa kisiasa nchini. Nilisema CCM itafanya kila iwezalo ili kushinda Arumeru. Kilichotokea ni wingi wa kura uliokuwa dhahiri kuwa CDM wameshinda. Pamoja na ulizini madhubuti wingi huo wa tofauti ya kura uliweka mazingira 'magumu

Kwa msingi huo CCM ilipeleka timu yote tena ikitumia rsilimali za taifa ili kulitwaa jimbo la Arumeru ambalo lilikuwa ni ngome isiyohitaji kampeni kwao.

Arusha ni 'hot spot' kutokana na ushawishi wake katika duru za siasa nchini.
Kama ilivyokuwa kwa Tarime na wimbi la mageuzi kanda ya ziwa, Arusha ni sehemu muhimu sana kisiasa.
Ambukizo lake linatoka Karatu na Kilimanjaro sasa limeingia Arumeru.
Hakuna jimbo salama tena mikoa ya Kilimanjaro na Arusha

Ni muhimu kukumbuka kuwa mbio za urais 2015 zinategemea sana wagombea watakavyojipanga na kuungwa mkono.
Jimbo la Arusha lilikuwa na mgombea mwana mama Matilda Buriani ambaye anahusishwa sana kisiasa na waziri mkuu aliyejiuzulu Lowassa.

CCM wanafahamu kuchukuliwa kwa ngome zao watakuwa wamepoteza ilenafasi ya kwenda vijijini na sehemu nyingine kwasababu itabidi wapige kambi mikoa michache yenye ushawishi kama Arusha, Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.
Wanaelewa hali haitabiriki Kagera wala Kigoma na Iringa ni tia maji tia maji.

Kwa maneno mengine ngome imeingiliwa na kuvunjwa.Mikoa kama ya Tanga, Mtwara, Pwani, Dodoma, Sumbawanga, Katavi itabaki kuwa mikononi mwao, swali ni je ina wapiga kura wakutosha achilia mbali wenye ushawishi?

Kutenguliwa kwa ubunge wa Mh Lema kumeleta kiwewe sana kambi ya upinzani.
Sote tunaimani na yombo vyetu vya sheria maana hata Chadema wasipotendewa haki huenda huko.
Pamoja na imani yetu hakuna shaka kuwa mfumo wetu wa sheria unawalakini mkubwa sana.
Vongozi na majaji huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.

Wasi wasi siyo tu unasemwa na watu mitaani, hata jaji mkuu mstaafu Barnabas Samata, Nyalali wameshasema hayo.
Wiki mbili zilizopita jaji mkuu wa Tanzania Mh Othman alikaririwa akisema serikali inaingilia utendaji wa mahakama.
Ingawa hakusema ni vipi lakini inatosha sana kufahamu kuwa kuna tatizo na limesmwa tena ndani ya wiki mbili tu zilizopita

Tukirudi nyuma tunakumbuka hukumu ya marehemu jaji Rugakingira kuhusu mgombea binafsi. Hadi sasa hakuna haki iliyotolewa na mahakama. Jaji Augustino Ramadhani ameingia na kuikuta kesi na amestaafu na kuiacha.
Wazungu wanasema 'justice delayed justice denied' ucheleweshaji wa sheria ni unyimaji wa haki kwa tafsiri isiyo rasmi.

Tumeshuhudia msuguano wa mihimili ya dola kama bunge na serikali na ilifikia mahali mahakama ikawa katika msuguano na bunge. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo katika mgawanyo wa madaraka na serikali ina nguvu sana katika kutunga sheria na kusimamia sheria hizo hizo ikiwa ni pamoja na kutoa haki.

Kilichonishtua kuhusu hukumu ya Lema ni jinsi Ikulu ilivyojibu haraka sana tuhuma hizo chini ya masaa 12 tangu zitolewe.
Ikulu yetu haina utamaduni huo hata kidogo. Hata pale Rais anapohusishwa na kashfa nzito na zenye aibu hatujawahi kuona Ikulu ikijibu au kutolea ufafanunuzi. Hili la Mh Lema lina nini? Kwanini kurugenzi ya mawasiliano iwe 'effective na efficient' kwa Lema? Kwani Lema ni nani zaidi ya mbunge nchi hii. Hapa lipo jambo.

Tukiunganisha dot yanaweza kupatikana majibu ya kweli na ya uongo lakini yote yakawa ya kweli kimazingira.
Haiwezekani Rais ahusishwe na Kagoda Ikulu ikae kimya, ahusishwe na Richmond Ikulu ikae kimya n.k halafu hili la Lema lijibiwe masaa chini ya 12 tangu kutokea? Why Lema! who is Lema? Kuna jambo

Kisiasa maana yake ni kuwa tuhuma hizo zitatibua mpango mzima wa kulitwaa jimbo la Arusha. Wananchi wataingiwa na hasira na kupiga kura ya hasira endapo tuhuma hizo zitaachwa zienee vichwani mwao.
Huo ndio mtazamo wangu kisiasa na kila mmoja wetu anaweza kuwa na wake.

Chadema wafanye nini?
Ningewashauri CDM wasikate rufaa kwasababu mazingira yanaashiria kutokuwa na haki, yamegubikwa na mazingira yanayotatiza sana. Waitumie fursa waliyopewa na Ikulu kufikisha kesi Mahakama ya juu ya wananchi.
Kitengo chao cha uenezi kifanye kazi hiyo kikamilifu.

Kwa vile bado kuna joto la Arumeru,CDM watumie nguvu hiyo kukabiliana na uchaguzi ndani ya siku 90.
Tatizo la kukata rufaa ni kuwa hukumu inaweza kutolewa mwezi wa 12. Wakati huo suala litakuwa mahakamani na ni kosa la kisheria kulizungumzia. Hapo CDM watakuwa wamefungwa mdomo wakati CCM wakijijenga kutokana na makovu ya Arumeru. Hukumu ikija kama inavyotarajiwa basi CDM watakuwa wamepoteza nafasi iliyo wazi kwa sasa.

Chadema wafikirie sana mtego huu wa CCM na serikali yake. Kinachofanyika ni kupitisha muda 'buy the time' suala likiwa mahakama kuu, wakati huo huo CDM wakiwa wamefungwa midomo kisheria na CCM wakijijenga.

Kupitisha muda kuna maana ya kuua nguvu na moto wa kisiasa walio nao CDM kwa sasa na kampeni zikianza mathalani mwezi wa 12 hakuna atakayekumbuka Arumeru na wote watakuwa wameanza upya.

Tusemezane
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli, nikukusoma humu, najisaikia kama niko darasani!, japo sikubahatika kusoma political science, kupitia uchambuzi kama huu, kufikia 2015 nita graduate!.

Hivi hawa Chadema waliomo humu huwa wanakusoma?, kuna nondo unamwaga humu zinahitaji implemtation yao ili kujihakikishia 2015 njia ni nyeupe pee!.

Asante, endelea!.

Pasco.
 
Changamoto inayovikabili vyama vya upinzani ni migogoro ndani yake na uendeshaji wa vyama kama taasisi za kisiasa.
Hatari kubwa ni ile itakayotokana na wimbi la wanaCCM wanaojiandaa kuondoka. Hawa wapokelewe kama wanachama na si viongozi kwasababu kuhama kwao si kwa kufuata itikadi au kuongoza mabadiliko ni kuchumia tumbo na wengine wakiwa mamluki.

Tusemezane

Mkuu, hakika hitimisho lako ni la kuzingatia sana, haswa kwa kuzingatia kwamba wanaCCM watakaoweza kujitoa na kujiunga na CHADEMA wanaweza kuwa ni wale "wazito". Hivyo pengine kupelekea CHADEMA kuvutika kuwatunuku nafasi nyeti za chama, kwa kuamini kwamba wanaweza kusaidia katika kukitangaza na kukiweka chama midomoni mwa watanzania walio na imani na "wazito" hao.
 
KATIBA:TUME YENYE UTATA NA USHIRIKI WA WAZANZIBAR

Awali niseme kabisa mimi sikuridhika na mchakato mzima wa katiba hata pale wapinzani wakiongozwa na Chadema walipokubali na kuupitisha bungeni. Katiba ni chombo cha wananchi na kinatakiwa kiundwe na kwaongoza wananchi

Baada ya shinikizo la kudai katiba mpya, nilishtushwa sana kusikia mwenyekiti wa CCM ambayo imekataa katiba hiyo miaka nenda rudi akijinasibu kusimamia mageuzi hayo. Mageuzi ambayo mwenyekiti wa tume ni Jaji Warioba aliyewahi kuyakataa alipokuwa mwanasheria mkuu.

Tatizo ninaloliona ni kuwa mchakato wa kupata katiba unatakiwa uratibiwe na wananchi kwa kupitia taasisi zao na uwakilishi mbali mbali. Serikali ni mdau muhimu kama ilivyo bunge na Mahakama. Serikali haipaswi kuratibu utaratibu bali kufuata utaratibu ulioratibiwa na wananchi wenyewe. Serikali inapaswa kusimamia taratibu za kupatikana katiba hiyo na si kuandaa kuratibu na kisha kushiriki kama mdau. Hapa ni kuwa na kocha mchezaji ambaye ni refarii pia!!
Huo ndio mtazamo wangu tangu awali.

Niliwahi kuwaasa CDM kuwa mazungumzo yao na Rais ambaye chama chake kilikataa mabadiliko mara zote hayalengi kuleta tija. Nikawauliza hivi kwanini tume iundwe na rais ambaye ni mdau wa kuandika katiba?

Hata mara ya pili mswada ulipoletwa na kuungwa mkono na wabunge wote bado nikabaki na swali, kwanini tume iliyo huru ikusanye maoni halafu yapelekwe kwa Rais? Ili yafanyiwe nini. Maana yake Rais kwa mujibu wa mswada anaweza kuwa kikwazo cha maoni ya watu milioni 40. Ndiyo anauwezo huo hata kama tutaficha vichwa vyetu ardhini

Swali la pili nililouliza, hivi tunatengeneza katiba ipi? Ya Tanganyika au Tanzania?
Kuna malaumbano ya jinsi muungano unavyokwenda. Ni dhahiri kuwa Wzbar kwa maneno na vitendo hawautaki muungano. Imejidhihiri mara nyingi kwa wao kuchukua maamuzi hata kama ni ya muungano na kujifanyia kivyao.

Chuki yao imefikia mahali wanachoma moto Watanganyika na mali zao na waliohusika hakuna hata mmoja anayechukuliwa hatua mbali na kuwaweka mahabusu kwa siku kadhaa. Hii maana yake serikali ya mapinduzi Zbar inayaunga mkono matendo maovu wanayofanyiwa Watanganyika wanaoishi huo na kwa unafiki tu wanajifanya hawakubaliani na maovu

Juzi wamedhidhirsha chuki zao baada ya kutangaza ubaguzi usiohitaji certificate au diploma kuubaini.
Wameweka wazi kuwa adui yao kwenye ajira ni mbara, siyo mkongo, Mkenya, Mchina,, Mwarabu au Mhindi
Hili limekuja baada ya hoja ya mafuta kufa kutokana na nchi za ukanda huu kugundulika kuwa na uwezekano wa mafuta ya kutosha. Pwni ya Mtwara, ziwa Tanganyika, Uganda na Kenya,hivyo kiburi kischo na usomi kimekoma

Niseme tu kuwa Wzbar wanaupenda muungano pale wanapofaidika. Wakihitaji ajira muungano kwao mzuri, wakihitaji biashara muungano kwao mzuri , wakihitaji mishahara kwa kodi za Watanganyika kwao mzuri, watoto wao wakisoma kwa kodi za Watanganyika muungano mzuri, wakipewa mapande ya ardhi muungano safi.

Kwa maneno machache wanataka kufaidika na muungano bila kuchangia chochote.
Ndiyo maana huwa hawasemi muungano ufe, la hasha wanataka serikali tatu au mkataba wa muungano, vitu ambavyo havielezeki kwa mantiki ya fikra komavu.
Vinginevyo wao ni changu ni changu chako ni chetu. Halii hii haivumiliki na imeshaleta hasira sana miongoni mwa Watanzania bara.

Kwa maneno mengine wanachotaka wenzetu ni muungano utakaowanufaisha basi. Mathalan, Mkataba wa muungano ni kujumuisha yale yanayowagusa, serikali tatu ni kuwa na ya tatu inayoshughulikia matatizo yao. Ukiwauliza serikali ya tatu itaendeshwaje, hawana jibu kwasababu wao ni wapokeaji na si watoaji,lakini hata kama ni kutoa watatoa nini!!

Idadi ya Wbar ni takribani 1.5M ukilinganisha na Milioni 40. Uchumi wao ni kidogo hata kufikiri wanaibiwa ni kichekesho.
Wabunge wao wanawakilisha mitaa yenye watu 10,000. Kwa maana ya kuwa jimbo la Ubungo tu ni sawa na uwakilishi wote wa wabunge wa Jamhuri kutoka Zbar.

Tume ya kukusanya maoni ya katiba imeshaundwa hata kama wengine hatukubaliani na utaratibu uliotumika. Kinachoshangaza ni kuona wajumbe 15 kutoka Zanzibar na 15 kutoka bara.

Hii maana yake ni kuwa maamuzi yatakayohitaji kura basi yatajumisha nusu ya Wazanzibar.
Uwakilishi wa watu milioni unakuwa sawa na milioni 40.

Swali la kujiuliza ni kuwa hii ni katiba ya nini? Nauliza kwasababu Wzbar wamekuwa wanafanya maamuzi hata ya kukiuka katiba ya JMT kwa kiburi tu. Wamekuwa wakijemega kutoka JMT isipokuwa tu pale wanapofaidika.
Sasa hii katiba inamhusu nani zaidi, Mtanganyika au Mzbari asiyeutambua muungano na mwenye serikali yake inayofuata taratibu zake?

Kwanini Wazanzibar washikirishwe katika kuandika katiba waisoitambua? Kwanini watu milioni 1 wapewe uwakilishi wa watu milioni 40 na Mbunge wa Ubungo asipewe nafasi katika kamati ili hali anawakilisha idadi kubwa zaidi kuliko Zbar yote?

Ni kwanini wzbar wasiulizwe kama wapo tayari kwa muungano au waachwe waende zao kwanza ili tuandike katiba inayokidhi mazingira yetu? Ni kigezo gani kimetumika kupata wajumbe 15 kutoka Zbar!

Je katiba tunayotegemea iandikwe itakidhi haja ya kumaliza vurugu za wzbar? Je chuki inayoonyeshwa kwa Watanganyika kama kuchomwa moto na kubaguliwa katika ajira zitamalizwa na katiba mpya?

Ikifika hapo naliona tatizo mbele ya safari.

Tusemezane
 
EALA: TUNAGOMBEA NINI? WAPINZANI MLIKUWA WAPI?

Uchaguzi wa wabunge wa Afrika mashariki unafanyika kesho kukiwa na taarifa za wapinzani kujitoa.
Ni uchaguzi ambao ni tofauti kidogo na huko nyuma kimazingira.
Tunakumbuka katika miaka ya 90 mfumo wa vyama vingi ulipoanza idadi ya wabunge wa vyama vya upinzani ilikuwa ni ya kuhesabu. Msisimko wa kisiasa bado ulikuwa ndani ya chama tawala na wakati huo CCM haikuwa na upinzani

Hakika demokrasia yetu bado ni changa lakini hatua imepigwa. Idadi ya wabunge wa upinzani sasa ni ya kiwango cha kutishia upatikanaji wa 2/3 majority. Nguvu yao katika bunge na sauti zao zinasikika nyikani.
Kikubwa zaidi ni ile nguvu ya umma iliyopo nyuma ya upinzani ambayo sasa imeligawa taifa kiitikadi.

Ni uzembe na ujinga kama yupo au wapo watu wanaodharau nguvu ya upinzani. Chama tawala kinajua hili fika na hakika viongozi wake hawapati usingizi kila wakifikiria upinzani. Ni kwa muktadha huo lazima busara zitawale katika mambo yanayolihusu taifa ili kujenga na si kuleta ufa.

Wabunge wa EA wanakwenda kuliwakilisha taifa. Hata kama wote watatoka CCM au upinzania agenda yao ni kusimamia masilahi ya taifa. Lakini inaleta maana zaidi pale pande zote zinapounganisha nguvu za utaifa na kusahau tofauti zao za kiitikadi. Tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?

Uchaguzi ni lazima uongozwe na kanuni, kanuni zilizoandikwa na wanadamu tena watanzania na zikakubaliwa na Watanzania. Kanuni hizi siyo maandiko matakatifu yasiyohitaji kuangaliwa kila ikabidi. Hivi kwanini busara zisitumike kuzirejea kanuni hizo ili tuwe na timu moja ya taifa itakayotuwalikisha kama 'taifa stars' na wala siyo yanga au simba?

Kuna kitu gani kinacholeta UCCM au Upinzani na si utanzania? Kuna maana gani ya kupeleka timu ambayo si ya taifa kutuwkilisha? Hivi ni nani atakayefurahi timu yote ya taifa ikiwa imechaguliwa kwa kanuni za mwaka 1962 tena si kwa uwezo wa wachezaji ! halafu ikaitwa timu ya taifa?

Tunafahamu kinachogomba hapa si masilahi ya taifa ni masilahi binafsi kwa gharama ya taifa. Tutakapokuwa na watu waisoweza kutetea taifa dhidi ya wanachama wa EA ambao wanaiangalia Tanzania kwa jicho upande, tutakuwa tumedhulumu nafsi zetu na za vizazi vijavyo.

Rai yangu, busara zitumike kusikiliza na kuangalia mazingira kama yanaruhusu ubabe. Hii si Tanzania ya mwaka 62,72, 82 au 92. Ni Tanzania yenye kizazi kipya kilicho na njaa na matamanio ya mabadiliko.Twende na wakati na kizazi kabla hatujazua tusiyoyatarajia. Sijui mbele tunakoelekea kukoje kwa mwendo huu wa kuligawa taifa.

Kwa upande mwingine wapinzani wamekuwa wazito sana wa kufikiri. Hapa nina haki ya kusota kidole kwa Chadema kwani ndicho chama kikuu cha upinzani. Sidhani vyama havina kalenda za kujua matukio. Ubunge wa EA ulijulikana mapema sana wala haukutokea kama mvua.

Mara zote nimekuwa nikisema, upinzani ni kama mkusanyiko wa watu na si taasisi. Haiwezekani chama kikuu cha upinzani ndani ya taasisi yake kusiwe na watu wa mkakati au mipango wanaoweza kuona kile wengi wasichokiona.

Leo Chadema wanakimbilia koti kuu ya Afrika mashariki! Yaani hawakujua kuwa walipaswa kuliangalia jambo hili mapema sana. Kama kungekuwa na umakini uchaguzi unaolazimishwa kesho ungeshawekewa pingamizi. Kwenda koti kuu lilikuwa jambo la kufanyika mapema kadri ilivyowezekana. Bahati mbaya hakuna anayeliona na kila siku ni kutuhumiana tu na mizozo ndani ya vyama hivyo

Wapinzani iangalieni dunia kutoka pande zote, muwe na fikra za mwaka 2020 na si kila jambo kukurupuka kana kwamba mlikuwa katika usingizi wa Pono. Ingawaje hamjachelewa lakini hamku-act kama taasisi. Nitty gritty!

Tusemezane
 
Nguruvi3: hapo juu nilieleza kuhusu majimbo moto na yenye ushawishi wa kisiasa nchini. Nilisema CCM itafanya kila iwezalo ili kushinda Arumeru. Kilichotokea ni wingi wa kura uliokuwa dhahiri kuwa CDM wameshinda. Pamoja na ulizini madhubuti wingi huo wa tofauti ya kura uliweka mazingira 'magumu kuibwa kwa kura
Nguruvi3: CCM wana hali ngumu kwa kuupoteza mkoa wa Arusha, na madhara yake sasa yanasambaa. Ninaweza kusema chaguzi yoyote mkoani Arusha kwa siku za karibuni haiwezi kuwasaidia tena CCM. Madhara ya uchaguzi sasa yameambukiza sehemu kama Mwanga na Same, Simanjiro na Manyara. Arumeru ilikuwa ngome kubwa, na kitendo cha kuvunjwa ni hali inayomtisha kila mwana CCM hata kama hakubali hadharani. Kama nilivyosema awali hii ni hot spot na CCM wamepoteza
Changamoto inayovikabili vyama vya upinzani ni migogoro ndani yake na uendeshaji wa vyama kama taasisi za kisiasa.
Hatari kubwa ni ile itakayotokana na wimbi la wanaCCM wanaojiandaa kuondoka. Hawa wapokelewe kama wanachama na si viongozi kwasababu kuhama kwao si kwa kufuata itikadi au kuongoza mabadiliko ni kuchumia tumbo na wengine wakiwa mamluki

Katika mabandiko yaliyopita tumekuwa tunajadili mwelekeo wa kisiasa kama nilivyochua nukuu chache kutoka katika mabandiko # 66, 70 na 72.

Miongoni mwa mwambo tuliyosema ni suala la maambukizo ya kisiasa(political contagion), na kwamba CCM wanalifahamu vema. Walipotuma kikosi kamili Arumeru walijua hilo. Tulisema, Arusha ni mkoa wenye ushawishi sana katika siasa za nchi yetu. Kijiografia, Arusha inapakana na mikoa mingi sana na ni kituo muhimu sana cha biashara hivyo kuongeza mwingiliano wa watu kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Tunachokiona sasa ni kitu kinachowatia wasi wasi sana CCM na kutoa matumaini kwa Upinzani. Kuhama kwa watu kutoka chama kimoja hadi kingine hakumaanishi ni utiifu wao juu ya sera au itikadi. Ni dalili ya kuchoka na kutafuta mbadala.

Kwa siasa za nchi yetu, si ajabu nusu yao wakarudi kule walikohama. Jambo moja la muhimu ni kuwa imefika mahali ambapo watu hawaogopi tena kusema mimi siyo CCM. Imefika mahali watu wametambua kuwa upinzani si uharamia kama walivyoaminishwa, imefika mahali watu wanarudisha kadi hata kama ni kwa wiki moja lakini maana yakae ni pana sana.

Watu sasa wanatafuta mbadala baada ya kubaini kuwa kufanya jambo moja kwa karne nzima bila mageuzi ni kujidanganya. Wimbi hilo la wananchi linawatia hofu sana wale waliobeba mikate minono ya CCM kama wabunge.

Hali hiyo ndiyo inawalazimisha wasiamame na kusema 'hovyo' bungeni dhidi ya chama chao. Hiyo haina maana kuwa wamekosa utiifu, la hasha kila kilichofanywa na serikali yao wameshiriki, kwa bahati mbaya sana muda unawatupa mkono

Viongozi sasa wanatafuta mbadala iwe kwa itikadi za kisiasa au kujifanya. Wanachojua sasa ni kuwa ile chanjo ya CCM ijulikanayo kama 'CCMvaccine' sasa haifanyi kazi. Utegemezi wa hisani ndani ya CCM haupo ila ni jino kwa jino.

Survival inategemea upo kundi gani. Utegemezi wa' kura za vijiji' kwa msaada wa tume ya uchaguzi haufanyi kazi, wapo wanaotumia piki piki kulinda kura zao. Sasa hamkani si shwari tena kila mtu na msalaba wake. Ndicho kinachotokea

Hata hivyo vyama vya upinzani vichukue tahadhari kubwa sana dhidi ya wanachama wanaohama.
Siyo wote wanaopenda mageuzi. Wapo mamluki ndani yake.

Pili, ujio wa wageni usilete mtafaruku kwa kudharau waliopigania haki wakabaki na vilema na wengine kupoteza maisha.
Atakayejiunga apewe haki lakini si lazima apewe haki ya uongozi. Wanahitajika wanachama wa kuimarisha vyama si matumbo yao. Na upinzani usiache mbachao kwa msala upitao

Tusememezane
 
Mh RAIS NA JOTO LA KISIASA TANZANIA

Kwanza kabisa tuzirejee duru za siasa duniani kwa ufupi.
Ni wazi kuwa mgombea wa urais Marekani kwa chama cha Republican atakuwa Mitt Romney,gavana wa zamani wa state ya masachussetts na mfanyabiashara maarufu. Wiki iliyopita alishinda majimbo 5 akiwa hana upinzani kwasababu Rick Santorum alijitoa. Waliobaki hawana nafasi yoyote labda tu kama wanataka umaarufu wa kisiasa.

Changamoto inayomkabili Romney ni kuwaleta wahafidhina(conservative) kwa pamoja. Yeye ni muumini wa kanisa la Mormon na hili linapunguza morali kwa evangelists ambao ni sehemu muhimu sana ya chaguzi za Marekani.
Anachangamoto za kupata pesa kwasababu hadi sasa Obama anamshinda kwa 10:1
Nguvu ya Republican katika sera za ulinzi sasa haina nguvu hasa baada ya Obama kukata mzizi wa fitna na Osama.

Tatizo linalomkabili Obama ni uchumi. Japo kuna dalili za kukua lakini changamoto ni kubwa kuelekea November.
Ni mapema mno kuongelea mwelekeo kwa vile wagombeaji bado wanajipanga.

MISRI:
Hali ya mambo kama nilivyowahi kuandika si shwari. Kuenguliwa kwa wagombea hasa yule wa chama cha Brotherhood kunaleta wasi wasi sana. hali bado ni tete Tahariri square (Tutaieleza kiundani bandiko lijalo).

TANZANIA:
Hali ya kisiasa ni tete sana baada ya shinikizo la wabunge kutaka mawaziri 8 wajiuzulu la sivyo Waziri mkuu aende na maji. Tumeona hata baada ya wabunge kuomba muda bila posho, Spika ambaye ni kiongozi wa umma na si wa CCM kwa mantiki yoyote ametumia mbinu kuua hoja.
Waziri mkuu aliahirisha bunge kwa hotuba dhaifu sana ikiwa ni dalili ya kuwa majeruhi.

Waziri mkuu ni majeruhi wa siasa za Rais JK. Ameadhiriwa mara nyingi kwa maamuzi anayoyaona ni sahihi kwa masilahi ya nchi kama lile la Posho za wabunge,Jairo na mgogoro wa madaktari.

Bila kujua kuwa mkuu wake anapenda kuonekana mtu mwema kwa kila mtu, waziri mkuu amejikuta kila mara akiwa ni 'victim of circumstance'. Kila jambo linalokuwa na utata hasa unaokinzana na msilahi binafsi ya Rais, waziri mkuu amekuwa anatupiwa zigo na sasa anaonekana kuelemewa na hafai.

Inabidi waziri mkuu ajilaumu. Inapotokea kutoelewana na mkuu wa kazi hasa kisiasa, jambo muhimu ni kujiuzulu.
Kinyume chake waziri mkuu angewajibishwa na bunge na kumwacha na aibu isiyofutika kama ile ya EL

Usanii uliotukuka kwa kumtumia Spika kuficha uozo sasa unafanya kazi iliyokusudiwa. Tunasikia Rais amepata baraka za kamati kuu kuvunja baraza la mawaziri. Hakuna kifungu chochote cha kanuni au sheria kinachohitaji Rais awasiliane na kamati kuu katika kuunda au kuvunja baraza la mawaziri, haijatokea huko nyuma.
heria ipo wazi kuwa Rais aliyechaguliwa ndiye atakayeunda serikali.

Hili la kuwasiliana na kamati kuu ni mwendelezo wa udhaifu wa kiongozi wetu. Ni hatua ya kutotaka kuwaudhi wateule wake kama yeye, bali kama kamati kuu.
Haingii akilini kudhani kuwa Rais hakujua kuwa baraza lake la mawaziri lina matatizo.

Kumekuwepo na malumbano kati ya waziri na waziri, waziri na naibu wake, mawaziri na makatibu wakuu, mawaziri na serikali yao. Malumbano ndani ya vyombo vya habari na tulishasema hakuna uwajibikaji 'collective responsibility' katika timu ya Rais. Rais alifumba macho na kuziba masikio, leo anatuaminisha alikuwa hajui uozo wa baraza lake!!

Inashangaza kuona Rais anataka baraka za kamati kuu ili hali yeye ndiye alipokea taarifa ya CAG na kamati kuu haijaiona. Ni hadi pale ilipofikishwa bungeni eti mkuu wa nchi ndiyo anazinduka kuwa kuna uhalifu.

Inshangaza kuona anataka baraka za kamati kuu. Mbona hakutaka iwe hivyo akina EL, Karamagi n.k walipoondoka madarakani tena kwa shinikizo kama hili.

Inashangaza kuona mkuu wa nchi anataka ruhusa ya kamati kuu wakati kuna suala la Jairo, Kagoda, Dowans, Meremeta, Mwanyika,Hosea n.k ambayo ameamua kuyanyamazia bila kutaka ushauri wa kamati kuu. Kwanini asiyaingize yote hayo kwa pamoja anachagua hili la sasa?

Ni jambo la kusikitisha sana kuona Rais kama kiongozi wa mhimili mmoja wa dola akiingilia haki na maamuzi ya bunge ambalo ni chombo cha wananchi. Kwasasa tubaki kuamini kuwa kamati kuu ya CCM ndicho chombo chenye nguvu kuliko bunge na kwamba kamati kuu ni mhimili wa nne wa dola.

Lakini ni jambo la hatari sana ni pale Spika wa bunge anapochukua kazi za bunge na kuzikasimu kwa kamati kuu. Spika Makinda anayelipwa posho na mshahara mnene na walipa kodi ameamua makusudi kupotosha taratibu za bunge kwa kupoteza muda ili akumfurahisha aliyemteua. Hii si mara moja au mbili Spika amelidhalilisha bunge.

Kwa mtazamo huo bunge la sasa limebaki kijiwe cha soga na kukusanya posho. Wabunge hasa wa CCM lazima wajisikie dhalili sana kwa namna chama chao kilivyowafinya na kufinyanga akili zao.

Ni bunge lenye wasomi katika viwango vya master na PhD lakini kwa hakika thamani yake ni mbovu sana.
Wabunge wa CCM wasubiri hukumu ya wananchi kuelekea 2015. Kwa wakati huo Makinda na Kikwete watakuwa wastaafu na bahati mbaya wabunge wengi wa CCM vijana wataonja hasira za wananchi.

Njia rahisi ni kumwajisha Spika wa bunge kwa kulidhalilisha na kuwaweka katika wakati mgumu mbele ya wananchi.
Hilo lispotokea Chadema itaendelea kuzoa umaarufu kwa kutumia udhaifu wa bunge linaloendeshwa puta na Makinda.

Kubadilisha baraza la mawaziri hakutoshi kuwa ufumbuzi wa matatizo. Kumbu kumbu zinaonyesha kuwa JK aliwahi kufanya hivyo na badala ya manufaa ile kiu ya kuipora nchi imefikia hatua ya kutisha na kusikitisha.
Labda wabunge wafikirie pia uwezekano wa kumwajibisha Rais vinginevyo wasubiri hukumu itakayotolewa kwa jina la CCM.

Tuhuma za EL na RA zilitosha kabisa kukibomoa chama na sasa tunasubiri nguzo zianguke ili tuweze kuandika makala za kifo cha CCM, KANU, UNIP kwa uchache. Mola akitupa uhai tutashuhudia haya hakuna shaka.

Kuna maswali muhimu, je, ni kwanini Rais anaogopa kuwachulia hatua watendaji wake akiwa na haki zote za kiutawala na kisheria? Kwanini JK anapenda akujificha nyuma ya kivuli cha kamati, tume n.k wakati wa matatizo na misuko suko inayohitaji busara, akili na uwezo wa Rais? Na kwanini JK ni kiongozi dhaifu sana katika historia ya nchi yetu.

Tutayaangalia haya katika bandiko linalofuata pengine kupata sehemu ya majibu.

Tusemezane
 
KWANINI RAIS ANASITA KUWACHUKULIA HATUA 'WAHALIFU'

Tuyarejee maswali katika aya ya mwisho bandiko lillopita.
Katika nchi yenye utawala wa sheria hatutegemei Rais awachulie hatua za kisheria kwa kuwahukumu watuhumiwa. Anachoweza kufanya ni kutoa adhabu ya kikazi kama kuwafukuza kazi wahusika na kuamuru vyombo vya dola na sheria vifanye kazi zao bila kumuonea yeyote. Kwa bahati mbaya Rais wetu hajaweza kufanya chochote kwa vilivyopo ndani ya wezo wake.

Matokeo yake ni kuona kiburi kama kinachoonyeshwa na mawaziri, kuwaacha 'wahalifu'' watumie walichokivuna kwa amani na starehe kama walivyokuwa mawaziri wa baraza lak la kwanza, makatibu wakuu na mwanasheria aliyepita.

Utamaduni huu wa kuwaacha wahalifu eti kwa adhabu ya kubadilisha baraza ndiyo unachochea sana ubadhirifu mtu akielewa kuwa anaweza kupata kiinua mgongo kizuri kwa dili moja kuliko kusubiri miaka 30 ya kustaafu.
Tunaona kufuru ya manunuzi ya vitu ambavyo waziri katika nchi ya Uingereza hawezi kuifanya. Jeuri kuu !

Moja ya sababu kubwa zinazomfunga rais mdomo na mikono ni njia aliyopata madaraka.
Rais baada ya kubwagwa aliunda mtandao tunaoujua leo. Fadhila za kwanza za waliomfikisha magogoni ni kuunda baraza la mawaziri 60, baraza kubwa kuliko lile la Uingereza, Ufaransa na hata India. Uwaziri ukawa zawadi kwa kila aliyeshiriki.

Wengi waliounda mtandao ni vijana na washirika wake wa karibu ili kuwalipa fadhila.
Kinachomuumiza Rais ni hali ilivyo sasa hasa baada ya EL kujiuzulu.
Lowassa ambaye ni 'king maker' bado ana hasira kwa mambo mawaili.
Moja, kutoswa na mshirika wake na pili vijana wake waliotarajiwa kumweka madarakani kuondolewa kinyemela katika safu za uongozi.

Hofu ya Rais Kikwete ni kuwa mawaziri na makatibu wakuu na viongozi wa taasisi wanajua vema udhaifu wake. Itakapotokea anawatosa vijana kama atabeba lawama, lakini hatari zaidi ni kuwa uwepo wake madarakani kwa muda uliobaki unakuwa wa shaka zaidi.
Jaribio la kumuondoa waziri mkuu limefikisha ujumbe kuwa uwezekano wa bunge kumwajibisha unazidi kukua.

Njia muafaka ni kushirikisha watu wengi ili mchawi asipatikane na hapa ndipo kamati kuu inapoingia.
Lakini pia hulka ya Rais Kikwete ni ujanja ujanja wa mjini na ile hali ya kutaka kumpendeza kila mtu bila kumuudhi pia.
Hili nalo linachangia rais kukosa ari, uthubutu na ujasiri wa kushughulikia matatizo ya taifa.

Ni kwa muktadha huo, kama alivyomsema Mkapa aachwe apunzike, naye akampuzisha mwanyika, Jairo na kuwaacha huru akina Karamagi, Msabaha huku akiwalinda mapapa wa EPA, DOWANS, RICHMOND n.k
Hivyo ndivyo atakavyowapa hisani hawa wanaopigiwa kelele za kujiuzulu. Kwamba, adhabu ya 'kamati kuu' ni kuwaondoa uwaziri na kuwaacha wakamilishe miradi yao kwa fedha haramu za walipa kodi.

Na sababu ya mwisho ni wafanyabiashara ambao walichangia sana kampeni yake ya mwanzo. Hawa wanafaidika moja kwa moja kama tulivyoona mtu mmoja akiwa na makampuni zaidi ya 10 na yote yanapewa zabuni za serikali, wakifanya kazi chini ya viwango n.k

Kwa namna nyingine vijana wao waliopewa madaraka ndiyo inakuwa njia 'conduit' ya miradi yao.
Makundi hayo ndiyo yanamtesa na kumfunga mikono JK.

Ikifika hapo inashangaza sana kuona watu wakiwa na kiumuhe muhe cha baraza jipya la mawaziri.
Kinachofanyika si kutafuta suluhu bali kuepusha watu na dhahma na kelele. Hakuna hata mmoja atakayeadhibiwa kwa ubadhirifu, ushiriki au uzembe. Adhabu kubwa ni kubadilisha baraza kwa mtindo wa ;huo ni upepo unaovuma utapita tu'

JK anadhani kuwa sasa hivi haitaji kuomba kura na lolote liwalo na liwe. Amesahau kuwa majaribio ya kuwajibishana yanayoanza yanaweza kumkuta wakati wowote. Ikizingatiwa kuwa kuna makundi hayo mawili yanayomuona kama 'msaliti' ni lazima awe macho sana. Makundi hayo yana nguvu na lolote linaweza kutokea hasa karibu na kuelekea uchaguzi

Kibaya zaidi ni kuwa 2015 chama kitafia mikononi mwa JK. Hili sasa halihitaji utabiri au unajimu. Dalili zipo wazi. Inapofikia vijijini sasa wanasema CCM basi, sijui chama kinategemea nini tena.

Tusemezane
 
BARAZA LA KIKWETE, MKUTANO WA CHADEMA
Siamini kuwa kubadilishwa kwa baraza la mawaziri ni suluhisho la matatizo yaliyopo. Mfumo mzima umeoza na hizi tunazoziona ni mbio za kubadilishana vijiti. Mfumo mzima unatakiwa ubadilishwe.

Rais ameteua mawaziri na manaibu wapya. Kama nilivyowahi kuandika hii ni njia tu ya kupunguza joto la kisiasa na kupambaza umma. Haiwezekani kutengua uteuzi iwe adhabu kwa mtumishi alihyesababisha au kuhusika na ubadhirifu au uzembe uliolitia taifa hasara. Ni mwendelezo wa Kagoda, Meremeta, Kiwira Richmond n.k.

Ningeshangaa kama Rais angemuacha January Makamba katika huu ulaji. Baba yake JM mzee Makamba aiwahi kumsifia mwanae kuwa na akili na kushangaa kwanini hayupo katika baraza la mawaziri. Makamba na JK wana mahusiano ya kikazi na uswahiba kwa muda mrefu. Kauli ya January kuhusu Zitto ilikuwa ni ashirio kuwa kuna kitu alikuwa anasubiri. Wajanja waliliona hili mapema.

Mkuchika anakabiliwa na tuhuma za uzembe, naye kama Mzee Makamba wana uhusiano na Jk tangu wakiwa jeshini. Ningesahangaa kama Jk angekuwa na uthubutu wa kumpiga chini. Alichokifanya Rais ni kitu cha kushangaza na kulidharau bunge. Huyu mtu kama alivyo Maghembe wanatuhuma za uzembe. Kuwabadilisha wizara ni ujumbe kwa bunge kuwa Rais ni kila kitu na hawezi kufanywa lolote.

Hussein Mwinyi ambaye alihusika na uzembe wa kulipuka kwa mabomu naye kabadilishwa wizara. Huyu ni mtoto wa Rais mstaafu na kilichofanyika ni 'kumsitiri' hata kama ni kwa gharama ya wanadamu na taifa. Sasa tusubiri 'mabomu' ya afya yatakapolipuka tena. Ni mtindo huo huo uliomrudisha waziri Malima. Huyu naye anahusika na kashfa zisizo na majibu lakini katika kulindana basi mchezo wa karata tatu umechezwa

Kama Rais angekuwa makini hii ndiyo nafasi iliyokuwepo kuwaweka kando wote wenye kashfa za uzembe kama Mwinyi, Malima, Maghembe na Mkuchika lakini wapi!

Hawa ghasia aliyeshindwa wizara ya utumishi kama ilivyokuwa kwa Haji Mponda naye hakupaswa kurudi. Inasikitisha kuona watu kama hawa waliopoteza imani kwa umma bado wanapewa dhamana kubwa namna hiyo.

Mwandosya amepewa wizara isiyokuwapo ili kuwatuliza watu wa Mbeya. JK ndiye ameanzisha utaratibu wa kanda kiasi kwamba kila kanda na pengine dini iwe na mwakilishi na siyo uwezo. Katika watu walichochea mgawanyiko wa taifa hili ni JK kuanzia kampeni hadi Urais. Wizara isiyokuwepo ni wizara gani kama si kuongeza mzigo tu kwa matakwa ya kisiasa.

Kituko kingine ongezeko la ukubwa wa baraza la mawaziri. Kwa nchi masikini kama Tanzania, mawaziri wote hao wanafanya kazi gani? Upo uwezekano wa kuwa na wizara chache zenye idara. Unapokuwa na genge la watu 60 unawezaje kuwa 'manage'? Hapa kweli unakuwa na cabinet au chaos!

All in all, hakuna cha ajabu kilichotokea tusichokijua kutoka serikali hii dhaifu. Pengine kilichowazi ni jinsi Rais anavyolidharau na kulidhalilisha bunge na waziri mkuu wake!

CHADEMA NA MIKUTANO
Katika mkikutano inayoendelea ijulikanayo kama M4C CDM lazima wawe waangalifu sana. CCM inajua kuwa ipo ICU na inatafuta mahali popote kupata oksijeni. CCM ni wazuri sana wa 'spinning' kama tulivyowahi shuhudia huko nyuma.
Wamefanikiwa kutumbukiza mbegu za ukabila na udini zinazochanua kila uchao. Kwa bahati nzuri umma sasa unaanza kuelewa hali hiyo na kukataa kusikiliza propaganda.

Kauli za vijana kama Nasari ni za hatari sana kwa afya ya chama. Ingawa mwenyekiti amekisafisha chama kutokana na matamshi hayo, hiyo haitoshi. Inapaswa CDM wamtake Nasari aombe radhi mwenyewe ili kuua hoja zinazojengwa dhidi ya Chama. Kisiasa ni kama amekichafua chama na lazima asimame yeye kama Nasari na si kupitia mbowe kuomba radhi.

CDM lazima wawe 'organized'. Haiwezekani mkutano mkubwa kama ule kila kiongozi aende na ajenda yake. Ni muhimu wakatoa utaratibu na hadidu rejea za nini viongozi wanapaswa kusema. Nadhani M4C ina maana na siyo vurugu mechi.
Kama kuna tatizo ninaliona CDM ziku za mbeleni ni kutokuwa na utaratibu wa kuratibu shughuli kisayansi.

Sina uhakika kama leo hii CDM wana 'moral authority' ya kumnyooshea kidole Lusinde wa CCM. Inakuwaje Chama mbadala kinakosa umakini wa kujifunza kutokana na makosa ya wengine. Siasa ni kama mchezo wa mpira ambapo ushindi hutegemea kosa la mpinzani. Endapo nyote mnafanya makosa yale yale basi mchezo huishia kuwa suluhu na kukosa ladha. CDM amkeni mtangaze sera zenu na dira ya taifa na siiyo kelele kutoka kwa kila anayepokea kipaza sauti

Tusemezane
 
CHADEMA: HILI LA SHIBUDA LITAWAGHARIMU

Wapenda mageuzi walionyesha wasi wasi baada ya mbunge wa CHADEMA John Shibuda kutofautina na wenzake kimitazamo hasa ile inayohitaji umoja wa chama. Sakata lilianzia bungeni na baada ya hapo Shibuda hajashiriki katika shughuli zozote za Chama.

Tumewahi kuonya CDM kuchukua 'makapi' na kuyaingiza ndani ya chama chao. Shibuda anafahamika vema kwa mambo yake hata alipokuwa CCM. Ingawa CDM walimkubali ni wazi kuwa hilo lilifanyika ili kuongeza idadi ya wabunge na kwamba CDM haikuwa imetayarisha wagombea katika baadhi ya sehemu.

Kelele nyingi zilipigwa Shibuda aondolewe katika uongozi kwasababu hakuwa msaada (assert) isipokuwa mzigo(liability).
Pengine kwa kuogopa kupunguza idadi ya wabunge au kutaka kuonekana kuwa kuna demokrasia ya kweli,uongozi ulitoa karipio kali na kumuacha aendelee kuwa kiongozi hata kama hakuwa na mchango.

Hapa CDM walifikiri mali zaidi ya hali. Mkakati huo ulikuwa mbovu sana nami niliandika mahali, 'Shibuda atawagharimu' na leo yanajitokeza

Juzi Shibuda katoa kauli za kuonyesha kuwa yeye hakubali upinzani na kuwa yupo tu kwa manufaa(convinience) na si kwa itikadi(ideology). Mbunge wa chama anaposimama na kusema chama chake hakipo tayari kuchukua madaraka, basi hapo lipo jambo.

Ni haki ya msingi kabisa ya Shibuda kutoa mawazo yake tena kwa uhuru lakini anapofanya hivyo mbele ya chama pinzani(CCM) ni jambo linalofikirisha. Linafikirisha kwasababu kama chama hakipo tayari yeye kama John Shibuda amefanya nini kukifanya kiwe tayari na anafanya nini katika Chama analodhani halipo tayari?

Baada ya BAVICHA kutoa kauli zinazoashiria mwisho wa ubunge wa Shibuda, sasa ameibuka na kujibu tuhuma hizo.
Majibu yake hayakulenga kujibu hoja za BAVICHA bali kujaribu kugeuza mada kwa njia mbili.

1. Kumshambulia John Heche kana kwamba kauli ile ni yake ili ajenge uhalali wa kuendelea kubaki ndani ya chama kwa vile hatakuwa na mgogoro na chama bali John Heche.

2. Kutumbukiza mbegu za ukanda na ukabila ili viongozi wa CDM wasite kumchukulia hatua kwa kuogopa malumbano yatakyaozidi kukichafua chama.

Hayo mawili ndiyo silaha anazotumia kujikinga kwa kuelewa wazi kuwa alichokifanya kimechefua Chadema na umma wa wapenda mabadiliko waliochoka na hadithi zisizokwisha kwa miaka 50.

Kuna mambo ambayo Chadema ni lazima wayafanye, tena wayafanye haraka sana.

1. Achilia mbali tuhuma zilizotolewa na BAVICHA, kitendo cha Shibuda kusema anashambuliwa kwa usukuma wake ni tusi kubwa sana kwa CDM.

Shibuda anamaanisha bila kificho kuwa ukiwa kabila X basi wewe ni 'victim' ndani ya CDM. Hili linapinga na falsafa ya chama na kibaya zaidi limeipa CCM nguvu ya kueneza propaganda za kijinga kama tulivyomsikia NAPE akisema bila haya. Wimbi la mageuzi limeifanya CCM isiweze kueleza inafanya nini au imefanya nini na sasa imedandia propaganda za kipuuzi. Shibuda anamkono mkubwa kwa hili na anapaswa kuondolewa katika siku 3 zijazo ili kuzuia uharibifu(damage control)

2. Uwepo wa Shibuda unakimaliza Chama kwasababu hana mchango wowote zaidi ya kuwa tatizo.
Siku za mbeleni ataleta mtafaruku mkubwa sana ndani ya chama. Historia inaonyesha hivyo na historia ina tabia ya kujirudia. Bila kumondoa Shibuda historia itaihukumu CDM kikamilifu na kwa usawia

CDM wafanye nini kwa wakti huu:
1. Kumfukuza Shibuda mara moja. Hili litajenga yafuatayo

a} Watu kuheshimu taratibu za chama na kujua kuwa chama ni watu na si mtu Katika kufanya hivyo, CDM wasifikirie idadi ya wabunge au mgao wa ruzuku. Waangalie hatari mbele yao

b) Litawaaminisha watu kuwa CDM ni chama chenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu bila kusita ili mradi yawe sahihi na kwa wakati sahihi

c) Litawaaminisha wananchi kuwa tuhuma za ukabila si kweli na CDM inasimamia kile kilicho sahihi bila kuogopa uzushi au uongo

d)Litaepusha mvurugano(distraction) wakati huu chama kikihitajika kila kona ya nchi

Chadema wajiepushe na nini?

1. Wasiingie katika mtego wa Shibuda wa kulumbana kuhusu ukanda, ukabila n.k. Huko ndiko Shibuda anapotaka waende ili awamalize kwasababu yeye ni fundi wa eneo hilo. Kuna msemo unaosema ukibishana na mjinga, jambo la kwanza atakurudisha uwe katika level yake, halafu atakushinda kwasababu katika level hiyo yeye ni mzoefu

2. Chadema wasimamie hoja zao bila kuyumba au kutetereka na wanahoja za kummaliza Shibuda bila haya

Nimalize kwa kusema, yote haya ni matokeo ya CDM kupuuza ushauri na hatari kubwa ipo mbeleni kama watendelea na utamaduni wa kuoneana haya. CCM yamewafika sasa nani anafuata?
 
Nguruvi3 uchambuzi wako ni wa makini sana na nimejifunza mengi humu.Hii ni shule ambayo ni lazima kwa wapenda maendeleo ni muhimu kuelewa somo na kusoma alama za nyakati.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli sikuwahi kuona uchambuzi wa namna hii kwa jukwaa hili kabla ya leo. Naanza kujifunza siasa. Nguruvi3 utaendelea kuwa mwalimu wangu.
Kwa hili la Shibuda ni kweli hata mimi nadhani ni muda wake wa kumuondoa maana hawezi kuwa msaada tena katika chama.
Na asipoondolewa itafanya kuonekana kwamba uongozi ndio unampa mwanya na kiburi wa kufanya upuuzi anaofanya. Maana kwa maneno yake mwenyewe anatamba kwamba Mbowe hawezi kumfukuza maana ameshamuelewa kitabia na ameshakubali kuchukuliana naye. Ni lazima Chadema wachukue hatua maana wanachama wengi wameshakelwa na tabia yake hiyo.
Kuondoka kwake ni faida sana kwa chama kuliko kukaa kwake.
Shibuda ni mzigo katika chama.
 
Hapo kidogo ningependa ni tofautiane na wewe!
Kwa muda sasa toka baada ya uhuru wetu, kumekuwa na hii dhana ya kuwajenga watz katika kuamini katika vyama vya siasa kila linapokuja suala la siasa!

Kuna haja ya kuwajengea watz uwezo wa kimtazamo katika kujitambua zaidi wao kama wao,
Ni lazima tujenge kada nje ya hizi za kisiasa, kwa mfano za kijamii ambazo zitakuwa na jukumu lakujenga UMMA wenye nguvu..

Automatically UMMA wenye nguvu utazaa vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuleta tija tarajiwa!
Ukiangalia njia ambazo tunapita kama taifa, utagundua kuwa kuna nafasi ya chama chenye nguvu cha siasa (CHADEMA)... hata kikishika dola kitakuwa kama vyama vingine vilivyoleta uhuru Afrika- kwamba kinapokelewa kama mwokozi na kinapata ushindi wa kutosha na anayekipinga anaonekana msaliti.... enzi za "chama kushika hatamu".... hii hutokea kwa UMMA usioamka na unaotegemea mustakabali wake kwa chama cha siasa. Hii si sahihi!

Mjadala nadhani ni lazima tuwe na taasisi za UMMA ie vyama vya kijamii, vyama vya kumlinda mlaji, vyombo vya habari na hii mitandao ya kijamii kama JAMIIFORUMS na Blog makini na vingine,

Hivi vyote vikifanya kwa ukaribu hakika tutakuwa UMMA wenye nguvu, UMMA wenye kuweza kujenga mustakabali wake wenyewe bila kutegemea vyama fulani kwamba hivyo vyama vitatokana na msimamo wa huo UMMA...!

Hivyo naomba nikubaliane na "MimiBaba", kuwa tunahitaji kujenga WATU imara sababu huo ndio msingi wa mamlaka zote na vyama vyote..

Na hamna damage inayoumiza zaidi historia kama ile inayoathiri UMMA kwa ujumla wake.

Tujifunze Libya!

kwani jouneGwalu unayozungumzia hayapo? Kwani hakuna media zenye nguvu? Kwani hakuna vyanzo vya taarifa kila sehemu? Huwezi ukawajenga WATU nje ya taasisi. Lazima ziwepo taasisi imara ambazo zitawa mobilize hawa WATU katika kufikia malengo yao. Kwa hiyo hata chama cha siasa ni taadisi
 
Last edited by a moderator:
kwani jouneGwalu unayozungumzia hayapo? Kwani hakuna media zenye nguvu? Kwani hakuna vyanzo vya taarifa kila sehemu? Huwezi ukawajenga WATU nje ya taasisi. Lazima ziwepo taasisi imara ambazo zitawa mobilize hawa WATU katika kufikia malengo yao. Kwa hiyo hata chama cha siasa ni taadisi


Tuache ligi ndugu yangu nisome kati ya mistari bwana!
 
MADHARA YA ARUMERU YANAZIDI KUSAMBAA, SAFARI YA CCM KUELEKEA UPINZANI INACHUKUA KASI

Tumeandika kati safu hii mara nyingi kwanini CCM ilitumia nguvu sana kukabiliana na upinzani kule Arumeru.
Kwa kifupi tulisema madhara ya Arumeru yatasambaa na ilichokuwa inakifanya ni kuzuia madhara hayo na wala si jimbo kwa maana ya wingi wa wabunge au ruzuku.

Yale tuliyosema sasa yanatimia. Nimeshtuka sana kuona 'athari' za Arumeru sasa zinasambaa kwa kasi ambayo sikuitegemea ingawa nilitegemea hilo kutokea. Huko Same ambako kuna 'waumini' wa damu wa CCM sasa hali shwari.
Anapotokea kiongozi wa jumuiya ya Chadema kutikisa vijiji hakika hali ni mbaya.

Morogoro ambako wananchi hawajui kitu kingine zaidi ya CCM nako si shwari kwani tumeona wakirudisha kadi mmoja baada ya mwingine. Nasikia wimbi linaelekea mikoa ya kusini na sijui nini kitatokea huko.
Kwa mwendo uliopo CCM haina mahali salama pa kujificha au kujitetea. Kila mahali lazima itumike nguvu.

Kwanini wananchi wameamua liwalo na liwe?
1. CCM imeacha misingi ya chama na kuwa genge la mafia. Kwamba kama huna pesa wewe ni mwananchama wa kura tu.
Chama kimeondoka katika misingi ya kutetea wanyonge na kubaki kuwa gulio la wafanya biashara waliovaa nguo za kijani wakitetewa na viongozi waliowanunua.

2. CCM imekuwa chama kisicho na sheria,kanuni wala maadili. Kwamba mweye kisu kikali ndiye atakula nyama. Tumeshuhudia waovu wakitetewa kwa kila hali tena za dhihaka dhidi ya wananchi. Kila kilichowagusa wananchi kiliundiwa tume na hapo imekuwa mwisho.

3. Kosa kubwa ni lile la CCM kuwapa wapinzani umaarufu bila gharama. Mh Spika Makinda amekuwa mstari wa mbele kuwanyima wapinzani sauti kuhusu masilahi ya taifa. Hilo hakujua kuwa wananchi pamoja na kuenea teknoloji wanaliona na lina waudhi sana. Kila anapowakalisha chini au kuwadhihaki wapinzani masikini hajui kuwa anawapandisha chati.Matokeo yake wananchi wanajua kuna kinachofichwa!

Matumizi ya vyombo vya dola yanazidi kuwatia wananchi hasira. CCM haijui kuwa vitabu vipo wazi kuanzia Tokyo hadi London, Cairo hadi Cape town. Nguvu za mabomu ya machozi zinachochea hasira kuliko kuleta utangamano na hakuna nguvu ya dola iliyowahi kushinda nguvu ya umma duniani.

4. Uongozi dhaifu. Hakika hakuna kipindi ambacho CCM imekuwa na uongozi dhaifu kuliko kipindi hiki. Mwenyekiti amekuwa ndumila kuwili akicheza karata za mjini kwa ulaghai wa maneno matamu.

Ameshindwa kuvunja makundi aliyoshiriki kuyaunda na ameonekana kutoheshimu hata sheria za nchi.
Umasikini umetamalaki huku kukiwa na takwaimu za uongo. Majuzi Rais amesema Tanzania itapokea trilioni 1 kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kilimo. Hakuna mwananchi anayejali trilioni moja itamsadia vipi huku akishindwa kununua kibaba cha unga kwa inflation iliyofikia asilimia 20.

5. Genge la wahalifu: Wananchi wamebaini mwizi wa mali zao na asiyewajali hatoki nje ya nchi.
Ni miongoni mwa wale waliovaa nguo za kijani. Mwananchi asiyeweza kununua kilo ya sukari kwa sh 1500/= anajiuliza hivi inakuwaje mwenzake awe na akaunti yenye sh Milioni 700 achilia thamani nyingine.

Wakati mwananchi akiwa hawezi kununua aspirini yupo anayelipwa lakin 2 kwa kukaa katika kiti pale Dodoma. Wananchi wanasoma na kuelewa madudu kama ya maliasili, Dowans, Richmond n.k na kila wakilipa gharama mathalani za umeme wanajua kuwa wanachangia mifuko ya genge la watu wasiozidi 100.

Ikifika hapo wananchi hawana jinsi wanatafuta mwelekeo na mwelekeo huo sasa ni Chadema.
Laiti chama cha CUF kisingekuwa kimejengwa katika personality ya Maalim Seif, kikaacha kujitambulisha kama chama chenye misingi ya imani fulani hakika leo kungekuwa na patashika.
Makosa yameshafanyika na CUF haiwezi kurudi katika enzi. Uzembe wa CUF ni uongozi, kitu muhimu sana katika siasa.

Hatuwezi kusema CDM wanauongozi thabiti, la hasha! nao wana matatizo lakini kwa wakati huu angalau mtu anaweza kutafuta kivuli. Ni kivuli hicho ndicho kinawapa 'momentum' kama hawatafanya makosa ya ubinafsi, kuiga template za CCM, ulafi na husuda, njia inazidi kupanuka.

Changamoto waliyo nayo ni kuunda chama katika misingi ya taasisi ikiwa na sheria, kanuni na maadili.
Ni lazima waonyeshe umma kuwa wapo tayari kutwaa na kuingoza dola si kwa maneno jukwanii bali kwa vitendo ndani ya chama kwanza.
Kitu walichoanza kufanikiwa kidogo ni kundoa 'personality'. Kwasasa tunaona hata vijana wanauwezo wa kufanya mambo makubwa bila kutegemea haiba au mvuto wa wakubwa.

Tatizo ninalo liona ni lile ninalozungumza kila uchao. CDM wanafanya baadhi ya mambo kwa 'template ya CCM', Hawajaweza kupata 'brand' yao. Mifano, hivi ugomvi wa BAVICHA ulitakiwa ufike redioni kweli! CDM hawajui mtovu wa nidhamu ni nani? Juliana Shonza kwa vigezo vyovyote vya kisiasa alipaswa aachie ngazi bila kusubiri vikao.
Tunaona dana dana zile zile za CCM kuhusu kuvu gamba. Shibuda sasa ni Lowassa au Chenge wao.

Nilitaraji wangekuwa na brand ya uwajibikaji bila kusukumwa, bahati mbaya hilo halijatokea. Ingawa inaonekana hali ni shwari, kitendo cha kushindwa kusimamia kanuni kama ilivyo kwa Juliana Shonza na Shibuda kinaharibu taswira ya chama na kujenga kambi zitakazoleta machafuko.

Nasema kama hawatabadilika ndani ya miezi 18 kutatokea mtafaruku mkubwa sana. Ni suala la muda tu.

Tusemezane
 
Ndugu Wana Jamii,

Nimesoma mada hii na hakika nimefurahia sana na michango ya wachangiaji wengi kwa uchambuzi makini na kuwa na maono,

Binafsi napenda kuchangia kwa kifupi sana, katika siasa za kisasa Lazima vyama vya siasa viwe na ma "SURROGATE" ambao kazi yao ni kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea talking point za chama ili ku dominate media cycle.

Hivyo basi katika kuhakikisha kuwa ujumbe wa chama unakuwa alive ni muhimu sana kwa chama kutumia SURROGATE, Tena surrogates wanatakiwa watu wenye reputation flani katika jamii au ndani ya CHAMA, na chama Lazima kihakikishe kinakuwa na ma surrogate wa kutosha ikiwezekana katika kila wilaya
 
Ndugu Wana Jamii,

Nimesoma mada hii na hakika nimefurahia sana na michango ya wachangiaji wengi kwa uchambuzi makini na kuwa na maono,

Binafsi napenda kuchangia kwa kifupi sana, katika siasa za kisasa Lazima vyama vya siasa viwe na ma "SURROGATE" ambao kazi yao ni kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea talking point za chama ili ku dominate media cycle.

Hivyo basi katika kuhakikisha kuwa ujumbe wa chama unakuwa alive ni muhimu sana kwa chama kutumia SURROGATE, Tena surrogates wanatakiwa watu wenye reputation flani katika jamii au ndani ya CHAMA, na chama Lazima kihakikishe kinakuwa na ma surrogate wa kutosha ikiwezekana katika kila wilaya
Ndugu yangu George, Nikushukuru sana! Hili tumeliongelea mwaka wa pili sasa na sijui kwanini hawalioni. Siasa za zama hizi ni za kisayansi na si za kudai uhuru.
Hao Surrogate na Pundits kama ulivyonena ni lazima wawe watu wenye weledi na reputation.

Nimeshangaa kusikia hata BAVICHA ambapo tunadhani ni vijana zaidi kuliko wale wa TANU-YL na pengine wangekuwa na maono tofauti! hawana hata msemaji wa jumuiya! Matokeo yake kila mtu anaamka nakuita waandishi wa habari kusema kile anachodhani kipo kichwani kwake.

Hili la ku-dominate media nalo ni muhimu sana. Safu zilizopita nilisema japo basi watumie FM, nashukuru Mbowe ameliona japo mara moja. Vyombo vya habari kama TBC redio na TV vinajulikana vipo kwa masilahi ya CCM.
Kulalamika kuwa havitendi haki ni sawa na kumlaumu Nape Nnauye kuwa hatendi haki kuisemea CCM.

Kuna tofauti kati ya msemaji(spokesperson) ambaye kauli yake ni kauli ya chama au taasisi.
Halafu kuna mwenezi (mass mobilization and propaganda) ambaye kazi yake ni kushadidia hoja za chama au taasisi
Na kuna surrogates ambao wao huchukua nafasi za watu wengine katika kuzungumzia mambo
Mwisho kuna Pundits, tofauti na wengine wao hutoa maoni yao katika vyombo vya habari kuhusiana na mada fulani

Katika mazingira kama ya BAVICHA siku za karibuni, Surrogates wangefanya kazi ya kuweka msimamo wa chama kuhusu Shibuda kwa lugha ya kueleweka, kufafanunua tatizo lililojitokeza, kuweka sawa hoja za Heche kwanini alimjibu Shibuda na hoja zipi zilikuwa kiini cha majibu.
Wangeenda mbali na kuziweka hoja na hata kuonyesha jinsi shibuda alivyobadili mada

Pundits wangeingia kutoa maoni ni wapi Shibuda amekosea, ni wapi Juliana Shonza amekiuka taratibu na ni hatua zipi zichukuliwe na chama. Yote hayo ni katika lugha nzuri isiyoleta sintofahamu zaidi ya ufahamu.

Kwasababu hakukuwa na chaguo jingine, ilibidi watu waombe uongozi uingilie kati. Kwa bahati mbaya Mbowe ameingia na kujaribu kutuliza mtafaruku. Kwa hali yoyote ile atakuwa amejiweka katika wakati mgumu. Wanachama watasubiri kusikia suluhisho na ni wazi kuhusu Juliana na Heche. Atakaposhindwa kutoa suluhu yenye kueleweka ni tatizo kwake na chama!

Kwa vile tuhuma zimeshaingiza hisia za mankundi na 'mahusiano' si ajabu hiyo ikatumiwa kama silaha kumchafua endapo hatua muafaka zinazozingatia sheria, kanuni na maadili hazitafuatwa.
Mzozo umemuacha Shibuda na sasa unakivuruga chama!
Kunapokuwa hakuna maridhiano kati ya Mwenyekiti na Makamu wake, team work ipo wapi zaidi ya majungu na kuwindana!

Ninachotaka kuonyesha hapa ni kuwa Surrogates na Pundits wangeweza kuiweka hali vizuri kabisa na huenda Shibuda angekuwa anakabiliana nao na si Dr Slaa ambaye ameshaingia katika mzozo kiaina.
Dr Slaa wala hakupaswa kumjibu mpuuzi kama Shibuda lakini afanye nini! hakuna wa kumsemea au kumjengea hoja kwa mbadala.

Siasa za sasa ziishie kwenye mikutano,ziwe siasa za kisayansi zaidi.
 
MADHARA YA ARUMERU YANAZIDI KUSAMBAA, SAFARI YA CCM KUELEKEA UPINZANI INACHUKUA KASI

Tumeandika kati safu hii mara nyingi kwanini CCM ilitumia nguvu sana kukabiliana na upinzani kule Arumeru.
Kwa kifupi tulisema madhara ya Arumeru yatasambaa na ilichokuwa inakifanya ni kuzuia madhara hayo na wala si jimbo kwa maana ya wingi wa wabunge au ruzuku.

Yale tuliyosema sasa yanatimia. Nimeshtuka sana kuona 'athari' za Arumeru sasa zinasambaa kwa kasi ambayo sikuitegemea ingawa nilitegemea hilo kutokea. Huko Same ambako kuna 'waumini' wa damu wa CCM sasa hali shwari.
Anapotokea kiongozi wa jumuiya ya Chadema kutikisa vijiji hakika hali ni mbaya.

Morogoro ambako wananchi hawajui kitu kingine zaidi ya CCM nako si shwari kwani tumeona wakirudisha kadi mmoja baada ya mwingine. Nasikia wimbi linaelekea mikoa ya kusini na sijui nini kitatokea huko.
Kwa mwendo uliopo CCM haina mahali salama pa kujificha au kujitetea. Kila mahali lazima itumike nguvu.
Huu ukweli CCM hawataki kukubaliana nao na wanajipa matumaini eti vijana wa CDM wananunua kadi na kuvamia mikutano ya vyama vyao na kurudisha kama vile ni wana CCM.
 
NGOME ZA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Kabla hatujaingia katika muhtasari kama unavosomeka hapo juu, tuziangalie siasa za nyakati 'current affairs'

Marekani: Mtifuano bado ni mkali kati ya Obama na Mitt Romney. Takwimu za uchumi zinazotoka kila ijumaa ya kwanza ya mwezi zinaonyesha ongezeko kidogo sana katika ajira na kiwango cha wasio na ajira kimepata hadi 8.2 asilimia.

Takwimu hizi si nzuri kwa Obama na chama chake na Republican wanazitumia kuonyesha kudodorora kwa uchumi.
Historia inaonyesha kuwa hali ikiwa hivyo ni vigumu kwa rais kurejea madarakani hasa kiwango cha kutokuwa na ajira kikifikia hapo kilipo. Kuna nafasi ya miezi minne ya kubadilisha hadithi, vinginevyo Obama ana hali ngumu

Misri: Duru la pili linatarajiwa katika muda si mrefu. Duru hili linampambanisha aliyekuwa waziri mkuu wakati wa mubarak na mgombea wa chama cha Brotherhood. Wote wawili wana kasoro.
Waziri mkuu anaonekana kama mabaki ya mubarak na kwamba amewekwa na jeshi kitu wananchi wasicho kitaka.

Kwa upande wa Brotherhood, wamisri wanogopa sana kwasababu sharia za kiislam zinaweza kuwekwa taratibu rais akitoka huko. Ingawa kuna uislam na chimbuko la usomi wa kiislam ( Al Azar University) wamisri wengi ni 'progressive' wenye msimamo wa kati kwahiyo wanaoona sheria za dini zitawarudisha katika nyakati za nyuma wasizozitaka.

Kutokana na hukumu ya Mubarak hasa watoto wake kuachiwa huru, hasira za wamisri zina mchanganyiko wa mambo na kama nilivyowahi kuandika hali bado ni tete sana. Tutaendelea kufuatilia kinachojiri Tahariri square

NGOME ZA VYAMA VYA SIASA
Kwa wenzetu wanaita 'political base' na tumeangalia mifano michache sana ya nchi kama marekani.
Ngome hutokea kutokana na mvuto wa chama kwa kundi fulani iwe kisera au ushawishi wa viongozi.
Kwa wenzetu sera ndizo zinaongoza 'base'. Vyovyote iwavyo political base zipo tu hata katika nchi zenye demokrasia changa.

CUF: Chama hiki kina kauli mbiu haki sawa. Uanzishwaji wake ulilenga kutoa upinzani kwa kutumia uzooefu wa wazee kama Mapalala. Bahati mbaya Chama hakikujengwa kwa misingi ya chama bali haiba ya mtu hasa baada ya Mapalala kufukuzwa.

Kwa vile maalimu Seif si muumini wa muungano, alikibadilisha chama kuwa cha visiwani na si Tanzania kwa ujumla.
Chama kiliungwa mkono na Wazanzibar ambao asilimia 98 ni waislam. Hata kiliposambaa Tanzania bara yale madhara 'effect ya udini' hayakuisha. Kwa bahati mbaya Maalimu alilenga kutawala visiwani na hivyo alitaka kuungwa mkono tu kwa kiasi bara. Hakuwa na cha kupoteza hivyo akatafuta kuungwa mkono na waislam.
Kila jambo likawa katika mahadhi ya kidini na hata chama kufanya dini kama 'political base'

Kwa nchi kama Tanzania yenye mwingiliano wa kijamii hili lilikuwa kosa kubwa sana kisiasa.
Ili kuonyesha Seif asivyoijali CUF bara, yeye aliruhusu chama chake kwa vurugu na bila mpangilio kufikisha rasimu ya katiba mpya bila hata kujua mchakato mzima ukoje.
Kibaya zaidi rasimu hiyo haikuzingatia kauli mbiu ya haki sawa. Rasim alizingatia mambo ya kidini.
Kitendo cha kufanya political base kuwa ya kidini kimekimaliza CUF kisiasa na sasa kimebaki visiwani.

Hata huko visiwani, CUF imeudhi political base yao ambayo inajulikana ni waislam kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. 'Base' inaonekana kukasirishwa na kitendo cha CUF kushirikiana na CCM. Hata huko hali si nzuri.
Kwa ufupi CUF ilichagua political base kwa misingi ya udini na hilo limeshindikana na sasa inaelekea katika vitabu vya historia.

CCM: Chama kikongwe barani ambacho kina sifa ya kuwa na hazina kubwa ya wajuvi na wajuzi wa kisiasa kuanzia zama za ukoloni. Chama kilichojengwa katika misingi ya utaifa hasa kikiwa cha wakulima na wafanyakazi. Chama kilichoonekana kujali sana tabaka la chini na kupiga vita ukabila na udini katika siasa zake.
Kwasasa yote hayo yamebaki katika historia huku chama kikiwa katika hali mbaya sana kisiasa kuliko wakati mwingine wowote ule.

Kimetokea nini katika 'political base' ya chama hiki hadi kufikia wakati kinapukutisha wanachama mithili ya majani nyakati za kipupwe?

Itaendelea.......
 
Inaendelea.....
CCM imeacha misingi yake kama chama cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi. Wajanja walikusanyika Zanzibar na kupitisha azimio lao. Ni lao kwasababu lilifungua mianya ya wenye nacho kukichukua chama.
Hapo tukaona wafanyabiashara wenye mabilioni wakigombea ujumbe wa halmashauri kuu,kamati kuu n.k.
Tusiojua tuliwaona mazuzu kumbe walikuwa na akili yao. Walijua umiliki wa serikali haupo serikalini bali ndani ya chama.

Wakajipanga vyema katika kamati za chama,kununua wajumbe kwa gharama yoyote. Kupitia chama wakaweza kuidhibiti serikali. Hapo ndipo dili za kuipora nchi zikaanza kwa kutumia chama. Uanachama wa CCM na uongozi ukawa lulu kwamba mtu anahonga milioni 150 awe diwani.
Chaguzi zikawa za kununua. Wananchi wakafurahia matunda ya chaguzi,khanga na kofia za bure.

Hali za maisha zinakuwa mbaya kila uchao lakini neema inazidi miongoni mwa wana CCM. Mabilionea wanachipuka kila siku. Chama kikawa kimetekwa na serikali ikapoteza nguvu. Hata ilipojulikana wahalifu ni nani hakuna anayeweza kuwashughulikia maana wao ndio wapo kwenye chama wakipanga sera.

Mfano ni tukio la Spika Sitta ambaye amejikuta akiadhibiwa na kamati za chama za wenyewe.
Mafisadi hawawezi kuchukuliwa hatua kwasababu wamedhibiti chama.
Chama kimebaki jina lakini si chama cha siasa ni mkusanyiko wa genge la mafia.

Wanachama wameshtuka kuona umasikini unawakabili kupita kiasi huku wakiambulia khanga na kofia.
Imefika mahali wamejiona hawana sauti na wala si sehemu ya chama.
Umuhimu wao ni kwenye sanduku la kura baada ya hapo tukutane baada ya miaka 5.

Political base ambayo ni tabaka la wakulima na wafanyakazi limechoka, taratibu chama kikaanza kupoteza political base ya wafanyakazi. Huko vijijini kwenye ngome ya wakulima nako habari zimefika, wamejionea kila siku wakidanganywa huku viongozi wao wakizidi kuneemeka. Sasa wamesema khanga na kofia haziwasaidii na umasikini unazidi kuwanyanyasa

Ngome zote tatu, tabaka la wanyonge, wakulima na wafanyakazi sasa zimeasi. CCM haina ngome 'political base' yoyote.
Tunachokiona ni matokeo ya kuanguka kwa ngome na watu wanasema liwalo na liwe, kudanganyika sasa basi.

Kuanguka kwa CCM si matokeo ya udhaifu wa Kikwete, ni mlolongo wa matukio 'cascade of reaction'.
Mzee Mwinyi alipovunja miiko ya uongozi na kuruhusu siasa na biashara ndio ulikuwa mwanzo.

Rais Mkapa ndiye aliyewaruhusu wafanyabiashar kukimiliki chama kwa kuwapa uongozi.
Kikwete amekuta wajanja wameshajipanga ingawa naye ni sehemu ya wajanja.
Udhaifu wake kama kiongozi, kuruhusu kundi lake kuwatosa wazee a chama kuna mchango mzuri sana ulioua ngome.

Chama kinafia mikononi mwa Kikwete na yeye hatakwepa lawama. Leo hii CCM haina mahali inapoweza kusimama na kusema hii ndiyo ngome yetu. Wamebaki na ukabila na dini kama silaha ya mwisho.

Tabaka la wasomi wajuu na wa kati limewakimbia, wafanyakazi wameasi na wakulima hawataki tena kusikia hadithi.
Ukijumuisha na makundi ndani ya chama, CCM ipo njiani kuungana na UNIP na KANU. Suala ni muda wala siyo kwanini.

NCCR:
Chama kiliundwa na tabaka la wasomi wa juu na kati. Hakikuwa na wafuasi katika matabaka mengine.
Ili kuleta mvuto NCCR iliwaalika viongozi kama mrema aliyejipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge.
Kwa bahati mbaya chama kilikuwa kama kundi la harakati na si la kisiasa.

Chama hakikufuata misingi na taratibu. Migongano ya uongozi ikaanza na kupelekea political base yao kuvunjika moyo. Hakuna msomi aliyetaka kujishirikisha na NCCR tena kwasababu ilipoteza maana nzima ya chama cha siasa na kubaki genge la wanaharakati wanaotaka madaraka. Viongozi wote waliishia kutafuta masilahi yao kwingineko.
ngome ikaanguka na sasa hakuna anayejua Political base ya NCCR ni ipi.
NCCR haiwezi kukwea ngazi tena na uwezekano wa kupotea kama CUF ni mkubwa

CHADEMA
Chama kilianza taratibu kwa kuwa na safu ya viongozi wastaafu, hakikuwa na ngome hasa ya kujivunia.
Ukuaji wake umekuwa taratibu na kwa umakini. Ni chama kilichobadilisha viongozi mara tatu bila mtafaruku.
CDM imekabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na tuhuma za ukabila na udini
Sifa ya kubadilisha viongozi ilikaribia kuingia nyongo katika maika ya karibuni na hilo limebaki kuwa changamoto.

Pamoja na hayo ukuaji wa CDM umechukua kasi isiyotarajiwa. CDM kimeweza kuvunja ngome za vyama vyote licha ya changamoto nyingi za kisiasa. Kama ilivyo kwa vyama vingine CDM nayo ina ngome 'political base'.

Ngome ya kisiasa ya Chadema inayokipa chama umaarufu wa kimbunga ni ipi? Kwanini kuna changamoto ndani ya ngome yao na CDM ifanye nini!

Itaendelea.....
 
Back
Top Bottom