Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Inaendelea.......

Ngome ya kisiasa ya Chadema ni tabaka la wasomi. Kuna sababu nyingi za kutokea hili
1. Ni kutokana na tabaka la wasomi kuona mambo yanavyokwenda CCM. Wamebaini kuwa mabadiliko sasa ni muhimu.
Tabaka hilo lina wale wanaoamini kuwa kuibadilisha CCM lazima mtu awe na fedha.
Miongoni mwao wanaamini kuwa ili uwe sehemu ya 'system' ni lazima uwe ndani ya chama. Hili la pili ndilo liliobaki na CCM

2. Juhudi za Chadema kuwaingiza katika siasa vijana 'recruit' . Vijana hao wameonyesha wazi kuwa kuna tofauti za mitizamo kwa vizazi vilivyopo(wazee na vijana).

Katika ngome hii ya kisiasa tabaka la wasomi linaundwa na vijana. Hii ndiyo inapelekea wasomi wengi makazini na vyuoni kuunga mkono CDM. Kwa hilo tu linazaliwa tabaka la wafanyakazi ambao wengi ni wasomi hasa kada ya kati.
Kada hii ya wasomi vijana imekuwa na ushawishi mkubwa sana kisiasa kiasi cha kugeuza wakulima kuunga mkono. Ndiyo maana CDM sasa inavuna wanachama huko vijijini.

Hata bila kada ya wasomi, kuna jambo moja linaiumiza sana CCM. Mgawanyiko ndani ya chama umekifanya chama kidumae kimaamuzi. Lipo Kundi la wenye chama na pesa na kundi linaloamini chama kimepoteza mwelekeo.

Kibaya zaidi ni uongozi wa CCM kuwatenga na kuwanyanyasa viongozi wazee. Haya yote yamekifanya chama kionekane kama genge la waporaji. Matokeo ya haya ni wanachama kutoona siku za usoni 'future' na hivyo kutafuta mbadala ambao ni CDM kwa wakati tulionao.

Ingawa CDM ina ngome kubwa ya vijana na wasomi, ni lazima ichukue tahadhari. Vijana ni watu wenye matamanio, mbinu na wakosefu wa busara kwa baadhi ya nyakati. Tumeona misuguano ndani ya Chama ikiwa na chanzo cha vijana. Tumeona baadhi wakikosa uzooefu wa kisiasa hasa kwenye majukwaa n.k.

Kibaya zaidi ni CDM kuiga mbinu za CCM katika kushughulikia matatizo hasa ya vijana ndani ya chama.
Migogoro inayoimaliza CCM ni zao la migogoro ndani ya UVCCM. Vijana hao walitumiwa na wazooefu kuleta mtafaruku ambao unafukuta hadi sasa. Tunakumbuka akina Guninita, Nchimbi, Malisa, Masauni, Nape, Mkalla, Francis n.k walivyopita katika mitifuano.

Hali si tofauti ndani ya Chadema, kuna migongano na makundi yasiyo rasmi ndani ya chama.
Makundi ndani ya vyma hayawezi kuepukwa kwa asilimia mia, lakini yanaweza kupunguzwa nguvu yasilete uharibifu.
Habari za ndani ya chama zinavuja na kuna mashambulizi ya chini chini hata hapa JF yanaonekana.
Akina Kafulila hawakufanya waliyoyafanya 'solo' bado wana wafuasi waliojificha.

Kiklichotokea siku za karibuni ni ushahidi kuwa kuna mgogoro ndani ya BAVICHA. Sipendi kurejea kiini cha mgogoro lakini inatosha kusema kuna vita kati ya Mwenyekiti na makamo wake ushahidi wa wazi kuwepo kwa makundi.

Tatizo ninaloliona ambalo ni kubwa ni lile lile la kushughulikia mambo ki-CCM, kwamba kuna tatizo lakini litatafutiwa maelezo, mbinu na hadithi katika utamaduni ule ule wa kulindana.

Sioni kwanini hatua za nidhamu hazijachukuliwa kwa Juliana Shonza ambaye ni wazi kwa vigezo vyovyote vile ni mkosefu na mtovu wa nidhamu. Ni mtumiwa wa kuleta vurugu

Tumeona jitihada za kumlinda kwa maneno matamu kama vile, bado ni mdogo, afundwe n.k. Ni kulindana kule kule kwa CCM kulikodhoofisha ngome yao.

Matarajio ya wengi ni kuona mbadala wa CCM kwa vitendo na si maneno. Kwa hili la kulinda watovu wa nidhamu kama Juliana kuna madhara mengi yatokanayo

1. Kuendeleza makundi kwasababu tayari makamu mwenyekiti amejihakikishia ulinzi ndani ya chama
2. Kudhoofisha nguvu za ngome ya vijana kwa kuwagawa, kutofanya kazi pamoja n.k.
Leo ni uongo kujidanganya kuwa Heche na Juliana wanaweza kufanya kazi pamoja hapo ndio mwanzo wa mparaganyiko

3. Kuwavunja nguvu wote wanaodhani CDM inaweza kuja na jipya. Kama hawawezi kumwadhibu mtovu wa nidhamu wa maneno sijui watawezaje kumwadhibu fisadi aliyebobea. Swali linabaki je CDM wana preach what they do!

4. Inaondoa uhalali wa CDM kuikemea CCM kwasababu utawezaje kumwambia JK amwajibishe Waziri mkuu ikiwa wewe huwezi kumwadhibu simple person Juliana Shonza makamu wa BAVICHA?

Ni malizie kwa kusema kuwa wenzetu wanathamini sana 'political base' zao katika siasa. Na hakika kama chama kinataka kuanguka kisiasa basi kianze na ku-demoralize ngome zake. CCM ilipo ni matokeo ya kudharau ngome zilizoifanya isimame kama chama kwa nusu karne.

Nitahadharishe tu kuwa kuchanua kwa Chadema kutakuwa na maana kama ngome yao itaridhika na mwenendo wa chama.Migogoro ya chini chini inakiweka chama mahali pa gumu hata kama si dhahiri.

Tusemezane
 
Inaendelea.......

Ngome ya kisiasa ya Chadema ni tabaka la wasomi. Kuna sababu nyingi za kutokea hili
1. Ni kutokana na tabaka la wasomi kuona mambo yanavyokwenda CCM. Wamebaini kuwa mabadiliko sasa ni muhimu.
Tabaka hilo lina wale wanaoamini kuwa kuibadilisha CCM lazima mtu awe na fedha.
Miongoni mwao wanaamini kuwa ili uwe sehemu ya 'system' ni lazima uwe ndani ya chama. Hili la pili ndilo liliobaki na CCM

2. Juhudi za Chadema kuwaingiza katika siasa vijana 'recruit' . Vijana hao wameonyesha wazi kuwa kuna tofauti za mitizamo kwa vizazi vilivyopo(wazee na vijana).

Katika ngome hii ya kisiasa tabaka la wasomi linaundwa na vijana. Hii ndiyo inapelekea wasomi wengi makazini na vyuoni kuunga mkono CDM. Kwa hilo tu linazaliwa tabaka la wafanyakazi ambao wengi ni wasomi hasa kada ya kati.
Kada hii ya wasomi vijana imekuwa na ushawishi mkubwa sana kisiasa kiasi cha kugeuza wakulima kuunga mkono. Ndiyo maana CDM sasa inavuna wanachama huko vijijini.

Hata bila kada ya wasomi, kuna jambo moja linaiumiza sana CCM. Mgawanyiko ndani ya chama umekifanya chama kidumae kimaamuzi. Lipo Kundi la wenye chama na pesa na kundi linaloamini chama kimepoteza mwelekeo.

Kibaya zaidi ni uongozi wa CCM kuwatenga na kuwanyanyasa viongozi wazee. Haya yote yamekifanya chama kionekane kama genge la waporaji. Matokeo ya haya ni wanachama kutoona siku za usoni 'future' na hivyo kutafuta mbadala ambao ni CDM kwa wakati tulionao.

Ingawa CDM ina ngome kubwa ya vijana na wasomi, ni lazima ichukue tahadhari. Vijana ni watu wenye matamanio, mbinu na wakosefu wa busara kwa baadhi ya nyakati. Tumeona misuguano ndani ya Chama ikiwa na chanzo cha vijana. Tumeona baadhi wakikosa uzooefu wa kisiasa hasa kwenye majukwaa n.k.

Kibaya zaidi ni CDM kuiga mbinu za CCM katika kushughulikia matatizo hasa ya vijana ndani ya chama.
Migogoro inayoimaliza CCM ni zao la migogoro ndani ya UVCCM. Vijana hao walitumiwa na wazooefu kuleta mtafaruku ambao unafukuta hadi sasa. Tunakumbuka akina Guninita, Nchimbi, Malisa, Masauni, Nape, Mkalla, Francis n.k walivyopita katika mitifuano.

Hali si tofauti ndani ya Chadema, kuna migongano na makundi yasiyo rasmi ndani ya chama.
Makundi ndani ya vyma hayawezi kuepukwa kwa asilimia mia, lakini yanaweza kupunguzwa nguvu yasilete uharibifu.
Habari za ndani ya chama zinavuja na kuna mashambulizi ya chini chini hata hapa JF yanaonekana.
Akina Kafulila hawakufanya waliyoyafanya 'solo' bado wana wafuasi waliojificha.

Kiklichotokea siku za karibuni ni ushahidi kuwa kuna mgogoro ndani ya BAVICHA. Sipendi kurejea kiini cha mgogoro lakini inatosha kusema kuna vita kati ya Mwenyekiti na makamo wake ushahidi wa wazi kuwepo kwa makundi.

Tatizo ninaloliona ambalo ni kubwa ni lile lile la kushughulikia mambo ki-CCM, kwamba kuna tatizo lakini litatafutiwa maelezo, mbinu na hadithi katika utamaduni ule ule wa kulindana.

Sioni kwanini hatua za nidhamu hazijachukuliwa kwa Juliana Shonza ambaye ni wazi kwa vigezo vyovyote vile ni mkosefu na mtovu wa nidhamu. Ni mtumiwa wa kuleta vurugu

Tumeona jitihada za kumlinda kwa maneno matamu kama vile, bado ni mdogo, afundwe n.k. Ni kulindana kule kule kwa CCM kulikodhoofisha ngome yao.

Matarajio ya wengi ni kuona mbadala wa CCM kwa vitendo na si maneno. Kwa hili la kulinda watovu wa nidhamu kama Juliana kuna madhara mengi yatokanayo

1. Kuendeleza makundi kwasababu tayari makamu mwenyekiti amejihakikishia ulinzi ndani ya chama
2. Kudhoofisha nguvu za ngome ya vijana kwa kuwagawa, kutofanya kazi pamoja n.k.
Leo ni uongo kujidanganya kuwa Heche na Juliana wanaweza kufanya kazi pamoja hapo ndio mwanzo wa mparaganyiko

3. Kuwavunja nguvu wote wanaodhani CDM inaweza kuja na jipya. Kama hawawezi kumwadhibu mtovu wa nidhamu wa maneno sijui watawezaje kumwadhibu fisadi aliyebobea. Swali linabaki je CDM wana preach what they do!

4. Inaondoa uhalali wa CDM kuikemea CCM kwasababu utawezaje kumwambia JK amwajibishe Waziri mkuu ikiwa wewe huwezi kumwadhibu simple person Juliana Shonza makamu wa BAVICHA?

Ni malizie kwa kusema kuwa wenzetu wanathamini sana 'political base' zao katika siasa. Na hakika kama chama kinataka kuanguka kisiasa basi kianze na ku-demoralize ngome zake. CCM ilipo ni matokeo ya kudharau ngome zilizoifanya isimame kama chama kwa nusu karne.

Nitahadharishe tu kuwa kuchanua kwa Chadema kutakuwa na maana kama ngome yao itaridhika na mwenendo wa chama.Migogoro ya chini chini inakiweka chama mahali pa gumu hata kama si dhahiri.

Tusemezane

Could you please list 10 the so called wasomi from CHADEMA camp? Include their intellectual feats in parentheses .
 
Could you please list 10 the so called wasomi from CHADEMA camp? Include their intellectual feats in parentheses .
Tunaposema wasomi hatuna maana mtu mmoja mmoja. Na wala hatumaanishi PhD au master. Tunaposema wasomi tunaangalia katika mizania ya nchi yetu ya kwamba kundi linaloweza kuelezwa kitu na kuhoji, kukubali, kukataa au kuwa na mashaka (doubts)

Hata makundi ya wasomi yana ngazi zake na kama umesoma vizuri nimetumia neno wa kada ya kati, siyo wajuu au waliobobea.

Ukiangalia kukubalika kwa CCM katika kada zote, vyuo na taasisi ni mdogo sana. Mzee Msekwa alikiri hili.
Kwa nchi masikini kama yetu japo hao tunathubutu kuwaita wasomi kuliko yule anayengoja kusikia ahadi tamu hata kama hajui zitafanyikaje. Si rahisi ukaenda katika taasisi ukawaambia watu unaweza kubadili Kigoma ikawa Dubai wakakuelewa achilia mbali kukutemea mate. Ukiyaeleza hayo kwa wale tunaojua 'hawakubahatika' watapiga makofi na vigele gele.

Endapo tutawataja mmoja mmoja basi huenda CCM ikawa na wengi ndani ya chama chake, lakini je hao ndio CCM au CCM ni mkusanyiko wa wanachama? Je, wananchama wanaopewa khanga na kofia na kisha kusahau machungu yao ya kila siku wanakiwango gani cha uelewa na wapo kumdi gani?
 
MUUNGANO; TANGANYIKA IJIHADHARI NA MBINU CHAFU
UNDUMILA KUWILI WA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD

Vugu vugu la muungano limepamba moto hasa baada ya Wazanzibar kuonyesha hisia zao na safari hii kwenda mbele na kuchoma moto mali za watu. Sioni tatizo kwa watu kujadili muungano lakini basi iwe katika njia za ustaarabu na weledi.

Ukifuatilia malalamiko ya Wazanzibar ima unaweza kujikuta unapatwa na hasira au kubaki unacheka kutwa nzima.
Malalamiko yao ni ya muda mrefu na yanabadilika kutokana na nyakati.
Ukisikiliza mijadala ya nyuma hoja kubwa ilikuwa ni kwanini Rais wa muungano hatoki Visiwani.
Hilo likafa baada ya Mwinyi kuwa Rais. Sasa hivi kuna hoja kwanini mkuu wa Polisi IGP hajawahi kutoka visiwani!

Endapo wasingekuwa na husuda chuki au fitina na kama wangelikuwa wanaongozwa kwa weledi Rais wa sasa angekuwa Mzanzibar. Fitna dhidi ya Salim Ahmed Salim ambaye anakubalika sana Tanzania bara ilifanywa na Wazbar kwa vile tu anadamu ya kiarabu. Haya yameelezwa kwa kina na mwandishi Ally Salehe, mtu mwenye ushawishi wa juu sana katika siasa za visiwani. Ally katika makala yake ameenda mbali na kubainisha kuwa Waunguja wanasema hawatatawaliwa tena na Waarabu na hata kumtetea Nyerere kuwa kama angalikuwa hai asingeweza kuvumilia hali hiyo

Mwandishi wa makala za gazeti la Raia mwema bw Ahmed Rajabu yeye amemlaumu Nyerere kama chanzo cha fitna dhidi ya wanunguja na wapemba. Hakubali ukweli wa Ally Salehe na kuliangalia tatizo kwa undani bali amechukua mfumo wa kundi la UAMSHO wa kutojadili tatizo la muungano na kukimbilia kuchoma moto makanisa hata kama waumini wake hawajui muungano ni mdudu gani.

Ahmed anadhani tatizo la muungano ni Nyerere hata kama hayupo na ameshindwa kuliona tatizo halisi.
Makala zake zinawatetea UAMSHO na wiki hii ameonyesha chuki ya wazi dhidi ya Watanganyika.

Malalamiko mengine ya Wzbar ni ni kuhusu uwiano katika bunge. Hadi sasa wabunge wa wa bunge la muungano kutoka Zbar wanawakilisha idadi ya watu 10,000 au chini ya hapo. Wabunge hao wana hadhi sawa na mbunge Zitto Kabwe anayewakilisha watu milioni au John Mnyika anayewalisha zaidi ya watu milioni 1.5. Bado Wzbar wanataka wabunge zaidi pengine kila mmoja awakilishe nyumba 10. Hapa ndipo unaweza kupata kicheko ksicho cha lazima.

Lalamiko lingine ni kuhusu misaada. Wao wanadai kuwa kama kuna msaada wa sh 10 basi wanapaswa kupata sh 5 kwa vile ni nchi iliyoungana na nyingine.
Idadi ya Wazbar ni takribani milioni 1.2 na hiyo inalinganishwa na milioni 40.Hizi ndizo hoja za UAMSHO na Wzbar.
Mwendelezo wa malalamiko ni mkubwa sana kiasi cha kutotambua hasa wanataka nini.

Huko nyuma waliwahi kutaka bendera na wimbo wa taifa, vyote wakapata si kwa idhini ya mtu yoyote bali idhini yao.
Wamekiuka katiba ya JMT mara nyingi na hakuna anayewakemea.
Wamepitisha hata mabadiliko ya muundo wa serikali ambao kisiasa unaathari huku bara na hakuna anayewalalamikia.
Wamedai mafuta si ya muungano hakuna aliyewakataza, wameunda vyombo vyao hakuna aliyewazuia.
Kwa ufupi hakuna wanachotaka na hawajapewa hata kama hawastahili bado wamepewa

Nikumbushe tu kuwa katika mambo 11 ya muungano asilimia 98 inawahusu wao. Hata yalipoongezwa na kufikia 22 bado yanawahusu wao. Kwa bahati mbaya wao wanongozwa na jazba zaidi kuliko weledi vinginevyo wangekaa chini na kufikiri

Nimelazimika kutoa usuli huo kwa ufupi(feedback) ili hoja zitazaofuta ziwe na mahali pa kusimamia.
Tuangalie na kujiuliza hivi Wzbar wanataka nini?
1. Kuna kundi la UAMSHO wao wanatka muungano uvunjwe ili Zbar huru ipatikane
2. Kuna kundi la wasomi linaloona hatari ya kuvunjika muungano kwa Zbar
3. Kuna kundi la wafanyabiashara na waajiriwa wao wanaona muungano uwe tofauti na tulio nao
4. Kuna kundi la masilahi, hili halijulikani linasimamia wapi na lina viongozi na wabunge

Uwepo wa makundi hayo ndicho chanzo cha Wbar kutojua nini wanataka na kushindwa kujenga hoja zenye maana na mashiko. Wapo watu wakaosema hoja ya Zbar ni kuwa Jamhuri, hiyo ni sawa! lakini wzbar wote wanakubaliana na hilo?

Ama baada ya kuandika hayo tuangalie japo kidogo misimamo ya makundi hayo na kwanini inakuwa ngumu kuwa na msimamo wa pamoja.

Tuangalie madai ya muundo wa muungano wanoutaka, na kwanini wanataka hivyo
Tuichambue hotuba ya kinara na mchochezi mkubwa wa siasa za Zbar bw. Seif ya wiki hii
Halafu tuangalie Tanganyika ipo katika mtego gani

Itaendelea........
 
Inaendelea.....
Katika makundi yaliyotajwa misimamo yao juu ya muungano ni'
1. UAMSHO- Wao hawataki muungano na wanaamini zanzibar nje ya muungano itakuwa nchi ya kiislam na itafaidika na fursa kama misaada kutoka Uarabuni. Ni kundi linaloangalia mambo kwa mtazamo mfupi likiongozwa na jazba zaidi na udini

2. Kundi Masilahi- Hili halijulikani linasimamia nini kwasababu uwepo wa muungano kwao ni mafao kama tunavyoona wabunge na viongozi katika serikali. Ni kundi lililotekwa na masilahi na kuuza uhuru wa kujieleza.

3. Kundi la Wasomi linaona hatari ya Zanzibar kama kisiwa kidogo kuwa peke yake. Linaamini kuwa huenda nchi hiyo ikapigwa udalali siku moja. Kubwa zaidi linaamini Znbar ipo katika kivuli cha Tanganyika kisiasa, utamaduni, jamii na kicuhumi. Kwahiyo kuvunja muungano si jambo jema kwa upande wa visiwani

4. Kundi la wafanyabiashara na waajiriwa nalo lina watu wenye weledi. Tatizo la kundi hili ni kukinzana kwa masilahi ya muda mrefu na hatima yao nje ya muungano. Nalo halipendi kuvunjwa kwa muungano.

Ukiacha kundi 1 na 2, kundi 3 na 4 ndio wanaounda hoja za kujibanza karibu na Tanganyika. Wanasema hivi;
1. Ziwepo serikali 3
au
2. Mkataba wa ushirikiano
au
3. Mahusiano kama ya EAC na EU kati ya nchi mbili tu.

Tutaziangalia hoja zote kwa nguvu zake na udhaifu wake tukiifikriri Tanganyika ina nafasi gani katika hayo hapo juu.

Kwasasa turudi kwenye hotuba ya maalimu Seif aliyoitoa juzi. Ukiiangalia kwa makini utabaini undumila kuwili wa maalim Seif. Ikumbukwe kuwa Maalimu hana sifa ya kutetea muungano kwa kile anachodai muungano umempoka Urais.
Maalim pia ni mshiriki mzuri wa UAMSHO hata kama anakana lakini hilo lipo wazi hata kwa mjinga.

Katika hotuba maalimu ameuliza maswali ya kuwakubumbusha Wzbar kuwa muungano ulikuwa una kikomo cha miaka 10. Hayo ni moja ya madai yao. Akasema Yeye na wenzake watalinda masilahi ya Zanzibar na kusema atafanya hivyo kama wanavofanya Watanganyika

Huyu ni mtu aliyetumikia serikali zote katika ngazi ya juu na hatukuwahi kumsikia hata siku moja akionyesha 'concern' juu ya muungano badala yake yeye ndiye alikuwa nyuma ya mpango mzima wa kumhujumu Aboud Jumbe aliyekuwa anatetea masilahi ya Zanzibar.

Maalim Seif akasema wachache wasikilizwe na wengi wapewe, akasisitiza Wzbar wajitokeze kutoa maoni.
Hapa Seif alikuwa anashadidia hoja za UAMSHO kama 'wengi' akiwatetea kuwa wanapaswa kusikilizwa.
Hilo la utetezi halina shida, tatizo ni pale aliposhindwa hata kulaani uhuni wa UAMSHO ambao ni Boko Haram, Alshaabab au Alqaeda ya kanda hii. Sura ya mtazamo wa Seif ni kuvunja muungano.

Katika kuhofia madhara yatokanyo, Seif akasema tuwe na serikali 3, mbili au ushirikiano kama wa EU na EAC.
Hakuweza kueleza kwanini tuwe na serikali 3, 2 au Uhsirikiano kwasababu hana hoja za kutetea msimamo huo.
Maalimu anaelewa kuwa serikali 3 Zbar itapaswa iwe mshiriki wa masilahi na si porojo hivyo swali la itaendeshwaje hatakuwa na jibu.
Serikali 2 kwa mkataba nalo pia litamletea swali mambo yapi yawe ya mkataba, na hana jibu
Ushirikiano wa EU, Seif anasema huo ndio mtazamo mpya.

Anamalizia hotuba kwa kusema muungno ni muhimu sana. Ukisoma hotuba yake haitakuchukua muda kujua kuwa huyu ni ndumila kuwili. Hakuna ubishi yeye ni UAMSHO na jitihada zote za uamsho zina mkono wake.

Kujaribu kutetea muungano ni unafiki kama ule wa kuwatanguliza watu katika maandamano na yeye kukimbia Ulaya Ziarani.Kwa ufupi Seif hana mamlaka ya kiroho 'moral authority' ya kuongelea muungano kwasababu historia inamsuta na undumila kuwili ni sehemu ya hulka yake. Nadhani ni jambo jema kumpuuza

Swali muhimu kujiuliza ni kwanini Wzbar wanaolaani muungano hadi kuchoma moto watu na mali zao, hao hao wanataka kuwe na ima Serikali 3, Mkataba au uhusiano maalumu. Kuna nini cha muhimu ambacho tunadhani kwasasa si muhimu kwa muungano lakini kitakuwa muhimu tukiwa na serikali 3, makataba au uhusiano maalumu kama wa EU?

Ni kwanini Wzbar ambao wanauwezo wa kuvunja muungano kama walivyowahi kufanya ukiukaji wa taratibu wanasita kuvunja muungano? Why? Kuna kitu gani wanacho vizia hawa!

Itaendelea.........
 
Inaendelea.....

Serikali 3:
Wazbar anataka uwepo wa serikali 3, ya Tanganyika, Zbar na Muungano. Hii ya Muungano haijulikani itakuwa na mamlaka gani na itashughulikia nini. Haieleweki kwa sababu katika nchi nyingine serikali ya muungano ndiyo inayoshughulikia mambo ya ulinzi na siasa za nje. Zanzibar wanadai wawe na kiti UN, AU na EAC, kwa mantiki hiyo mambo yanayopaswa kuwa ya muungano hawataki yawe hivyo.

Ukweli ni kuwa wanataka serikali ya muungano ili kuwasaidia katika mambo mazito. Mathalani, Wazanzibar wanasoma kwa mikopo kutoka muungano. Wakijitenga hilo litakuwa mzigo mkubwa sana. Wanafahamu bajeti ya ulinzi ilivyo na gharama kwa Zanzibar. Ajira ni tatizo kubwa sana kwa kisiwa cha Zbar. Idadi ya Wzbar wanaofanya kazi muungano au Tanzania bara ni zaidi ya mara mbili ya wale wa SMZ. Nje ya muungano idadi kubwa itabaki bila ajira.

Katika uwekezaji, Wzbar wanafahamu kuwa hakuna mahali popote dunia watakapo pata fursa kama Tanzania bara. Fursa hizo ni pamoja na kutoulizwa kwa namna yoyote uwekezaji uwe katika nyanja yoyote ile. Hii inaitwa 'free ride'

Kiuchumi wanafahamu kuwa soko kubwa la mzanzibar ni bara, hata milango ya ushirikiano na nchi za jirani ni kwa kupitia Tanzania bara. Hivyo nje ya muungano hakuna atakayeweza kufanya shughuli zake katika ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa starehe kuliko ilivyo sasa. Kwa kupitia Tanzania bara, Zanzibar inapakana na nchi zote zinazopakana na Tanzania.

Ukiangalia mambo hayo utagundua kuwa faida za wao kuishi Tanzania bara ni pamoja na kuwasaidia wale waliobaki Zbar.
Nje ya muungano kila Mzanzibar ataonja machungu hayo kwa dhati, awe Zbar au popote pale alipo.
Hayo ni miongoni mwa mengi ambayo nje ya muungano mzanzibar wa kawaida hatayapata isipokuwa tabaka la mamwinyi.

Ni sababu hizo ndizo zinawasukuma waje na hoja za mkataba au ushirikiano kama wa EU/EAC.
Wanaoweza kuliona hili ni wasomi na wala si UAMSHO(Boko haram) ambao wao wanadhani ustawi wao ni utegemezi wa dini na mahusiano na Uarabuni.

TANGANYIKA IJIHADHARI
Ni ukweli usio na kificho kuwa Tanganyika haina chochote inachofadika nacho zaidi ya kubeba zigo hili la misumari.
Uwepo au kutokuwepo kwa Zanzibar hakuna athari yoyote kiulinzi, uchumi au kisiasa.

Kwa vile Zbar haiukbali mahusiano na bara na kwa vile chuki zao dhidi ya Mtanganyika zimefikia kikomo hakuna budi kuwaacha waende zao. Tena waende kwa amani kwasababu tutakuwa tumepunguza mzigo mzito sana

1. Nafasi za upendeleo katika mambo ya elimu zitabaki kuwa za Watanganyika na hivyo hakuna sababu kijana aliyefaulu vizuri anyimwe fursa kwa gharama za upendeleo kwa mzanzibar ambaye amefaulu katika kiwango cha chinii sana.
Kwa vile wameunda baraza lao la mitihani sasa ni wakati vyuo vyetu vifanye udahili kwa kigezo cha elimu na siyo nafasi maalumu. Vinginevyo wapeleke watoto wao katika vyuo vyao na si vya kwetu kwa gharama zetu.

2. Kwa vile hakuna Mtanganyika anyepata ajira kwa kigezo cha Uzanzibar, hakuna haja ya kuwaacha vijana wetu wakizurura na CV zao mikononi ili hali nafasi za kazi katika nchi yao wanayolipia kodi wao na wazazi wao zichukuliwe na Wazbar. Ni wakati sasa kuwepo na mkakati maalumu wa kuwaondoa katika ajira ili ziwasadie watu wetu kama wanavyofanya wao. Kinyume chake Watanganyika wenye uchungu na nchi yao wanadhima ya kuchukua hatua za kuzuia, kuwaondoa au kuwafukuza Mzanzibar yoyote yule anayefanya kazi bara.

3. Wawekezaji wote kutoka Zanzibar nao pia wapitie kituo cha uwekezaji kama Waingereza, makaburu au wakenya.
Ni hatari sana kuwaacha wzbar wajitwalie mapande ya ardhi tukijua kuwa huo ndio mwanzo wa kukaribisha UAMSHO na boko haram nchini na pia kwa ukweli kuwa hakuna Mtanganyika atakayepewa ardhi visiwani.

4. Serikali ya Tanganyika iache kufadhili vitu kama umeme kwa gharama za wananchi wake. Haiwezekani bili ya umeme alipe Mtanganyika kwasababu tu Mamwinyi hawataki kulipa. Huu ni uonevu wa hali ya juu kwa Mtanganyika.
Ni uonevu kama wa kulipia ada Wazbar wanosoma huku bara huku tukiwaacha watoto wetu wakiwa hawana pa kwenda.

5. Serikali ya Tanganyika sasa iache kulipa mishahara ya SMZ na pesa hizo zitumike katika miradi ya kuwasaidia wananchi. Ni dhambi kuchukua kodi ya Mtanganyika ili ikalipie mshahara mfanyakazi wa Zbar ambaye hataki muungano na wala haoni faida yake.

6. Ni wakati sasa Tanganyika iache kutumia pesa za walipa kodi na iache Zanzibar igharamie huduma zake kama
a) Kulipia bili za umeme kama Mtanzania mwingine yoyote yule na hakuna ruzuku za umeme
b)Kulipia gharama za jeshi lao la ulinzi na polisi
c)Kulipa mishahara ya wafanyakazi wa SMZ bila ruzuku kutoka bara
d)Ibebe dhama ya kueleimisha watu wake kwa gharama za kodi za Wzbar
e)Kuzuia mianya ya kodi kwa kigezo cha muungano

Katika kikao kinachoendelea cha bunge Watanzania bara tunawataka Wabunge wetu wasimamie masilahi yetu kikamilifu.
Nina imani akina Zitto Kabawe, John Mnyika, Kigwangala, Fikunjombe,Mdee Haliama, Mbowe na wengine wengi tu watasimama kidete kuwaambia ukweli kuwa Wazanzibar kadri walivyotuchoka nasi tumewachoka.

Kwa Watanzania wengine, hakuna kukubali serikali 3, 2, uhusiano maalumu au upuuzi na ujinga unaofanana na huo.
Akina Maalim Seif, Ahmed Rajab, Salehe Ally hawawezi kuelezea ni kwanini tuvunje muungano halafu tuwe na vitu hivyo.
Hawawezi kutetea hoja zao ingawa wana siri moyoni. Hatuwezi kukubali ushauri wa kijinga na kipuuzi usioweza kujengewa hoja za maana. Huu ni upuuzi kwasababu huwezi kutamka jambo usiloweza kulitetea.

Tusikubali hoja za wababishaji na wapuuzi kuhusu muundo wa muungano hadi watakapokuja na takwimu za nini maana ya serikali 3, 2 au uhisiano maalumu.Kuna siri nyuma ya haya na siri hiyo ni kuendelea kumnyonya Mtanganyika.

Tunawaomba Watanganyika wote waelewe kuwa hoja iliyopo mbele yetu ni kuvunja muungano.
Anayepaswa kufanya hilo ni Mzanzibar. Kura ya maoni ni kwao kwasababu sisi hatuhitaji kura hiyo.
Hoja iliyo mbele yetu ni moja tu, LET ZANZIBAR GO!
 
KWANINI BUNGENI KUNAWAKA MOTO?

Kikao kinachoendelea cha bunge kimeanza kwa tambo, majibizano na lugha zisizo za kawaida. Ni rahisi sasa kusikia wabunge wamefunga milango kama mabungeni mengine duniani na kuanza kurushiana makonde.
Ule uvumilivu na kustahamiana sasa kunafikia kikomo.

Kwa haraka haraka mtu anaweza kudhani ni uzalendo unaotawala! ukweli ni kuwa hali ya kisiasa nchini ndiyo inabadilisha hesabu 'The equation' na wala si uzalendo halisi. Hili haliondoi ukweli kuwa wapo wazalendo na hao wanajulikana kwa maneno na matendo yao. Hawakuanza leo walikuwepo na watakuwepo

Kasi ya huu uzalendo wa ghafla inachagizwa sana na hali ya kisiasa. Kama nilivyosema awali wananchi wamebadilika na ndio wanabadili mtazamo wa kila jambo. Huko nyuma wananchi walidhani bunge ni sehemu tu ya serikali na wao hawana hoja, ushiriki wao wa bunge unaisha baada ya uchaguzi. Hali sasa ni tofauti sana, aghalabu utamuona kijana mdogo kabisa baada ya kuangalia Manchester na Arsena anabadilisha TV kusikiliza bunge linasemaje

Wananchi wameweza kuvuka hata mistari ya kisiasa na si ajabu kumsikia mshabiki, mpenzi au mwanachama wa chama pinzani akimsifia mbunge wa upande wa pili kwa hoja zake za nguvu.

Tumeona wabunge wakishinda chaguzi bila kujali udogo wa vyama vyao.
Tumeona wabunge vijana sana katika kumi la pili la umri wao na hata jinsia wakitawazwa.
Tumeona jinsi pesa ilivyo na ukomo katika ushawishi wa kisiasa n.k

Ni kutokana na nguvu hizo za mabadiliko zinazolamishwa na wananchi wabunge nao wanabadilika kwenda na wakati.
Ule wakati wa kutegemea chama sasa umepitwa na wakati wa kutumia fedha sasa naona muda unakwisha.

Tulipo ni mahala pa mtu kujijenga na kujenga hoja ili awe mbunge na si vinginevyo.
Ni wazi kuwa wabunge wanaofanya mambo yanayoligusa taifa sasa wanaonekana dhahiri mbele ya wananchi na wanapewa heshima stahiki. Kwa sasa ubunge ni 'how you stand out of the crowd' unawezaje kujitokeza katika kadamnasi
ya washindani wako ukaonekana.

Jambo hili linatokea kwasababu kuu mbili;
1. Wabunge na wagombea kuamini kuwa siasa za uchama ni utumwa na wala huhitaji kuwa mtumwa ili upate ubunge
2. Wananchi ndio wanaochagua mbunge na si chama
3. Ukimya na utiifu wa uongo ni kujimaliza kisiasa

Kwa muktadha huo, tumeona jinsi wabunge kama wa CCM wanavyoasi chama chao hadharani bila woga tena wakijinasibu kuwa kama ni kufkuzwa na iwe hivyo. Hili lilikuwa mwiko mkubwa ndani ya chama zama hizo

Tumeona ulaghai wa bunge na kamati za chama kama CCM zisivyofanya kazi hadi kufikia mahali pa kutaka kumwajibisha mwenyekiti wa kamati ya wabunge wa chama ambaye ni waziri mkuu.

Kutokana na kubadilika kwa hali ya kisiasa nchini na hofu ya siku za usoni, utawala ndani ya bunge hasa kwa chama tawala sasa ni mgumu sana kuliko wakati mwingine.

Tunakoelekea 2015 huenda tusifike huko au tukifika tutakuwa na majeruhi wengi sana wa kisiasa. Watarajiwa wa majeruhi ni wale walioamua kukaa kimya au kutetea uozo. Majeruhi ni wale wanaoficha nafsi zao kwa utiifu wa vyama vyao.

Tunafahamu hali ya kudorora kisiasa kwa chama tawala, na hakika hali ni mbaya sana hata kama yupo atakayejifariji.
Kwa upande wa pili wabunge wa upinzania ambao wamekuwa na misimamo ya utaifa 'vocal' wanazidi kujitwalia umaarufu na kuimarisha vyama vyao.

Kuna chaguo moja tu lilo mbele ya wazalendo, na wale wanaoingalia 2015 kwa jicho mujarabu. Ni kuonyesha wapiga kura wao kuwa nao wanajali. Ikifika hapo muungano wa wapinzani na wale wa chama tawala hautakuwa rasmi bali utakuwa wa asili 'natural'.

Tutashuhudia serikali ikiwa katika wakati mgumu sana.
Mbunge wa chama tawala anaposimama mbele ya vipaza sauti na kusema bajeti ya serikali ya chama chake haifai, hapo lipo jambo.

Lakini pia hakuna msafara wa mamba usio na kenge, wapo watakaosimama na kutetea hata uozo kwasababu hapo ndipo karata yao ilipo. Wapo watakaohalifu au kutetea uozo kwasababu zao za kisiasa hasa kimakundi kuelekea 2015

Nimalizie kwa kusema kuwa upepo wa kisiasa unaovuma umebadilisha mandhari na hali ya kisiasa nchini.
Ni upepo wenye dhoruba utakaotuletea mvua, gharika, mafuriko masika na mbu.
Mwenye akili, upendo, uzalendo na ushawishi atakuwa salama vinginevyo tamati ya wengi sasa ni dhahiri shahiri

Kama ulidhani Lusinde ni bingwa wa matusi subiri kidogo, kama ulidhani matumla tu ndiye anaweza za ulingoni nakutahadharisha unaweza kupata pambano la bure lisilo na uzani kutoka Idodomya.
Ni suala la muda tu wala siyo lini na wapi.

Tusemezane
 
CHADEMA: SIMBA AKINYESHEWA MVUA USIDHANI NI NYANI

Huu ni msemo wa wahenga unao maanisha kuwa simba ni simba tu hata kama amenyeshewa mvua na kuonekana kama nayani. Maana halisi ni kuwa usimdharau simba eti kwasababu manyoya yake yaliyonyeeshewa yamenfanya aonekane nyani

Tumeshuhudia siku za karibuni mdororo wa chama tawala. Ni kweli mdororo huo unakipeleka chama mahali pabaya na si ajabu CCM ikarudi kwenye vitabu vya Historia kama KANU, UNIP n.k.

Wananchi hawachukii chama au sera zake, wanachokichukia ni uongozi wa chama uliotoka ndani ya malengo na misingi yake na kuwa genge zuri tu la wahalifu. Viongozi wamewaacha wanachama njia panda wakisubiri kukutana nao siku ya kura

Kinachowafanya wananchi waichukie CCM ni kukata tamaa na hali za maisha bila kuona mwanga 'light at the end of tunnel'. Kwahiyo ni makosa sana kusema wananchi wanaichukia CCM, la hasha, wananchi wanachukia matendo ya viongozi wa CCM ikiwa ni pamoja na mparaganyiko wa uongozi na udhaifu wake.

Vikao vya siku za karibuni vilimshambulia katibu mwenezi Nape Jr kuwa ni mmoja wa watu wanaoua chama.
Historia ya Nape ndani ya CCM inajulikana na ni dhahiri hata kama angegawa keki kwa kila mwanachama bado atakamatwa uchawi. Waliotoa mashambulizi dhidi ya Nape ni viongozi waandamizi ambao kwa hakika wanatumika vema na kundi hasimu la Nape

Viongozi hawa wametumika ili kuhifadhi wazee wenye kiu na tamaa zao za uongozi. Hawa wapo chini ya kundi la 'mgombea mmoja tajwa' ambaye anaamini alizaliwa kuwa Rais wa Tanzania lakini muda haujafika.
Licha ya misuko suko na mawimbi ya kisiasa mtu huyo bado hajakata tamaa.

Kundi hasimu kwa Nape lina pesa za kutosha na linaamini katika matumizi ya pesa.
Ndilo kundi lililoingiza rushwa na mikakati ya kifedha ndani ya CCM.

Katibu mwenezi Nape kwa kutambua kuwa alikuwa anashambuliwa na ukweli kuwa yeye na mwenyekiti wake huenda chama kikawafia mikononi, ameamua kueneza uhai wa chama kwa kujibu mapigo ya wapinzani.
Amekuwa anazunguka mikoani katika mikutano kama mtoto yatima.
Haungwi mkono na chama haswa, bali watu wachache ndani ya chama.

Umoja wa vijana nao unamtenga kwani si kawaida yake katika kujibu mapigo ya wapinzani ukae kimya kiasi hicho.
Kwa ufupi Nape anafanya kampeni 'solo' peke yake akisaidiwa na wbunge wachache sana.

Kundi nililolitaja hapo juu ni matokeo ya kumeguka kwa mtandao. Ingawa bado upo na unamuunga mkono mwenyekiti lakini washawishi wa mtandao wapo nje na hakika wana hasira sana.

Kinachotokea sasa ni mambo mawili;
Ima kundi lenye nia ya urais likitaka chama kifie mikononi mwa'msaliti'
au liibuke kwa kishindo.

Uwezekano wa hili la kuibuka kwa kishindo ni mkubwa sana kwa kutambua kuwa nje ya CCM madarakani hakuna atakayekuwa salama.

Tunataraji baada ya kampeni za Nape kuendelea kushindwa, kundi tajwa litaibuka na kujinasibu kuwa lina uwezo wa kurudisha hadhi ya chama. Fedha itatumika ili kukijenga tena chama ikiwa ni pamoja na kuwawezesha vijana(UVCCM) kuendesha kampeni. Hii itawajengea uhalali kuwa wao wanakubalika ndani ya chama na uhai wa chama upo mikononi mwao

Ingawa wengi wanaona Chadema inashika kasi na ni ukweli usiopinga, na pia kuwa viongozi wa CCM wamechukiwa bado hali ni tete sana kwasababu siku moja kisiasa ni muda mrefu kama alivyowahi sema kiongozi mmoja Uingereza.

Ni kwa muktadha huo Chadema wasibweteke na mafanikio wanayoyaona, wanapaswa kukaza kamba na kuhakikisha kuwa ushindi wa kuiteka jamii ni endelevu 'sustainable'.
Vionginevyo inaweza kujikuta ina 'lose ground' katika wakati nyeti sana.

Ndiyo maana nasema Chadema iiangalie CCM kama simba na wala si nyani.

Tusemezane
 
BAJETI: UDHAIFU WA SERIKALI

Kauli ya mbunge Mnyika kuhusu udhaifu wa Rais Kikwete imeleta sintofahamu kubwa sana katika jamii. Wapo wanaosema imemdhalilisha Rais na wapo wanaosema ni sawia. Kwa hali yoyote iwayo kauli hiyo haina makosa kwa mtazamo wangu kwasababu udhaifu si tusi na limetumiwa na watu mbali mbali kama wanasiasa, viongozi wa serikali na asasi za jamii.

Kitendo cha kumtoa nje ya bunge Mh Mnyika siyo tu kilikosa uungwana na uvumilivu wa kisiasa bali kimeendelea kumdhalilisha Rais.

Sasa watu wengi wanafikiria ukweli juu ya udhaifu wa rais kwa undani zaidi kuliko hapo awali.
Hili kisiasa linaitwa political blunder iliyofanywa na naibu spika na wabunge wa CCM kwa makofi na nderemo zao.

Tukiangalia madhaifu ya mheshimiwa Rais hakika tutajaza kurasa na kurasa. Si mara moja, bili au tatu ameshindwa kuonyesha uongozi katika kiwango tarajiwa na ndiyo maana wapo wanaosema kuna ombwe la uongozi nchini.
Ombwe kwa kiingereza ni 'vacuum' ambalo ni baya zaidi kuliko udhaifu.

Udhaifu ninao uona ni katika kusimamia rasilimali za nchi ili ziwasaidie watarajiwa.
Ni pamoja na kusimamia matumizi ya kidogo tulichona nacho kwa faida ya wengi.
Ukiisoma bajeti ya mwaka huu utagundua udhaifu hasa aliosema JJ.Mnyika

Udhaifu wa kwanza ni usuli (feedback). Kwamba bajeti imesoma kukiwa na ahadi za pesa za maendeleo.
Hakuna ajuaye zile za mwaka jana zimefanya nini kukamilisha yaliyokusudiwa. Mathalani kama pesa zilitarajiwa kujenga bara bara, je zimefanya hivyo? Na je ni kwanini tunatakiwa tutenge bajeti nyingine kwa miradi ile ile tuliyoitengea fedha miaka 2, 3 au 4 iliyopita!

Pili, kwanini serikali iwe na matumizi makubwa kuliko mapato? Je, tumeangalia chanzo cha ukubwa wa matumizi hayo?
Unawezaje kuwa na mshahara wa sh 100 ukawa na matumizi ya sh 150! hivi hapo hakuna uwalakini.

Je, tumeangalia ni mambo gani yanayoongeza gharama na je, mambo hayo yanamsadiaje mtanzania.
Hakuna maana ya kutenga bilioni 400 au 500 kwa ajili ya posho za viongozi.Maana yake ni kuwa kundi dogo la watu lianapata mgao mkubwa binafsi kuliko halamashauri yenye mamailioni ya watu. Je, hii ni sawa?

Katika kubana matumizi wenzetu wamekuja na kitu kinaitwa 'austerity measures' ikiwa ni pamoja na kuondoa huduma zisizo za lazima au kuhamishia gharama hizo kwa watumiaji wanaolazimika.
Tumeona haya kuanzia ulaya hadi marekani, japan hadi nchi za mashariki ya kati. Ni hawa ndio wanatupa asilimia 40 ya bajeti, sasa swali ni kuwa kwanini sisi tusianze kujitutumua kwanza kabla ya kupitisha bakuli la aibu?

Tatu, deni la taifa linazidi kuongezeka na hakuna ajuaye linaongezwa kwa nini. Maana ya hii ni kuwa pamoja na asilimia za misaada bado tuna asilimia za mikopo na hizo ni mzigo wa wananchi. Ni nani anawajibika kwa hili kama si Rais, na je, huo si udhaifu katika uongozi.

Nne, vyanzo vya mapato vimekuwa vile vile kwa miaka 50 sasa. Tulidhani uwepo wa wasomi katika nyanja za utawala, uchumi na sheria zingaliweza kutupa jibu. Jibu ni kuwa hatujaweza.

Nashangaa kwanini mtu kama Dr Mgimwa(waziri wa fedha) bado anadhani vyanzo vya mapato ni vocha za simu za wanafunzi na wajasirilia mali! Kwanini Dr adhani kuwa boda boda ni chanzo kizuri cha mapato ikiwa ni pamoja na soda na bia? Bahati mbaya watu wakigoma kunywa soda, bia au kutumia boda boda nchi imekwama! kweli! I mean serious!
Hapa kama si udhaifu ni nini kwa lugha nyingine labda.

Katika nchi kubwa iliyojaliwa rasilimali na jiografia nzuri (strategic geographical position) kama Tanzania, kwa mtu mwenye uelewa kodi za vocha za simu, soda na bia ni kitu cha mwisho kabisa kufikiria kama chanzo cha mapato.

Tulitegemea mapato yapatikane katika mambo yafuatayo
1. Kubana matumizi ya ukubwa wa serikali. Hili ni pamoja na kupunguza utitiri wa viongozi wasio na kazi.
Mathalani, mkoa mmoja kama wa Dar es Salaam una wabunge 5, DC 3, Mkuu wa mkoa, Meya wa jiji, Afisa tawala mkoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri n.k.

Ukiangalia viongozi hawa hawana tija yoyote kwasababu wote wanawajibika kwa waziri mwenye naibu, katibu mkuu na wakurugenzi wa wizara. Utitiri huu unaongeza makongamano ya kipuuzi, nauli za usafiri za kijinga, gharama za kuwahudumia wao na familia zao za kipuuzi na mengine yatokanyo.
Hakuna sababu ya kuwa na utitiri huo wote.

2. Kubana mianya ya kodi. Nchi yetu haiwezi kuomba trilioni moja kama misaada wakati huo huo ikiachia wajanja wakwepe kodi kwa misamaha ya kipuuzi kiasi zaidi ya hicho.
Tumeona mashirika ya dini na mafisadi wanavyotumia mianya hiyo nchi ikiwa na viongozi ngazi zote.
Huu si udhaifu ni nini?

3. Kukusanya kodi kutoka sekata zifuatazo
a) Madini (b) Uvuvi (c)Utalii (d) biashara (e) Huduma za jamii zinazolipiwa kodi

Kinyume na hayo niliyoyataja hapo #3, serikali yetu imejikita katika kumtwisha mzigo wa kodi mfanyakazi na mkulima ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi za vocha za watoto wa sekondari wanazotumia katika 'text za kutongozana'
Bado najiuliza, serious! haya yanaweza kuwa chanzo cha mapato ya nchi tena kama kipaumbele!

Hebu safu inayofuata tuangalie kwa uchache tu hayo ya #3 na kujiuliza tungewezaje kuayatumia kama vyanzo vya mapato halafu tupime kama kweli serikali yetu ni 'mashujaa' au ni dhaifu na hadi lini uzezeta huu utaisha!
Tujiulize kama CCM haiwezi kwanini tusidhani kuwa sasa ni wakati wa mabadiliko.

Itaendelea...............
 
NGOME ZA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Kabla hatujaingia katika muhtasari kama unavosomeka hapo juu, tuziangalie siasa za nyakati 'current affairs'

Marekani: Mtifuano bado ni mkali kati ya Obama na Mitt Romney. Takwimu za uchumi zinazotoka kila ijumaa ya kwanza ya mwezi zinaonyesha ongezeko kidogo sana katika ajira na kiwango cha wasio na ajira kimepata hadi 8.2 asilimia.

Takwimu hizi si nzuri kwa Obama na chama chake na Republican wanazitumia kuonyesha kudodorora kwa uchumi.
Historia inaonyesha kuwa hali ikiwa hivyo ni vigumu kwa rais kurejea madarakani hasa kiwango cha kutokuwa na ajira kikifikia hapo kilipo. Kuna nafasi ya miezi minne ya kubadilisha hadithi, vinginevyo Obama ana hali ngumu...

Duru za siasa ndio jina la hii thread yako tumeona mabandiko yako kwenye Duru la siasa umetaja ngome tatu za vyama vya siasa Tanzania. CCM, Chadema, CUF.

Vyama kama NCCR Mageuzi, TLP, ngome zao za kisiasa zipo wapi Tanzania hivi ni vyama siasa ambavyo vinawawakilishi kwenye bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...au kwenye duru za siasa Tanzania havimo!
 
Duru za siasa ndio jina la hii thread yako tumeona mabandiko yako kwenye Duru la siasa umetaja ngome tatu za vyama vya siasa Tanzania. CCM, Chadema, CUF.

Vyama kama NCCR Mageuzi, TLP, ngome zao za kisiasa zipo wapi Tanzania hivi ni vyama siasa ambavyo vinawawakilishi kwenye bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...au kwenye duru za siasa Tanzania havimo!
Ni vyama katika bunge vyenye uwakilishi. Kwasasa havina ngome kwasababu ya udhaifu. Mparaganyiko wa NCCR ndio uliokipa CUF ngome ya wana mageuzi. Kwa bahati mbaya CUF wakaelekeza nguvu zao kujenga ngome kwa misingi ya udini na aliyefanya haya ni maalim Seif. Chama kikapoteza mwelekeo na wengi kutafuta mbadala ambao ni Chadema.

TLP si chama kwa maana ya chama! ni mkusanyiko unaomshangaa au kumpenda mtu mmoja Lyatonga mrema. Ngome ya TLP ilikuwa watu wa vijiweni na mitaani ambao nao wameondoka baada ya kubaini kuwa Mrema si mwana demokrasia na yupo kwa masilahi yake na wala si ya wananchi. Haiwezekani mwenyekiti wa chama Mrema aende katika mkutano wa CCM Dodoma na kuisifia CCM haishikiki huku mgombea wa chama chake akipita mitaani kujinadi.

Kwa ufupi NCCR na TLP hawana political base na ni rahisi kusema hawa ni opportunists na seasonal politicians simply for personal gain, nothing else!
 
Ni vyama katika bunge vyenye uwakilishi. Kwasasa havina ngome kwasababu ya udhaifu. Mparaganyiko wa NCCR ndio uliokipa CUF ngome ya wana mageuzi. Kwa bahati mbaya CUF wakaelekeza nguvu zao kujenga ngome kwa misingi ya udini na aliyefanya haya ni maalim Seif. Chama kikapoteza mwelekeo na wengi kutafuta mbadala ambao ni Chadema.

TLP si chama kwa maana ya chama! ni mkusanyiko unaomshangaa au kumpenda mtu mmoja Lyatonga mrema. Ngome ya TLP ilikuwa watu wa vijiweni na mitaani ambao nao wameondoka baada ya kubaini kuwa Mrema si mwana demokrasia na yupo kwa masilahi yake na wala si ya wananchi. Haiwezekani mwenyekiti wa chama Mrema aende katika mkutano wa CCM Dodoma na kuisifia CCM haishikiki huku mgombea wa chama chake akipita mitaani kujinadi.

Kwa ufupi NCCR na TLP hawana political base na ni rahisi kusema hawa ni opportunist na seasonal politician simply for personal gain, nothing else!

Mkuu Nguruvi3 mabandiko yako ni makini na tunajifunza kutoka kwako kwenye uchambuzi wako kwenye duru za siasa umetufahamisha kama political base ya CUF ni Pemba, na umetufahamisha NCCR Mageuzi na TLP aina ya siasa zao wanazofanya lakini kwa upande wa Chadema naona unapingana na ukweli kusema political base yao ni Kaskazini kwa ushahidi wa idadi ya wabunge wa Chadema wa kuchaguliwa na idadi ya wabunge wa viti maalaum sijui wewe kwenye duru zako za siasa uoni kama Kaskazini ndio political base ya Chadema.
 
Nguruvi3,
Mkuu wangu unamwaga vitu kisawasawa. Je unayo blog au mahala ambapo huandika zaidi ya hapa JF nangependa sana kukusoma mara kwa mara..
 
Mkuu Nguruvi3 mabandiko yako ni makini na tunajifunza kutoka kwako kwenye uchambuzi wako kwenye duru za siasa umetufahamisha kama political base ya CUF ni Pemba, na umetufahamisha NCCR Mageuzi na TLP aina ya siasa zao wanazofanya lakini kwa upande wa Chadema naona unapingana na ukweli kusema political base yao ni Kaskazini kwa ushahidi wa idadi ya wabunge wa Chadema wa kuchaguliwa na idadi ya wabunge wa viti maalaum sijui wewe kwenye duru zako za siasa uoni kama Kaskazini ndio political base ya Chadema.
Ritz, nadhani ulinielewa tofauti kuhusu CUF.

CUF kilipoanza kilikuwa na kauli mbiu ya haki sawa ikimaanisha kuwa raia wote wapewe haki sawa bila kubaguliwa. Unakumbuka wakati huo walikuwepo akina James Mapala, marhum Shaaban Mloo, na akina maalim Seif.
Hakukuwa na wasi wasi wowote na political base yao ikawa kwa wale wanaoitafuta haki.

Kwa bahati mbaya au nzuri James Mapalala akaenguliwa katika uongozi. Aliyetakiwa kuwa mwenyekiti alikuwa ni Maalim Seif lakini kwa mtazamo wa kisiasa ilibidi atafutwe mtu ili kuleta uhalisia wa bara na visiwani.
Lakini pia ukumbuke kuwa Maalim alikua na shauku ya kuongoza visiwani kwahiyo angelikuwa mwenyekiti basi nafasi hiyo asingeipata kwa vile angegombea urais wa muungano ambao haIkuwa nia yake na alijua ugumu uliopo.

Maalimu akachukua hatamu zote za uongozi kama katibu mkuu. Akahamishia nguvu za chama chake visiwani alipokuwa na matarajio ya Urais. Visiwani kuna asilimia 98 waislam na hao wakafanya CUF kama chao, wakageuza kauli mbiu ya haki sawa kuwa kauli mbiu inayosimamia na iliyotokana na dini. Hili likawavuta waislam wa bara ambao nao bila kujali mkakati wa kisiasa wakaamua kuifanya CUF kama chama chao.
Mikutano ikawa inafanyika Ijumaa baada ya swala na mambo mengi tu yaliyokifungamanisha chama na dini.

Uungwaji mkono ukawa mkubwa katika misingi ya kidini na hapo maalim Seif akaona ndiyo political base yake.
Na kwa vile hakuwa na shauku na uongozi wa Tanzania kwa ujumla political base yake ya kidini ilitosha kabisa kumfikisha kule alikotaka hata kama madhara yangetokea bara. Hapo ndipo CUF ikiwa na political base ya kidini nakupoteza mvuto wake kisiasa, mvuto ambao hauwezi kurejea tena kwasababu ya Stigma.

Ninachosema hapa ni kuwa political base siyo base ya kijiografia, ni base inayojenga chama kwa hamas.
Mathalan, political base ya Democrat kule marekani ni tabaka la kati na walala hoi ikiwa ni pamoja na wapenda mabadiliko(progressive). Political base ya Republican ni wahafidhina na Mamwinyi wasiotaka mabadiliko na wanaoamini katika mabavu. Kwa ufupi demoocrat wanaamini katika ustawi na Republican wanaamini katika survival for the fittest

Kuna nchi nyingine ambazo political base yao ni vyama vya wafanyakazi kama ilivyokuwa ANC, ndio maana vyama vya wafanyakazi vina nguvu sana katika siasa za nchi kama South Afrika.

Kuhusu Chadema, political base yao inaundwa na kundi la watu wenye elimu ya kati kwa viwango vya nchi yetu.
Ni kutokana na hilo CCM walifanya kosa kubwa uchaguzi uliopita kwa kufunga vyuo. Lengo lao lilikuwa ni kulinda majimbo yenye vyuo na taasisi. Hilo liilisadia sana kuisambaza political base ya CDM huko vijijini na matokeo yake ni kuwa chama rasimi cha upinzani. Kundi hili la kati kieleimu lina ushawishi na hakuna ubishi kuwa CCM haikubaliki katika maeneo hayo.

Mkakati wa CCM ulikuwa kuzuia majimbo mawili au matatu ya Dar/Mwanza na Arusha na matokeo yakawa kupoteza majimbo mengi sana. Hawakuangalia political base ya CDM kwasababu walikuwadefensive zaidi ya offensive.

Ukitaka kujua political base ya CDM ni vijana wa kada ya kati kielimu fuatilia hotuba ya Mh Mbowe bungeni leo.
Pamoja na kuongelea mambo ya kitaifa kwa ujumla wake, alijikita kuongelea hata mgogoro wa chuo kama cha UDOM na unyanyasaji wa wanafunzi kwa ujumla. Hapa kisiasa inasemwa kuwa Mbowe alikuwa ana-connect na political base yake na kui-excite (Anaunganisha mahusiano ya CDM na ngome yao pamoja na kuitia hamasa ngome yao kisiasa)

Siyo kweli kuwa ngome ya kisiasa ya CDM ipo Kaskazini kwa maana tu ya eneo. Ngome ni kundi linaloleta hamasa kisiasa.
CCM ilikubalika sana pwani na mikoa ya kanda, hii haina maana ni political base yao, hakika political base yao ilikuwa wakulima na wafanyakazi na walipoiacha na kuunda kundi la wafanyabiashara basi wali-demoralize political base yao na matokeo yake wakulima wanahama CCM kwa vijiji.

Hata kama tutakubaliana kuwa political base ya CDM ni kanda ya kaskazini, hoja hii itazidi kuibomoa sana CCM kwasababu tutaanzia Tabora na Dar wakati wa TANU kabla hatujaenda Pwani.
Hoja hii ingawa inaonekana kuwaumiza CDM ukweli ni kuwa hawajaweza kuijibu kikamilifu na nina uhakika wangeimaliza CCM

Political base ninayoiongelea ni ile ya makundi yaliyohamasika kisiasa yenye ushawishi kwa chama husika na wala si maeneo.
 
Ritz, nadhani ulinielewa tofauti kuhusu CUF.

CUF kilipoanza kilikuwa na kauli mbiu ya haki sawa ikimaanisha kuwa raia wote wapewe haki sawa bila kubaguliwa. Unakumbuka wakati huo walikuwepo akina James Mapala, marhum Shaaban Mloo, na akina maalim Seif.
Hakukuwa na wasi wasi wowote na political base yao ikawa kwa wale wanaoitafuta haki...

Mkuu Nguruvi3 nimekusoma nashukuru kwa analysis yako murua...
 
Duru za siasa
Tukianza na CCM tumeiona ikiyumba ama kuelekea kukosa ubunifu tumeona mkutano wake wa hivi karibuni kwenye viwanja vya Jangwani umeacha somo kwa wale wapendao kujifunza.

Kuna CCM tatu ndani ya chama kimoja, CCM inapaswa kurudisha uhai wa chama ili watu waione CCM iliyo hai na pia waone faida ya CCM kwenye maisha yao, watu wanataka wasikie CCM inasema nini badala ya watu wanasema nini, kwenye mkutano wa pale Jangwani CCM haikuwa moja na pia CCM haikusema chochote badala yake watu binafsi ndio waliosema kwa kutumia nyadhifa zao na na nafasi zao.

Ninapozungumzia kauli ya cha nina maana pana, kwanza kuna mengi ambayo CCM inapaswa kuyatolea kauli ama kuyatolea ufafanuzi ili watu wasikie chama kimesema nini. Kitendo cha kuwaalika Wawaziri ili waje wawaeleze Wananchi mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM ni kujikanyaga, chama ndicho kinapaswa kuitetea serikali na sio serikali kujitetea mbele ya Wananchi ili kukisafisha ama kukinufaisha chama tawala.

Mawaziri wanalo jukwaa lao ambalo wananchi huwasubiri na kuwasikiliza ni bungeni wakati wa kuwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara zao.

Tutaendelea na Duru za siasa.
 
Nguruvi3,
Mkuu wangu unamwaga vitu kisawasawa. Je unayo blog au mahala ambapo huandika zaidi ya hapa JF nangependa sana kukusoma mara kwa mara..
Mkuu Mkandara, awali ya yote shukran. Kwakweli sina Blog, siku za nyuma nilikuwa naandika makala Raia mwema lakini sasa ni zaidi ya mwaka na nusu sijatuma.
Nimependelea hapa kwasababu nisehemu muhimu kwa mawasiliano hasa kupata mawazo na mitazamo tofuti.
Kama unavyoelewa JF ni two way traffic as opposed to one way. JF ni 'total package', ukitaka kulia, kucheka,kutabasama, kuchota busara n.k ha ha ha ha!
 
Mkuu Mkandara, awali ya yote shukran. Kwakweli sina Blog, siku za nyuma nilikuwa naandika makala Raia mwema lakini sasa ni zaidi ya mwaka na nusu sijatuma.
Nimependelea hapa kwasababu nisehemu muhimu kwa mawasiliano hasa kupata mawazo na mitazamo tofuti.
Kama unavyoelewa JF ni two way traffic as opposed to one way. JF ni 'total package', ukitaka kulia, kucheka,kutabasama, kuchota busara n.k ha ha ha ha!
Poa kinachonitatiza na JF siku hizi ni kwamba inakuwa vigumu sana kumfuatilia mtu pengine tuanzishe mpango wa ku Tag mtu mjadala inapopaswa. Mada ni nyingi sana huwezi kusoma zote hadi unategea kuona wakali wako wamechangia wapi zaidi ndio unajiunga. Kuna watu natafuta michango yao huwa siwapati japokuwa huwaona wame log in..
 
Mkuu Nguruvi3,

Nina kawaida ya kukwepa kusoma makala ndefu lakini hali ni tofauti ninapokumbana na nondo zako za uhakika siachi hata nukta nafyonza kila kitu bila kukinai.

Ombi kama utakuwa na nafasi ningependa uelezee siasa za EA namna zinavyoweza kuikwaza Tanzania kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.
 
Back
Top Bottom