Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

UTETEZI LAINI USIO NA MASHIKO WA DR KITILA MKUMBO

Hbari ifuatayo ni kwa hisani ya gazeti la Raia Mwema.
NCHI yetu ipo katika mhemko wa kisiasa. Kwa vijana na tabaka la wananchi wa kawaida, ambao hawana maslahi ya moja kwa moja na mfumo wa sasa wa utawala, mhemko huu unawasukuma kukichukia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupenda upinzani. Na kwa mazingira ya sasa ya kisiasa wanalazimika kuipenda CHADEMA.


Wananchi hawa wana haki na wajibu wa kuichukia CCM kwa sababu serikali yake imewaangusha. Na hili la serikali ya CCM kuwaangusha wananchi wake sio suala la mjadala tena kwa sababu hata Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahama Kinana, amekiri hivyo waziwazi katika mikutano ya hadhara.
Kimsingi, Kinana kwa siku za hivi karibuni amekuwa akifanya kazi za upinzani sijui ni kwa sababu ya kuchoka kuwa chama tawala au kwa kuona kwamba upinzani wameshindwa kuibana serikali sawa sawa kama inavyopaswa.

Pengine kitendo cha wabunge wa upinzani kuidandia na kuunga mkono hoja ya mawaziri mizigo kama ilivyo ni kielelezo kingine kwamba upinzani bado hawataki kutenda zaidi ya upinzani.

1. Katika hali ya kawaida, ambapo upinzani ni imara na upo tayari kuchukua nafasi ya serikali wakati wowote, ilitarajiwa kwamba Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na wabunge wake wangeenda zaidi ya kuwashughulikia mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo na hao waliokutwa na hatia na Kamati ya akina Lembeli.


2.Wangekuwa makini vya kutosha hii ilikuwa ni fursa adimu kwa upinzani kusababisha dhahama kubwa zaidi katika utawala wa CCM na hata kusababisha Uchaguzi Mkuu kuitishwa mapema. Samaki huoza kuanzia kichwani.


Haiwezekani uwe na mawaziri mizigo halafu usiwe na serikali mzigo. Wabunge wa upinzani wamejikuta wanacheza ngoma ya CCM na wamewasaidia sana kujipanga kwa ajili ya chaguzi zijazo na hoja yao kwamba ni chama kinachosikiliza (chama sikivu) imeimarika zaidi.
Tutajadili zaidi jambo hili katika siku zijazo. Kwa sasa acha niendelee na mada yangu ya leo.


Kwa kuwa watu wengi wanaotaka mabadiliko katika mfumo wa utawala wameweka tumaini lao kwa CHADEMA, hawataki chama hiki kiguswe. Wanataka kitulie tuli hadi 2015. Wanataka chama hiki kilelewe kama yai.

3.Kisingizio cha wengi ni kwamba hawataki yatokee yaliyokikumba NCCR – Mageuzi miaka ya tisini.
Viongozi wa CHADEMA wanajua sununu iliyomo miongoni mwa wanachama na washabiki wa CHADEMA. Nao bila ajizi wameitumia sununu hii kama fursa ya kisiasa ndani ya chama. Hawataki waguswe. Hawataki wakosolewe. Na kikubwa zaidi hawataki wapingwe katika chaguzi za ndani ya chama. Hata wakifanya makosa yatahalalishwa kwa njia mbalimbali.


4.Yeyote anayejaribu kuwagusa na kuwakosoa viongozi na hasa akionyesha kwamba anatamani mabadiliko ndani ya uongozi atadharauliwa na uana-CHADEMA wake utatiliwa shaka.

5.Na katika siku za karibuni mtu yeyote ambaye haonekani kuunga kila la viongozi wa chama ataaibishwa mbele ya jamii kwa kutangazwa kwamba ni msaliti na mhaini.


6.Jambo ambalo litakuwa ni kosa likifanywa na kiongozi ‘A’ litaonekana ni kosa, lakini jambo hilo hilo likifanywa na kiongozi ‘B’ halitakuwa kosa. Hiki ndicho Mwalimu Julius Nyerere alikiita katika kitabu chake cha ‘Tujisahihishe’ kwamba ni fitina na ni unafiki wa kiuongozi.


7. Kwa hiyo tunachojaribu kuambiwa hapa ni kwamba harakati za kidemokrasia ndani ya vyama vya siasa vya upinzani ziahirishwe hadi CCM itakapotoka madarakani. Hata hivyo ukweli wa siasa haupo hivyo.
Katika siasa za vyama vingi ushindani ni jambo lisiloepuka na haliwezi kuwa hisani ya uongozi uliopo madarakani.


Kinachotokea ndani ya CHADEMA sio jambo geni hapa duniani. Nitatoa mfano wa hivi karibuni katika nchi ya Afrika Kusini ambayo demokrasia yao bado ni changa kama ya kwetu. Baada ya Mzee Nelson Mandela kumaliza muda wake mwaka 1999 na kuamua kwamba asingegombea tena nafasi yake katika chama ilichukuliwa na Thabo Mbeki, aliyekuwa Makamu wake wa Rais. Thabo Mbeki ndiye pia akamrithi urais Mzee Mandela.

Kwa kufuata utaratibu na nafasi yake ndani ya ANC, Mbeki alilazimika kumteua Jacob Zuma kuwa Makamu wake wa Rais, pamoja na kwamba yeye mwenyewe asingependa awe. Kwa kuwa Mbeki tangu mwanzo hakumpenda Zuma, walikuwa na msuguano usio kwisha. Hatimaye Rais Mbeki akamchomekea kesi Zuma inayohusu matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa maadili. Hii ikampa fursa Rais Mbeki kumfukuza Jacob Zuma kutoka kwenye nafasi ya umakamu wa Rais.

Wafuasi wa Jacob Zuma wakakasirika na kununa. Kesi ikaendeshwa kwa zaidi ya mwaka na hatimaye Mahakama Kuu ya Afrika Kusini haikumkuta Jacob Zuma na hatia yeyote na ikamwachia huru.

Jacob Zuma hakurudi katika nafasi yake ya umakamu wa Rais. Badala yake aliamua kuusaka urais wa ANC. Vita ilikuwa kubwa na ANC ikagawanyika makundi mawili.

Kundi moja, ambalo wao wanaita ANC rasmi, wakiunga mkono Mbeki katika uchaguzi huo, wakati vijana wa ANC, chama cha wafanyakazi (COSATU) na chama SACP, ambao ni washirika muhimu wa ANC, wakimuunga mkono Jacob Zuma.


8. Uchaguzi ulipofanyika huko Polokwane, Jacob Zuma akaibuka kidedea kwa zaidi ya asilimia 60 na ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa urais wa Thabo Mbeki. Uchaguzi Mkuu ulipofanyika mwaka 2009 Jacob Zumma akakabidhiwa kiti cha urais baada ya ANC kushinda kwa mara nyingine tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1994.


Kwa hiyo mapambano ya kidemokrasia ndani ya vyama hayawezi kuahirishwa na ndio utamaduni wenyewe wa kidemokrasia tuliochagua kuufuata. Katika harakati hizi za kidemokrasia viongozi watapingwa na watapingana.
Wanachama mbalimbali watatamani nafasi za uongozi. Katika michakato ya namna hii migogoro itatokea.

9. Muhimu ni kwamba vyama lazima viwe na njia ya kutatua migogoro ndani ya vyama bila kusababisha madhara kwa vyama husika.


10. Katika hili ni muhimu tukasisitiza kwamba namna moja ya kupima uwezo wa kiuongozi ni uwezo wa kutatua migogoro bila kusababisha madhara kwa taasisi.


Kama kiongozi anatatua mgogoro kwa namna ambayo taasisi inaathirika ujue kiongozi amepungukiwa moja ya sifa ya msingi ya uongozi.

12. Na namna moja ya kuutatua mgogoro uliopo ndani ya CHADEMA bila kuathiri zaidi chama ni kuruhusu demokrasia ifanye kazi yake. Tuwaachie wanachama wawaadhibu hao wanaoitwa wasaliti na wahaini katika uchaguzi huru.

13

Wanachama wa CHADEMA wanaodhani kwamba chama kitakuwa salama kwa kundi moja katika mgogoro kufukuza uanachama kundi jingine wanakosea kimantiki. Ufuasi wa vyama vya siasa kwa kiasi kikubwa hujengwa juu ya ufuasi wa viongozi.


14. Ni umbumbu wa kisiasa kudhani kwamba utamfukuza kiongozi aliye mbunge na mwenye ufuasi, tena katika mazingira ya sababu tatanisha kama yalivyo sasa, na chama kikibaki imara.

Ni tofauti kabisa na kufukuza uanachama watu kama mimi nisiye na mfuasi yeyote kisiasa, lakini sio kwa kiongozi aliyefanya kazi ya siasa maisha yake yote ya ujana na kujijengea ufausi wa kila kundi katika jamii.

Unaweza ukapata sifa za muda mfupi kwamba una uwezo wa kufanya uamuzi mgmu, lakini ni uamuzi usio makini na uliyokosa busara na ndiyo maana unauita mgumu.

15. Ndio maana vyama vingi duniani hutatua aina ya mgogoro unaoikumba CHADEMA kwa viongozi kuzungumza na kuyamaliza au kuitisha uchaguzi ili wanachama waamue kwa nia ya kura.

Hii ndio njia ya kidemokrasia na ya kistaraabu ya kumaliza migogoro ndani ya vyama bila kuathiri taasisi husika.
Ndugu wanajamvi, nimeona ni vema kujadili mada hii ya kwasababu kuu mbili.
1. Imelenga kupotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mgogoro
2. Kwa kiasi fulani umeonekana kujibu au kujadili hoja za wana duru kwa njia ya kiufundi.

Nimezigawa hoja katika namba ili ziweze kusomeka na kuangaliwa kwa macho mawili.

UPOTOSHAJI
1. Dr Kitila hakueleza chanzo cha mgogoro. Alichokieleza ni watu kuumbuliwa kama wasaliti na wahaini wanapopingana na uongozi(point#5).

Kitila anafahamu kuwa yeye na wenzake hawakuongoza jitihada za kupinga uongozi, walichokifanya ni jitihada za kuleta mtafaruku.

Kwanza, kutumia waraka ambao kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa inatoa hoja za waraka kwa vipengele(Rejea bandiko#92 kwa mfano).

Kitila anapingana na hoja yake#10 kwamba migogoro ya kisiasa hutatuliwa kwa mazungumzo. Kitila na wenzake hawakutumia mazungumzo,walitumia waraka.

Lakini pia anapingana na hoja yake#15 ya viongozi kuyamaliza na kuitisha uchaguzi.
Kitila hakutumia njia hizo alichokifanya ni kujificha na kuandika waraka ambao amekiri kushiriki.

2. Hoja#8, Kitila amepotosha kusema Mbeki aliondolewa na Zuma katika uchaguzi.
Ukweli ni kuwa Mbeki aliondolewa na kamati kuu ya ANC miezi 8 kabla ya uchaguzi.
Aliyekaimu nafasi hiyo ni K.Motlanthe.

Hoja ya Urais wa A.kusini ulitoka kwa Mbeki na kwenda kwa Zuma kwa njia ya kura ni upotoshaji

Hata hivyo, Kitila atambue kuwa kamati kuu ya ANC ilichukua hatua baada ya kubaini Zuma hakuwa na makosa mbele ya mahakama.

Ni uamuzi kama huo ambao kamati kuu ya CDM iliutumia katika kuwavua vyeo wahusika ingawa halikuwa suala la mhakamani. Hivyo hapa anajichanganya kwa kulaani maamuzi ya CC ya CDM na kuunga mkono maamuzi ya CC ya ANC.

3. Hoja#14, Kitila anaueleza umma kuwa sababu viongozi kuondolewa wadhifa ni za utatanishi. Hakuna utatanishi katika waraka aliokiri ameuandika na ambao ulishaanza kufanyiwa kazi.

4.Hoja#10, Kitila anasema njia ya kutatua migogoro ni kuhakikisha haisababishi madhara kwa taasisi. Ukweli kuwa waraka haikuwa njia nzuri na mgogoro uliopo ni matokeo tu.

Laiti angekuwa ana 'walk the talk' asingeandika kitu kinachosababisha mgogoro na kuzorotesha upinzani.Kitila na wenza hawakutimiza hoja# 9 inayowataka kutatua migogoro kwa kukaa pamoja.

5. Katika hoja#1 na 2, Kitila amemtaja kiongozi wa upinzani kushindwa kushughulikia suala la mawaziri na amesema hiyo ilikuwa fursa ya kuimaliza CCM kwasababu samaki huoza kuanzia kichwani. Amesahau aliyekuwa naibu kiongozi wa upinzani alianzisha tuhuma ambazo CCM wangekuwa makini tuhuma huenda zingeimaliza CDM, Kitila anahubiri kitu ambacho anafahamu kingiemaliza CDM lakini akitaka kiimalize CCM. Double standards.

Mkumbo aelewe kuwa kiongozi wa upinzani ni mtu lakini upinzani ni kundi ambalo washirika wake wamo. Ingelikuwa busara angetumia neno upinzani bila kumtaja kiongozi, tunajua ni Mbowe.

Kwa hili ameonyesha sentiment zaidi ya kujenga hoja kama alivyoonyesha katika waraka na kama alivyoonyesha katika hoja#10.

6, Hoja#14, si kweli kuwa vyama vya siasa vinajengwa na wafuasi.
Ukweli ni kuwa wafuasi wanajenga chama kwa kuamini katika sera za chama na misimamo yake.

Chama kinachojengwa na mtu ni genge la watu na si chama au taasisi.
Hoja ya kusema mbunge mwenye wafuasi akifukuzwa chama kitakufa au kutetereka ina mashiko tu kwa chama kinachoamini katika personality na si policy.
Sijui CDM ambayo yeye alikuwa mshauri kinaamini katika nini.

7. Hoja#13, Kitila anasema wanachama wanaodhani kufukuza watu wanakosa mantiki, nadhani Kitila anakosa mantiki kabla yao.
Mifano ipo hai, TANU iliwahi kugawanyika na kuundwa kwa AMNUT na UTP.
ANC imegawanyika makundi mawili, lile lililounda chama kumuunga mkono Mbeki na lile la Malema.Huko nyuma ANC iliwahi kuvunjika na kuunda PAC.
Rainbow alliance ilivunjika na kuunda ODM na Jubilee.

Mifano hiyo inaonyesha kuwa kama lipo kundi lisiloridhika na mambo na jitihada za kurekebisha zimeshindika ipo plan B ambayo ni kujitenga na kuondoka na wafuasi kwa kuanzisha chama kingine. Mrema aliawahi kufanya hivyo bila kuathiri taasisi nyingine

Nadhani hiyo suluhu ingeweza kutumiwa na akina Mkumbo na washirika wake badala ya kujificha na kuandika waraka wa uchochezi.Makundi niliyoyataja yalifanya mambo yao hadharani na si chini ya kapeti kama ilivyokuwa kwa Kitila and associates.

Nyerere, Mandela, Clinton, Blair, Washington, Gandhi n.k. walikuwepo na wameondoka na vyama vyao bado vipo.

Mrema aliondoka na wafuasi na CCM ipo, Lamwai aliondoka na wafuasi na NCCR ipo, Mapalala alindoka na wafuasi na CUF ipo n.k.

Sidhani katika siasa za kileo chama kinajengwa kwa jina. Kama ni hivyo Kitila anavyodai hakuna sababu za CDM kunadi sera, kianchotakiwa ni kunadi sura ya mtu.
Siasa za kileo hazikubaliani na hilo.

MAONI
Ukisoma makala ya Dr Kitila ni dhahiri bado anaamini kuwa alichotaka kukifanya kwa kuandika waraka kilikuwa sahihi.

Kitila anaweza kuamini hivyo na wala si kosa, lakini kiongozi kama yeye anapojitokeza na kuomba radhi halafu kurudi magazetini kuandika kile kile alichokiombea radhi inatia shaka na kusikitisha.

Kitila na wenzake hawakutumia njia za kidemokrasia katika kupingana ndani ya chama chao. Walichokifanya ilikuwa ni uchochezi kwa kutumia mitandao ya jamii.
Hili ndilo kitila analosema ni demokrasia na lazima vyama vivumilie.

Zuma hakuandika waraka wa siri alipambana kwa uwazi.
Kitila na timu yake hawana historia ya kujitokeza na kupambana wazi katika misingi ya demokrasia, leo anapata wapi ushujaa wa kuhubiri demokrasia ambayo hakuwahi kuifanya?

Kitila anasema ni vema mgogoro ukamilizwa kwa njia ya uchaguzi.
Hilo ndilo alipaswa kusema hata kabla ya kuandika waraka.

Alichokifanya ni kaundika waraka ili kuchochea uchaguzi na si kudai uchaguzi.
Ni makosa kudhani kuwa demokrasia inaruhusu uchochezi na si taratibu, hiyo si demokrasia ni vurugu.

Endapo anadhani wanachama wana haki ya kumaliza mgogoro kwa uchaguzi, Kitila ana halalisha maasi ndani ya chama kama sehemu ya demokrasia.

Leo Zitto anaweza kuwa kiongozi wa CDM, anachosema Kitila ni kuwa atokee mwanachama na kuleta vurugu ili suluhu iwe uchaguzi.

Chama hicho sijui ni cha kisiasa au ni Simba na Yanga.
Sidhani CDM wamefika huko na kama huo ndio ushauri basi lipo tatizo kubwa zaidi.

Tena anasisitiza kuwa kuandika waraka na kutuma katika mitandao ili uchaguzi ufanyike ni njia ya kiistaarabu ya kumaliza mgogoro.

Dr amesahau kuwa waraka haukuwa njia ya kistaarabu na ndio chanzo cha kufumua timbwili la sasa na kwamba vurugu zilianza siku nyingi tangu alipomtetea Juliana kwa hoja 'aachwe abalehe'.

Hivi vurugu zinakuwaje sehemu ya demokrasia? Mimi nilidhani demokrasia ndio sehemu ya suluhisho la vurugu, inaonekana bado nahhitaji kusoma maana ya demokrasia zaidi, nitafanya hivyo na namshukuru Dr Kitila kwa kunisukuma nirudi maktaba.

Hadi hapo nitakapokubaliana naye, kwasasa nabaki kusema kuwa anachokifanya ni kuendeleza mgogoro, kumtetea mshirika wake asifukuzwe.

Kufukuzwa au kutofukuzwa hilo ni suala la wanachama wa CDM lakini muhimu ni Kitila kutambua kuwa CDM ijengwe kama taasisi na si mtu.

Mandela alisema watu na viongozi wapo na wanapita, taasisi ipo siku zote.
Hii dhana ya kuwa fulani amefanya kazi sana na anawafuasi ni dhana hafifu.
Umaarufu utumike kujenga chama na si kubomoa chama.

Kwa andiko la Kitila nadhani anchochea kuni badala ya kutia maji.

Tusemezane.
 
Nguruvi3 mpaka sasa sitaki kuamini kama ule waraka pamoja na hilo bandiko uliloliweka hapo linatoka kwa kijana msomi na aliyebobea katika siasa. Siwezi kubishana nae sana maana kiusomi, ni mtu aliyeniacha kwa mbali lakini kwa uelewa wangu mdogo, naona mapungufu mengi sana katika namna wanavyojaribu kujikosha katika sakata hili walilolianzisha wenyewe.

Makosa yao kisiasa ni yepi hasa? Nitajaribu kuainisha mawili ambayo naona ndio makubwa zaidi.

Mosi, mbali na kukosea kabisa katika kuandaa huo mkakati wao kwa njia ya siri na hatimaye kuja kujulikana kwenye public, inaonekana hawakuwa kabisa na plan B ambayo ingewakwamua pindi waraka wao wa siri ungekuja kugundulika. Inavyoonekana walikuwa na uhakika kabisa huo waraka wao hautaweza kuvuja.

Wakati sakata zima linaanza, ni kweli nilianza kuingiwa na woga kwamba hawa vijana wangeweza kukitikisa chama. Woga wangu mkuu ulikuwa kwamba huenda walikuwa na plan B ya kukiangamiza kabisa chama na hivyo kukilazimisha kiendane na matwaka yao. Badala yake, hawa jamaa wamekuwa all over the place. Inavyoonekana haya maamuzi ya kamati kuu yamewaacha wakiduwaa wasijue cha kufanya na aina yao ya kujisafisha inawaacha wenyewe na mabaka na makando kando yasiyoeleweka.

Mimi nilifikiri kete yao muhimu ilikuwa ni kujaribu kukaa kimya kwanza bila kuweka mboga yote mezani ili wajue chama kingewachukulia hatua gani kabla ya kuanza ku-attack. Hilo lingewafanya kuendelea ku-maintain support ya wanachama wengi ambao bado walikuwa wanaona kwamba hayo maamuzi yalikuwa ni ya uonevu kwao. Pia huenda haya masuala kama wangetaka kuyamaliza kiutu uzima, basi wangeyapeleka kwa njia sahihi ndani ya vikao halali ambako wameshtakiwa navyo badala ya kutafuta sympathy nje kwa wanachama ambao sasa wanazidi kuwaelewa na kuwaona wanapotoka.

Pili, katika kosa kuu ambalo Zitto na wenzake wamelifanya ni kujaribu kushindana na chama kwa kulazimisha sympathy kutoka kwa wanachama kwa kujaribu kupita kule ambako Dr. Slaa alipita na kufanya mikutano yake. Mwanzo niliona ile plan ya Dr. Slaa kwenda kigoma wakati hili suala bado halijamalizika lilikuwa kosa kubwa kwake lakini kimantiki kwa sasa nimeelewa kwanini alifanya vile. Reaction ya Zitto imekuwa ya kitoto na sasa wanachama ambao mwanzo walikuwa wanamuona kama alikuwa anaonewa, wameanza kumuangalia kwa jicho la tatu. Huwezi kutafuta sympathy kwa wanachama kwa kujaribu kukichafua chama ambacho wewe mwenyewe unataka kuja kukiongoza. Hapo pekee ameonyesha failure ya hali ya juu kabisa. Hakuna yeyote aliye juu ya chama! Na hivyo ndivyo watu wa kawaida wanafahamu.

Zitto na wenzake wamefikia hatua ya kufikiria kwamba idadi ya watu waliojitokeza pale kwenye mikutano yake ndio support kuu aliyonayo kama mtu binafsi. Anasahau kuwa, idadi kubwa ya hao wanaojifanya kumpenda ni either wanatoka chama pinzani (CCM) au ni kwasababu tu ya hali halisi ya watanzania kupenda kushadadia matukio. Kama atataka kuendana na hao watu waliojitokeza kwenye matukio, hakika litatokea tukio lingine ambalo litawatoa hao walimfuata na kumwacha peke yake. Hili la kwake litaenda na kupotea kabisa especially kipindi hiki ambacho imewapa nguvu chama kuja na maamuzi sahihi ya kuwavua uanachama wenu.

Mimi bado naamini katika uwezo binafsi wa kisiasa aliokuwa nao Zitto. Kama ataweza kupata washauri makini, basi huenda anaweza akapona katika ajali kubwa sana kisiasa ambayo inaonekana anaikaribiria lakini ni ajali ambayo amejitengenezea mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu DittoAhsante sana kwa mchango wako makini.
Nikubaliane nawe akina ZZK hawakuwa na mkakati thabiti na plan B.
Waliamini mpango wao ungewamaliza kabisa viongozi, siyo kidemokrasi, walitaka uasi.

Kwanza, walitakiwa wasubiri uchaguzi ili washinikize kuondolewa utamaduni wa mgombea pkee.
Huo si utamaduni mzuri,nasikitika ZZK aliukubali kwa makubaliano rasmi kama waraka ulivyosema.

Pili, waraka haukuandikwa kama njia mbadala bali vifungu vya kejeli, matusi na kashfa.
Ukisomwa tu mbele ya jamii, waraka unawatia hatiani hata kabla ya kesi kuzungumzwa tatizo ambalo wasomi hawakuliona.

Waraka ungekuwa na maudhui mwanana ingetoa benefit of doubt and offer the second chance to think, kwa jinsi ulivyo tu haionekani kama umeumgwa mkono isipokuwa kwa Zitoism ambao hawabadiliki hata kitokee nini.

Tatu, hawakuwa na sababu za kuandika waraka, walikuwa na nafasi ya kusimama na kusema hili ndiyo hili hapana.Wanachama wangewaona wana demokrasia wa kweli zaidi ya wapika majungu.
Mrema aliungwa mkono si kwasababu ni mahiri wa hoja bali alisimama na kusema ABCD hakubaliani nayo NA alipomfukuza bado alikuwa na rally kwasababu watu waliamini alichosimamia.

Nne, hawa waandika waraka inaonekana ni 'woga' kwasababu hawakuwahi kutumia fursa kutetea wanachokiona si sahihi.Ningeungana nao kama wangefukuzwa katika kikao kwa kuhoji tenda za mwenyekiti wao au hesabu za fedha ndani ya vikao na kwa uwazi.

Tano, ninabaki kuAmini ziara ya Dr Slaa haikuwa na umuhimu. Dr Slaa alipaswa ashughulikie matatizo makao makuu na kukiweka chama katika nidhamu na mstari,si kwenda kujenga hoja kwa wapiga kura.
Watu wa Kigoma wanaamini ZZ ana uwezo sana, kuwabadilisha ni muda tu watarudi katika falsafa ya Zitoism

Sita, tukamshauri ZZK asikimbilie katika vyombo vya habari kwasababu kufanya hivyo anazidi kuchochea mgogoro na ni ukosefu wa nidhamu. Huwezi kuwa na press conference moja ya kuomba radhi kesho ukawa na nyingine ya kutetea ulichoombea radhi. Hiyo ni political immaturity ya hali ya juu.

KWANINI ZITTO AMEKWENDA KIGOMA
Kwenda kwake kulikuwa na maana kuu mbili
1. Kutaka kuonyesha jinsi anavyoungwa mkono na kuwa hukumu yake izingatie hayo.
Alikwenda Kigoma kwasababu huko anaungwa mkono si kama CDM bali mtoto wa nyumbani.

Sijui hiyo anawezaje kuifanya kama political platform ukizingatia kuwa imeshatoa picha mbaya.
Zitto hataungwa mkono tena na sehemu nyingine kwasababu inaonekana hoja yake ni 'sisi dhidi ya wao'

Kisiasa amejiweka katika wakati mgumu. Hata kama atagombea atakuwa ameshapoteza sehemu kubwa ya uungwaji mkono. Yale madai ya uchaga na ukanda yanayosemwa na 'wafuasi wa waraka' yataenda mbali na kuchukua sehemu kubwa ya uungwaji mkono katika kanda ingine.
Yaani anashadidia hisia zilizokuwepo akiungwa mkono na maaskofu na masheikh waliosema 'wenzako wanakuogopa'

2. Ziara ya ZZK imelenga katika kuimarisha political base yake. Anafahamu matokeo ya kesi yanaweza kwenda either way. Akipoteza ubunge ni rahisi kwenda NCCR,CUF au CCM kupigania nafasi yake.
Ni possible na anaweza kushinda. Tatizo laitakuwa ni mwanzo wa mwisho wake.
Huwezi ku sustain political pressure kwa kutumia watu wa nyumbani, atakuwa amepoteza trust kubwa sana.

Nimgekuwa ZZK ningetafuata muafaka na viongozi mambo yaishe bila kuacha kusema kile anachodhani ni sahihi katika sehemu sahihi na muda muafaka.

Ningekuwa viongozi nisingeacha hili suala liwe talk of the day. Kungefanyika damage control ya haraka kwa kufikia uamuzi wa tatizo mapema ili yaachwe nyuma na waendelee na mambo mengine.

Leo mzozo unaonekana kufifia, baada ya wiki moja utakuwa mbichi na healing process takes alot of their time.
Hawana muda wa kushughulika na individual bali mass.
Kutozuia uharibifu ni udhaifu wa uongozi wa CDM wa muda mrefu. Wataendelea hivi hadi lini?

Talk za radio na makala magazetini yanazidi kuwavuruga bila wao kujijua.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3
Nami natoa Udhaifu wa Hoja hii
""6, Hoja#14, si kweli kuwa vyama vya siasa vinajengwa na wafuasi.
Ukweli ni kuwa wafuasi wanajenga chama kwa kuamini katika sera za chama na misimamo yake.

Chama kinachojengwa na mtu ni genge la watu na si chama au taasisi.
Hoja ya kusema mbunge mwenye wafuasi akifukuzwa chama kitakufa au kutetereka ina mashiko tu kwa chama kinachoamini katika personality na si policy.
Sijui CDM ambayo yeye alikuwa mshauri kinaamini katika nini."""Unachokisema kuwa Wafuasi wanafuata Sera sio kweli ni kujaribu kuutaa Ukweli"siasa ya vitendo"na kuikumbatia "siasa makaratasi"
Wafuasi wanaangalia Je huyo mtu au kiongozi ana Uwezo kutekeleza kilicho andikwa,ndo imani inakuwepo,Kama maandishi ya Sera yanavuta watu,kwanini watu Wahame CCM na Waende CDM,CUF,UDP,NCCR,kwa akili ya Kawaida hivi vyama vya Siasa vya Tanzania kipi kinasera inayoonekana kujali watu wa chini,kama ni CCM, kwanini watu Wahame?je Kama CDM kina Sera Mzuri Kwanini nacho watu wanahama.....Siasa afrika watu wanaangalia Mtu,Ukweli ndo huo
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 naendelea kupinga Utabiri wako wakutaka kutuambia Zitto asipofuata ushauri wako hapo JF basi ni mwisho ni kujidanganya,eti unafananisha Zitto na Mrema,Vitu tofauti,Zama za Zito sio za Mrema,tofauti kabisa...Zitto hajawai kuwa Mwenyikiti wa chama wala hajawai kugombea Urais,na hajawai kushika nafasi katika serikali,Maisha ya Zitto tokea akiwa mtoto ni ya Upinzani tu...tatizo wanaduru tumekuwa tukitafuta mifano ya watu walioanguka katika siasa na kumuonyesha Zitto hili haogope kutetea Ukweli,yaani unadiliki kusema Zitto hatokubaliwa mikoa mingine sababu alirudi Kigoma,Tafiti hiyo imeifanya Lini mkuu,tuwe wakweli ule waraka hauna tatizo lolote kwa CDM.
Alafu unajifanya ujui kama vyama au taasisi zetu zinaongozwa na ubabe....unadai Zitto na Kitila kwanini malalamiko yao hawakuyatoa ndani ya chama,mbona Zitto kasema alishasema sana na mpaka hakahamua kujiondoa kuwa mtia sahihi.....
"Akisema Zitto muongo ila akisema Slaa ni Ukweli"duuh
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 naendelea kupinga Utabiri wako wakutaka kutuambia Zitto asipofuata ushauri wako hapo JF basi ni mwisho ni kujidanganya,

eti unafananisha Zitto na Mrema,Vitu tofauti,Zama za Zito sio za Mrema,tofauti kabisa...Zitto hajawai kuwa Mwenyikiti wa chama wala hajawai kugombea Urais,na hajawai kushika nafasi katika serikali,Maisha ya Zitto tokea akiwa mtoto ni ya Upinzani tu...tatizo wanaduru tumekuwa tukitafuta mifano ya watu walioanguka katika siasa na kumuonyesha Zitto hili haogope kutetea Ukweli,yaani unadiliki kusema Zitto hatokubaliwa mikoa mingine sababu alirudi Kigoma,Tafiti hiyo imeifanya Lini mkuu,tuwe wakweli ule waraka hauna tatizo lolote kwa CDM.

Alafu unajifanya ujui kama vyama au taasisi zetu zinaongozwa na ubabe....unadai Zitto na Kitila kwanini malalamiko yao hawakuyatoa ndani ya chama,mbona Zitto kasema alishasema sana na mpaka hakahamua kujiondoa kuwa mtia sahihi.....
"Akisema Zitto muongo ila akisema Slaa ni Ukweli"duuh
Adharusi, kwanza kabisa nadhani unasoma nilichoandika kwa hamaki na kukosa hoja muhimu sana.
Tafadhali tulia kwanza uelewe watu wanaongelea nini.

Pili, tunatoa maoni kwa mitazamo yetu na wala hatufanyi utabiri. Mawazo yanaweza kuwa sahihi au la na hivyo ni msomaji kama wewe utakayeamua kutokana na maono yako.

Hivyo tutaendelea kuandika kutokana na mitazamo tofauti na tungekushauri nawe pia uungane nasi katika kukosoa, kuhoji, kufafanua, na kueleza kile unachokiona kwa mtazamo wako, huo ndio utaratibu wa duru.

Hatukubaliani bali tunaweza kukubaliana au kutokubaliana lakini kwa hoja na si kunyosheana vidole tu bila kujibu hoja, kufafanua, kuweka mbadala au kukosoa. Hivyo sivyo tunavyofanya.

Tatu, umekosa hoja muhimu sana, mimi sijamfananisha Mrema na Zitto.
Nilichokifanya nikuonyesha mienendo ya kisiasa.

Nilisema Mrema aliondoka CCM na kufuatwa na kundi kubwa kwasababu tu waliamini alisimamia kile alichokiona ni sahihi.

Nikaendelea kusema wapo wanaoitwa Zittoism (nadhani wewe ni mmoja wao) ambao wanamuona Zitto kama kiongozi wao bila kuangalia maeneo mengine.

Nikaendelea kujenga hoja za namna Mrema na Zitto walivyo katika nyakati za kisiasa kwa sasa na wala si kuwafananisha. Unapaswa kuelewa kitu kinaitwa reference ili uweze kujenga au kubomoa hoa.

Nne, nimesema kuwa kitendo cha Zitto kukimbilia nyumbani kwao kilikuwa na sababu mbili nilizozitaja.

Nikaendelea kufafanua kuwa kuna tuhuma za ukanda ambazo zinaenezwa dhidi ya CDM.
Kitendo cha Zitto kwenda kwao katika wakati huu hakikuwa na busara kwasababu kauli za viongozi wa dini zinaonyesha kuwa Zitto hana tatizo, bali tatizo ni wenzake wa kanda zingine wanaomuogopa.

Nikasema kuwa hilo linaingia katika akili za watu wengine kirahisi kwasababu tuhuma zilikuwepo na itaonekana kama ZZ anazifanyia kazi. Matokeo ya ziara zake ni kupata wakati mgumu siku za usoni. Ukielewa political landscape ya Tanzania hutashindwa kunielewa.

Tano, kuna kitu kinaitwa research na kingine kinaitwa analysis.
Katika siasa kuna uchambuzi na kuna utafiti na hivyo kilichofanyika ni uchambuzi na wala si lazima kiwe na takwimu.

Hapa napo nakushauri uangalie maudhui ya research na uchambuzi ili uweze kuelewa unatumiaje maneno hayo, wakati gani na kwasababu zipi.
Mfano, JK alipomteua Rose Migiro kuwa mbunge hakukuwa na data kwasababu ni JK na Rose Migiro. Lakini ukifanya analysis utaweza kupanua hoja hiyo kwa kuangalia shughuli alizofanya tangu arudi kutoka UN, kwanini amemchagua sasa hivi na si mwaka jana na uwezekano wa Rose kama mbunge wa kuteuliwa kuwa MP ni upi.
Hapo huhitaji data, unachohitaji ni wazo na kulifanyia uchambuzi.

Sita, kuhusu Zitto kusema sana hiyo haitoshi alipaswa aachie ngazi na si kuacha kusaini documents. Kuachia ngazi maana yake ni kupata attention na kuungwa mkono zaidi.
Kanuni za demokrasia zingemsaidia sana katika utetezi. Hili la kudai alisema alisema hatujui kama alisema au la, angejiuzulu tungekuwa na ushahidi wa alisema.

Saba, umedai waraka hauna tatizo. Wengine tumeeleza tatizo la waraka tena tukiungwa mkono na Kitila aliyeomba radhi kwa kushiriki kuandika.

Ulipaswa utujibu na kuonyesha kwanini waraka hauna makosa kama ambavyo tumeonyesha una makosa. Huko ndiko kujibizana kwa hoja, kusema tu hauna makosa ndio falsafa za kuamini mtu na si ukweli.

Najua unampenda ZZ na hilo si kosa, lakini kwenye hoja tunasimama katika maoni ya kila mmoja ili kupata ukweli.

Nane,Hiyo Kauli yako ya mwisho inavuruga maana ya mjadala. Hapa hatupambanishi watu. Tunapambanisha hoja zinazotokana na watu. Hakuna mahali nimesema ni muongo wala hakuna sehemu nimesema Slaa ni mkweli.

Endapo ungefuatilia majadiliano ya duru katika nyuzi zilizopita utaona wazi kuwa Dr Slaa alishapata dozi, Mbowe alishapata dozi,Nape alishapata, Mwigulu amepata, Tindu Lisu amepata n.k Nina maana kuwa hakuna kiongozi anayefyonga tukamuacha.

Hebu rudi katika suala la katiba uone asili ya neno 'Togwa ya Ikulu' na Mbowe. Hatukumuacha Slaa wala Mbowe tuliwapa moja kwa moja.

Tafadhali sana si vema uka insinuate mambo yasiyokuwepo.
Katika mijadala kama hii uvumilivu unahitajika na hilo ni muhimu ukalizingatia.

Tunaheshimu sana michango na mawazo yako, lakini litendee jamvi haki.
Kusema waraka hauna kosa ni kosa kwasababu hujaonyesha wapi ukweli ulipo na kwasababu zipi.kutunga maandishi na kusema fulani kasema si kweli na haki

Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 nimekuelewa ushahuri wako naahidi kufanyia kazi mapungufu yangu
"Nikaendelea kusema wapo wanaoitwa Zittoism (nadhani wewe ni mmoja wao) ambao wanamuona Zitto kama kiongozi wao bila kuangalia maeneo mengine"nimenukuu bandiko lako naomba kukuambia sijawai kumtetea Zito zaidi ya ishu hii ya "Waraka"na nilianza kuwa upande wa Zitto baada ya bandiko la Mh Lema kumshutumu,nilimtetea si kwa sababu namfaham hapana,niliona CDM uongozi uko kimya,nimetofatiana na ZKK mara nyingi sana katika Mitandao ya kijamii kuliko nilivyo mtetea.naamin umenielewa
Ila siku zote nimechagua upande wa Haki
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 nimekuelewa ushahuri wako naahidi kufanyia kazi mapungufu yangu
"Nikaendelea kusema wapo wanaoitwa Zittoism (nadhani wewe ni mmoja wao) ambao wanamuona Zitto kama kiongozi wao bila kuangalia maeneo mengine"nimenukuu bandiko lako naomba kukuambia sijawai kumtetea Zito zaidi ya ishu hii ya "Waraka"na nilianza kuwa upande wa Zitto baada ya bandiko la Mh Lema kumshutumu,nilimtetea si kwa sababu namfaham hapana,niliona CDM uongozi uko kimya,nimetofatiana na ZKK mara nyingi sana katika Mitandao ya kijamii kuliko nilivyo mtetea.naamin umenielewa
Ila siku zote nimechagua upande wa Haki
Mkuu wangu umemaliza na kama ulikuwa moyoni mwangu maana hata mimi nimekuja mtetea Zitto ktk sakati hili. Mpaka sasa uongozi wa Chadema haujaniridhisha ktk maamuzi yake ikiwa hoja kubwa ni waraka huu.

Mkuu Nguruvi3, haya matusi tunayompa JK kama angetumia fikra hizi hizi leo hii tungekuwepo?.. ni mara ngapi JF ilitaka kufungiwa kwa sababu tunayasema wazi mapungufu ya JK na ilifikia hadi Mnyika kumwita JK rais Mdhaifu na watu tukaungana naye maana kuna ukweli. Mangapi tumeyasema juu ya rais na hata wengine kufanya mikutano ya siri ktk kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015.

Huwezi kuuita UASI ama uhaini ikiwa mipango yenyewe imelenga maguzi ktk Uchaguzi ujao ambapo wajumbe walikuwa na nafasi ya kuchagua mgombea wanayemtaka, hakuna atakaye wekewa bunduki usoni. Hivyo mipango ya kina Kitila isingeweza kufanikiwa ikiwa kweli wanachama wengi bado wanaamini uongozi uliopo unaweza kuwaletea ushindi na pengine mwenyekiti angekuwa mtu mwingine kabisa.

Na nikwambie tu ya kwamba binafsi yangu kama ZZK angegombea Uenyekiti na mimi niwe ktk mjumbe wa baraza kuu nisingempa kura yangu kwa sababu sidhani kama ana uwezo wa kuongoza chama. Huo upambe uko wapi?..Hivyo ndio maana sioni tatizo kabisa na waraka isipokuwa waraka huo umenifunua zaidi kujua kinachoendelea makao makuu na hii ndio siri ambayo viongozi hawakuta itoke nje.

Yaliyopo ktk waraka, ndio usaliti wanaoutazama viongozi, kamati kuu na watu kama nyie.. Ni kutoa siri za chama ktk matumizi na uendeshaji wa chama ambao unawapa miliki baadhi ya watu walojiweka ktk nyadhifa - Kwa madai kwamba wangeyapeleka madai hayo ktk vikao, yaani kundi lile lile linalokifisadi chama ndio wapokee madai hayo ili iiweje?. nachoomba mimi kuanzia sasa zungumzieni madai ya waraka huo na ukweli tuupate kama hawa kina Kitila walisema uongo wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu umemaliza na kama ulikuwa moyoni mwangu maana hata mimi nimekuja mtetea Zitto ktk sakati hili. Mpaka sasa uongozi wa Chadema haujaniridhisha ktk maamuzi yake ikiwa hoja kubwa ni waraka huu.

Mkuu Nguruvi3, haya matusi tunayompa JK kama angetumia fikra hizi hizi leo hii tungekuwepo?.. ni mara ngapi JF ilitaka kufungiwa kwa sababu tunayasema wazi mapungufu ya JK na ilifikia hadi Mnyika kumwita JK rais Mdhaifu na watu tukaungana naye maana kuna ukweli. Mangapi tumeyasema juu ya rais na hata wengine kufanya mikutano ya siri ktk kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015.

Huwezi kuuita UASI ama uhaini ikiwa mipango yenyewe imelenga maguzi ktk Uchaguzi ujao ambapo wajumbe walikuwa na nafasi ya kuchagua mgombea wanayemtaka, hakuna atakaye wekewa bunduki usoni. Hivyo mipango ya kina Kitila isingeweza kufanikiwa ikiwa kweli wanachama wengi bado wanaamini uongozi uliopo unaweza kuwaletea ushindi na pengine mwenyekiti angekuwa mtu mwingine kabisa.

Na nikwambie tu ya kwamba binafsi yangu kama ZZK angegombea Uenyekiti na mimi niwe ktk mjumbe wa baraza kuu nisingempa kura yangu kwa sababu sidhani kama ana uwezo wa kuongoza chama. Huo upambe uko wapi?..Hivyo ndio maana sioni tatizo kabisa na waraka isipokuwa waraka huo umenifunua zaidi kujua kinachoendelea makao makuu na hii ndio siri ambayo viongozi hawakuta itoke nje.

Yaliyopo ktk waraka, ndio usaliti wanaoutazama viongozi, kamati kuu na watu kama nyie.. Ni kutoa siri za chama ktk matumizi na uendeshaji wa chama ambao unawapa miliki baadhi ya watu walojiweka ktk nyadhifa - Kwa madai kwamba wangeyapeleka madai hayo ktk vikao, yaani kundi lile lile linalokifisadi chama ndio wapokee madai hayo ili iiweje?. nachoomba mimi kuanzia sasa zungumzieni madai ya waraka huo na ukweli tuupate kama hawa kina Kitila walisema uongo wapi?

Kweli mkuu!sipati Picha Rais Kikwete angekuwa kama Mbowe,na watu wanamzunguka Mbowe ndo wangekuwa kwa Kikwete!Leo Mnyika na Tundu Lisu wanauwezo wa kusema neno lolote na kumtukana Rais wa nchi lakini hao hao awawezi kumkosoa Mbowe na Slaa hata kwa Lugha ya upole,wanawaona Malaika
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA ILIPO NA IENDAKO

Mgogoro wa CDM umezidi kutitia na kuhusisha watu nje ya chama chao.
Hali ilivyo si shwari na kile tulichokisema katia duru za siasa tarehe 7 October 2012 kwamba kati ya June 2013 na January 2014 kutakuwa na mtafaruku mkubwa sana.

Kama utafuatilia uzi huu unaoendelea tulionya uongozi wa CDM kuhusu ukubwa wa tatizo.
Tuliwauliza Mbowe na Dr Slaa kama kulikuwa na umuhimu wa kufanya ziara za mikoani baada ya kuwavua uongozi watuhumiwa wakubwa wa timbwili hili.
Tulisema busara hazionyeshi umuhimu wowote wa ziara hizo.

Tulitoa sababu kuu mbili:
1. Kwamba mgogoro si wa wanachama au mashabiki wa CDM.
Mgogoro upo makao makuu, ushughulikiwe haraka kuzuia uharibifu unaoweza kutokea ukiachwa kuwa endelevu kama ilivyo sasa.

2. Kwamba, kuwazuia wanachama wasiondoke kwa mikutano ni mbinu dhaifu sana.
Wapo wanachama wanaoamini katika sera, wapo wanaotaka mabadiliko, wapo wanaoamini katika watu na si chama wala sera. Hawa wanaoamini katika watu huwezi kufanya lolote kuwabadilisha kwasababu uaminifu wao ni kwa mtu baasi!kukimbizana nao ni kupoteza muda.

Kwa taarifa zilizopo, kikao cha kamati kuu wiki hii kilikuwa cha dharura.
Sioni sababu za udharura kwasababu kila jambo lilikuwa wazi, madhara ya mgogoro ni makubwa

Suala la ZZK lilikuwa litafutiwe ufumbuzi wa haraka kwamba ni suala lililoko makao makuu na wala si vijijini au mitaani. Uongozi ulizembea na kukimbizana na dharura ukitoa mwanya zaidi wa haribifu

ZZK anafahamu hatima yake ndani ya CDM ni majaaliwa na hivyo yeye hana cha upoteza lakini anaweza kufanya jambo la kupoteza.

Kitendo cha ZZK kutaka rufaa isikilizwe na baraza kuu kilikuwa na maana kuu mbili.
1. Ima ana wajumbe watakaomuunga mkono
2. Kugawa baraza ili CDM iwe na makundi na huenda ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa CDM.

Wiki chache zilizopita ZZK alisema ni mwanachama mtiifu na mtu wa mwisho kuihujumu CDM. Well, mambo yanayoendelea yamedhihirisha kuwa hizo ni kauli za kisiasa maana hujuma aliyoifanya ni kubwa kwamuonekano tu kwa kuanzia.

Kwa upande wa uongozi nako kumekuwa na tatizo.
Kwanza kama ilivyosemwa hapo juu, tatizo halikupewa udharura na kuendelea kwa muda mrefu.

Pili, nao pia wakavutika katika mtego wa ZZK na kujikuta katika malumbano yasiyo na maana wala tija bali kuzidi kubomoa chama chao.

Uongozi unawajibika katika kuzembea kulishughulikia tatizo na ndio sehemu kubwa ya uharibifu unaoendelea. Huwezi kuchukaua hatua nusu nusu ukipima mambo ya kisiasa kwa litmus test.

Kwa upande wa ZZK, ingawa inaonekana ameshinda kubaki mwanachama hadi hatua za kisheria zikamilike na kuonekana kama shujaa wa wakati fulani, jitihada zake zinazidi kummaliza kisiasa.

1. Ile dhana kuwa anatumiwa kubomoa upinzani, na zile hisia kuwa zipo bilioni 3.6 kwasababu hiyo zinaweza kuzama vichwani mwa watu bila kujali ukweli au uongo uliopo.

2. Ni dhahiri hata wapenzi na wafuasi wake wanakereka na hali ya mambo ilivyo.
Hakuna sababu za ZZK kueleza mambo aliyoyajua leo hii.
ZZK alikuwa na fursa na aliamua kukaa kimya, leo ushujaa wa kusema anaupata wapi? Ndio viongozi wanaotegemewa na taifa siku za usoni?

3. Wengi watahoji je hii ni mwaga mboga nimwage ugali na inasaidiaje hatima ya siasa za nchi hii siku za usoni.

Kwavile ZZK amekuwa focus ya mgogoro, kuanguka kwa upinzani hakutaweza kutenganishwa na ZZK. Hapo ndipo hoja namba 1 inapokuwa na mashiko hata kama ni dhana tu

Kikubwa kinachomsukuma ZZK si chama tena ni ubunge tu.
Hata kama atafanikiwa kuongoza chama chochote cha siasa , kwa mwenendo wake wa sasa ni dhahiri amepoteza sifa ya uongozi sifa ya kuaminika na sifa ya nia yake.
ZZK atabaki kuangaliwa kwa jicho upande.

Hatima yake itakuwa kama ya Mrema aliyehana na kundi la wafuasi na leo yupo peke yake.
Hata anaposimama na kusema hakuna anyejadili kwasababu Mrema amepoteza nguvu na uhalali wa kisiasa. Naye yupo kwasababu ya ubunge tu. Ndiko anakoelekea ZZK

Tafsiri kuwa ZZK atakuwa martyr au shujaa haitatokea kwasababu ameshindwa kutumia mikakati ya kisiasa katika kufikia malengo yake na malengo aliyoaminiwa na umma.

All in all, kuacha suala hili lizidi kuzungumzwa ni kushindwa kuelewa dhana ya damage control.
Ni muhimu CDM wakachukua hatua za haraka na dharura kuumaliza mgogoro kwa njia yoyote wanayodhani ni muafaka si kwa manufaa yao bali kwa ustawi wa chama chao.

Tusemezane
 
CHADEMA ILIPO NA IENDAKO

Mgogoro wa CDM umezidi kutitia na kuhusisha watu nje ya chama chao.
Hali ilivyo si shwari na kile tulichokisema katia duru za siasa tarehe 7 October 2012 kwamba kati ya June 2013 na January 2014 kutakuwa na mtafaruku mkubwa sana.

Kama utafuatilia uzi huu unaoendelea tulionya uongozi wa CDM kuhusu ukubwa wa tatizo.
Tuliwauliza Mbowe na Dr Slaa kama kulikuwa na umuhimu wa kufanya ziara za mikoani baada ya kuwavua uongozi watuhumiwa wakubwa wa timbwili hili.
Tulisema busara hazionyeshi umuhimu wowote wa ziara hizo.

Tulitoa sababu kuu mbili:
1. Kwamba mgogoro si wa wanachama au mashabiki wa CDM.
Mgogoro upo makao makuu, ushughulikiwe haraka kuzuia uharibifu unaoweza kutokea ukiachwa kuwa endelevu kama ilivyo sasa.

2. Kwamba, kuwazuia wanachama wasiondoke kwa mikutano ni mbinu dhaifu sana.
Wapo wanachama wanaoamini katika sera, wapo wanaotaka mabadiliko, wapo wanaoamini katika watu na si chama wala sera. Hawa wanaoamini katika watu huwezi kufanya lolote kuwabadilisha kwasababu uaminifu wao ni kwa mtu baasi!kukimbizana nao ni kupoteza muda.

Kwa taarifa zilizopo, kikao cha kamati kuu wiki hii kilikuwa cha dharura.
Sioni sababu za udharura kwasababu kila jambo lilikuwa wazi, madhara ya mgogoro ni makubwa

Suala la ZZK lilikuwa litafutiwe ufumbuzi wa haraka kwamba ni suala lililoko makao makuu na wala si vijijini au mitaani. Uongozi ulizembea na kukimbizana na dharura ukitoa mwanya zaidi wa haribifu

ZZK anafahamu hatima yake ndani ya CDM ni majaaliwa na hivyo yeye hana cha upoteza lakini anaweza kufanya jambo la kupoteza.

Kitendo cha ZZK kutaka rufaa isikilizwe na baraza kuu kilikuwa na maana kuu mbili.
1. Ima ana wajumbe watakaomuunga mkono
2. Kugawa baraza ili CDM iwe na makundi na huenda ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa CDM.

Wiki chache zilizopita ZZK alisema ni mwanachama mtiifu na mtu wa mwisho kuihujumu CDM. Well, mambo yanayoendelea yamedhihirisha kuwa hizo ni kauli za kisiasa maana hujuma aliyoifanya ni kubwa kwamuonekano tu kwa kuanzia.

Kwa upande wa uongozi nako kumekuwa na tatizo.
Kwanza kama ilivyosemwa hapo juu, tatizo halikupewa udharura na kuendelea kwa muda mrefu.

Pili, nao pia wakavutika katika mtego wa ZZK na kujikuta katika malumbano yasiyo na maana wala tija bali kuzidi kubomoa chama chao.

Uongozi unawajibika katika kuzembea kulishughulikia tatizo na ndio sehemu kubwa ya uharibifu unaoendelea. Huwezi kuchukaua hatua nusu nusu ukipima mambo ya kisiasa kwa litmus test.

Kwa upande wa ZZK, ingawa inaonekana ameshinda kubaki mwanachama hadi hatua za kisheria zikamilike na kuonekana kama shujaa wa wakati fulani, jitihada zake zinazidi kummaliza kisiasa.

1. Ile dhana kuwa anatumiwa kubomoa upinzani, na zile hisia kuwa zipo bilioni 3.6 kwasababu hiyo zinaweza kuzama vichwani mwa watu bila kujali ukweli au uongo uliopo.

2. Ni dhahiri hata wapenzi na wafuasi wake wanakereka na hali ya mambo ilivyo.
Hakuna sababu za ZZK kueleza mambo aliyoyajua leo hii.
ZZK alikuwa na fursa na aliamua kukaa kimya, leo ushujaa wa kusema anaupata wapi? Ndio viongozi wanaotegemewa na taifa siku za usoni?

3. Wengi watahoji je hii ni mwaga mboga nimwage ugali na inasaidiaje hatima ya siasa za nchi hii siku za usoni.

Kwavile ZZK amekuwa focus ya mgogoro, kuanguka kwa upinzani hakutaweza kutenganishwa na ZZK. Hapo ndipo hoja namba 1 inapokuwa na mashiko hata kama ni dhana tu

Kikubwa kinachomsukuma ZZK si chama tena ni ubunge tu.
Hata kama atafanikiwa kuongoza chama chochote cha siasa , kwa mwenendo wake wa sasa ni dhahiri amepoteza sifa ya uongozi sifa ya kuaminika na sifa ya nia yake.
ZZK atabaki kuangaliwa kwa jicho upande.

Hatima yake itakuwa kama ya Mrema aliyehana na kundi la wafuasi na leo yupo peke yake.
Hata anaposimama na kusema hakuna anyejadili kwasababu Mrema amepoteza nguvu na uhalali wa kisiasa. Naye yupo kwasababu ya ubunge tu. Ndiko anakoelekea ZZK

Tafsiri kuwa ZZK atakuwa martyr au shujaa haitatokea kwasababu ameshindwa kutumia mikakati ya kisiasa katika kufikia malengo yake na malengo aliyoaminiwa na umma.

All in all, kuacha suala hili lizidi kuzungumzwa ni kushindwa kuelewa dhana ya damage control.
Ni muhimu CDM wakachukua hatua za haraka na dharura kuumaliza mgogoro kwa njia yoyote wanayodhani ni muafaka si kwa manufaa yao bali kwa ustawi wa chama chao.

Tusemezane
Mkuu Nguruvi3, unachambua vizuri lakini bahati mbaya sana umezidiwa na ushabiki katika mada hii. Labda nikuzindue kwa mambo yafuatayo:-
Ikitokea Zitto amekamatwa na madawa ya kulevya pale JKNIA na picha zikapigwa na zikasaamba kwenye magazeti na kuonyeshwa kwenye televishen, siku hiyohiyo Zitto anapoteza wasapoti(wapenzi, washabiki) wake wote-rapidly and absolutely. Nataka kusema nini? Ni kwamba nakubaliana na wewe huu mgogoro ulikuwa ni mdogo sana kama busara, kweli na open agenda zingetawala. Kilichopo sasa hivi au kilichotokea ni kwamba, jamii/public imeshidwa kuthibitishwa bila chenga uovu na kosa halisi la Zitto ndio maana makundi mawili yameibuka. Badala yake, ni kama viongozi wa Chadema au walio karibu na Chadema ndio wanaojua bila changa uovu wa Zitto kwa Chama chake na kwa umma. Kwakuwa public haina "uhalisia" huo ndio maana tuko divided, na kwa kuwa viongozi au walio karibu na Chadema ndio wanaojua hilo, wanalofanya ni kutumia tactic strategy kuuaminisha umma mabaya ya Zitto badala ya vivid evidence kama nilivyotolea kwenye mfano wa madawa ya kulevya hapo juu. Na mbaya zaidi ni hatua ya kukumbushiana mabaya waliyoyafanya katika kipindi wakiwa marafiki. Kwa kawaida unapokuwa na rafiki ambaye ukifanya maovu anakuona na kutosema maovu yako, maana yake ni kwamba na wewe kuna maovu huwa unafanya na yeye hayasemi. Ikitokea siku wewe ukiyasema maovu ya mwenzako yaliyofanywa mkiwa marafiki baada ya kugombana, ni wazi kwamba mwenzako naye atatoa maovu yako aliyokuwa anakufichi. Katika hali kama hii, umma unazidi kugawanyika kila mmoja ataendela kuamini yaliyotoka kwa mwingine bila kujali ushahidi wowote.

Kinachoonekana ndicho hicho CDM(viongozi na wapambe), wameshindwa kuuthibitishia umma uovu wa Zitto, na simply kwasababu tuhuma zinazomkabili(ziwe kweli au sikweli) hazina ushahidi wa moja kwa moja (hakuna risiti ya rushwa wala hakuna mwenye uwezo wa kujua ukweli kutoka kwenye nafsi ya Zitto kama ana dhamira ya kukiua chama au hapana). Kutokana na mazingira haya, umma unatumia hisia zao katika kutoa judgement, ndio unaona wapo wanaoamni ni kweli zitto msaliti na wengine wanaona kinachoendelea ni vita ya uongozi ndani ya chama. Huu ndio ukweli na utaendelea kubaki hivi mpaka "empirical evidence" zipataikane ambapo hakuna mtu atakaye-doubt ushahidi huo.

Nini kifanyike, au kilichotakiwa kifanyike: CDM haikupaswa kucheza na media katika suala hili ilipaswa kucheza na mikakati ya ndani. Kwa kupitia Waraka uliokuwa wanaundaa akina Kitila, wangeupindua na kuwa mkakati wao, wangetumia wajumbe wa mikutano ya chama "kumnyima" kura Zitto katika uchaguzi(hili naamini lilikuwa jambo rahisi sana kwani siamini kama Zitto ana wapiga kura wa kutosha ndani ya chama). Ingawa hili lingewashtua iwapo angeshinda. Aidha katika kufanya hili, wangeweza hata "kumuondolea" vigezo vya kuwa mgombea (Mathalan, wangechomoa hata baadhi ya requirements katika harakati zake za kuomba, au wangelijaza upya hata fomu zake na kuonyesha amejaza kimapungufu). Ingawa jambo hili lingejulikana, lakini lingelianzishwa na Zitto mwenyewe hivyo umma ungemuona yeye ndiye kikwazo na angekosa public rally. Naamini ziko njia nyingi tu kama makao makuu wangeweza kuzitumia kumtoa nje ya ulingo Zitto.

Sasa nini kifanyike sasa hivi: Hii nafasi bado ipo:-

1. Baraza Kuu limrudishie vyeo vyake vyote. Kwa vile sintofahamu baina ya wadau wa makao makuu ni kubwa, ni wazi Zitto hataweza kufanya kazi nao (Ni ngumu sana kwa mtu mwenye akili kufanyiwa dharau na hata na maskretari). Jambo hili lingemuweka Zitto kama kiongozi ceremonial.
2. Baraza Kuu limrudishie vyeo vyake na kisha kuanzisha suluhu ya ndani ya chama bila kushirikisha umma. Hili lina faida kubwa zifuatazo, kwanza litawaunganisha kwa mara nyingine mashabiki wanaotofautiana katika chama (yaani wa Mbowe et. al na wale wa Zitto). Siamini kama kwa hali iliyopo, ndani ya chama Zitto atakuwa na uwezo wa kufurukuta kwani watawekeana makubaliano ya kulinda umoja wa chama, badala ya kumuacha nje ya chama ambapo Zitto anapata media coverage. Pia hili, lingebadilisha media propaganda na kubaki na agenda kuu moja tu "CDM yanywea kwa Zitto", agenda ambayo haitabomoa chama bali itatoa image kwamba CDM wamerejea kwenye suluhu ya kidiplomasia jambo amabalo sidhani kama kuna asiyelipenda. Juu ya kuendelea "kuhujumu" chama kama atakuwa ndani ya Chama, sidhani kama ina nguvu kwani pindipo "mchawi" akijulikana, hana tena uhuru wa kutumia uchawi wake, na pia ni jukumu la CDM kumbania fursa za kuweza "kukisaliti" chama kama wanavyodai. Katika kufanya hivi, (suluhu ya muda); CDM wangeapata muda wa kujipanga vyema njia nyingine ya "kumuondo" kwenye chama bila kuathiri chama kwani hii ya sasa si muafaka. Hili hata hivyo lina madhara yake kwani linaweza kumpaisha zaidi Zitto kitu ambacho naona CDM hawakipendi kiwepo. Lakini ijulikane tu, hata samaki anavuliwa kwa kupewa samaki au nyama. Au hii ni gharama ya kukipa uhai chama kwa malipo ya baadaye kwa vile ni jambo lenye mkakati wa baadaye.

Kwa kifupi ni kwamba, tunaitaka CDM itakayotokea kwenye media huku Zitto, Mbowe na Slaa wamekumbatiana ili kubadilisha attention ya umma na media(japo ukweli ni kwamba mgogoro utakuwa unashughulikiwa ndani ya chama). Kinyume cha kutumia hii siasa ya Kenya, tusahau CDM imara hata kama tutamuandamana kila siku kwa mabango kwamba Zitto msaliti a CDM. Pia napenda kurudia wito wangu mara nyingi; CDM ibadilishe Sekretarieti yake au watendaji wake wa Makao makuu haraka, wawapeleke mikoani au wasiwe watu wa karibu na information pot ya CDM.
 
Mkuu nguruvi,

Mgogoro huu kwa hakika unaitikisa zaidi CDM na natumaini wataweza kukaa chini na kutafakari ili kujifunza kutokana na makosa yaliokwisha fanyika. Kwa kuanzia waache kucheza game ya ZZK kulumbana kwenye media na kutoboleana siri za nani kamhonga nani etc. Katika hili hawataweza kufanikiwa kwa sababu mwenzao anatumia vema kadi ya "victim" inayompa alama zaidi mbele ya jamii. Kama alivyonena Mkuu Zinedine hapo juu mpaka hivi sasa umekosekana ushahidi wenye nguvu usio shaka wa kumning'iniza ZZK....Hivyo basi, wanachopaswa kufanya sasa ni kujipanga upya na ushahidi wote juu ya maovu ya ZZK...na hapa namaanisha kila kitu bila kuficha chochote, waweke mambo hadharani mbele ya baraza kuu na mbele ya wananchi ili mbivu na mbichu zijulikane.

Kwa upande wa ZZK pamoja na kupita kwenye hatua hii lakini asishangilie ushindi bado akumbuke kuwa bado uanachama wake uko rehani...alichofanikiwa kwa sasa ni kuithibitishia mahakama kuwa taratibu za kumwondoa hazikufuatwa lakini hii haijamsafisha juu ya tuhuma zinazomkabili. Aachane na mambo ya kujibu tuhuma kwa kurusha tuhuma zake kwa kina Mbowe...mwisho wa siku haitamsaidia sana ikiwa ana nia ya kuja kukiongoza chama hicho siku za usoni. Unless kama nia yake ni "kuondoka wa mwisho CDM" akiwa amekiacha chama kiko hoi kimesambaratika. Ajipange kujibu tuhuma dhidi yake mbele ya baraza kuu na sio kuwarushia madongo viongozi kwa uhafidhina.
 
Wakuu zangu kuna hili la Mkono aloibuka na kusema yeye alimuuzia Zitto gari na jingine alimkodisha olakini wakati huo huo ukimsoma Zitto anasema magari alokuwa nayo ni tofauti kabisa na yale alodai Mkono.

Sasa katika kuumiza kwangu kichwa, nimeshanganzwa kwanza na madai ya Mkono kumuuzia Zitto ile Land Cruiser yake ya Ubunge. hapa nimepigwa na butaa maana huyo huyo Zitto alikataa gari kama hilo tena jipyaa linalotolewa kwa Wabunge wote kwa madai ya kuwa ni matumizi mabaya ya serikali, leo iweje aje kununua gari tena chakavu kwa huyo Mkono ambaye sii ajabu bado analipia deni? Hii inaingia akilini kweli?

Je, kuna uwezekano kuwa Mkono anatumiwa kumwaga mafuta zaidi ktk mgogoro huu au hii habari sii ya kweli imetungwa na mtu akijifanya ndiye Mkono.
Pili, Je sheria za magari hayo ya bunge inaruhusu mbunge kuuza gari ambalo kapatiwa japo kwa mkopo ili kufanyia kazi za kibunge? Kama ni ruksa hamuoni tatizo hapa!..

Mimi nafikiri mgogoro huu sasa unachukua sura mbaya zaidi hasa baada ya kumsoma Mzee Mtei akisema Zitto hatakiwi Chadema na uamuzi wa kamati kuu ndio wa mwisho. Statement hii inaliweka chini Baraza kuu la chama japo ndilo lenye mamlaka kisheria. Mimi nadhani na sintoshangaa ikiwa kuna mambo tunafichwa. Kuna maswala mazito zaidi wananchi ama wanaChadema wamefichwa kutokana na uzito wa shauri lenyewe maana nashindwa kabisa kuunganisha picha hii.
 
Mkuu Mkandara

Ni kweli kabisa mgogoro huu unachukua sura isiyopendeza hata kidogo,

Kinachoniogopesha zaidi ni hili sakata la kutekwa na kuumizwa vibaya kwa mwenyekiti wa CDM Temeke ambako sasa kunahusishwa na mgogoro unaoendelea kati ya ZZK na uongozi wa CDM. Tayari watu wameanza kufananisha yanayomtokea ZZK na yaliyomkuta marehemu Wangwe...(Hata ZZK mwenyewe anasema haya).
 
Last edited by a moderator:
Mkuu@Nguruvi3 nimeona umeshauri CDM ichukue hatua za haraka na dharura,lakini ujasema hatua gani?ili kumaliza mgogoro au kufifisha mgogoro!kama kikao cha dharura kimetufikisha hapa?Je wewe ndo ungekuwa Kamati Kuu ungefanya Uamuzi gani ili kuhiuwisha CDM?
 
Mkuu Zinedine
Kwa hali ilivyo washabiki siyo wanaosema kile kilichopo, washabiki ni wale wasiokubali tatizo na chanzo cha tatizo ni ZZK na tatizo la kiungozi kama tulivyowahi kusema.

Wasichokubali Zittoism ni ukweli kuwa kafanya makosa mengi ambayo pamoja yanamweka pabaya kisiasa na kuhatarisha hata utangamano ndani ya chama chake.

Hakuna usawa katika tatizo, kila mmoja ana shea yake na atajadiliwa kwa hilo hivyo sijui nifanyaje ili nimbambikizie Mnyika makosa ili kuleta uwiano na ZZK na kuondoa ushabiki, sijui kwakweli.

Pili, ZZK keshapoteza imani CDM. Akirudishiwa nyadhaifa zake zote bado atapata ugumu wa kutenda na kukisaidia chama chake. Tuhuma zinazomkabili ambazo ni malimbikizo ya muda ni nyingi na nzito, huo ndio ukweli

Kwamb, unahitajika ushahidi wa wazi kumtia hatiani, tumelieleza vema kwa uzi wa Mwanakijiji.
Ni kwamba ZZK amehusika na njama lakini siku zote huwa nyuma na kutanguliza wenzake.
Kama ingekuwa ni 'madawa' basi tungesema ZZK ndio wale malodi na wengine ni punda wa kubeba mzigo.

Hata hivyo fikiria kuwa masalia walimtaja kwa ufadhili, sehemu alizofadhili, email na ID feki, sijui unahitaji ushahidi gani.

Kitila amesema ZZK ndiye aliyelengwa, sijui unahitaji ushahidi gani.
Mawasiliano kati ya ZZK na Chadema mpya yamenaswa, ZZK hajakanusha sijui unahitaji ushahidi gani.

Nikudokezee kidogo kuwa nikisema ZZK amekula rushwa utanitaka ushahidi.
Ukweli ni kuwa sina ushahidi wa ZZK kula rushwa.

Ushahidi nilio nao ni ule wa ZZK kuwashambulia Barrick Gold kwa mambo ya mirahaba n.k.
Baada ya muda Barrick wakaenda jimboni kwa ZZK( Sina ushahidi kama walialikwa,waliombwa au walikwenda wenyewe). Ninachojua walitoa Milioni 10 kwa halmashauri ambayo ZZK ni mjumbe wake.
Pesa hizo zikaenda kujenga na kukarabati shule katika jimbo la uchaguzi la ZZK.

Katika mazingira ya kawaida ZZK alitakiwa ku declare conflict of interest, ima kutohudhuria vikao vyote vya halamashauri au ku-divert hizo pesa kwenda halmashauri nyingine asiyoingia kama mbunge, na muhimu sana kukataa mchango wa Barrick. ZZK akakaa kimya hadi wajanja wakaliona hilo.

Obvious ZZK hakukuchukua rushwa kwasababu hakuna ushahidi wa yeye kupokea rushwa, technically amekula Mlungula kwa mlango wa nyuma, sijui kama kuna kosa nikisema amekula rushwa, wengine watasema hakuna ushahidi.
 
Mkuu Mkandara
Nina bandiko la siku nyingi niliweka na kusema wakati CCM inapita kipindi kigumu CDM isibweteke na kudhani CCM ni nyani. Niliwaonya kuwa japo anaonekana kama nyani huyo ni simba aliyemyeshewa mvua, makali yapo pale pale.

Katika uzi huu tulijadili kuhusu mkono wa CCM katika mzozo huu. Hata hivyo nilisema kuwa chanzo cha tatizo ni CDM wenyewe siyo CCM.

CCM ni opportunists waliokuwa wanasubiri wakati muafaka waingie kiulaini na kuleta uharibifu. Aliyeaandaa mazingira hayo ni mgogoro ambao watu wachache wameamua kuivuruga CDM.Kwamba mkono wa CCM upo hilo halina shaka.

Utashangaa CCM wapo mstari wa mbele kabisa kumtetea ZZK, hivi lini CCM wanaosali kila siku upinzani ufe wamekuwa wazuri sana kiasi cha kusimamia 'demokrasia' ndani ya upinzani.

Hivi ilikuwaje wao wasione tatizo kumfukuza Mansour Himid waone tatizo la CDM.
Demokrasia gani wanasimamia hawa watu!!

Kuna minong'ono (isiyo rasmi) mitaani kuwa katika kesi ya CDM vs CDM makada maarufu wa CCM walikuwa karibu mahakama kuu kufuatilia timbwili hilo.

Kwa kweli nawapongeza CCM kwa uchungu wa demokrasia! wamefikia mahali hawataki kabisa upinzani usambaritike, wamebadilika kabisa! CDM wajiulize huyu ni kondooo aua mwana kondoo?

Hili la Mkono, ni zito na kama ulivyojionyesha ZZK anajichanganya, Mkono anajichanganya.
Ni kama bomu limedondoshwa watu wanataharuki.

Sijui Mbunge ambaye gari ni la mkopo wa kodi tena likiwa halikulipiwa kodi anawezaje kuliuza kwa mwenzake, sijui.
Sifahamu ZZK aliyekataa posho huku kukiwa na makando kando inakuwaje, kwakweli sijui.

Kwamba CCM wanachochea mafuta hilo halina shaka kabisa.
Lakini wanachokifanya ni sawa sawa maana ndio kazi yao kuhakikisha wanaua upinzani ili waendelee na yao kama zamani.

Tatizo lipo CDM ambao badala ya kumaliza matatizo kama chama kilichokomaa imekuwa mwaga mwaga magazetini. Najiuliza hivi hawa kweli wana utayari wowote kwa hali ilivyo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu@Nguruvi3 nimeona umeshauri CDM ichukue hatua za haraka na dharura,lakini ujasema hatua gani?ili kumaliza mgogoro au kufifisha mgogoro!kama kikao cha dharura kimetufikisha hapa?Je wewe ndo ungekuwa Kamati Kuu ungefanya Uamuzi gani ili kuhiuwisha CDM?
Adharusi Nilishaeleza wapi kamati kuu ilikosea na nilishaeleza makosa ya viongozi kwenda mikoani na kuacha tatizo makao makuu.

Ninaposema wamalize mgogoro haraka nina maana kadri wanavyouacha kama walivyofanya uharibifu ni mkubwa mno.
Wanapaswa wamalize tatizo kwa namna yoyote wanayoona inafaa. Hoja ni kuwa tatizo lifike mwisho.

Kuna namna nyingi, na moja ni baraza la wadhamini la CDM wakae na kuangalia namna ya kumaliza mgogoro.
Sijui kama umenielewa au nahitaji kutoa ufafanuzi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara

Ni kweli kabisa mgogoro huu unachukua sura isiyopendeza hata kidogo,

Kinachoniogopesha zaidi ni hili sakata la kutekwa na kuumizwa vibaya kwa mwenyekiti wa CDM Temeke ambako sasa kunahusishwa na mgogoro unaoendelea kati ya ZZK na uongozi wa CDM. Tayari watu wameanza kufananisha yanayomtokea ZZK na yaliyomkuta marehemu Wangwe...(Hata ZZK mwenyewe anasema haya).
Mwalimu, ZZK atatumia kila mbinu kuhakikisha analinda masilahi yake. La kusema kama atafanywa kama Wangwe ni kutafuta sympathy tu. Yeye kama anaona hatari kwanini asikubaliane na maamuuzi akaondoka kwa salama?

ZZK anacheza karata nyingi na chafu zikiwemo za Udini, Ukanda na Ukabila.
This guy ni hatari sana na anaweza kufanya lolote.
Najua zidane yupo njiani akitaka ushahidi, well, kuna mamabo mengi ndugu yangu.

Kuhusu kupigwa kwa mwenyekiti, not once not twice imetokea ndio maana tuliwaonya CDM kuwa lazima chama kiwe na nidhamu.

Hakuna mafanikio bila nidhamu. Sioni cha ajabu Temeke kwasababu imashatokea sana na viongozi hawaonekani kushtushwa na hali hiyo.

Nisichokubali ni ZZK 'kutumia' matukio kujenga uhalali wake ndani ya chama.
He must come out clean. Anatakiwa aeleze tuhuma zinazomhusu.

Alishawahi kudai kuwekewa sumu sembuse hili, ni master wa spinning ndio maana tunasema he is a problem to begin with. Nasema tena ZZK ana tatizo katika busara na hekima.
 
Nguruvi3,
Mkuu wangu nimekupata isipokuwa wana CDM bado kabisa hawataki kukubali ukweli kwamba ni wao wanatakiwa kuamka toka usingizini. Hili sakata la ZZK toka mwanzo mimi naamini kabisa kwamba CCM ina mkono ndani byake na sii rahisi kuwalaumu CDM isipokuwa inashangaza kwamba hata wao wanashindwa kutoa tongo na kufikiri ama kuamini CCM ina mkono ndani vadala yake kwa asili ya mtu mweusi tunatafuta mchawi.

Hadi sasa hivi mchawi alokwisha patikana ni ZZK na hata aje na ushahdi wa aina gani, hataaminika maana mchawi huwa haachi ushahidi ila maafa na manyanga yake huyafanya usiku wakati watu wamelala hivyo ni dhan tu hutumika kumuumbua mchawi. Kwa kweli tumefikia mahala hata Busara zetu zinaonekana ujinga mtupu maana tunafuata imani za kichawi.

Kisha huwezi kusema chanzo cha tatizo ni CDM wenyewe sio CCM. Hapo sikubaliani nawe kutokana na mtazamo wangu kwamba siku zote demand iliyopo ndio husukuma supply na hupanga bei ya kitu kinachotakiwa. Leo hii ni rahisi kuwasema vijana wetu wanaouza Unga huko China na Ulaya lakini ukweli ni kwamba pasipo kuwepo kwa soko la unga huko China na Ulaya basi hawa vijana wasingebeba unga. Huo ndio ukweli japo siku zote waadhibiwa ni wabebaji sio wanunuzi wenye mirija hadi ktk utawala. Na ili kukomesha biashara ya Unga, ukweli ni kwamba inahitajika zaidi kuweka nguvu kubwa kuwasaka wanunuzi na kuwatia ndani, maana ukiondoa soko, mali haitakuwa na mnunuzi, mchezo umekwisha.

CCM ndio walojengea hii imani ya kwamba ZZK ni pandikizi wa CCM na yupo pale kukusanya siri na CDM na kuwahakikishia ushindi CCM. Binafsi siamini hili hata chembe, maana hata ukichukulia swala dogo sana la Kafulila, ni ZZK pekee alopinga kumnyang'anya uanachama kwa maana ya kwamba tutapoteza jimbo lake. Sisi hatukujali matokeo ya ushindi wala hatukujipanga kuhakikisha jimbo la Kafulila tunalichukua baada ya kumfukuza. Na tuliposhindwa ktk uchaguzi mkuu, tukamtupia lawama hizo ZZK maana ndiye mchawi wetu lakini ukweli unabakia makosa yalikuwa yetu hatukujiandaa kulichukua jimbo wakati tunaelewa ZZK hakukubaliana na maamuzi yetu. Na sasa imefikia hadi kumlaumu kwa jimbo la Musoma Mjini, tunazidi kuumbuana wenyewe..kama vile ZZK ndiye huchagua wagombea wa Chadema, mtu ambaye tuna mashaka naye toka 2009. Inaingia akilini kweli? pengine am too smart for this bullshit inayoendelea.

Binafsi yangu, hizi dhana za wana Chadema na hasa pale wanapofikia kusema sisi wote tulosimama kumtetea Zitto ni mapandikizi wa CCM, hapo ndipo naamini kabisa kwamba huu ni mchezo ulopangwa makusudi pasipo ukweli wowote maana binafsi yangu najijua sii pandikizi, sijawahi na wala sina mahusiano na ZZK nje ya CDM. Na najua hata nikijitetea vipi sintoaminiwa, nimesha wekewa lebel ya upandikizi au nalipwa na ZZK kumtetea, sawa kabisa na tuhuma za ZZK ambaye kila mtu anaamini kuwa ni pandikizi la CCM pasipo kuwa na ushahidi wowote. Sasa kama inaaminika sisi ni mapandikizi kwa dhana zenu, mnaweza kweli kuniaminisha vipi mimi kuwa ZZK ni pandikizi ikiwa najua imani zenu zinasukumwa na dhana.

Dhana hii ni potovu na imetengenezwa na watu makusudi kutuvuruga CDM na hapana weak link isipokuwa kupitia kwa ZZK ambaye kisiasa bado hajaiva na mwepesi kuropoka asipopaswa. CCM wanazijua wekness za ZZK na weakness za CDM pia na wameliona hilo mapema wakati akiwakilisha hoja zake Bungeni kama hoja binafsi na sii za chama, hivyo CCM wakajua hapa tunaweza kabisa kufanya ya Myahudi. Yaani Wayahudi walipogundua kwamba madhehebu ya kiislaam ya Sunni na Shia hua picha haziivi, wakatumia mwanya huo kuwachonganisha, leo hii waarabu ama nisema waislaam wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa jina la Mola wao, sijui nani dua zake zinapokelewa kama sii Ujinga! .

Pamoja na makosa yote ya ZZK ambayo nimewahi kumpa usia wangu hapa hapa JF, bado CDM ilitakiwa kufuata taratibu zake ktk kumvua uongozi na kupa nafasi ya kujitetea iwe kupitia rufaa ama ktk kikao. Wangemsimamisha nafasi yake ya uongozi, kisha wakampa barua ya hukumu ilofikiwa ili kumwezesha kupinga hukumu hiyo kwa kukata rufaa baraka kuu kama akitaka. Ni baraza kuu ndilo mwakilishi na sauti ya wanachama wote nchini. Hivyo kuogopa kumpa nafasi ZZK kuipeleka kesi hii baraza kuu badala yake tunasikia mzee wetu Mtei akisema kwamba hukumu ya kamati kuu ndio ya mwisho - Zitto hatakiwi Chadema! inaongeza maswali mwngi badala ya majibu. Tunaogopa kipi kuhakikisha sheria inafuatwa ikiwa ZZK anataka hukumu yake ijadiliwe na baraza kuu? au ndio runahofia yale ya Lowassa na magamba waloshindikana?

Je, kuna uwezekano kwamba ZZK tayari ana nguvu kubwa baraza kuu kama Lowassa huko CCM na wale magamba walotaka kuvuliwa uanachama?. Ikiwa ndivyo, basi ndio kusema kuna hesabu kubwa ya wajumbe walotakiwa kufukuzwa uanachama zaidi ya hawa wallotajwa. Na ikiwa kamati kuu ya CDM ina hakika ZZK hawezi kushinda rufaa yake kwa nini wanagoma kumpa hukumu yake ktk maandishi ili apate kukata rufaa kama anavyodai? hapa nachelea kusema inaonekana kuna wasiwasi mkubwa makao makuu kiasi kwamba wamekiuka wenyewe sheria kwa sababu siwezi kuamini kiongozi kama Tundu Lissu mwanashieria hakuliona hili ama hata hili la mahakamani kuwa ZZK atashinda hatua ya kwanza.

Na umezungumzia ZZK kutumia matukio kujenga uhalali wake ktk chama. Mkuu wangu ZZK akikubali hukumu na kujivua uanachama atakuwa amefanikisha lipi?. Huyu ni sawa na mgonjwa aliyeko ktk life support, ni kama Mandela ambaye kupigania uhai wake ni haki kwake maana kifo ni lazima isipokuwa lini na wakati gani. Kwa hiyo kina Mzee Mwanakijiji wanaposema ZZK akubali kujivua unachama mwenyewe sijui wanafikiri nini maana haitamsaidia lolote angejivua. Hivi mnafikiri ZZK angejivua uanachama ndio angeilinda hadhi yake ama angekuwa marehemu tayari kisiasa! Sasa kwa nini sisi tunataka ZZK ajivue mwenyewe life support badala ya kupigania uhai wake na anapopigania uhai wake linakuwa kosa jingine..Siwaelewi kabisa!

A true CDM supporter lazima apiganie haki yake hadi mwisho, isipokuwa yule pandikizi ndiye angeachia na kukubali matokeo maana kisha umbuliwa. Tuliwaona kina Kabourou na wengine walokimbia CCM bila kuaga wala kukata rufaa na tukasema kweli walikuwa mapandiki leo mtu anapigania uhai wake bado watu hamtaki!.. what else mnachotaka ZZK afanye ili awahakikishe ni mwana CDM wala sii pandikizi.

Nitamalizia kwa kusema mimi binafsi sioni sababu ya kumuogopa ZZK kiasi hiki, iwe alitaka kupindua ama kujiandaa ktk uchaguzi ujao maadam alisha gundulika kabla ya uchaguzi, wangeendelea na uchunguzi wakalipata kundi zima kisha mnawaumbua siku ya uchaguzi lkama alivyofanyiwa Mzee Malecela.

Leo hii ukivamia nyumba yangu ukakuta nyaraka zinazomhusisha tuseme Mwalimu ama Adharusi na ujangili, utaratibu wa kiintelejensia huwezi kunikamata miye kama khusika bali unazifanyia utafiti hizo nyaraka kama zina ukweli wa hao walengwa na sii kunikamata mimi, mke wangu na watoto kwa sababu tu huamini kwamba Mwalimu ama Adharusi wanaweza kuwa majangili. Unachotakiwa kufanya ni kuchunguza miaya yote ilojadiliwa ktk Ujangili na sii mpango wangu wa kuwanasa hawa majangili kwani Ufisadi ndani ya Chadema ni haramu ya kwanza ktk sera zetu na hivyo madai ya kina Kitila yaliytakiwa kuchunguzwa kwanza kabla hawajahukumiwa wao kwa utunzi wa mpango wowote ule.

Na haiwezekani kabisa kesi hiyo apelekewe mwalimu na Adharusi waisikilize kisha watoe hukumu sio ya tuhuma hiz bali mpango wa wao kukamatwa. Mashtaka 11 sote tumeyasoma, na yote yanahusu uongozi wa juu ambao hadi leo hii tunavyozungumza hapa hatujapatiwa majibu kupingana na madai ya huo waraka ulowatia fdoa viongozi wetu. Sasa tunapomfukuza ZZK tutakuwa tumetatua hilo tatizo la uongozi ktk maswala yaloainishwa? Hapana! Ila ukweli ni kwamba tutakuwa tumeondoa udadisi wa wajumbe na viongozi wengine na pengine kuonyesha mfano kwa wanaChadema wote ya kwamba msitake kujua yanayofanyika makao makuu, mkiingiza mguu pale yatawakuta yalomkuta ZZK.

Hii kusema kweli sikubaliani nayo, Linalofanyika makao makuu lazima lifiuate misingi ya Uongozi maana CDM sio chama cha Mzee Mtei, Mbowe, Slaa wala ZZK. hawa wote wanawajibika kwa wananchi na hivyo kaa hakuna baya lilotendeka kesi hii ipelekwe bazaza kuu japo binafsi dikupenda kabisa swala hili lifikie huko maana nazijua siasa Za Bongo. Kila miiongozi amna madudu yake na tusipende kabisa kuyapa nafasi yatoke nje, tutaumbuana. CCM walijua hayo na ndio maana Lowassa hakufukuzwa na sii kwa sababu ya Uhodari wake bali kama alivyosema - KUKINSURU CHAMA na leo hii CCM wanapeta. Kama wangetumia jeuri ya kumfukuza Lowassa basi nina hakika CCM hii ilikuwa inakufa!..

CCM watendelea kumtetea ZZK kwa sababu ndivyo ushabiki wa kisiasa ama Uadui hufanya kazi. Sisi wenyewe tulikuwa tukimshabikia Lowassa humu, tukisema CCM haiwezi, waseme kafisadi nini na kadhalika ili mradi kuwatia moto CCM wamfukuze Lowassa, lakini wao wakatumia busara zaidi hawakumeza mkenge huo. Sisi kwa upande wetu yametukuta badala ya kutumia akili, tumefukanya kama mifisi na sasa tunaanza kuaibishana. Hili hamkuliona bali mimi nililiona mapema na ndio maana ninaendela kusema swala la ZZK ni swala la CDM linaweza kabisa kumalizwa ndani ya vikao vya chama na sio magazetini. Tunaogopa nini baraza kuu kupokea mashataka, kusikiliza utetezi wa ZZK na hata hao kina Kitila hadi tuchukue njia za mkato?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom