Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #221
UTETEZI LAINI USIO NA MASHIKO WA DR KITILA MKUMBO
Hbari ifuatayo ni kwa hisani ya gazeti la Raia Mwema.
1. Imelenga kupotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mgogoro
2. Kwa kiasi fulani umeonekana kujibu au kujadili hoja za wana duru kwa njia ya kiufundi.
Nimezigawa hoja katika namba ili ziweze kusomeka na kuangaliwa kwa macho mawili.
UPOTOSHAJI
1. Dr Kitila hakueleza chanzo cha mgogoro. Alichokieleza ni watu kuumbuliwa kama wasaliti na wahaini wanapopingana na uongozi(point#5).
Kitila anafahamu kuwa yeye na wenzake hawakuongoza jitihada za kupinga uongozi, walichokifanya ni jitihada za kuleta mtafaruku.
Kwanza, kutumia waraka ambao kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa inatoa hoja za waraka kwa vipengele(Rejea bandiko#92 kwa mfano).
Kitila anapingana na hoja yake#10 kwamba migogoro ya kisiasa hutatuliwa kwa mazungumzo. Kitila na wenzake hawakutumia mazungumzo,walitumia waraka.
Lakini pia anapingana na hoja yake#15 ya viongozi kuyamaliza na kuitisha uchaguzi.
Kitila hakutumia njia hizo alichokifanya ni kujificha na kuandika waraka ambao amekiri kushiriki.
2. Hoja#8, Kitila amepotosha kusema Mbeki aliondolewa na Zuma katika uchaguzi.
Ukweli ni kuwa Mbeki aliondolewa na kamati kuu ya ANC miezi 8 kabla ya uchaguzi.
Aliyekaimu nafasi hiyo ni K.Motlanthe.
Hoja ya Urais wa A.kusini ulitoka kwa Mbeki na kwenda kwa Zuma kwa njia ya kura ni upotoshaji
Hata hivyo, Kitila atambue kuwa kamati kuu ya ANC ilichukua hatua baada ya kubaini Zuma hakuwa na makosa mbele ya mahakama.
Ni uamuzi kama huo ambao kamati kuu ya CDM iliutumia katika kuwavua vyeo wahusika ingawa halikuwa suala la mhakamani. Hivyo hapa anajichanganya kwa kulaani maamuzi ya CC ya CDM na kuunga mkono maamuzi ya CC ya ANC.
3. Hoja#14, Kitila anaueleza umma kuwa sababu viongozi kuondolewa wadhifa ni za utatanishi. Hakuna utatanishi katika waraka aliokiri ameuandika na ambao ulishaanza kufanyiwa kazi.
4.Hoja#10, Kitila anasema njia ya kutatua migogoro ni kuhakikisha haisababishi madhara kwa taasisi. Ukweli kuwa waraka haikuwa njia nzuri na mgogoro uliopo ni matokeo tu.
Laiti angekuwa ana 'walk the talk' asingeandika kitu kinachosababisha mgogoro na kuzorotesha upinzani.Kitila na wenza hawakutimiza hoja# 9 inayowataka kutatua migogoro kwa kukaa pamoja.
5. Katika hoja#1 na 2, Kitila amemtaja kiongozi wa upinzani kushindwa kushughulikia suala la mawaziri na amesema hiyo ilikuwa fursa ya kuimaliza CCM kwasababu samaki huoza kuanzia kichwani. Amesahau aliyekuwa naibu kiongozi wa upinzani alianzisha tuhuma ambazo CCM wangekuwa makini tuhuma huenda zingeimaliza CDM, Kitila anahubiri kitu ambacho anafahamu kingiemaliza CDM lakini akitaka kiimalize CCM. Double standards.
Mkumbo aelewe kuwa kiongozi wa upinzani ni mtu lakini upinzani ni kundi ambalo washirika wake wamo. Ingelikuwa busara angetumia neno upinzani bila kumtaja kiongozi, tunajua ni Mbowe.
Kwa hili ameonyesha sentiment zaidi ya kujenga hoja kama alivyoonyesha katika waraka na kama alivyoonyesha katika hoja#10.
6, Hoja#14, si kweli kuwa vyama vya siasa vinajengwa na wafuasi.
Ukweli ni kuwa wafuasi wanajenga chama kwa kuamini katika sera za chama na misimamo yake.
Chama kinachojengwa na mtu ni genge la watu na si chama au taasisi.
Hoja ya kusema mbunge mwenye wafuasi akifukuzwa chama kitakufa au kutetereka ina mashiko tu kwa chama kinachoamini katika personality na si policy.
Sijui CDM ambayo yeye alikuwa mshauri kinaamini katika nini.
7. Hoja#13, Kitila anasema wanachama wanaodhani kufukuza watu wanakosa mantiki, nadhani Kitila anakosa mantiki kabla yao.
Mifano ipo hai, TANU iliwahi kugawanyika na kuundwa kwa AMNUT na UTP.
ANC imegawanyika makundi mawili, lile lililounda chama kumuunga mkono Mbeki na lile la Malema.Huko nyuma ANC iliwahi kuvunjika na kuunda PAC.
Rainbow alliance ilivunjika na kuunda ODM na Jubilee.
Mifano hiyo inaonyesha kuwa kama lipo kundi lisiloridhika na mambo na jitihada za kurekebisha zimeshindika ipo plan B ambayo ni kujitenga na kuondoka na wafuasi kwa kuanzisha chama kingine. Mrema aliawahi kufanya hivyo bila kuathiri taasisi nyingine
Nadhani hiyo suluhu ingeweza kutumiwa na akina Mkumbo na washirika wake badala ya kujificha na kuandika waraka wa uchochezi.Makundi niliyoyataja yalifanya mambo yao hadharani na si chini ya kapeti kama ilivyokuwa kwa Kitila and associates.
Nyerere, Mandela, Clinton, Blair, Washington, Gandhi n.k. walikuwepo na wameondoka na vyama vyao bado vipo.
Mrema aliondoka na wafuasi na CCM ipo, Lamwai aliondoka na wafuasi na NCCR ipo, Mapalala alindoka na wafuasi na CUF ipo n.k.
Sidhani katika siasa za kileo chama kinajengwa kwa jina. Kama ni hivyo Kitila anavyodai hakuna sababu za CDM kunadi sera, kianchotakiwa ni kunadi sura ya mtu.
Siasa za kileo hazikubaliani na hilo.
MAONI
Ukisoma makala ya Dr Kitila ni dhahiri bado anaamini kuwa alichotaka kukifanya kwa kuandika waraka kilikuwa sahihi.
Kitila anaweza kuamini hivyo na wala si kosa, lakini kiongozi kama yeye anapojitokeza na kuomba radhi halafu kurudi magazetini kuandika kile kile alichokiombea radhi inatia shaka na kusikitisha.
Kitila na wenzake hawakutumia njia za kidemokrasia katika kupingana ndani ya chama chao. Walichokifanya ilikuwa ni uchochezi kwa kutumia mitandao ya jamii.
Hili ndilo kitila analosema ni demokrasia na lazima vyama vivumilie.
Zuma hakuandika waraka wa siri alipambana kwa uwazi.
Kitila na timu yake hawana historia ya kujitokeza na kupambana wazi katika misingi ya demokrasia, leo anapata wapi ushujaa wa kuhubiri demokrasia ambayo hakuwahi kuifanya?
Kitila anasema ni vema mgogoro ukamilizwa kwa njia ya uchaguzi.
Hilo ndilo alipaswa kusema hata kabla ya kuandika waraka.
Alichokifanya ni kaundika waraka ili kuchochea uchaguzi na si kudai uchaguzi.
Ni makosa kudhani kuwa demokrasia inaruhusu uchochezi na si taratibu, hiyo si demokrasia ni vurugu.
Endapo anadhani wanachama wana haki ya kumaliza mgogoro kwa uchaguzi, Kitila ana halalisha maasi ndani ya chama kama sehemu ya demokrasia.
Leo Zitto anaweza kuwa kiongozi wa CDM, anachosema Kitila ni kuwa atokee mwanachama na kuleta vurugu ili suluhu iwe uchaguzi.
Chama hicho sijui ni cha kisiasa au ni Simba na Yanga.
Sidhani CDM wamefika huko na kama huo ndio ushauri basi lipo tatizo kubwa zaidi.
Tena anasisitiza kuwa kuandika waraka na kutuma katika mitandao ili uchaguzi ufanyike ni njia ya kiistaarabu ya kumaliza mgogoro.
Dr amesahau kuwa waraka haukuwa njia ya kistaarabu na ndio chanzo cha kufumua timbwili la sasa na kwamba vurugu zilianza siku nyingi tangu alipomtetea Juliana kwa hoja 'aachwe abalehe'.
Hivi vurugu zinakuwaje sehemu ya demokrasia? Mimi nilidhani demokrasia ndio sehemu ya suluhisho la vurugu, inaonekana bado nahhitaji kusoma maana ya demokrasia zaidi, nitafanya hivyo na namshukuru Dr Kitila kwa kunisukuma nirudi maktaba.
Hadi hapo nitakapokubaliana naye, kwasasa nabaki kusema kuwa anachokifanya ni kuendeleza mgogoro, kumtetea mshirika wake asifukuzwe.
Kufukuzwa au kutofukuzwa hilo ni suala la wanachama wa CDM lakini muhimu ni Kitila kutambua kuwa CDM ijengwe kama taasisi na si mtu.
Mandela alisema watu na viongozi wapo na wanapita, taasisi ipo siku zote.
Hii dhana ya kuwa fulani amefanya kazi sana na anawafuasi ni dhana hafifu.
Umaarufu utumike kujenga chama na si kubomoa chama.
Kwa andiko la Kitila nadhani anchochea kuni badala ya kutia maji.
Tusemezane.

NCHI yetu ipo katika mhemko wa kisiasa. Kwa vijana na tabaka la wananchi wa kawaida, ambao hawana maslahi ya moja kwa moja na mfumo wa sasa wa utawala, mhemko huu unawasukuma kukichukia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupenda upinzani. Na kwa mazingira ya sasa ya kisiasa wanalazimika kuipenda CHADEMA.
Ndugu wanajamvi, nimeona ni vema kujadili mada hii ya kwasababu kuu mbili.
Wananchi hawa wana haki na wajibu wa kuichukia CCM kwa sababu serikali yake imewaangusha. Na hili la serikali ya CCM kuwaangusha wananchi wake sio suala la mjadala tena kwa sababu hata Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahama Kinana, amekiri hivyo waziwazi katika mikutano ya hadhara.
Kimsingi, Kinana kwa siku za hivi karibuni amekuwa akifanya kazi za upinzani sijui ni kwa sababu ya kuchoka kuwa chama tawala au kwa kuona kwamba upinzani wameshindwa kuibana serikali sawa sawa kama inavyopaswa.
Pengine kitendo cha wabunge wa upinzani kuidandia na kuunga mkono hoja ya mawaziri mizigo kama ilivyo ni kielelezo kingine kwamba upinzani bado hawataki kutenda zaidi ya upinzani.
1. Katika hali ya kawaida, ambapo upinzani ni imara na upo tayari kuchukua nafasi ya serikali wakati wowote, ilitarajiwa kwamba Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na wabunge wake wangeenda zaidi ya kuwashughulikia mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo na hao waliokutwa na hatia na Kamati ya akina Lembeli.
2.Wangekuwa makini vya kutosha hii ilikuwa ni fursa adimu kwa upinzani kusababisha dhahama kubwa zaidi katika utawala wa CCM na hata kusababisha Uchaguzi Mkuu kuitishwa mapema. Samaki huoza kuanzia kichwani.
Haiwezekani uwe na mawaziri mizigo halafu usiwe na serikali mzigo. Wabunge wa upinzani wamejikuta wanacheza ngoma ya CCM na wamewasaidia sana kujipanga kwa ajili ya chaguzi zijazo na hoja yao kwamba ni chama kinachosikiliza (chama sikivu) imeimarika zaidi.
Tutajadili zaidi jambo hili katika siku zijazo. Kwa sasa acha niendelee na mada yangu ya leo.
Kwa kuwa watu wengi wanaotaka mabadiliko katika mfumo wa utawala wameweka tumaini lao kwa CHADEMA, hawataki chama hiki kiguswe. Wanataka kitulie tuli hadi 2015. Wanataka chama hiki kilelewe kama yai.
3.Kisingizio cha wengi ni kwamba hawataki yatokee yaliyokikumba NCCR Mageuzi miaka ya tisini.
Viongozi wa CHADEMA wanajua sununu iliyomo miongoni mwa wanachama na washabiki wa CHADEMA. Nao bila ajizi wameitumia sununu hii kama fursa ya kisiasa ndani ya chama. Hawataki waguswe. Hawataki wakosolewe. Na kikubwa zaidi hawataki wapingwe katika chaguzi za ndani ya chama. Hata wakifanya makosa yatahalalishwa kwa njia mbalimbali.
4.Yeyote anayejaribu kuwagusa na kuwakosoa viongozi na hasa akionyesha kwamba anatamani mabadiliko ndani ya uongozi atadharauliwa na uana-CHADEMA wake utatiliwa shaka.
5.Na katika siku za karibuni mtu yeyote ambaye haonekani kuunga kila la viongozi wa chama ataaibishwa mbele ya jamii kwa kutangazwa kwamba ni msaliti na mhaini.
6.Jambo ambalo litakuwa ni kosa likifanywa na kiongozi A litaonekana ni kosa, lakini jambo hilo hilo likifanywa na kiongozi B halitakuwa kosa. Hiki ndicho Mwalimu Julius Nyerere alikiita katika kitabu chake cha Tujisahihishe kwamba ni fitina na ni unafiki wa kiuongozi.
7. Kwa hiyo tunachojaribu kuambiwa hapa ni kwamba harakati za kidemokrasia ndani ya vyama vya siasa vya upinzani ziahirishwe hadi CCM itakapotoka madarakani. Hata hivyo ukweli wa siasa haupo hivyo.
Katika siasa za vyama vingi ushindani ni jambo lisiloepuka na haliwezi kuwa hisani ya uongozi uliopo madarakani.
Kinachotokea ndani ya CHADEMA sio jambo geni hapa duniani. Nitatoa mfano wa hivi karibuni katika nchi ya Afrika Kusini ambayo demokrasia yao bado ni changa kama ya kwetu. Baada ya Mzee Nelson Mandela kumaliza muda wake mwaka 1999 na kuamua kwamba asingegombea tena nafasi yake katika chama ilichukuliwa na Thabo Mbeki, aliyekuwa Makamu wake wa Rais. Thabo Mbeki ndiye pia akamrithi urais Mzee Mandela.
Kwa kufuata utaratibu na nafasi yake ndani ya ANC, Mbeki alilazimika kumteua Jacob Zuma kuwa Makamu wake wa Rais, pamoja na kwamba yeye mwenyewe asingependa awe. Kwa kuwa Mbeki tangu mwanzo hakumpenda Zuma, walikuwa na msuguano usio kwisha. Hatimaye Rais Mbeki akamchomekea kesi Zuma inayohusu matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa maadili. Hii ikampa fursa Rais Mbeki kumfukuza Jacob Zuma kutoka kwenye nafasi ya umakamu wa Rais.
Wafuasi wa Jacob Zuma wakakasirika na kununa. Kesi ikaendeshwa kwa zaidi ya mwaka na hatimaye Mahakama Kuu ya Afrika Kusini haikumkuta Jacob Zuma na hatia yeyote na ikamwachia huru.
Jacob Zuma hakurudi katika nafasi yake ya umakamu wa Rais. Badala yake aliamua kuusaka urais wa ANC. Vita ilikuwa kubwa na ANC ikagawanyika makundi mawili.
Kundi moja, ambalo wao wanaita ANC rasmi, wakiunga mkono Mbeki katika uchaguzi huo, wakati vijana wa ANC, chama cha wafanyakazi (COSATU) na chama SACP, ambao ni washirika muhimu wa ANC, wakimuunga mkono Jacob Zuma.
8. Uchaguzi ulipofanyika huko Polokwane, Jacob Zuma akaibuka kidedea kwa zaidi ya asilimia 60 na ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa urais wa Thabo Mbeki. Uchaguzi Mkuu ulipofanyika mwaka 2009 Jacob Zumma akakabidhiwa kiti cha urais baada ya ANC kushinda kwa mara nyingine tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1994.
Kwa hiyo mapambano ya kidemokrasia ndani ya vyama hayawezi kuahirishwa na ndio utamaduni wenyewe wa kidemokrasia tuliochagua kuufuata. Katika harakati hizi za kidemokrasia viongozi watapingwa na watapingana.
Wanachama mbalimbali watatamani nafasi za uongozi. Katika michakato ya namna hii migogoro itatokea.
9. Muhimu ni kwamba vyama lazima viwe na njia ya kutatua migogoro ndani ya vyama bila kusababisha madhara kwa vyama husika.
10. Katika hili ni muhimu tukasisitiza kwamba namna moja ya kupima uwezo wa kiuongozi ni uwezo wa kutatua migogoro bila kusababisha madhara kwa taasisi.
Kama kiongozi anatatua mgogoro kwa namna ambayo taasisi inaathirika ujue kiongozi amepungukiwa moja ya sifa ya msingi ya uongozi.
12. Na namna moja ya kuutatua mgogoro uliopo ndani ya CHADEMA bila kuathiri zaidi chama ni kuruhusu demokrasia ifanye kazi yake. Tuwaachie wanachama wawaadhibu hao wanaoitwa wasaliti na wahaini katika uchaguzi huru.
13
Wanachama wa CHADEMA wanaodhani kwamba chama kitakuwa salama kwa kundi moja katika mgogoro kufukuza uanachama kundi jingine wanakosea kimantiki. Ufuasi wa vyama vya siasa kwa kiasi kikubwa hujengwa juu ya ufuasi wa viongozi.
14. Ni umbumbu wa kisiasa kudhani kwamba utamfukuza kiongozi aliye mbunge na mwenye ufuasi, tena katika mazingira ya sababu tatanisha kama yalivyo sasa, na chama kikibaki imara.
Ni tofauti kabisa na kufukuza uanachama watu kama mimi nisiye na mfuasi yeyote kisiasa, lakini sio kwa kiongozi aliyefanya kazi ya siasa maisha yake yote ya ujana na kujijengea ufausi wa kila kundi katika jamii.
Unaweza ukapata sifa za muda mfupi kwamba una uwezo wa kufanya uamuzi mgmu, lakini ni uamuzi usio makini na uliyokosa busara na ndiyo maana unauita mgumu.
15. Ndio maana vyama vingi duniani hutatua aina ya mgogoro unaoikumba CHADEMA kwa viongozi kuzungumza na kuyamaliza au kuitisha uchaguzi ili wanachama waamue kwa nia ya kura.
Hii ndio njia ya kidemokrasia na ya kistaraabu ya kumaliza migogoro ndani ya vyama bila kuathiri taasisi husika.