Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Sijui kama nitakuwa nimelielewa veama swali lako, nitajaribu kufafanua kadri nijuavyo. Insider kama Tuko anaweza ku chip in

Waraka ulikamatwa kutoka katika lap top ya Mwigamba. Mwigamba ndiye mchapaji aliyetajwa kama M3. Ni huyu bwana alikuwa anatumia ID ya mkulima masikini. Nadhani walifuatiliwa kwa ukaribu na mtu wao ambaye alikuwa mshirika wa kundi la waandika waraka. Huyu ndiye alivujisha habari zote kwasababu kukamatwa kwa waraka kulikuwa na precision ya hali ya juu sana.

Kundi. Uwepo wa kundi haujulikani. Kama ulivyosoma waraka ni watu wachache sana waliojua mpango huo.
Kwa bahati mbaya wengi wa vijana waliotumika hawakujua nini kipo nyuma yake. Walipewa maelekezo na ahadi kem kem mambo yakishakamilika. Leo wengi wanatazama nyuma na kuona walivyolishwa hujuma dhidi ya chama chao.

Kwahiyo hili si kundi lenye kadi ni elite wachache sana waliofanya mazingaombwe na kubeba wengi bila kujijua.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa uwepo wa kundi hili haukuanza leo.

Kiongozi wao ni Zitto ambaye ametajwa kuhusika na tuhuma kubwa tatu
1. Wakati wa Kafulika alikuwemo
2. Wakati wa Juliana alikuwepo
3. Masalia M7 alikuwepo.

Baada ya kugundua kuwa kuwatumia vijana kuna madhara kwasababu ya kutokuwa na simile au subra ndipo wakaamua na mwenziwe waanzishe kitu kukiwa na watu wachache kama waraka unavyoonyesha.

Utakumbuka wakati wa sakata la kufukuzwa kwa Juliana, Kitila Mkumbo aliandika makala raia mwema si kulaani uhalifu bali akiwataka viongozi wa CDM wawasamehe 'hawa ni vijana waachwe wabalehe'. Leo tunajua kubalehe ilikuwa kuwalinda kwasababu ni watu wao.

Sijui kama nimeeleweka kutokana na swali lako, kama kuna mapungufu wengine wachangie kwa kadri yao.

Kundi la waandika waraka naomba lijulikane kama 'ZIKI' (Zito & Kitila)

Thanks Nguruv3. You have answered my question. Hawa watu wasipoangalia watakuja kutoana maisha. Haya mambo ya kutumia mbinu za kijasusi kupata information wangewaachia CCM au vyama vya kikomunisti.

To me something is fishy here and both sides are trying to take pre-emptive actions to cover their butts.
 
Wakuu for one second, do you really think ZZK is for real? Does he carry any aspirations of the youth? Nina wasiwasi sana na hilo. I may agree that the guy is a good orator and charismatic,m lakini sioni kama ni honest politician anayeweza kuaminika kuliko wanasiasa wengine.

Kama ni kweli kuwa jamaa anatumika na CCM, kama kweli tuhuma zinazotolewa juu yake ni za kweli, kama ni kweli alikuwa na ambitions za kuwa mwenyekiti wa chama (power maniach) tunatakiwa tujiulize kama kweli huyu jamaa, ndiye sumaku ya vijana kwa Chadema.

Siku zote huwa nasema Chadema inatakiwa kuinvest kwa Zitto kwa ajili ya 2020 au hata 2025, too early for 2015 kwa ZZK Ukiangalia track record ya ZZK kidogo inatia shaka kwa yeye kuwa kiongozi wa juu.
 
Sijui kama nitakuwa nimelielewa veama swali lako, nitajaribu kufafanua kadri nijuavyo. Insider kama Tuko anaweza ku chip in

Mkuu Nguruvi3, mimi sio insider wa CDM kwa namna yeyote ile. Niliwahi tu kidogo kufanya kazi za chama hiki wakati wa uchaguzi 2010, kwenye jimbo langu kumsaidia mikakati mgombea. Natamani siku moja nipate nafasi ya kutembelea ofisi zao (nasikia ziko Ufipa sijui) angalau nishauri mambo mawili matatu...

Kuhusu kunaswa kwa waraka, nadhani hypothesis uliyoeleza inakubalika zaidi. Hata hivyo binafsi naamini kuna picha kubwa zaidi ya hiyo nyuma ya pazia. Kama CCM wanadhani kuwa wana watu wao ndani ya CDM, wasisahahu kuwa CDM wana watu wao pia ndani sa CCM na usalama wa taifa.

Huwa tu najiuliza ni kwa nini Mwigamba aliamua kupost ile 'thread' akiwa ndani ya kikao cha CDM. Ni kwa nini Lema alichelewa kwenye hicho kikao, na ni kwanini alipoingia kwa kuchelewa aliamua kuingia JF na kusoma post ya Mwigamba... Hizi ni zama za digitali...

Kuna karata tatu (actually ni zaidi ya tatu), zinachezwa kwenye siasa za Tz kwa sasa na Zitto ni mmoja wa hizo karata. Binafsi mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wanampa Zitto benefit of doubt na kumtetea kwa muda mrefu, nikiamini kuna siku atabadilika na kucheza game ya CDM style. Lakini naona Zitto alizidi kupata "power" na badala ya kujirudi, amejitahidi kuongeza momentum kwenye hiyo movement yake. Ukweli ni kwamba Zitto alikuwa amejijengea mtandao mkubwa zaidi ya tunavyofikiri. Katika kipindi hiki ambacho CDM mikoani na mawilayani iko mikononi mwa viongozi ambao wana uwezo mdogo saana (huo ndio ukweli), ilikuwa rahisi sana kwa Zitto kupenyeza ushawishi wake. Kinachomponza Zitto naamini ame underestimate sana uwezo wa Mbowe. Hata ukisoma ule waraka wao, wanamdescribe Mbowe kama mtu "local, uneducated, na incapable kitu ambacho wamekosea.

Mbowe alijua sana mbinu na hatua zote za Zitto kujijengea mtandao na huu waraka ni uthibitisha mdogo sana, lakini alipuuzia akaamua kutumia tu 'gia ndogo' kuhakikisha hazifanikiwi na hazikiathiri chama. Ila kwa sasa baada ya kuona Zitto anaongezewa power na wabaya wa CDM, Mbowe ameamua kuweka gia namba moja... and that is it...
 
Thanks Nguruv3. You have answered my question. Hawa watu wasipoangalia watakuja kutoana maisha. Haya mambo ya kutumia mbinu za kijasusi kupata information wangewaachia CCM au vyama vya kikomunisti.

To me something is fishy here and both sides are trying to take pre-emptive actions to cover their butts.

Kwenye siasa huwezi kuepuka ujasusi ndugu yangu, maana hata mkeo anaweza kuwa pandikizi, sembuse wenzako katika chama...
 
Ushahidi wa kimazingira wa maandishi ya waraka unaonyesha wazi mkakati ulishaanza, tumeonyesha hilo.

Sure... Maana usingekuwa umeanza, ingekuwaje waandae mkutano wa waaandishi wa habari kujibu tuhuma pamoja? Zitto asingekuwa anahusika angekuwa anamlaumu Kitila kwa kumuingiza matatizoni, but kwenye ule mkutano akampa Kitila verse, yeye akamalizia na chorus..
 
Kwenye siasa huwezi kuepuka ujasusi ndugu yangu, maana hata mkeo anaweza kuwa pandikizi, sembuse wenzako katika chama...

Kuna ukweli na unachosema. Lakini kuna wakati ni lazima waiachie process waliyoweka wenyewe kufanya kazi. Kama shughuli za uendeshaji wa chama ungekuwa transparent na watu wangekubali katika taratibu za kidemokrasia kuna kushinda na kushindwa haya mambo yasingekuwepo.
 
Mkuu Mchambuzi
Katika bandiko #32 umejasdili scenario 3 ambazo kamati kuu inazo kwa sasa.
Sijaona scenario inayoweza kutumika bila kuacha matatizo.

CDM wamepalilia hali hiyo kwasababu zifuatazo.
1. Double standard:
a)Wamekuwa na double standard kufikia maamuzi. Waliwaacha akina Kafulila wakaondoka wenyewe hata pale walipotakiwa kuwafukuza ili wasiondoke na heshima kama walivyowagomea Kitila na Zitto.

b)Walishindwa kuwafukuza akina Juliana na Mwampamba kupitia kamati kuu.
Walitumia BAVICHA ili kutoa nafasi ya kamati kuu kuwa neutral.
Ukweli ni kuwa waliogopa kuwaudhi akina Zitto na Kitila ambao walishatoa ushauri 'waachwe wabalehe'.

c)Chadema ikawafukuza madiwani wa Arusha kupitia kamati kuu na kamati za mikoa

d)Chadema ikasita kuchukua hatua dhidi ya Shibuda na kumwacha aendelee bila kuwa na mchango wowote.

e)CDM hawakuwahi kumchukulia hatua Zitto za kinidhamu japo onyo alipotajwa bila kuwa kinara wa makundi 3 sasa

Swali linakuja, ni standard gani CDM wataitumia ili kuhakikisha kuwa maamuzi yao hayakinzani na baadhi ya maamuzi ya siku za nyuma?

2.
CDM wamejichanganya kwa kuchukua kesi hii bila kujua ramifications wakiwa washtaki, waendesha mashtaka na mahakimu. Kulikuwa na nafasi ya kutumia chombo 'neutral'

Endapo wangefanya hivyo kazi ya kusimamia mamuzi ingekuwa rahisi, na wangeweza kuepuka lawama zisizo na ulazima ambazo zinaweza kupandikizwa kukidhi haja.

3
kamati kuu haikuwa na muda wa kutafakari tatizo zima kwa ujumla na upana wake.
Kitendo cha kuondoa mtu na kumweka mwingine ni hukumu tayari.
Sijui katika siku 14 ni kukata rufaa au ni kujitetea! Maamuzi ya hasira yanawaweka mahali pagumu kwa sasa.

Wafanye nini?
Wakusanye ushahidi usio na shaka, wasikilize upande wa utetezi kwa umakini na hukumu izingatie facts na si hisia.
Kitengo cha elimu na utafiti ulichosema kinaweza kabisa kusawazisha hali kama kitakuwa na watu makini.
Madiwani walifukuzwa Arusha, na CDM wakshinda viti vile vile walivyokubali kuviachia.

Maana yake ni wananchi wanaelewa wakielezwa, wanakereka na mambo kama ya waraka na wapo tayari kubadilika. Ikibidi kumfukuza mtu kwa vigezo sahihi na vyenye ushahidi let it be.

Kuendelea kulea personality kama walivyofanya huko nyuma hakutatoa matokeo tofauti na haya.Ni kuahirisha tatizo.

NCCR iliwahi kuondokewa na Mrema na kundi zima. Wale waliobaki wameendeleza NCCR na sasa ni bora kuliko TLP. Kwanini CDM waendelee ku entertain personality iliyowatesa, inayowatesa na itakayowatesa?

Sisi wananchi wa kawaida tunauliza, endapo CDM hawawezi kujenga nidhamu ndani ya chama, hawawezi kusimamia haki kwa makundi kwa standard moja na wanaogopa persnality kwasababu ya kura itakuwaje wakipewa nchi?
Je, wataweza kukabiliana na wezi wakiletewa taarifa ya CAG, Uswiss, visiwa vya Jersy au ufisadi wa bandari?
 
Last edited by a moderator:
Sure... Maana usingekuwa umeanza, ingekuwaje waandae mkutano wa waaandishi wa habari kujibu tuhuma pamoja? Zitto asingekuwa anahusika angekuwa anamlaumu Kitila kwa kumuingiza matatizoni, but kwenye ule mkutano akampa Kitila verse, yeye akamalizia na chorus..
Kilichotokea kwa Kitila ulikuwa ni ushahidi usio na shaka na alijua kuwa aatpoteza wadhifa. Alichokifanya ni kuhakikisha kuwa anamuondoa Zitto katika kashfa kwa kusema yeye hahusiki.

Ukisoma waraka, Kitila alishauri 'mtu wao' awe mbali na viongozi wa chama tawala. Sikumbuki siku za karibuni Zitto kuwa na ukaribu uliokuwa umezoeleka na nyakati nyingine ulikuwa uhusiano mzuri tu usio na tatizo.

Waraka umesema ajishughulishe katika operesheni zote. Sina kumbu kumbu baada ya Operesheni Sangara kuhamia mikoa ya nyanda za juu, lini Zitto alishiriki tena operesheni. Ni ajabu siku za karibuni ameibuka kama kiongozi wa kanda na kutembeza mikutano kwa kasi sana.

Ikumbukwe waraka uliponda sana kanda walizounda CDM, sijui ilikuwaje kanda zile zile wasizozitaka ndizo Zitto amekuwa akifanyia kazi. Na waraka umesema CDM inafanya makosa kuandaa mikutano na maandamano, lakini Zitto siku za karibuni ameshiriki vizuri tu.

Lema aliomshambulia Zitto hakukuwa na majibu kama watu walivyotegemea. Waraka unasema wanayemtaka asiwe na hasira na atumie busara na afanye mawasiliano na wazee kabla ya kujibu tuhuma. Zitto hakujibu tuhuma kinyume na ilivyotarajiwa.

Waraka umesema ajifanye kama hatagombea ili kupumbaza wapinzani wao. Baada ya tuhuma za Lema mtandaoni Zitto alisema 'hakuna mgogoro CDM' bali kuna watu kutoka nje wanaka kutumbukiza chuki.

Waraka ukasema mtu wao awe mwiba mkali kwa serikali ndani na nje ya Bunge, na hivyo ndivyo amekuwa mwiba kuhusu masuala kama Uswiss aliyosema yupo tayari kufa akitetea. Kumbuka ni huyu aliyewahi kusema 'hakutabaki hata panya' leo inakuwaje!

Mwisho waraka ukamtaka ajiepushe na majadiliano katika mitandao. Siku hizi ni mtu wa twitts kuepuka malumbano.
 
Mkuu Nguruvi3, mimi sio insider wa CDM kwa namna yeyote ile.
Niliwahi tu kidogo kufanya kazi za chama hiki wakati wa uchaguzi 2010, kwenye jimbo langu kumsaidia mikakati mgombea. Natamani siku moja nipate nafasi ya kutembelea ofisi zao (nasikia ziko Ufipa sijui) angalau nishauri mambo mawili matatu...

Kuhusu kunaswa kwa waraka, nadhani hypothesis uliyoeleza inakubalika zaidi.
Hata hivyo binafsi naamini kuna picha kubwa zaidi ya hiyo nyuma ya pazia.

Kama CCM wanadhani kuwa wana watu wao ndani ya CDM, wasisahahu kuwa CDM wana watu wao pia ndani sa CCM na usalama wa taifa.Huwa tu najiuliza ni kwa nini Mwigamba aliamua kupost ile 'thread' akiwa ndani ya kikao cha CDM.
Ni kwa nini Lema alichelewa kwenye hicho kikao, na ni kwa nini alipoingia kwa kuchelewa aliamua kuingia JF na kusoma post ya Mwigamba... Hizi ni zama za digitali...

Kuna karata tatu (actually ni zaidi ya tatu), zinachezwa kwenye siasa za Tz kwa sasa na Zitto ni mmoja wa hizo karata. Binafsi mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wanampa Zitto benefit of doubt na kumtetea kwa muda mrefu, nikiamini kuna siku atabadilika na kucheza game ya CDM style.

Lakini naona Zitto alizidi kupata "power" na badala ya kujirudi, amejitahidi kuongeza momentum kwenye hiyo movement yake. Ukweli ni kwamba Zitto alikuwa amejijengea mtandao mkubwa zaidi ya tunavyofikiri. Katika kipindi hiki ambacho CDM mikoani na mawilayani iko mikononi mwa viongozi ambao wana uwezo mdogo saana (huo ndio ukweli), ilikuwa rahisi sana kwa Zitto kupenyeza ushawishi wake. Kinachomponza Zitto naamini ame underestimate sana uwezo wa Mbowe. Hata ukisoma ule waraka wao, wanamdescribe Mbowe kama mtu "local, uneducated, na incapable kitu ambacho wamekosea.

Mbowe alijua sana mbinu na hatua zote za Zitto kujijengea mtandao na huu waraka ni uthibitisha mdogo sana, lakini alipuuzia akaamua kutumia tu 'gia ndogo' kuhakikisha hazifanikiwi na hazikiathiri chama. Ila kwa sasa baada ya kuona Zitto anaongezewa power na wabaya wa CDM, Mbowe ameamua kuweka gia namba moja... and that is it...
Tuko ha ha ha, ni kutokana na jinsi unavyonasa habari nikajua ni insider, niwie radhi nimekuelewa.

1. Kuhusu picha kubwa juu ya waraka hilo nakubaliana nalo. Najaribu kufikiri kuwa miezi michache iliyopita CDM walimtaja afisa usalama kwa jina anayehusika kuihujumu. Kilichoshangaza hakukuwa na reaction yoyote kutoka TISS au serikalini.
Maana yake ni kuwa
1. Kulikuwa na ukweli kuhusu hilo, swali ni kuwa CDM waling'amua vipi kama hawana watu wao ?
2. Inawezekana usalama walikaa kimya ili kutoendeleza habari inayoweza kudhuru vyanzo vyao. Ni theory tu.

2.Zitto amecheza na karata za umaarufu sana. Sidhani kama angepewa pass kwa matukio ambayo ametajwa wazi.
Tukio kama la Ben Saanane kujilipua na kumtaja ilishangaza Zitto hamjui! Tukio la Juliana na Kafulila na bado watu wanafikiria umuhimu wake ndani ya chama!!

3. Ni Mbowe aliyefanya recruitment ya Zitto. Ni mtu aliyechukua uongozi kutoka kwa wahafidhina wenyewe.
Ni mtoto wa mjini. Kuna under estimation kubwa sana na hilo lime cost political career ya Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu for one second, do you really think ZZK is for real? Does he carry any aspirations of the youth? Nina wasiwasi sana na hilo. I may agree that the guy is a good orator and charismatic,m lakini sioni kama ni honest politician anayeweza kuaminika kuliko wanasiasa wengine.

Kama ni kweli kuwa jamaa anatumika na CCM, kama kweli tuhuma zinazotolewa juu yake ni za kweli, kama ni kweli alikuwa na ambitions za kuwa mwenyekiti wa chama (power maniach) tunatakiwa tujiulize kama kweli huyu jamaa, ndiye sumaku ya vijana kwa Chadema.

Siku zote huwa nasema Chadema inatakiwa kuinvest kwa Zitto kwa ajili ya 2020 au hata 2025, too early for 2015 kwa ZZK Ukiangalia track record ya ZZK kidogo inatia shaka kwa yeye kuwa kiongozi wa juu.
Tatizo la wanachama, mashabiki na wapenzi wa CDM ni kulewa kilevya kinachoitwa 'loveness''

Utashangaa kusikia matamko kutoka kanda, taasisi yakumuunga mokono Zitto bila uetetezi juu ya tuhuma zake.
Wanajua kuwa mara 3 Zitto amekirudisha chama chao nyuma lakini hawaelewi wala hawasikii, kilevi kimawakolea

Kwa ushahwishi wa kisiasa alio nao hasa kwa makundi uliyosema lilikuwa suala la muda tu angefika pale anapotarajia.
Tatizo la ZZK ni kukosa subra, busara na kudhani ni smart kuliko watu wengine.

Mimi binafsi nili m-doubt sana pale alipochukua hatua hata zinazopingana na wenzake.
Kilichonitoa wasi wasi na huyu kijana ni pale alipokuwa Mwiba mkali kwa Barrick.
Barrick 'wakamfungia' kitita cha milioni 10 kwa kupeleka msaada wa shule jimboni mwake.

ZZK alikana kwanza hakuhusika(kumbu kumbu zipo hapa JF), tukambana hadi alipokubali kuwa zilipitia halmashauri ya wilaya ambayo yeye ni mjumbe pia.

It was obvious alikula mlungula in very smart way.
Ni kama kukataa kuwa kaka/dada yako hajazini lakini umewahi kumuona mtoto wake!
Toka hapo ZZK na Barrick kimya!

ZZK alikwenda kuosha jumba la bilioni 2.5 la gavana tulimsgangaa sana katika mazingira yale.

Historia yake haitoi nafasi kwa kuaminiwa tena! he has lost public trust isipokuwa kwa walevi wa loveness malta.

Ameongoza makundi 3 ya kihaini, huyu ni wa kuaminiwa kweli.
Anahubiri demokrasia wakati anapanga mapinduzi huyo ni wa kumwani kweli.
 
3. Ni Mbowe aliyefanya recruitment ya Zitto. Ni mtu aliyechukua uongozi kutoka kwa wahafidhina wenyewe.
Ni mtoto wa mjini. Kuna under estimation kubwa sana na hilo lime cost political career ya Zitto.

Sisi wananchi wa kawaida tunauliza, endapo CDM hawawezi kujenga nidhamu ndani ya chama, hawawezi kusimamia haki kwa makundi kwa standard moja na wanaogopa persnality kwasababu ya kura itakuwaje wakipewa nchi?
Je, wataweza kukabiliana na wezi wakiletewa taarifa ya CAG, Uswiss, visiwa vya Jersy au ufisadi wa bandari?
Mkuu Nguvuri

Nimekuwa naufwatilia mjadala ambapo umetoa point za msingi sana, isipokuwa na wewe naona umeshaweka maamuzi yako ya kuwa Zitto ni tatizo. Bila ya kutaka kupekuwa upande wa pili wa shillingi na kuutendea haki kwa kina kwenye argument zako kama unavyo tetea maamuzi ya kamati kuu indirectly, thus either kwa makusudi ya kuhitisha hoja ya ukorofi wa Zitto ama kutopendezewa na siasa za Zitto as a person.

Kilichobaki sasa naona kama vile unatafuta namna ya kuhitimisha hoja ya fair justification on the standing accusation bila ya kutaka kuuliza uhalali wa mashataka na mtoa mashtaka, wakati the whole thing is undemocratic, ntarudi kukwambia kwanini wahaini ndani ya CDM ni Dr.Slaa na Mbowe (with neutral arguments) kwa matumizi mabaya ya kamati kuu kutimiza agenda zao na ukandamizaji wao wa demokrasia za ndani ya chama.

Of-course chanzo cha yote ni misingi mibaya ya Taasisi (hapo nakubaliana na wewe kwenye weakness ya taasisi kwa sasa, hila sioni ubovu wake kwa jicho lako, ni sawa na Dr. Kitila na waraka wao wasivyokubaliana na mbinu za sasa na uongozi uliopo).
 
Wakuu for one second, do you really think ZZK is for real? Does he carry any aspirations of the youth? Nina wasiwasi sana na hilo. I may agree that the guy is a good orator and charismatic,m lakini sioni kama ni honest politician anayeweza kuaminika kuliko wanasiasa wengine.

Kama ni kweli kuwa jamaa anatumika na CCM, kama kweli tuhuma zinazotolewa juu yake ni za kweli, kama ni kweli alikuwa na ambitions za kuwa mwenyekiti wa chama (power maniach) tunatakiwa tujiulize kama kweli huyu jamaa, ndiye sumaku ya vijana kwa Chadema.

Siku zote huwa nasema Chadema inatakiwa kuinvest kwa Zitto kwa ajili ya 2020 au hata 2025, too early for 2015 kwa ZZK Ukiangalia track record ya ZZK kidogo inatia shaka kwa yeye kuwa kiongozi wa juu.

Mkuu Bongolander,
Binafsi siamini kama Zitto anatumika directly na CCM kuiangamiza CDM. Wanachofanya CCM wamegundea udhaifu wa Zitto, na WANAUTUMIA kuiangamiza CDM. CCM wanajua kuwa ZZK ni strong na anapenda kuwa kiongozi wa CDM. Lakini wanajua kuwa CDM hawapo tayari kumpa chama kwa sasa. Hivyo huo ukawa uchohcoro wa CCM kumtumia zzk, yaani wamuwezeshe kuzidi kuwa strong na kuutaka uenyekiti, ili mwisho wa siku CDM ipasuke. Umeyasikia sana maneno kama "wameshindwa kushughulikia migogoro ya ndani, wataweza kushughulikia ya taifa"? Hiyo ndiyo principle watakayoitumia kuimaliza CDM pale itakapopasuka...

CCM wamekuwa wazuri sana kwenye dhana ya "wagawe uwatawale"... Ni kutokana na mafanikio waliyoweza kuyapata wakitumia dhana hiyo kule Zanzibar (unguja na pemba), na kwa baadhi ya vyama vya siasa, ndio maana wakanogewa wakaingiza dhana hiyo katika uchaguzi uliopita wakitumia dini. Hawakufanya risk assessment ya kutosha, ndio maana kwa kiasi kikubwa dhana hiyo imeanza kuwatafuna, na kutokana na hilo wameamua kurudisha nguvu zao kwa Lowassa, ili kusawazisha mambo.

Tukiachana na hayo tukarudi CDM, ni kuwa zzk alijua kuwa CCM wanatumia udhaifu wake kuivunja CDM. Zitto angeweza kuwaepuka, lakini kwa miezi kama 10 (baada ya kuvunjwa PM7) zzk amegundua kuwa sio rahisi kupata upenyo CDM kama akiamua kucheza fair play. Ameamua kurudia mbinu zake, akijua kuwa zinawafaidisha CCM, lakini akijiamini kuwa akifanikiwa kupata uenyekiti CDM ataweza ku-fight back na kuirudisha CDM ulingoni. Hata hivyo hypothesis ya CCM ikafanikiwa kuwa there is no way CDM watamruhusu zzk kuingia na hivyo migogoro itaendelea na pengine chama kupasuka. CCM wameshtushwa sana na uamuzi wa CDM kumvua zzk uongozi, na itakuwa pigo kwao kama CDM watamvua zzk uanachama...
 
Tuko;

Kwenye siasa au maisha kitu chepesi zaidi ni kumweka mpinzani wako kwenye kambi ya adui yako. Kwa mfano Oscar Kambona alikuwa ni mkomunisti. Lakini alipokosana na Nyerere, alipewa sifa zote za ubepari. Hivyo yanayotokea CDM ni mambo ya kawaida. Hata ndani ya CUF na NCCR, kila asiyetakiwa anaitwa mtu wa CCM.

Wamekamata na waraka. Kwanini wanachadema wengi wanashindwa kujadili waraka? Wanatumia muda kujadili links zilizokuwepo kati ya Zito na CCM.
 
Binafsi hili kuitendea haki argument yangu juu ya mgogoro wa sasa ndani ya CDM naona ni vyema nikatenganisha kati ya ‘individual goals' within the party and ‘group ambitions/goals' in relation to their long term objectives of both the individual and the political party.

Zitto
Nianze na ZZK ingawa anatimiza criteria za kuwania nafasi za uongozi wa ngazi zote ndani ya chama as a character amekuwa too ambitious for most of us liking including me, especially alipokuwa analazimisha hata suala la uraisi ilihali hana vigezo vyote vya kupewa fursa hiyo kikatiba. Hivyo hata sasa ambitions zake za ndani ya chama kwa kutaka uongozi wakati wengine wanaona muda wake bado kwa sababu wazijuao wao pengine kwa mkakati wasasa zinaweza kuwa kero kwao (binafsi nisichoafiki hapa ni mbinu wanazotumia, kuhakikisha hilo aliwi kwa sasa).

On the other hand ZZK amekuwa honest from the outset of his ambitions ya kuwa hiko siku anataka kukiongoza chama chake na taifa kwa ujumla. He is entitled to that like any other politician meeting the requirements my problem with that is, his timing is not set appropriately. Ingawaje anayo haki ya kujiamulia maamuzi yake mwenyewe.

Sasa basi huwezi kuwa na goals bila ya kuwa na mkakati wa kuzifikia, hivyo ZZK yupo responsible kujiaminisha kwa watu kuhusu utendaji wake na misimamo yake kwenye siasa. Hivyo tunaweza ona ya kuwa ana kiherehere cha kuomba vyama vya siasa kupeleka hesabu zao kumbe ndio njia ya kujionyesha ni kiongozi wa aina gani mbele ya umma wa watanzania. Kwamba yeye ni responsible kwa watu na mwajibikaji kikazi bila ya woga hili kuleta maendeleo na mengineyo kama alivyokomalia suala la hela zilizofichwa nje huku akishirikiana na CCM in a bipartisan spirit, ukwepaji kodi wa mashirika ya kigeni na mengineo.

Utamlaumu vipi hapo katika utekelezaji wakati hata Mwakyembe na Magufuli leo wameanza kuaminiwa na watanzania mpaka kuzungumziwa uraisi ingawa wao wenyewe hawajatoa matamko, yote hayo kwa sababu hizo hizo za uwajibikaji, ingawa maraa kazaa na wao wamekinzana na viongozi wenzao katika kutekeleza majukumu yao.

Pili ZZK si mjinga kukubalika nje na ndani ya nchi ni kitu kimoja hila hili malengo yake yafikie anapotaka particulary kuweza kuwa mgombea wa uraisi lazima ashike hatamu ya juu. Waraka umeonyesha jinsi gani wanavyotaka chama kielekee. Nashanga kwanini umeitwa uhaini wakati that is just normal planning kwa mtu yeyote anaewania kuendesha an organisation, liwe shirika la kutengeneza toys ama chama cha siasa. Lazima mtu ujue hupo wapi, unataka nini na utafikia vipi malengo yako hivyo lazima uandae action plan na kuzielewa challenges za mbeleni na ndio kitu ambacho ule waraka ulicholenga.

Kwenye utangulizi kuonyesha wanaijua CDM wameelezea mwanzo wa taasisi yao, sababu zake, viongozi wao wa mwanzo na kuwashukuru kuwafikisha hapo walipo including huyu wa sasa. Isipokuwa wahusika wanataka kusogea mbele na kwa sasa wanaona uongozi uliopo umefikia kikomo cha mawazo mbadala na uwezo kwenye safari yao ya ukombozi.

Those are the facts that needs to be addressed na kuzijua mbinu za kumpiku mpinzani maana nafasi inayowaniwa ni ya kushindania si ya kupewa, hivyo lazima ujue unaenda kupambana nae vipi sidhani kama huo ni uhaini maana hata ‘Ed Milliband' wa labour alielewa ya kuwa kule juu kaka yake amuwezi ni kwakuwa alikuwa part of the establishment iliyoshindwa na ana aminiwa zaidi, yeye akapanga mkakati wa kutumia electorate ya chini ndani ya labour kujichukulia kura za ushindi. Kwa hivyo ni muhimu kumjua mpinzani wako yukoje na unamshinda vipi aina maana unajenga uhasama kama mnavyotaka kutoa picha, its just the nature of the political business.

Chadema as a weak institution
How does one go about measuring the maturity of an organisation? To me the answer is lies in analyzing their purpose of existence, their strategy and achievements towards their goals.

Sasa basi CDM kama chama cha siasa kipo kwa sababu ya kuwania kutuongoza watanzania, na kina miaka takribani ishirini ya maisha. In other terms ni sawa na muda wa CCM/TANU tokea Uhuru mpaka mwalimu anan'gatuka. Je mpaka sasa kipo imara kama au kimekua kama CCM ilivyofikia wakati mwalimu anatoka madarakani.

Hapa naangalia timu waliyonayo, huwezo wao wa kustahimili vishindo hata kama kweli kuna mapandekizi ndani yao na mwisho as a political ‘brand' mtu yeyote ukimwambia CDM what is the first thing to come to his/her mind mfano: mpinzani wa CCM, wale jamaa wamaandamano, chama cha kina Zitto, Dr Slaa na Mbowe au ni chama kitakacho nitoa A to B realistically kutokana na kuzielewa sera zao na kuwakubali viongozi wao.

Kwakua kina omba ridhaa ya uongozi sidhani kama wengi wanaamini ya kuwa CDM kwa sasa kitatatua matatizo yao na chama kina eleweka hasa ki-mlengo na mkakati wa kutatua matatizo yaliyopo kwa wengi. Isipokuwa labda ni mbadala as mbadala kwa kuwa mpinzani mkuu tu kwa sasa. Alikadhalika kwa wajuvi wa mambo ni magumashi wa longolongo maana CDM amna sera za kweli wala timu imara na misingi yake bado sana kuifikia CCM.

Sababu za kwanini CDM kina mature at small pace lies na uongozi unaopwya wa juu (leadership directions), poor husbandry skills zilizojitokeza, and party priorities in order to mature; those concerns are also shared by their party members including waandishi wa waraka.

Leadership: Kiongozi wa chama licha ya kuwa na washauri wengi yeye ndiye responsible kwa mwelekeo wa chama na kuhakikisha dira linaeleweka, hivyo basi hata washauri wanapotoa mapendekezo ni kutokana na direction mkuu wao anazotarajia zinakinzana na nadharia ya chama hata kwenye sera. Na baadae kutoa top down effect, washauri wameshaona kuwa kiongozi wa sasa amefikia kikomo cha uwezo hili chama kiweze kuonyesha uwezo wa timu kamili iliyopo na hivyo wanapendekeza candidate wanayeona atawasogeza mbele.

Kibaya zaidi kwa sababu ya utambuzi wa weakeness zake mwenyekiti wao na watu wake wa karibu wamejenga a ‘nuclear family' ambapo wao kwa wao kila mtu anajua role yake katika kuulinda uongozi wa sasa na wengine wamekuwa kama extended family bila ya kuelewa nini kinaendelea ndani na matokeo yake kuaribu njia mawasiliano na maelewano, kiasi kwamba watu inabidi watumie media to indirectly voice their concerns juu ya hali ya chama. Huku ni kuwavunja mioyo makamanda wengine wa ndani na kujenga tabaka analo liamini yeye tu.

Ukishaanza hivyo hata wanaharakati wapya wanaoingia tayari wanakuwa hawajui nini hasa cha kufanya baada ya kujiunga maana amna central command of orders and ideologue ya kufuata zaidi ya kujikuta the common goal ni kumshinda CCM, lakini amna mkakati wala mbinu na hilo ndio lililowachosha waliondika waraka.

Huo ni uhaini kwa makamanda wapya ambao baada ya muda wanajikuta inabidi wachague kambi, chagua kambi nyingine na yake na wewe unakuwa mhaini wa chama umetumwa na CCM au kina Zitto kuwahujumu wakati chanzo cha impasse ndani ya chama ni yeye mwenyewe kiongozi mkuu. Na amefanikiwa kuwaweka wengi ndani ya mstari kwa kuhakikisha asilimia kubwa ya watu waliokuwa ndani ya kamati kuu na nafasi zingine muhimu ni wake yeye.

Hivyo wanachama wenye madukuku amna proper grievence policies within za watu kutoa malalamiko na an independent third party to decide. Sana sana wao wanatumia kanuni sijui katiba za chama kuwakomoa wanao lalamikia pembeni na kutumia kamati kuu kuua demokrasia ya ndani kwa namna za kuwafukuza au kuwaweka katika msatari sawa kwa mbinu za ‘restoration justice' either kwa kutaka utubu, uombe mshaha au ufukuzwe kwa kujaribu kupingana nao, hivyo inakuwa tabu kumkosoa mtu kama huyo asiejiamini nani coward in my books.

Poor Husbandry Skills: Hela kwenye vyama vya siasa ndio kila kitu na matumizi yake lazima yajulikane kwa kila mwanachama vinginevyo kutakuwa na mfarakano ndani ya chama especially matumizi yanapokuwa ayalengi kwenye ujenzi wa chama kama wengine wanavyotegemea.

Na ukitaka kuhujumu maendeleo ya chama tumia hela ovyo na hapa ndipo mtaona jinsi gani Mbowe anavyohujumu CDM na watu wake wa karibu kuliko mtu yeyote.Matumizi muhimu ya hela za chama zipo kwenye sehemu tatu.

(i) Kwenye gharama za campaign hapa CDM ndio sehemu pekee unaweza sema inajitutumua, ingawa kuna wengine wamehoji baadhi ya watu kushirikishwa pasipo uhalali kwenye campaign kupitia mgongo wa viongozi wao kiupendeleo kutokana na kwamba kuna uhusiano na posho unaposhiriki (binafsi nimeridhika ni maamuzi yao wenyewe nani aende wapi)

(ii)Kwenye shughuli za chama makao makuu, hapo ndipo utaona jinsi gani mbowe anavyo kididimiza chama kwa makusudi au kuto kujua. Makao makuu ni ndio nguzo ya chama na ambapo hela inatumika sana licha ya mishahara, vitendea kazi na gharama zingine. Makao makuu ndio sehemu ambayo vipanga wa chama wasio taka kukaa mbele walipo.

Kazi yao kubwa ni kuwasaidia viongozi kutunga sera na kuwafanyia research mbali mbali sana zikiwemo za field hili kupata sera mbadala. Bila ya researchers chama kinakuwa ni cha kubahatisha tu kwenye matukio au makadirio ya matumizi hili kuitimisha sera kama watakuwa wamepewa ridhaa ya uongozi. It is where the heart of the party lies. Sasa jiulize ni percentage ngapi ya hela za chama zinaelekezwa huko au ushangai kwanini, hizi ndio sababu hata yeye anachoongea kwenye majukwaa zaidi ya ppl power na kutusi serikali tu amna la ziada.

Ajabu kuna watu ndio wanaona hiyo ni sababu tosha ya mabadiliko.

(iii) Kulipia ofisi zilizo muhimu nje ya makao makuu: ni muhimu sana kuwa na sehemu zilizotapakaa nje ya makao makuu ambazo zipo imara maana hizi ndio nguzo za kujua kero za wananchi na kusajili wanachama si mpaka viongozi wajuu wanapokuja na kuripotiwa local kero za wananchi ndio makao ya chama ijue. Unatakiwa uviimarishe hivi viofisi kama franchise maana ni vyombo vya karibu kuwafikia wananchi na kukurahishia kupata habari local kujua nguvu zako na weakness zako huko.

Kero zinazo orodheshwa humo ndio utumiwa pia makao makuu na vipanga wao kuzitafutia suluhisho la pamoja kisera kukidhi matatizo muhimu ya sehemu mbali yanayo lingana, hivyo ni muhimu kuwe na ‘wherewithal' iliyopo kwa ajili hawa watu kuwepo na kufanya campaign, kutengeneza vipeperushi na things of amassing nature.

Kero zinapotungiwa sera unarudisha kwanza katika hizi ofisi ndogo na wao kutoa mwongozo, mwishowe mnajikuta kuanzia viongozi wa juu mpaka wa ngazi za chini mnaongea kitu kimoja na hivyo ndio party policies zinavyosambazwa na kujenga taasisi ya watu inayolingana kimawazo, hivyo kuifanya kazi ya adui ngumu kuwagawa kwa mbinu chafu maana msimamo na agenda unajulikana kwa wanachama husika na kuna proper channels of liaison.

Sasa wao kila kukicha ofisi ndogo zinafungwa kwa kukosa kulipa kodi, mara sijui wafanyakazi hawana mishahara zaidi ya kujitolea na wameamua mbinu sahihi za ku-recruit ni M4C ikipita na ikitoka basi na ndio chanzo kila kukicha huko chini kunahujumiwa kwa sababu watu hawana majukumu wala hawajui nini kinachoendelea huko juu CCM ikienda unasikia wanachama kadhaa warudisha kadi including local leader. Maana baada ya viongozi kuondoka watu hawajui nini majukumu yao kwa mtaji huo chama akiimariki zaidi ya watu kujifunza makundi yaliyopo na kuchukua upande lakini amna cha kunada kisera.

Priorities za Chama: Kutokana na mwenendo wa kiongozi sio tabu kuona ni nani muhujumu halisi ndani ya chama, mwenyekiti amekuwa akitumia kanuni za chama ambazo anajua atajibanza wapi kuvunja ukuaji wa chama, demokrasia, namna za kusikia mawazo mbadala ambayo kinyume na kile anacho tarajia.

Chama amekigezua uwanja wa majungu vikao ambavyo vyama vya siasa uvitumia kuelezea mafanikio yao na kuwasiliana directly na wanachama wenzao ambao wako nao mbali kwa muda mwingi, kuwasikiliza concerns zao, kuwapa majibu, kuongeza morale za wanachama: yeye amekuwa akivitumia vikao kuanzisha majungu na kuwachongea viongozi wenzake na kuzua mfarakano.

Kinyume kabisa na chama ambacho kinataka kuwa imara kama viongozi wenzake walivyoona kiongozi wao wa sasa amefikia kikomo wa challenge za mbele na anakihujumu chama hawezi kuunganisha watu na amekuwa akitumia madaraka yake vibaya.

Chama kimebaki palepale kilipo ingawa kina idadi ya wabunge lakini si kwa sababu sahihi za mabadiliko ni wabunge ambao wengi wao wapowapo tu hawana lolote zaidi ya local populace zilizowaweka, chama kimeshindwa kukamata watu makini at local levels to help with the cause, kuja ni njia mbadala za recruitment processes kazi kusherekea bongo flavor artist wanaojiunga, matter of fact anything to give it a positive attention; lakini si mkakati wa kweli kushinda chaguzi kuu.

Surely his position must be challenged CDM inahitaji mtu wakukipeleka mbele na kukipa sura ya utayari. Its time to let go wameshakilea CDM vya kutosha wawache wenye huwezo wakipeleke mbele na wakipe sura ya 'catch all party'.
 
Mkuu Nguvuri

Nimekuwa naufwatilia mjadala ambapo umetoa point za msingi sana, isipokuwa na wewe naona umeshaweka maamuzi yako ya kuwa Zitto ni tatizo. Bila ya kutaka kupekuwa upande wa pili wa shillingi na kuutendea haki kwa kina kwenye argument zako kama unavyo tetea maamuzi ya kamati kuu indirectly, thus either kwa makusudi ya kuhitisha hoja ya ukorofi wa Zitto ama kutopendezewa na siasa za Zitto as a person.

Kilichobaki sasa naona kama vile unatafuta namna ya kuhitimisha hoja ya fair justification on the standing accusation bila ya kutaka kuuliza uhalali wa mashataka na mtoa mashtaka, wakati the whole thing is undemocratic, ntarudi kukwambia kwanini wahaini ndani ya CDM ni Dr.Slaa na Mbowe (with neutral arguments) kwa matumizi mabaya ya kamati kuu kutimiza agenda zao na ukandamizaji wao wa demokrasia za ndani ya chama.

Of-course chanzo cha yote ni misingi mibaya ya Taasisi (hapo nakubaliana na wewe kwenye weakness ya taasisi kwa sasa, hila sioni ubovu wake kwa jicho lako, ni sawa na Dr. Kitila na waraka wao wasivyokubaliana na mbinu za sasa na uongozi uliopo).
Hapana ndugu yangu, nenda kule duru za siasa ukasome nilichoandika wiki mbili kabla ya kamati kuu ya CDM haijakaa. Fuatilia nyuzi hii uone watu wanavyoongelea jinsi kamati kuu ilivyokurupuka.
Wamesema wengi tu na nakumba mmoja ni Mchambuzi.

Nimesimama kusema kuwe na 'neutral organ'.
Hilo haliwezi kuzuia ukweli kuwa tuna waraka wa zitto na Kitila ambao ni jaribio la mapinduzi.
Mengine yanaweza kujadilika lakini la mapinduzi lipo wazi na wamekiri wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Hilo haliwezi kuzuia ukweli kuwa tuna waraka wa zitto na Kitila ambao ni jaribio la mapinduzi.
Ni sehemu gani ya waraka ambayo inayokufanya utoke kwenye mkakati wa kuboresha chama kwa maoni ya waliouandika, mpaka unakuwa wa mapinduzi?

Na kweli unaamini kiongozi wao ni msikivu iwapo angeambiwa aachie ngazi angesikia (maana anayo haki na yeye ya kubakia kwa kanuni sijui katiba aliyo ichakachua kumpa muda kwa mujibu wa waraka), kama hivyo si wanachama wengine pia wanahaki ya ku-challenge uongozi na kuweka mkakati wa ushindi ni vipi unakuwa uhaini?
 
Eric Cartman, Sijui mkakati wa CDM wa kuimarisha chama chao na wala sijui mipango yao.

Ninachokijua ni kuhusu mgogoro unaoendelea, labda kama utanisahihisha kuwa hakuna mgogoro.
Pili, Unatka kusema waraka ule hauna makosa? Hebu tuwekee sawa kwa maoni yako.

Kwa upande wangu tafadhali anza mwanzo wa uzi huu, nimejitahidi kwa uelewa wangu mdogo kuonyesha kuna tatizo.

Sasa ni sehemu na nafasi yako utuonyeshe hakuna tatizo kwa njia mbili
1. Kuelezea mkakati uliokuwa unapangwa ulilenga vipi kuimarisha Chama chao (CDM)
2. Katika niliyoyaeleze kama makosa ya waraka, wapi unapingana nami na kwa msingi gani.
 
Sijui mkakati wa CDM wa kuimarisha chama chao na wala sijui mipango yao.
Hiyo ndio sababu kubwa ya waraka unless message una interpret differently kiongozi hana vision, sasa mkakati utatoka wapi, waraka ni mipango ya mwanzo ya maandalizi ya kumweka kiongozi ambae waandishi wanaona anafa agombee kum-challenge wa sasa hili chama kisoge.
Ninachokijua ni kuhusu mgogoro unaoendelea, labda kama utanisahihisha kuwa hakuna mgogoro.
Pili, Unatka kusema waraka ule hauna makosa? Hebu tuwekee sawa kwa maoni yako.
Si ndio tunachojadili hapa mgogoro uliopo, utautendea vipi mjadala haki kama chanzo chake unakikwepa mpaka umefikia hapo, na hapo ndio jibu lako la swali la pili lilipo waraka hauna makosa ukiusoma vizuri, jaribu kupitia jarida la organisation behaviour: mission, objective and strategies ndio pretty much waraka wameuweka kisiasa tu. Its pretty much an entry strategy in marketing only conveyed into political rationale. The aim of it was looking at changes and adressing their barriers to entry.
Kwa upande wangu tafadhali anza mwanzo wa uzi huu, nimejitahidi kwa uelewa wangu mdogo kuonyesha kuna tatizo.
OK i will

Sasa ni sehemu na nafasi yako utuonyeshe hakuna tatizo kwa njia mbili
1. Kuelezea mkakati uliokuwa unapangwa ulilenga vipi kuimarisha Chama chao (CDM)
2. Katika niliyoyaeleze kama makosa ya waraka, wapi unapingana nami na kwa msingi gani.

1.Kumtoa kiongozi kwakuwa amekuwa akiminya demokrasia, huwezo wake mdogo kukipeleka chama mbele na kujaribu kuweka mtu ambae anaoneka ana huwezo zaidi yake kwa faida ya chama.

2. Napinga kwa sababu waraka unauchukulia kama mbinu chafu za kumtoa kiongozi, wakati ni mkakati tu wa namna ya kubadilisha uongozi usiotaka kujua nini maana ya kikomo na unaotumia mbinu za autocracy na kujihusisha na watu wachache something ambapo waandishi wanaona ni unacceptablde and things have to change (wanahaki hiyo kwa sababu uongozi wa CDM umeundwa kidemokrasia na si royalty).
 
Hiyo ndio sababu kubwa ya waraka unless message una interpret differently kiongozi hana vision, sasa mkakati utatoka wapi, waraka ni mipango ya mwanzo ya maandalizi ya kumweka kiongozi ambae waandishi wanaona anafa agombee kum-challenge wa sasa hili chama kisoge.
Si ndio tunachojadili hapa mgogoro uliopo, utautendea vipi mjadala haki kama chanzo chake unakikwepa mpaka umefikia hapo, na hapo ndio jibu lako la swali la pili lilipo waraka hauna makosa ukiusoma vizuri, jaribu kupitia jarida la organisation behaviour: mission, objective and strategies ndio pretty much waraka wameuweka kisiasa tu. Its pretty much an entry strategy in marketing only conveyed into political rationale. The aim of it was looking at changes and adressing their barriers to entry.
OK i will

1.Kumtoa kiongozi kwakuwa amekuwa akiminya demokrasia, huwezo wake mdogo kukipeleka chama mbele na kujaribu kuweka mtu ambae anaoneka ana huwezo zaidi yake kwa faida ya chama.

2. Napinga kwa sababu waraka unauchukulia kama mbinu chafu za kumtoa kiongozi, wakati ni mkakati tu wa namna ya kubadilisha uongozi usiotaka kujua nini maana ya kikomo na unaotumia mbinu za autocracy na kujihusisha na watu wachache something ambapo waandishi wanaona ni unacceptablde and things have to change (wanahaki hiyo kwa sababu uongozi wa CDM umeundwa kidemokrasia na si royalty).
Mkuu Eric Cartman, Kutojua mkkati hakuna maana kuwa siwezi kujali kilicho wazi kama waraka huo.
Ninachokisema ni kuwa mikakati ndani ya CDM siijui, lakini mkakati uliowekwa wa waraka si mkakati.
Lakini jiulize mkakati huo ni CDM au ni wa kundi la watu, na kama baadhi ya watu ukiwemo mnaujua je hiyo inafanya uwe mkakati wa CDM? Nitakupa mfano, hivi kujadili mapenzi ya Dr Slaa ni sehemu ya mkakati wa CDM?

Pili, hujajibu hoja nilizoweka, ulianza katikati na sasa unarudi nyuma.
Hukunitendea haki kwasababu ulitakiwa upitie uzi kwa undani ujiridhidhe kuwa unachokisema kina ushahidi na mantiki.

Tatu, tafadhali sana onyesha mkakati ndani ya waraka kipengele kimoja hadi kingine.
Nimeonyesha makosa kipengele kimoja hadi kingine.

Nne, pitia vipengele nilivyoainisha uonyeshe wapi unadhani kulikuwa na matatizo.

Tano, Kumuondoa kiongozi hatujasema ni kosa, kosa ni njia zinazotumika kumuondoa.
Kuandaa mapinduzi katika chama chenye nembo ya demokrasia si vision au mission ni treason.
Mkakati ni tendo, hata mapinduzi ni sehemu ya mkakati. Sijui unaongelea ni huu wa mapinduzi au wa kuendeleza CDM?

Sita, bado hujajibu swali,je unadhani waraka huo ni sahihi?
Hapa tunataka tuelewe position yako ili tujue tunajadiliana katika muktadha upi.
Mimi nasema tena waraka una makosa.

saba; Ukipitia nyuzi yangu nimesema si kila kitu ni trash kuna sehemu hoja zina mantiki ya kuzihoji nakiziorodhesha kwa kutoa nafasi uongozi ujibu(pitia nyuzi), lakini sehemu kubwa ya waraka haina mantiki.
Na namalizia hapa kwa kurudia kusema ule si waraka wa wasomi na nipo tayari kukuonyesha kwanini si wa kisomi.

Nane, hebu tuonyeshe mission, objective and strtategies katika waraka kipengele kimoja hadi kingine.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3

Turudishe kumbukumbu nyuma. Ben Saanane alinekana shujaa kwa kufanya uspy na kuvumbua wasaliti ndani ya Bavicha.

Kazi hiyo Ben Saanane aliifanya kwa muda mrefu na haijawahi kujadiliwa kwenye kikao chochote halali cha chama.

Katika kikao cha Bavicha kujadili sakata hilo Ben Saanane alihukumiwa kwa kumchafua Zitto kwenye mitandao na sio kwa kuwa na mikakati ya siri. Ben alipewa adhabu ya kutokugombea uongozi kwa mwaka mmoja, mwaka ambao hakuna uchaguzi wowote ndani ya chama.

Je, uhalali wa Ben Saanane kufanya kazi ya upelelezi wa viongozi bila Kamati Kuu kujua inatoka wapi?

Je, Ben Saanane alikuwa anapeleka ripoti yake ya upelelezi kwa nani?

Ben Saanane alipata wapi fursa ya kuaminiwa zaidi kuliko wajumbe wa Kamati Kuu? What special did he or does he offer?

Haya ndio mambo yanyoleta mgogoro.

Ben sio kiongozi hata wa ngazi ya tawi lakini anachokisema kinapewa imani kubwa kuliko viongozi wa kamati kuu ya chama taifa. Why?

Katika mazingira kama haya, kuamini kwamba unaweza kufuata nyia za uwazi kuutoa uongozi madarakani kidemokrasia ni kujidanganya kulikopindukia. Uamuzi wa Kitila wa kuandaa mkakati wa siri ni sahihi na ulilenga kukinusuru chama na kukipa chama sura ya chama cha siasa kinachotaka kuongoza nchi.

Soma waraka pale unaposema kwamba "Mida Eight" yaani Ben Saanane anatumiwa na Dr. Slaa kwa kazi ya uspy na fitina mitandaoni. Hili linajulikana lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa!!!

Vilevile nadhani unakumbuka Josephine Mushumbusi alivyokuwa anazunguka mikoani kutengeneza mtandao wa Dr. Slaa. Hili lilimalizwa kwa kumwambia Dr. Slaa aache kumtumia Josephine kwa shughuli hiyo, lakini Slaa hajapewa adhabu yoyote.

Yaani ni bayana kuwa ndani ya Chadema kuna misaafu ya aina mbili ya kutoa hukumu kutegemeana na nani anayeshutumiwa.

Kitila was right.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom