Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #201
Mkuu Mkandara ,ahsante na nianze na hoja ya Mwenyekiti wa CDM Singida.Mkuu wangu ebu turudi nyuma ktk historia yetu. Wale wadhamini wa TANU walomsaidia mwalimu kwa fedha na gharama zote unataka kusema ndio walikuwa wamiliki wa chama?.
Ikiwa hivyo, basi bila shaka yule mhindi alotupa mabillioni alitakiwa kuwa mmiliki maana sidhani kama hata mzee Mtei kisha toa fedha hiyo.Na kama ndivyo mbona yule mwenyekiti wetu wa Singida leo anaitwa Mhaini na msaliti wakati katumia mali na rasilimali zake kuliko hata wewe na mimi hapa! Uzalendo wa kiongozi ama mwanachama haupimwi kwa mali na rasilimali anazotumia bali ushirika wake, jasho lake na kujitoa mhanga kama kina Mandela, Oliver Tambo na Steve Biko.
Vyama vyote duniani huwa vina wafadhili wake na hawa hutokana na mapenzi yao kwa mrengo na sera za chama hicho iwe kwa kuelewa waakuja faidika pindi sera gizo zikipita ama wakisaidia mageuzi. Chama chochote cha kisiasa kinachomilikiwa na mtu ama watu fulani basi jua kuwa hawa ni MADIKTETA wanaotaka kutawala wao kwa kutumia nguvu ya fedha zao. Na sidhani kama kweli kina mMbowe wanafanya haya kwa nia ya kuwa madikteta lakini ndivyo itakavyo someka.
Sahihisho:- Huu waraka sisi wote tumeusoma na hakuna mahala hata pamoja imeonysha Zitto anahusika na uandishi wa huo waraka - HAKUNA. Yeye ni mtajwa tu, ndiye alopendekezwa na hicho kikundi iweje matusi na chuki yote yawe kwa ZItto?. Kwa nini haswa kupendekezwa kwake ndiko kunauma ama? Kw ahiyo ukiondoa jina la Zitto kama mwandalizi wa mageuzi hayo ya waraka huo, Uhalisia wa maelezo yako yote unaondoka...
Swali,ingiwa huu waraka unaitwa wa siri - ati kama walikuwa na mashaka walitakiwa kuyapeleka malalamiko hayo ktk vikao vya chama..Je, hivi kweli haya malalamiko ndio kwanza hata sisi ndio tumeyasoma ktk waraka huo ama yamezungumzwa na viongozi wengi walokwisha pita!..Binafis nimeoana machache sana mageni lakini kila kilichoandikwa nimesha kisoma tena hapahapa JF na hatukuona majibu wala mabadiliko yoyote ktk utekelezaji wake isipokuwa wote walodai hivyo huitwa wasaliti na mapandikizi wa CCM - Jamani mwee What's going on?..
Ikiwa ni kweli mahesabu ya chama hiki yanajulikana na watu watatu tu, toka 2010 hakuna mwaka wajumbe wa kamati kuu waliwahi kusomewa matumizi ya mwaka ulopita! mkuu huoni kama hili ni janga kubwa sana maana kwa tabia hii tukija shika nchi itakuwaje?. Na hii sio siri ama huko inaitwa jina jingine?. Mkuu wangu hata co-ops, asasi na Jumuiya za Watanzania nje na ndani huonyesha matumizi yao kwa kila mwaka ktk vikao vyao vya kufunga mwaka, iweje Chadema chama kubwa (mbadala) iwe siri ya watu watatu tu, kiasi kwamba hata Naibu katibu wa chama hajui kinachoendelea?..Hii ni kusema kwamba Zitto hakuaminika toka ameingia madarakani sasa tujiulize kwa nini alipewa nafasi ile ikiwa haaminiki?. Na wajumbe wengine pia hawaaminiki? kina ani haswa wanaoaminika kuwa kweli ndio i wana Chadema damu.
Sidhani ni jambo la Mwenyekiti kuivunia nyumba yake na sanduku la posta kutumiwa na CDM.
Mwenyekiti ni mwanachama wa kwanza Singida na wa 300 kitaifa kama alivyobainisha.
Kwa miaka 20 amekuwa mwenyekiti wa mkoa. Kipindi hicho ni kikubwa kwa mtu kufanya jambo katika chama chake.
Wenyeji wa Kilolo Iringa walikutwa na maswaibu ya Mwangosi wakiwa katika jengo lao walililojenga wenyewe.
Kumbuka hawa si viongozi wa mkoa ni kaeneo tu.
Leo mwenyekiti anastaafu na kusema CDM watumie sanduku lake la posta.Huyu hakufaa kuwa mwenyekiti na nadhani kuondoka kwake ni jambo jema kwa CDM kuliko uwepo wake. 20 yrs doing nothing!
Pili, mwenyekiti amejiuzulu kwasababu Zitto kachukuliwa hatua. Akiwa mwenyekiti hakuwahi kusikika akitoa sauti dhidi ya malalamiko, alikuwa loyal kwa Zitto kuliko chama. Hawa ni wa kupuuzwa ,Tanzania miaka 50 haiwezi kuendelea kuwa na viumbe wa aina hii iwe kwa CDM, CUF au CCM.
Kuhusu wafadhili wa chama, nakubaliana na Zakumi kuwa uwepo wao usiwe ndiyo sababu ya kuwanyang'anya wanachama umiliki. Tuhuma dhidi ya Mbowe kuwa na tenda ni matokeo ya ufadhili.
Waraka umelalalmikia kutokuwepo kwa mapato na Mkandara ameshadidia.
Hoja ya Zakumi inakuwa na nguvu zaidi kuwa ruzuku zinachangia kiasi cha migogoro.
Umiliki wa chama kwa kutumia matajiri umeifikisha CCM kushindwa hata kusimamia nidhamu.
Mafisadi wanalipwa 430,000 KWA SIKU kuandaa mipango ya serikali.
CC na NEC zimeshindwa kuchukua hatua kwa kuogopa nguvu ya matajiri na CCM si cha wakulima au wafanyakazi ni biashara tu kama huna kitu wewe ni CCM Pilau na Kofia. Je, Zakumi hana hoja kwa mtazamo huo.
Malalamiko yamekuwepo siku nyingi. Kwa bahati mbaya yalioenekana majungu kwasababu yaliletwa na watu wasiojulikana. Zaidi yalilenga kuchafua watu na kupoteza maana yake halisi au hoja iliyoyabeba.
Leo tuna ushahidi usio na shaka waliokuwa wanaleta malalamiko hayo na kuonekana ni wengi ni vijana wa Kitila/Zitto kama alivyo Mwigamba. Mwigamba alikuwa anaandika kwa ID ya 'masikini mkulima'Mkuu soma post#92 uniambie kama ipo tofauti kati ya waandika waraka na huyo aliyeandika JF.
Kuhusu Zitto kuhusishwa na waraka, ukiusoma unaeleza wazi kabisa 'ataombwa' kuwa mshiriki mkuu (MM) na atafundwa kufanya mambo ABCD. Kuna kila sababu za maana kuamini kuwa hatua zilizokuwa zimefikiwa na waandika waraka zilikuwa za juu zaidi kuliko waraka ulivyosema. Nitafafanua hapa chini.
1. Kwanza hatujui waraka uliandikwa lini kwasababu hakuna tarehe. Matukio ya tuhuma katika mitandao kama iliyoanishwa katika waraka yalIanza kutokea miezi zaidi ya minne iliyopita.Maana yake hatua ya utekelezaji ilishaanza.
2. Waraka umesema watafutwe watu wachache waaminif. Waraka umekamatwa kwa Mwigamba ambaye ni mwenyekiti wa Mkoa. Maana yake ule uundwaji wa kanda na watu waaminifu ulishakamilika.
3. Waraka umemtaka Zitto awe mwiba kwa serikali ndani na nje ya Bunge.
Tumeshuhudia jinsi alivyokuwa mkali kwa masuala ya 'kitaifa'
4. Waraka umesema wazi njia ya kubomoa uongozi ni kurusha kombora. Tuhuma za ukaguzi wa fedha za vyama amezitoa Zitto akiwa mwenyekiti wa PAC. Tuhuma hizo ni sambamba kabisa na maagizo ya waraka ulivyosema.
Zitto alikshatekeleza agizo la waraka kwa kurusha kombora la ukaguzi wa fedha.
5. Waraka umemwagiza Zitto ashiriki kampeni. Hivi karibuni alishiriki kampeni kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
6. Ukamtaka asijibu tuhuma, ndivyo alivofanya wakati anashambuliwa na mbunge mwenzaek. Ukimya si hulka ya Zitto hata waraka umeshuhudia hilo, leo ushujaa huo kautoa wapi.
7. Waraka ukasema wenye ID wataanza kumpamba Zitto, rejea bandiko#92
8. Wakati wa kikao cha CC kuna tuhuma hakuwepo.Ilibainika alitaka kujiuzulu nafasi yake na Kitila.
Kwanini alitaka kujiuzulu kama hakuwa na jambo lolote baya alilofanya katika chama. Alitaka kuzuia sakata lisiingie katika public domain 'funika kombe'
Kama ilikuwa kujiuzulu angefanya hivyo kabla ya Mwigamba hajauza ghala la silaha.
Kinyume chake ni kutambua kuwa hujuma dhidi ya chama chake, usaliti kama kiongozi ndani ya chama chake, matusi, kashfa kejeli na dharau dhidi ya viongozi wenzake kulikuwa na mkono wake mrefu sana.
Zitto hakuandika waraka kama alivyookolewa na Kitila, lakni ameshiriki katika utekelezaji wa maagizo ya waraka kikamilifu. Hili limemuodolea public trust, limemshushia hadhi na heshima, na limemuanika mbele ya uso wa Watanzania.Jitihada za kujisafisha kwa kutumia vyombo vya habari haziwezi kumrudishia hadhi na uaminiFu aliyokuwa amepewa na jamii.
Na mwisho kuhusu mahesabu ya chama kujulikana na watu watatu, ningefarijika kama Zitto na Kitila wangejitoa na kuyasema. Leo ningesimama upande wao bila kusita. Hawakufanya hivyo wakakimbilia embe kiburugwa kuandaa jungu badala ya kutoka na kusema uozo ndani ya chama chao. That is too low the least to say.
Madai hayo yanaweza kuwa na mashiko lakini Zitto akiwa mtendaji msaidizi amepoteza heshima ya kuyazungumzia.
Kitila akiwa mshauri wa chama amepoteza hadhi ya kUsikilizwa.
Yazungumzwe na mtu mwingine, hawa wawili hawana moral authority ya kuieleza jamii jambo lolote ikaaminika tena.
Hawana public trust. Watulie na waanze kununua nguo za kujisetiri
Last edited by a moderator: