Tunakufuatilia sana mkuu, wating for analysis. So far nimeipenda sana democracy ya wenzetu maana kuna uhuru wa kutosha na wamejipanga kisawa sawaTathmini ya leo inafuata
Tathmini ya leo inafuata
Mkuu mag3 wakati tunasubiri analysis ya HC kutoka kwa nguruvi3. Hebu kwa faida ya wanajukwaa wengi tukumbushe mara ya mwisho hawa wamarekani kukipa uongozi chama tawala awamu mbili mfululizo. Hapa namaanisha kwa mfano,Democrat wamepata fursa ya kuongoza miaka yote 8 ya obama. Mara nyingi hapa wamarekani wakikipa chama uongozi wa miaka 8 mfululizo,uchaguzi unaofuata(km huu) mara nyingi huwa wanafanya mabadiliko. Nataka unikumbushe mara ya mwisho chama kupata uongozi kwa miaka 12 au 16 mfululizo ilikuwa mwaka gani!!?? Najua chama kikivurunda huwa kinaishia miaka 4 km ilivyokuwa kwa George bush senior miaka ya 90.Wakati tukisubiri tathmini murua kutoka kwa Nguruvi3, mimi nadhani Democrats wamejikita zaidi katika hizi wanazozioana kama tofauti zao kimsingi na za Republicans.
Tofauti hizi zimeonekana katika kauli zao na mabango yaliyotamalaki kwenye Convention yao yakisomeka...
- Upendo dhidi ya chuki (love vs hate)
- Umoja dhidi ya utengano (unity vs division)
- Matumaini dhidi ya wasiwasi (hope vs cynicism)
- Love trumps hate (Upendo hushinda chuki)
- Together we are strong (Umoja ni nguvu)
- America is great. (America ni taifa kubwa)
Democrats: We don't build walls around us, we build bridges to unite us.
Republicans: We are going to build a wall and Mexico will pay for it.
Hayo maneno yamenivutia sana kutoka kwa Mtoto WA Trump...Ni muda wa Rais atakayeifanya America great again kwa budget
- Ninamuona baba kama mtu anayeipenda nchi yake na aliyetayari kuifanya great again
-Nina charity inayoongozwa kwa maadili na uadilifu na siyo charity zenye 'corruptions'
-Kwa wasio na ajira, baba anagombea kwa ajili yenu
-Kwa veteran waliopuuzwa baba anagombea kwa ajili yenu
-Kwa undocumented illegal worker , baba anagombea kwa ajili yenu
-Kwa single mom na walemavu, baba anagombea kwa ajili yenu
-Nov nawaomba mpige kura kwa mgombea anayejua kwanini anagombea, ambaye si mwanasiasa na ambaye hajui gov cheque
-Mgombea asiyenunulika au kushawishika.
-Pigeni kura kwa mgombea asiyehitaji hii kazi. Najivunia Trump na mtoto wake, na najivunia kuwa sehemu ya kampeni. Baba ulitufundisha kwa mifano, ni shujaa na rafiki na Rais ajaye wa America
Nguruvi3 Kwani USA ina vyama viwili tu vya siasa.. Na ndio vimesimamisha wagombea Urais.. Je mgombea binafsi anapewa nafasi gani, maana kama yupo na hapewi nafasi, je kwa Nchi yetu ambayo watu wanataka mgombea Urais.. Je itakua na tija ganiTaratibu za uchaguzi wa Marekani
Mwaka 2008 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Democrat
Mwaka 2012 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Republican
Na mwaka 2016 mkutano mkuu wa kwanza ni Republican
Naomba nichangie tukimsubiri mkuu Mag3 atusaidie zaidiMkuu mag3 wakati tunasubiri analysis ya HC kutoka kwa nguruvi3. Hebu kwa faida ya wanajukwaa wengi tukumbushe mara ya mwisho hawa wamarekani kukipa uongozi chama tawala awamu mbili mfululizo. Hapa namaanisha kwa mfano,Democrat wamepata fursa ya kuongoza miaka yote 8 ya obama. Mara nyingi hapa wamarekani wakikipa chama uongozi wa miaka 8 mfululizo,uchaguzi unaofuata(km huu) mara nyingi huwa wanafanya mabadiliko. Nataka unikumbushe mara ya mwisho chama kupata uongozi kwa miaka 12 au 16 mfululizo ilikuwa mwaka gani!!?? Najua chama kikivurunda huwa kinaishia miaka 4 km ilivyokuwa kwa George bush senior miaka ya 90.