Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

America muslims for Trump

Anaongea Sajid Tarar

Anaanza kwa maombi kwanza.

Kama waaamerika tuna wajibu wa kuchagua kiongozi. Ananukuu kitabu cha Buhar akizungumzia value za viongozi.

Hakuzungumzia siasa bali maneno machache tu

Hakuzungumzia lolote kuhusu 'fear' waliyo nayo Waislam kwa Trump.
Kwa maneno mengine hakuwa na impact ya aina yoyote Zaidi ya kuboa.

Tunasema hivyo kwasababu kazi aliyofanya ni sala na wakati watu wanasubiri kusikia neon linalohusu uchaguzi, akawa amemaliza.

It was off point kwasababu hakutumia fursa kusema lolote tofauti na matarajio ya watu
 
Theme ya Leo

Make America work again'' kwa maana kuwa ilikuwa suala la uchumi

Tathmini

Kilichoonekana ni kumshambulia Hillary Clinton badala ya kuiongelea mada ya leo

Hili ni pengo kubwa katika mkutano huu mkubwa.

Ni kwamba wazungumzaji walikuwa derailed na suala la Clinton badala ya kutumia uchumi kujenga hoja

Ukiacha Donald Trump Jr na Spika Paul Ryan waliogusia masuala ya uchumi, wengine walijielekeza katika mashambulizi dhidi ya Democrat

Hatari yake ni kuwa, Democrat wakiongelea mambo kama ajira, ujira, umasikini na uchumi wataonekana kuwa bora hata kama si hivyo.

Kitakachoangaliwa ni nani kagusa 'nerve' za watu.
Kwa leo theme haikutendewa haki kama ilivyotendewa ya usalama jana
 
WAKIRI KUBEBA HOTUBA YA MICHELLE

Hatimaye mwandika hotuba wa Trump Org Meredith Mclver amekiri kuwa kulikuwa na plagiarism kutoka katika hotuba ya Michelle Obama.

Ameomba radhi na kusema ameomba kujiuzulu

Meredith alikiri kuwa Melania Trump ana mu-admire Michelle na alisoma kipande cha hotuba yake kwavile ilimgusa sana.

Bila kutarajiwa kipande kikaingizwa katika hotuba kwa alichosema 'innocent mistakes'

Hata hivyo, Trump na Melania wamekataa kujiuzulu na haijajulikana hatma yake

Kama mtakumbuka, habari hizi zilipotoka tulisema,Trump alikuwa na machaguo mawili
1. Kuomba radhi
2. Kumwajibisha mhusika

Kampeni manager Bw Mafort alisistiza hakuna tatizo na wala haikuwa plagiarism.

Alichoshindwa kuelewa,kufanya hivyo kulirefusha habari hiyo na kuleta madhara zaidi

Zaidi ya siku mbili habari imevuma na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa kampeni nzima

Mwisho wa siku wanafanya kile walichopaswa kufanya kuanzia siku ya mwanzo.

Hapa kuna funzo la damage control, kwamba uharibifu unaweza kurekebishwa kwa hatua za haraka na zenye weledi.

Na kwamba kuomba radhi si kosa bali sehemu ya uungwana

Tunaona hapa nchini kukiwa na uharibifu usio wa lazima unaoendelea kila siku kwasababu ya kutokuwa na ''damage control strategy'' kama lilivyo suala la marufuku ya mikutano
 
LEO RNCinCLE

Wazungumzaji miongoni mwa wengi ni Ted Cruz, Mark Rubio, Spika mstaafu Gingrich na Gav Scott Walker

Lakini usiku wa leo ni wa mgombea mwenza Mike Pence

Ted atahutubia kukiwa na swali la kwanini haja mu-endorse Trump

Kuna mixed feeling kuhusu mgombea na chama Je, watu wanaungana dhidi ya Democrat , wanaungana dhidi ya Clinton au wanaungana kuendeleza agenda ya Republican?

Na kwanini mahasimu waliosema hawatahudhuria convention baadhi yao wanabadili misimamo? Ni nini kinawasukuma hasa?

Tufuatilie mkutano usiku wa leo
 
First NASA Female Pilot Eleen Collins

Anasema Obama alizuia space program muhimu kupata info kuhusu planet yetu

Anasema kwenda katika space ni leadership na hivyo upo umuhimu wa kupata mtu atakaye 'make America great again'

Ujumbe wake ni mfupi
 
Seneta wa Kentuck state senate Dr Alvarado

Ni Mlatino na anasema, Latino wanaamini falsa ya Republican kama family values

-Rais amefeli racial tension na kuligawa taifa Zaidi

-Kuna Rais anayedanganya kwa Waamerika kutoka Obamacare, VA Scandal, Immigration etc

- Clinton atakuwa tatizo, je, America wanataka mtu honest au

- message kutoka kwa Walatino (anazungumza kilatino)

- Hillary amefeli Spanic community na hastahili kura zao, anasema
 
Pastor kutoka Cleveland (Darrell Scott)

Anasema anamfahamu Trump kwa miaka 20

Anaongelea mambo ya kiroho. Anasema Trump ni patriot

- Marekani si Taifa kama taifa jingine ni Taifa tofauti na wanajivunia patriot

- Anazungumzia one nation under one God, na wapo hapa bila kujali rangi ,dini au kingine

-Trump atajenga broken trust kati ya wananchi na serikali.

-Trump ni master negotiator, na kwamba atawaleta watu pamoja

- Ata solve problem na kuleta watu pamoja, ata strike deal nzuri kwa America

- Hakuna kitakachomzuai trump kuwa kiongozi ambaye kila mtu atajivunia

Anaongea kwa nguvu za mahubiri na kushangiliwa.

Huyu Pastor ni mweusi
 
Gav S.Walker wa Wisconsin

Huyu ali mui-endorse Ted Cruz katika kinyang'anyiro

- Anaongelea kuhusu college tuition kupungua Wisconsin

-Ongezeko la ajira n.k

- Anawataka Waamerika wachague wabunge, maseneta na Rais

- Anawatakia kila heri Rais na makamu wa Rais mtarajiwa

Kwa sehemu kubwa Walker ameongelea Republican Zaidi kuliko mgombea na value zake.
Kuna 'reservation' ndani kwa ndani na unaweza kuiona kupitia kauli zao
 
Lynn Pattorn

Huyu ni kiongozi wa Eric Trump foundation

-Ni mweusi na anaongelea kuhusu ....live matter, akitaja kila kundi.

-Anasema Taifa limegawanyika kuliko miaka 8 iliyopita

-Biblia inasema unaweza kuu judge mti kwa matunda na hapa akisema ni Trump

-Anawasifia watoto wa Trump na kuwaita heroes
 
Mark Rubio

anaongea kupitia video, na kumshambulia Clinton

- Anawazungumzia Obama na Clinton kuhusu suala la uteuzi wa majaji
 
Ted Cruz

Anasema

- Mungu wabariki wote, na kwamba yeye na mkewe wanafuraha kuwepo Cleveland

- Ana congratulate Trump kwa kushinda nomination jana

-Anataka kuona principle za GOP zikifanyika November

-Anaongelea kuhusu mtoto ambaye baba yake aliuawa Dallas (Polisi) Michael Smit

- Anasema maisha yake aliyatoa kulinda watu hata waliomdhihaki.

-Anaongelea kuhusu Oerlando, Nice na Paris (Mauaji). Anasema muda wa kufanya jambo kwa nchi yake. Anasema hii ndiyo maana ya uchaguzi.

-America ni symbol ya freedom na power.

- Anasema America hawana queen or king au dikteta, na kwamba wananchi ndio wanaoimiliki nchi. Anasema nchi ya America iliundwa kwa lugha ya kiingereza

-Chuki zinaigawa America na wanasiasa wanaodharau watu

-Mashujaa wanadai Zaidi ya hapo. Obama na Clinton nao watasema wana care kuhusu watoto. Lakini kuna tofauti.

- Anazungumzia Benghaz na deal ya Nuclear na Iran. Anasema Obama ni mtu anayefanya kila kitu kinyume, Anataka kufunga Gtimo na kufungua mipaka. Anataka kutoa kazi kwa mataifa ya nje. Inatosha

- kuna siku njema usoni za kurudi katika ubora

- Anzungumzia freedom, kwa kila uhai unathamani na lazima ulindwe.
Freedom ina maana supreme court kufuata katiba.
Na kutambua states kuchagua policy wanazotaka kulingana na mazingira.

-Hillary anaamini serikali lazima ifanye kila chaguo la maisha yako

-Kitu chenye nguvu kinatokea, tumeona UK ikijitenga na EU

-Wapiga kura huwakataa political establishment. Huo ndio ushindi ambao kila mmoja anapaswa kuuzingatia. Watu wamechoka na rushwa ya elite badala ya watu

-Tunataka immigration inayoweka America kwanza, na yes! kujenga ukuta

-Serikali inayozuia ISIS kama wakimbizi. Serikali inayojali masilahi ya wakulima, na wenye viwanda. Freedom itarudisha ajira, kuondoa umasikini.
37 yrs ago America ilipeleka mtu mwezini. GOP ilianzishwa kupinga utumwa

Lincoln, Rais kutoka GOP alisaini emancipation, na sharia ya haki za binadamu.
Hizo ndizo sifa zetu vyombo vya habari haviongelei.

- Askari wote husimama kulinda freedom na radical Islam.

- Tunahitaji kiongozi anayesimama kwa principle, na ndicho kiwango tunachokitaka. Tafadhali usikae nyumbani November. Nathamini msisimko wa ujumbe wa NY

-Hoja yetu kwa America ni kulinda freedom na kutii katiba. Tutaunganisha nchi kwa value za uhuru

Amemaliza, ingawa anazomewe pia. Haieleweki kwanini anazomewa
 
Ted Cruz amezomewa na wajumbe wa NY

Hili ni kwasababu haku mui-endorse Trump.
Kauli zake nyingine zilionekana ku suggest kuwa Trump si kiongozi 'aliyefikiriwa'

Wajumbe wa NY walisikika wakisema Trump! we need Trump , endorse Trump! endorse Trump

Hapa kulikuwa na tatizo na kwakweli. Ted atakuwa gumzo katika siku ambayo ni kubwa

Inaonekana Ted ametumia jukwaa kujijenga kisiasa badala ya kumsaidia Trump

Hili linaweza kuwa hesabu za siku za baadaye
 
ERIC TRUMP

Anazungumzia kuhusu baba yake

-Hakuvumilia second amendment attack

-Hakuvumilia kuona neon XMas linaondolewa katika mashule na sehemu nyingine

-Baba amechagua kutoa mafanikio kwa kutumikia Taifa

-Nini anaweza kwa vitendo kufanya biashara kama baba. Nani anaweza ku implement tax reductions? Nanai anaweza ku negotiate makampuni kurudi America kuliko mtu aliyeajiri mamia ya watu

-Ni muda wa Rais anathamnini tax dollar, anayesaini mbele ya cheque na si nyuma

-Ni muda wa Rais atakayeifanya America great again kwa budget

- Ninamuona baba kama mtu anayeipenda nchi yake na aliyetayari kuifanya great again

-Nina charity inayoongozwa kwa maadili na uadilifu na siyo charity zenye 'corruptions'

-Kwa wasio na ajira, baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa veteran waliopuuzwa baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa undocumented illegal worker , baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa single mom na walemavu, baba anagombea kwa ajili yenu

-Nov nawaomba mpige kura kwa mgombea anayejua kwanini anagombea, ambaye si mwanasiasa na ambaye hajui gov cheque

-Mgombea asiyenunulika au kushawishika.

-Pigeni kura kwa mgombea asiyehitaji hii kazi. Najivunia Trump na mtoto wake, na najivunia kuwa sehemu ya kampeni. Baba ulitufundisha kwa mifano, ni shujaa na rafiki na Rais ajaye wa America

Amemaliza
 
SPIKA MSTAAFU NEWT GINGRICH

Anazomewa kwanza kabla ya kuanza

Anasema

- Najivunia kuwa hapa kama GOP kwa jitihada za Trump kuleta Rep pamoja

-Bila kudai endorsement alialika wapinzani wake. Anafanya clarifications ya maneno ya Ted Cruz

-Tunaiwekaje America salama , jamabo muhimu kwa America

- Donald Trump anasema ukweli kuhusu national security. Mfano, tupo katika vita na Islamic terrorist. Tofauti na Trump Clinton hawaongelei ukweli huo

- Kama ajali ikitiokea LBGT, Wanawake, na kila mtu atasilimishwa kwa upanga. Hakutakuwa na uhuru, usawa. Kama una shaka na vita. Mfano, Jumatatu, Afghanistan anayeishi Ujerumani alicharaza watu visu

-Wiki mbili, 300 watu waliouawa na watu Baghdad, Istanbul, Afghanistan. Mwezi uliokwisha Paris, aliuawa askari na radical. Shambulio la Orlando.
Yote haya ni katika siku 37 zilizopita

- Tuwe wakweli, Trump yupo sahihi, tupo katika vita na radical islamists, tunashindwa vita na tubadili mwelekeo

-Hatuna cha kuogopa kuhusu waislam wengi wa Amerika au dunia. Ni victims, changamoto ni sehemu ndogo inapochochea vurugu. Ingawa tunapoteza vita na radical, hatari inayotukabili ni mbaya kuliko yanayotokea Paris na Ujerumani. Ni mbaya kuliko yanayotokea Israel

-Anakumbusha 9/11. Tunaweza kupoteza block after block n.k. Magaidi wanasema tutatumia silaha za nyuklia kuimaliza America. Iran ipo karibu kuwa na silaha za maangamizi

-Haya ni kwa usalama wetu, hatuwezi kuweka waongo waliotufikisha hapa. Ndio maana kila mtu aogope ugombea wa Clinton, tunajua Clinton na Obama wanaongopa

-Clinton anataka kuongeza wahamiaji, halafu kuna email. Kutokuwa na uadilifu kwa Clinton ni hatari kwa America.

-Trump anaelewa ulinzi na usalama ndiyo maana anazungumzia uimara wa jeshi

-Atalinda mipaka na ku enforce immig law, ataangalia veteran n.k.

-Ataondoa sharia mbovu n.k. Trump infrast program itarudidha hadhi ya US

-Atarudisha law and order na hatavumilia wanaoshambulia Polisi

-Trump na Pence watalinda America, hivyo leo naomba wote tusimame Zaidi ya siasa.

-Tusimame na Mike Pence na Trump kuifanya US njema Zaidi

Amemaliza

-
 
Kama kuna spelling error tunaomba radhi, tunaleta habari in real time.
Mtu akimaliza, nasi tuna post right away

Anfuata Mgombea Mwenza
 
Paul Ryan, Spika anamtambulisha mgombea mwenza

-Najivunia VP , tumefanya kazi naye, nimeona alivyo

-Pence ni mtu wa solid character. Ametumikia kwa uadilifu na heshima

-Kama Gov amepitisha tax cut in history, amebalance budget. Ni kama Reagan

-Ni baba wa watoto watatu, anamwita mkewe the best part of hisi life

-Ni mtu wa Imani, ushawishi, unayeweza kumwamini na kutoka kitovu cha conservative

-Sina shaka ataleta mabadiliko Washington

Nina heshima ya kumtambulisha kwenu Gav Mike pence

Anshangiliwa
 
MIKE PENCE

MGOMBEA MWENZA NA VP MTARAJIWA

Anasema
- Ahsanteni wote na nawashukuru sana,nakubali nafasi ya ugombea kama VP

- Mimi ni mkristo na conservative Republicans

-Mumemteua mshindi, na asiyekata tamaa, Donald trump

-Tutashinda kwasababu tunagombea katika hoja. America wamechoka kusikia wanasiasa wakisema tutafanya kesho, tukiongeza deni kwa watoto wetu kila siku.

-Uchaguzi ni kuhusu kura itajayohakikisha Hillary Clinton hawi Rais wa US

-Clinton, ana offer 3rd Obamacare, na deni la taifa limeongezeka. Kama Obama anafikiria sharia , madeni na serikali kubwa. Wanasema huu uchumi ni bora, ni bora kwao si kwetu

-Indiana wanatumia conservative principle, na inafanya kazi vema Indiana

-Leo taifa lina deni la 19 Trilioni , Indiana ina surplus ya bilioni 2. Tuna ajira Zaidi na hayo ndiyo tunataka na Trump ndiyo atakayopeleka white house

-Trump anaelewa, ni mtendaji . Hazungumzi kisiasa

- Trump anajali watu wanaolifanya Taifa liendelee. Inasikitisha kwa askari wetu, wajue kuwa tutasimama na Polisi.

- Nimemjua kwa ukaribu Trump, ni mtu anayeheshimu watu.

- Clinton ni establishment na secretary of status quo. Tunaweza kuchagua walioshindwa, au kuchagua viongozi. Trump ataleta change, na change will be Huuuge!!!!

-Chini ya Trump, veteran watapata wanachostahili, mipaka italindwa na taifa litanyanyuka

-Hii haitakuwa rahisi, matokeo yanatutegemea. Clinton machine in action kama Bernie Sanders anavyosema. Kwa muda huu atakuwa na wakati mgumu. Hatapata attention kama ya Trump kwa issue by issue

-Tuna agenda ya stronger and prosperous America

- Union member hawataki Rais atakayewaweka coal miners out of business

- Trump ata fight kwa black America, ataheshimu kazi n.k.

-Chama cha Lincoln kilianzishwa kwa usawa na haki na agenda ni kuhakikisha kila mwamerika anafanikiwa

-Tuhakikishe Rais atakayechagua jaji wa supreme court ni Trump

-Rekodi ya Clinton in foreign affairs ni mbaya. Iran, Benghaz n.k.

Kuna kelele zinasema Obama, Obama!

- Kwa mtu aliyefanya ya Hillary, hapaswi kuwa kamanda in chifu wa US

-7 yr ya Obama na Clinton, terroristic attack na attempted coup in Turkey , foreign policy yao ya ku lead from behind n.k ni ushahidi wa haya. Hatuwezi kuwa na miaka mingine 4

-Trump katika uso wa dunia ataongoza kwa nguvu, atajenga jeshi na kuharibu radical Islamists. Dunia inajua hivi, America inasimama na Israel

-Mwisho wa Obama kuna mengi yanayotugawa kuliko kutuanganisha. Sote ni ni one nation under God, indivisible and Liberty.

-Naahidi kuwa mtiifu kama VP na kuomba kila siku. Naamini tumefika mahali na nina Imani kwa waamerika , na Imani kuwa mungu ataiponya nchi yetu.

- chaguo ni Rais atakayakabiliana na ISIS,atakaye restore law and Order, atakayekuza uchumi na kuondoa ukiritimba, atakayejenga mipaka imara, atakayepambana na Washington DC, tuna chaguo moja, timu ipo tayari na chama kipo tayari na tukimchagua Trump tutafanya Amerika great again

Amemaliza
 
TATHMINI YA RNC

Habari ya leo ni Ted Cruz ambaye amezomewa na wajumbe wa New York
Ted alialikwa kuzungumza kwa matarajio ya kufanya endorsement kwa Trump

Wagombea wengine waliokuwa katika kinyang'anyiro kama Rubio,Walker, Dr Carson wame mui-endorse Trump kama makubaliano wakati wa chaguzi za ndani

Kilichosahangaza wajumbe ni kuongelea mambo ya freedom na constitution Zaidi ya kumwelezea Donald Trump na kile anachosimamia.

Na mwisho alisema ' Nov watu wapige kura kwa utambuzi' wa nani wanampigia kura

Ni wakati huo wajumbe walianza kumzomea kwa nguvu na yeye kusema ana appreciate msisimko wa wajumbe wa New York

Wakati huo huo Trump akaingia ukumbini kana kwamba ilipangwa ili kuzima zomea

Ted na mkewe waliondolewa ukumbini chini ya ulinzi, kwani baadhi ya wajumbe walionekana kuwa tayari kuteremsha kipigo

Tweets zimeendelea kati yao Trump, na Ted kwa namna Fulani, huku gavana Christie Christie akimwelezea Ted kama 'self fish'

Katika majukwa ya wachambuzi 'pundits' wafuasi wa Trump wameonekana kukasirishwa na Ted na kumshambulia hadharani

Hili limepunguza nguvu ya ujumbe mzito wa spika mstaafu Gingrich na mgombea mwenza Mike Pence. Story sasa si hao bali timbwili la Ted cruza

Ujumbe wa wasemaji leo waliokuwa organized kuliko siku nyingine ilikuwa kuhusu ugaidi na uchumi. Kwa sehemu kubwa mashambulio ya Paris, na USA yametawala maongezi yakisemwa kuwa America ipo katika hatari kubwa ya kushambuliwa

Hili lilifanywa kiufundi katika kumfungamanisha Obama na Clinton. Jambo moja la kujiuliza , mashambulizi ya Paris au coup ya Turkey ingewezaje kuzuiwa na USA?

Wazungumzaji hawakumwacha Clinton, kila mara alitajwa na kuhusishwa na Obama.

Kuna faida na hasara zake. Kwa baadhi, bado Obama ni maarufu na hili litawaumiza GOP
Kuna sehemu Obama hana umaarufu na hilo litasaidia GOP

Kwa bahati mbaya, wiki ijayo itakuwa ni Democrat. Watajibu hotuba na tuhuma zote bila GOP kuwa na fursa nyingine ya kujibu. Hii ni disadvantage kwa Republican

Lakini muhimu katika siku ya leo, wazungumzaji hawakufafanua kwa kina ni kipi wanachoweza kufanya tofauti. Hilo ndilo linaweza kuwakwaza katika kidahalo ijayo

Suala la Polisi nalo litakuwa katika midahalo. GOP wanatoa kauli ambazo si kwamba zinazidi kuwatenga na baadhi ya makundi ya jamii, lakini lina encourage Zaidi makundi hayo kushiriki katika kura

Tayari kuna record number ya Walatino kujiandikisha katika states zingine

Ujumbe kuhusu uchumi, na siasa za nje haupo coherent, kwa maana kuwa anachosema VP na high profile speakers wanapingana na mgombea Urais.

Yaliyotokea leo yanaonyesha bado ufa ni mkubwa kwa Republican

Tusemezane
 
TRUMP NA NEW YORK TIMES

Kabla ya kukubali uteuzi kesho, Trump inaelekea kafanya kosa jingine la kiufundi
Amezungumza na New York Times kuhusu masuala mbali mbali

Kuna njia mbili anazoweza kufanya kwa risk
1. Kusimama na kile alichosema akiwa na NY Times
2. Kubadili msimamo kufuatana na maoni ya wachambuzi

Kuelekea usiku mkubwa kwake, kiufundi hili linamweka mahali pagumu

Tutaeleza Zaidi kuhusu maongezi ya leo, ingawa sehemu moja amesema Marekani haiwezi ku lecture mataifa mengine. Wakati huo huo wanalaumu siasa za nje za Obama
Lakini pia ni kinyume cha sera za GOP na hivyo kuzusha timbwili Zaidi

Tunafuatilia kwa ukaribu yote

Tusemezane
 
Back
Top Bottom