Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Trump

- Nitalinda free speech kwa waamerika wote wakiwemo w dini ambao haki yao imechukuliwa

-Tunatakiwa kuamini nchi na sisi wenyewe

-Ni wakati kuonyesha dunia, US is back bigger and stronger than ever before

-Ninabahati ya kuwa na mkewe na watoto wangu karibu. Mtakuwa vyanzo vya furaha

-Kutokana na baba yangu, nimejifunza kuheshimu watu na heshima kwa kazi

-Mama alikuwa mwaminifu na mwenye hekima

-Kwa dada na kaka zangu , nitawapata upendo ni muhimu na wa kipekee kwangu

-Nina mafanikio katika biashara, na sasa mpango wangu ni kuwafanyia kazi na kutoa ushindi kwa Waamerika ili tushinde tena

-Ili kufanikiwa, tuondoke katika siasa za kichwara. Watu wote wanaosema huwezi kuwa na nchi unayotaka, ndio waliosema Trump hana nafasi. Tunafurahi kuwashinda hao watu

-Tusiwaamini katika media na siasa waakaosema lolote kulinda rigged system. Historia inatuangalia kama tutafanikiwa na kuonyesha dunia kama tupo free independent na strong

- nawaomba kuungwa mkon ili niwe mshindi wenu WH

-Clinton anaomba support kwa maneno matatu, I am with her, nasema Iam with you

Inaendelea
 
Trump

Ni sauti yenu, nitawapigania na nitawashindia nyote

-Kwa wote katika miji na vijiji, naahisi, kuifanya amerika yenye nguvu, ya kujivunia, salama na kuifanya America great again. God bless you

Amemaliza
 
Asante Nguruvi3, unafanya kazi nzuri kweli kweli na sina cha kuongeza kwa sasa...

n-DONALD-TRUMP-628x314.jpg


We will make America strong again
We will make America proud again
We will make America safe again
We will make America great again.

 
Mag3 ahsante

Wanajamvi, tathmini ya mkutano mkuu itafuata.
Tutaangalia kila kona ya mkutano mkuu wa Republican tukitarajia mtinage uchaguzi mkuu

Tukumbuke, Hillary Clinton atatangaza mgombea mwenza kati ya kesho na Jumamosi
Na mkutano mkuu wa Democrats utakuwa wiki ijayo kule Philadephia

Nao kama huu tutawaleta habari zote ni 'real time'

Tathmini inafuta

Tusemazane
 
TATHMINI YA MKUTANO MKUU WA REPUBLICAN

Sehemu ya I

Mkutano ulianza kwa 'tension' ya uwepo wa kundi la 'never trump' kutaka kuuzuia
Hilo lilishindikana kutokana na ulinzi mkali uliokuwepo

Katazo halikuwa nje, bali ndani ya ukumbi.
Tunaona vyombo vya ulinzi vinavyosimamia haki kwa kila kundi bila upendeleo.

Siku mbili za awali zilikuwa na mada ambazo wachangiaji hawakuzieleza kutokana na kuvutwa na shambulizi dhidi ya Clinton kama mgombea na si Democrats kama chama.

Kilichoonekana ni kuwa Reoublican wameungana dhidi ya Mrs Clinton zaidi ya Democrats
Hii inatokana na ukweli kuwa GOP walipinga hoja nyingi za Dem katika seneti na congress(bunge)
Kuishambulia Democrats kungewarudi

Rep walitambua kuwa udhaifu mkubwa wa Clinton ni kumshambulia yeye kama alivyofanya Bernie Sanders. Badala ya kukosoa sera za chama alijikita kumkosoa Clinton

Hoja kubwa ya Republican ilikuwa kumuonyesha Clinton katika hoja ya kutoaminika (honest) na maamuzi mabaya (poor judgement). Ndio maana walishadidia sana mambo ya utawala kama Benghaz,emails n.k

Siku mbili za awali zilikuwa na wazungumzaji 'celebrity' ambao kimtazamo ni wa 'low profile'
Kuonekana sana kwa watoto wa Trump kunaeleza ombwe linalotokana na kukosekana watu maarufu

Ilitegemewa mkutano huo uhutubiwe na Marais wastaafu kama Bush wote, wagombea kama McCain, Romney, Rubio, Kasich wenye heshima katika GOP. Pia wapo akina Condoliza, Colin Powell n.k.

Kutokuwepo kwao kulipunguza sana hamasa, na kutoa picha ya kutoafikiana na uteuzi wa Trump
Watu hao wana sehemu kubwa ya jamii inayowaunga mkono, na hiyo ni missed opportunity kwa Trump

Sehemu ya II inaendelea..
 
Sehemu ya II Tathmini

Kitendo cha mkewe Trump kubeba hotuba ya Michelle kilitoa doa.
Melania ana uwezo wa kujieleza na laiti isingetokea, sehemu ya 'first lady' mtarajiwa ingalikuwa na nguvu

Tukio hilo lilifunika sana ujumbe wa wasemaji na kuwa kubwa kuliko tukio zima.

First lady ni mtu anayemjua mgombea, na wengi walitaraji kumsikia akieleza undani wa mwandani wake. Hotuba ya Michelle ikachukua nafasi ya mazungumzo, kosa la kiufundi

Kosa kubwa ni kampeni ilivyo ''handle'' tatizo. Hakukuwa na shaka ya ukweli mtupu, kampeni ilipaswa kukiri na kuomba radhi, au kumfukuza mhusika kama ishara ya kukasirishwa na tukio.

Kampeni ikatumia muda mwingi kuongopa na mwisho wa siku ikakiri.
Katika kipindi cha kuongopa, habari ilifunika mkutano,wazungumzaji kutosikika hoja zao

Picha inayoonekana hapa ni kukosa uaminifu wanaomtuhumu Clinton kutokuwa nao(contradictions). Inaeleza kampeni ilivyo disorganized katika muda wa 'crisis'

Wengi hawataliona, wachache wenye weledi wanalizungumzia katika muktadha mpana.

Baada ya tukio, vyombo vya habari vikizama kutafuta ukweli wa hoja zinazojengwa

Nalo pia lili expose kampeni katika kile kinachosema unnecessary scrutiny

Inaendelea..
 
Sehemu ya III

Sakata la Ted Cruz kama ilivyokuwa la Melania likafunika sehemu ya 2 ya mkutano siku ya 3 na 4
Media zikiwa zimepata 'chakula' , hoja ilikolezwa na Trump katika Tweets.

Trump alipaswa kukaa kimya ili umma uamue kuhusu Cruz na hatua alizochukua kujijenga badala ya kumjenga. Watu maarufu walijitokeza kukemea tabia ya Cruz, sauti zao zikafunikwa na tweets za Trump

Trump ni mzuri sana wa ku-divert attention ya hoja kwa kutumia Tweets.
Kwa bahati mbaya, washauri hawakuona tatizo akiwa mgombea wa Urais.

Hadhi ya Trump kwasasa si kama ya mgombea ndani ya chama.
Ni hadhi ya mtu wa 'oval office' hivyo hupimwa kwa kiwango cha juu' high bar'

Habari ya Ted Cruz ilifunika hoja za VP Mike Pence ambaye wengi walitaka kumfahamu zaidi.

Pence alikuwa na hoja nzito akijionyesha kama mtu atakaye mdi-discipline Trump.
Bahati mbaya, naye alifunikwa na hoja ya Ted Cruz

Hizo ni distractions zilizotokea na kufunika hoja za mkutano mkuu.

Kwa upande mwingine, sintofahamu hizo zilisaidia sana kampeni ya Trump kuondoka katika hoja za waliompinga nje ya ukumbi.

Hapa napo sakata la Meania na Cruz likawezesha 'never' Trump kufutika katika media.

Tofauti ya hali hizo mbili, yaani faida ya sakata la melania na Cruz, na faida za kutoweka kwa never Trump zinaangaliwa kwa mtazamo huu.

1. Melania na Cruz walifunika hoja au agenda katika tukio lililo onekana na watu wengi .
Ina maana kampeni ya Trump haikuwafikia watazamaji kwa mamilioni katika kiwango tarajiwa

2. Kuhusu never Trump, hawa wanaongozwa na imani kuwa Trump hafai. Hivyo reservation zao bado zipo na zitaendelea kama tulivyoona usiku wa jana walipoingia na kumpinga Trump akihutubia

Hasara ni kubwa kuliko faida kwa matukio hayo mwaili

Inaendelea
 
Sehemu ya IV tathmini

Ujumbe wa Mkutano

Kama tulivyoeleza, wazungumzaji walijikita katika kumshambulia mgombea
Hilo ni jema kwa kuonyesha udhaifu wake. Hata hivyo lina tatizo kubwa mbeleni.

Swali, nini ni agenda ya Republican kwa nchi? Inaelezwaje na inatakelezwaje?

Kutokana na maswali hayo, kulijitokeza mambo mengi ya kujichanganya
1. Habari ilionekana kama personal badala ya matatizo ya America
2. Hakukuwa na mbadala wa matatizo yaliyoanishwa
3. Walicheza na Template ya Bernie Sanders,kuvutika katika hoja za Dem kuliko misingi ya Republican

Kumshambulia Clinton kama mtu kulisaidia kuwaunganisha GOP dhidi ya adui yao mmoja, Clinton
Hata hivyo, waliomchukia Clinton kwasababu zao wamebaki na hilo pengine kuimarisha imani zao

Kwa uapnde mwingine, inaonekana kumpa sympathy Clinton kama mtu na mwanamke.
Hoja kwamba, ni mwanamke na Republican hawakubali hilo, inamuongezea 'jinsia' Clinton

Ukiacha kujenga ukuta hakukuwa na hoja nyingine mbadala inayowea kubadili mawazo ya watu
Wanaoamini katika Trump watabaki hivyo, na wasioamini watabaki hivyo

Kilichotakiwa ni maelezo ya kina, ulinzi na usalama wa ndani utafanyikaje, uchumi utakuzwa kwa mbinu gani, na nini falsafa mpya ya siasa za nje za Marekani.

Kutaja law and order kwa matukio ya kuuawa askari, au kumaliza ISIS akiingia madarakani au kufanya deal nzuri za trade, kunaacha maswali na kumfanya Trump awe vulnerable katika details siku za usoni

Ndio maana wachambuzi na waandishi wengi wanauliza, atatekelezaje yale anayoona si sawa?
Kwa maana ya kuwa hakuna details na kuna kujichanganya. Huu ulikuwa udhaifu mkubwa

Tuangalie Republican walivyotumia template ya Bernie Sanders wa Democrat kuimaliza Democrats

Inaendelea
 
Sehemu ya V

Hoja za Bernie Sanders zataumika GOP

Katika uzi huu Uchaguzi Marekani tukisema mwendo wa Sanders katika chaguzi za Democrats na hasira alizojenga pamoja na chuki ni mwiba

Republican wamezitumia zote na kwa wazungumzaji wote

1. Emails ambayo Sanders alitumaini ingemwangusha Clinton sasa inavuma

2. Trade, ambazo Sanders alimtuhumu Clinton sasa zinatumika

3. NGO ambazo Sanders alisema zinapokea pesa 'za magaidi' sasa

4. Kuongeza mishahara ilikuwa hoja ya Sanders, GOP wameinyakua

5. Hoja ya Bengazh alishikia bango, sasa inatumika vema na GOP

6. Hoja ya special interest na pesa za wall street inatumiwana GOP

7. Hoja ya deal la Iran ambayo Sanders hakuipenda, inatumika dhidi ya Democrats

8. Hoja ya rigged system katika uchaguzi, Trump anaitumia dhidi ya Democrats

Katika hotuba yake jana, Trump alifikia mahali pa kumnukuu Sanders moja kwa moja
Aliwataka wafuasi wa Sanders wamuunge mkono ili kuondoa rigged system, kubbadili trade deals n.k.

Mwandishi wa habari Farid Zacharia wa CNN aliwahi kuandika na kusema ' Trump hakuhitaji mgombea mwenza mwingine, Bernie Sanders alitosha' Hicho ndicho kinachotokea

Kwa kuziangalia hoja hizo, Republican wana sababu za kusema, wasemayo yanatoka Dem

Dem na Clinton wana wakati mgumu sana kushawishi umma vinginevyo
Sanders hatameza maneno yake kwa kauli alizotumia mara nyingi na muda mwingi

Kama lipo anguko la Democrats, si kwasababu ya Trump. Ni kwasababu ya 'self distractions'

Inaendelea...
 
Sehemu ya VI

HOJA KINZANI ZA TRUMP NA GOP

Tukio lisilo la kawaida, mwanzilishi wa Paypal,nguli la Silcon Valley Bw Thiel amezungumza akiwa ni Republican na Gay

Ni mara ya pili kwa Gay kuzungumza mkutano mkuu wa GOP akiwa amejitangaza.
Iliwahi kutokea bila kujitangaza hakuzungumzia ushoga kama alivyofanya Thiel

Kwa maneno mengine Republican wanakubali jamii ya LBGT
Hili ni jambo geni katika desperate ya kutaka kuungwa mkono na jamii

Linakuja na gharama zake, kwamba Republican ni evangelical.
Wanaamini katika Ukristo na Evangelical ni sehemu ya wapiga kura wao

Bado suala la LBGT lina utata, kwamba, linakinzana na misingi ya Republican.
Ndivyo lilivyo suala la abortion na marriage

Masuala hayo matatu yanamgusa Trump, ameoa wake 3 kinyume na Evangelical dogma, anaunga mkono(abortion) na ushoga unaopingwa na Evangelicals

Kuna baadhi watamuunga mkono,Republican inatakiwa kuwa 'progressive'.
Tatizo, conservatives watamuona yupo out of touch

Haya yakiibuka one on one ktk midahalo, Trump atakuwa na wakati mgumu.

Itabidi atose kundi moja la Republican, progressive au conservatives
Haya ni makundi yanayojinasibisha sana na Republican katika chaguzi

Swali linabaki, ilishindaje maeneo ya 'Evangelicals' ikiwa ana mauza uza yake? Tutajadili

Inaendelea...
 
Sehemu VII

Hoja ya Trump kuungwa mkono na 'Evangelical' inasimama sehemu moja.
Ameahidi kuondoa sheria inayozuia taasisi za dini kutoa matamko ya kisiasa.

Marekani, taasisi zinazojihusisha na sias hufutiwa misamaha ya kodi, tax exemption na zinawajibika kulipa kama taasisi zingine

Pili, katika uchaguzi wa ndani, hakukuwepo na 'Evangelical' wenye mvuto M. Huckabee na hivyo kutoa mwanya kwa 'chaguo lolote'

Tatu, ile second ammendment ya kumiliki silaha inamsaidia Trump.

Kwamba watu wana haki ya kujilinda na kutumia silaha kwa 'recreational'.
'Evangelical' vijijini na wana miliki silaha. Wanamuona Trump mtetezi wao

Kuelekea uchaguzi mkuu, hoja zitakuwa na kina na hapo pana tatizo

Kama tulivyosema, ni ima abaki na progressive au au aungane na conservatives

UMILIKI SILAHA
Trump anaungwa mkono na NRA taasisi ya umiliki wa silaha.

Hoja yake ni kuwa umiliki wa silaha ni jambo la kikatiba'second amendment '
Kwamba, wanaofanya uhalifu si watu wema wanaomailiki silaha.

Wakati huo huo anaongelea law and order kutokana na matukio ya kuzagaa silaha kali kama zilizotumiwa na wahalifu kufanya mauaji siku za karibuni

Japo hoja yake ina nguvu kikatiba, mabadiliko ya usalama yana favor mtazamo mpya
Republican wamekataa hoja iliyopelekwa bungeni kuhusu udhibiti wa silaha

Ikitokea Democrats wakajenga hoja,usalama hafifu unaotokana na kuzagaa silaha, Trump itababidi aeleze law and order ataitekeleza vipi.

Suala la law and order, immigration, na Ugaidi yana matatizo kutokana na maelezo ya Trump. Kwa jinsi alivyoeleza, hoja zake zinazidi kutenga makundi katika jamii.
Tutajadili

Inaendelea
 
Sehemu VIII

GOP wamengelea sana kusimama na askari, na kuonyesha udhifu huo unatokana na serikali ya Obama
Trump anataka kurejesha law and order kwa kuweka mwendesha mashtaka mahiri kwa mujibu wake

Katika racial tension iliyopo, anawezaje kurudisha law and order?
Kauli yake ililenga balck lives matter, kwani GOP wanasema blue lives matter

Itachukuliwa na makundi ya 'colored people' kuwa madai yao mbele ya Trump hayana maana

Immigration
Trump ana hoja hasa kuzingatia mauaji yanayotokea Duniani, iwe US, Paris, Belgium na Leo Munich

Hoja yake inapata nguvu mbili kubwa
1. Kwamba, kuchukua wahamiaji kuzingatie back ground check na mfumo wa Uhamiaji
2. Ametumia hofu iliyotanda kujaza hofu kwa kueleza zaidi

Trump amebadili msimamo wa kuzuia Waislam.
Alichosema jana ni kuwa watu wanaotoka mataifa yenye Ugaidi ndio watakaozuiliwa.

Katika kauli zake alisema' those who share our values' Hapa alimaanisha value za imani

Hoja yake in anguvu pia, kuwa kama wapo wasiotaka maisha ya magharibiwasikaribishwe
Na mtazamo wa watu wengi ni huo, bila kujali kuwa mamilioni ya watu hao ni wema

Kwa kauli 'to share our values' evangelical watamwelewa, watu wa rangi hawatamwelewa

Tayari anapata maswali, je, msimamo wake umeyumba? flip flop?

Msimamo wake mpya ni kama ule wa kujenga ukuta. Tutajadili

Inaendelea....
 
andersoncooperciaspokesman.png

Wakati tunaendelea kufanya tathmini ya yaliyotokea Cleveland, hebu tuchungulie kidogo huko Philladelphia tutegemee nini kuanzia Jumatatu hii ijayo. Ingawa hivi leo Clinton anategemewa kumtaja mgombea mwenza wake, kwa kauli mbiu ya love trumps hate tayari mwelekeo wa Democrats umejionesha.

love-trumps-hate.jpg


Love Trumps Hate...bila kujali rangi, jinsia, dini...​
 
Breaking News: Presumptive Democratic nominee for President, Hillary Clinton, has picked Tim Kaine, a former Governor for Virginia, as her running mate.

750x422
 
CLINTON ACHAGUA MGOMBEA MWENZA

Tukielekea Philadelphia Jumatatu, kilichosuburiwa kimetimia
Kama tulivyoeleza habari itakuwa ni mgombea mwenza wa Clinton

Ni Timoth Michael Kaine(Tim) junior senator wa Virginia ambaye pia aliwahi kuwa gavana wa jimbo hilo. Ni mzaliwa wa Minnesota.

Kaine ni kiongozi alianzia ngazi ya udiwani, Umeya. Luteni jeneral, Gavana , Seneta na sasa mgombe wa makamu wa Rais

Kisiasa ni progressive. Kitaaluma ni mwanasheria kutoka Havard ambaye pia alikuwa lecturer katika shule ya sharia ya Richmond

Kaine atatambulishwa rasmi kesho kule Miami.
Ilikuwa itokee leo , kutokana na tukio la Munich ilibidi iahrishwe.

Tukio hili ni sawa na la Trump kumtambulisha Pence na kuingiliwa na shambulio la Paris

Kumtambulisha Miami kuna umuhimu wa kisiasa.

Na kumchagua kutoka Virginia, pamoja na sifa nyingi kuna umuhimu wa kisiasa

Tutaendelea kuwajuza
 
Mkuu Nguruvi3 unafanyakazi nzuri sana kutupasha yanayojiri ktk uchaguzi huu unaofuatiliwa Dunia nzima! Umejitahidi pia kufanya uchambuzi vizuri kuhusu mkutano mkuu wa GOP ingawa uchambuzi umeegemea sana upande wa wakosoaji wa Donald Trump badala ya uchambuzi wa hoja..!! Ngoja tusubiri mkutano wa Democrat ndo tutafanye uchambuzi wa kina. Zaidi sana bado nawafuatilia sana!! Nguruvi3 na Mag3
 
Mkuu Nguruvi3 unafanyakazi nzuri sana kutupasha yanayojiri ktk uchaguzi huu unaofuatiliwa Dunia nzima! Umejitahidi pia kufanya uchambuzi vizuri kuhusu mkutano wa mkuu GOP ingawa uchambuzi umeegemea sana upande wa wakosoaji wa Donald Trump badala ya uchambuzi wa hoja..!! Ngoja tusubiri mkutano wa Democrat ndo tutafanye uchambuzi wa kina. Zaidi sana bado nawafuatilia sana!! Nguruvi3 na Mag3
Usiwe na shaka magode, sisi ni binadamu na hakuna binadamu asiye na mapungufu...kwa ufahamisho tu huu uzi hauko mahsusi kwa Nguruvi3 au Mag3, yeyote anaweza kuchangia pamoja na wewe. Kwa kusema uchambuzi umeegemea sana upande wa wakosoaji wa Donald Trump, umeonesha kwamba na wewe ni mfuatiliaji mzuri tu wa hizi harakati za uchaguzi Marekani. Kwa hilo tupo pamoja sana ndugu yangu na karibu sana.

Hata hivyo naomba uwe huru kukosoa pale unapodhani pamekosewa na kwa bahati uhuru wa JF haukutakiwa kuwa na mipaka ingawa karibuni pameanza kujitokeza hali tofauti. JF imeanza kuwekewa mipaka ambayo miaka ya nyuma hatukuishuhudia na hili jambo limeanza kutusononesha tulioamini kwamba JF is where we dare. Upo usemi kwamba the guilty always feel insecure whenever the truth starts to show signs of refusal to stay buried.

Wiki hii ilikuwa ni ya GOP na Donald Trump na kuanzia Jumatatu ijayo itakuwa ni ya DNC na Hillary Clinton. Kwa kweli siasa ya Marekani iko karne nyingi mbele ya siasa zetu na kwa bahati mbaya hapa Tanzania tofauti hii inazidi tu kupanuka kila leo. Yako mengi ya kujifunza yanayoendana na dunia ilipo na ilikotoka na ukweli ni kwamba, kuwa Raisi katika nchi kama Marekani hakumgeuzi binadamu kuwa mungu-mtu kama ilivyo hapa kwetu, hapana, anakuwa mtumishi. Tuendelee...
 
Mkuu Mag3 ahasante kwa ufafanuzi hapo juu. Niongeze kidogo kwa Mkuu magode . Tulianza na Republican na tunaleta in real time kama wasemaji wanavyohutubia.

Tunaangalia hoja kama maoni kutokana na yanayosemwa. Kwa Trump, kama amekuwa na 'controversies' ambazo huamsha curiosity isiyo ya lazima.

Kwa mfano, alisema uhalifu umeongezeka kuliko wakati mwingine wowote. Well, takwimu zinaonyesha umepungua kuliko wakati wa Reagan au Bush alipomwachia Obama. Hili kwa upanda wake linapoteza zile hoja zake bila sababu

Lakini pia ukifuatilia ,tumeonyesha hoja za trump zenye nguvu.

Lengo ni kuelekea November tuweze na weledi electral colleges zitakavyokuwa

Kama livyosema Mag3 ni ukumbi huru na tutafarajika kusikia maoni tofauti ili sote tuchangie na kujifunza kutoka siasa zilizokomaa, zilizojaa mbinu na zilizo na tija.

Tafadhali , jisikie huru na unakaribishwa kwa maoni na mtazamo sote tupate manufaa. Palipo na mushkeli usiiste kuonyesha kwa uwazi, sisi sote ni wanadamu tusio na utimilifu kama alivyosema Mag3

Democrats convention inaanza kesho, tayari kuwa distractions zimetokea

Inafuata
 
MKUTANO MKUU WA DEMOCRATS (DNC)

Kesho mkutano mkuu wa DNC unaaza. Huo ndio utakaomthibitisha Hillary Clinton kama mgombea Rasmi kama ilivyokuwa kwa Trump na RNC

Mkutano wa RNC uligubikwa kwa 'distractions' kama ile ya Mealania Trump kukopi hotuba ya Michelle Obama. Kisha nusu ya pili ya mkutano, Ted Cruz akaja na yake. Mkutano ukawa umepoteza ujumbe kwa sehemu kubwa

Mzimu huo haujaishia kwa Trump, kwasasa Clinton hata kabla ya kuanza mkutano tayari amepata tatizo katika kampeni yake, 'kashfa ya emails'

KASHFA YA EMAILS
Hapa ieleweka zipo aina mbili, email akiwa secretary of state.
Leo kuna emails ambazo zimeibuliwa jioni ya leo zikimhusisha mwenyekiti wa DNC Debbie Wasserman

Mwenyekiti amelazimika kujiuzulu nafasi zake kutoka na emails hizo ambazo zilikuwa na kauli 'zenye ukakasi'

Habari iliyopo mbele ya vyombo vya habari jioni na usiku wa jana ni kuhusu suala hilo badala ya ku focus katika waongeaji na nini wataongea siku zijazo
Hili limeharibu sana maandalizi ya mkutano mkuu

Kuna nadhari mbili kuhusu hili suala
Russia: Msemaji wa kampeni ya Clinton anadai hackers wa Russia ndio wameibua hizo emails ili kumsaidia Trump!

Bernie Sanders: Ipo nadhari inayosema, haya yalikuwa maandilizi ya Sanders endapo uchaguzi ungekwenda DNC kama ilivyotaka. Wachambuzi wanasema, email za awali zingechanganywa na hizi katika kubadili wajumbe

Ieleweke hizi ni nadharia za pundits, na hakuna anayejua kwa uhakika nini kimetokea, ingawa ni kweli emails hizo zipo na zimesababisha mtafaruku katika kampeni.

Madhara ya suala hili kwa Democrats na Clinton
1. Kupoteza msisimko na focus ya mkutano
2. Silaha njema kwa Donald Trump
3. Mgawanyiko mkubwa utakaoamsha vidonda vinavyopona

Tutafafanua
 
KUJUIZULU KWA Ms.WASSERMAN

Democrats wamefanya damage control mapema kwa kumshinikiza Ms Wasserman ajiuzulu. Licha ya kujiuzulu,ameonekana ukumbini akiendelea na maandalizi ya mwisho

Habari hii haimgusi Bi Clinton moja kwa moja kama mhusika.
Inamgusa kupitia maandalizi ya mkutano,kampeni na distractions zinazoambata nalo

Bado details za nini kimetokea zinasubiriwa, lakini ni mpango mahususi kuamkia siku muhimu kwa Democrats

Nani anahusika, linabaki swali, tunaona siasa zikiwa na timing! 'mchezo mezani'

Madhara kama tulivyoeleza bandiko la hapo juu yapo katika maeneo haya

1. Kupoteza Focus: Habari iliyotanda imefunika mkutano mkuu kwa siku nzima.
Na haineokani kama itapotea siku za karibu.

Hii inaweza kuwa kibwagizo na pengine kati kati ya mkutano yakatokea makubwa

Kesho anaongea Michelle Obama na Benie Sanders miongoni mwa wengi.

Ilitarajiwa wa set tome ya mkutano, kinyume chake emails zimechukua nafasi.
Hili ni pigo kubwa kwa kampeni ya Clinton

2. Trump apata silaha: Kama anavyomwita crooked Clinton na sasa hili linahusu Democrats, Trump atasema Sanders hakutendewa wema a system ipo rigged.

Hili atalifanya kila siku na athari zake ni kama namba 1 hapo juu
Lengo ni kuwavuta wafuasi wa Sanders ambao bado wana uchungu na chaguzi

3. Vidonda kuvuja damu: Sanders amesha mui endorse Clinton,tofauti na Cruz aliyesababisha timbwili bila endorsement.

Hata hivyo Sanders alisema Bi Wasserman anampendelea Clinton katika hatua za awali

Hoja ya Sanders ililenga kumshinikiza Wasserman akubali wazo la kuwa na chaguzi kwa taratibu anazotaka. Kwamba, kwenye closed elections, zifanywe open.

Hii ni kwasababu aliamini kushinda katika open na si closed. wasserman alikataa

Hoja ya pili,'super delegates' wasihesabiwe kabla ya mkutano mkuu,nalo lilikataliwa

Hoja ya wasserman ilikuwa kuwa, kubadili kanuni mchezo ukiendelea halikuwa jambo la haki. Kwamba, Sanders alifahamu taratibu, akazikubali na ku sign

Sasa, hili la emails Sanders anasema. 'alishasema hatendewi haki'
Na kwavile zime leak, hakuna atakayejali ni haki gani hakutendewa bali kuona hakutendewa haki tu.

Wafuasi wake wenye machungu wataamka kwa hasira na litawagawa democrats.
Trump atakapoisukuma hoja hiyo, hasira na vidonda vilivyoanza kupona vitaibuka upya.

Nini kitatokea Sanders atakapoongea kesho haijulikani.
Je, atamwaga mboga kama Cruz? Atafanikiwa kushawishi wafuasi wapuuze suala hili?

Ikizingatiwa wafuasi wa Sanders walikuwa waandamane kudai sera ya dollar 15 kwa saa kama kima cha chini, huenda kesho kukawa na maandamano zaidi

Katika fukuto hilo democrats wapo katika mtafaruku pengine mkubwa kuliko wa Trump. Tusubiri nini kitatokea

Tutawaletea habari za mkutano in 'real time' mambo yakienda kama tunavyotaraji

Tusemezane
 
Back
Top Bottom