Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

TRUMP 'AACHANA NA REPUBLICAN'

WIKILEAKS YATOA Emails

Trump ameeleza alichokiita 'kufunguliwa pingu' na kwamba sasa anakwenda 'solo'

Hayo yanatokea baada ya Spika Paul Ryan kutangaza kutoshiriki katika kampeni yake

Wakati huo huo, mwenyekiti wa RNC Bw Priebus ameeleza kuendelea kumuunga mkono

Hali hii imezidi kuleta kiwewe miongoni mwa Democrats kwani si kawaida kutokea

GOP wamegawanyika wakiwemo wanaomuunga mkono Trump na wanaokataa

Kwa upande wa Democrats na Hillary, Wikileaks wametoa mzigo mwingine wa emails

Hakuna kilichoonekana kizito kwa kuathiri kampeni. Ni mawasiliano ya ndani tu

Tutakumbuka DNC walilalamika emails zao kuwa hacked siku za nyuma

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, Donald Trump ametangaza vita dhidi ya chama chake na haya ndiyo mashambulizi yake ya mabomu (tweets) baada ya uamuzi wa Spika Ryan...

1. It is so nice that the shackles have been taken off me and I can now fight for America the way I want to.

2. Our very weak and ineffective leader, Paul Ryan, had a bad conference call where his members went wild at his disloyalty.

3. Despite winning the second debate in a landslide (every poll), it is hard to do well when Paul Ryan and others give zero support!

4. The very foul mouthed Sen. John McCain begged for my support during his primary (I gave, he won), then dropped me over locker room remarks!

5. Disloyal Republicans are far more difficult than Crooked Hillary. They come at you from all sides. They don’t know how to win - I will teach them!

6. With the exception of cheating Bernie out of the nom the Dems have always proven to be far more loyal to each other than the Republicans!

Na bado anaendelea na tweet zake na leo hatalala kabisaaa...tweets mpaka asubuhi! Jamaa anapigana kufa na kupona (life or death) na asipoupata Urais anaweza akameza sumu.
 
TRUMP NA TWEETS

Ukisoma moja ya tweets bandiko la Mag3, utaona anakiri wazi 'it's hard...with zero support

Wengi wanajiuliza kwanini Republican wana mtosa mtu wao?

Well, GOP wana tatizo na kundi la wanawake na watu wa rangi siku nyingi

Jitihada zao ilikuwa kuyaleta makundi haya yaliyopoteza imani.

Kauli za Trump zinaelekea kuyafukuza makundi na si kuyaleta

Pili, kuna uchaguzi wa maseneta na wabunge. Hawa hukumbana na maswali ya wapiga kura wao yakimhusisha Trump. Wameona ni vema wajitoe hadharani kuliko kujibu pembeni ikawagharimu

Tatu, kwa Paul Ryan , huyu ana future kama ilivyo kwa Mike Pence.

Naye kwa kutazama siku za usoni, anaona ni vema rekodi yake ibaki safi

Mike Pence anaogopa kumtosa Trump. Anafahamu, pamoja na mambo yote Trump ana wafuasi

Kumtosa sasa hivi ni kulitosa kundi muhimu siku za mbeleni.

Ni kundi muhimu kwa sabababu ni ''real right wing''. Pence anaamini ni rahisi kuleta makundi mengine yaliyo katika mtafaruku na Trump kuliko kulileta kundi la far right siku atakapolihitaji
 
Kulingana na Trump, hakuna hata haja ya uchaguzi...kashinda tayari!​

CubfzaBVMAAXabD.jpg:large

Donald Trump hana tofauti na Alnacha...ni mapacha na ndoto zao zafanana!
Hizo polls za Breitbart ndizo anazoziamini na kuzitumia...
  1. Donald Trump...93%
  2. Hillary Clinton...7%

Trump on the Commission for Presidential Debates: It’s a ‘Rigged Deal’ and ‘I’m Done’

Donald Trump blasted the Commission for Presidential Debates on Wednesday, claiming the bipartisan group is “rigged” and declaring himself “done” with it.

“The head guy worked for Bill Clinton. Ay yai yai. What a rigged deal this is,” Trump said at a rally in Florida. He was referring to CPD co-chair Mike McCurry, who served as Clinton’s press secretary for three and a half years. What Trump did not mention is that McCurry’s co-chair is Frank Fahrenkopf, chairman of the Republican National Committee while Ronald Reagan was president.

Trump went on to suggest that he might skip the third debate, scheduled for October 19 in Las Vegas. “I have no respect for that group, by the way, I’m done,” he said of the CPD. Trump spokesperson Jason Miller told the Daily Beast’s Olivia Nuzzi that Trump does, in fact, plan to participate in the third debate.

Trump’s debate diatribe also included mention of the recent allegations that Hillary Clinton was fed a question by current DNC head Donna Brazile before a CNN town hall during the Democratic primary. “Oh man, why can’t the Republicans do that?” he joked. “Why can’t Reince feed me information prior to a debate? I am so angry at the Republicans. I want to be fed information like Hillary gets.”

Trump on the Commission for Presidential Debates: It’s a ‘Rigged Deal’ and ‘I’m Done’

Huyu jamaa kachanganyikiwa sasa...
 
TRUMP NA SAKATA LA WANAWAKE

MBINU ZA 'PRIMARIES' ZINAONEKANA KUTOFANIKIWA

Wiki nzima imetawaliwa na mjadala wa wanawake wanaotuhumu kutenda visivyo na Trump siku za nyuma

Wengi wanajiuliza iwapo hayo yalitokea miaka 10, 20 au 30 kwanini wanawake hao wayaseme leo?

Tatizo lilianza kwenye mdahalo wa pili wiki iliyopita.

Kuelekea mdahalo huo Trump alikuwa na tuhuma za video iliyodhalilisha wanawake kwa maoni yao.

Moderator Anderson Cooper wa CNN alimuuliza Trump endapo aliwahi kufanya aliyoyasema katika video.

Trump alikanusha na kusema hayo ni maneno ya locker room

Kauli ya kukanusha imeibua wanawake 8 kutoa ushuhuda wakisema alivyowatendea

Wanawake hao wanajitokeza kama reaction ya jibu la Trump kuthibitisha alichotenda

Kuanzia wakati huo maongezi ni juu ya wanawake na anapoteza kuungwa mkono nao

MBINU
Katika chaguzi za awali ndani ya Republican , Trump alikuwa na mbinu ya kubadili mijadala anapokumbana na hali asiyoitaka.

Tunakumbuka alivyomwita Heid Mkewe Ted Cruz kwa kumlinganisha na mkewe Melania

Mbinu kubwa iliyowabwaga Republican ni kubadili maongezi mambo yakiendea kombo

Katika uchaguzi mkuu, tulijadili, mbinu hiyo ni vigumu kufanya kazi. Ni wagombea wawili tu

Baada ya wiki ya dhahma ya akina mama, Trump ametumbukiza vibwagizo kubadili mwelekeo

Amenukuliwa ''uchaguzi utaibiwa, hana Imani na taasisi inayoandaa midahalo, hatashiriki mdahalo wa tatu''

Akingia katika malumbano na GOP,, ofisi za GOP N.Carolina kushambuliwa.

Amefikia mahali pa kusema mtuhumu wake si chaguo lake la kwanza kama ingalitokea akimaanisha 'hamfai

Yote hayo yanawezaonekana kama ni mambo ya 'kipuuzi'. Hapana! Trump anajua anachofanya, na lengo ni kuua mjadala wa wanawake unaomwelemea. Kwa bahati mbaya mbinu zake za awali zimeshindwa

Kinyume chake, sasa anaonekana kupoteza mwelekeo hata kufikia Republican kusema bila kificho

Kampeni yake inakwenda kwa jinsi anavyojua yeye na hali haionekani kuwa shwari kwa upande wake

Tusemezane
 
Email za wikileak, tupende tusipende, zina madhara kwa HRC. Nadhani ndiyo maana chama kimechukua hatu kukata link ya Assange na ulimwengu kupitia Internet.

Julian Assange's internet link has been intentionally severed by a state party - WikiLeaks

Mkuu vipi kuhusu tuhuma za Trump dhidi ya HRC kuwa anafanya "doping "? .Kudhibitisha ,Trump kasema wapimwe utumiaji madawa kabla ya mdahalo wa mwisho. Testesi zilizopo ,DEMO wanapanga kujitoa kwenye mdahalo huo wa mwisho. Huoni sasa Trump mbinu yake ya kubadili mjadala inaweza kufanya kazi mara hii tena kwa ufanisi?
 
Emails zilizopitiwa ni maelfu na kikubwa ni mawasiliano ya ndani na mikakati ya kampeni.
Impact ni ku reveal mambo ambayo huenda yangeudhi baadhi wa Dem ndani ya chama.

Hadi sasa hakujaonekana lolote kubwa

Utakumbuka, email zilizopokuwa 'hacked' Dep of state, DOJ, FBI waliingilia kati si kwasababu ya uchaguzi bali usalama.

Walisema kitendo hicho ni cha ku influence uchaguzi wa US kutoka nje

Watuhumiwa wa kwanza walikuwa Snowden na Assange ambapo sasa ni Assange

Swali wanalojiuliza ni uwezo wa watu hao kupenyeza katika system ya serikali.

Huko nyuma walishatoa siri za serikali kutoka State dept.
Hivyo kuingilia kati ni katika usalama wa US kwa ujumla na wala Democrats hawana uwezo wa kufanya kazi za FBI na Agency zingine.

Endapo Trump angekuwa makini, pengine emails chache zingekuwa mazungumzo.

Kama unafuatilia, distractions anazofanya zinabadili mwelekeo wa mazungumzo

Impact ya emails ni katika 'suppression' ya wapiga kura, lakini wangapi wana access na muda wa kusoma 12,000 plus emails?

Na katika hali anayoonyesha Trump ni lipi kubwa at least kwa mtazamo wa voters?

Kuhusu Doping, haya ndiyo mambo tunayosema yanamvuruga wenyewe.

Hili alilisema katika jitihada za kubadili maongezi kuhusu wanawake.

Hata hivyo linachukua sura nyingine.
Kuna tangazo ametoa likionyesha Hillary alipokuwa anaingia katika gari siku alipoumwa

Ilitegemewa tangazo lile lingekuwa na impact na kubadili mwelekeo. Halikufanikiwa

Anaposema 'doping' amelenga kuonyesha siku alipotaka kuanguka na kwamba ilikuwa ulevi

Siasa za US zipo tuhuma zinazoweza kuwa serious zikitolewa na mtu mwenye heshima

Kwa mfano, tuhuma za doping zingetolewa na mtu mwingine zingekuwa maongezi, kwa Trump na kauli za wiki nzima, inaonekana ni kuhangaika tu.

Tuhuma hizo na rigged election zinatofauti gani?

Inposemwa fulani afanye doping test, lazima kuwe na sababu za kuridhisha

Trump aliyeshindwa kutoa Tax leo anaomba doping!

Habari kuwa Dem wanataka kujitoa katika mdahalo sijazipata at least kwa kupitia vyombo vyote vikubwa vya habari.

Hizi zingechukua uzito sana labda kuna nisilolifahamu.

Unaweza kutusaidia japo source moja ya wapi Dem wamesema watajitoa katika mdahalo?
 
.
-----
Unaweza kutusaidia japo source moja ya wapi Dem wamesema watajitoa katika mdahalo?
Fact: Trump alikuwa anazungumzia kuishiwa nguvu Hillary Clinton mwishoni mwa mdahalo wa pili.
********
'Athletes, they make them take a drug test right?' Trump mused. 'I think we should take a drug test prior to the debate.'

'Why don't we do that? We should take a drug test prior, because I don't know what's going on with her, but at the beginning of her last debate, she was all pumped up at the beginning, and at the end it was like, "Oh, take me down,"' Trump said, doing an impression of Clinton. 'She could barely reach her car. So I think we should take a drug test. Anyway, I’m willing to do it,' Trump said

source: Dailymaill
********

Ushahidi huu:
============
David Axelrod, one of President Barack Obama's top strategists, floated the idea that maybe Hillary Clinton should skip the final presidential debate.

'Drug testing?!? You have to wonder if @HillaryClinton will/should reconsider next debate, given the depths to which this has sunk,' the political operative who helped Obama get to the White House twice tweeted Saturday.

SOURCE:David Axelrod suggests Hillary Clinton SKIP final debate over Trump's drug test suggestion | Daily Mail Online
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Clinton kwa unipolar yake ya kutete hegemony ya Marekani duniani; atasababisha US kuanguka vibaya sana. Akianzisha vita na Russia, nchi inayoungwa mkono na nchi nyingi zinazochukia ubabe wa US kwa nchi nyingine kiuchumi, kisiasa na kitamaduni; vita itaimaliza kabisa US. Russia anathamini sana sana multipolar kwenye masuala yote kwa ajili ya kudumisha amani duniani. Ni kwa sababu hii na nyingine ninashauri US wamchague the Trumps ambaye atasaidia kuangamiza US taratibu na bila madhara makubwa kwa ulimwengu kuliko Hillary atakayeingamiza US kwa fujo na haraka kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa ulimwengu. Kinachonishangaza ni kwa nini vyombo vya usalama vinamkingia kifua namna hii huyu mama (FBI releases Clinton probe documents)

yangu ni hayo.
 
Ushahidi huu:
============
David Axelrod, one of President Barack Obama's top strategists, floated the idea that maybe Hillary Clinton should skip the final presidential debate.

'Drug testing?!? You have to wonder if @HillaryClinton will/should reconsider next debate, given the depths to which this has sunk,' the political operative who helped Obama get to the White House twice tweeted Saturday.

SOURCE:David Axelrod suggests Hillary Clinton SKIP final debate over Trump's drug test suggestion | Daily Mail Online.
Mkuu Axelrod ni political pundit hana wadhifa katika kampeni.

Pili, tweet siyo kitu official na mtu yoyote anaweza kutumia. Je, ndio ukweli?

Muhimu sana katika lugha kuna kitu kinaitwa semantic.

Nadhani uliposoma hiyo tweet hukuendelea kusoma kwa 'semantic'.
ukaisoma kama habari kamili, rudia kuisoma unaweza kuelewa kitu

Mkuu kwa hili kwakweli sijadili
Source yake ni sawa tu na Nguruvi a tweet Hillary ni mwendawazaimu na ukaamini !
 
Ushahidi huu:
============
David Axelrod, one of President Barack Obama's top strategists, floated the idea that maybe Hillary Clinton should skip the final presidential debate.

'Drug testing?!? You have to wonder if @HillaryClinton will/should reconsider next debate, given the depths to which this has sunk,' the political operative who helped Obama get to the White House twice tweeted Saturday.

SOURCE:David Axelrod suggests Hillary Clinton SKIP final debate over Trump's drug test suggestion | Daily Mail Online
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Clinton kwa unipolar yake ya kutete hegemony ya Marekani duniani; atasababisha US kuanguka vibaya sana. Akianzisha vita na Russia, nchi inayoungwa mkono na nchi nyingi zinazochukia ubabe wa US kwa nchi nyingine kiuchumi, kisiasa na kitamaduni; vita itaimaliza kabisa US. Russia anathamini sana sana multipolar kwenye masuala yote kwa ajili ya kudumisha amani duniani. Ni kwa sababu hii na nyingine ninashauri US wamchague the Trumps ambaye atasaidia kuangamiza US taratibu na bila madhara makubwa kwa ulimwengu kuliko Hillary atakayeingamiza US kwa fujo na haraka kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa ulimwengu.

yangu ni hayo.
Pengine leo internet yangu ikitengamaa nitaweza kuchangia kikamilifu lakini duh jitegemee! Wewe ungefaa sana kuwa msemaji wa Donald Trump [emoji1][emoji1][emoji1].

Asange anayo matatizo ya siku nyingi na serikali ya Obama. Ni kwa sababu hiyo hadi leo kaikimbia nchi yake na kujifungia ubalozini Equador mjini London.

Siyo Marekani tu inamtafuta, hata nchi yake Sweden anatafutwa kwa kosa la jinai. Asange anajulikana kama a fugitive from justice na kwa Trump kampata mshikaji wanayeendana.
 
Clinton kwa unipolar yake ya kutete hegemony ya Marekani duniani; atasababisha US kuanguka vibaya sana. Akianzisha vita na Russia, nchi inayoungwa mkono na nchi nyingi zinazochukia ubabe wa US kwa nchi nyingine kiuchumi, kisiasa na kitamaduni; vita itaimaliza kabisa US. Russia anathamini sana sana multipolar kwenye masuala yote kwa ajili ya kudumisha amani duniani. Ni kwa sababu hii na nyingine ninashauri US wamchague the Trumps ambaye atasaidia kuangamiza US taratibu na bila madhara makubwa kwa ulimwengu kuliko Hillary atakayeingamiza US kwa fujo na haraka kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa ulimwengu. Kinachonishangaza ni kwa nini vyombo vya usalama vinamkingia kifua namna hii huyu mama (FBI releases Clinton probe documents)yangu ni hayo.
Hapa kuna maswali

1. Nitajie Rais mmoja tu wa Marekani aliye waive US hegemony akiwa Oval Office

2. Nini foreign policy ya Hillary Clinton?

3. Ni ipi Foreign policy ya Trump?
 
Mkuu Axelrod ni poltical pundit hana wadhifa katika kampeni.
Pili, tweet siyo 'official' document or ' a stand of any well established org'

Muhimu sana katika lugha kuna kitu kinaitwa semantic.
Nadhani uliposoma hiyo tweet hukuendelea kusoma kwa 'semantic'. ukaisoma kama habari kamili

Mkuu kwa hili kwakweli sijadili maana source yake ni sawa tu na Nguruvi aandike Hillary ni mwendawazaimu na ukaamini. Mkuu niwie radhi , sijadili kwakweli!
Red: Yamekuwa hayo mkuu? Hivi Dailymaill watakuwa nao wanatuchezea shere kujadili msimamo wa mtu wa karibu wa Obama aliouto akupitia Tweeter,? Mkuu, au kwa sababu HRC ndiye muhanga wa msimamo huo? Nimeuliza maswali yote haya kwa sababu hapo juu kwenye uzi huu ulijenga hoja juu ya udhaifu wa waRepublican kwa kutumia ushahidi wa tweet.

TRUMP NA TWEETS

Ukisoma moja ya tweets bandiko la Mag3, utaona anakiri wazi 'it's hard...with zero support

Wengi wanajiuliza kwanini Republican wana mtosa mtu wao?

Well, GOP wana tatizo na kundi la wanawake na watu wa rangi siku nyingi

Jitihada zao ilikuwa kuyaleta makundi haya yaliyopoteza imani.

Kauli za Trump zinaelekea kuyafukuza makundi na si kuyaleta.....
 
Red: Yamekuwa hayo mkuu? Hivi Dailymaill watakuwa nao wanatuchezea shere kujadili msimamo wa mtu wa karibu wa Obama aliouto akupitia Tweeter,? Mkuu, au kwa sababu HRC ndiye muhanga wa msimamo huo? Nimeuliza maswali yote haya kwa sababu hapo juu kwenye uzi huu ulijenga hoja juu ya udhaifu wa waRepublican kwa kutumia ushahidi wa tweet.
No no! Kwakweli tunahitaji credible source, ndiyo maana nimeomba.
Tweet ya Axelrod! Hapana mkuu, tafuta nyingine. Huyu ni afisa wa juu wa Obama, ukisoma tweet yake kwa semantic, anachosema ni hivi, kama ya kujadili ni doping kuna haja ya mdahalo?
Halafu ukaichukua na kuifanya ni source ya Democrat! please

Hebu tuwelee kipande cha Daily mail tusome
 
Hapa kuna maswali

1. Nitajie Rais mmoja tu wa Marekani aliye waive US hegemony akiwa Oval Office

2. Nini foreign policy ya Hillary Clinton?

3. Ni ipi Foreign policy ya Trump?
Mkuu, ni kiri kuwa kwa muda huu siwezi kukupa jibu sahihi la maswali yako. Maana yanahitaji back up yenye uzito.
 
Mkuu, ni kiri kuwa kwa muda huu siwezi kukupa jibu sahihi la maswali yako. Maana yanahitaji back up yenye uzito.
Sasa kama huna ''back up'' unawezaje kuzungumzia hegemony ya US?

Na umepata wapi mawazo kuwa kati ya wawili mmoja ana 'unipolar' na mengine uliyosema?

Kama huna idea ya foreign policy za wawili hao, unawezaje kuzungumzia misimamo yao duniani?
 
Pengine leo internet yangu ikitengamaa nitaweza kuchangia kikamilifu lakini duh jitegemee! Wewe ungefaa sana kuwa msemaji wa Donald Trump [emoji1][emoji1][emoji1].

Asange anayo matatizo ya siku nyingi na serikali ya Obama. Ni kwa sababu hiyo hadi leo kaikimbia nchi yake na kujifungia ubalozini Equador mjini London.

Siyo Marekani tu inamtafuta, hata nchi yake Sweden anatafutwa kwa kosa la jinai. Asange anajulikana kama a fugitive from justice na kwa Trump kampata mshikaji wanayeendana.
RedItalic: Trump ana sense of humor ukilinganisha na yule mama. Hata hivyo ana matatizo yake kama binadamu ambayo sidhani kama ni hatarishi sana kwa ulimwengu ka ya yule mama. Trump can easily be rehabilitated ukilinganisha na yule mama ambaye kuomba msamaha tu kwake ni shida.
Facts(red): Assange ni raia wa Australia na si wa Swedeen.
 
Sasa kama huna ''back up'' unawezaje kuzungumzia hegemony ya US?

Na umepata wapi mawazo kuwa kati ya wawili mmoja ana 'unipolar' na mengine uliyosema?

Kama huna idea ya foreign policy za wawili hao, unawezaje kuzungumzia misimamo yao duniani?
Mkuu unajua mimi ninajifunza mengi kutoka kwako? Hapo mkuu ulitakiwa uniweke sawa mimi mwanafunzi wako kwamba hapa hii iko hivi na hivi. Mkuu kumbuka mimi ni mwanafunzi wako ingawa naweza kuonekana nauliza maswali au natoa hoja ambazo zina utata. Na kudhibitisha hili nikasema nisije nikamuabisha mwalimu wangu lazima niende 'chimbo' ndipo nakapojibu maswali yako matatu. Mwalimu kumradhi kama nimekukwaza. Nahitaji elimu yako sana. I am sincerely serous. Sitanii.
 
Back
Top Bottom