Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Mkuu nimeweka link inayokupeleka kwenye dailymaill moja kwa moja (Post [HASHTAG]#370[/HASHTAG])
(Yawezekana nimepisha na semantic iliyotokana na hiyo tweet)
Axelrod was shocked that Donald Trump called for 'drug testing?!?' of Hillary Clinton, which the nominee said this weekend in New Hampshire The Obama adviser suggested Clinton pulling out 'given the depths to which this has sunk'

Kiswahili, tafsiri isiyo rasmi
Alexrod alishtushwa kwamba Trump ametoa wito wa 'kufanywa test ya madawa'? kwa Hillary ambayo mgombea Trump amesema mwisho mwa wiki New Hampshire

Mshauri huyo wa Obama ameshauri Clinton ajitoe kwa kuzingatia kina cha ''chini kilichofikiwa''
 
Facts(red): Assange ni raia wa Australia na si wa Swedeen.
Ni kweli Assange ni raia wa Australia ila huko Sweden anatuhumiwa kwa kuwakamata wanawake kwa nguvu, makosa yale yale ya Trump...kumbuka birds of a feather flock together!

Pona yake Assange ni Trump kushinda Urais kitu ambacho hakitawezekana. Clinton atakapotangazwa Rais, asubiri tu maumivu na ndiyo maana halali akimpigania pacha wake Trump!
 
Ni kweli Assange ni raia wa Australia ila huko Sweden anatuhumiwa kwa kuwakamata wanawake kwa nguvu, makosa yale yale ya Trump...kumbuka birds of a feather flock together!

Pona yake Assange ni Trump kushinda Urais kitu ambacho hakitawezekana. Clinton atakapotangazwa Rais, asubiri tu maumivu na ndiyo maana halali akimpigania Trump!
Ahahaa...!!!Sasa hao ndege mbona wanamuacha Mama Clinton!? Au wanamuadhibu kwa sababu vurugu zake zilisababisha mwenzao Bwana Clinton 'kupopolewa'...! Mkuu Mag3 , nadhani nawe unafaa kuwemo kwenye timu ya kampeni ya HRC!!
 
Bahati mbaya natumia simu, ningekupa michapo ya uhakika.
 
Ahahaa...!!!Sasa hao ndege mbona wanamuacha Mama Clinton!? Au wanamuadhibu kwa sababu vurugu zake zilisababisha mwenzao Bwana Clinton 'kupopolewa'...! Mkuu Mag3 , nadhani nawe unafaa kuwemo kwenye timu ya kampeni ya HRC!!
Ugomvi wa Assange si baina yake na Clinton tu, unaanzia mbali kidogo

Wakati Hillary akiwa Secretary of states, na baada ya kuuawa Osama,

Wikileaks walitoa emails'classified information' jinsi US walivyofanikiwa.

Habari hizo ni muhimu,zinazonyesha mbinu ambazo bado zinatumika

Obama kupitia DOJ wakaanza harakati za kumatfuta Assange.
DOJ ilifanya kazi na FBI na CIA kwa kutambua lilikuwa suala la security

Tangu hapo, Assange akawa na Ugomvi na US ukimgusa Hillary kwa nyadhifa

Anachokifanya Assange ni ku revenge dhidi ya Dem na eneo analoona linaweza kuwa na impact ni katika uchaguzi mkuu.

Kumbuka, link ya ugomvi, secretary of state, na mgombea Hillary kwa sasa
 
RedItalic: Trump ana sense of humor ukilinganisha na yule mama. Hata hivyo ana matatizo yake kama binadamu ambayo sidhani kama ni hatarishi sana kwa ulimwengu ka ya yule mama. Trump can easily be rehabilitated ukilinganisha na yule mama ambaye kuomba msamaha tu kwake ni shida..
Republican 50 waliotumikia serikali ya Marekani katika mambo ya ulinzi na usalama, walitoa waraka wa kumkataa Trump 'Hafai na ni hatari kwa nchi'

Hao ni Republican kumbuka.
Unaposema si hatari sijui kama waliotoa waraka ni wendawazimu.

Katika hao, yupo Robert Gates alikuwa waziri wa Ulinzi wakati wa Bush na Obama. Moja ya legacy yake ni kuuawawa OBL. Think about that

Pili, inawezekana huoni hatari yake. Policy za Trump kuhusu mambo ya nje(foreign policy) ni vague.

Kwanza, ana advocate kujitenga na NATO
pili, anataka kuondoa majeshi ya Marekani yaliyoko maeneo mengine
Tatu, anatenga washirika ambao ni muhimu sana katika mikakati ya ulinzi

Sera hizo zimekuwa zikibadilika kila muda, ni ngumu kusema sera zake ni zipi hasa unless una inforamtion ambazo unaweza kutusaidia

Mfano aliulizwa swali, kule Syria angefanya nini tofauti hasa Allepo?

Nadhani hakuwa na jibu, pengine kama ulisikia utufamishe.
Nakumbuka alichojibu ni kumtuhumu Hillary, hakueleza atafanya nini.

Nne, huyu ni mtu anayesema anafahamu vita zaidi ya majenerali!
Wakati huo huo hana ufahamu nini kinaendelea kule Cremia Ukraine

Tano, Trump anasema nuclear proliferation is OK. Huoni hatari hiyo?

Kwa upande wa sera za Hillary, nyingi hazitofautiani na za Obama
Kwamba, Marekani ifanye kazi na washirika na pili, kuondoa dhana ya 'Hegemony'.

Ndicho kilichotokea Libya, kwamba NATO waliongoza mashambulzi.
Marekani ilihitajika kwasababu ya unique technology katika wakati critical.

Suala hapa si sera gani nzuri, bali uwepo wa sera.

Je, ya Trump ni ipi ambayo unasema itaondoa Hegemony ?

Haya ni kwa ufupi sana
 
Mkuu unajua mimi ninajifunza mengi kutoka kwako? Hapo mkuu ulitakiwa uniweke sawa mimi mwanafunzi wako kwamba hapa hii iko hivi na hivi. Mkuu kumbuka mimi ni mwanafunzi wako ingawa naweza kuonekana nauliza maswali au natoa hoja ambazo zina utata. . I am sincerely serous. Sitanii.
Sera za Marekani zipo za aina mbili. Kuna sera zinazobadilika kutoka kiongozi mmoja hadi mwingine. Hizi nyingi ni za mambo ya ndani, biashara, uchumi na jamii kama afya na elimu.

Kuna sera za Marekani na hasa za mambo ya nje. Hizi zipo zisizobadilika kwa kiongozi yoyote anayeingia oval office.

Moja ya sera hizo ni ulinzi na usalama zinazolenga kile unachokiita 'Hegemony'

Kwa mfano, sera za Marekani kuhusu mashariki ya kati hazibadiliki.

EU wamejaribu kuishinikiza Israel kupata suluhu ya mzozo wa Palestina.
Mara zote nchi iliyo 'veto' ni Marekani

Pamoja na Obama kuwa na mtazamo tofauti kuhusu mzozo, ikifika katika maamuzi US itasimama na Israel.

kuepusha tafrani mzozo wa BB Nyahu na Obama umekwaza suala zima
Obama ameliacha kwasababu analazimika kufuata sera za US no matter what

Sera ya Marekani ni kuwa na majeshi karibu na maadui wao(adversaries)

Uwepo wa Majeshi ya Marekani Japan, Korea kusini, Ujerumani na kwingineko ni katika ulinzi na usalama wa US na katika ku maintain hegemony

Kwa mfano, wapo wanaosema Korea kaskazini inaweza kusimama kidete na US kutokana na majaribio ya silaha zake za masafa marefu.

Watu wasichokumbuka, Marekani haihitaji makombora ya masafa kuifikia Korea kaskazini, tayari ipo mita chache kutoka pyong Yang, ipo Korea kusini.

Uwepo wa Majeshi Japan ni katika kumiliki South China sea na eneo lote

Ujerumani ni kituo muhimu sana katika Ulaya hasa ukaribu na Warusi

Tazama pamoja na flip flop za Erdogan wa Turkey bado ni ally wa NATO

Angalia ramani uone umuhimu wa Turkey kwa NATO

Ndiyo maana wajuzi wanamcheka Trump anaposema majeshi yanaigharimu Marekani. Of course yanaigharimu lakini hiyo ndiyo greatness ya US

Huwezi kuwa great bila hegemony,hilo aliliona George Washington to Obama

Sera hiyo haitabadilika hata kama Rais atakuwa Trump
 
Pamoja na kwamba LA Times haijawahi kumpa Clinton ushindi kwenye polls za Urais Marekani, ramani yao (electoral map) kwa siku ya leo iko hivi...!

The race to 270

Hesabu zote zinaonesha Donald Trump ataanguka vibaya sana na huo ndio ukweli.​
 
MDAHALO WA 3 UMEMALIZIKA

Mdahalo uliofanyika kukiwa na kura za maoni zinazoonyesha hali kutokuwa nzuri kwa Trump
Hata hivyo hizo ni kura za maoni ambazo hubadilika kila mara na hutegemea sample

Pamoja na ukweli huo, debate 2 za mwanzo Trump alikuwa na wakati mbaya ukilinganisha na Clinton

Matarajio ya leo yalikuwa makubwa , kwamba ni fursa ya mwisho kabla ya wiki 3 kuelekea uchaguzi

Wagombea wote walikwenda katika mdahalo wakiwa na mazonge zonge yao.
Clinton aliandamwa na emails WikiLeaks zilizotoka kwa muda wote tangu mdahalo wa pili kuelekea wa 3

Kwa upande wa Hillary emails zilitarajiwa kuwa na maswali mengi na magumu.
Kwa Trump, kashfa ya wanawake ingetawala.

TATHMINI I

Mwongozaji mdahalo alikuwa mzuri sana kwa kuhakikisha mjadala hauendi nje kwa majibizano
Maswali yalikuwa fair kwa wote na jambo zuri kila mmoja alikuwa na aina ya swali ingawa yanahusiana
Hii ilizuia mzungumzaji wa pili kuwa na advantage ya kuandaa jibu kutokana na swali la msingi

WAGOMBEA
Hillary Clinton alikuwa mtulivu kama ilivyokuwa awali, Trump alikuwa mtulivu dakika za awali kisha akaanza kutumia lugha ya kuingilia kati mijadala

Clinton alilenga kunadi sera na makundi hasa wanawake, watu wa rangi n.k.
Trump alilenga kushambulia rekodi ya Clinton na kumhusisha na matatizo ya leo na yaliyopita

Kujibu maswali
Trump hakujibu maswali kama yalivyoulizwa, mara nyingi alichomeka mambo aliyojiandaa kabla ya mdahalo

Kwa mfano aliulizwa sera yake ya uchumi na inavyopingwa na Republican wengine.
Hakueleza kwanini anaamini ni bora na kwanini wanaoompinga wanakosea. Hili lilikuwa swali zuri sana kwa Trump kutumia uzoefu wake wa biashara kueleza kwa kina. Alichofanya ni kuzungumzia yasiyo na uhusiano

Hillary alijua maswali atakayokumbana nayo na alionekana kujiandaa vema.

Kwa mfano suala la abortion alilieleza vizuri hata kama msimamo wake haukubaliki na wenye mitazamo tofauti

Trick
Hillary alitambua udhaifu wa Trump na aliweza kumtibua kwa urahisi.
Hayo yalisababisha Trump ajibu ima kwa jazba au apoteze uelekeo wa mjadala hata pale ulipomsaidia yeye.

Kwa mfano, mwongozaji alimbana Hillary kuhusu emails zinazoonyesha uhusiano wa ofisi ya umma na Clinton foundation. Hillary kwanza alionekana kukubali swali hilo kama zuri.

Hili lilianza kuwatoa hofu watu waliodhani ni gumu. Halafu akaelekeza mjadala kwenye umuhimu wa foundation

Mwngozaji alirudia kumbana Hillary ili atoe jibu kulingana na swali. Kwa mshangao Trump akaingilia kati na kuanza kuongelea kuhusu foundation inavyo kuwa funded na nchi zinazotesa wanawake.

Mabishano yakahamia Clinton foundation na Kuwaiti na hivyo kumsaidia Clinton kwa urahisi sana kuepuka swali

Tathmini ya II inafuata
 
TATHMINI YA II

MAKOSA YA KIFUNDI

Clinton alitambua udhaifu wa Trump katika kujenga hoja na alijua hoja za Trump
Udhaifu ulitokana na hoja kutoka mjadala wa 1 , kwamba Clinton ni status quo for 30yrs

Mdahalo wa pili, Clinton alitumia hoja hiyo kuweka rekodi yake ya utendaji vema.
Alielezea alivyofanya kazi na wanawake, watoto na alivyoshiriki miswaada 400

Hoja hiyo ya Clinton kuwa insider kwa miaka 30 bila matokea, Trump ameirudia tena leo
Clinton akaitumia kueleza kwa mafanikio kwa miaka 30 akifikia makundi muhimu

Hili ni kama Trump alikuwa anajenga hoja ambazo Clinton alikuwa na majibu yake

Mfano wa pili. Trump alitumia rekodi ya Bill Clinton kuhusu mikataba ya NAFTA.
Clinton akaeleza rekodi ya mumewe kutoka deficit hadi surplus, alijua Trump atalizungumzia.

Kiufundi Trump alikuwa anamwelekeza Clinton kujenga hoja, lilikuwa kosa la kifundi

KOSA LA PILI
Trump ana matatizo na watu wa rangi.
Kauli ya kilatino aliyoitumia inaonekana kuudhi Walatino. Hili litamsaidia?

KOSA LA TATU
Trump aliulizwa kama kauli yake ya rigged election , je atakubali matokeo ya uchaguzi?
Hili ni baada ya VP Mike Pence na bintiye Ivanka kusema, ndiyo watakubali

Trump kasema hilo analicha 'suspense' kwa maana hawezi kulizungumiza
Hili limewaudhi watu wengi kwani America inaonekana itakuwa kama third world

Obama amesema Trump akishinda atamwongoza na kumpa kila ushirikiano
Trump kukataa kukubali matokeo kinachukua vichwa vingi vya habari kuliko ilivyotarajiwa

Kama lipo tatizo, pengine angesema 'atakubali matokeo ikiwa hakutakuwa na matatizo'

KOSA LA NNE

Wakati Clinton akiongelea suala aliloulizwa na kumhusisha Trump, Bwana Trump akainamia microphone na kusema 'Nasty woman'.

Hili nalo halionekani kuwa zuri hasa ukizingatia matatizo aliyo nayo.

TEMPERAMENT
Hili limeendelea kuwa tatizo kwa Trump,hajaonyesha hali ya Urais/control ya hasira zake

FACT
Trump amebadili misimamo yake kuhusu Nuclear au Allepo na Iraq.
Hili nalo linaonekana tatizo hasa kwa wasomi wanaofuatilia mambo kwa undani.
Kwa watu wa kawaida inawezekana isionekane

Tathmini itaendelea, isipokuwa inatosha kusema Hillary Clinton hakuwa na gaffe na hilo litamsaidia .Trump alikuwa na unforced error na na gaffe nyingi na hayo yatamuumiza

Je, mdahalo umesadia upande wowote?
Jibu lake si rahisi kwasasa isipokuwa kwa ramani ya electoral college ilivyo mdahalo unaweza kusaidia Trump kurudisha majimbo yanayoegemea Demo kama Utah na Arizona

Mdahalo utazua utata zaidi kuhusu kauli zake na una expose weakness zake

Majimbo ya Republican yanaelekea kuwa toss up kwa disadvantage ya Trump

Je, Trump amefanikiwa kushawishi wanawake na college educated people?

Itaendelea....
 
TRUMP NA RIGGED ELECTIONS

Katika tathmini ya jana tulisema, yapo mambo mawili yatakayomwandama Trump kwa kauli zake za jana

Habari kubwa ni ile aliyokataa kusema atakubali au atakataa matokeo
Kauli hii ilikuwa na maana mbili

kwanza, hakuweka msimamo wake wazi
pili kawatosa VP Mike Pence na mwanaye Ivanka

Hii si mara ya kwanza kumtosa VP, mjadala uliopita alimtupa 'under the bus'

Hoja kubwa ya Trump kuhusu rigged election ni media kutoa habari zake

Ni Trump aliyewahi kusema hatumii pesa media zinafanya kazi kwa niaba

Leo, baada ya kauli za 'rigged election' na 'Nasty woman' kupamba habari, Trump amebadili mwelekeo wa mazungumzo akiwa Ohio.

Trump anasema atakubali matokeo ikiwa na endapo tu atashinda

Hili nalo litaendeleza mjadala wa jana na litakuwa na impact yake kivyake

Hivyo anayewalisha habari waandishi ni Trump mwenyewe
Mwisho analalamika uchaguzi utakuwa rigged kwasababu ya media

Huu ni uchaguzi wa aina yake kwakweli na Wamarekani wanasababu za kujiuliza sana

Tusemezane
 
Nguruvi3 kwa mara ya kwanza lazima tukiri na hili hata baadhi ya wamarekani wamekiri kuwa uchaguzi huu ni wa aina yake. Vyama vyote viwili vimesimamisha wagombea wa ajabu...!! Wakati mwingine unajiuliza,nchi inayojinasibu kuwa na demokrasia na iliyoweka misingi bora ya kupata wagombea wake,imekuaje ikateua wagombea wa aina hii!??
 
Trump anazidi kulikoroga...duh! Huyu mhuni Urais atausikia tu.
Lakini ujue, huyo Mama ataharakisha kuizamisha Marekani. Kwanza kwa sasa kunamgawanyiko ndani ya EU (mshirika mkubwa wa US) kuhusu maelekezo ya kuendeleza sera za Marekani ambazo haziinufaisha EU. Leo wameshindwa kuafikiana juu ya kuongeza vikwazo kwa Russia. Hii ni dalili mbaya kwa US anayetaka kuitumia EU kuiadhibu Russia kwa manufaa yake. Philipine mshirika wake muhimu, huko Asia, juzi ameamua kuiangukia China. Na kwa China kwa ukarimu wake amemruhusu Durtete (Rais wa Philipino) kutumia visiwa vile vilivyona utata bila wasi. Wamesaini karibu mikataba dazeni mbili ya kiuwekezaji na ulinzi. BRICS iko speed mia kuikwepa ' Petroldollar', petrodollar ni uhai wa US. Juzi kati nadhani kwa kuona Dollar yaweza kuwa reject katika baadhi ya masoko ya fedha, IMF imeamua kuiongeza ela ya China katika sarafu za kuwekea 'bond'. Wanafedha na wachumi wanajua sana hii ina maanisha nini. Kwa staili hii na Speed na kiburi cha 'mama' huyu, US run a risk of being isolated and exterminated (kiuchumi na kiulinzi) kama ataingia kwenye jumba jeupe.

"Mama" hana simile...ebu fikiria alivyochekelea kifo cha Comred Ghaddaf (R.I.P); kwa kicheko cha haja, 'mama' huyu alisema ' We came, we saw, he died'. Ishara ni nyingi, ambazo inaonyesha, huyu 'mama' ambaye hana simile kutangaza hegemony ya nchi yake, ataizamisha US kwa mwendokasi wa kushushu majengo pacha ya Umoja wa Biashara Ulimwenguni huko kwao kipindi kile.

US wajitazame...na waamue wanataka nchi yao izame kwa mwendokasi ama mwendotaratibu..!
Nawashauri wachague mwendotaratibu.
 
Nguruvi3 kwa mara ya kwanza lazima tukiri na hili hata baadhi ya wamarekani wamekiri kuwa uchaguzi huu ni wa aina yake. Vyama vyote viwili vimesimamisha wagombea wa ajabu...!! Wakati mwingine unajiuliza,nchi inayojinasibu kuwa na demokrasia na iliyoweka misingi bora ya kupata wagombea wake,imekuaje ikateua wagombea wa aina hii!??
Misingi ya demokrasia ya Wamerkani ni mizuri .

Kwamba sauti za watu ndizo zinazungumza. Ndiyo maana kauli ya Trump kuhusu kukubali au kuktaa matokeo imepokewa kwa hisia sana. Watu ndio wanazungumza si mtu

Ni misingi hiyo ndiyo imewezesha Trump ambaye tukubali tu kuwa uwezo wake kisiasa ni mdogo kufika hapo alipo.

Nasema hivi kwasababu ukiwasikiliza, Trump hajaongelea sera, anachofanya ni kukosoa sera za mwenzake.Hilo ndilo linamfanya Hillary pengine aonekane afadhali

Ukimsikiliza John Kasich utaona tatizo kubwa kwa GOP. Tatizo lilianza na Tea party ambap badala ya kusikiliza na kurudisha katika misingi ya chama, Republican waliwaogopa

Ni tea party ndiyo imemfikisha Trump alipo. Katika uzi mwingine tulionyesha ile core constituent ya Trump ambayo hadi sasa ipo intact

Wale wangine waligawana kura 70% na hivyo kutoweza kumshinda Trump

Hakuna sera nzuri au mbaya, kinachotakiwa ni ulinganifu na uwezo wa kuzitetea

Tuliona misimamo ya McCain na Obama, Romney na Obama
Ilikuwa clear kabisa nani anasimamia wapi

Kama umefuatilia mijadala, Trump hajaongelea sera zake zozote.
Kwa mfano, anaulizwa Syria kule Allepo angefanya nini tofauti?

Jibu ni Obama katengeneza ISIS.
Facts zipo kuwa ISIS ilianza wakati wa Bush.Je, alitakiwa afanye nini? hana jibu

Hillary anaweza kueleza nini atafanya hata kama si sahihi.
Msikilize Hillary na sera za nje, halafu tafuta ulinaganifu wa sera hizo kutoka kwa Trump

Mfano wa pili, kaulizwa, plan yake ya medicare itazuiaje ukosefu wa fedha ikifika 2020? Jibu lake Obamacare imeleta matatizo.

Hivi ni vitu viwili na hainonekani anaweza ku connect au kuvitetea

Ukifuatilia kwa undani mtifuano wa Democrats ulikuwa kuhusu issue
Mtifuano wa GOP ulikuwa personality

Hata hivyo, system ya Marekani inafanya kazi kwasababu mwisho wa siku Republican na Democrats walipata wagombea kwa sauti za watu. Hilo ndilo linaeleza demokrasi.

Marekani mgombea hateuliwi anapatikana kwa process na process ita determine si kikundi cha watu
 
Nguruvi3 kwa mara ya kwanza lazima tukiri na hili hata baadhi ya wamarekani wamekiri kuwa uchaguzi huu ni wa aina yake. Vyama vyote viwili vimesimamisha wagombea wa ajabu...!! Wakati mwingine unajiuliza,nchi inayojinasibu kuwa na demokrasia na iliyoweka misingi bora ya kupata wagombea wake,imekuaje ikateua wagombea wa aina hii!??
magode, magode, magode...mbona unabadilisha magoli? Msimamo wako muda wote umekuwa ni Marekani kumhitaji mtu kama Donald Trump, mtu sahihi asiyemung'unya maneno, mtu akayeirudisha Marekani katika mstari na mtu ambaye hana makandokando ya establisment. Baadhi yetu tumesema toka awali kabisa kwamba mtu kama Donald Trump hafai na Marekani tunayoijua haiwezi kufanya maamuzi ya kijinga kama hayo ya kumpa madaraka tapeli, mkurupukaji na mdhalilishaji.

Sasa unasema unataka sote tukiri kwamba wagombea wote hawafai na unashangaa nchi kama Marekani inayojinasibu kuwa na demokrasia na iliyoweka misingi bora ya kupata wagombea wake, imekuaje ikateua wagombea wa aina hii! Ngoja nikusahihishe kidogo...wakati ilijulikana toka mapema kabisa kwamba Hillary Clinton ana sifa zote za kugombea Urais Marekani, vivyo hivyo ilijulikana kwamba Donald Trump hakuwa na sifa yoyote ya kugombea Urais na kujitokeza kwake kulichukuliwa kama utani!

Mwaka 2012, Hillary Clinton alipigiwa kura kama mwanamke mashuhuri namba moja duniani akifuatiwa na wengine kama malkia wa Uingereza na wengineo kama Oprah Winfrey. Wakati huo tayari alipewa nafasi kubwa ya kuwa mgombea wa chama cha Democrats na hivyo kuwapa mahasimu wao wakuu, Republicans, muda tosha wa kufanya jitihada za kumchafua. Maswala ya Emails na Bengazi, kama uliyafuatilia, yalivaliwa njuga kumjengea taswira ya kutokuwa mwaminifu na kwa kweli walifanikiwa.

Kuna msemo kwamba uongo ukirudiwa rudiwa bila kukanushwa kwa nguvu, ni rahisi kwa watu kuanza kuamini na kwa kweli wengi waliweza kurukia hiyo hoja ya udanganyifu. Jitihada hizi zikafuta kwa kiasi kikubwa historia na sifa zote alizokuwa nazo huyo mama hadi kupewa heshima duniani kama nilivyotaja hapo juu. Nakiri kabisa kwamba Republicans ni wazuri sana katika hili...hebu unganisha na jitihada zao katika kutaka kufuta mema yote ya Rais Obama katika kipindi chake chote cha miaka minane.

Je Donald Trump alikuwa na sifa zipi za kujitokeza kugombea Urais wa Marekani? Alipewa nafasi gani kati ya wagombea wote 17 waliojitokeza hadi awashinde kwenye kura za awali ndani ya chama chake? magode, ukipata muda tafakari haya maswali halafu jiulize kwa nini wewe na baadhi ya wana JF humu jamvini mlikuwa mnamshupalia huyo limbukeni?
Kwa lipi alilowafanyia wananchi wa kawaida? Mimi ninayo rekodi ya kuwa upande wa Republicans (kwa mfano uchaguzi wa 2004...Bush/John Kerry)

Nitaendelea...

Hillary Clinton, "While I was monitoring the raid that brought Osama Bin Laden to justice he was hosting the Celebrity Apprentice"
Donald Trump, "Such a nasty woman"
 
Labda hujanielewa tangu mwanzo ktk michango yangu,nilisharudia mara nyingi sana ukisoma michango yangu hapa. Namuunga mkono na mguu Donald trump mpaka kesho,kwa sababu sijawahi kuwaamini wanawake ktk mambo makubwa..! Na sina sababu ya kuwaamini. Kuna kitu usichokielewa hapa,kuhusu sifa za kugombea Donald trump anazo ndo maana aliruhusiwa kugombea.

Nnachosema hapa,wagombea wote,wameonekana kuwa na makando makando mengi sana kiasi kwamba km kungekuwa na umakini mkubwa ktk uteuzi wangeweza kuwaacha.

Naona unataka kutetea hata dhambi ambazo clinton mwenyewe amekiri na kuomba radhi...lkn kwako ni uongo uliopikwa na republican!!! Sisi kazi yetu ni kuangalia wanavyotifuana,lkn mwisho wa siku wamarekani wenyewe ndo wataamua.
 
Mag3
Kuongezea kidogo, Dem walikuwa na wagombea 3 na mmoja alijitoa mapema
Sander alikiri kuwa kuingia kwake ilikuwa jukaribu kabla ya kupata moto

Hili linaonyesha kuwa Dem walikuwa tayari wanafahamu ukubwa wa mgombea wanayetaka abebe bendera yao

Katika ule uzi wa primaries tulijadili tatizo la Republican.

Walijitokeza akina Dr Carson na takribani 17. Kati yao, wazuri walikuwa 4.

Hawa wangeweza kuwa tofauti na Trump

Trump aliwashinda kwasababu alichukua agenda za Tea party.
GOP walifanya kosa la kuacha Tea party itawale.

Ukifuatilia primaries Trump alipata wastani wa chini ya 30% kila mara

Kwa maneno mengine 70% iligawanywa kwa 16 na mwisho akawa mshindi. Ndilo zao la Tea party iliyoundwa katika misingi ya chuki dhidi ya Obama.

Pamoja na hayo, GOP walimkataa Trump mapema
Leo akina Magode wanakiri ni tatizo wakati lilionekana toka mwanzo.
 
Labda hujanielewa tangu mwanzo ktk michango yangu,nilisharudia mara nyingi sana ukisoma michango yangu hapa. Namuunga mkono na mguu Donald trump mpaka kesho,kwa sababu sijawahi kuwaamini wanawake ktk mambo makubwa..! Na sina sababu ya kuwaamini. Kuna kitu usichokielewa hapa,kuhusu sifa za kugombea Donald trump anazo ndo maana aliruhusiwa kugombea.

Nnachosema hapa,wagombea wote,wameonekana kuwa na makando makando mengi sana kiasi kwamba km kungekuwa na umakini mkubwa ktk uteuzi wangeweza kuwaacha.

Naona unataka kutetea hata dhambi ambazo clinton mwenyewe amekiri na kuomba radhi...lkn kwako ni uongo uliopikwa na republican!!! Sisi kazi yetu ni kuangalia wanavyotifuana,lkn mwisho wa siku wamarekani wenyewe ndo wataamua.
Hapa kuna 'women-phobia'

Najaribu kufikiria Ujerumani ni Taifa kubwa katika Ulaya na dunia.

Katika kipindi cha mpito kuunganisha Ujerumani mbili haikuchukua muda mrefu Angeal Merkel akawa Chancellor.

Ni Angela aliyeongoza Ujerumani katika kipindi kigumu sana cha recession duniani akiwa na mzigo mkubwa wa kubeba kutoka EU

Ni Angela anayeongoza uwepo wa EU baada ya Brexit

Tunamkubuka Iron Lady Thatcher aliyeongoza UK
Tunawakumbuka akina Indira Gandhi walioongoza 'robo ya dunia'
Wapo akina Benaziar Bhuto walioongoza hotspot kama Pakistan

Hivyo kudhani kuwa mwanamke hawawezi, sidhani kama ni sahihi

Lakini pia ukumbuke Marekani Rais ni sehemu ya uongozi wa nchi si mtu pekee kama vinchi vyetu. Rais anafanya kazi kwa misingi iliyowekwa.

Hofu yako ndiyo wasi wasi waliokuwa nao baadhi ya Wamarekani kuhusu mtu mweusi. Leo approval rate ya Obama ipo katika 50%.
 
Back
Top Bottom