Hivi unadhani ukishinda tu unapewa Visa eeeh.
Kwa taatifa yako unaweza ukashinda lottery na bado usipewe visa; kitu unachotakiwa kujua lazima uende kwenye interview. Fuatilia itawkewa ni nini namaanisha.
Jwa kifupi naona tunajaribu kupungua kitu ambacho huna uelewa nacho. Kwa taatifa yako watu wote chini ya miaka 25 ukienda lazima ujiunge na kesho na usipofanya hivyo ujue itakusumbua baadae. Nina mifano mingi hai katika Hili.
Kama ni kweli unacho chanzo Cha taarifa, uwe makini na hicho chanzo.
Hapo palipokolezwa;
Hakuna kitu kama hicho.
Wageni hasa wenye umri mdogo huwa wanakimbilia Jeshini kutokana na fursa wanazozipata wakilitumikia Jeshi lakini si kuwa wanalazimishwa.
Narudia tena
hulazimishwi,
hushawishiwi wala kubughudhiwi uingie Jeshi,
Wageni wenyewe ndio wanaopenda na pia si mserereko kuingia jeshi, ni mchakato ambao wengi wanachemsha pamoja na kutamani kuingia.
Kuhusu umri;
Anaeruhusiwa kushiriki DV maelekezo kwa mujibu wa rejea dvlottery.state.gov/instructions (chanzo pekee cha taarifa sahihi)
Ni kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea.
Haijatamkwa ukomo.
Maelekezo haya kila mwaka yatoka na huwa kunakuwa na maboresho madogomadogo ila sijawahi kuona ukomo wa umri hata mwaka mmoja Kati ya mingi iliyopita ambayo huwa Mimi nafuatilia.-
Ukihitaji pdf ninazo naweza kukupatia miaka mingi tu.
KWAHIYO HAKUNA UKOMO WA UMRI KUSHIRIKI UWE NA VIGEZO TU, UMEO/KUOLEWA/UNA WATOTO/ HUNA HAIJALISHI NA HAIKUNYIMI NAFASI.
Upendendeleo;
Kuhusu upendeleo/kipaumbele kwa mujibu wa maelekezo rasmi Hakuna kundi lolote linalopewa upendeleo kwa sababu yoyote Ile.
Labda tueleweshane kidogo;
Hii Bahati nasibu inachezwa kwa Komputa na Komputa yenyewe inachagua kwa style wanaita 'random' haiangalii nani, wawapi,mwenye rangi gani wala anaumri gani.
Kingine,
Ingekuwa lengo lao ni umri fulani tu unadhani wao ni wajinga kusema yeyote anaweza kucheza?
Kwani wanashindwa nini kusema wanataka vijana waende Jeshini kwao moja kwa moja?
Ili Mtu aamue mwenyewe mapema.
Kingine;
Hivi ina maana vijana wote waliowahi kupata DV wapo Jeshini huko Marekani sasahivi?
Someni Maelekezo rasmi kwa lengo la kuelewa.
Rai: Usimuamini sana mtu kwa kila anachokisema eti kwakuwa tu yupo Marekani hayo mambo ya zamani sana.