Hivi kweli Jussa amesema na kushauri haya? Kama kweli kasema basi leo ndio mie nahakikisha kweli wanasiasa woooooote wa Tanzania wanaweka mahitaji yao mbele na wanawatumia wananchi kufikia malengo yao tu!
Hivi Jussa amesahau ule msemo wa unakula na kipofu lakini humshiki mkono? Kuna manufaa gani yatakayofikiwa kwa kuwa na serikali ya umoja wa kimataifa Zanzibar? Si tuliwahi kuwa nayo huko nyuma? Nini kilipatikana na nini kilibadilika? Hakuna kilichobadilika punda alikuwa yule yule lilibadilika ni soji tu!
Siamini kiongozi kama Jussa ambae mwenyewe amepewa kichapo cha mbwa, anataka watu waliopewa vichapo vya mbwa na kujikuta na ulemavu wa milele, watu waliopoteza maisha yao, mali zao na nguvu zao, watu waliopoteza ndugu zao, wazee wao na watoto wao washau yote hayo na wakubali Seif sharif na viongozi wenzake wapewe nyadhifa katika serikali ya umoja wa kitaifa. Siamini Jussa anataka Wazanzibari wa ACT baada ya yote waliyoyafanya na maumivu yote waliyoyapata kwa sababu ya kuunga mkono chama cha ACT, Jussa yuko tayari kukaa meza moja na CCM. CCM hii hii ambayo iliidhinisha na kufumbia macho vipigo vya wanachama wa CUF.
To be honest hata sijui kwa nini nashangaa, ACT inaongozwa na Seif Sharif ambae ni mahiri sana katika kuwaendea kinyume wenzake kwa manufaa yake binafsi. Aliwaendea kinyume akina Aboud Jumbe na wenzake pale viongozi wa serikali ya Zanzibar (akiwemo Seif Sharif) walipokwenda kwa Nyerere kutaka Tanzania iwe na serikali tatu.
Sote tunajua aliwaendea kinyume mara tu alipoahidiwa na Nyerere kuwa atamtayarisha kuwa Rais wa zanzibar siku za mbeleni. Seif huyu huyu akaamua kuwaendea kinyume CCM baada ya kuona kuwa ahadi aliopewa na Nyerere haikuwa ya kweli na akaamua kuleta matata ndani ya chama na hatimae kufukuzwa CCM mwaka 1987.
Seif huyu huyu aliwaendea kinyume wazanzibari wenzake mwaka 2010 akiwa kiongozi wa CUF pale alipokubali kuingia katika serikali ya mseto na CCM ilhali wanachama wake walijitoa mhanga na kuhakikisha kuwa anashinda uchaguzi na alishinda. Alisahau kuwa watu wamepigwa, wamepoteza mali zao na wengine kuuliwa kwa sababu tu ya kutaka CUF ishinde, lakini alipoonyeshwa fupa tu, Seif alilirukia na kuchukua cheo cha chief of minister of zanzibar.
Na sasa anataka kufanya yale yale tena!!!!!!!!!