e-GA inahujumiwa

e-GA inahujumiwa

Hawa watu Nape na wenzake muda sio mrefu watakuja kulazimisha mifumo ya Usalama itengenezwe NMB , ni aibu na ushamba wa technolojia.
 
maana yake wanaweza kutengeneza hata passport maana namba wana generate wao
Kwani hata sahivi ambapo passport number ipo issued na immigration hakuna watu wasio na sifa wanapata passport au VISA?

Mbona hata NIDA kuna wasio raia wamepewa NIDA za uraia?

Kama Mnachohofia NMB kimeshatokea immigration na NIDA sasa kuna nini mnagain kwa kuogopa NMB?

Kingine passport utaipata kwa utaratibu huu huu wa sasa tofauti tu ni kwamba instead wakupe namba mpya wanatumia ile ile uliyokwishapewa na NIDA, TIN etc kwa urahisi wa coordination na sio kwamba eti passport zitakua issued na NMB!!
 
Hao jamaa itakuwa hawaifahamu eGa, au ni miongoni mwa wapigaji, maana Ega ipo Kwa ajili ya kuzuia mianya yote ya upigaji.

Nakupa mfano mmoja tu wa Mfumo wa taifa wa kuunganisha mifumo yote GOVESB watu walikuw wanakula Hela kwenda mifumo yao taasisi Kwa taasisi, sisi tukatengeneza GOVESB Kila taasisi isajili Mfumo wake hapo, then atakae taka data za mwenzie anazikuta hapo kwenye GOVESB shughuli imeisha tena free of charge.
Kwahiyo zile fedha za kwenda kuunganisha taasisi Kwa taasisi watu hawapati tena mana sasa kupata data ni Bure.

Nadhan Kwa mfano huo mmoja inatosha,

Bado sijagusa GEPG , unadhan Serikali inaingiza mapato kiasi gani kupitia GEPG ni zao la EGA , so mtu yeyote anayeisema vibaya EGA jua kabisa mirija yake ya ulaji imezibwa au haifahamu vizuri EGA.

Kwa maelezo zaidi kuhusu EGA tembelea tovuti yetu ya e-GA | Mwanzo
 
Nape ni Godfather wako, mtetee sana lakini unatakiwa kujua ame commit treason , na ipo siku atalipa kwa uhuni alio ufanya.
Actually nilikuambia uko emotional without being analyitical

Comments zangu zote zimemkwepa nape and now it proves una issue za siasa na sio technology

Read all my posts again, nimeongelea mandate ya eGA, rushwa, scope etc.

Sijataja mtu wala kulenga siasa

Finally you have come clean you idiot

I have no interest na watu…
 
Bado hujasema sheria ipi inampa mamlaka Nape Godfather wako kuipa tender NMB ya mifumo ambayo ipo tayari e-GA
Umesikia hapo? Sheria inasema "integrate with the government systems" na sio "Generate/create/initiate new systems" means sheria haina tatizo kwa kampuni binafsi kutoa huduma kwa mifumo ambayo ipo e-Ga tayari kama tu itaongeza ufanisi.
 
Hao jamaa itakuwa hawaifahamu eGa, au ni miongoni mwa wapigaji, maana Ega ipo Kwa ajili ya kuzuia mianya yote ya upigaji.

Nakupa mfano mmoja tu wa Mfumo wa taifa wa kuunganisha mifumo yote GOVESB watu walikuw wanakula Hela kwenda mifumo yao taasisi Kwa taasisi, sisi tukatengeneza GOVESB Kila taasisi isajili Mfumo wake hapo, then atakae taka data za mwenzie anazikuta hapo kwenye GOVESB shughuli imeisha tena free of charge.
Kwahiyo zile fedha za kwenda kuunganisha taasisi Kwa taasisi watu hawapati tena mana sasa kupata data ni Bure.

Nadhan Kwa mfano huo mmoja inatosha,

Bado sijagusa GEPG , unadhan Serikali inaingiza mapato kiasi gani kupitia GEPG ni zao la EGA , so mtu yeyote anayeisema vibaya EGA jua kabisa mirija yake ya ulaji imezibwa au haifahamu vizuri EGA.

Kwa maelezo zaidi kuhusu EGA tembelea tovuti yetu ya e-GA | Mwanzo
EGA ni regulator and that is their job kabisa

Kudos to them
 
Miezi takribani sita imepita niliandika juu ya njama za viongozi waandamizi wa serikali kuihujumu mamlaka ya serikal mtandao(e-GA). Mipango ya e-GA kuzuiwa kufanya majukumu ya uundaji wa mifumo ya serikali ili waandamizi watafute kampuni binafsi kufanya hayo imeanza kufanikiwa.

Leo Wizara ya TEHAMA imeingia makubaliano na NMB ili NMB iwe inalipwa na serikali kutengeneza mifumo ya TEHAMA ya serikali.

Kwa mujibu wa MOU iliyo sainiwa leo , NMB atatoa wataalamu wa TEHAMA(Software developers) kutengeneza mfumo utakao replace NIDA na RITA ,kama mnavyofahamu ,serikali inakuja na jamii number ,namba ambayo mtoto akizaliwa atakuwa nayo na atakua nayo ,initiative nzuri sana lakiniiiii, kulikua na ulazima gani wa mradi nyeti kama huu kupewa taasisi binafsi? wafanyakazi wa NMB wana proper vetting kuanza kushika mifumo ya siri namna hii?

Achana na jamii bima, ESB ambayo tayari ipo e-GA na inafanya kazi, Wizara ya TEHAMA imeamuru NMB kupewa tender kupitia MOU hio wao ndio watengeneze ESB ya serikali, yaani mawasiliano ya mifumo yote ya serikali ananyang'anywa e-GA na anapewa NMB why?

Hivi nchi hii tuna mawaziri wanaofikiria kweli? Haya ndio mambo ya waziri alikuja na kufuta physics akasema iwe physics with chemistry, waziri huyo wa zamani alifuta masomo ya biashara na kilimo pia kabla ya serikali ku reverse maamuzi hayo, lakini kama mnakumbuka kuna watanzania walifutiwa masomo hayo.

Waziri wa TEHAMA unaua e-GA kwa maslahi ya nani?

Waziri wa TEHAMA unaua e-GA kwa kumkomoa nani?

View attachment 2883959
Kuna kikao walishawahi kukaa wizara ya fedha na mipango toka JPM hajaondoka.
Nape hakuwa waziri muda huo ,muda huo Eng Kundo alikua naibu waziri wa TEHAMA, alishiriki kikao hicho
Nape anaweza kuwa ameingizwa ku execute plan ambayo hajui ilipoanzia .
Kikao hicho alikuwepo mkuu wa IT wa Wizara ya fedha na mipango Sausi , Dotto James alikuwepo , mtu wa TRA na BOT pia.
Kulikua na heavy weight senior IT leaders, walikua wanasuka mipango ya kuiondoa e-GA kwenye ramani.
Mipango hio ilipojulikana watu kadhaa walifukuzwa kazini na wengine kuhamishwa ,mmoja wapo ni Mushiru alikua e-GA ,huyu alikua anatumika na waandamizi hao kuiua e-GA from within na alikua anauza ramani ya vita kwa waandamizi hao.

Sasa hivi baada ya JPM kufariki Mushiru alirudishwa na hilo genge na sasa ni Director wa IT PPRA ni uhujumu mkubwa sana ,Nape ni mbuzi wa kafara tu.
Big plan e-GA atavunjwa atakua kama department na kuhamishiwa wizara ya TEHAMA , na mifumo itakua inanunuliwa toka nchi za nje na makampuni binafsi,

This is just a tip of the big plan to come .

Vijana wa e-GA kama wanataka kulinda ujuzi wao waanze ku apply kampuni binafsi ,hakuna future e-GA as long as Nape and the elite do exit
 
EGA ni regulator and that is their job kabisa

Kudos to them
Ni regulator mwenye jukumu la kutengeneza mifumo na standard za matumizi wa IT serikalini .
uzuri sheria hii hapa isome na kama una changamoto wewe una nafasi serikalini pelekeni mswaada ifutwe simple like that, lakini kuiua kihuni sio jambo legit
 
Attachments

Kwani hata sahivi ambapo passport number ipo issued na immigration hakuna watu wasio na sifa wanapata passport au VISA?

Mbona hata NIDA kuna wasio raia wamepewa NIDA za uraia?

Kama Mnachohofia NMB kimeshatokea immigration na NIDA sasa kuna nini mnagain kwa kuogopa NMB?

Kingine passport utaipata kwa utaratibu huu huu wa sasa tofauti tu ni kwamba instead wakupe namba mpya wanatumia ile ile uliyokwishapewa na NIDA, TIN etc kwa urahisi wa coordination na sio kwamba eti passport zitakua issued na NMB!!
unataka kuruhusu waislamu wawe wanakula nguruwe kwa kua kuna baadhi ya waislamu wasio safi hua wanakula?
 
Ni regulator mwenye jukumu la kutengeneza mifumo na standard za matumizi wa IT serikalini .
uzuri sheria hii hapa isome na kama una changamoto wewe una nafasi serikalini pelekeni mswaada ifutwe simple like that, lakini kuiua kihuni sio jambo legit
Excellent

Imesema ni yeye pekee?

I think hoja kuu hapa hi why duplicating efforts

ILA sio hizo emotions zako za kibwege
 
Tuna very strong government

That will never happen
una taarifa ya kikao walichokaa wizara ya fedha na mipango few days kabla JPM hajafariki elit wa IT?
Walitaka e-GA ife kipindi cha JPM wakashtukiwa lakini sasa wako full na watafanikiwa ,wameweka watu kila sehemu yenye maamuzi .Development ya mifumo serikalini iko kwenye miezi sita ya mwisho
 
Excellent

Imesema ni yeye pekee?

I think hoja kuu hapa hi why duplicating efforts

ILA sio hizo emotions zako za kibwege
uko sahihi kwenye kuto duplicate effort , suala la msingi ambalo limeainishwa na e-GA regulation ni kuwa kwenye utengenezaji wa mifumo,hawajazuia taasisi yeyote kutengeneza mifumo,wametaka taasisi kutoa report e-GA ili kama mfumo huo upo tayari wasihangaike kutengeneza tena.
Swali la msingi ESB ipo e-GA au haipo? jibu ni rahisi sana ESB ipo na iko operational
then why Wiraza ya TEHAMA imeipa tender NMB kutengeneza mfumo ambao upo?

PIli Jamii number ni mradi ambao tayari developer wa serikalini wana miezi minne sasa morogoro wanatengeneza ,why Wizara imegawa tender kwa NMB tena?

Kama lingekua jambo la ufanisi wa mifumo ,wangetangaza tender ya wazi ili makampuni yaombe tender
Kufanya single source procurement inaenda kinyume na sheria za procurement na ni audit query.
Single source inaruhusiwa tu kwa taasisi kama usalama wa taifa ,wanapofanya manunuzi ya zana zao wanafanya tafiti na kupata kampuni yenye hio bidhaa then wananunua . Hii ni kutokana na usiri na unyeti wa taasisi wa usalama wa nchi.
NMB ana vigezo gani au ESB na jamii number system zina vigezo gani kuingia kwenye single source procurement?
 
Nadhani wewe umetenda haki kwenye mjadala… siyo Yule kinabo olimpio

Hapa ipp changamoto… pia umegusia very important issue ya single source kwenye ununuzi… ni banana skin hiyo

Uko very constructive mkuu
 
Umesikia hapo? Sheria inasema "integrate with the government systems" na sio "Generate/create/initiate new systems" means sheria haina tatizo kwa kampuni binafsi kutoa huduma kwa mifumo ambayo ipo e-Ga tayari kama tu itaongeza ufanisi.
Sheria haina tatizo kabisa ,inasema wataarifu e-GA kama unataka kuanza utengenezaji wa mfumo mpya ili kuepuka duplication ya mifumo ,mfano mailing system tayari e-GA wameshatengeneza ,ukitaka kutengeneza wako lazima useme nini unakikosa kwenye mailing system ya serikali.
Sasa ESB waliyopewa tender NMB kutengeza ipo tayari e-GA , kwa nini NMB anatengeneza nyingine?
Jamii number system tayari developer wa serikali wako morogoro wanaendelea kutengeneza sasa ni mwezi wa nne , kwa nini wapewe NMB?
By the way kwa nini haijatangazwa tender ili CRDB ,NMB ,NBC ,na kampuni nyingine zenye uwezo ziombe ili washindanishwe mwenye uwezo achukue?
walijuaje NMB pekee ndiye mwenye utaalamu wa kutengeneza mifumo hio na sio CRDB?
wali wa engage bank nyingine wakakataa?
kunamaswali mengi sana hapa.
Kumbuka hawa waheshimiwa walisha kaa kikao cha kuihamishia wizara ya TEHAMA e-GA ili waweze kuimiliki na ku control kazi zake ,badala waiimarishe wanaibomoa.
 
una taarifa ya kikao walichokaa wizara ya fedha na mipango few days kabla JPM hajafariki elit wa IT?
Walitaka e-GA ife kipindi cha JPM wakashtukiwa lakini sasa wako full na watafanikiwa ,wameweka watu kila sehemu yenye maamuzi .Development ya mifumo serikalini iko kwenye miezi sita ya mwisho
Hawatafanikiwa
 
Nadhani wewe umetenda haki kwenye mjadala… siyo Yule kinabo olimpio

Hapa ipp changamoto… pia umegusia very important issue ya single source kwenye ununuzi… ni banana skin hiyo

Uko very constructive mkuu
Nchi ni yetu sote , sina shida CRDB akishirikishwa lakini kuwe na uwazi tu wa namna tender imepatikana , ili kuondoa maswali kama ya mleta maada olimpio , kukiwa na maelezo huenda wako sahihi ,we just need the information
 
Sasa mwanahisa tokea lini akapewa code,configuration mimi na zungumzia wafanyakazi wa nje wanaofanya kazi NMB, wenye access na mifumo na network ya NMB ambao wanafanya kazi kwa mikataba (Technical Part)...... hivi unajua ramsomware attack? Halafu akuache baada ya mkataba wake kuisha wakati chocho zote anazijua.......

Niletee audit report ya NMB upande wa IT....... kama haipo ushajiuliza why hawaiweki hadharani?Wewe najua hutaki na siasa umezijaza kichwani,ila bank zote zinapigwa kila siku na wewe huwezi jua na hautokuja kujua, sababu taarifa zake haziendi public. Kuna taasisi naijua nishafanya nayo kazi 2019,network/mifumo yao ipo chini ya wahindi ila walipigwa na Ramsomware attack wakalipa hela ndefu.

Hivi source kuu ya Cybersecurity attack unazijua ?

Unaijua Ramsomware Attack,White and black hat wanavyo fanya kazi ........?

Hivi ushawahi kuingia kwenye device yoyote ile server,storage au any network device.....au hata kudisplay "hello world... " kwa kitumia programing language yoyote ?

Naona kama naongea na wanasiasa,kwani nazani hutonielewa.

Vitu vingine ukikaa kimya hupungukiwi kitu, ila duniani halipo taifa linalo wapa watu wasio waamini mifumo yao na network yao halipo taifa hilo na hamna tasisi yyt ambayo haijawa attacked kama sio leo basi kesho.

CIA,FBI, MOSSAD nk washapigwa, pamoja wamewaajili watu wanao wajua na walio wafanyia vetting.
Acha mambo ya darasani ya kukariri notes ulizodanganywa

Bado unaamini mambo ya darasani ,Naona unatao lecture wakati walimu wako hata mwana sesere hawawezi tengeneza
 
Wewe kichwa maji sana 40% ndio inakufanya uamini NMB apewe hiyo kazi?

-Wafanyakazi wa NMB wanalipwa na kuajiriwa na nani? What's the vetting process?
-sera ya usiri katika kazi NMB ipoje
-NMB ni taasisi ya kifedha, inawezekana vipi wapewe kazi ya mifumo ya kielectronic wakati business line yao ni kudeal na fedha na sio technology.
-Kumbuka mwenye hisa kubwa ndiye muamuzi mkuu, sasa serikali itaweza kusema nini kuhusu mambo yakienda tofauti?

Moja, tunaitaka NMB na SERIKALI watuwekee business license kwamba NMB pia wana deal na kuendesha biashara au huduma za kiteknilojia

Pili, mfumo wa ega unahusisha malipo na huduma mbalimbali kwa serikali, hivyo serikali ituhakikishie kuwa hakuna taarifa au malipo yatakayochepushwa kwenda NMB.

Tatu, sasa ni wakati wa ofisi ya CAG watumishi wake wachaguliwe hasa Chief officer asiteuliwe na rais ili awe huru kupitia na kukagua taasisi mbalimbali.

NB. Kuna mfumo wa malipo serikalini GePG hasa upande wa manunuzi ya umeme kuna wizi wa uchepushaji fedha za manunuzi ya umeme unafanyika huko, yaan ni kufuru huko hatari.
Mkuu inaonekana unataarifa za wizi wa uchepushaji wa pesa za manunuzi ya umeme hebu tuelekeze kwa kina inakuwaje?
 
Back
Top Bottom