EAGT na TAG wamaliza tofauti zao na minyukano ya miaka mingi

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) limefikia maridhiano ya kumaliza tofauti za muda mrefu zilizotokana na mgawanyiko wa kihistoria wa Assemblies of God nchini Tanzania. Mzizi wa mgawanyiko huo ulianza mwaka 1982, wakati TAG ilipogawanyika na kundi lililokuwa likimuunga mkono Askofu Moses Kulola kuunda EAGT, huku kundi jingine likiendelea na TAG chini ya uongozi wa Askofu Emmanuel Lazaro.

Moja ya migogoro iliyodumu kwa miaka mingi ilihusu umiliki na matumizi ya mali na maeneo ya makanisa, ikiwemo eneo la Temeke, Dar es Salaam. Katika kesi iliyofikishwa Mahakama Kuu mwaka 2021, EAGT ilidai kuwa imekuwa ikilitumia eneo hilo tangu miaka ya 1970 na kwamba iliomba rasmi kugawiwa eneo hilo tangu 1978. Mahakama ilibainisha kuwa TAG, ambayo baadaye ilihusishwa na EAGT katika historia hiyo, pia ilikuwa miongoni mwa waombaji wa eneo hilo.

Miaka kadhaa baadaye, tofauti hizo zimefikia hatua mpya. Agosti 21, 2026, katika Mkutano Mkuu wa TAG unaofanyika Dodoma, viongozi wa TAG na EAGT wamekubaliana kumaliza tofauti hizo kwa njia ya maridhiano, kuacha mashauri na migogoro ya mali iliyotokana na historia hiyo na kuanza ukurasa mpya wa ushirikiano. Uamuzi huo umeelezwa kuwa hatua ya kuimarisha amani, umoja na upendo wa Kikristo, huku pande zote zikikubaliana kutotumia tena tofauti hizo kama chanzo cha mgawanyiko.

Hatua hiyo inaweka alama mpya katika historia iliyoanza zaidi ya miaka 40 iliyopita, kutoka kwenye mgawanyiko wa 1982 hadi maridhiano ya viongozi wa makanisa hayo mawili mwaka 2026

USSR
FB_IMG_1787394387902.jpg
 
Sasa waungane. Sio mnahubiri upendo, umoja na mshikamano kumbe nyie wenyewe .Waterbeach na chuki na vinyongo
 
Mungu ana kazi sana. Mwaka 1982 Roho Mtakatifu akawaambia wagawanyike, leo mwaka 2026 Roho huyohuyo amewaambia waungane tena baada ya miaka 44! Tuseme tu ukweli, ule ulikuwa ni mgogoro wa ego za viongozi na maslahi, ila wakaamua kutumia tu mgongo wa kanisa.
 
1. MASLAHI BROTHER..
 
Haya Makanisa ya kilokole hayawezi kuungana maana yamekaa kimaslahi sana,kila mtu ana kanisa lake ndani ya hiyo TAG au EAGT, na kila jumapili anahubiri yeye tu, na makanisa yao yapo mjini tu maana mjini washiriki wana uchumi mzuri na wanatoa hela,
 
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) limefikia maridhiano ya kumaliza tofauti za muda mrefu zilizotokana na mgawanyiko wa kihistoria wa Assemblies of God nchini Tanzania. Mzizi wa mgawanyiko huo ulianza mwaka 1982, wakati TAG ilipogawanyika na kundi lililokuwa likimuunga mkono Askofu Moses Kulola kuunda EAGT, huku kundi jingine likiendelea na TAG chini ya uongozi wa Askofu Emmanuel Lazaro.

Moja ya migogoro iliyodumu kwa miaka mingi ilihusu umiliki na matumizi ya mali na maeneo ya makanisa, ikiwemo eneo la Temeke, Dar es Salaam. Katika kesi iliyofikishwa Mahakama Kuu mwaka 2021, EAGT ilidai kuwa imekuwa ikilitumia eneo hilo tangu miaka ya 1970 na kwamba iliomba rasmi kugawiwa eneo hilo tangu 1978. Mahakama ilibainisha kuwa TAG, ambayo baadaye ilihusishwa na EAGT katika historia hiyo, pia ilikuwa miongoni mwa waombaji wa eneo hilo.

Miaka kadhaa baadaye, tofauti hizo zimefikia hatua mpya. Agosti 21, 2026, katika Mkutano Mkuu wa TAG unaofanyika Dodoma, viongozi wa TAG na EAGT wamekubaliana kumaliza tofauti hizo kwa njia ya maridhiano, kuacha mashauri na migogoro ya mali iliyotokana na historia hiyo na kuanza ukurasa mpya wa ushirikiano. Uamuzi huo umeelezwa kuwa hatua ya kuimarisha amani, umoja na upendo wa Kikristo, huku pande zote zikikubaliana kutotumia tena tofauti hizo kama chanzo cha mgawanyiko.

Hatua hiyo inaweka alama mpya katika historia iliyoanza zaidi ya miaka 40 iliyopita, kutoka kwenye mgawanyiko wa 1982 hadi maridhiano ya viongozi wa makanisa hayo mawili mwaka 2026

USSRView attachment 3654881
Makanisa ya kilokole ni makanisa ambayo yanalenga fedha ndiyo maana makanisa yao yanamilikiwa na watu na siyo Taasisi. na ndiyo maana huwezi kusikia mchangaji au Askofu amehamishwa. Walokole wameharibu sana ukristo.
 
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) limefikia maridhiano ya kumaliza tofauti za muda mrefu zilizotokana na mgawanyiko wa kihistoria wa Assemblies of God nchini Tanzania. Mzizi wa mgawanyiko huo ulianza mwaka 1982, wakati TAG ilipogawanyika na kundi lililokuwa likimuunga mkono Askofu Moses Kulola kuunda EAGT, huku kundi jingine likiendelea na TAG chini ya uongozi wa Askofu Emmanuel Lazaro.

Moja ya migogoro iliyodumu kwa miaka mingi ilihusu umiliki na matumizi ya mali na maeneo ya makanisa, ikiwemo eneo la Temeke, Dar es Salaam. Katika kesi iliyofikishwa Mahakama Kuu mwaka 2021, EAGT ilidai kuwa imekuwa ikilitumia eneo hilo tangu miaka ya 1970 na kwamba iliomba rasmi kugawiwa eneo hilo tangu 1978. Mahakama ilibainisha kuwa TAG, ambayo baadaye ilihusishwa na EAGT katika historia hiyo, pia ilikuwa miongoni mwa waombaji wa eneo hilo.

Miaka kadhaa baadaye, tofauti hizo zimefikia hatua mpya. Agosti 21, 2026, katika Mkutano Mkuu wa TAG unaofanyika Dodoma, viongozi wa TAG na EAGT wamekubaliana kumaliza tofauti hizo kwa njia ya maridhiano, kuacha mashauri na migogoro ya mali iliyotokana na historia hiyo na kuanza ukurasa mpya wa ushirikiano. Uamuzi huo umeelezwa kuwa hatua ya kuimarisha amani, umoja na upendo wa Kikristo, huku pande zote zikikubaliana kutotumia tena tofauti hizo kama chanzo cha mgawanyiko.

Hatua hiyo inaweka alama mpya katika historia iliyoanza zaidi ya miaka 40 iliyopita, kutoka kwenye mgawanyiko wa 1982 hadi maridhiano ya viongozi wa makanisa hayo mawili mwaka 2026

Ni hatua nzuri
Nai hatua nzuri
 
Kwann FPCT, sjui mashahidi, mara efatha TAG na ministries Hawa wote si walokole ama ? Mtu anaruka kanisa la FPCT mbagala anaenda calvary church kwa mwamposa
 
Back
Top Bottom