EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!


Wewe umejua kumshauri.

Ukipata Kuracya MUNGU umekula bingo
 
Mkuu Paskali, wewe ni mtu muhimu sana hapa nchini kwetu, natambua kuna siku tu "many potentials within you" zitakuja kufahamika, kuhitajika, kutatafutwa mbele ya umma na hata kuthamininika.
 


Mzee wangu pole sana.

Ila mimi nina haya machache ya kukuambia:

Kwa umri wako ulipofikia, kwa sasa unapaswa uweke kambi ya kisiasa maeneo yako unayoishi. Either iwe kata, tarafa, wilaya au mkoa. Ulipaswa uanzie maeneo hayo.

Usitake kukimbilia makubwa angali madogo bado hujayafulfulil mzee wangu. Kauli yako ya kusema kwamba u DC hauna hadhi kwako ni kauli yenye kuonesha tabia ya "Sizitaki Mbichi Hizi". Na wengi wamepitia huko kabla hawajajiupgrade juu zaidi. Huwezi kutembea kabla hujatambaa mzee wangu

Hiyo degree yako ya uzeeni isikupe kiburi mzee wangu, be humble, start from the grassroots na one day kama muda utakuwa bado unakuruhusu basi utaweza kufika juu pale unapopataka.

Hivi mzee wangu nikuulize swali, hivi ukigombea nafasi ya uenyekiti wa mkoa/wilaya wa CCM wa mkoa gani unahisi winning probability yako itakuwa >80%. Kama hakuna basi jua wewe bado kidagaa sana kwenye siasa za nchi hii.
 

Kazi unayo bro.
 

[emoji3]
 
Dah! Pole sana mkuu. Kwa hiyo ile milioni 1 imekwenda na maji! Achilia mbali gharama nyingine ulizoingia!!!

Mimi ndiyo maana naiyogopa sana siasa kuliko ilivyo kawaida.
Hiyo 1m bora angeenda beach kidimbwi, kuliko kuchangia chama dola chenye miradi mingi,
Mojawapo kununua na kwanyamazisha wapinzani wapinzani,
 
Doris Mollel ni bingwa wa Rushwa sijui anatoa wapi Hela huyu mwanamama, aligombea uwakilishi wa UVCCM ubunge vijana akatoa PESA za kutisha na wajumbe wakala kichwa
 
Hili tulihesabu limepita, maisha yaendelee na kazi iendelee.
Na mimi kwa upande wangu, naendelea kumuomba sana Mungu, anifundishe kunyamaza!.[emoji818][emoji817][emoji1534]
 
Hivi mwashishi nguli, unamiliki kampuni PPRA, wakili wa kujitegemea,

Unahangaika na siasa kiasi cha kudhalilika hivi, ina maana huna hata washauri?

CCM hawakutaki, hata makala zako kabla ya kujipeleka CCM zipo humu jamvini,

Mojawapo ni hii, Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuichagua CCM?

Siasa imekukataa fanya mambo mengine,
 
Pole sana Paschal.
Mimi si mwanasiasa lakini nawaheshimu sana wanasiasa.
Kazi uliyoifanya ni kubwa mno.
Kupata si werevu na kukosa si ujinga.

Wanaokubeza wewe wanasemaje kuhusu Rails Odinga?

Usiku mwema mpambanaji.
 
Nchi hii imeoza na ili uwe kiongozi lazima umwage rushwa na sio rushwa ndogo ni rushwa kubwakubwa .Hii Hali haikubaliki kwa mstakabali wa nchi yetu manake tunakuwa na vhiongozi vilaza ambao hawana mchango wowote kwa Taifa zaidi ni kupiga hela za nchi yetu. Hii ni aibu kubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuacha hii hali iendelee.

EE MUNGU WA MBINGUNI ULIE JUU NAKUOMBA ULIKUMBUKE TAIFA LAKO LA TANZANIA.
 
Mimi naona ungekubali tu kuwaona 'wahusika' kama ulivyoshauriwa kwani kwa maelezo yako ni kuwa hivyo ndiyo vigezo na masharti yenyewe short of that ni kutwanga maji kwenye kinu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…