East Africa Federation na Hatma ya Tanzania

East Africa Federation na Hatma ya Tanzania

IJUE EAC na MAONO YAKE

Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EAC) ni shirika la kikanda la Serikali za nchi 7 Washirika: Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kenya, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Sudan Kusini, Jamhuri ya Uganda, Na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na makao yake Makuu Huko Arusha, Tanzania.

EAC ni nyumbani kwa takriban raia milioni 320, ambao zaidi ya 30% ni idadi ya watu mijini. Kwa eneo la ardhi la kilomita za mraba milioni 4.8 na jumla ya Pato la Ndani la dola bilioni 305.3 za MAREKANI, utambuzi wake una umuhimu mkubwa wa kimkakati na kijiografia na matarajio ya eac iliyosasishwa na kuimarishwa tena.

Kazi ya EAC inaongozwa na Mkataba wake ambao ulianzisha Jamii. Ilitiwa saini tarehe 30 novemba 1999 na kuanza kutumika tarehe 7 julai 2000 kufuatia kuridhia Kwake Na Nchi Tatu Za Awali Za Washirika - Kenya, Tanzania na Uganda. Jamhuri ya Rwanda Na Jamhuri ya Burundi zilijiunga Na Mkataba WA EAC tarehe 18 juni 2007 na zikawa Wanachama kamili wa Jamii hiyo kuanzia tarehe 1 julai 2007, Wakati Jamhuri ya Sudan Kusini ilijiunga na Mkataba huo tarehe 15 aprili 2016 na kuwa Mwanachama kamili tarehe 15 agosti 2016. Mwanachama mpya Wa Jumuiya hiyo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alijiunga na Mkataba wa EAC mnamo 8 aprili 2022 na akawa mwanachama kamili mnamo 11 julai 2022.

Kama moja ya makundi ya kiuchumi ya kikanda yanayokua kwa kasi zaidi duniani, EAC inaongeza na kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi Washirika katika nyanja mbalimbali muhimu kwa faida yao ya pamoja. Nyanja hizi ni pamoja na kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa sasa, mchakato wa ujumuishaji wa kikanda unaendelea kikamilifu kama inavyoonyeshwa na maendeleo ya kutia moyo Ya Jumuiya ya Forodha Ya Afrika mashariki, kuanzishwa Kwa Soko La Pamoja mnamo 2010 na utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya ya Fedha Ya Afrika mashariki.

Hali ya sasa
Mchakato wa Kuelekea Shirikisho La Afrika mashariki unafuatiliwa kwa haraka, ukisisitiza dhamira kubwa ya uongozi Wa Afrika mashariki na wananchi kujenga kambi ya kiuchumi na kisiasa yenye Nguvu na endelevu Ya Afrika mashariki. Mnamo Mei 2017, Wakuu wa Nchi ZA EAC walichukua Shirikisho la Kisiasa kama mfano wa mpito wa Shirikisho la Kisiasa La Afrika mashariki.
 
Tukiamua tunaweza na ndio itakuwa moja ya ukombozi wa kweli wa mwafrika.
Ukombozi pekee wa mwafrika ni kuwa na akili timamu ( kuwaza vyema na kufanya maamuzi bora kwake na kizazi chake) miungano haita leta jipya lolote zuri zaidi ya migogoro isiyo na tija.

Zanzibar na Tanganyika imeshindikana kuwa nchi moja mpaka sasa zaidi ya kutumia majeshi kulinda na hapo ni eneo dogo sasa uongeze hao wengine wenye political instability kubwa si ndio majanga makubwa kujitokeza na mauaji yasiyo koma, think twice.
 
Unapenda Afrika iwe nchi moja ?
Afrika haiwezi kuwa nchi moja kama ambavyo ulaya sio nchi moja.
Lakini muunganyiko wa afrika utasaidia kutatua changamoto nyingi na pia afrika kuwa na usemi mmoja duniani.
 
U.S.A mpaka leo sio stable kuna majimbo yanataka kujitenga hizi huwa ni failed ideas huwezi unganisha watu wasio ona faida ya kuungana. Ndio hiki hiki cha Tanganyika na Zanzibar muungano wa kipumbavu hata huo wa EAC utakuwa version 2.0 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kama ungekuwa unakuja kwa facts ingefaa zaidi. Mimi huwa napenda kuongea maneno kwa facts

Hapo kwenye rangi ya kijani hizo zote ni federal states

1693897064120.png

Ukiunganisha ni hizo nchi zingine tunakuwa na nguvu katika nyanja za kimataifa. Faida ni nyingi kuliko hasara
 
Afrika haiwezi kuwa nchi moja kama ambavyo ulaya sio nchi moja.
Lakini muunganyiko wa afrika utasaidia kutatua changamoto nyingi na pia afrika kuwa na usemi mmoja duniani.
AU ni picha hali ya mwafrika alivyo na EU ni picha halisi ya mzungu alivyo
 
View attachment 2739420

Kabla ya wakoloni kuja Africa tuliishi kwa namna yetu. Bahati mbaya historia ya Afrika imepotezwa kwa makusudi au kupotoshwa.
EAST AFRICA COMMUNITY KWA SASA

  1. The Republic of Burundi
  2. The Democratic Republic of the Congo
  3. The Republic of Kenya
  4. The Republic of Rwanda
  5. The Republic of South Sudan
  6. The Republic of Uganda
  7. The United Republic of Tanzania
Nchi zinazotarajiwa kujiunga
  1. Somalia
  2. Comoros
  3. Mozambique
  4. Sudan
  5. Ethiopia
  6. Angola
  7. Republic of Congo
  8. Zambia

Kuna mpango ambao ulianzishwa wa kuelekea kwenye Political Federation of the East African states. Tayari kuna hatua ambazo zinatakiwa kupitiwa ili kufikia katika hatua hiyo:-
  1. Customs Union
  2. Common Market
  3. Monetary Union
Na mwisho wa siku tunafikia katika kujenga nchi moja itakayokuwa na kiongozi mmoja.

Tayari Custom Union ilishapitishwa tangu mwaka 2005. Unaweza ukaipitia hapa na kusoma mambo kadha wa kadha Customs
Tayari Common Market ilishasainiwa mwaka 2010 na ilikuwa inatarajiwa kuanza kutumika mwaka December 2015. Kuna mambo kadha wa kadha yalitokea lakini ipo katika hatua za kuanza kutumika. NB: Kama sisi watanzania tutaendelea kulala mabadiliko yatafika na sisi bado tunabishana ndani ya nchi huku wenzetu wakijiandaa kutumia fursa.
Monetary Unioni ilishasainiwa mwaka 30th November 2013. Na ilikuwa inatakiwa ndani ya miaka 10 iweze kuanza kufanyiwa mikakati. Tayari kwa sasa tumo ndani ya miaka hiyo. Huenda baada ya muda hii itawekwa kwenye action.

NINI HATMA YA TANZANIA NA SIASA ZETU?
Tusipowekeza katika human capital na kuendeleza siasa hizi za kizamani, watu wa Tanzania watakuja kuachwa kutokana na fursa zitakazoendelea katika nchi mpya itakayozaliwa. Hili jambo kuna wengine wanaliona kama ndoto. Lakini kutokana na mabadiliko ya siasa za kidunia naliona linaenda kutokea siyo muda mrefu.

Sasa basi viongozi wetu wanawaandaa vipi watanzania kuweza kuingia katika hatua hizo zinazokuja? Itafikia wakati Tanzania itashindwa kuwa na sauti kutokana na kuzidiwa kura na wengine. Maana nchi zinazidi kuwa nyingi na influence ya Tanzania inazidi kupotea.

Tanzania tulikuwa tunaringa kwa kuwa na rasilimali nyingi. Ona sasa kiburi hatuna tena kutokana na jambo hilo maana DRC tayari naye ni member. Tanzania imekuwa nchi ya kawaida tu ndani ya EAC. Kama tutaendelea kuchelewesha mambo haya wenzetu watafanya wao na kutukuta sisi tunaachwa, au wachache wananufaika na mtangamano huu.

Nitaendelea kweka Statistical Data na References ili kufumbuana macho.....
Wanaokwamisha ni Watanzania kutokana na mawazo ya ujamaa mbuzi.

Umbumbumbu uliopitiliza.
 
Kama ungekuwa unakuja kwa facts ingefaa zaidi. Mimi huwa napenda kuongea maneno kwa facts

Hapo kwenye rangi ya kijani hizo zote ni federal states

View attachment 2739503

Ukiunganisha ni hizo nchi zingine tunakuwa na nguvu katika nyanja za kimataifa. Faida ni nyingi kuliko hasara
Unataka facts gani zaidi ya kukuelezea hicho kinacho endelea kwenye hayo maeneo uliyotaja au unataka yafanyike mauaji ya kutokomeza wakazi wa asili ili patawalike bila nguvu kubwa iliyo against utawala ?
 
Hata hiyo hiyo Russia Chechnya ina vuguvugu la kumeguka since wayback
Nadhani unaandika vitu tu bila kufanya research. Hapa tunaongea kwa data siyo propaganda za kitoto kama hujasoma.
Taarifa zote zipo kwenye mtandao usizike kichwa chako kwenye mchanga.
Hii ramani ni Russia ndani yake kuna Republic 21 na kila republic wapo na constitutions zao. Na wanafanya uchaguzi ndani ya Republics zao.
1693897594902.png

Ukitaka ujifunze zaidi hebu jaribu kupitia hapa:
 
Wanaokwamisha ni Watanzania kutokana na mawazo ya ujamaa mbuzi.

Umbumbumbu uliopitiliza.
Nadhani zama hizo zimepitwa na wakati. Kuanza kuendelea na mambo ambayo hayana faida ni kupoteza muda. Madamu Tanzania ndio waanzilishi lazima mkakati huu uendelee

Haya hapa chini ni maneno ya waanzilishi wa EAC

"The balkanization of Africa into 53, mostly sub-optimal States, has meant that Africa cannot have a large internal market under one Political Authority; have no
power to negotiate with the rest of the world. This balkanization must stop
”- H.E. Yoweri Kaguta Museveni President, Republic of Uganda

"We have everything to gain in East African Federation in terms of political stability, greater feeling in safety in numbers and as an economic entity better able to fight poverty" - H.E. Benjamin William Mkapa President, United Republic of Tanzania

''I firmly believe that regional integration is not a choice but a necessary strategy for sustainable development. On a cultural level, regional integration solidifies the unity of communities with personalities and common history, language and culture" - H.E. Mwai Kibaki President, Republic of Kenya
 
Nadhani unaandika vitu tu bila kufanya research. Hapa tunaongea kwa data siyo propaganda za kitoto kama hujasoma.
Taarifa zote zipo kwenye mtandao usizike kichwa chako kwenye mchanga.
Hii ramani ni Russia ndani yake kuna Republic 21 na kila republic wapo na constitutions zao. Na wanafanya uchaguzi ndani ya Republics zao.
View attachment 2739511
Ukitaka ujifunze zaidi hebu jaribu kupitia hapa:
Kwa hiyo 1994 na 2009 Russia na Chechnya walikuwa wanacheza mziki ? Unajitoa ufahamu
 
Nadhani zama hizo zimepitwa na wakati. Kuanza kuendelea na mambo ambayo hayana faida ni kupoteza muda. Madamu Tanzania ndio waanzilishi lazima mkakati huu uendelee

Haya hapa chini ni maneno ya waanzilishi wa EAC

"The balkanization of Africa into 53, mostly sub-optimal States, has meant that Africa cannot have a large internal market under one Political Authority; have no
power to negotiate with the rest of the world. This balkanization must stop
”- H.E. Yoweri Kaguta Museveni President, Republic of Uganda

"We have everything to gain in East African Federation in terms of political stability, greater feeling in safety in numbers and as an economic entity better able to fight poverty" - H.E. Benjamin William Mkapa President, United Republic of Tanzania

''I firmly believe that regional integration is not a choice but a necessary strategy for sustainable development. On a cultural level, regional integration solidifies the unity of communities with personalities and common history, language and culture" - H.E. Mwai Kibaki President, Republic of Kenya
Jidanganye, unadhani kelele za Nchi kupigwa mnada zinatokana na mawazo yapi kama sio ujamaa mbuzi?
 
Kwa hiyo 1994 na 2009 Russia na Chechnya walikuwa wanacheza mziki ? Unajitoa ufahamu
Mzee unaleta issue za kipuuzi tu hazina kichwa wala miguu. Nimekueleza ndani ya Russia 22 ukiunganisha na Crimea. Sasa unaongea vita vilivyotoke miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Njoo na points na uandike kama mtu mwenye akili na uliyeenda shule.
 
Jidanganye, unadhani kelele za Nchi kupigwa mnada zinatokana na mawazo yapi kama sio ujamaa mbuzi?
Mzee unahamisha mada. Kama unataka tujadili ili watu waweze kujifunza jikite kwenye mada.
Tuandike Changamoto na faida. Siyo kuandika mipasho kama tunajadiliana na walevi.
 
Mzee unaleta issue za kipuuzi tu hazina kichwa wala miguu. Nimekueleza ndani ya Russia 22 ukiunganisha na Crimea. Sasa unaongea vita vilivyotoke miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Njoo na points na uandike kama mtu mwenye akili na uliyeenda shule.
Acha kuwa na mawazo ya ajabu huo upuuzi unao ufikiria hauwezekani kamwe kutokea.
 
Back
Top Bottom