East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Kwea upande wangu mimi naona hii kiini macho, Kamala hata hajamaliza kukusanya maoni tayari Rwanda na Burundi wameruhusiwa! sasa serikali likuwa inapoteza pesa za nini kukukusanya hayo maoni kama walishaamua? BTW why rush so much? kuna kitu tunafichwa au?
 
Hivi Wasomali wakiomba kujiunga Kenya itawaruhusu? Huu ni mzigo sisi Watanzania tumetwishwa na hii Jumuiya.

Wanasema tumepanua uwigo wa biashara!! Kwanini watu hawa wanazungumzia biashara, na siyo UZALISHAJI na AJIRA?? Warundi na Wanyarwanda wanaongeza WATU, ARDHI, na RASILIMALI kiasi gani from what we already have?

Wakenya wanatusengenya kwamba Watanzania tu wajinga, wavivu, hatujui Kiingereza. Now, why do they want to unite with us. Watanzania kila walipozungumza wamepinga uanachama wa Rwanda na Burundi. Ninashangaa kwanini serikali imepuuza maoni hayo.
 
HIVI INAKUWAJE KAMA MMOJA WA MARAIS WA JUMIA NI MCHOKOZI MF AKIIPIGA CONGO INA MAANA ITABIDI TUWE NA MSIMAMO WA PAMOJA NASISI TUMPIGE CONGO AU KUMUIBIA?

position yetu katika tukio la kushambuliwa kwa mmoja wa wanachama ikoje?? nadhani mnajua namana tulivochoma pesa na damu kwenye vita za ukombozi na ile ya kagera ,,sasa tupo na mabwana wa vita bora jeshi letu lianze kujiandaa kwenda kusaidia iwapo jirani anaingia vitano...kodi na dhahabu si zipo ,tutagaramia ,,watanganyika hatuna neno!!!
 
Any suggestion that Tanzanias are xenophobic about their Kenyan and Ugandan compatriots is at the least ludicrous. We are a counrty that was willing to deffer our its independence to allow our countries emerge as a federation. History records the selfishness of some leadrs that sabotaged that aspiration. History also illustrates why the former EAC collapsed at the hands of selfishness. No. Tanzanians are not exenophobic; just smart. Once beaten twice shy.

The truth of the matter is, Kenyan are more driven by economic interests, hence the catalogoe of economies of scales that are thrown our way. This is where our friends have never come to undestand us as a people. Tanzanians are more about our sense of unity and way of live. Economics are fine but we value our the being more. This expains why tanzania was willing to sacrifice economic prosperity in support of the liberation struggle while Kenya was in bed with the apartheid regime. It is also true that for Kenyans the EAC it more about econmics and space for expansion.

Look here. Kenyans see vast expanses of land lying idle in a country without the kind of population pressures as theirs. But which Tanzania can move to Kenya and get a peace of land? You will have to excuse me but our friends can accuse us of so many things but they need to come to grips with the fact that Nyerere gave them their best chance, and they blew it. He might have been naive.

The current leadership cannot afford to make a mistake or the opposition will eat them alive.
 
mikael,
Mkataba wa Jumuiya ya SADC unaelekeza kwamba nchi mwanachama ikishambuliwa kivita, SADC ina jukumu la kuitetea kutokana na shambulizi hilo.

Kipengele hicho ndicho kilichohalalisha Zimbabwe,Angola,na Namibia kuingia DRC, na kuzima mashambulizi ya Rwanda, na Uganda. Operesheni ya majeshi ya SADC iliitwa "operation restore sovereignity."

Tanzania tulikuwa na kikosi chetu ndani ya DRC wakati Rwanda wanavamia lakini askari hao waliondolewa kwa msaada wa ndege za Afrika Kusini!!

Ninavyoona mimi, pamoja na kuwepo kwa mikataba ya ulinzi, nchi wanachama zina hiari ya kuangalia maslahi yake binafsi kabla ya kushiriki ktk utekelezaji wa mikataba hiyo.

Ninaamini Tanzania na Afrika Kusini ziliona ni bora kusaidia kidiplomasia kuliko kijeshi ktk mgogoro wa DRC.
 
Sasa haya maswali ya ulinzi na usalama wa nchi wanachama si yatakuwa yamejibiwa kwenye katiba ya EAC. Hiyo Katiba iko wapi au ndio yale yale kuonekana sisi wadanganyika hatujui kitu hivyo no one is even bothered to offer it.
 
Binafsi sioni ubaya wa Rwanda na Burundi kuingia kwenye jumuiya ya AM kwani idadi ya nchi inavyozidi kuwa kubwa ndiyo kunapatikana upoaji zaidi wa tabia za binafsi hasa zilizo hasi za kila nchi kama vile ukabila,rushwa nk.

Tukiwa na jumuiya kubwa kiasi cha kutosha yaliyo mema ya kila mwana chama yanakuwa makuu na kuyameza yaliyo mabaya.

Tatizo langu ni kwa nini baada ya kupokelewa kwa Rwanda Na Burundi makao makuu yasihamie Mwanza au Shinyanga, yaani magharibi kidogo kutoka Arusha ili kudumisha hali ya makao hayo kuwa katikati ya jumuiya hiyo? (shift of centre of gravity to reflect alteration in body dimensions)
 
Chinga,

Nimesoma ujumbe wako. Nashukuru leo nimefanikiwa kuingia. Uliyoyasema hayana ukweli. Kwa sasa utanisamehe kwamba mfululizo wa vikao unanikosesha kujibu kila hoja kwa kina. Nimeingia ghafla UK. Kwa wale mliohuku tunaweza kuwasiliana ingawa naondoka kesho kurudi Tanzania. Wakati huu nimekosa wasaa wa kuitisha mkutano. Ila nitafika wakati mwingine na kufanya mkutano. Niko kikazi mahali kwingine lakini malazi yako:

Chumba no. 105

Hamilton House Hotel
60 - 64 Warwick Way
Victoria - London
SW1V 1SA
United Kingdom
Tele: + 44 (0) 20 7821 7113
Fax: + 44 (0) 20 7630 0806

Kwa kawaida huwa natoa mawasiliano nilipo kwa email kwa watu mahususi kwa sababu za kiusalama lakini kutokana na kuchelewa kutoa taarifa naomba ujumbe uwafikie wote kwa njia hii kwa haraka.

Last promise, pindi nikifika nyumbani tarehe 5/12 nitajibu hoja zote

JJ
 
Mnyika
kila hoja ukiiulizwa unasema una shughuli nyingi, sasa hujawahi mbunge tayari una shughuli nyingi.

suala lako la wewe kubebwa na kanisa na kufanyiwa mitihani, ulikimbia na kudai una shughuli nyinyi na hili nalo, kwani majibu ya hoja zangu nadhani hayahitajii hata dakika 4.

Mzee Kaburu aliyaona haya ndiyo akaona bora aanze kwenda CCM, aliona ukaskazini na udini umejikita Chadema na pia chama kimekosa mwelekeo ni NGO ya wajanja wa kaskazini tu, haiwezekani chama kiongozwe na DJ Mbowe, na hata mambo yake ya club Bilicanas yamechangia sana kuliangamiza taifa na ukimwi, lakini kwa vile ni mkwe wa mwenye NGO (CHAMA) basi amepewa uenyekiti taifa.

Sasa mmeleta utapeli mwinyine kuwa atasoma degree mbili kwa miaka mitatu tena nchi tatu. Japan.uk na marekani huo ubabaishaji wa chadema.
usitokose chochote toka kwa Cameroon David. ila wenzeo huwa wanawekwa five star hotel, wewe vipi? na hapo ulipo nenda buckingham palace ukamuone Queen hapo unatembea tu kwa miguu kama dakika tano, ili akupe mikakati ya utawala wa kifamilia kama wa Mtei na chadema.kwani Queen huenda akampa mjukuu wake Prince William hivyo na chadema itabidi mjukuu wa Mtei apewe.

Pia naomba utupe ukweli wa biashara ya dhahabu anayofanya mwenyekiti wako na jamaa wa Cameroon.?
tunaposema NGO tuna kila nukta ya ushahidi.
 
Chinga:

Kwa dakika 4 uzilizosema:

1. Si kweli kwamba nilipata division ya mwisho kidato cha sita. Ukweli ni kuwa nilipata division 2.

2. Si kweli kwamba nilibebwa na kanisa katika matokeo yangu ya kidato cha nne ambapo nikapata div 1.7 nikiwa na A tisa. Ukweli ni kwamba matokeo yangu kielimu yamekuwa juu kipindi chote. Katika maisha yangu yote kuanzia msingi na kuendelea nimekuwa nikishika nafasi ya kwanza. Sasa ambalo linahitaji muda kuelezea ni flactuation kati ya O-level na level.

3. CHADEMA si chama cha wakristu. Tembelea tovuti uangalie safu ya viongozi uangalie kama wachaga ni wengi kuliko wengine. Infact watu wa kigoma na wasukuma tuko wengi zaidi ya wengine.

4. Si kweli kuwa wakristu ndio wengi zaidi katika safu za kitaifa za uongozi. Ukweli ni kuwa CHADEMA ndio chama pekee kikubwa chenye balance ya kidini katika safu zake. Nitachambua.

5. Nani atarithi uongozi wa CHADEMA baada ya Mbowe? Kwa yoyote anayefuatilia siasa ndani ya CHADEMA jibu hili liko wazi,labda yatokee mabadiliko baadae. Nitachambua.


6. Suala la Helikopta. Nitachambua.

7. BOT dyanasty. Nitachambua.

Ndio maana sikutaka kujibu kwa ufupi. Nitaongezea tarehe niliyosema.

Wakati mnasubiri uchambuzi,

Endelea kutafakari yafutayo;

Ni mkoa gani una mawaziri zaidi?

JJ
 
Good job John Mnyika,
achana na hawa kina chinga, ameshapewa vijihela na makamba huyu kuharibu status yako.

Hakikisha unajiwekea good international reputation huko uliko.
good luck.
 
Quarz
Kwani chadema haiwezi kujadili ila mtu hadi apewe pesa? jee wanaoijadili CCM wamepewa vijehela na nani? au hii forum ni ya chadema?maana utaona kuna misemo karibu ujiunge chadema n.k,

Mnyika kasema kuna undugu na kujuana ccm. mie nimehoji kama undugu basi upo chadema amnbako Mbowe kapewa uenyekiti na baba mkwe wake, na hata Mnyika hajajibu hilo. kuna mtoto wa Ndesamburo kapewa ubunge viti maalum hilo kakimbia kujibu.

kuna akina Mdee wamepewa sababu wa wanatoka kasikazini.
yeye mnyika kapewa kwa vile mama ni mtu wa kaskazini otherwise angesikia kwenye bomba.

suala la matokeo ya form six ya Mnyika nililiona humu na nilipofuatilia nimeona ana division three, lakini ana uongopea umma kuwa ana division two. wanabodi fuatilieni muone uongo wa Mnyika. au ndio akirudi Dar atatupa full story?

hakuna mwenye nia ya kuharibu personality ya mtu.
 
Unajua lazima tuwe makini tunapoongelea matatizo haya na ukweli wake. Kwa mafano, USA, Republican inajulikana kama chama cha watu weupe na matajiri na Democratic ni watu wenye asili ya kiafrika na watu wa kati. Ukiuliza ni kwa nini watu wanaamini hivyo hakuna mtu atakayekuambia kuwa Democratic in viongozi wengi wenye asili ya kiafrika kuliko Republican.

Sasa ni kwa nini watu wanaamini hivyo? Vyama vya CHADEMA na CUF havina sura ya kitaifa kama CCM. Na hayo matatizo siyo matatizo ambayo hawawezi kufanyiwa kazi. CHADEMA siyo chama cha ukoo au kabila fulani, ni chama cha kitaifa kisicho na sura ya kitaifa. Nadhani hivi vyama viwli ambavyo ni tegemeo pekee letu lililobaki, vinatakiwa kuchukua na kukubali haya matatizo na kufanyia kazi.

Chinga, unaposema Mnyika amebebwa na serikali ya CCM kwa kuwa ni mkristo unamaanisha kuwa serikali ya CCM ina udini. Nirekebishe kama sijakuelewa vizuri.
 
Chinga hapo ni logic ndogo sana,
chadema ina ungwa mkono kaskazini kuliko maeneo mengine,hiyo inakuwa ni sababu tosha kwanini wabunge wengi wanatoka mikoa hiyo.

pili kuhusu mnyika kitaaluma sidhani kama anahitaji kukuonyesha wewe uwezo wake kitaaluma, ila ungefuatilia tu historia yake au uwaulize watu waliosoma naye watakupa majibu ya uwezo wake kitaaluma, hata kama alipata div 3 hiyo haijashusha bado uwezo wake kitaaluma, au wewe unafikiri kuwa na akili sana ni kupata div I tu, kama wewe umekuwa kwenye taaluma utafahamu kuwa mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa lakini
kwenye mitahani ya mwisho akateleza kutokana na sababu mbalimbali, hiyo haimfanyi huyo mtu kuwa hana uwezo wa kitaaluma.

na zaidi ni kuwa john ana talent ya uongozi ambayo ni tofauti na ile ya taaluma, na kumalizia hakuna chama duniani ambacho hakina mapungufu, kwani wote hawa ni wanadamu na zaidi wengine wametumwa na ccm kuvuruga demokrasia.
 
Chinga huna hoja kama undugu upo ccm ambako wabunge zaidi ya 15 ni wanandoa, karume karithi urais akitoka anaingia mdogo wake ALI akitoka anaingia hussein mwinyi, wabunge wa east africa juzi kuna wanandoa ,mtoto wa mwinyi ,mdogo wake BILLALI

chinga ndugu yangu kama wewe baba yako ni mchimba chumvi hata kama una elimu hutatoka utabakia kuwa mchabiki .....l have a ccm card but i see a need for a stronger opposition ,and this dede mnyika is kind good ,tuunahitaji vijana aiana hii, kabla hujapoteza muda kutaka kujibiwa majibu ya mambo personel na mnyika kawatafute wale richmond wanaomkosesha kalala jk,kwalete umeme!
 
Sam
nilikuwa na maana alibebwa na kanisa si CCM, kwani yeye ni mkatoliki na kuna mpango wa kikatoliki kutawala nchi.

nilijibu hoja za mnyika alipoonyesha kuwa ccm kuna undugunaizesheni, wakati suala hilo jikoni kwake ni chadema, mfano mzuri mwenyekiti wa ccm ametoka bagamoyo na muislam,huku makamu wake akitokea dodoma. na hata ukitiza wenyeviti wanne waliopita ccm wametoka kona 4 tofauti.

Chadema mwenyekiti katoka moshi na makamu wake ni moshi, halafu katibu mkuu hapo hapo Arusha.ni sura ya kikanda pia Mtei, makani na mbowe wote walikuwa benki kuu halafu wakaja kuanzisha Chadema, kama unafuatilia sana siasa utaona kuna kitu hapo NGO fULANI na si sura ya kitaifa.
Mnyika alitaka kudanganya kuwa kuna usafi chadema wakati huko ndio kumeoza zaidi ya ccm, mie si mwana ccm lakini huwezi kumsema mwenzako wakati wewe mchafu zaidi.

Suala la chadema kujiunga na conservative kwa mwafrika yeyote halina maslahi ya kiafrika wala kitaifa, msimamo wa conservative katika siasa za u.k ni kama za chama cha BNP. toka uongozi wa thatcher na Wiliam hague ambao waliweka wazi chuki zao dhidi ya wageni hasa waafrika.

Chama ambacho kina mapenzi na wageni ni Labour na Lib.dem hata mambo mengi ya maslahi ya wageni na afrika yanafanywa na vyama hivyo.
waziri wa kwanza mweusi amechaguliwa na labour na hata dada amos naye kalamba dume.hata misaada ya africa inafikiriwa na kuongezwa na labour.hawa conservative kama lilivyo jina lao hawana interest na nje zaidi ya kwao tu, lakini wenzetu chadema wameona maslahi yao yatafanikiwa kama NGO hayo mengine hayawahusu.David Cameroon anasema akiingia tu madarakani wageni warudi kwao.amesahau kuwa wao walikuja kwetu bila mzozo.

Quartz.
Mbona mnajichanganya wewe unasema Mnyika ana division three na yeye kadanyanga humu ana division 2.kulikuwa na mjadala wa watu kupendelewa na kanisa hasa ktk mitihani ya taifa kwa wanaosoma seminary na case study ikawa mnyika. hapo tuliihitaji maelezo ya kutosha.

una kubali kuwa kila mahala kuna mapungufu nami nakuunga mkono. ndio waswahili wakasema ukimnyooshea kidole kimoja mwenzio kumbuka vitatu vinakunyooshea wewe. ndiyo nikamwambia Mnyika kwanza asafishe kwake kabla ya kwenda nje, na ingekuwa chama makini mngenishukuru na kusema asante kwa ushauri wa bure, lakini imekuwa napingwa vijembe kuwa nimetumwa na makamba, nadhani makamba hana ubavu wa kunituma mimi na wala si ktk viongozi ninawazimia namuona mganga njaa tu kama mbowe.

Chadema bado mna safari ndefu katika siasa kama hamkubali ushauri, mawazo au kukosolewa.
 
Mikael
Karume hajarithi urais kumbuka baba yake kafa 1972 na yeye kachukua 2000 timaza gap hilo tena hafanani hata na Bush junior.
pia kama karithi kwa baba yake sawa, leo chama cha chadema anapewa mkwe?huoni tofauti? karume karithi kwa baba lakini mbowe karithishwa na Mkwewe naomba majibu?

mie si msemaji wa richmond wala jk. labda wewe uliyejua kuwa jk usiku anakosa usingizi kwa ajili ya richmond unaweza kuwa msemaji wa jk. inaonekana uko karibu naye sana hadi unajua ratiba zake za kulala ambayo ni personal zaidi.

mimi nimeuliza utata wa elimu ya Mnyika kama wengine wanavyohoji phd ya Nchimbi, kamala, nagu, NA degree ya mrema au nao wanahoji mambo personal?

Chadema mbona wabishi hivi?
kama unasema ccm mtoto wa mlalahoi hapati kitu. jee husemi chadema watoto wa akina ndesamburo ndio wanaokula? kama alivyokula mkwe wa Mtei bila ya elimu wala nini?
 
chinga mbona hujaongelea wabunge wa ccm kuwapa wake zao na vimada ubunge kwa kuanzia na spika huoni huko ni kudumaza demokrasia....kuhusu utawala wa urthi ,...kweli mwenye mapenzi haoni ...unasemaje kuhusu ALI karume ..nakupa changamoto pitia web ya bunge tazama who is who ,,,,you will find that has become a fammily affair .
kuhusu kurithi mbowe naye tuseme alipokezana na bob nyanga makani ,chadema wanapokezana kistaarabu...tizama hata kama wewe ni ccm ona umuhimu wa upinzani imara kwa maendeleo ya nchi yetu ,,,lets support these guys...issue hiyo ya undugu hata kama chadema kuna traces ccm kuna kansa.....
unless otherwise but still telling you if your father is msaka tonge the era for you to acsend has long elapsed.,,,twende zetu kigogo sambusa tukapange mitumba ya chupi...si ndio ajira milioni moja tulizoahidiwa ,si unajua hata kama una degree wahindi wameshaajiriwa nafasi yako ?
 
Chinga,
kama hujatumwa na makamba, basi ninawasiwasi wa utashi wako wa ufahamu, kwanza hakuna mahali ambapo nimesema mnyika alipata div3, nilikuwa jaribu kukuelewesha kitu tofauti halafu hiyo post ya mnyika nilikuwa sijaisoma bado.

Lakini yeye mwenyewe amekuhakikishia alipata dv 2 kwahiyo hilo limeisha.
pili kitendo cha wewe kufikiria kuwa kanisa linaweza kumbeba mtu kwenye mitihani linanifanya mimi niwe na wasiwasi na mitazamo yako.
 
Chinga,

Narudia tena kusema. Nina div 2 point 12 kidato cha sita na si div 3 pointi 17 kama ambavyo mmekuwa mkiandika ikiwemo katika post zilizopita. Na humu kwenye forum wako wengi niliosoma nao Tambaza na wengine walikuwa mbele yangu. Ningeongopa wangekuwa wa kwanza kunipinga. Na yoyote anayetaka ushahidi si akaangalie kwenye vitabu baraza?

Nafahamu mkakati ulioko wa kunichafua kwa kila namna baada ya kukataa 'kununuliwa' na CCM. Uvumilivu ni kipimo cha uongozi.

Kama nilivyoahidi. Nitajibu hoja zote, sasa kwa kuwa sijaanza kujibu usije kabisa na allegation kwamba kuna hoja sijajibu. Nyerere once said, urgue don't shout.

Nikupe mfano mdogo-umesema makamu mwenyekiti wa CHADEMA anatoka kaskazini. Hivi hujui kwamba makamu wenyeviti wa CHADEMA ni Said mzee(Zanzibar) na Kaborou(ambaye sasa amekwenda CCM)?Huyo wa kaskazini unayemsema ni nani? Maandiko yako yamejaa uzushi, selectivity and twisting of facts. Nakaribia kupoteza diplomasia na kuandika maneno makali. Lakini siwezi kufanya hivyo...........

JJ

Ps: Nasisitiza. Nitajibu hoja moja baada ya nyingine. Kwa sasa tuache speculations! I need time, post zako ni vyingi. And I have other commitments kwa sasa. Na kesho naanza safari ya kurudi
 
Back
Top Bottom