Sam
nilikuwa na maana alibebwa na kanisa si CCM, kwani yeye ni mkatoliki na kuna mpango wa kikatoliki kutawala nchi.
nilijibu hoja za mnyika alipoonyesha kuwa ccm kuna undugunaizesheni, wakati suala hilo jikoni kwake ni chadema, mfano mzuri mwenyekiti wa ccm ametoka bagamoyo na muislam,huku makamu wake akitokea dodoma. na hata ukitiza wenyeviti wanne waliopita ccm wametoka kona 4 tofauti.
Chadema mwenyekiti katoka moshi na makamu wake ni moshi, halafu katibu mkuu hapo hapo Arusha.ni sura ya kikanda pia Mtei, makani na mbowe wote walikuwa benki kuu halafu wakaja kuanzisha Chadema, kama unafuatilia sana siasa utaona kuna kitu hapo NGO fULANI na si sura ya kitaifa.
Mnyika alitaka kudanganya kuwa kuna usafi chadema wakati huko ndio kumeoza zaidi ya ccm, mie si mwana ccm lakini huwezi kumsema mwenzako wakati wewe mchafu zaidi.
Suala la chadema kujiunga na conservative kwa mwafrika yeyote halina maslahi ya kiafrika wala kitaifa, msimamo wa conservative katika siasa za u.k ni kama za chama cha BNP. toka uongozi wa thatcher na Wiliam hague ambao waliweka wazi chuki zao dhidi ya wageni hasa waafrika.
Chama ambacho kina mapenzi na wageni ni Labour na Lib.dem hata mambo mengi ya maslahi ya wageni na afrika yanafanywa na vyama hivyo.
waziri wa kwanza mweusi amechaguliwa na labour na hata dada amos naye kalamba dume.hata misaada ya africa inafikiriwa na kuongezwa na labour.hawa conservative kama lilivyo jina lao hawana interest na nje zaidi ya kwao tu, lakini wenzetu chadema wameona maslahi yao yatafanikiwa kama NGO hayo mengine hayawahusu.David Cameroon anasema akiingia tu madarakani wageni warudi kwao.amesahau kuwa wao walikuja kwetu bila mzozo.
Quartz.
Mbona mnajichanganya wewe unasema Mnyika ana division three na yeye kadanyanga humu ana division 2.kulikuwa na mjadala wa watu kupendelewa na kanisa hasa ktk mitihani ya taifa kwa wanaosoma seminary na case study ikawa mnyika. hapo tuliihitaji maelezo ya kutosha.
una kubali kuwa kila mahala kuna mapungufu nami nakuunga mkono. ndio waswahili wakasema ukimnyooshea kidole kimoja mwenzio kumbuka vitatu vinakunyooshea wewe. ndiyo nikamwambia Mnyika kwanza asafishe kwake kabla ya kwenda nje, na ingekuwa chama makini mngenishukuru na kusema asante kwa ushauri wa bure, lakini imekuwa napingwa vijembe kuwa nimetumwa na makamba, nadhani makamba hana ubavu wa kunituma mimi na wala si ktk viongozi ninawazimia namuona mganga njaa tu kama mbowe.
Chadema bado mna safari ndefu katika siasa kama hamkubali ushauri, mawazo au kukosolewa.