Wacha: Nilisahau swali lako kuhusu education:Hili ni swali kubwa linalohitaji muda na nafasi zaidi, labda ungekuwa specific. Kuhusu nini katika elimu: ubora, gharama, na elimu gani: ya msingi, sekondari au ya juu?
Kwa sasa nikwambia tu kuwa CHADEMA hairidhishwi na ubora wa elimu tuliyo nayo. Moja ya sera za CHADEMA ni kuongoza fedha kwenda katika mashule. Kwa mawzo yangu kama mwana CHADEMA na wala sio kama chama (maana hili linahitaji kiongozi) ningependa pesa zaidi ziende mashuleni sio kubaki pale makao makuu ya wizara ya elimu. Ni rahisi sana kusema bajeti ya elimu imeongezeka. Kitu kigumu kujua ni pesa kiasi gani hasa imefika mashuleni. Ningependa pesa zaidi zitengwa kwa ajili ya mafunzo ya walimu, vitendea kazi, kulipa walimu mishahara yenye hadhi, nk. Hasa katika ku-train walimu katika kiwango kinachokubalika. Kwa kuanzia, kiwango cha chini cha mwalimu kiwe diploma katika elimu inayopatikana kwa mafunzo yasiyopungua miaka miwili. Serikali ya awamu ya nne ilianza na kuitukana fani ya ualimu na elimu kwa ujumla kwa kuwafundisha vijana waliomaliza form siksi kwa wiki 4 na kuwapatia kazi ya kufundisha. Haya ni matusi, lakini kama kawaida ya wtanzania tuliona hamna neno maadamu athari zake sio za papohapo kama za umeme.
Mpango wa muda mrefu ni kuwa na walimu wenye ngazi ya kuanzia shahada. Shahada za ualimu lazima ziwe kwa ngazi husika. Kwa mfano shahada katika elimu ya msingi, sekondari, nk. Mtindo wa sasa hivi wa kutoa shahada ya ualimu tu inatupa walimu walio bora katika taaluma (academics) lakini sio katika ujuzi wa ualimu (professional teachers).
Kubwa sana katika walimu, itabidi kulipa walimu mishahara itakayowawezesha angalau kumudu maisha ya kawaida. Sio lazima kuwalipa mishahara itakayowafanya wawe matajiri, bali mishahara yenye kuipa ualimu hadhi. Watanzania tuna shida sana katika hili. Tumekubali kukabidhi watoto wetu watu ambao serikali inawadharau na iliyowafikisha mahala pa kutokuthamini kazi zao. No wonder, tunatoa vijana wa ajabuajabu katika mashule yetu. Kwa hiyo hatua moja kubwa ni kurudisha heshima ya walimu kwa kuwalipa mishahara kama wafanyakazi wengine wa serikali au zaidi. Ni kwa njia hii tutavutia vijana wanaofaulu vizuri kujiunga na vyuo vya ualimu.
Kama nilivyosema hapo juu, swali lako Wacha ni pana mno; inabidi ujifunze kuuliza maswali, usiwe kama waandishi wa habari wa bongo! if you ask a too general question, you get a too general answer!