East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Mimi ni Mkenya na sioni haja ya kujiunga na watanzania. Watanzania wengi ni WAZEMBE na kwa hivyo hawana MALI yoyote ya kununua bidhaa zetu- "Buying power". Haina maana kuwa na soko kubwa la watu wamasikini na hawaoni hoja ya kujitoa katika umaskini. Leave them to wallow in poverty. They have NOTHING to offer us but sit down and spread hatred. Umasikini kweli uleta WIVU na Chuki. Uchumi wa Tanzania bado upo nyuma sana na watanzania hawana haraka ya kuutoa pale ulipo. Kuungana na Tanzania ni Kujirudisha nyuma. Mbona Romania bado yakatazwa kujiunga na EEC? Mbona USA yafunga mipaka ya Mexico lakini inawafungulia Canada?
Our economies are worlds apart and we HONESTLY DO NOT NEED this union.

Surely this is the concensus we all need to arrive at. As a Tanzanian, my position is clear, I don't want the damned federation. We need more Kenyans like you and the whole idea will die a natural death.
 
Baptist J Mutesasira
East African
+447944268259

It is good to hear from you. My opinion and my fellow countrymen do not want this dubious federation. We have come to learn so many things good and bad about everyone. At the moment we don't want to join with you, do not try to cheat people in Africa like the white when they came who wanted us to believe that everything is rosey in EU. Even now UK doesn't want to join the european currency ask yourself WHY?

Stay in Kenya or UK but we dont want to share the president, its a very big responsibility and we don't want to complicate issues.

Just to let you know remember what VITA VITA said below.
 
nashanga sana viongozi wetu wa kibongo wasivyo makini, jinsi tunavyosaini mikataba isiyo ya manufaa kwa watanzania, wanataka watuingize kwenye shirikisho la EA kwa manufaa yao kisiasa.

mimi kwa maoni yangu naona ni mapema mno kwa nchi yetu kuungana na nchi zenye matabaka ya kikabila na uchu wa madaraka kama tunavyoshuhudia. Kama baba wa taifa JK Nyerere na utashi wake wa kisiasa alishindana na nchi hizo, basi viongozi wetu wawe makini sana juu ya shirikisho. ninachoona hapa tubaki na ushirikiano kama ilivyo SADC na nyinginezo kama waafrika na si katika nyanja ya kisiasa.

MUNGU wetu awape hekima viongozi wetu ili waikoi nchi na wavamizi wanaonyemelea ardhi yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Huo ugomvi wa ardhi umeanza Uganda

Scramble for Uganda
By BENON HERBERT OLUKA
FOR THE PAST 10 YEARS, Ramsey Owor from the Acholi sub-region in northern Uganda has lived in Sasira village in Buganda’s Nakasongola district — more than 200 kilometres from his home village.
In his adopted home, Owor was accepted as a member of the community. He acquired a large piece of land, put up the Nakasongola Agricultural Centre where he is director, as well as running a bee-keeping training project.
In a turn of events however, in the first week of December last year, Owor’s honeymoon with the locals of Sasira village ended when his family and those of two other people — also from Acholi — were raided in a bloody attack.
“The whole village of Sasira descended on us on December 10, shouting that the Acholi must go. They beat us unconscious. We were only saved by the local community (LC5) chairman,” Owor told journalists at a press conference held at Uganda’s Parliament building 10 days after the ordeal.
For Owor, who has invested time and money in Nakasongola, a future away from his adopted home is unimaginable. As he pondered his next move, he could only lament: “I don’t know what the future holds.”
Owor is not the only Acholi immigrant in Nakasongola whose future is in the balance.
According to him, the Acholi in Sasira village started getting threats to leave Nakasongola after Members of Parliament from the Acholi sub-region threatened violence against anyone who dared to “grab” their land.
Apparently they were reacting to the Uganda government’s recently announced plans to allocate land in northern Uganda to foreign and local investors. Acholi MPs are against the plans, saying it is a ploy by elements in the government to grab land in the region.
The MPs’ protests and the subsequent violence that rocked Nakasongola are the culmination of tensions that have been rising in Uganda over land from the beginning of 2006.
President Yoweri Museveni’s government has in the past one year given away large chunks of prime land within Kampala city to mostly foreign investors at no cost. In allocating and reallocating the land to the investors, the government has sometimes had to relocate important national institutions.
One of them, the Uganda Broadcasting Service Television (UBS-TV), located on 14.5 acres of land in Nakasero near the president’s official residence in Kampala, was relocated to pave way for the new allottees of the land, Aya Investments, who are expected to construct a 5-star hotel worth $90 million on the site, in time for the Commonwealth Heads of Government Meeting to be held in Uganda in December.
WHILE EXPLAINING the controversial land give-aways last year, the Minister for Lands, Housing and Urban Development, Daniel Omara Atubo, announced that Aya Investments was not paying a coin for the land.
“The value of the land is Ush5.5 billion ($3.1 million) but this has been waived as an incentive by the government. The investment is expected to employ over 2,000 Ugandans and offer other direct services,” Mr Atubo told journalists at a press conference last July. Such waivers were made on nearly all the land given away, with the government forfeiting Ush5 billion ($2.9 million) for Shimoni Primary School, which was leased to Ms. Kingdom Holdings of Saudi Arabia for the construction of a 5-star hotel.
Another 15 acres worth Ush3.5 billion ($2 million) occupied by the Chieftaincy of Military Intelligence was given to businessman Sudhir Ruparelia. Other pieces of prime land in the city set for allocation to investors include 64 acres of land belonging to the Luzira Prison, Uganda’s prime incarceration centre; part of the army barracks at Mbuya near Lake Victoria; part of Nsambya police barracks, and 10 acres of the land housing Kitante Primary School.
Mr atubo argues that the government needs to make the most out of prime land in the city centre, which is currently under-exploited, to spur a meaningful growth of the capital.
“Clearly, as Uganda continues to industrialise, change of land use is a must, as we should be putting much of the land under factories, hotels, IT centres and other industries. Similarly, extravagant use of land has to stop in order to get the most out of this inelastic resource, which is now under pressure from high population growth,” said the minister.
When the city ran out of prime land to give away, the government targeted land in the countryside. So far, a large chunk of forest land in Kalangala district had been given to the Bidco Palm Oil Project, while the Mehta Group, which owns a sugar producing factory, was allocated a portion of Mabira forest to expand its sugarcane acreage.
In a meeting of MPs aligned to the ruling National Resistance Movement party last December, President Museveni defended the decision to allocate parts of the forests to investor,s saying, “There is no free land” to give away.
Mr Museveni is reported to have told the MPs that he was personally involved in the land allocations because, “It is on account of the urgent need for industrialising our very backward but rich country in terms of natural resources and raw materials. Our backwardness, at this stage, is on the account of the absence of industries.”
While many Ugandans agree with the president and his Lands Minister on the government’s plan to allocate land to investors, they do not share their leaders’ views on the way it has been done so far.
“I think the intention is good but the procedure is not proper,” said Chris Baryomunsi, an NRM MP. Mr Baryomunsi was speaking to the Daily Monitor, a sister paper of The EastAfrican. “Overthe forests,” Baryomunsi added, “I have many reservations. I think they should not just be given away. Giving them away is irrational because the forests have everlasting advantages. The same cannot be said of the investors.”
MPs from the Acholi region have sworn that they will not allow their land to be given away in the same fashion as that in the central part of the country.
The MPs have however been accused by Acholi paramount chief and cultural leader Rwot David Onen Acana II of politicising the issue.
Speaking at a sensitisation workshop that was organised by the Ministry of Lands, Housing and Urban Development in Gulu district on December 4, but boycotted by nearly all MPs from the Acholi region, the leader said: “The land issue is a matter of life and death; it should not be mixed with politics.”
Whether Onen Acana II’s words had struck a chord with the adamant Acholi politicians was put to the test days later when President Museveni called for a meeting with Acholi politicians to dissolve the apparent tension generated by the land issue.
But apparently, the chief’s words were considered just that, mere words, especially by the opposition MPs many of whom declined to attend the December 29 meeting with the president at his country home in Rwakitura. The meeting was expected to explain the government’s position and convince the MPs that it was for the good of the country.
HOWEVER, IN THE RUN up to the meeting, Livingstone Okello-Okello, an MP from Acholi, expressed the misgivings of northern Uganda legislators, saying they preferred to meet the president in their home area, not his.
“We are ready to raise important concerns on Acholi land with President Museveni, but we should meet him in Gulu or any other district in Acholiland, not Rwakitura. The land he wants to discuss is in Acholi and not Rwakitura,” said Okello-Okello.
As it happened, President Museveni ended up meeting with only a pro-NRM delegation of Acholi leaders and elders. They were led by Minister of Agriculture, Animal Industry and Fisheries Hillary Onek.
The president’s address did nothing to win over those who had boycotted the meeting when he asked those present not to “associate yourselves with misguided elements because they will lead you to failure.”
With such uncompromising stands on both sides, the scramble for land in Ugandalooks like becoming a very hot issue indeed.
 
na Happiness Katabazi


SERIKALI imekiri kwamba, uelewa wa Watanzania wengi kuhusu mchakato wa kuelekea kuundwa kwa Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2010, ni mdogo.


Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, wakati alipokuwa akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu shirikisho hilo.


“Uelewa huo mdogo ndiyo unawapelekea wananchi wengi kupinga shirikisho,” alisema Dk. Kamala na kuongeza:


“Nia ya semina hii siyo kuvitaka vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi mambo mazuri tu kuhusu shirikisho, hapana… nawaomba mtumie taaluma yenu kuielimisha jamii kuhusu faida na hasara za kujiunga au kutojiunga katika shirikisho.”


Hata hivyo, Dk. Kamala alisema, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake kupitia kamati ya kitaifa inayokusanya maoni kuhusu kuanzishwa kwa shirikisho hilo.


Alisema, serikali imekuwa ikijitahidi kutoa elimu ya aina yote katika masuala mbalimbali, lakini kwa hili la shirikisho, serikali pamoja na vyombo vya habari, vinatakiwa kuzidisha kasi ya kutoa elimu kwa jamii.


Dk. Kamala, alisema uharakishaji wa mchakato ni utekelezaji wa mkutano wa wakuu wa nchi tatu, uliofanyika Dar es Salaam, Mei 2005, ambao uliridhia kuwapo kamati itakayokusanya maoni ya wananchi.


Ingawa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unataja hatua zitakazopitiwa hadi shirikisho, Waziri Kamala alisema mkataba huo hauzuii nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa hatua hizo.
 
So if Rwanda and Kenya are far ahead what has that got to do with us. It is good for them and good luck.

We don't want the union period!

Who said Kenyans want a union with ya clowns.U Tanzanians either wanna ride shotgun with Kenyans or not.It's ur call.Whatever u decide is fine with us coz for starters ur role an significance is dimming with every passing day.This is ludacris.U tanzanians wanna always play the Juliet game.U wanted to screw with the Soviets,they fhucked u.

Then u tried with the South Africans,bama,they got problems of their own.Now u trying to kiss up to the Americans only to realise there is a China.Guess how Kenyans represent in this whole theater.No need for lessons.I'm not saying Kenya is rich.But i have to say this.

We have put up with a lot of crap from our neighbours u included.The Kenyans have had it.Check out the Kenyan popular media an u will know this is true.Good neighbourliness is dead.We exactly don't wan't Tanzania to be part of Kenya's future.Hell no.
 
I think due to economical unbalance too early to have it but because some leaders wants to make their CVs lets go.

The history will judge.
 
Who said Kenyans want a union with ya clowns.U Tanzanians either wanna ride shotgun with Kenyans or not.It's ur call.Whatever u decide is fine with us coz for starters ur role an significance is dimming with every passing day.This is ludacris.U tanzanians wanna always play the Juliet game.U wanted to screw with the Soviets,they fhucked u.Then u tried with the South Africans,bama,they got problems of their own.Now u trying to kiss up to the Americans only to realise there is a China.Guess how Kenyans represent in this whole theater.No need for lessons.I'm not saying Kenya is rich.But i have to say this.We have put up with a lot of crap from our neighbours u included.The Kenyans have had it.Check out the Kenyan popular media an u will know this is true.Good neighbourliness is dead.We exactly don't wan't Tanzania to be part of Kenya's future.Hell no.

So let's settle at this: WE DON'T WANT A FEDERATION. PERIOD!
 
I thought Tanzania was clean from corruption as portrayed by some people on this forum. surprise surprise!.maajabu ya n'gamia hucheka nundu ya n'gombe.



<< Previous Topic | Next Topic >> Return to Index

fraud fraud by uk companies in africa
January 16 2007 at 1:15 PM fmatatizo

--------------------------------------------------------------------------------

Tanzanian tycoons divulge getting $12m secret payout

2007-01-16 10:15:02
By London


TwoTanzanian business moguls have admitted they were secretly paid $12m/- by UK`s biggest arms supplier in a controversial deal in, which Tanzania bought an obsolete military radar system.

The tycoons, Sailesh Vithlani and business partner, Tanil Somaiya made the admission to British detectives who recently flew into the country to investigate graft allegations in the controversial sale of the radar by BAE.

Vithlani, who acted as a middleman in the deal and has a long-standing relationship with military and government figures, has admitted that the sum was covertly moved to a Swiss account by BAE Systems, which is under investigation by the Serious Fraud Office.

The SFO, which was recently forced to abandon its investigation into commissions paid on a massive arms contract with Saudi Arabia, is now focusing its attention on Tanzania.

The back-door payment represented 30 per cent of the contract value. Tanzania had to borrow to finance the deal, which critics said was unnecessary and overpriced.

The duo is expected to act as prosecution witness in the BAE`s corruption case.

In Dar es Salaam, Vithlani`s business partner, Tanil Somaiya, told the London Guardian that British police had already flown out to trace and interview both men as potential witnesses.

The admissions by Vithlani, has led to calls in London for BAE?s prosecution if the allegations were proved.

Vithlani was the majority shareholder in Merlin International Limited, Somaiya said, while he had a small token interest himself. BAE paid $400,000 down this route in stage payments, Somaiya said, as the radar equipment was delivered.

Vithlani acted as agent not only on the radar deal but also in the 2002 purchase from the US of a top-of-the-range Gulfstream official jet for the then Tanzanian president, Benjamin Mkapa, at a cost of more than $40m.

Police sources in Dar es Salaam said the agreement to use Vithlani as an agent had been signed off by the then chairman of BAE, Sir Dick Evans.

Sir Dick, who has been at the centre of many of the arms deals under investigation, has already been interviewed by the Serious Fraud Office during their two-year inquiry.

When asked about the BAE money, Vithlani told the Guardian he had made no disbursements from the Swiss cash to public officials ?in Tanzania?. Asked if he had disbursed any of the $12m to third parties outside of Tanzania, he declined to comment.

``When the UK police travelled to Tanzania, we met them at their request and answered all their questions,`` he said.

At the same time, it has emerged that British Premier, Tony Blair supported the 2002 sale, a move that was fiercely opposed by former cabinet minister Clare Short and the chancellor, Gordon Brown.

Clare Short said the prime minister had been personally responsible for forcing the licence for the Tanzania deal through the cabinet. ``It was always obvious that this useless project was corrupt,`` she said.

He said BAE had made two parallel arrangements with the middlemen. In the first, a conventional agency agreement was signed.

Under this, 1% commission was to be paid if the $40m radar deal went through, to a Tanzania-registered firm, Merlin International Ltd.

But under a second, more unusual agreement, BAE`s secretly owned offshore company Red Diamond deposited another $12m, representing 30% of the contract price, in Switzerland.

That money was under the personal control of Vithlani, Somaiya said, and this had been admitted to UK police.

When asked if he would allow British police to inspect all the transactions on his Swiss account, he declined to comment.

In the secretive world of international arms deals, a commission of 1% to local agents would generally be regarded as legitimate.

The government?s export credit agency, the Export Credits Guarantee Department, has guidelines under which a ``commission`` of more than 5-10% is automatically regarded as questionable.

BAE System?s payment of as much as 30%, coupled with the use of a Swiss bank account and apparent double sets of agency agreements, would normally arouse suspicions of possible bribery, investigators say.

BAE Systems were yesterday asked why they had made a 30% payment to Vithlani`s Swiss account.

The company refused to answer, saying: ``We will not be commenting on any point of substance. This cannot of course be taken as any kind of admission.``

The SFO also refused to discuss their investigation. President Jakaya Kikwete, is due in London today to speak at a meeting with Hilary Benn, the international development secretary, on efforts to overcome corruption in Tanzania.

Later this week, the UK is expected to have to defend its actions over BAE at a meeting of the anti-bribery group of the OECD in Paris.

SOURCE: Guardian




Respond to this message

Current Topic - fraud fraud by uk companies in africa

<< Previous Topic | Next Topic >> Return to Index
 
Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
BURIANI TANZANIA ... AU KILA LA HERI AFRIKA MASHARIKI?
Na Mlenge Fanuel

"Mtu akikushauri jambo la kijinga, huku anajua jambo hilo analokushauri ni la kijinga, na wewe ukakubali, basi atakuona, wewe zuzu!"
-- Mwalimu Julius K. Nyerere, 1994/5

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali isome barua hii ya wazi ya kukufikishia ujumbe kwamba Tanzania haiko tayari kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki (East African Federation, EAF) wala “Soko la Pamoja” la Afrika Mashariki, na kwamba Watanzania hatutaki Tanzania ijiunge na Shirikisho hilo.. Yatakuwa ni maafa makubwa kwa Tanzania na Watanzania iwapo Tanzania itajiunga na EAF hasa kwa mpangilio ulioko wa “fast track”. Ndiyo maana nimeanza na nukuu ya Mwalimu Nyerere, ambaye tayari baadhi ya watu, hasa wa nchi jirani za Kenya, Uganda na Rwanda, wameanza kumsingizia kwamba kwa kujiunga na EAF tutakuwa "tunamuenzi" Mwalimu Nyerere, huku wakijua fika ushauri wanaotupa wa kujiunga na Shirikisho na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki hauna manufaa yoyote kwa Tanzania, wakidhania sisi Watanzania ni mazuzu tunaoendekeza wema wa mshumaa kuwaangazia wengine huku wenyewe unateketea, kwa minajil ya kupata misifa isiyo na tija.

Ni kweli Mheshimiwa Rais umeunda Tume ya Kupokea Maoni kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini inatia mashaka iwapo huo siyo tu ni utaratibu uliouweka kuhalalisha maamuzi yaliyokwishafikiwa ya kuidumbukiza Tanzania kwenye EAF. Hii inatokana na muonekano kwamba Tanzania kujiunga na EAF kumeshaamuliwa tayari -- kutaka watu tujadili siyo kiinimacho tu? Mheshimiwa Rais, palikuwa na muswada uliopelekwa Bungeni wa Tanzania kujiunga na EAF, ambao Waheshimiwa Wabunge waliukataa, na serikali ikabidi iuondoe. Lakini mchakato wa Tanzania kujiunga na EAF ukaendelea tu, na kupuuza maoni ya Wabunge wetu tuliowachagua watuwakilishe. Ikiwa sikusikiliza vibaya, katika Bunge la Bajeti 2006/2007, Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki aliliambia Bunge kwamba patakuwa na KURA YA MAONI kuhusu Afrika Mashariki. Matokeo yake tumeletewa Tume badala ya kura ya maoni! Kana kwamba hiyo haitoshi, iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa wewe Mheshimiwa Rais wetu, ulimhakikishia Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwamba utafanya kila unaloweza kuhakikisha kufanikiwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, kwenye mkutano wenu uliofanyika Mwanza. Je, maoni tunayotoa Watanzania kukataa kujiunga na shirikisho si "kilio cha samaki -- machozi yanakwenda na maji?" Wenyewe "wenye nchi" mshaamua mloamua?

Pana maswali mengi mheshimiwa Rais ambayo ukitupatia majibu utakuwa umetuwezesha Watanzania tulio wengi kuelewa kuhusu mustakabala wa maisha yetu na Tanzania yetu:

* Je, Ni sera ya CCM Tanzania kujiunga na EAF au Soko la Pamoja la Afrika Mashariki?

* Je, Ilikuwa kwenye ilani ya Uchaguzi 2005 ya Chama Tawala CCM Tanzania kujiunga na EAF?

* Je, Nani aliyependekeza Tanzania ijiunge na EAF? (Inabidi tumfahamu ili tuweze kumpamba maua iwapo Tanzania itafanya tunalodhani ni kosa la maisha la kujiunga EAF kumbe ikathibitika EAF ni manufaa tele kwa Tanzania ; vinginevyo inabidi tumfahamu ili tuweze kumzomea na kumuimbia nyimbo za kumsimanga pindi machungu ya EAF yatakapoanza kudhihirika muda si muda iwapo Tanzania itafanya kosa la maisha kujitumbukiza kwenye EAF. Vinginevyo itakuwa kama mikataba ya madini -- hatuelezwi nani aliwaalika na kuingia mikataba na 'wawekezaji' kwenye migodi.)

* Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshajitangaza kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki -- ikiwa na maana yote mengine yanayojitokeza sasa ni kuhalalisha na kusafisha njia ya Museveni kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki, hasa ukitilia maanani Rais wa Kenya na wewe Rais wetu mko kimya, ikielekea mmekubaliana na matamshi ya Museveni. Si hivyo?

(end of part 1)
* Kutokana na maneno yanayosemwa na Wakenya na Waganda, Wanyarwanda na Warundi, inaonekana kama vile serikali ya Tanzania HAINA UBAVU wa kusema HAPANA kwa EAF -- kila mara Tanzania inazomewa inapohoji maslahi yake kwenye EAF -- au inapotaka kutumia uhuru wake ISIJIUNGE na EAF. Hivi karibuni Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania alisemwa kwenye vyombo vya habari kwamba hahudhurii vikao vya Afrika Mashariki -- na kumfanya Mheshimiwa Waziri Mkuu ajitokeze kumtetea -- na baadaye Waziri yule akaondoshwa toka Wizara ya Afrika Mashariki kwenye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri uliyoyafanya hivi karibuni Mheshimiwa Rais. Ina maana Tanzania ni kama mbwa anayeelekea kwenye mdomo wa chatu EAF -- amefyata mkia, anatoa kilio cha mwisho, na hana la kufanya zaidi ya kufanywa asusa na kumezwa -- au si hivyo?

* Ni kwa nini Kiswahili SIYO lugha rasmi EAC, na badala yake ni kiingereza?

* Kama shida ni ushirikiano, kwa nini Tanzania isijiunge na Msumbiji na Zambia , na kutengeneza shirikisho?

* Kwa nini EAF inaharakishwa namna hii?

* Ni nini Tanzania inahitaji kwenye EAF ambacho haiwezi kukipata bila kuwemo kwenye shirikisho hilo ? (Mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na watu fulani kupata posho za vikao vya EAC na baadhi kuandikwa kwenye vitabu vya historia, vitu ambavyo havimsaidii Mtanzania mpiga kura wako anayesubiri neema tele na maisha bora...)

* Pana bidhaa zipi za Tanzania hazifiki kwenye soko Kenya au Uganda , ambazo EAF itazifanya zifike sokoni?

* Nani atakuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Afrika Mashariki, na ni upi mchango wa EAF kwenye uvamizi dhidi ya DRC?

* Mheshimiwa Rais, hivi "Usalama wa Taifa" wa Tanzania una majukumu gani makubwa zaidi ya kulinda (uhuru) "Sovereignty" ya nchi yetu? Kwa nini "Usalama wa Taifa" haukupi picha kamili ambayo itakufanya usijisumbue hata kuja kutuuliza iwapo tunataka uhuru wa nchi yetu uondoke kupitia "soko la pamoja" na "Shirikisho la Afrika Mashariki", badala yake tukaendelea kulijenga taifa "letu changa" na kuulizana maswala ya maendeleo kama vile tutanufaikaje na maliasili tulizojaaliwa nchini mwetu?

* Kwa kuitumbukiza Tanzania kwenye "Soko la Pamoja" la Afrika Mashariki, huoni kwamba utakuwa umekiuka kiapo ulichokula cha kuulinda uhuru wa, na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ?

* Kulikuwa na sababu gani ya kupambana na Idd Amin aliyetaka kipande "kidogo tu" cha nchi yetu, ikiwa leo tunaigawa sandakarawe nchi nzima kwa kisingizio cha soko la pamoja?

* Tanzania itaondoka SADC? (Tayari nchi nyingine za Afrika Mashariki zimeanza kutuamuru tutoke SADC. SADC imeweka bayana kwamba wakati umefika wa kuchagua kati ya EAF au SADC.) Unadhani itakuwa ni busara kuondoka SADC? Kwa nini usitoe tamko kwamba Tanzania ya kesho ni ndani ya SADC?

* Je sisi wananchi wa Watanzania tutaulizwa kuhusu kujiunga na "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki" au ni uamuzi uliofikiwa tayari kwamba tutajiunga na soko la pamoja la Afrika Mashariki?

* Huo Mkataba wa EAC/EAF uko wapi ili tuweze kuuona na kuusoma? Ni Watanzania gani waliousoma na kuuridhia kwamba SASA tunaanza kuwa kwenye mchakato wa kuelekea kwenye Shirikisho? (Inaripotiwa kwamba Tume yako ni sehemu tu ya taratibu ‘chovu’ za mchakato huo...)

Watanzania tutafanyaje ili kuondoka kwenye EAF, iwapo Tanzania ijajikaanga yenyewe kwa kuingia kwenye EAF? Vipengele vya kujiondoa kwenye EAF viko wapi? Hautakuwa ni uhaini kuzungumzia kujitoa EAF, kama ambavyo si ruksa kuzungumza kujitoa kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ?

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, maswali hayo na mengine mengi yanaleta changamoto kwako binafsi kwamba zawadi kubwa kuliko zote unazoweza kutupa sisi Watanzania, ni kutukabidhi Tanzania yetu yenye "sovereignty" ileile au zaidi ya uliyokabidhiwa pale utakapoacha madaraka mwaka 2010 au 2015, panapo majaaliwa.
 
Kwa taarifa yako Mheshimiwa Rais , Tanzania ndiye "Mbuzi wa Shughuli" kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki. Na mbuzi huyu amepangwa "kuchinjiwa kwenye maji" ili hata ukelele wake wa mwisho usisike. Hawatarudia makosa ya Jumuia ile iliyokufa 1977, kwa kutuacha bado tunafurukututa. Kujiunga kwa Tanzania EAF kwafanana na Punda wa kwenye hadithi moja iliyochapishwa Tanzania ambamo Simba baada ya kujeruhiwa, alishindwa kuwinda; na Sungura, Fisi na Punda wakaenda kumpa pole. Kumbe Fisi na Sungura walikuwa na lao jambo.

"Simba kwa kuwa huwezi kuwinda naomba unile mimi", alianza kusema Sungura.
" Asante sana kwa kunijali, siwezi kukula wewe rafiki yangu. Sasa nimefahamu wewe ni rafiki yangu wa kweli katika kipindi hiki kigumu cha dhiki!" alijibu Simba.
Fisi naye akajitoa aliwe na Simba, ambaye pia alikataa kumla, akitoa sababu zilezile.

Sasa Punda akawa njia panda: "Nikikaa kimya nitaonekana mbaya kwa Simba. Kwanza Simba mwenyewe kakataa kuwala wenzangu, na mimi atakataa... acha nijisemee tu kwamba najitolea anile..." aliwaza.
Akaropoka, "Simba kwa kuwa huwezi kuwinda naomba unile mi..." Kabla hajamaliza maneno yake alirukiwa na kuraruliwa palepale.
Kenya, Uganda , Rwanda na Burundi zina ajenda kadhaa kwenye EAF: mbali na zile "rasmi" zinazotangazwa hadharani. Ili ajenda zao zitimie, lazima "Punda" Tanzania awemo kwenye EAF ili aweze "kuliwa". Mheshimiwa Rais, ni wajibu na heshima kwako kuhakikisha Tanzania haijiungi na EAF kwa kuwa Tanzania haina ajenda mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na posho za vikao kwa baadhi ya watu.

wanza Tanzania siyo lazima ijiunge au ikubaliane na kila kitu kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wachache wanaounga mkono kujiunga na shirikisho la afrika mashariki, wanadai upo umuhimu wa kujiunga kwa vile "dunia nzima mwelekeo ni kujiunga pamoja, kama vile Jumuia ya Ulaya, EU". Kama sababu ni hiyo, kwa nini tusibakie SADC tuliko? Hivi tulipigania uhuru wa kusini mwa Afrika ili iweje? Watanzania tulitoa damu zetu, mali na uhai wetu, kukomboa Ndugu zetu walio Kusini mwa Afrika, sasa ukombozi umepatikana, pana wakati gani muafaka zaidi ya huu kuendeleza undugu wetu? Majirani zetu wa Afrika Mashariki tutaendelea kushiriana nao, kama tunavyoendelea kushirikiana na majirani zetu wengine. Kutojiunga kwenye shirikisho siyo maana yake tutakuwa maadui!

Tanzanialazima ikae mbali na EAF, hata ikibidi kwa miongo kadhaa ijayo, ikiwa si moja kwa moja. Kwanza , Muungano wetu wenyewe una "mipasuko" ambayo haijasilibwa bado. Kabla ya kuulizwa kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki, tuulizwe basi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Tanganyika na Zanzibar , mara baada ya kupata Uhuru, hazikutimiza miaka mitano, "zikaishia" na kuwa Taifa moja Tanzania . Sasa jamani, Tanzania hata miaka hamsini haijafikia, nayo "iishie", tena kusikoeleweka? Tanzania ina manufaa tele SADC, kuliko kwenye shirikisho la Afrika Mashariki. Hivi, wakati tulipokuwa "Mstari wa Mbele wa Ukombozi Kusini mwa Afrika", majirani zetu wa Kenya na Uganda walikuwa wapi? Leo hii tukiwakubalia kuondoka SADC, watatuona timamu kweli?

Mheshimiwa Rais Kikwete, kiasi inaeleweka ikiwa unaona pana ugumu wa wewe kuonekana unakwenda tofauti na Watawala wetu waliotutangulia, ambao huenda wanapendelea kuona EAF ikizinduliwa, Tanzania ikiwemo. Lakini mheshimiwa Rais, ndiyo maana kukawa na kikomo cha utawala cha vipindi viwiliviwili! Kwa kuwa umechaguliwa kwa ushindi "wa kishindo", imani yetu Watanzania imekuwa kwako kwamba utaweza kuipeleka Tanzania kule tunakotaka. Na tunakotaka sisi Watanzania siyo kwenye "soko la pamoja la afrika mashariki" wala EAF. Huo Muungano tu wa Forodha wa Afrika Mashariki unatekelezwaje? Matatizo na mizengwe iliyoko panaashiria nini pindi tukiwagaia nchi hii yote kwenye Shirikisho au "soko la pamoja"? Siyo maafa, Mheshimiwa Rais?

Mheshimiwa Rais Kikwete, kwenye Jumuia ya Ulaya --EU, Uingereza na Jamhuri ya Ireland SIYO mataifa yaliyoko kwenye "Mkataba wa Schengen" wa Jumuia ya Ulaya, mkataba unaoondoa mipaka na vizuizi baina ya nchi za Jumuia ya Ulaya kwenye masuala ya Uhamiaji, japo Uingereza na Jamhuri ya Ireland ni wanachama kamili wa Jumuia ya Ulaya. Hii haikuzuia Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani na nchi nyinginezo za EU zilizokubali kusaini kuendelea na "Makubaliano ya Schengen". Kadhalika , Iceland , Norway na Uswisi zimesaini "Mkataba wa Schengen" japo nchi hizo SI zanachama Jumuia ya Ulaya. Kila taifa linaangalia maslahi yake kama taifa. . Ulipoanzishwa umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki takriban karne moja iliyopita, Tanganyika haikujiunga mpaka ilithingya vema kwamba itakuwa ni kwa maslahi yake kujiunga.

Hii haikuzizuia Kenya na Uganda kuanzisha Umoja wao wa Forodha. Tanganyika ilijiunga baadaye! Hata ile Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika, ilianzishwa baada ya kupita MIAKA HAMSINI tangu kuanzishwa ule Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, japo nchi hizi zote tatu zilikuwa zinatawaliwa na Mkoloni mmoja takriban muda wote huo. Haraka ya sasa hivi ya nini? Wanajua wakituachia muda, tukienda hatua kwa hatua, hawataweza tena kuigeuza Tanzania koloni lao. Tanzania iendelee kuwa mwanachama wa SADC, na kuendelea kuwa imesaini kwa muda makubaliano ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki mpaka pale SADC itakapoanzisha Umoja wa Forodha wa SADC, ambapo Tanzania itajitoa kwenye Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki. Au busara zaidi, ni vyema Tanzania ikajitoa SASA HIVI toka Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, na kuelekeza nguvu zake kwenye SADC. Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi zinaweza kuendelea na Umoja wao wa Forodha, Soko la Pamoja na Shirikisho (waliite vyovyote wapendavyo), bila Tanzania kuwemo.

Mheshimiwa Rais, ukubwa wa eneo la ardhi ya Tanzania ni zaidi ya Jumla ya eneo lote la ardhi ya Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi ukizichanganya pamoja -- bila kuzungumzia rasilmali zilizoko. Halafu wanasema tuchanganye ardhi yetu na zao, halafu tugawane sawasawa kwa jina la "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki". Hivi tukikubali ujuha huo, ni kwa nini wasituone sisi mazuzu?

Swali kuu tunaloulizwa Watanzania na Tume yako mheshimiwa Rais ni iwapo Watanzania tunaona bado kuna sababu za Tanzania kuendelea kuwa nchi huru ambayo ni "dola", wakati ambapo kuna shinikizo nchi yetu igawe uhuru wake kwa kisingizio cha "soko la pamoja" na "shirikisho la Afrika Mashariki". Tuchukulie kwa mfano, tume itawahoji na kupokea maoni toka kwa watu laki mbili. Kati yao 80% wakasema Tanzania ijiunge kwenye "Soko la Pamoja" na "Shirikisho la Afrika Mashariki", 20% wakasema tusijiunge. Je, Mheshimiwa Rais, hiyo itakuwa na maana uamuzi utakuwa umesilibwa wa Tanzania kufikia mwisho wake, kwa kujiunga na Soko la Pamoja na Shirikisho la Afrika Mashariki?

Je, hutatumia busara kama ilivyotumika kwenye Tume ya Nyalali ya Vyama Vingi pale Tanzania ilipoangalia maslahi ya taifa, na kuruhusu mfumo wa vyama vingi, bila kuangalia asilimia zilizotokana na tume? Ikiwa kweli kabisa umedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye mwisho wake machinjioni Afrika Mashariki, kwa nini usiweke KURA YA MAONI kwa kila Mtanzania kupiga kura yake, badala ya kutumia Tume, angalau basi kuchelewesha kwa muda mauti ya Taifa Tanzania? "Soko la Pamoja" na pacha wake "Shirikisho la Afrika Mashariki" maana yake ni mwisho wa uhai wa Taifa la Tanzania . Ikiwa Tanzania itajinyonga (Mungu apishie mbali!) kwa kusaini mkataba wa "Soko la Pamoja la Afrika Mashariki" au ule wa "Shirikisho la Afrika Mashariki", basi Watanzania tutasahau "maisha bora kwa kila Mtanzania" na itabidi tujiandae kwa "Bora Maisha kwa kila Mtanzania", na kwamba wewe Rais wetu, Jakaya Kikwete, utakuwa umefeli vibaya kabisa jukumu lako la msingi tulilokupa -- kulinda uhuru na umoja wa Taifa la Tanzania na kubakisha Taifa la Tanzania kuwa dola huru kwa manufaa ya Watanzania mpaka pale utakapomkabidhi madaraka ya Urais wa dola la Tanzania huru Mtanzania mwingine.

Kwa kuandika barua hii, imani yetu Watanzania kwako Rais wetu kwamba utaweza kuhimili mashinikizo yote ya nje, na kutusikiliza sisi raia zako, tunaotaka tubakie na taifa letu huru la dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Mwenyezi Mungu akujalie. Amin.

Ndimi,

Mlenge Fanuel
Raia na Mwananchi wa Tanzania,
Simu: +255 75 4372902,
Email: mlenge@yahoo.com,
Dar es Salaam, Tanzania
 
well nakubaliana na kuundwa kwa shirikisho hilo but sasa ni wakati muafaka wa tanzania kuwekea mkazo elimu maana wakenya na wayuganda wapo mbali na tunahitaji kukabiliana nalo.

Ukweli ni kwamba kiingereza ndio kinachowabeba lakini kwa utaalam sis we are fine,juhudi za lugha nazo ziongezwe tuweze kabiliana nao.

Bora umasikini wetu na amani na furaha tuliyonayo.wenzetu utu nyuma mali mbele,kwa hiyo viongozi wawe makini
 
Hivi sasa tunao muungano wa Zanzibar na Tanganyika wenye umri zaidi ya miaka 40! lakini hauna faida yoyote bali lalamiko ktk pande zote huku wengine wakidai kumezwa na matatizo mengi ama iwe kisiasa au kiuchumi kwa kweli hii ni dalili tosha kabisa kuwa Tanzania bado hatujakomaa barabbara kujiunga ktk shirikisho la A.M.!

Kabla hatujajinga na shirikisho la A.M. tuimarishe muungano wetu wa Zanzibar na Tanganyika, pande zote mbili zifaidike kihaki ktk uchumi na halafu kisiasa tukomae vizuri tuache kuuwana na kukamatana ovyo kwasababu za kisiasa kama ilivyotokea huko Pemba! tuunganishe serikali zetu na kuwa na Rais mmoja, bunge moja, jeshi moja, pasi moja nk. baadae tuangalie natija hapo ndipo tufikirie kujiunga na shirikisho la AFRIKA MASHARIKI! kinyume chake ni mfupa uliomshinda fisi.........
 
nimekuwa napitia majibishano mengi kuhusu muungano (EAC) sijafika mahali nikashawishika kujiunga lakini nakereka kwa mtu kusemea nafsi yangu.

Acheni hoja muflisi namna hiyo eti muungano tutabuluzwa na waganda na warundi wao ni nani?

wajibu wa kila Mzazi (baba au Mama)mwenye busara ni kuwahakikishia watoto wake maisha bora yenye maendeleo kadri ya uwezo wake na kila nafasi ya mafanikio inayomjia machoni mwake anaelekeza kwa wanawe.

wajibu wa mzazi ni upi mali au hazina,Amana alizohangaikia wakati wote maishani zinawafikia walengwa yani wanawe. Tuamke sasa toka kwenye usingizi wa ulevi(ezembe) tuwaulize wazazi wapi ardhi yetu,wapi madini yetu, wapi ajira zetu kila ofisi ya selikali, mashirika ya kimataifa na binafsi.

Tuache kutoa hoja za vijiweni wakati huu wa mstakabali wa maisha yetu sisi vijana. Tutoke kwa ujasili tuwahoji kaka na dada zetu waliopo huko (Kenya) wanavyo nyanyaswa na ku-uawa kama kuku kwa sababu wao si wazawa(unafatwa ukiwa bar na mgeni usiemjua anajongea mahali ulipo na kukuambia wewe si mukenya uwende umwachie Mkenya hiyo post)
"WE HAVE TO TAKE THE SAME MEASURE" WAMEJAA KWENYE SEKTA YA BENKI, BIMA, VYOMBO VYA HABARI NA MASHILIKA YA KIMATAIFA.hilo ndilo baba mwenye busara angeweza kufanya na ndilo wanalo tufanyia huku kwao.
 
Mimi ninafikiri Arusha ni better, kuna hotel nzuri , majengo ya mikutano, barabara nzuri, usafi, airport mbili KIA na ile ya Arusha. Arusha ni mji wa kitalii na wageni hivyo sitashauri makao makuu yahame. Kama hizo nchi hazima pesa za ndege basi hawataweza kuwa nasi kwani hii program inacost.

Wataka makao makuu A/Mashariki yawe Mwanza

na Jovin Mihambi,

WAKATI watu wapo kwenye mchakato wa kutoa maoni kuhusiana na kuharakisha uundwaji wa shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki, wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kondo (DRC), wametaka makao makuu ya jumuiya hiyo yahamishiwe Mwanza kutoka Arusha.

Wakiongea na waandishi wa habari jijini hapa, wafanyabiashara hao walidai kuwa iwapo nchi zao zitaruhusiwa kujiunga na jumuiya hiyo kama dalili zinavyoonesha, Mwanza ndiyo itakuwa jiji lililo katikati na si Arusha.

aidha, walidai kuwa kwa upande wa usafiri, Jiji la Mwanza ni muafaka kwa vile liko katikati na nchi hizo na ni rahisi kufika hapo kutokea nchi yoyote kati ya hizo.

“Arusha ni mji mzuri, ila tatizo ni ugumu wa usafiri wa kufikia mji huo, usafiri wa uhakika kufikia mji huo ni kwa kutumia usafiri wa anga peke yake, kwa upande wa barabara, mji huo haufikiki kwa urahisi kutokana na barabara ziendazo kuharibika nyakati za mvua,” alisema Bizima Ndikumana, raia wa Rwanda ambaye hufanya biashara ya usafirishaji wa dagaa na samaki kutoka jijini Mwanza hadi Rwanda.

Walisema kuwa endapo nchi zao zitakubaliwa kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwanza itakuwa ni karibu na nchi zote wanachama.

Aidha, wafanyabiashara hao walidai kuwa Mkoa wa Mwanza ni maarufu kwa shughuli za kibiashara, ikiwamo biashara ya samaki, dagaa, dhahabu na mazao mbali mbali ya maliasili, chakula na nafaka nyingine za biashara ambazo zimekuwa ni kivutio kikubwa kwa wananchi wa nchi hizo.

Nao wafanyabiashara pamoja na wananchi ambao ni wazaliwa wa Tanzania katika mahojiano na waandishi wa habari, walisema kuwe na uangalifu wakati wa kuzipatia uanachama nchi nyingine za Maziwa Makuu.

Walitaka hali ya usalama idhibitiwe kwanza katika nchi hizo kabla hazijakubaliwa kuwa wanachama.

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki katika mahojiano hayo ni pamoja na Pierre Nguza kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zuberi Athumani kutoka Ngozi nchini Burundi na Kiwanuka Asiimwe kutoka Kampala nchini Uganda.
 
Jamani hili jambo mimi linaniingia kivingine kama aqlivyosema Junior kuna sehemu namuunga mkono na kwengine sikubaliani nae..

Kwa ujumla mimi silikubali Shirikishi hili hasa kwa maslahi wa watanzania wote wa mijini na vijijini kwani hata wenye nchi yao (watanzania) hawaelewi chochote juu ya jumuiya hii, tumeona sehemu zote tume inapozunguka wanapingwa na watanzania hawaoni kuwa hatutaki?

Mimi binafsi sioni faida hebu mmoja anitajie ni idara gani Nchini Kenya ama Uganda inatoa ajira kwa Watanzania? lakini Ukija mahoteli yote ya kitalii tanzania kuanzia General Manager, Oparetion Mangers mpaka Wahudumu wa Room ni wakenya je Jumuia ikikamilika na kukawa na Rais Mmoja tena usiombe Museveni (Mpenda Madaraka) ninaimani hata mfumo wa siasa Utabadilika ikiwemo Rais Kutawala milele kama atakavyo Museven
Balaa lengine nio huko Burundi na Ruanda laba watanzania watafaidika kuoa watoto wa Kinyaruanda na waruni kiulaini lakini maendeleo ziro afadhali ya sasa
 
Kuhusu kuundwa kwa shirikisho la Afrika mashariki mimi naona ni wazo zuri,lakini kwanza inabidi tupate muda wa kufikiri kuona tutanufaika vipi na umoja huo
 
mimi naunga mkono suala la TZ kujiunga na shirikiso la Afrika Mashariki.
Maalim seif hamad
 
Mhhh wewe sio Maalim Seif! Confirm... Jisajili halafu turuhusu tukuulize maswali kadhaa kuweza kuamini kuwa WEWE NDIYE. Fanya kama alivyofanya Mbowe akaulizwa maswali na akajibu anayoweza ambapo tuliweza kung'amua kwamba YEYE NDIYE.

Vinginevyo; usitumie Maalim Seif nick bila idhini yake kwani ni mtu mwenye hadhi yake katika taifa letu na tamko lake lina uzito mkubwa sana!

Binafsi nashauri serikali iwasikilize wananchi wanasemaje na si kwenda kwa maslahi ya wachache ambapo majuto huenda yakaitwa MJUKUU.

Wasalaam
 
Back
Top Bottom