Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukishauriwa jambo la kijinga usikubali,utaonekana zuzu
Juma Mohammed
HabariLeo; Monday,January 22, 2007 @00:02
Juma Mohammed
La mgambo limelia kuna jambo Tanzania tena kubwa, mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu kuharakishwa au kutoharakishwa kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki umeanza kwa nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.
Ningepanda Watazania wenzangu tujadili na kutafakari kwa makini matamshi haya ya Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa mwaka 1994, alisema: Mtu akikushauri jambo la kijinga, huku anajua jambo hilo analokushauri ni la kijinga, na wewe ukakubali, basi atakuona, wewe zuzu!
Nimelazimika kunukuu matamshi hayo ni kwa sababu kwa maoni yangu si wakati Muafaka kwa Taifa letu kujiunga katika Shirikisho la aina hiyo. Nasema hivyo kwa sababu, Tanzania ni zao la Mataifa huru mawili, Zanzibar na Tanganyika ambazo ziliungana Aprili 26, 1964.
Kwa kuwa ni Muungano wa nchi mbili, kuna mambo yalikubaliwa katika hati ya Muungano ambayo na hakika suala la Shirikisho la Afrika Mashariki halimo, sasa swali liko hapa je nafasi ya Zanzibar katika mambo yasiyokuwa ya Muungano nani msimamizi wake?
Kwa Mujibu wa mkataba wa Muungano, kutakuwa na Serikali mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatakayokuwa na kujumu la kusimamia mambo ya Muungano na yale yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika( Tanzania Bara) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayosimamia masuala ya Zanzibar yasiyokuwa ya Muungano.
Tanzania kujiunga katika Shirikisho yatakuwa ni maafa makubwa kwa Watanzania iwapo tutajiunga hasa kwa mpango wa "fast track". Wenzetu wanadhani kwamba Watanzania kutokana na upole wao, ukarimu ni mazuzu tunaoendekeza wema wa mshumaa kuwaangazia wengine huku wenyewe tunateketea, kwa minajili ya kupata sifa isiyokuwa na tija, hilo haliwezekani.
Ulipoanzishwa umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki miaka iliyopita, iliyokuwa Tanganyika kwa wakati huo haikujiunga harakaharaka hadi ilipofahamu maslahi yake, lakini suala hilo halikuzuia nchi za Kenya na Uganda kuanzisha Umoja wao wa Forodha.
Tanganyika ilijiunga baadaye! Hata ile Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 ilianzishwa baada ya kupita miaka 50 tangu kuanzishwa Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki. Sasa hii haraka ya sasa hivi ya nini? Ni faida gani itapatikana ? Mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na watu fulani kupata posho za vikao vya EAC na baadhi kuandikwa kwenye vitabu vya historia, vipi hasa vinatakiwa kutusukuma katika fast track?
Huo Mkataba wa EAC uko wapi ili tuweze kuuona na kuusoma? Ni Watanzania wangapi waliousoma na kuuridhia ikawa sasa tunaanza kuwa kwenye mchakato wa kuelekea kwenye Shirikisho? Je wale waliosababisha Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki kuvunjika hawatarudia makosa waliyoyafanya mwaka 1977 kwa kutuacha bado tunafurukuta? Mimi naona kujiunga kwetu kwafanana na Punda wa kwenye hadithi moja iliyochapishwa Tanzania ambamo Simba baada ya kujeruhiwa, alishindwa kuwinda; na Sungura, Fisi na Punda wakaenda kumpa pole.
Kumbe Fisi na Sungura walikuwa na lao jambo, punda akawa kitoweo.
Nimejaribu kutafakari maoni ya watanzania kwa muda sasa juu ya kujiunga na shirikisho. Maoni ya watanzania wengi ni kuwa hatujawa tayari. Nami najiuliza ni lini tutakuwa tayari? Halafu hoja kwamba wakenya wapo mbali kiuchumi, hivi ni nani amesema kuwa wakati sisi tukijiweka sawa wakenya watakuwa wanatusubiri ili tuwe sawa?
Maoni yangu ni kuwa kutokuwepo usawa ndio hasa ingekuwa sababu ya kuungana. Kila nchi ina mapungufu na mazuri yake, tunajiunga ili kupiga hatua pamoja. Hata huo umoja wa ulaya ambao watu wanatolea mfano sana, mbona nchi nyingi tu hazifanani kiuchumu, kisiasa, n.k.
Hao ndugu zetu wa Burundi na warwanda wakija tutawaambukiza ustaraabu na pengine upuuzi wao wa kupigana ukaisha maana katika muungano itakuwa hamna cha mtusi wala mhutu. Na sisi Tanzania tutafaidika sana hasa katika maeneo mengi, kwa mfano:
i) kuchangamka kibiashara na katika kazi maofisini. Hii longolongo ya watanzania kupiga story maofisini badala ya kuchapa kazi itaisha
ii) kuvipiga msasa vyombo vyetu vya habari. Ilivyo sasa vyombo vyetu vingi vya habari kazi yake ni kuitukuza serikali tu kama vile viongozi wa serikali ni malaika. Shirikisho litawaamusha waandishi wetu waweze kuandika with a critical mind na waache kulamba viatu vya viongozi.
iii) Kukuza demokrasia: Sio siri wenzetu wa Kenya wametuacha katika hili. Angalau sasa wamefikia hatua ya kuwa na uwezo wa kubadilisha serikali kwa njia ya kura. Sisi tupo nyuma katika hili. Tunafikiri hakuna maisha nje ya CCM. Yaani tunaogopa mabadiliko. Shirikisho litatuamsha tupende mabadiliko. Hii itakuwa nzuri maana chama chochote kitakachokuwa madarakani kitakaa sawa kikijua kuwa tukicheze atakuja mwingine. Leo ilivyo, CCM wanajua iwe mchana au usiku ni wao tu hata wakifanya makosa namna gani. This is not healthy.
Having said that I must warn Kenya contributors in this forum who come by unergistered identity. Why you guys like swearing, you can't finish your contributions without the word f***k. Can't you do better than this? Again, stop cheating yourself that you are far better than us. We are all poor. Carefully examine who is owning the wealth you claim to possess in Kenya, and you will realise that it is a handful of people. At the end of the day the majority of our people in all sides (Kenya, TZ and Ug) are miserably poor. There is nothing to be proud of. it is this mentality of yours that scare most of Tanzanians to join this noble body.
Yote uloongea YOU ARE RIGHT MAN! The prob is not Kenya... Not Uganda! No... Why Tanzanians fear Uganda? Labda hiki ndo wengi wanashindwa kuelewa. Ukisoma mawazo ya wengi utaona wanawapenda waganda kama waganda lakini HAWAMPENDI MU7. Wanamjua huyu kiumbe! Si wa kumchekea. Ajabu ndo anahaha ili tuungane aone kama anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwa rais wa Afrika Mashariki. Hana maana huyu!
Kuhusu Kenya: Nilikuwa naangalia EATV na nikawa nasikiliza mawazo ya watanzania walio wengi. Wengi walionekana kutopenda kuungana na wakenya sababu zikiwa kuu 3.
a) Wakenya hawana UTU. Hii imeongelewa na wengi wakidai wakenya dhamira yao kwenye muungano huu si kuwa na udugu na kusaidiana kuinuana kiuchumi. Wanadai wakenya kwao ardhi imekuwa aghali sana na ajira ni mzozo. Wanatamani wahamie kabisa Tz lakini bado wanaona kuna kiwingu. Hapa wanafanya kila liwezekanalo tuwe sote ili wajidunge Bongo kirahisi kwakuwa firms nyingi ambazo zimetokea Kenya zinapenda kuwaajiri wakenya kwa kigezo kuwa WAMESOMA SANA.
b) Wakenya wametuzidi kielimu: Hapa naona watanzania wanashindwa kuelewa maana ya ELIMU. Kama elimu wanayoiongelea watanzania ni Kiingereza (kama watangazaji wa kipindi husika walivyoonekana kusema) basi wamepotea sana. Kuna haja ya kuwafanya wajue maana ya elimu. Pia nasi ni wasomi sana hadi kuwa na lugha moja inayoweza kuongeleka nchi nzima hadi nje ya nchi. Kiswahili ni lugha ya kujivunia. Nilitarajia watanzania waone kuwa hii ndo fursa ya kuwafanya hawa watu wakithamini kiswahili na waache kuutukuza u-kiingereza ili kwa sauti moja tuweze kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
3. Kuwa wakenya ni wajanja sana kuliko sisi: Hapa bado napingana na wenye mwelekeo huu. Huu ni woga ambao sijui nani kawajengea watanzania. Mara zote niendazo Nairobi huwa nawaona vilaza hawa wakiwa hawajui mambo mengi hasa ya teknolojia. Wale wanaoiona Kenya imeendelea sana au wanadai wana ujanja kuliko sisi basi wanashindwa kuelewa maana ya ujanja. Hawa si wajanja NI WEZI. Tena wizi wao wanakuibia kwa wewe kutojua lugha ya kiingereza (udhaifu wa watanzania walio wengi). Aidha wao si wasomi kama wadhaniavyo walio wengi. Hawa ni wasanii tu na ukiwajulia basi unawaliza kila siku.
Nasikitika watanzania hawajithamini na kujiona wao wanyonge. Ni kweli polepole ya kobe humfikisha mbali. Wanachofanya wakenya si ujanja... Ni usanii tu ambao mwisho wake daima huishia kama walivyo sasa. Hawana uhakika na ajira. Halafu kwa usanii huu ndo wanaishia kuonana ubaya. Ki-demokrasia sidhani kama wao ni wajanja kwa njia wazitumiazo kudai haki. Mwanasiasa naona huenda hawa jamaa hujajua upungufu wao. Kushinda kwa Kibaki kumekuja baada ya SOTA NDEFU SANA. Najua una background yote. I believe hata Freeman akiendelea hivi we can beat these Kenyans tena kwa njia ambayo wewe utakubali watanzania wana akili kuliko wadhaniwavyo!
Anyway, yote ni kheri... Mimi sipendi kuwa na muungano na jamaa hawa lakini kwakuwa wakubwa wameshaamua hatuna jinsi... Ni kelele za vyura baba!