East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Kaka umeambiwa soma email, huyo anaweza kuwa babako. Msalimie huyo maana anaonekana anakujua hata kama ni Unregistered. Poa lakini inapendeza kwani raha ya mtandao ni kufahamiana.

Natamani nami nipate ndugu humu
 
Hey
Watanzania wezangu kitu muhimu kuna tofauti kati ya shirikisho na jumuia
shirikisho la sasa linalotaka kuundwa yani ni kutokomeza jina kenya jina tanzania jina rwanda jina uganda jina burundi na kuwa nchi moja inayoitwa shirikisho ya afrika mashariki.
ile jumuia ya mwanzo ilikua inajumuisha mambo kadhaa na mambo mengine yalikua yanashugulikiwa na nchi husika ,hivyo basi kutakua hakuna wizara ya tanzania ila wizara ya shirikisho,kutakua hakuna hospital ya tanzania ila ya shirikisho
sasa basi watanzania tunachokataa ni ikitokea Raisi akatokea kenya wizara zote na sehemu nyeti zote si watajaa wakenya si kwamba eti wakenya wamesoma wanatuzidi hakuna hilo halipo mbona wako shallow balaa si tunao ila watatumia ukabila na ukenya
kama mnataka kukubali hili, saizi wanauchaguzi angalieni kampeni zinavyoendeshwa yani ni unakuru ,ukarejing u kisumu,u lift valley ndio siasa zao
ukirudi rwanda kama ni mtusi vigongo wa juu ni watusi ,uganda da burundi ndio basi
jumuia ya ulaya hii ni jumuia tu na haikuvunja nchi na kua na raisi mmoja kila nchi inafanya kama nchi ila wana mambo machache wanayoshirikiana
hili swala lakua nchi moja jamani watanzania tuliangalieni kwa makini
ukiangalia babu, mama na bibi zetu wana mashamba na nyumba lakini hawana hati miliki za mali hizo
upande mwingine wewe mwenyewe huna dokomenti inayokubainisha kua ni mtanzania jamani mtanyaganywa kila mlichonacho kuweni makini
hawa manyang'au wa kikenya na kiganda wamejiaandaa siku nyingi kutuvamia wao ardhi yote wameigawa na hati miliki pia wanavitambulisho
jeje wewe mtz ?
tukaeni pamoja tulikatae shirikisho bila hivyo watanzania tumeliwa
Asili ni asili tu hakuna asili mbovu ikiwa nchi moja bado kuna LRA watataka kuingia madarakani kwa silaha ,bado wanyarwada watataka kutawala ,warundi maana asili haipotei kabisa na bado watakua na ushawishi maana
wana majeshi mwisho wa mwisho tutashangaa na sisi tunakua wakimbizi
wa kivita kongo au malawi
Peter Mkama -Poaland

Ni woga tu ndugu yangu. Ukisoma mkataba hausemi kwamba eti majina ya nchi yatauwa. Shirikikisho sio sawa na muungano. Halafu kwa nini unaogopa kwamba Rais lazima atatoka Kenya, mbona sisi tupo wengi kuliko wao kiidadi? Actually, katika taasisi zingine ambazo tunashirikiana hizi nchi tatu, Tanzania huwa na camp na Uganda na mara zote huwa tunawatoa wakenya katika kura. Hili lisikuogopeshe hata kidogo.
 
Woga wangu
sio raisi atatoka kenya ila mzazingira yaliyowekwa na serikali ya tz kuwalinda watu wake ni zero, hii nitofauti kabisa jinsi serikali za kenya na uganda zilivyojiaanda.

Nimesema ukienda kenya ardhi yote imemilikiwa na kila mmiliki ana hati miliki yake hali vivyo hivyo uganda, sasa ukiangalia kwetu asilimia karibu zaidi 70 hawana hata haki miliki za nyumba zao hawana ndioo, pia hata sisi wenyewe wabongo hatuna vitambulisho tu vyakutujulisha yani balaa tupu
Pia ktk nchi hizi kuna warafi mno wa madaraka, ikitokea hapo ukawa raisi kuna jamaa hawatavumilia hilo.

Mfano wewe umeshindwa kuongoza uenyekiti wa kitongoji je utaweza kuongoza nchi ukiwa kama raisi?

Angalia raisi kibaki wa kenya ODM kile chama cha chungwa kiliendesha kampeni zake na bunge likataka kumpigia kura ya no confidence alichofanya ni kuvunja bunge na kusambaratisha baraza la mawaziri
ukirudi uganda mseven ameshindwa kuunganisha kagroup kadogo tu ka LRA
huko burundi kila mmoja anajua.

Leo hawa viongonzi ndio wanataka kutuunganisha na watuongoze
jamani mbona hatuwezi kujiuliza hata swali kidogo kama hiki
leo wewe hapo nenda kenya ukajaribu kutafuta kazi utakchokipata huko hutarudi tena kufikiria hilo lishirikisho, na hata hivyo hiyo katiba na yaliyomo humo si wa yaweke bayana kwanza badala ya kuanza kulaghai wananchi kujiunga wakati hatujui yaliyomo ni yale yale ya CHIEF MAGUNGO WA USOVELO

Peter Mkama
 
Suala hapa ni shinikizo tu. Binafsi nionavyo ni kwamba viongozi wetu hutoa maamuzi makubwa yanayohusu maslahi na uhuru wa nchi kana kwamba Tanzania ni familia ya mtu fulani. Sijaona kabisa utashi wa wananchi kuhusishwa katika mambo ya msingi yahusuyo Tanzania. Bunge la Tanzania kwa mtu anayejua ukweli ni chombo cha serikali cha kipitishia malengo yake kwa faida ya "the high cream" ambayo imeshika nchi tangu Tanganyika kupata uhuru wake. Kwa mpenda ukweli yeyote hawezi kusema Bunge ni la wananchi wakati kule ni lazima kusema "ndiyo" kwa lolote linaloletwa. Ukisema hapana utaweka kitimoto kwenye kikao cha wabunge wa chama husika na hata kupigwa biti la kuvuliwa kiti chako. Je kwa mtindo huo hata EAC inaridhaa ya Watanzania?

Mwananchi wa Tanzania hana mamlaka yeyote kuanzia kuamua kama Tanganyika na Zanzibar aiungane mpaka leo hii wakati wa East African Community na EAF. Hawa watoa uamuzi ndio wale wale walio radhi sisi tule nyasi mradi tu wao waweze kununua dege la kifahari. Ni watu ambao wamejaa tamaa za kijineemesha, hawajali kabisa maslahi ya taifa na Watanzania, wanachojali ni kitu kimoja tu, watapata nini kujazilizia pale ambapo hawajaweza kuziba.

Binafsi nasikitika sana kwani wananchi wa Tanzania tu wageni katika nchi yetu wenyewe, hatuhusishwi katika mambo yanayoathiri uchumi na uhuru wetu. Tutahusishwa tu kwa mgongo wa chupa mwishoni ili katika historia inayoandikwa na hao watawala isomeke kuwa “wananchi walitoa mawazo yao na wakakubali kuwa tuwe na EAF”.

Katika hili la federation serikali iliisha waanda wananchi kujua federation ni nini? Au kama kawaida yetu tunakurupuka tu? Kumeshawahi jiunga na Regional associations ngapi baadae tukagundua kuwa tulifanya makosa?

Kenya binafsi sihofii sana maendeleo yao, lakini nadhani ni nzuri tujue pia wana political ideology tofauti sana na Tanzania tangu uhuru wao, kila kitu Kenya kimemilkiwa na mtu binafsi. Tanzania tumeanza tu suala la privatization, tena katika makampuni yaliyokuwa ya kiserikali. Kwenye ardhi bado, tunahitaji tuzoee kwanza maisha haya mapya kabla ya kuingia ndoa na wazoefu hawa.

Enyi watanzania wenzangu, tusiamuliwe katika hili, tuwe na msimamo mmoja, tusubiri tuwe kwanza na hii EAC kwa muda wa kutosha ndipo tuingie federation. Kwa yeyote mwenye uwezo wa kuona na kufikiri atakuwa ameisha hata stukia tu migogoro ambayo ipo EAC sasa (mfano wa majaji) na kujua EAF itakuwa vipi. Kenya kupata tu wabunge wa EAC inasumbua vile, majaji nao wa EAC wapo njia panda sijui EAF itakuwa vipi.

Tufikirie pia hawa jamaa walivyo na malengo ya ajabu ambayo walianza kuyaonyesha tangu zama za Mlima Kilimanjar uko Kenya mpaka enzi hizi za Mbuga ya Serengeti ipo Kenya. Nadhani kuna baadhi ya wenzetu hawafikirii kuwa na Federation kwa lengo zuri, lengo pengine ni kupora na kunyang'anya raslimali za nchi nyingine. Ukweli huu unaweza kuthibitisha zaidi na TOWARDS AN EAST AFRICAN FEDERATION: utapata article nzima toka Kituo cha Katiba through link hii http://www.kituochakatiba.co.ug/eac2.htm


Tuwe macho
 
Kenya wamechukua miaka 26 kuwalipa WTZ mafao yao baada ya kuvunjika kwa jumuiya lakini waliwalipa wenzao wakenya zamani sana (i.e. charity begins at home). Je ni kwa nini wanalipa sasa? Jibu ni rahisi sana wanataka Muungano sio jumuiya tena irudi ili waendelee kufaidi …………………………………………..

Kenya: Country Pays Tanzanian EA Airways Pensioners

The East African (Nairobi)
January 16, 2007
Posted to the web January 16, 2007
Nairobi
Kenya's National Social Security Fund has paid terminal dues to former Tanzanian employees of the defunct East African Airways Corporation (EAAC), ending a dispute that has raged since 1980, when the regional carrier was placed under receivership.
The Fund last week issued a cheque for just over Ksh7 million ($94,594) to representatives of 287 Tanzanian nationals who have over the years pursued payment of their terminal benefits from the Kenya government without success………………
Endelea kusoma story hii hapa: http://allafrica.com/stories/200701160509.html
 
Hey
Watanzania wezangu kitu muhimu kuna tofauti kati ya shirikisho na jumuia
shirikisho la sasa linalotaka kuundwa yani ni kutokomeza jina kenya jina tanzania jina rwanda jina uganda jina burundi na kuwa nchi moja inayoitwa shirikisho ya afrika mashariki.
ile jumuia ya mwanzo ilikua inajumuisha mambo kadhaa na mambo mengine yalikua yanashugulikiwa na nchi husika ,hivyo basi kutakua hakuna wizara ya tanzania ila wizara ya shirikisho,kutakua hakuna hospital ya tanzania ila ya shirikisho
sasa basi watanzania tunachokataa ni ikitokea Raisi akatokea kenya wizara zote na sehemu nyeti zote si watajaa wakenya si kwamba eti wakenya wamesoma wanatuzidi hakuna hilo halipo mbona wako shallow balaa si tunao ila watatumia ukabila na ukenya
kama mnataka kukubali hili, saizi wanauchaguzi angalieni kampeni zinavyoendeshwa yani ni unakuru ,ukarejing u kisumu,u lift valley ndio siasa zao
ukirudi rwanda kama ni mtusi vigongo wa juu ni watusi ,uganda da burundi ndio basi
jumuia ya ulaya hii ni jumuia tu na haikuvunja nchi na kua na raisi mmoja kila nchi inafanya kama nchi ila wana mambo machache wanayoshirikiana
hili swala lakua nchi moja jamani watanzania tuliangalieni kwa makini
ukiangalia babu, mama na bibi zetu wana mashamba na nyumba lakini hawana hati miliki za mali hizo
upande mwingine wewe mwenyewe huna dokomenti inayokubainisha kua ni mtanzania jamani mtanyaganywa kila mlichonacho kuweni makini
hawa manyang'au wa kikenya na kiganda wamejiaandaa siku nyingi kutuvamia wao ardhi yote wameigawa na hati miliki pia wanavitambulisho
jeje wewe mtz ?
tukaeni pamoja tulikatae shirikisho bila hivyo watanzania tumeliwa
Asili ni asili tu hakuna asili mbovu ikiwa nchi moja bado kuna LRA watataka kuingia madarakani kwa silaha ,bado wanyarwada watataka kutawala ,warundi maana asili haipotei kabisa na bado watakua na ushawishi maana
wana majeshi mwisho wa mwisho tutashangaa na sisi tunakua wakimbizi
wa kivita kongo au malawi
Peter Mkama -Poaland

Sasa ndugu yangu Peter, kukimbia kwetu kutoka EAC kunatatua vipi matatizo yote haya uliyoyaorodhesha?
 
Mwanasiasa
Jambo si kukimbia jambo ni kuandaliwa mchakato ulio makini na unaolinda masilahi
ya Wananchi na Taifa kwa ujumla
Ndugu yangu, waafrika tunatatizo la planning, mara nyingi tukiplani hua mitizamo yetu inakomea kwa watoto zetu tu
ndio maana utakuta babu zetu wakifufuka leo watakuta tofauti ndogo sana au isiwepo kabisa kutokana na mipango mibofu mibofu ya serikali zetu za kiafrika
plani nzuri ni ile inayoangalia zaidi ya miaka 200
sasa basi ukiangalia huu mpango wa shirikisho ni kitu kilicho jandaliwa na watu wasiozidi 10 eti kwa maamuzi ya watu zaidi ya 150000
ndio tumewachagua watuongoze si kwa ridhaa yao ila yetu na sio kwamba kwa vile wanatuongoza wanamawazo na maauzi yaliyo bora kuliko wanaongozwa

hivyo basi kwa vile viongozi wetu walikaa na kuonelea hivyo ilitakiwa sasa swala hilo riludishwe kwa wanachi walijadili kwa mda unao faa waongeze au wapunguze vipengele vilivyomo au walikatae kabisa kwa masilahi yao na si kitu mmeshaunda eti wananchi watoe maoni ,maoni gani sasa atoe wakati hajui yaliyomo, Je wewe unaweza kukubali kuuziwa kuku aliyefungashwa ndani ya junia kwa kuaminishwa tu kuwa kitu kilicho humu ndani ya junia ni kuku??

au wewe ulishawahi nunua kiatu bila kujua kiatu hicho ni namba ngapi?
Mhimu hapa mchakato huu uwekwe bayana upewe mda na wanachi toka kitongojini wajue nini shirikisho ,nini kilichomo ndani ya shirikisho ,mwananchi atanzue faida na hasara za shirikisho na bado mwananchi apige kura yake ya ndio au hapana
na si THE SAID FAST TRACKING tena kwa maoni na tena kwa baadhi ya maeneo ,je tutaamini vipi? kama hao watu wanaotoa maoni hawajaandaliwa??
hey YOU TIME TIME BEFORE TIME TIMES YOU
Peter Mkama
 
Kwanza tungemalizana na tatizo la Zanzibar. vipi hatukubali kuwaacha wapinzani tu wa kisiasa kuchukuwa madaraka hata wanaposhinda uchaguzi halafu tunganganie Shirikisho la afrika Mashariki!!!?

Kwani ni nini hasa tunachotafuta? Jee ni sifa? Kama hatuwezi kumalizana na wanaotupinga kwenye sanduku la kura Tutajiunga na wanaopigana wenyeewe kwa wenyewe kila siku!!?

Watanzania tuweni macho, na hala hala ujiti na macho ncha una hoho.
 
Kwa maoni yangu naona Tanzania haina haja ya Shirikisho kwa miaka kadhaa ijayo. Wala sasa si wakati tena wa kuburuzana. Tutazame tatizo la Muungano na Zanzibar linavyotusumbuwa na yet hatujataka kulitatua. Fikra za watu wawili tena marehemu zinatusumbuwa hadi leo. Bora tuweni makini na infact wananchi tukataeni kwa nguvu zote.

Ikibidi tushikamaneni kuona kuwa Muungano na Zanzibar uulizwe upya au uvunjwe kabisa kwani sioni kwa dhahiri tunachofaidika zaidi ya kuwa siku moja tutaadhirika. So far Zanzibar walio wengi wanalalamika sana basi natutatuwe hili kabla hatujatafuta kuungana na wanaopigana kwa mitutu kama Uganda,Ruanda na Burundi. hata hao Kenya sioni kama wana nia safi nasi. natutizame suala la Mlima Kilimanjaro wanvyolitangaza nje, na actually hata mbua za Serengeti kwamba ni zao.

Jamani nini tunalofata kwa Muungano huu mara hii!!!???? TUSEMENI HAPANA TENA DAIMA.
 
Adm. vipi tena hapo juu, mambo gani haya humu! Hamna namna ya kuzuia haya kabla huyu mjinga hajapost ushetani wake humu?
 
Ndugu yangu Mwanasiasa nahangaika sana na haya madude lkn bado yatajisajili tu. Ila nadhani haichukui hata dakika 10 nakuwa nimeondoa. Aidha narejea kauli yangu ya awali. DO NOT FOLLOW ANY LINKS YOU GET FROM THESE SPAMMERS.

Anything at free cost will cost you in turn. DO NOT CLICK ANY OF THE PHOTOS OR LINKS. I kindly request you. We gave you an opportunity of posting without being registered but we're facing probs b'se of this offer.

We're doing our best!

Regards
 
The Nation (Nairobi)
OPINION
January 27, 2007
Posted to the web January 26, 2007
Peter Kimani
Nairobi

The ambition to form the East African political federation has been alive for the past few years. It is expected to climax in 2013 - if the people of Kenya, Uganda and Tanzania endorse the plan through referenda.

For generations, border communities in the three countries have embraced the idea of oneness by way of trade, marriage or simply migrating across the border to start a new life.
On a trip across the region in 2004, a Nation team assessed the people's attitude towards this political vision, and their own understanding of its meaning and future implications. However, not many understood what the bureaucrats in Arusha, the seat of the East African Community, were doing, or even how a federation would benefit them.

Immigration

It did not help much either that the bureaucracy at the immigration offices in the three countries had made the movement of goods and people excruciatingly slow.
Besides the duplication of paperwork, where one is required to fill out forms repeating what had been revealed only a few metres away, there are the fees to be paid for business visas. It costs a lot more to transit goods from one country to another, as the fees are charged per axle and distance from the point of origin. This may have been sorted with the introduction of the Customs Union on January 1, 2005, when the protocols to harmonise tariffs on goods imported into the region were ratified.

However, there are still other teething problems.

Doing business

The cost of doing business in the region remains high, at times, ridiculously so. In 2004, for instance, it cost twice as much to transport goods from Mombasa to Nairobi than it would have cost to ferry the same from Durban to Mombasa, 4,000 kilometres away.
And due to the high taxation, some petty traders opt to use panya (illegal) routes to smuggle goods, thereby denying the three countries millions of shillings in revenue.

Skills transfer has also been stunted as the three nations attempt to insulate their limited job markets from skilled foreign workers. The deportation of Nation journalists from Dar es Salaam, over a year ago, for instance, exposed this rivalry.
But traders, whether small or medium scale, are not always in need of a job; in fact, they help create jobs and other opportunities by opening up businesses.

Reluctance to allow fellow East Africans to move freely within the region has benefited Europe and North America, where immigrants are encouraged to travel through established channels.
Political analysts, however, are not very convinced that East Africa is ready to federate.

Develop currency

Prof Ali Mazrui, who is the also the Chancellor of the Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology, says the region will take up to 40 years before this project can be feasible.

For that to happen, the region would first have to develop its own currency and establish joint policies on transport and communication among others.
Such structures existed in the colonial times. The three countries inherited and operated them successfully until 1977 when things fell apart. For instance, the Customs Union between Kenya and Uganda was first established in 1917 and Tanganyika later joined in 1927.
Then there was the East African High Commission (1948-1961); the East African Common Services Organisation (1961-1967) and the East African Community that lasted from 1967 to 1977.

Differences

The collapse of the community was precipitated by ideological differences among the region's leaders: Uganda's Idi Amin who became a dictator; Tanzania's Julius Nyerere who adopted socialism; and Kenya's Jomo Kenyatta who embraced capitalism.
Full East African cooperation operations started on March 14, 1996, when the secretariat of the Permanent Tripartite Commission was launched at the headquarters of the EAC in Arusha, Tanzania. While the three countries are likely to remain autonomous, there will be a new flag and anthem for the region, with a rotational, largely ceremonial presidency, only six years away - if voters from the three countries give their green light.



New flag, new anthem and rotational ceremonial president. I think we have more important things to do than this ceremonial presidents; this shows how narrow minded are those entrusted in power.

At the moment the UK though not publicily would be happy to get rid of the useless queen but us we are trying to introduce one useless ceremonial president, absolutely stupid! How is this going to help development? (Tanzania will end up with almost three top leaders from Zanzibar, TZ bara and a ceremonial one being paid by poor people of EAC union, just creating monsters to chew tax payers money and more bribery).
 
phuck it.I want Kenya to remain Kenya as it is, with it's beautiful flag an fun Anthem.I want Nairobi,Mombasa,Kisumu,Laikipia,Kakamega,Lamu,Kisii ,Busia to remain Kenyan as it's always been an i wouldn't trade anything Kenyan for a zillion dollars.Tanzanians,we Kenyans are so proud about our country,we just love to hate it.Now that's a neighbour u don't wanna be friendly with.Point is we
are just be gonna be Kenyans.We will come to Tanzania an do business.Then we shall go to Malawi,Mozambique ,wherever.Who gives a shyt.U Tanzanians can whine all year about Kenyans but u got to get this,Kenya is the the country to ur north that is there to stay.Now what u gonna do about that?????????.
 
We dont care about anybody we care about our country. We dont need to import corruption or violence from anybody. East Africa should remain as it is right now, and yes we are not afraid of business because we are better in that field.

Kenyans need to understand Tanzanians are happy people and not show off like you guys who like to start fight with everybody. We are Tanzanians and not your other tribe, you can still do business in TZ now but we dont want to rush to be the same thing with your corrupt and tribal nation.

Most people are making a big deal out of our Economy, Tanzania GDP is $12B and Kenya $16B that is not as big deal as you think because that is not a huge difference. You should also consider what we imports from you guys is mostly domestic supplies and the fact that most of minerals like Tanzanite are under radar and should well be above $2b a year which is not considered in GDP.

Tanzania GDP in reality is bigger than $12B and everybody know it. Kenya problem is the fact that you have 50% of the population under poverty level the highest in East Africa, the solution is for Kenya to create middle class, joining TZ and Uganda is not going to make as much difference as you think. Nobody is going to give you guys land and you can not do business by force.
 
Kama kuna matatizo nchini Tanzania basi utaona ni kuwa moja kati ya hayo matatizo ni kuwa Viongozi wanaokuwa madarakani hujiona kuwa wana akili kuliko watu wote wanaowatawala.

Kwa kudhihirisha haya ni pale linapokuja suali la kuundwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Kwani hivi karibuni tumesiki kuwa imeundwa tume ya kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu kuanzishwa kwa shirikisho hilo.

Cha kujiuliza ni kuwa hao Wananchi wanaotakiwa maoni yao hususan vijijni wanao uwelewa wa kutosha nini hasa kinachotaka kufanyika?.

Pili, ndani ya Tanzania kuna matatizo kibao ambayo hayatatuliwa hasa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jinsi kila siku unavyozidi kudidimia na kero kuzidi badala ya kupungua.

Tatu, Tanzania yenyewe haiko tayari kuheshimu utawala wa kideokrasia kwa kukubali ushindi wa chama cha upinzani hasa Zanzibar na athari zake nikusababisha kuvunjwa haki za kibinaadamu kwa kufanyiwa vitendo viovu na askari wa Jamhuri wa Muungano kwa kubaka, kuuwa na kuiba mali za wananchi wema.

Nne, Rwanda na Burundi ni nchi ambazo wamechinjana vya kutosha na hata kufikia kuwa Rais wao anatakiwa akajibu mashitaka juu ya kuongoza mauaji hayo. Jee, sisi tutakuwa tayari kuwakumbatia wauaji. Pia Karume wa hivi sasa wa Zanzibar ameuwa Wazanzibari 24 baadae aliwapongeza vikosi kwa kazi nzuri ya mauaji na kupora mali za raia. Jee na huyu nafasi yake atawekwa wapi kwenye Shirikisho.

Tano, kwanini kwanza sheria ya kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki imetungwa mwanzo kabla ya kukusanya maoni ya wananchi. Jee ikiwa Wananchi watakataa itakuwaje au ndio wataburuzwa kama magombe tu.

Kwa maoni yangu hili shirikisho la Afrika Mashriki halifai kwani linaonesha kuwa lina ujanja ujanja fulani umefichwa na hautakiwi ujulikane.
 
Tufanye subira kujiunga na Shirikisho - NCCR

2007-01-29 09:31:36
Na Dunstan Bahai

Chama cha NCCR-Mageuzi kimeishauri serikali ifanye subira wakati ikijiandaa ipasavyo kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki, vinginevyo itakuwa imefanya kosa kubwa la kihistoria.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema kwamba, chama hicho hakikatai Tanzania kujiunga kwenye shirikisho hilo, lakini kabla ya kufanya hivyo kuwe na muda wa kutafakari ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya faida na hasara za kujiunga.

Akifafanua zaidi, alisema kwamba, kinachotakiwa kufanywa katika kipindi cha kuelekea kujiunga na shirikisho hilo, ni serikali kutoa mchanganuo wote kwa wananchi juu ya shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na katiba yake.

Kwa mujibu wa Bw. Mbatia, kushirikiana katika masuala ya kiuchumi, kibiashara, kuwa na sarafu moja si tatizo, lakini tatizo analoliona yeye ni kuwa na dola moja.

Katika mazingira hayo, alisema kuwa, hakutakuwa na nchi ya Tanzania kama ilivyo sasa na hakutakuwa na Rais wa nchi moja moja bali kutakuwa na Rais wa Shirikisho na kwamba hakutakuwa na raia wa Tanzania bali ni wa Afrika Mashariki.

`Tunachotaka sisi ni kila nchi ibaki na Rais wake, utawala wake na ndipo kuwe na Rais wa Shirikisho,` alisema na kuongeza kuwa hali hiyo itasaidia kila nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake badala ya kumezwa na nyingine.

Dk. Sengodo Mvungi ambaye ni Mkurugenzi wa masuala ya sheria ya chama hicho, alisema Tanzania kama Jamhuri ya Muungano, inajumuisha nchi mbili, hivyo kuingia kwake kwenye shirikisho kunahitajika mjadala mkubwa wa kutafakari jinsi ya kuingia, tofauti na nchi kama Kenya na Uganda ambazo zinaingia kama nchi moja moja.

`Hatupingi kuingia kwenye shirikisho, tunachotaka ni mchakato wa shirikisho lenyewe.

Ieleweke kwamba raia wote wataingizwa kwenye kapu moja, Rais mmoja na nchi wanachama zinabakia kama majimbo, alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Mvungi, hata wawakilishi wa kibalozi watatambulika kama wawakilishi wa Afrika Mashariki na si wa nchi moja moja kama ilivyo sasa na mipaka yote itakuwa wazi.

Kutokana na migogoro ya baadhi ya nchi wanachama watarajiwa wa shirikisho hilo, alionyesha wasiwasi wake kwa madai kwamba upo uwezekano wa kuhamia katika nchi zisizo na migogoro wala historia hiyo.

Alisema, kuingia kwenye shirikisho ni rahisi lakini kujitoa baada ya kuona matatizo itakuwa ni ngumu kwani upo uwezekano wa wanachama wengine kuishambulia nchi inayojitoa.

`Tukiingia kichwa kichwa tutafanya kosa kubwa sana la kihistoria. Watoto wetu watalaani kosa hilo na wataona njia rahisi ni kuingia msituni ambako itakuwa ni vigumu kuwatoa.

Kuwa na shirikisho inamaanisha kuwa na dola moja,` alisema na kuongeza kuwa, unahitajika muda wa kutoa elimu kwa wananchi ambao hasa ndio wenye maamuzi badala ya kukurupuka.

Dk. Mvungi alisema pia kuwa hata sasa wapo wananchi wengi watakaopinga pindi wakipata elimu ya mikataba ya shirikisho hilo na wakiamua kuingia msituni kuwatoa itakuwa ngumu.

Alisema taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Woka, juu ya kuharakisha kuundwa kwa shirikisho hilo, inaelekeza Rais wa shirikisho atakuwa ni Rais aliyekaa madarakani muda mrefu kuliko wenzake ambaye kwa sasa ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Wiki iliyopita, chama hicho kilimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete kwa kuunda tume ya Profesa Samwel Wangwe ya kukusanya maoni kwa wananchi kuwa Rais alikosea kwa kwenda kinyume na katiba.

Chama hicho kiliishauri serikali kutumia muda mrefu wa maandalizi vinginevyo kitakwenda kwa wananchi kuwashawishi kugoma kujiunga na shirikisho.

Hata hivyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta na waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mary Nagu kwa nyakati tofauti wakijibu hoja hizo walisema katiba ya Nchi inampa mamlaka Rais kuunda Tume.

Sitta pia alionyesha kushangazwa na kiongozi mkubwa wa chama kama Bw. Mbatia kwa madai ya kuwapotosha wananchi.

* SOURCE: Nipashe
 
Samahani wana furum
Naomba kujua haya maoni tunayotoa yatashughulikiwa namna gani?
je yatafikishwa kunako husika au ni vipi?
Naomba kuelimishwa ili kasi ya uchangiaji imalike zaidi
 
Vema,

Ingawa hujajisajili naomba kukujibu kama ifuatavyo:

1. Kamati inayofuatilia maoni ya wananchi juu ya EAF naamini kuna mmojawapo huingia kuona mnasema nini mtandaoni. Hiyo ni shortcut inayosaidia kwa namna moja ama nyingine.

2. Binafsi nimekuwa nahakikisha kila mwisho wa wiki natuma maoni ya hapa kwenda kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini ili wajue watanzania, wakenya na waganda + Wanyarwanda na Warundi wana mawazo yepi kuhusu Jumuiya hii. Njia pekee ya kusaidia katika hili ni kuwaomba wale wenye ukaribu na wahusika kuwaelekeza wajaribu walau siku moja kuingia mtandaoni kuona watanzania wana mawazo gani juu ya Federation hii.

3. Kuna waandishi wa habari wengi nimesoma makala zao kwenye magazeti ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wamejaribu kuyachambua mawazo ya wananchi wa nchi hizi zote 5 juu ya Jumuiya hii. Wengi ingawa hawataji kuwa wamenukuu mawazo ya wachangiaji wa http://www.JamboForums.com lakini ni wazi wamenukuu mawazo ya hapa na ndo yamewasaidia kuufikisha ujumbe kwa wahusika.

Una wazo la namna gani tufanye ili maoni haya yaende mbali zaidi? Nijulishe haraka tafadhali.

Shukrani
 
Back
Top Bottom